.

MDAU ATHUMANI HAMISI KUREJEA NCHINI MEI 8

Apr 30, 2010

Athumani Hamis
MDAU  muhimu wa siku nyingi katika sekta ya habari, Mpigapicha Mkuu wa gazeti la HABARILEO Athumani Hamis ambaye amekuwa akitibiwa nchini Afrika Kusini kwa zaidi ya miaka miwili sasa, baada ya kupata ajali ya gari mjini Dar es Salaam, mwaka juzi. atarejea nchini Mei 8, mwaka huu.
  " Aslaam, safari imeiva. Narudi Tanzania Mei 8, saa 12 jioni.
Msisikitike kuniona ktk kiti wheelchair, mikono na miguu haifanyi kazi. Ni kazi ya Mungu, haina makosa". huu ndiyo ujumbe ambao Athumani Hamis ameutuma leo jioni kwa mtayarishaji wa Blog hii. nami nimeona ni vema nanbyo wadau muupate ujumbe huu. 

BARAZA LA MITIHANI LARANGAZA MATOKEO KIDATO CHA SITA

KATIBU MKUU WA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA (NECTA) DK. JOYCE NDALICHAKO AKIZUNGUMZANA WAANDISHI WA HABARI KUTANGAZA MATOKEO HAYO LEO

JK ARIVES IN KAMPALA FOR THE EAST AFRICA INVESTMENT CONFERENCE!

 Uganda's Vice President Prof.Gilbert Bukenya welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived at Entebbe International airport for The 3rd East Africa Investment conference
A young ugandan girl Clarissa Kanyenjeka presents a bouquet of flowers to president Jakaya Kikwete shortly after he arrived at Entebbe International Airport for the EAC investment conference to be held ta Munyonyo Speke Resort in Kampala.
 Traditional dancers intertain President Jakaya Mrisho Kikwete and his entourage shortly after he arrived at Entebbe airport for the crucial EAC conference on investment

 Uganda's Vice President Prof.Gilbert Bukenya escorts president Jakaya Kikwete through Entebbe airport shortly after he arrived for the 3rd East Africa Investment conference to be held at Munyonyo speke Resort in Kampala(Photos by Freddy Maro)

U20 ZA TANZANIA NA MALAWI KUUMANA LEO DAR

TIMU ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes inashuka dimbani leo kuivaa timu ya umri kama huo ya Malawi.
   Mechi hiyo ya marudiano ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Afrika kwa vijana wa umri huo, imepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
   Kwa ujumla mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu kutokana na ukweli kwamba, katika mechi ya kwanza ya kinyanga'anyiro hicho iliyochezwa Malawi takriban wiki mbili zilizopita, Ngorongoro walilazimisha sare ya mabao 2 - 2.
  Hivyo ni wazi kuwa vijana wa Malawi nao watashuka uwanjani, lakini kikubwa kwenye pambano hilo watakuwa wamekuja kusaka ushindi ili waweze kusonga mbele na mzunguko wa pili wa michuano hiyo.
  Wakati Wamalawi hao wakidhani hivyo, naye Kocha Mkuu wa Ngorongoro, ambaye ni raia wa Brazil, Rodrigo Stockler atakuwa na jukumu linalofanana na lile la wapinzani.
  Jukumu hilo ni kucheza kwa kujituma, nidhamu na kwa ustadi mkubwa ili kuweza kuibuka na ushindi wa aina yoyote ile ili kusonga mbele.
   Bila shaka, Ngorongoro kama iliweza kutoka sare ugenini, na sasa inacheza kwenye dimba la nyumbani ina kila sababu ya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo ambayo inatarajiwa kushuhudiwa na idadi kubwa ya mashabiki wa soka.
  Ili kuhakikisha kuwa Ngorongoro wanasonga mbele kwenye michuano hiyo, tayari Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limeondoa viingilio kwa upande wa mzunguko wa uwanja wa Uhuru ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kujitokeza na kuishangilia timu hiyo.
  Akizungumzia maandalizi ya pambano hilo, Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kuwasili kwa Wamalawi na waamuzi wa mechi hiyo.
  "Uamuzi wa TFF kutoa ofa kwa mashabiki wa soka wa upande wote wa mzunguko kuingia bure, ili kutoa fursa kwa idadi kubwa ya mashabiki kujitokeza uwanjani na kuishangilia timu hiyo," alisema.
  Mechi hiyo ambayo itaamua timu itakayosonga mbele, itachezeshwa na mwamuzi na wasaidizi wake kutoka Elitrea. Aliwataja waamuzi hao ni Gebremichael Luelseged ambaye atasaidiana na Mohamed Berhane na Tesfagiorghis O'Michael, wakati mwamuzi wa akiba ni Ibada Ramadhan(Tanzania).
   Mshindi katika mechi hiyo anatarajiwa kuvaana na timu ngumu ya vijana ya Ivorycoast, ambapo kulingana na ratiba mechi hiyo itachezwa Juni, mwaka huu wakati fainali za michuano hiyo itachezwa Libya, mwakani.
  Viingililo vingine vvya mechi hiyo ni sh.10,000 kwa viti vya VIP, sh.5,000 kwa viti vya jukwa kuu, wakati sh.3,000 kwa viti vya jukwa la kijani.

