.

TATIANA IN ZE TOWN

Mar 31, 2010


BALOZIi wa ugojwa wa Matende (ELEPHANTIASIS DISEASE) kwa nchi za Mashariki na Afirica ya kati (Ambassador for Elephantiasis disease in East and Central Africa) ambae pia ni Mshindi wa BBA2 Tatiana Durao kutoka Angola , leo jijini Dar es Salaam amezungumza na wandishi wa habari kuhusu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Machi 31, 2010 pamoja na hilo atafanya ziara fupi katika kisiwa cha Unguja pamoja na kuwasaidia watoto wa KIWOHEDE wa jijini Dar es Salaam.Pichani akiwa katika picha ya pamoja na Msaidizi wake Ebmenalda Antonio (kulia) na (kushoto) Mmiliki wa Kampuni ya Truemedia mzaliwa wa Uganda Alice Mutumba. (miwani) Picha na Mwanakombo Jumaa-MALEZO.


MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA MAXIMO UMEIVA, 59 WAJIOTOKEZA KUOMBA ULAYA WAKIONGOZA.

NCHI za Ulaya zimeongoza katika kuwa na waombaji wengi kati ya waliojitokeza kuwania kazi ya ukocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars ambayo iliyotangazwa hivi karibuni na Shirikisho la Soka Tanzania TFF).  
    Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi uliopo jengo la Millenium Tower, Kijitonyama, Dar es Salaam, Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema, maombi kutoka nchi za Ulaya  ni  zaidi ya nusu ya maombi yote ambayo alisema ni  59.
   Tenga alisema, wakati Ulaya ikiongoza kwa kuwasilisha waombaji  48, waliojitokeza Tanzania ni watatu ukiacha mmoja ambaye aliomba ukocha msaidizi, nafasi ambayo Tenga alisema hakuna.
    Alitaja nchi nyingine ambazo raia wake wametuma maombo kusaka nafasi hiyo kuwa ni Kenya, Cameroon na Ghana ambazo ameomba mmoja kila nchi,  Mataifa ya Asia bila kutaja nchi kwa ujumla wameomba watatu na Amerika ya Kusini ikiwa imetoa wawili.
    Tenga alisema, kwa sasa TFF haitataja wagombea hao, lakini alieleza kuwa wengi wa alioomba nafasi hiyo ni wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya soka na kwamba mchakato safari hii utakuwa rahisi kutokana na kujitokeza idadi kubwa ikilinganishwa na mchakato uliopita ambao walikuwa watatu tu.
     Alisema, kumiminika kwa idadi ya maombi kutaka kuinoa Stars inamaanisha kwamba Tanzania ipo kwenye chati nzuri na yenye kujulikana zaidi kisoka kuliko miaka iliyopita, kazi ambayo alisema imefikiwa kutokana na utendaji wa viongozi mbalimbali wa usimamizi wa mchezo huo nchini ikiwemo TFF.
    Tenga alisema, hadi sasa tayari sekretairieti imeshafanya mchakato wake  kuhakikisha wanaoitwa kweneye kinyang'anyiro ni idadi ile yenye waombaji wenye sifa za uhakika na si wale walioomba kwa ajili ya kubahatisha tu huku wakijijua hawana sifa za kitaaluma ukiachilia mbali uozefu ambao alisema wengi wanao.
    Alisema, utaratibu uliowekwa unailelekeza TFF kuwa anayestahili kuionoa Stars lazima awe na kiwango cha elimu ya sekondari, lakini pia awe na cheti cha ngazi ya  diploma ya mafunzo ya ukocha na siyo vyeti vingine kama vya Saikolojia na mazoezi ya viungo tu na kusema kuwa wengi wa waombaji wanazo diploma.
    Tenga alisema wenye sifa hizo wameshapatikana na awamu iliyofuata ilikuwa kuwatumia maswali ambayo waombaji watatakiwa wawe wameshaleta majibu yao TFF kabla ya Aprili 15, 2010.
   Alitaja maswali waliyotumiwa kuwa ni yanayolenga kujua mambo kadhaa kama mwombajianafanya kazi wapi kwa sasa, atapatikana lini akikubaliwa na kiwango cha mshahara anachotaka awe analipwa.
   Tenga alisema baada ya majibu kuletwa, Kamati itakaa kujadili waliopatikana.
Nafasi ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars imetangazwa kuwa wazi kufuatia kocha mkuu wa sasa Mbazil, Marcio Maximo kukaribia kumaliza mkataba wake.
  Wakati huohuo, Tenga amezungumzia hatua ya kukamatwa na hivi karibuni Mhasibu wa Yanga kwa tuhuma za kuuza tiketi bandia, kwamba anaunga mkono hatua hiyo na kusema, ni hatua ambayo inaendelea kuifanya medani ya soka hapa nchini iheshimiwe.
     Tenga alisema,  nia ya TFF ni kuhakikisha kila jambo linakwenda kwa uwazi hasa la masuala ya fedha kwa sababu kinyume chake wajanja wanaweza kutumia nafasi hiyo kufanya wizi na kusababisha heshima ya soka iliyopo sasa nchini ishuke.
     Alisema, tangu aingine madarakani, amekuwa akisisitiza uwazi katika masuala ya fedha, jambo alilodai kwamba limefanikiwa na ndiyo hadi sasa wadhamini hawasiti kusaidia masuala ya soka katika maeneo mbalimbali.
     Katika mkutano huo, wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na Benki ya NMB wanaodhamini soka katika maeneo mbalimbali walikuwepo ambapo waliahidi kuendelea kuisadia TFF na soka kwa jumla hapa nchini.
    " kwa kweli sisi Serengeti na wenzetu NMB bado tunaridhishwa na hali ya usimamizi wa fedha ulivyo, hivyo tunaahidi kuwa tutaendeleza udhamini wetu kadri mikataba na yele yaliyo nje ya mikataba yatakavyokuwa na umuhimu", alisema Meneja Mkuu, Habari, Mawasiliano na Mahusiano na Jamii Teddy Mapunda
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga akifurahia jambo alipozungumza na Waandishi wa Habari leo kwenye jengo la Millenium Tower, Kijitonyama, Dar es Salaam.
    .
RAIS wa TTF Leodegar Tenga akizungumza na waandishi wa habari leo katika jengo la Millenium, Kijitonyama, Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela.RAIS wa TTF Leodegar Tenga akizungumza na waandishi wa habari leo katika jengo la Millenium, Kijitonyama, Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela.RAIS wa TTF Leodegar Tenga akizungumza na waandishi wa habari leo katika jengo la Millenium, Kijitonyama, Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela na kushoto ni Meneja Mkuu, Habari, Mawasiliano na Mahusiano ya Jamii wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda.

