.

KCB YATIMIZA AHADI YA MILIONI KUMI ILIYOITOA MBELE YA JK

Dec 31, 2010

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB, Dk. Edmund Mndolwa (kushoto), akimkabidhi bango la hundi ya sh. milioni kumi, mkuu wa wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla, katika hafla iliyofanyika leo makao makuu yaliyopo jengo la Harambee Plaza la Ubalozi wa Kenya hapa nchini. Katikati ni ,maofisa wa KCB,  Christina Manyenye na Ronald Kitti.
==========================================
STORI
BENKI ya KCB leo  imekabidhi Sh. milioni 10, kwa mkuu wa wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla, kutekeleza ahadi iliyotolewa na benki hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete, Julai mwaka jhuu.
KCB ilikabidhi fedha hizo kwa Sigalla, katika sherehe fupi iliyoifanyika , katika ukumbi wa ofisi za  makao makuu ya benki hiyo, katika jengo la Harambee Plaza la Ubalozi wa Kenya mjini Dar es Salaam.


 Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Tanzania, Edmund Mndsolwa, alisema, fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa darasa moja katika shuyle ya Sekondari Lyasikika, wilayahi Hai mkoani Kilimanjaro.


Mndolwa alisema, ahadi ya kutoa fedha hiyo, ilitolewa na KBC mbele ya Rais Jakaya Kikwete, June 18, mwaka huu, katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu Ndogo ya mjini Moshi.


Hafla hiyo ilikuwa imeandaliwa na serikali ya wilaya ya Hai na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kukusanya fedha kwa ajili yta kuchangia maendeleo ya elimu wilayani humo.


Katika makabidhiano hayo, Sigalla alisema, msaada huo ni muhimu sana na kuzitaka taasisi na wadau wengine kuiga mfano huo kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa elimu bora nchini. Alisema, hadi sasa, wilaya ya Hai ina jumla ya shule 24 za sekondari za kidato cha sita ikiwemo ya Lyasika.


Kuhusu ushiriki zaidi za KCB katika kuboresha huduma za jamii nchini, Mndolwa alisema, huo ni mwendelezo wa misaada mbalimbali ambayo benki yake imekuwa ikitoa kwa jamii kwama hadi mwaka kwenye sekta za elimu, afya, mazingira na michezo.


Alisema, mwaka jana, KCB ilisaidia shule 14 vifaa mbalimbali vya shule na pia kujenga vyoo na visima katika baadhi ya shule ambapo jumla ya sh. milioni 40 zilitumika.


Mndolwa alisema, upande wa Afya, mwaka jana KCBC ilitumia Sh. milioni 14.5 kusaiodia hospitali ya Taifa Muhimbili (sh. milioni 10) na hospitali ya Buguruni (sh. milioni 4.5, huku matumizi mengine kwa ajili ya jamii yakiigharimu benki hiyo sh. milioni 70.


Kwa mujibu wa Mndolwa KCB ndiyo benki inayoongoza Afriuka Mashariuki kwa wingi kwa matawi na rasilimali kwa kuwa na matawi zaidi ya 200 na mashgine 400 za kutolea fedha (ATMs), mtandao wa benki hiyo ukizifikia Tanzania, Kenya, Rwanda na Sudan ya Kusini.

YANAGA TOTO YALALA KWA SIMBA TOTO 3-1

BEKI wa Simba Mbwana (kushoto), akichuana na mshambuliaji wa Yanga Hussein  timu hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, katika mechi ya mashindano ya Vijana chini ya miaka 20 (U20). Simba iliibuka na ushindi wa mabo 3-1. 

MTIBWA SUGAR YAINYWESHA 4-0 MAJIMAJI, UHAI CUP YA U20

Dec 29, 2010

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar , Richard Jacob (kulia) akiumiliki mpira dhidi ya beki wa Maji Maji ya Sonhgea, Charles Haule, timu hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, katika michuano ya Uhai Cup, kwa vijana chini ya miaka 20 (U20). Maji Maji ililala kwa mabao 4-0

U20 WA YANGA NA AFRICA LYON WASHINDWA KUTANBIANA ZATOKA 0-0 UHAI CUP

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Onesmo Leonard (kushoto) akijaribu kuumiliki mpira dhidi ya mchezaji wa Africa Lyon, Haji Amir, timu hizo zilipomenyana  katika mechi ya michuano ya Uhai Cup kwa vijana chini ya miaka 20 (U20) kwenye Uwanja wa Karume,Dar es Salaam, jana. timu hizo zilitoka 0-0.