UCHAGUZI MKUU SIMBA WAWA KIMBEMBE

WAMBURA, KADUGUDA, ALMAS NA HANSPOPE WAONDOLEWA KUGOMBEA
KINYANG'ANYIRO cha uchaguzi mkuu wa klabu ya soka ya Simba, kimeendelea kukumbwa na mizengwe baada ya  wagombea wanne kati ya watano walioliokua wemewekewa pingamizi kuenguliwa.
   Kulingana na taarifa ambayo imetolewa na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Deogratias Lyatto uamuzi huo umefanywa baada ya kuridhika kuwa wagombea hao umewana upungufu ambao unawanyima nafasi ya kuwania uongozi.
   Alisema maamuzi hayo yamefanywa bila ya kuwa na lengo la kumharibia mtu yeyote, ila alisema yamefanywa na kamati yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu husika kuhusiana na pingamizi zilizowekwa.
  "Hayo ni maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya TFF, ambayo kulingana na katiba ya shirikisho bado wagombea wanahaki ya kupinga maamuzi hayo kwa Kamati ya Rufaa ya shirikisho hilo endapo kama kuna mgombea hatoridhika na uamuzi uliotolewa," alisema.
  Alisema kikao cha kamati yake kilifanyika kati ya Aprili 26 na 28, mwaka huu ili kuzijadili rufani hizo, ambazo alisema zilikatwa na wanachama wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.
  Lyatto aliwataja wagombea waliongeliwa na nafasi walizokuwa wakiwania katika mabano ni Chano K.H.Almasi(Ujumbe wa Kamati yaUtendaji) na Mwina Kaduguda(Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hans Poppe na Michael Wambura(Mwenyekiti).
  Lakini wakati wagombea hao wakikumbwa na panga hilo la kamati ya Uchaguzi ya TFF, lakini nuru ya Ismail Aden Rage ambaye alikuwa ni miongoni mwa wagombea waliokatiwa rufaa imeendelea kung'aa.
  Mgombea huyo ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania(FAT) na sasa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), ameibuka kifua mbele, baada ya rufani iliyokatwa dhidi yake na Nassoro Ally kupinga kuweko kwenye kinyang'anyiro hicho, kutupwa.
   Alisema kamati imepitia rufani ambayo ilikatwa na Ally dhidi ya Rage, kuwa kamati imeridhika kwamba kesi zote ambazo zimsababishia kuhukumiwa kifungo jela zilisafishwa na Mahakama Kuu baada ya mgombea huyo(Rage) kukata rufaa.
  "Kamati baada ya kungalia na kupitia rufani ya mwanachama Ally, iliona mgombea tayari alisafishwa na Mahakama Kuu katika kosa ambalo awali lilimtia hatiani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu," alisema.
   Akifafanua kuhusiana na kuenguliwa kwa Chano, ambaye aliwekewa pingamizi na mwanachama, Asha Kigundula, alisema baada ya kupitia ruafani ya Asha imebaini na imeridhika mgombea Chano, hakutimiza wajibu wake kulingana na katiba ya Simba ibara ya 19 kifungu namba 3,4,6,7 na 8 na ibara ya 21 kifungu (g)  na ( i).
   Alisema aidha kamati imebaini mkanganyiko wa majina ya mwombaji uongozi, akitoa mfano alisema kwenye maelezo binafsi ametumia jina la Karaha Hassani Almasi Chano, wakati kwenye kadi ya uanachama wa Simba SC ametambulika kwa jina la Chano K.H. Almasi.
   Hivyo kwa kutotimiza wajibu wake kulingana na matakwa ya katiba ya Simba na mkanganyiko huo wa majina, hakika umeitia dosari fomu ya mgombea husika na hivyo amekosa sifa ya kuwa mmoja wa wagombea," alisema.
  Akizungumzia kuondolewa kwa Kaduguda, alisema aliwekewa pingamizi na mwanachama, Asha Kigundula na kamati imebaini mgombea huyo hakutimiza wajibu kulingana na katiba ya Simba SC ibara ya 19, kifungu namba 3,4,5,6,7,8 na ibara ya 21 kifungu f,g,h,i na ibara ya 38 kifungu namba 4,5,6 na 7.
  "Baada ya kupitia pingamizi hiyo ya Asha, kamati imeridhika kuwa Kaduguda emeshindwa kukidhi matakwa ya kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF, ibara ya 9. Hivyo kamati imemwondoa mgombea kwenye mchakato," alisema.
  Kufuatia kitendo hicho ambacho kimezua minong'ono kwa baadhi ya walioenguliwa na wanachama, vile vile kumezua tetesi kuwa kuna uwezekano wa wanachama au waliongeliwa kulipeleka suala hilo mahakakamani.
  Lyatto alisema kuenguliwa kwa Hans Poppe, ambaye alikua amewekewa pingamizi na mwanachama, Issa Ruchaki, baada ya kubaini kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ibara ya 25(2).
