.

KILIMANMARATHON YATIMUA VUMBI LEO MKOANI KILIMANJARO

Feb 28, 2010

Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini Musa Samizi wa pili toka kushoto akimpatia zawadi yake mshindi wa kwanza wa mbio za kujifurahisha za 5 kilometa Vodacom Fun run Bw.Wilbrodi Kidaga aliyejinyakulia simu ya mkononi pamoja na muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi elfu 60 pamoja na fedha alizopewa kwa njia ya M pesa shilingi Elfu 70,Kushoto katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Filbati Bayi,katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru.
NAIBU Waziri wa Habari na Michezo Joel Bendera na Mkurugenzi Mkuu wa wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Nector Foya kushoto wakiwa tayari kwa kuanza mbio za 5 kilometa Vodacom Fun run zilizofanyika mjini Moshi leo.Baadhi ya washiriki wa mbio za 5 kilometa Vodacom Fun Run wakihudhuria mbio hizoBaadhi ya wanariasha walioshiriki mbio hizo
Wanariadha wakiwa katika mbio hizo za kujifurahisha za 5 kilometa Vodacom fun run

JK AONGOZA MAZISHI YA BALOZI MWAKAWAGO DAR

Feb 27, 2010

RAIS Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein na viongozi wengine waandamizi katika maziko ya Balozi Mwakawago kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo jioni.
Mwili wa marehemu, Balozi Mwakawago ukizikwa katika kaburi wakati wa mazishi hayo.
RAIS Jakaya Kikwete akimwaga udongo kaburini
 
RAIS mstaa Benjamini Mkapa akifuatia
Rais wa awamu ya pili, Ali Hassani Mwinyi naye akimwaga udongo kumzika Mwakawago.
Stori
RAIS jakaya Kikwete leo amewaongoza mamia ya wananchi kumzika aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Daudi Nwakawago ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 71.
Balozi Mwakawago aliyefariki juzi, amezikwa leo jioni kwenye makaburi ya Kisutu Dar es Salaam, ambako Mbali na wananchi wa kawaida viongozi mbalimbali wakiwemo Marais wastaafu, Ali Hassani Mwinyi na Benjamin William Mkapa walikuwepo.
Kadhalika Mawaziri Wakuu Joseph Warioba na Dk Salim Ahmed Salim.
Marehemu, Mwakawago  ameacha mjane na watoto watatu huku akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi kwenye baraza la mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili  na kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

 

HITMA YA MAREHEMU MZEE KAWAWA YASOMWA KITAIFA LEO

RAIS Jakaya Kikwete akishiriki Hitma ya kitaifa ya Mmoja wa waasisi wa Taifa, marehemu Rashid Kawawa, iliyosomwa nyumbani kwa marehemu, Madale Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa akisoma dua na kulia ni Vita Kawawa, mtoto wa marehemu. Kina mama wakiwa kwenye hitma hiyoWatoto wasliohudhuria wakipata chakula kwenye hitma hiyo.

Story
RAIS Jakaya Kikwete leo ameongoza viongozi, ndugu jamaa na Marafiki katika hitma ya 40 ya Mzee Rashidi Kawawa, nyumbani kwa marehemu, Madake nje ya jiji la Dar es salaam.
Kisomo cha hitma hiyo kiliongozwa na sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Malima na mtoto wa Marehemu, Vita Kawawa.
Kwa mujibu wa Vita, leo ndiyo siku ambayo simba wa Vita, alizawaliwa yaani  tarehe Februari 27, mwaka 1926. na pia imekuwa siku maalum zaidi kwa kuwa leo pia ni siku aliyozaliwa Mtume Muhammad (SAW) ambapo shamrashamra zilitawala Duniani kote kwa kusomwea Maulid usiku wa kuamkia leo.
Mzee Kawawa alifariki Dunia Desemba 31, mwaka 2009 mjini Dar es Salaa. Hitma yake ilikuwa awali isomwe Februari 16, mwaka huu, ikaahirishwa kwa kufuatia kifo cha Binti wa Mzee Kawawa  

MKESHA WA MAULID USIKU WA KUAMKIA LEO

SHEIKH wa njia wa Dar es Salaam, Alhad Mussa akimkaribisha Mwanazuoni na Mnajimu maarufu. Sheikh Hussein Yahya kwenye Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam, usiku wa kuamkia leo.Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam,  Alhad Mussa akitoa mawaidha kwenye Maulidi hayo.Baadhi ya viongozi mashuhuri waliohudhuria Maulidi hayo
Sheikh Yahya Hussein akisoma Quran tukufu ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Maulidi hayo yaliyofanyika viwanja vya Manazi Mmoja Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Sheikh Mohamed Khamis akisoma mlango wa kwanza . Kichwani ni noti ya sh. 500 aliyotuzwa na waumini waliovutiwa na sauti yake katika kughani
Mmoja wa waumini akiwa ametulia na mtoto wake katikamaulidi hayo
Kina mama wakiwa kwenye Maulidi hayo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.