STARS WAANZA KUJIFUA

Dec 28, 2010

WACHEZAJI wa timu ya Taifa, Taifa Stars, wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, LEO 
WACHEZAJI Nizar Khalfan (kushoto) na Athumani Machupa, wakishiriki katika mazoezi ya timu ya taifa, Taifa Stas, jana katika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam 
 WACHEZAJI wa Kimataifa, Saidi Maulidi (kushoto) na Athumani Machupa, wakifanya mazoezi huku Kocha wa timi hiyo Sylvester Masha (katikati) akiwafuatilia kwa makini, Taiafa Stars ilipofanya mazoezi, katika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

JK AMWAPISHA JAJI MKUU CHANDE

Dec 27, 2010

Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Jaji Mohammed Othman Chande kuwa  Jaji Mkuu, leo, Ikulu mjini Dar es Salam. katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo na kulia ni Jaji Mkuu aliyestaafu leo,  Augustine Ramadhani. 
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na jaji mkuu mpya, jaji mstaafu na Majaji wakuu wa Mahakama Kuu katika hafla hiyo.

US AMBASSADOR PROMOTES WOMEN'S ECONOMIC EMPOWEMENT

U.S. Ambassador Alfonso Lenhardt on Thursday, December 23, 2010, presented graduation certificates and a start-up kit (a sewing machine, scissors, tape measure and two vitenges) to 17 young women of Mabinti Center in Dar es Salaam. The center trains women who have undergone fistula surgery at the CCBRT hospital in life skills, sewing, beading and printing. Skills that will help them as they leave the center. The start-up kits were purchased using part of a U.S. Embassy grant of 70m/- presented to the center in September this year. (Photo courtesy of the American Embassy)

JK AMTEUA MOHAMED CHANDE OTHMAN KUWA JAJI MKUU MPYA

Dec 26, 2010

* NI MUISLAM WA KWANZA KUWA JAJI MKUU
*KUAPISHWA KESHO SAA NNE ASUBUHI
=====================
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA YA IKUU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, kuanzia tarehe 28 DIsemba, 2010.

Jaji Othman anachukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhani anayestaafu kwa mujibu wa sheria tarehe 27 DIsemba, 2010.
Kwa sasa Jaji Othman ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na pia ni mtaalamu binafsi juu ya hali ya Haki za Binadamu huko Kusini mwa Sudan, hadi mwezi Agosti 2011.

Jaji Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi.

Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda huko Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki.

Jaji Othman pia, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Jaji Othman ataapishwa kesho tarehe 27 Disemba, 2010 katika viwanja vya Ikulu saa 4:00 asubuhi.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Ikulu
Dar es Salaam
26 Disemba, 2010

ARUSHA KUWA MAKAO YA TAWI LA MFUMO WA KIMATAIFA WA KUSHUGHULIKIA MASHAURI YA MASALIA YA MAKAMA YA MAUAJI YA KIMBARI

Dec 24, 2010

NA MWANDISHI MAALUMNEW YORK
Katika kutunza na kudumisha hadhi ya mahakama za kimataifa za mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) na mauaji ya halaiki ya iliyokuwa Yugoslavia ya zamani ( ICTY).Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, limepitisha Azimio la kuanzisha Mfumo wa Kimataifa wa kushughulikia umaliziaji wa mashauri ya masalia ya Mahakama hizo mbili.


Wajumbe wa Balaza hilo (pichani)wamepitisha azimio hilo lililopewa namba 1966 linaloeleza kwamba, mfumo huo wa kimataifa(International Residual Mechanism), utakuwa na matawi mawili yaani tawi la ICTR ambalo makao(seating) yake yatakuwa Arusha na tawi la ICTY ambalo makao yake yatakuwa The Hague, Uholanzi.


Azimio hilo limepitishwa siku ya jumatano kwa kupigiwa kura na wajumbe 15 wa Baraza la Usalama. Katika kura hiyo wajumbe 14 wameunga mkono na mjumbe mmoja hakufungamana na upande wowote.


Kwa tawi la ICTR Mfumo huo utaanza kazi Julai Mosi 2012 na kwa Tawi la ICTY Mfumo huo utaanza kazi Julai Mosi 2013. Mfumo huo wa Kimataifa wa kushughulikia mashauri ya masalia utakuwa na haki, stahili na wajibu kama ilivyo kwa mahakama hizo ambazo zinatarajiwa kukamilisha kazi zake zote si zaidi ya desemba 31 2014.