  Alisema kamati yake ilibaini kamati ya uchaguzi ya Simba ilifanya makosa kwa kutumia ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuzingatia katiba ya klabu hiyo ibara ya 26(5) kwa kumpitisha mwombaji asiyekidhi matakwa ya kifungu hicho.
  Kuhusiana na kuenguliwa kwa Wambura, alisema mgombea huyo aliwekewa pingamizi na mwanachama, Daniel Kamna na kamati yake ilikubaliana na maamuzi ya yaliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi na Rufaa za TFF za mwaka 2008.
  Alisema uamuzi huo ulionyesha kuwa Wambura hakukidhi matakwa ya ibara ya 29(7) ya katiba ya TFF na ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa wanachama wa shirikisho hilo wakati alipokua kuwania nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF.
  "Hivyo kulingana na maamuzi yaliyotolewa na kamati hizo za Rufani na Uchaguzi za TFF, kamati yangu imemwondoa mgombea huyo,"alisema.
   Hivyo hofu imeendelea kushamiri kutokana na ukweli kuwa, endapo kama wanachama au mgombea yeyote yule atashindwa kufuata taratibu za kukata rufaa kwa Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kama inavyotakiwa na taratibu husika za shirikisho hilo.
  Badala yake mwanachama au mgombea akalipeleka suala hilo mbele ya mahakama ili kusaka haki yake, ni wazi kuwa uchaguzi huo huenda ukashindwa kufanyika Mei 9, mwaka huu.
  Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa kulingana na katiba ya TFF, Klabu na vyama shirikishi vya shirikisho hilo, hazituhusu masuala ya soka kupelekwa mahakamani.
Wambura acharuka
MGOMBEA nafasi ya Mwenyekiti kwenye uchaguzi mkuu ujao wa klabu ya soka ya Simba, Michael Wambura ambaye ameenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho, ameapa kupigana kufa na kupona ili kutetea haki yake.
   Akizungumza muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka(TFF), Deogratias Lyatto kutangaza matokeo ya pingamizi zilizowekwa kwa wagombea.
    Wambura aliyasema hayo kwenye ukumbi wa shirikisho hilo ulioko uwnaja wa Karume.
Tanzania(TFF), ikiwa ni muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF,
   Wambura alisema kwa sasa anasubiri kupatiwa nakala ya kuenguliwa kwake, ambayo alisema ataipata kutoka kwa kamati ya uchaguzi ya shirikisho.
   "Binafsi sishangazwi na taarifa ambazo zimetolewa leo(jana) na Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF, Lyatto. Kwani kilichokua kikiandikwa na vyombo vya habari ni ndicho hicho kilichotokea," alisema.
   Alisema anawasiliana na wanacheria wake ili kuona kuwa ni jinsi gani atafanya, ili kumwezesha kuitetea haki yake ambayo alisema inaonekana dhahiri kupokwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi.
   Wambura ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania(FAT) na sasa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), alisema tangu mchakato wa upitiaji wa majina ya wagombea ulipoanza katika kamati ya Uchaguzi ya Simba.
  Alisema tayari kuna watu(hakuwataja majina), ambao alisema walikuwa wanafanya mbinu chafu hata kutumia kiasi kubwa cha fedha ili kumchafua na asipate tiketi ya kuingia kwenye uchaguzi huo.
  "Pamoja na kuwa kanuni za uchaguzi zineelekeza tunaweza kukata rufaa kwa Kamati ya Rufaa ya TFF, lakini sitasema hivyo kwanza nasubiri nipate hiyo nakala na kisa nitazungumza na wanasheria wangu," alisema.
  Wambura alisema wanasheria wake ndiyo watakuwa na jukumu la kumweleza kuwa nini anapaswa kukifanya, baada ya kutangazwa kuengeliwa kwenye mchakato huo.
  "Kuna kipengele cha 'Integrity'(kukosa uaminifu) ambacho mara kwa mara wamekuwa wakikitumia juu yangu, lakini nitaka wanielezee zaidi ni kuhusiana na kitu hicho ambacho kinanichafua mara zote," alisema.
  Akijibu swali kama ana mpango wowote ule wa kulipeleka suala hilo mahakamani, alisema ni mapema mno kwake kuzungumzia jambo hilo.
  "Siwezi kuzungumzia suala la kwenda mahakamanin sasa, kwani kulingana na kanuni ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) ibara ya 12 inaelekeza mgombea kufuata taratibu na kukata rufani kwa Kamati ya Rufaa, kama ikishindikana baadaye Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo," alisema.
   Kuenguliwa kwa Wambura, Zacharia Hans Poppe na Hassan Dalali kwenye nafasi hiyo kumeifanya nafasi hiyo isaliwe na wagombea watatu, ambao ni Hassan Othman'Hassanoo' , Andrew Tupa na Ismail Aden Rage.