RAIS KIKWETE ATOA POLE KWA FAMILIA YA BALOZI MWAKAWAGO

Feb 26, 2010

RAIS Jakaya Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mwanadiplomasia, marehemu Daudi Mwakawago, Msasani Dar es Salaam, leo.
RAIS Kikwete akimfariji Daisy Mwakawago, Mjane wa Marehemu Balozi Mwakawago, Msasani Dar es Salaam, leo, Mwakawago alifariki juzi.

JOTI WA ORIJINO KOMEDI BADO AMELAZWA MUHIMBILI

AZUNGUMZIA HALI YA KE, ASEMA HAJAMBO
MSANII wa Orijino Komedi, Lucas Mhuvile 'Joti' aliyeumia shigo na kupata michubuko kadhaa mikononi, wakati akiwa kazini hivi karibuni, akijuliwa hali na jamaa zake, wodini alikolazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Muhimbili, Dar es Salaam. Kuhusu hali yake msanii huyo alimwambia mpigapicha Wetu kwamba anaendelea vema.

ALAN 'MASSAWE' TURNER WA EXECUTIVE SOLUTIUON AOMBOLEZWA

MWANAMUZIKI wa kujitegemea Mark Townsend, akiimba wimbo wa 'candle in the wind' katika hafla ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution, Alan 'Massawe' Turner, juzi, mjini Dar es salaam.

KESHO NI SIKUKUU YA MAULID

KIJANA A akishiriki maandamano maalum  (Dhafaa) ya kukaribisha Sikukuu ya Maulid, jana yaliyoandaliwa na Waislamu mjini Dar es Salaam.
 Waislamu wakiwa katika matembezi wa Kumbukumbu ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), ambayo huadhimishwa kwa sherehe za Maulidi. sherehge hizo zinaanza kwa mkesha usiku wa kuamkia kesho.

NAPE AIPIGA JEKI UHURU FC

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa jozi moja ya jezi, Katibu wa CCM Tawi la Uhuru Publications Ltd (UPL), wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Abubakar Muna jana, mjini Dar es Salaam, kwa ajili ya timu ya soka ya Uhuru FC inayojiandaa kushiriki michuano ya NSSF itakayoanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao. Wapili kushoto ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) tawi la UPL, Sophia Ashery na Nahodha Uhuru FC, Mussa Hassani

KATONI 13,036 ZA ALYWAS FEKI ZA MILIONI 1295.54 ZATEKETEZWA DAR

Alyws bandia

Vijana wakizisambaza katoni za pedi  bandia tayarai kuzichoma

Always bandia zikiteketea kwa moto

                                                                      Story
TUME ya Ushindani Nchini (FCC), imeteketeza katoni 13,036 za Pedi feki za sh. Milioni 195.5, leo kwenye dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam.
     Akizungumza na waandishi wa habari, ofisa uhusiano wa FCC, Frank Mdimi alisema Pedi hizo zimekamatwa katika miji ya Arusha na Dar es Salaam. kati ya Januari na Februari, mwaka huu na zinatoka nchini China kwa kuingizwa nchini na wafanyabiashara watano aliowataja kuwa ni  Mazeh Meghji ambaye alikamatwa na katomi 2,882, za sh. milioni 43.2, Elibariki Mollel katoni 1,221, za sh. Milioni 16.8, Gabriel Massawe katoni 253 za sh. Milioni 3.7.
    Wengine ni Ally Gulamali, katoni 570 za sh. Milioni 8.5, wote kutoka Dar es Salaam na Paulo Lema kutoka Arusha ambaye alikamatwa na katoni 8,110 za sh. Milioni 121.6.
    Mdimi alisema Pedi hizo zina madhara mengi kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kusababisha ukurutu au fangasi sehemu za siri.
    Aliwaomba wananchi kuwa makini wanaponunua bidhaa na iwapo wata kuwa na wasiwasi na bidhaa yoyote watoe taarifa kwenye vyombo vinavyo husika.
          Mdimi alisema jukumu la kukamata na kuwafichua waingizaji wa bidhaa bandi si la FCC pekee bali linahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali.

MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA NA VIKOSI WAAGIZWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI

Feb 25, 2010

BAADA ya minong'ono iliyokuwa ikipozwa kwa maneno ya hapoa na pale, hayimaye Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umetangaza kumng'oa madarakani Katibu Mkuu wake, Hasna Mnwilima kwa kileichodaaiwa  ni mdhaifu katika utendaji kazi.
Taarifa ya UWT iliyopatikana leo imeeleza kwamba  Mwenyekiti wa CCM, Rais jakaya Kikwete hahusiki na kung'olewa uongozi kwa Mwilima, na wanaoeneza uvumi huo wanakwenda kinyume na ukweli halisi.
Kung'plewea kwa Hasna kulitangazwa rasmi leo na Makamu wa UWT (Zanzibar) Asaha Bakari Makame na kusema nafasi inakaimiwa na Naibu Katibu Mkuu (Bara) Amina Makilagi.
Alsema Hasna amevuliwa uongozi katika kikao cha Baraza Kuu la UWT kilichofanyika Novemba 17, 2010 mjini Dodoma.

ILE HITMA YA KITAIFA YA SIMBA WA VITA KESHO

Tangazo la familia ya Mzee Rashid Kawawa 'Simba wa Viuta' aliyefariki dunia Desemba 31, 2009. mjini Dar es Salaam.

LIGI KUU YA VODA, SIMBA YASHINDWA KUITAMBIA AFRICA LYON LEO

Feb 24, 2010

BEKI wa African Lyon Hamis Shengo (kushoto) akikabiliana na mshambuliaji wa Simba, Ulimboka Mwakingwe, timu hizo zilipocheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, leo kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka suluhu ya bao 1-1.

TASWIRA KATIKA JAMII

HILI ni tangazo katika daladala linalofanya kazi kati ya Muhimbili na Buguruni jijini Dar es Salaam, lisome vizuri mdau halafu toa msaada tujue nini maana hasa ya tangazo hilo
Kijana akiwa amelala chini ya mti leo mchana karibu na jengo la Maktaba Dar es Salaam. Swali lakujiuliza ni je nini hatma ya mtu huyu katika taifa?
FUNDI cherehena akilazimika kupunga usingizi kidooogo katika eneo lake la kazi lililopo maeneo ya Kisutu Dar es Salaam, leo. Jea hali hii ni kutokana na uchovu wa kazi au uhaba wa wateja?

KWA WAVUTA SIGARA TU!

HIZI ndizo athari ziukutao mwili wa mpenda sigara maarufu kama tumbaku au fegi
new

MENGI ALIA WALEMAVU KUNYANYASWA KWA UVUMI

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Reginarl Mengi
Reginard Mengi

STORI
UVUMI ulionezwa jijini Dar es Salaam, kuhusu mwanamke kuota manyoa baada ya kumpa msaada mlemavu, umeelezwa kuwaathiri walemavu.
Hayo yalisemwa na Mwenkiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi katika mkutnao wake na waandishi wa habari, jana mjini Dar es Salaam.
     Mengi alisema, uchunguzi aliofanya tangu uvumi huo ulipoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari na watu mbalimbali, jijini walemavu kadhaa wamekosa amani na kutoweka katika maeneo walikokuwa wakikaa kusubiri misaada kwa wapitanjia.
     Alisema, mbali na kuwaweka katika mazingira magumu ombaomba wanaoendesha maisha yao kwa njia hiyo, hata wengine wenye ulemavu ambao hawaishi kwa kuomba omba wameonekana kudhalilika kutokana na uvumi huo.
       Mengi alisema, wenye ulemavu sasa wanajisikia kama tabaka lingine la binadamau kwa kuwa uvumi huo umewafanya kuonekana kama mlemavu ni aina fulani ya jinamizi au jini jambo ambalo ni hatari.
      Alisema, kama uvumi huo ulilenga kutaka wenye ulemavu wajitegemee imekuwa kinyume, kwa sababu sasa hata wale waliokuwa na shughuli zao ndogo ndogo za kuwaingizia kipato kama kuuza vocha za simu na wanakosa wateja kwa sababu yakihofiwa kuwa siyo watu wa kawaida.
     Aliviomba vyombo vya habari vilivyosaidia kuenea uvumi huo, kutumia nguvu ilele ile au zaidi kuielimisha jamii kuwa jambo hilo halikuwa kweli na bado walemavu ni sehemu ya jamii.
     Wiki iliyopita, ulisambaa uvumi katika jiji la Dar e Salaam na viunga vyake, kwamba kulikuwa na mwanamke ambaye aliposimamisha gari lake kusubiri taa, alimpa fedha ombaomba eneo la Selander Bridge, na ghafla akaota manyoa mkononi.