Kupitishwa kwa azimio hilo na kuanzishwa kwa mfumo huo, licha ya kwamba kunaziongezea muda mahakama hizo kukamilisha kazi zake, lakini pia kunahusisha suala zima la uhifadhi wa nyaraka na kumbukumbu zote muhimu zinazohusiana na shughuli zote za mahakama hizo za kimataifa.


Baraza Kuu la Usalama wa kupitia azimio hilo, limezitaka Mahakama hizo mbili kuweka mazingira mazuri ya kipindi cha mpito kuelekea kuanzishwa kwa mfumo huo wa kimataifa. Na pia kuhakikisha kwamba zinakamilisha kazi zake zote ifikapo desemba 31. 2014, ili kuruhusu mfumo huo kushughulikia mashauri ya masalia na kesi ambazo watuhumiwa kwake bado hawajapatikana.


Vile vile Baraza la limetoa wito kwa nchi zote kuhakikisha kwamba zinatoa ushirikiano madhubuti kwa Mahakama hizo katika kipindi chote cha kuelekea uhitimishaji wa kazi zake.


Ushirikiano huo ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa na wahalifu wote wanaosadikiwa kujificha katika nchi zao ili waweze kufikishwa mbele ya sheria.


Baadhi ya wajumbe waliozungumza mara baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, wameeleza kuwa kupitishwa kwa azimio hilo ni moja yahatua muhimu sana si tu katika kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa wahutuhumiwa kufikishwa mbele ya sharia, lakini ni kielelezo tosha kwamba hakuna mhalifu ambaye yuko juu ya sheria.


Kukamilisha na hatimaye kupitishwa wa Azimio hilo kuna hitimisha mchakato na majadiliano ya muda mrefu, ndani ya Baraza Kuu la Usalama na Jumuia ya Kimataifa, kuhusu hatima ya Mahakama hizo za Kimataifa pamoja na uhifadhi wa nyaraka na kumbukumbu zake baada ya kukamilisha kazi zake.


Tanzania kupitia taasisi zake mbalimbali ukiwamo Ubalozi wake katika Umoja wa Mataifa, na kama nchi ambayo ndiyo mweyeji wa Mahakama ya Rwanda iliendesha kampeni na kujenga hoja za nguvu za kutaka ifikiriwe kupewa stahili ya si tu kuhifadhi nyaraka na kumbumbuku za mahakama ya Rwanda bali pia kuwa tawi la kushughulikia ukamilishaji wa mashauri ya masalia ya Mahakama hiyo.

PROF. NDULU PRESENTED THE NEW TANZANIA SHILING CURRENCY NOTE TO PRESIDENT DK. KIKWETE THIS EVENING

Dec 23, 2010


The Governor of Bank of Tanzania Prof. Benno Ndulu, today presented the new Tanzanian shilling currency note to President Dr. Jakaya Kikwete at Dar es Salaam State House this evening. The New Currency Note will be in circulation from January next year and they will be used alongside with the current bank notes. In the Picture The Central Bank Governor Prof. Ndulu (left) presents a special album with new Tanzanian shilling currency notes to President Dr. Kikwete while the Minister for Finance Mustafa Mkullo,(right) looks on.

President Dr. Kikwete examines special security features in some of the new banknotes presented to him by the Governor of the Central Bank Prof. Ndulu at Dar es Salaam State House this evening.
A senior Principal bank Officer, from the Central Bank’s Directorate of Banking, Mr. Juma Hassan Kimwaga shows President Dr. Kikwete, special security features in the new Tanzanian shilling currency notes. (Photos by Freddy Maro).