AJALI YA BARABARANI TANGA YAUA WANAFUNZI 18 WA MADRASA, 25 WAJERUHIWA

Apr 29, 2010

WANAFUNZI 18 wa Chuo cha Kiislamu cha Shamsil-Maariff cha jijini hapa, wamekufa papo hapo na wengine 125 kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kupinduka.
   Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Adolphina Kapufi, alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 5.30 usiku katika eneo la njia panda ya Mabanda ya Papa jijini hapa.
  Waliokufa katika ajali hiyo na kutambuliwa ni Twalib Kunemu, Juma Idd, Faraji Habib, Jahshi Rashid, Hussein Bakari, Hajji Athumani na Yussuph Hussein na kwamba kazi ya kuwatambua inaendelea.
   Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Paschal Kanyinyi, alisema kazi ya kutambua maiti waliokufa katika ajali hiyo inakwenda sambamba na utambuzi wa majina ya majeruhi waliolazwa katika wodi ya Galanosi katika Hospitali ya Mkoa, Bombo.
  Alisema majeruhi 125 walifikishwa hospitalini hapo usiku baada ya ajali hiyo kutokea, ambapo 70 kati yao walipata matibabu na kuruhusiwa kurejea chuoni.
Wengine 55 wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo chini ya usimamizi wa timu maalumu ya madaktari na wauguzi.
    Majeruhi waliotambuliwa ni Jumaa Salim ambaye ameumia mbavu, Makame Ahmed, Ahmed Shehe, Selemani Said na Juma Akida. Hata hivyo, aliwataja majeruhi wengine ambao hali zao ni mbaya na wamepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam Kitengo cha Mifupa (MOI) kuwa Hemed Shaaban na Hassan Adam.
   Mwalimu wa zamu wa chuo hicho, Ustaadh Ajali Ramadhan, alisema wanafunzi hao walikuwa wakitokea kijiji cha Kibafuta ambako walikwenda kuhudhuria sherehe za Maulid.
   Hata hivyo, alishangaa kuona idadi kubwa ya wanafunzi waliopata ajali hiyo, kwani walioruhusiwa kutoka chuoni hapo ni 60 tu.
   Kaimu Mganga huyo alimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Raha Leo, Seleman Abdallah kwa kutoa msaada wa dawa kwa ajili ya kuwatibu majeruhi waliopata ajali hiyo.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Tanga, akichukua taarifa za majeruhi waliopata ajali katika ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwaMadaktari na wauguzi wakiwapatia matibabu majeruhi.Majeruhi Ali Maulid akiwa katika wodi ya Galanosi Hospitali ya Bombo baada ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwa.
Majeruhi aliyetambulika kwa jina moja la Hassan akiwa amekatika mokono amelazwa katika wodi ya Galanosi Hospitali ya Bombo baada ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwa. HABARI NA PICHA ZOTE NA MDAU SOPHIA WAKATI


.