YANGA YAKOMAA KWA ZESCO YA ZAMBIA ZATOKA SARE YA 1-1

Feb 23, 2010

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Steven Bengo akijaribu kumtoka beki wa Zesco ya Zambia Clive Hachilensa, timu hizo zilipocheza mechi ya kirafiki ya Kimataifa katika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, leo. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

AKUDO KUPAKUA ALBAMU YA 'HISTORY NO CHANGE'


Christian Bella, Rais wa Akudo Impact

WANAMUZIKI ambao ni waimbaji wapaya wa Akudo Impact
STORI
BAADA ya kutamba na albamu ya kwanza  ya Impact mwaka juzi na mwaka leo, bendi ya Akudo Impanct imesema imeandaa albamu ya pili ambayo imedai itakuwa mto wa kuopteaa mbali kuliko ya kwanza.
    Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Miuchael Loki alisema, nyimbo mbili  kati ya nane zitakazokuwa katika albamu hiyo zimekamilika.alisema, albamu hiyo ambayo imepewa
jina la 'History no Change'itaakuwa mitaani na katika vituo vya radio na televisheni hivi hivi karibuni.
    Rais wa bendi hiyto Christian Bella, alitaja nyimbo zilizopo tayari kuwa ni aliotunga wa 'Pongenzi kwa wenye ndoa' na 'ubinafsi uliotungwa na Tarsisi Masela.
    Alisema, nyimbo nyinginebado ni siri ukiwemo History No Change ambao umebeba albamu hiyo aliosema kwamba hangeweza kutaja mistari yake kwa waandishi wa habari kwa kuwa nfiyo silaha itakayomtoa nyoka pangoni. Bella alitamba kwamba pamoja na kwamba albamu ya Impact haikutumika sana kuingiza pato la bendi hiyo katika mauzo lakini ilifanya kazi kubwa ya kuifanya bendi ishike kwa wamashabiki.
    Alisema kazi ya albamu mpya itakuwa ile ile ya kuiweka juu Akudo na kuifanya izidi kupendwa zaidi na
zaidi na mashabiki. Bella alisema, pamoja na katika kufyatua albamu hiyo mpya, Akudo pia imeleta waimbaji wapya watatu kutola Jamhuri ya Kimokrasi ya Congo aliowataja kuwa ni Kabaston Mwanamulenda, Alain Frapa na Fredy Panzu.
    Albamu ya Impact ilikuwa na nyimbo kadhaa lakini ulioonyesha kutia fora ni 'Yako wapi Mapenzi' uliotungwa na Bella.

MSAJILI WA MAGAZETI ATEMBELEA OFISI ZA UHURU, MZALENDO NA BURUDANI LEO

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Josiah Mufungo (kushoto) akimwonyesha Maktaba ya UPL, Mkurugenzi Msaidizi na Msajili wa Magazeti wa Idara ya Habari (Maelezo) wa pili (Kushoto)  Raphael Hokororo alietembelea Ofisi hiyo kwa ajili ya kujifunza,na wa pili((Kulia) ni Msajili Msaidizi wa Idara ya Habari Ndugu Ismail Ngayonga,aliefutana nae.Na wa kwanza (Kulia) ni Mkutubi wa Maktaba hiyo ndugu Mussa Hassan akielezea kitu kwa Mkurugenzi huyo leo jijini Dar.Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd,  Josiah Mufungo akiwa Ofisi kwake ( Kulia) wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi msaidizi na Msajili wa Magazeti wa Idara ya Habari (Maelezo) wa (kwanza) jinsi Ofisi yake inavyofanya kazi ,Mkurugenzi huyo alienda kujifunza na kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Gazeti la Uhuru .Na wa pili (kulia) ni Msajili Msaidizi wa Idara ya Habari Ndugu Ismail Ngayonga aliefuatana na Mkurugenzi huyo

LIGI KUU YA VODA; YANGA YAINYUKA TOTO AFRICA SITA BILA!

Feb 22, 2010

MSHAMBULIAJI wa Yanga Jerry Tegete akijaribu kumtoka mlinzi wa Toto Africa Philimon Mwendasile, timu hizo zilipocheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, jana. Toto ilinyukwa mabao 6-0. (Picha kwa Hisani ya Mdau wa Chachandu Daily)

NI UZEMBE AU?

WATU wakihangaika kilikwamua gari  baada ya dereva kuliingiza mtaroni katika mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, leo

MSEKWA AKUTANA NA BALOZI WA CUBA LEO

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa akimkaribisha Balozi wa Cuba nchini, Ernesto Gomez Diaz katika ofisi Ndogoi ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Balozi Diaz akieleza jambo katika mazungumzo yake na Msekwa leo
Balozi Diaz akimkabidhi mwaliko wa viongozi wa CCM wa ngazi za juu kwenda kutembelea Cuba, wakati wa mazungumzo hayo.
ยช