KILI TAIFA CUP YAZINDULIWA LEO, KUANZA KUTIMUA VUMBI MEI

Mar 30, 2010

MICHUANO ya soka ya Kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup' mwaka huu itashirikisha pia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 (U20).
   Hayo yalisemwa jana mjini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela katika uzinduzi rasmi wa mashindano hayo,kwenye Klab ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni wadhamini kupitia bia yake ya Kilimanjaro.
   Alisema wanatakaounda timu ya U20 itakayoshiriki michuano hiyo ni vijana waliovuka umri wa miaka 18, na kwamba timu hiyo inashiriki kama mchagizaji tu kwa kuwa hata ikiibuka kuwa mshindi wa kwanza haitazawadiwa.
   "mwaka huu tumeamua kushirikisha timu hii (U2) kuwezesha timu hii kujiandaa na michuano ya kimataifa ijayo,na ikiwa wataibuka na ushindi timu itakayokuwa ya pili dhidi ya tumu hiyo ndiyo itakapata zawadi ya mshindi wa kwanza", alisema Mwakalebela.
   Alisema, mashindano yatanza Mei 8 na zitashirikishwa timu 24 zitakazocheza katika vituo sita abapo kila timu itacheza na mwenzake kwenye ngazi za mzinguko kisha zitakazopata poiti nyingi zaidi zitaingia kwenye hatua ya robo fainali.
   Mwakalebela alivitaja vituo sita zitakakorindima mechi hizo kuwa ni Mtwara, Arusha, Dodoma, Tanga, Iringa na Shinyanga na kuwamba robo fainali zitachezwa Mei 22, 2010 na fainali zitakuwa Mei 30,2010.
   Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni bia Tanzania (TBL) David Minja alisema, TBL imedhamini michuano hiyo kwa gharama ya sh. milioni 850, tangu maandalizi ya timu hadi zawadi za washindi.
  "Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Kilimanjaro Premium Lager, moja ya aina za bia za TBL kudhamini mashindano haya yanayosaidia kung'amua na kukuza vupaji mbalimbali kuanzia ngazi za chini hadi timu ya taifa", alisema Minja.
   Alisema, zawadi katika kwa washindi wa michuano huyo zitakuwa nono,lakini akasema ni mapema kutaja viwango vyake.
    Minja alisema mashindano ya mwaka huu yanafanyika kwa dhima ya kufikisha Tanzania kwenye kilele cha mafanikio katika medali ya mchezo wa soka.
MENEJA Masoko wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL), David Minja (wapili Kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela wakizindua  mashindano ya  Kombe la Taifa (Kili Taifa Cup), leo kwenye Klab ya TBL, Ilala, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe na kulia ni Ofisa Habari wa TFF Florian Kaijage.
  