VETA DAR YAFANYA MAHAFALI LEO

SHABANI Himidi (7) anayetarajiwa kuanza darasa la kwanza mwakani katika shule ya Green Hill, Dar es Salaam, akionyesha 'machejo' ya kucheza wimbo wa 'uwe' wa kundi la Makhiri khiri, katika mahafali hayo 

Polisi na watu wengine wakimtuza hela kibao mtoto huyo baada ya kuwachen gua kwa machejo yake
Wahitimu wa mambo ya ulimbwende na saluni wakijimwanyamwaya uwanjani wakati wa mahafali hayo 
Ilibidi wengine kuvua viatu ili kuufaidi muziki
Wahitimu wa ulimbwende na saluni wakiwa katika mahafali hayo
Wahitimu wa Katibu Muhtasi wakiwa kwenye mahafali hayo. 
Mapolisi wa usalama  barabarani , Joseph Mgeri na Anthony Ichuragiza, wakiwa na vyeti vayao walivyotunukiwa kwa kufuzu mafunzo ya ukaguzi magari katika mahafali hayo 
Wahitimu wa mafunzo ya udereva wa magari makubwa nao hawa hapa 
Waandishi wakipata press release ya shughuli hizo za mahafali

NAIBU WA MAJI AKAGUA MIUNDOMBINU YA MAJI MTONI, TMK

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Injinia Gerson Lwinge(kushoto) akipatiwa maelezo kutoka kwa Meneja mtambo wa maji wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco),  Masoud Omari, kuhusu hali ya uzalaishaji maji katika mtambo wa maji wa Mtoni, alipotembelea mtamo huo, LEO

NUNDU AWASHUKIA WATUMISHI TPA WANAOTAKA UTAJIRI WA HARAHARAKA KWA NJIA YA RUSHWA

Dec 22, 2010

WAZIRI wa Uchukuzi Omari Rashid Nundu (kushoto) na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi, Athumani Mfutakamba (wapili kushoto), wakimsikiliza kwa makini Meneja  wa Kitengo cha Kuhudumia makontena bandarini (TICTS), Donald Talawa (kulia) akiwaeleza kitengo hicho kinavyofanya kazi zake, alipotembelea kituo cha kitengo hicho, kilichopo Ubungo, Dar es Salaam, jana.
WAZIRI wa Uchukuzi Omari Rashid Nundu (kushoto) akikagua kituo cha kuhuhudumia makontena bandarini cha kampuni ya AMI, alipofanya ziara ya kukagua shughuli zinazohusiana na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Dar es Salaam, jana. Wapili ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Grant Lendrum. 
Mawakala wa kutoa magari bandarini wakitoa dukuduku lao mbele ya waziri Nundu katikaziara hiyo.
====================================

HABARI KAMILI

WAZIRI wa Uchukuzi, Omari Rashid Nundu ametaka mfanyakazi yeyote mwenye lengo la kujipatia utajiri wa haraka ikiwemo kwa njia ya rushwa katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ajitoe haraka katika mamlaka hiyo.


Pia ametaka kufanya hivyo mfanayakazi wa malaka hiyo atakayeona hawezi kwenda na kasi ya sasa ya utendaji kai wenye ufanisi wa hali ya juu anayotaka ambayo ametaka utekelewaji wake uwe umefikiwa katika kipindi cha mizi sita kuania sasa.

Akiunguma jana mjini Dar es Salaam, wakati wa majumuisho ya iuara yake ya sikuy mbili, kukagua shughuli mbalimbali za kazi na utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo, Waziri Nundu alisema kuania sasa ni lazima utendaji wa wafanyakai wa TPA uingatie maadili ya utumishi wa umma na matakwa ya wateja.

"Hii ina maana kwamba mawasiliano na wateja yawe ya haraka sana na yenye tija ya hali ya juu. Utendaji uwe wenye kuzingatia matakwa makuu ya mteja, nayo ni ufanisi wa hali ya juu ndanii ya ajenda moja tu kutoa huduma ya kuendeleza nchi bila masharti ya wazi au yaliyofichika. Vishawishi ni vingi hasa katika kutunuku miradi, hivyo tusishawishike kwa rushwa kutafuta utajiri wa haraka haraka", alisema Wairi Nundu.

Watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanania, wamekuwa wakishutumiwa baadhi yao kujihusisha na rushwa, wizi au upotefu wa vifaa kwenye magari, katika utendaji wao wa kazi, jambo ambalo limedaiwa kuvunja ari kwa baadhi ya nchi kutopitisha sasa mizigo katika badari hapa nchini.

Waziri Nundu ambaye aliambatana ba Naibu Waziri wake, Mhandisi Athumani Mfutakamba, aliwataka wafanyakazi wa TPA, kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM na maelekezo ya viongozi kwa nguvu zao zotena kuchangia kwa dhati kuifanya Tanzania kuwa lango la biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Aliagiza kuanza mara moja kujenga na kuimarisha miundombinu ya bandari kwa kuzingatia mpango mkuu wa TPA, ambao ni dira ya kutekeleza na hatimaye kufukiwa lengo hilo la kuifungua nchi kuwa lango kuu la biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati lengo ambalo alisema bila Tanzania kuwa na bandari zenye ufanisi mkubwa haiwezi kulifikia.