PINDA AZINDUA RASMI BARABARA YA DOM-MANYONI

Apr 28, 2010

*SASA BADO KM 20 DAR-MWANZA KUWA LAMI TUPU
UHAKIKA wa kutimia ndoto ya miaka mingi ya watu kuweza kusafiri kwa teksi na kwa muda mfupi kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, inaelekea kutimia kufuatia kusalia kilometa 20 tu kuifanya barabara hiyo yenye jumla ya kilometa 1,113 kuwa ya lami.
   Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Dodoma-Manyoni lenye urefu wa kilometa 126, ambayo ilizinduliwa rasmi juzi mjini Manyoni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda .
   Katika uzinduzi huo, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alimwambia Waziri Mkuu kwamba eneo lililobaki la kilometa 20 ni sehemu ya barabara ya Manyoni-Isuna yenye urefu wa kilometa 55 inayojengwa na kampini ya China Geo Engineering ambayo linatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.
  “Mheshimiwa waziri Mkuu na ndugu wananchi, naweza kusema kwamba sasa ile ndoto iliyokuwa ikisemwa amara kwa mara na Waziri mwenzangu wa Miundombinu aliyetangulia bwana Magufuli itafikia wakati mtu anatoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa teksi inakaribia kutimia kwa kuwa tumebakiza mkia kuifanya barabara ya eneo hilo kuwa ya lami yote”, alisema Kawambwa.
   Alisema, barabara ya Dodoma-Manyoni yenye urefu wa kilometa 126 ambayo ujenzi wake umegharibu kiasi cha sh. Bilioni 143, ulianza mwaka 2003 ukifanywa na kampuni ya Konoike ambayo baadaye ilinyang’anywa kazi hiyo baada ya kushindwa kukidhi utendaji na ikapewa kampuni ya ESTIM ya Kitanzania Februari 2009 ambayo imekamilisha ujenzi wote.
    Alisema eneo la barabara ya Manyoni-Isuna kwa mujibu wa mkataba linatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu, lakini kulingana na mjenzi wa barabara hiyo, kampuni ya Geo Engineering ya China huenda ikakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
    Dk. Kawambwa alisema akwa sasa eneo imejengwa kwa kuzingatia viwango na mahitaji yote ya watuamiaji wa barabara ikiwemo kuwekwa maeneo ya waenda kwa miguu, alama za barabarani na njia za waendesha baiskeli kwa maeneo yanayohitajika.
    Alisema, pamoja na kuweza kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa teksi na kwa mwendo mzuri zaidi kufuatia kukamilika kwa barabara ya Dar es Salaam hadi Mwanza, pia karibu itawezekana kufanya hivyo kutoka Mtwara hadi Mwanza kufuatia kukaribia kukamilika barabara za Mbwemkulu-Mingoyo (Kilometa 95), Nangurukuru-Mbwemkulu(km95) na Somanga –Matandu (kilometa 33).
    Hata hivyo, Dk. Kawambwa alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakiharibu au kuiba mioundombinu ya barabara i8kiwemo alama za barabarani, akitoa mfano kwa wizi wa lama za barabarani uliofanywa na baadhi ya wananchi katika eneo la Chikuyu , Dodoma-Manyoni.