FRED MPENDAZOE AZOLEWA NA CCJ

ALIYEKUWA Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya CCM, Fred Mpendazoe akizungumza na waandishi wa habari leo katika
ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dar es Salaam,  akitangaza kuondoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ). Kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi wa Udara ya Habari (Maelezo) Sise Mwirabi  na kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCJ, Dickson Nghilily. Mpendazoe akichekelea wakati akitoka kutangaza uamuzi wake huo, katika ukumbi wa Idara ya Habari leo.

JK AKABIDHIWA MISAADA NA WACHINA

RAIS Jakaya Kikwete, akipanda pikipiki aliyokabidhiwa na Balozi wa China nchini, Liu Xingshen (kushoto), Ikulu, mjini Dar es Salaam, leo ambayo ni moja ya bidhaa zenye thamani ya sh. milioni 51, zikiwemo baiskeli na vyerehani, zilizotolewa msaada na nchi hiyo kusaidia sekta mbalimbali.
RAIS Jakaya Kikwete, akiangalia mmoja wa mipira aliyokabidhiwa na balozi wa China nchini, Liu Xinsheng (kushoto) katika hafla iliyofanyika jana, Ikulu, mjini Dar es Salaam. chjo

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ZIARANI VIETNAM

PINDA akimtambulisha, Waziri wa Kilimo na Chakula , Stephen Wasira pamoja na wajumbe wa msafara wake kwa Waziri Mkuu wa Vietnam, Nguyen Tan Dung wakati wa mapokezi hayo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Iddi. WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, akikagua gwaride. WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Vietnam, Nguyen Tan Dung, wakipokea heshima kutoka kwa kamanda wa gwaride maalumu la mapokezi yake, Ikulu ya nchi hiyo mjini Honoi kuanza ziara ya kikazi nchini humo. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu).WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, akipokea zawadi ya maua alipowasili katika viwanja vya Ikulu ya Hanoi, nchini Vietnam, jana kuanza ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Vietnam, Nguyen Tan Dung.MNEC-CCM AWAPA WAZAZI OFA YA PUNGUZO 40% KUSOMESHA WATOTO SHULE YAKE YA ST. ANNE MARIE

Mar 28, 2010

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Jason Rweikiza akifungua ofisi ya CCM tawi la Msingwa, Kata ya Mbezi Dar es Salaam, jana. Rweikiza alitoa pia mchango wa sh. 500,000 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa ofisi hiyo.Rweikiza na viuongozi wa Kata ya Mbezi wakisalimia wanachama wakati wa sherehe hiyo ambayo iliambatana na kukabidhiwa bendera ya Chama Wajumbe 15 wa CCM waliochaguliwa hivi kiaribuni na katika kata hiyo.MWENYEKITI wa CCM Kata hiyo,  Amir Majembe akimvisha mkanda maalum Rweikiza ambao alipewa kwa hehima ya wazee wa Mbezi Deo Ndunguru (wapili kulia) na Juma Nkangaa.(kulia)Rweikiza akimkabidhi bendera ya CCM Mjumbe wa shina namba 13, Mussa Geuza, mmoja kati ya wajumbe 15 wa CCM katika kata hiyo ambao aliawakabidhi bendera hizo kufuatia kuchaguliwa kwao hivi karibuni.Rweikiza akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wazee wa Kata ya Mbezi baada ya kupewa heshimakwa kupewa mkuki wa kukihami Chama.MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Jason Rweikiza akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe 15 wa CCM, baada ya kuwakabidhi bendera za Chama, katika hafla iliyofanyika jana, katika kata ya Mbezi, Dar es Salaam.
Habari Kamili
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Jason Rweikiza ametoa punguzo aslimia 40 kwa kila mkazi wa Kata ya Msingwa, Mbezi, Dar es Salaam, atakayepeleaka mototo katika shule yake ya St. Anne Marie iliyopo eneo hilola Kimara.

