Breaking News

Your Ad Spot

Mar 22, 2010

MAADHIMISHO YA 22 YA WIKI YA MAJI YAFIKIA KILELE LEO

  WAZIRI Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha akiwasili katika viwanja vya Mwendapole, Kibaha mkoa wa Pwani kwenye kilele cha Maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji kitaifa, ambapo alikuwa mgeni rasmi leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza na wapili ni Mwenyekiti wa Kamati ya maadalizi ya maadhimisho hayo Lista Kongola.WAZIRI Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha akipatiwa maelezo na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha M.M. Industries Ltd, Imtiaz Kassam kuhusu ubora wa mabomba ya ukubwa wa inchi 16 , alipotembelea banda la kiwanda hicho kwenye kilele cha maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji, kwenye Viwanja vya Mwendapole, Kibaha mkoa wa Pwani. MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), Alex Kaaya (kulia) akimweleza Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, hatua mbalimbali za kutibu maji kabla ya kuwafikia wateja, Nahodha alipotembelea banda la la maonyesho la mamlaka hiyo kwenye kilele cha maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji, kwenye Viwanja vya Mwendapole, Kibaha mkoa wa Pwani. WAZIRI Kiongozi, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Enerweb pre pay Africa Limited, Gaston Melthus Francis kuhusu mita za kisasa za kulipia maji kabla,  alipotembelea banda la kampuni hiyo leo.WAZIRI Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha akimkabidhi cheti, Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Majisafi na Majitaka mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani (DAWASCO) Mary Lyimo kutambua ushiriki wa kampuni hiyo kwenye maonyesho ya maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji wakati wa kilele cha maadhimisho hayo, kwenye viwanja vya Mwendapole Kibaha, mkoa wa Pwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza. MRISHO Mpoto na mwanamuziki mkongwe hapa nchini Kassim Mapili wakiimba na bendi ya Mjomba, katika shamrashamra za kilele cha maadhimisho hayo.WAZIRI Kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai nahodha akifunga maadhimisho hayo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza, Mkuu wa mkoa wa Pwani Hajat Amina Mrisho na  Mbunge wa Kibaha mjini Zainab Gama.Nahodha akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa mabanda ya watoa huduma na teknolojia za huduma za maji walioshiriki maonyesho ya maadhimisho hayo.NAHODHA akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayoWafanyakazi wa Idara ya Huduma ya Maabara za maji Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakifurahia kombe walilopata kwa kuibuka  washindi wa pili katika kundi la Watoa huduma, katika maonyesho yaliyoambana na maadhimisho hayo kwenye viwanja vya Mwendapole Kibaha mkoa wa pwani.HAKI Ramadhani mwenye ulemavu wa miguu, akiwa amepakia mtoto wake, kwenye baiskeli yake ya miguu mitatu, wakati akifuatilia shamra shamra za kilele cha maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji kitaifa, jana kwenye viwanja vya Mwendapole, Kibaha mkoa wa Pwani. MOJA ya vivutio vilivyokuwepo kwenye maonyesho ya amaadhimisho ya 22 ya Wiki la Maji kwenye Viwanja vya Mwendapole, Kibaha mkoa wa Pwani ni tanki la kupakua majitaka lililoundwa kwenye pikipiki, lililokuwa likionyeshwa na Shirika la usafi wa mazingira (WEPMO) kwenye maonyesho hayo ambayo kielel chake kilikuwa jana.
MRISHO MPOTO AMKUNA NAHODA
Kwanza Waziri Kiongozi akampungia mkonoHalafu akamyooshea mkono kutaka wasalimiane.Mpoto naye akaona kumbe mkuu amenitunuku, akatoka jukwaani kumsogelea Nahodha huku kiongozi huyo naye akisogea zaidi.Kisha wakakaribiana kushikana mikono.Halafu wakashikana."Hujambo Mpoto", waziri Kiongozi akamsabahi."Sijambo Mkuu" Mpoto akamjibu Waziri Kiongozi na kuzungumza mawili, matatu basi.... Mkuu huyo akamwacha na kuondoka Uwanjani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages