.

SIMBA WA VITA AMEFARIKI LEO

Dec 31, 2009

  Marehemu, Mzee Rashiud Kawawa enzi za uhai wake  Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mzee Kawawa mapema mwaka huu.
RAIS Jakaya Kikwete akitangaza rasmi kifo cha Mzee Rashid Mfaume Kawawa leo, Ikulu, Dar es Salaam.

Stori
MWANASIASA maarufu na mkongwe Rashid Kawawa, amefariki dunia leo saa 3:20 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbuli mjini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa kisukari na figo.

Kifo hicho kilitangazwa rasmi leo na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam, akisema kifo cha Mzee Kawawa ni pigo na msiba mkubwa si tu kwa familia yake bali kwa taifa nzima, kwakuwa wakati wote wa uhai wake alijitoa kuliasisi na kuendeleza Taifa.

"Mzee Kawawa, Simba wa vita ametutoka, hatunaye tena , lakini atabaki daima katika nyoyo na fikra zetu, kwa miaka mingi, hata baada ya kustaafu uongozi aliendelea kuwa nguzo muhimu kwa taifa letu" alisema Rais Kikwete.

Kufuatia msiba huo, Rais Kikwete alitangaza kuwa Taifa litakuwa katika siku saba za maombolezo ambapo bendera ya taifa itapeperushwa nusu mlingoti nchi nzima na Watanzania watapata fursa ya kutoa salamu za mwisho uwanja wa Taifa kwa utaratibu utakaotangazwa.

Kikwete alisema Kawawa alikuwa akijiandaa safari ya nje ya nchi hivyo alikwenda kupima afya yake katika Hospitali ya Usalama wa Taifa, Kijitonyama ambapo hawakuona Malaria lakini wakiwa njiani na mkewe hali ya mzee ilibadilika ghafla nakupoteza fahamu ndipo walimpeleka Muhimbili.

"Baada ya kufikishwa hospitalini hapo, alipimwa nakugundua kuwa sukari katika mwili wake ilikuwa imepungua ndipo akaongezewa maji maalumu kupandishi hali hiyo na alipata nafuu, leo saa 12 asubuhi hali ilibadilika ghafla madakatari wakabaini kuwa sukari imekauka tena na figo zake zote mbili zimeacha kufanya kazi, wakaanza jitihada kusaidia maisha yake lakini pia wakagundua na moyo wake umeshindwa kufanya kazi, hatimaye saa 3:20 Mungu akapitisha uamuzi wake" alisema Rais Kikwete.

Mapema, Daktari bingwa wa magonjwa mahutiti Dk. Mpoki Ulisubisya, aliyekuwa akimtibu hospitalini hapo, alisema Kawawa alifikishwa hospitalini hapo saa 10 za jioni ya janai, akisumbuliwa na sukari na figo. baada ya kumtibu alipata nafuu na alikuwa akiendelea vizuri japo bado alikiwa chini ya uangalizi katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) kutokana na hali yake kubadilika badilika ambapo jana asubuhi aliamka vizuri na alikuwa anatambua watu. Mwili utaagwa rasmi leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
                        
PICHA ZAIDI.........

MZEE Kawawa akiwa  mgeni rasmi kwenye shindano la Miss Tanzania ambalo mshindi aliyeibuka Richa Adhia. Shindano hil;o lilifanyika katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

MZEE Kawawa akaiwa na Mwalimu Nyerere, Rais Wa Zanzibae Aboud Jumbe enzi hizo katika moja ya hafla za kitaifa. pembeni ni Samora Machel aliyekuwa rais wa Msumjibi.MZEE Kawawa akiungana na viongozi wengie akiwemo Mwalimu Nyrere  katika sherehe ya Uhuru wa Tanganyika.
MZEE Kawawa na Mwalimu Nyerere wakiwa na Kiongozi wa  Dhehebu la Ismailia Duniani HH The Agakhan.

SIMBA WA VITA ALAZWA

RAIS Jakaya Kikwete akimjulia hali Mzee Rashid Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jioni. Kulia ni Profesa Victor Mwafongo. Mzee Kawawa alipelekwa Muhimbili baada ya kujisikia vibaya Vipimo vinaendelea kujua anasumbuliwa na nini na hali yake ni stable.


Picha na Freddy Maro wa Ikulu

GABRIEL AMOSS MAKALLA AUKWAA UENYEKITI CHIPUKIZI TAIFA

Dec 30, 2009

Gabriel Amos KATIBU wa Siasa na Uenezi wa mkoa wa Morogoro, Kulwa Milonge, akimpongeza Gabriel Amos baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi wa CCM Taifa katika uchaguzi uliofanyika juzi, Chuo cha Ualimu Morogoro. Gabriel ni mtoto wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Uchumi na Fedha, Amos Makalla. (Picha na Latifa Ganzel).