     Rweikiza alitoa ‘ofa’ hizo, baada ya kufungua Ofisi ya CCM tawi la Msingwa katika hafla iliyoambatana na kuwakabidhi bendera za CCM wajumbe 15 wa mashina ya CCM waliochaguliwa katika wa kata hiyo.
    "kutokana na kwamba nimekuwa eneo hili na kufanya shughuli zangu hapa na wengi wenu hapani wana-CCM wenzangu, natoa ofa ya punguzo la asilimia 40 ya ada, kwa mzazi wa hapa atakayeleta mototo wake kwenye shule yangu ya St. Anne Marie iliyopo hapa Mbezi”, alisema Rweikiza.
     Shule hiyo ya St Anne Marie, inatoa masomo ya shule za awali, msingi, sekondari hadi kidato cha sita.
Pia aliahidi kutoa mchango wa sh. 500,000 kwa ajili yak umalizia ujenzi wa ofisi ya CCM aliyofungua, na kueleza kwamba ofa la punguzo la ada na msaada wa fedha hizo hatoi kwa sababu ya maadalizi ya kugombea ubunge kwa kuwa hana nia ya kuwania nafasi hiyo.
      Rweikiza aliwataka wanachama wa CCM kulitumia tawi hilokuzingumza mambo muhimu ya ujenzi wa Chama kwa kufanya vikaovyote vya chama kwamujibu wa Katiba.

SIKU MAKAMBA ALIPOJIANDIKISHA UPYA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGAKURA, WAZO

Alianza hivi....
Katibu Mkuu wa CCM Yussuf Makamba akijiandisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwenye kituo cha Wazo A, karibu na nyumbani kwake, Tegeta Dar es Salaam, jana. Awali alikuwa amejiandikisha kituo cha Bunge jijini wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.Makamba akitia dole gumba baada ya kujiandikisha kwenye daftari hilo.Baadaye alienda nyumbani kwake baada ya kujiandiksia ambapo aliwaonyesha wadau shughuli zake za ufugaji.KATIBU Mkuu Yusuff Makamba akimlisha nyanya kasuku ambaye ni moja ya mifugo aliyonayo nyumbani kwake, Wazo Kisanga, Wazo, Tegeta, Dar es Salaam.
Halafu akakutana na mwane Yusuf   BU Mkuu wa CCM Yuissuf Makamba akimvisha tai mwane, Yussuf (13) aliyewasili nyumbanKATIi akitokea shuleni
SIKU HIYO HIYO AKAVISHWA NISHANI NA UVCCM KWA KUTOA MCHANGO MKUBWA KWA JUMUIA HIYO
KATIBU Mkuu wa CCM Yussuf  Makamba akivishwa nishani na Katibu Mkuu wa Imoja wa Vijana wa CCM,  Martine Shigella kwa ajili ya kutambua mchango Makamba katika kuiimarisha UVCCM, hafla hiyo iliyoambatana na kusimika makamana wa Umoja wa Vijana ilifanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni Dar es Salaam.

AJALI NYINGINE KATIKA ENEO LILE LILE LILILOTEKETEZA ROHO ZA WATU KUMI KIBAMBA JUZI

Mar 27, 2010

WATU wakimsaidia abiria katika basi dogo aina ya Isuzu ambaye alipoteza fahamu baada ya basi hilo kukwanguliwa rishani na loro ambalo lilitokweka katika eneo la Kibamba, pale ambako watu kumi walikufa papo hapo baada ya hiace kuangukiwa na lori la mafuta.WATU wakimsaidia abiria katika basi dogo aina ya Isuzu ambaye alipoteza fahamu baada ya basi hilo kukwanguliwa rishani na loro ambalo lilitokweka katika eneo la Kibamba, pale amko watu kumi walikufa papo hapo baada ya hiace kuangukiwa na lori la mafuta. Sehemu iya vioo vilivyovunjika katika eneo alilokuwa mekaa mwanamke huyo katika basio dodo lenye namba  T 155 AKC

SERENGETI YAIPA STARS MILIONI 50 KWA AJILI YA MECHI YAKE NA SOMALIA

Mar 26, 2010

OFISA Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya bia ya Serengeti(SBL), Imani Lwiga akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 50 Katibu Mkuu wa Shirikishola Soka Tanzania (TFF), David Mwakalebela, kwa ajili ya timu ya taifa, Taifa Stars, ambayo inashuka dimbani leo kumenyana na timu ya taifa ya Somalia kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