Waziri Nundu aliagiza utekelezaji huo, uanze mara moja kwa matayarisho thabiti na upambe kasi barabara kuanzia mwaka wa fedha wa 2011/2012 na kuwataka wafanyakazi wa TPA kufanya juhudi za makusudi kuhakikisha wate waliozihama bandari za Tanzania wanarudi tena kuzitumia,

"Hii ina maana kwamba jitihada za makusudi kwa kushirikiana na wadau wengine kama TAZARA na TRL zifanywe kwa lengo la kuongeza ufanisi wa mtandao wa uchukuzi nchini na hivyo kuwarudisha wateja hawa ambao ni kutoka Uganda na Zambia" alifafanua waziri Nundu.


Aliagiza kwamba, wakati mkakati wa ujenzi wa bandari ya Mwambani, Tanga, ukiendelea kupangwa, Bandari ya Tanga ipatiwe vifaa ambavyo vitaongeza ufanisi wa matumizi ya bandari hiyo na kwamba vifaa hivyo vinajulikana na havina gharama kubwa na kutaka agizo hilo litekelezwe kabla ya Julai 2011.

Waziri aliitaka TPA kuanza mawasiliano na uongozi wa mkoa wa Tanga, ili maeneo ndani na nje ya bandari ambayo yanatumika kwa shughuli zisizo za kibandari zichukukliwe na kumilikishwa Mamlaka hiyo na maeneo ya bandari yaliyokwishachukuliwa yapatiwe hati miliki kuondoa uwezekano wa kuvamiwa na wananchi, na kuwa maeneo hayo ni yapo Mwambani Tanga na Mtwara.


Aliagiza pia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa eneo la Kisarawe kwa ajili ya matumizi ya kuhifadhi mzigo ufanyike mara moja hata kama ni kwa gharama za serikali na kama haitawezekana kabla ya mwaka wa fedha wa 2010/2011 eneo taratibu zifanywe ili limilkikiwe na serikali kuoitia TPA.


Katika ziara hiyo, jana Waziri Nundu alikagua vituo vya bandari za nchi kavu vya kuhifadhi makontena na vya magari kutoka bandarini, vilivyopo Kurasini, Chang'mbe na kimoja kipya kilichopo eneo la Gerezani, ambacho kitaanza kazi Januari mwakani.

Kwenye vituo hivyo, Upandishwani wa gharama za kutoa magari kwa mbinu mbalimbali ikiwemo maofisa kuchelewesha kwa makusudi kutoa vibali kwa muda unaotakiwa na badala yake kutoa vibali hivyo baada ya siku zinazowalazimu wahusika kulipia pia gharama za utunzaji magari.

Wateja ambao waziri aliwakuta kituo cha Farion Trading Limited, walimwambia Waziri kwamba baadhi ya maofisa kwenye kampuni hiyo wamekuwa wakifanya ucheleweshaji wa makusudi kutoa vibali, jambo ambalo huwalazimu kulipia gharama zaidi.

NDEGE YAPATA AJALI MBEYA

Dec 19, 2010

.

PIX-3.

(Picha zote na Solomon Mwansele).
Watu wakitazama ndege ya  CESSNA, 5H-PCN- U206 F, baada ya kuanguka leo  katika shamba la Taasisi ya Kilimo Uyole,  mjini Mbeya. Katika ndege hiyo  Iliyokuwa inamsafirisha mgonjwa kutoka Mbeya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa matibabu zaidi, daktari wa hospitali ya Rufani Mbeya, Jones Chitemo, aliyekuwemo amevunjika mkono . 
Ndege hiyo kwa mbele

FAMILIY DAY YA UHURU PUBLICATIONS LTD YAFUNIKA NDEGE BEACH DAR

FAMILIA ZIKAKAA KWA KUJINAFASI, KILA MOJA MEZA MOJA=====================================
BAADAYE FAMILIA ZIKAENDA UFUKWENI MWA BAHARI KUFANYA MICHEZO MBALIMBALI 

Mpira wa miguu


================================
RIADHA MITA 100 
   
ยช