HABARI KATIKA PICHA: KIFIMBO CHA MALIKIA KILIPOTINGA IKULU

Dec 29, 2009

RAIS Jakaya Kikwete akipokea kifimbo cha Malikia Elizabeth wa Uingereza, kutoka kwa mwanariadha Mary Naali, Ikulu, Dar es Salaam, leo
WATOTO wenye asili ya kiasia wakitumbuiza kwa kucheza muziki wemnye asili ya Kihindi wakati wa mapokezi ya kifimbo cha Malikia Elizabeth wa Uingereza, leo
BAADHI ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo leo
WADAU wa mchezo wa risha nchini wakiwa katikapicha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete.
WADAU  na  riadha na waratibu wa ujio wa kifimbo hicho wakiwa katikapicha ya pamoja na Rais jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam,
BAADHI ya vijana waliojitolea kukimbiza kifimbo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete leo.
WAWAKILISHI wa baadhi ya kampuni wadhamini wa ujio wa kifimbohicho wakiwa Ikulu, Dar es Salaam, wakati wa hafla hiyo leo.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, WILLIAM LUKUVI AFANYA ZIARA GHAFLA SOKO LA SAMAKI FERI NA KUKUTA...

WATU wakigombea maji bombani katika soko hilo, leoWAVUVI wakimsafisha samaki aina ya Papa, katika soko hilo la samaki la Feri
MZUNGU raia wa Italia,  Ivana Maglione akipiga picha, shughuli za upaaji samaki katika soko hilo, leo.
 WAVUVI wakitia nanga katika pwani ya Feri eneo la soko hilo, leo.

SEHEMU ya soko la smaki Feri, Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi akizungumza na mfanyabiashara ya samaki, JamilaOmari, katika soko la Feri, leo
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi akishuhudua mamalishe Mariam Hamadi akisonga ugali klwa ajili ya wateja wake katika soko hilo,leo.
MMOJA wa wafanyabiashara ya samaki wakukaangwa akiwapanga samaki hao wakati akisubiori wateja katika soko hilo, leo.(Picha zote na http://www.bashir-nkoromo.blogspot.com/

YANGA ILIPOINYUKA SOFAPAKA NA KUTWAA UBINGWA TUSKER CUP

Dec 28, 2009Watu kibao wakishuhudia mtanange huo, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

Kikosi kamili cha Sofapaka ya Kenya kilichopambana na Yanga


Kikosi cha Yanga kilichoinyuka Sofapaka


Athumani Iddi wa Yanga akipambana na  James Situma wa Sofapaka


Nurdin Bakari akimkabili Kamadi Michael wa Sofapaka


Kocha wa Yanga Papich akimfunda Abdi Kassim wakati wa mpambano huo

 Nahodha wa Yanga Abdi Kassim akifurahia Kombe

Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kupata bao la pili na la ushindi

Mwenyekiti wa Yanga Imani Madega (katikati) akifurahia kombe

MATUKIO KTK PHOTOS

Dec 27, 2009

Mpigapicha wa gazeti la mwananchi, Emmanuel Herman akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mkewe, Mary Bernad aliyefariki tarehe 24 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa maradhi ya figo na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Jumamosi hii.


Mpigapicha wa gazeti la Habari Leo, Mroki Mroki ni miongoni mwa ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wakimfariji  mpigapicha wa Mwananchi, Emmanuel Herman wakati wa mazishi ya mke wake Mary Bernad aliyefariki kwa maradhi ya figo siku ya tarehe 24 na mazishi yake yalifanyika katika makaburi ya Kinondoni, jumamosi


Meneja Masoko wa Kampuni ya Zain Tanzania Costantine Magavilla (kushoto) akiongea na mshindi wa gari aina ya Toyota Hilux lenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 40 Wilfred Maleko mkazi wa Dar es Salaam baada ya kuendesha promosheni ya 'Zawadi' inayoendeshwa na kampuni hiyo kulia ni Msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatsha Bw.Bakari Maggid.Promosheni hiyo ilifanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mwanamuzi wa Hip hop Mr. 11 akiwapagaisha mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa albam ya kumi ya VETO katika ukumbi wa Diamond jubilee wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Krismasi.


Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo leo Richard Mwaikenda akifurahia zawadi alizotwaa baada ya kuibuka mpigapicha bora katika shindano la Baraza la Habari Tanzania (MCT) mjini Dar es Salaam.

XMAS KATIKA PICHA

Dec 26, 2009SIMBA YAFANIKIWA KUWA YA TATU BAADA YA KUINYUKA TUSKER, TUSKER CUP


MSHAMBULIAJI wa Simba, Juma Jabu akimtoka mlinzi wa Tusker ya Kenya,Francis Oduor, timu hizo zilipopambana jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kuwania nafasi ya tatu ya kombe la Tusker. Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. (Na Mpigapicha Wetu).


KIKOSI cha Simba kilichokong'otana na Tusker team
KIKOSI cha Tuseker kilichobanjuliwa na Simba mabao 2-1


YANGA YAINYUKA SIMBA 2-1, TUSKER CUP

Dec 24, 2009


MCHEZAJI Shadrack Nsajigwa wa Yanga akichuana na Juma Jabu wa Simba, timu hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika mechi ya kuingia fainali ya kombe la Tusker. Yanga iliinyuka Simba mabao 2-1. (Na Mpigapicha Wetu).JERRY Tegete (kulia) wa Yanga akifurahi baada ya mechi kwisha ikiwa imeilamba Simba mabao 2-1. Tegete nduye aliyefunga mabao hayo.

MCHEZAJI Shamte Ally (kulia) wa Yanga akichuana na Joseph Owino wa Simba, timu hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika mechi ya kuingia fainali ya kombe la Tusker. Yanga iliinyuka Simba mabao 2-1. (Na Mpigapicha Wetu).

Kocha wa Yanga akishangilia baada ya mechi

ยช