YANGA KUMSIMAISHA KAZI MHASIBU WAKE KWA MADAI YA KASHA YA KUUZA TIKETI FEKI

MWENYEKITI wa Yanga, Imani Madega akizungumzia sakata la mweka hazina wa timu hiyo God Mwenje kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kuuza tiketi bandia wa bandia wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyozipambanisha Yanga na Moro United Machi 17, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika jana, hoteli ya Millenium Tower, Kijitonyama, Madega alisema Yanga inakusudia kumsimamisha kazi mhasibu huyo.

KILIMANJARO PREMIUM KWA KUSHIRIKIANA NA BASATA WATANGAZA NYIMBO NA WASANII WATAKAOCHUANA TUNZO YA MUZIKI TANZANIA

Mar 25, 2010

KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium kwa kushirikiana na Barza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo wametangaza wateule kumi walioingia katika mpambano wa tuzo za muziki Tanzania ambao utaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu.
    Akizungumza leo makao makuu ya TBL, Ilala jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tuzo hizo, Angelo Luhala kutoka Basata, amesema ushindani utakuwa katika kupata maimbaji Bora ambapo waliopatikana kuchuana katika fungu hilo ni Lady Jaydee, Mwasiti, Maunda Zoro, Vumilia na Khadija Yussuf .
    Kundi la pili ni Mwimbaji bora wa kiume Marlow, Banana Zorro, Mzee Yussuf, Ali Kiba na Chiristian Bella,
   Alisema kundi la tatu ni Albamu bora ya taarab ambazo ni  Daktari wa Mapenzi (Jahazi Modern Taarab), Riziki Mwanzo wa Chuki (5 Stars Modern Taarab), Kukupenda isiwe taabu (Coast Modern Taarab), Powa Mpenzi (New Zanzibar Star na kila mtu kivyake vyake ya East African Melody.
   Upande wa wimbo bora wa taarab, zitachuanishwa nyimbo za Daktari wa mapenzi (jahazi Modern Taarab), Wapambe Msitujadili (5 Stars Modern Taarab), Riziki mwanzo wa Chuki (Khadija Yussuf), Roho mbaya haijengi (Jahazi Modern Taarab ) na Kukupenda isiwe taabu (Coast Modern Taarab).
     Kwa upande wa Wimbo bora wa mwaka  ni Pii Pii-Missing my baby ( Marlow), Kamwambie (Diamond), Zoba (Banana Zorro),  Nikipata nauli (Mrisho Mpoto) na Kwa ajili yako (Hussein Machozi).
    Alisema kinyang'anyiro cha Bendi yenye wimbo bora wa Kiswahili (bendi) ni Nilizama (Machozi band), Mwana-Dar es Salaam (African Stars), Asha (Top Band), Vuta nikuvute (FM Academia) na Mjini Mipango wa Extra Bongo,  huku katika albamu bora ya bendi zikiumanishwa Mwana-Dar es Salaam (Aftrican Stars), Hilda (Diamond Muzica) na huna shukurani wa Masondo band.
    Katika wimbo bora wa asili ya Kitanzania ni Nikipata nauli (Mrisho Mpoto), Mtarimbo( Machozi  band), Samaki (Offside Trick),  Chei chei ( Wahapa Hapa band) na kupata majaaliwa wa Omari Omari.
    Nazo nyimbo bora za R&B zitakazochuana kuwania tuzo ni  Masogage (Belle 9), Kamwambie (Diamond),  Nipigie (Stara Thomas),Mapenzi ya wawili (Maunda Zorr) na sogea karibu wa Steve na kwa upande wa  wimbo bora wa Hip Hop ni  Stimu zimelipiwa(John Makini), Bullet (Quick Racka), Pom Pom Pisha (Chid Benz), CNN (Mangwea)  na Im Professional wa Fid Q.
     Zile za Reggae zitakazochuana kupata mmoja ulio bora ni Alcohol (Hemed),  dont let i go (Dabo na Mwasili), Barua (Man Snepa), Umoja ni Nguvu wa Matonya na Christian Bella na Leo (reggae Remix) wa AY.
Upande wa nyimbo za Ragga ni Shikide (Dully Sykes), Mungu yuko bize (Bwana Misosi), Wasanii 9Drezzy Chief) na fly wa Benjamini wa mambo jambo, huku mpambano wa rapa bora wa mwaka ukiwakutanisha  Khalid Chokoraa, Ferguson, Kitokololo, Totoo Ze Bingwa na Diof.
   Alisema, upande wa msanii bora wa Hip Hop watanyukana John makini, Fid Q, Chid Benz, Magwea na Profesa Jay huku watunzi bora wanaochuana kupata aliye bora wakiwa ni  Mzee Yussuf, Mrisho Mpoto, Lady jay Dee, banan Zorro, Mzee Abuu na Fid Q.
   Upande wa wimbo bora wa afrika Mashariki  ni Where you are ( Blue 3 na radio and Weasal (Goodlife), Haturudi nyuma (Kidumu na Juliana), Na wewe (Cindy), Bread and Butter (Radio and Weasal- Googlife) na umenikosea wa Kidumu.
    Upande wa mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka ni Marcol Chali, Hermy B. Allan Mapigo na Man Water huku upande wa video bora ya mwaka zikipambanishwa  Natamani kuwa malaika (Lady Jay Dee), Kamwambie ( Diamond), Leo( A.Y), Zoba (banana Zorro),  problem (C Pwaa).
    Alitaja nyimbo za afro Pop zitakazochuana kuwa ni  Zoba (Banana Zorro), Msiniseme (Alikiba), Pii Pii (Marlow), Mama mubaya (Mataluma na Karibu kiumeni wa Chege. huku wasanii bora wanaochipukia watakaochuana kumpata mwenzao bora kuwa ni  Belle9, Diamond, barnaba, quick Racka na Amini.
   Alisema, kwa upande wa wimbo bora wa kushirikiana kimbembe kitakuwa baina ya nyimbo za Nipigie (At-Stara Thomas), CNN ((Mangwea na Fid Q),  Njia panda (Barnabas, Prof Jay na Sugu) na utaipenda wa Hussein Machozi na John Makini
    Luhala alisema uteuzi wa nyimbo au wasanii wanaoingia kwenye kinyang'anyiro hiocho wamepatikana baada ya mchakato uliosimamia na Deloitte Consulting Company ambapo wadau 100 walikaribishwa kuwakilisha Tanzania kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga, Mbeya na Zanzibar.
      Alisema, kampuni hiyo ya Deloitte itaendelea kuwa msimamizi wa kuhakiki na kuhesdabu kura za wadau na kubaki na matokeo hadi utoaji wa tuzo utakapofanyika May 14, mwaka huu.
Ofisa Mshauri wa kampuni ya Delloitte, Neema Mwengu akikabidhi bahasha zenye uteuzi wa wasanii au nyimbo zitakazozishiriki katika kinyang'anyiro cha Tuzo la Muziki Tanzania (Kilimanjaro Muzic Award) kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) David Minja, leo katika ofisi za TBL mjini Dar es Salaam. Katikati ni Mtaribu wa shindano hilo Angelo Luhala kutoka Baraza la Muziki Tanzania (BASATA) ambaye baadaye alikabidhiwa na Minja kutangaza uteuzi huo.

WATU KUMI WAMEKUFA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA DALADALA KUANGUKIWA NA LORI KIBAMBA LEO

HIVI ndivyo hice lilivyoangukiwa na kupondwa vibaya na lori lenye tanki la mafuta, na kusababisha vifo vya watu kumi leo!!!!!
STORI
WATU wamekufa papo hapo leo saa 10.30 alfajiri, baada ya lori lenye namba T 189 ABP na tela la mafuta lenye namba T 192 ABP  lililokuwa likitokea  Dar es Salaam kwenda mkoa wa Pwani kupinduka hadi kuliangukia basi dogo la abiria la ina yaToyota Hiace lenye namba T 615 AJW katika eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,
     Basi hilo dogo la Hiace ambalo limepondwa vibaya  likiwa na abiria ndani lilijkuwa likitokea Kibamba kwenda Ubungo. Kamanda Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga , alisema kuwa basi hilo dogo aina ya Hiace lilikuwa na watu kumi ambao wote wamefariki dunia, na kati ya maiti hizo, ni maiti mbili tu ndizo zilizoweza kutolewa hadi muda huu tena zikiwa vipandevipande.
      Katika maiti hizo zilizotolewa, moja ni ya mwanamke ambae hakuweza kutambuliwa kwa wakati ule na na mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Shukuru Hussein, maarufu kama Kibwetere, mkazi wa Kibamba. Aidha Kamanda Mpinga aliongeza kuwa bado utaratibu unaendelea kwa kuwa lori lilikuwa limejaza mafuta hivyo imeleta ugumu katika utoaji hadi mzigo wote utakapoisha na kuweza kufanya utaratibu wa utoaji.
     Kamanda Mpinga aliweza kumtaja dereva wa lori ambaye amekimbia mara baada ya tukio hilo kutokea kuwa ni Kudura Adam na mmiliki wa Lori hilo ametambuliwa kwa jina la Mahamudu Mohamed.
      Hata hivyo baada ya ndugu wa mmiliki wa Hiace kupatikana na kudai mwenyewe yuko Mkoani Kilimanjaro, walisema kuwa mmiliki huyo anaitwa Selemani Khalfan na Hiace yake huwa inalala Ubungo Kibo maeneo ya Rombo na kumtaja Dereva wa Hiace hiyo kwa jina moja kuwa ni Seif na Kondakta wake Faraji Ismail Kalama ambao mpaka sasa bado maiti zao hazijatolewa eneo la ajali. Taarifa zaidi kuhusiana na ajali hizo zitaendelea kutolewa kadri zitakavyopatikana

MWENYEKITI WA CCM, TAIFA, RAIS JAKAYA KIKWETE ATINGA KATIKA OFISI YAKE YA UENYEKITI WA CHAMA, OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA, DSM

Mar 24, 2010

HABARI KATIKA PICHAHALI ilivyokuwa kwenye Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam, wakati akisubiriwa Mwenyekiti wa Chama taifa, Rais jakaya Kikwete,  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba wakati wakimsubiri Mwenyekiti wa CCM Taifa kuwasili kwenye ofisi yake ya Uenyekiti  leo.MHARIRI Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd ( UPL) Josiah Mufungo (wapili kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Uhuru FM, Mikidadi Mahamud (kulia) na Meneja Rasilimali Watu na Fedha wa UPL, Lucas Anthony Kisasa (wapili kushoto) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa kilichokuwa Cha Cha Soka Tanzania (FAT), Wambura.Baadhi ya wadau wa Chama wakimsubiri kwa hamu Mwenyekiti wa Chama, Rais Kikwete.MSAIDIZI wa katibu Mkuu wa CCM, kuhusu masuala la habari, Mwilapwa akifurahia jambo na Wapigapicha wa Rais, Juma Kengele na Freddy Maro wakati wa mida ya mwishomwisho kabla ya mwenyekiti wa Chama kuwasili.Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na Makamu wa CCM (Bara) Pius Msekwa alipowasiliMwenyekiti wa CCM taifa, Rais jakaya Kikwete akisalimia baadhi ya viongozi wa Chama waliomsubiri.Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwete baada ya kuwasili katika ofisi yake ya Uenyekiti wa CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) George Mkuchika,  Makamu Mwenyekiti (Bara) Pius Msekwa na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Yussuf Makamba .JK akitia saini kitabu katika ofisi yake ya Uenyekiti wa CCM taifa. KATIBU Mkuu wa UVCCM,  Martine Shigella akisalimiana na Ofisa wa Makao Makuu ya UWT, Sarah Msafiri wakati JK akiwa ofisini kwake. Kati yao ni Mkuu wa vipindi wa UHURU FM, Anjel AkilimaliKATIBU Mkuu wa UVCCM Martine Shigella akipena namba za simu na Edward M. au 'Edo' ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM Yussuf Makamba. Kwa sasa Edo anauguza mguu ambayo aliumia hivi karibuni.

STARS IKIJINOA LEO KWA MECHI YAKE YA 'CHAN' NA SOMALIA

WACHEZAJI wa timu ya taifa, Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa (kushoto) na Nurdin Bakari, wakichuana kuwania mpira, timu hiyo ilipofanya mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, leoWACHEZAJI Abdul Alim (kushoto) na Selemani Kasimu wa timu ya taifa, Taifa Stars, wakipambana kuwania mpira, wakati wa mazoezi ya timu hiyo, leo kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa Marcio Maximo akitoa somo kwa wachezaji wakati wa mazoezi hayo. Stars inatarajiwa kumenyana na Somalia kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, katika mchezo wa awali wa kuwania kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani yaani CHAN
ยช