   Kufuatia maelezo hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameagiza wakuu wa mikoa na watendaji wote wenye dhamana, kuhakikisha wanaweka udhibiti wa kuhakikisha inakomeshwa tabia ya baadhi ya watu kuhujumu miundombinu ya barabara kwa kuiba alama za usalama barabarani na kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo kwenye eneo la hifadhi za barabara.
    Waziri Mkuu aliwataka watendaji hao kusimamia kwa karibu ili kuhakikisha wananchi hawalimi hadi ndani ya mita 25 kutoka kwenye barabara kwa mujibu wa sheria na kuwataka kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika.
   “Nawaagiza wakuu wa mikoa na watendaji wote, hebu shughulikieni kwa dhati kuhakikisha udhibiti wa hawa wanaaoiba na kufanya shughuli za kilimo katika eneo la hifadhi ya barabara mnawachukulia hatua za kisheria, maana wanaofanya hivi ni maaudui wa maendeleo kwelikweli”, alisema Pinda.
    Pinda aliwataka wananchi wa Manyoni na Singida kwa jumla kutumia rasilimali walizonazo kuhakikisha barabara ya barabara hiyo inawapataia maendeleo wanayotarajia, na kuonya kuwa wasipofanaya hivyo watabaki kuona kuwa inawanufaisha wenye baiskeli na magari tu.
    Mapema, mkuu wa mkoa wa Singida, parceko Kone alisema, yeye na viongozi wenzake mkoani watahamasisha wananchi kuitumia barabara hiyo katika kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kuifanya chachu ya kukuza biashara baina yao na maeneo ya nye ya mkoa huo.

HABARI KATIKA PICHA
Hivi ndvyo jukwaa kuu llilivyokuwa liamenakishiwa kwa ajili ya uzinduzi wa barabara hiyo.Jiwe lamsingi la izinduziWAZIRI wa Miunfombinu,Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiwahoji taarifa mbalimbali watendaji wa TANROADS, kuhusu barabara ya Dodoma-Manyoni, alipoikagua kabla ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Crispian Ako. Kina mama wakicheza ngoma kushangilia uzinduzi huo.NAIBU Waziri wa Miunfombinu Ezekiah Chibulunje akisalimia wananchiWAZIRI wa Miundombinu,Dk. Shukuru Kawambwa akisalimia wananchi wa Manyoni, kabla ya hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu kuzindua barabara hiyo.Dk. Kawambwa, Katibu Mkuu wa wizara ya Miundombinu, Chambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, wakifuatilia kwa makini hotuba ya uzinduzi ya Waziri Mkuu.WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda akimtambulisha kwa wananchi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Baraara nchini (TANROADS) Ephraim Mrema, wakati wa uzinduzi wa barabara ya Dodoma-Manyoni uliofanyika mjini Manyini jana.WAZIRI Mkuu akizindua jiwe la msingi la kukamilika kwa barabara hiyoWAZIRI Mkuu Mizengo Pinda na mkewa, Tunu Pinda wakiodoka katika uwanja wa shule ya Tambukareli, wilayani Manyoni baada ya kuzindua barabara ya Dodoma-Manyoni. Kushoto ni Waziri wa Miundombinu, Dk.Shukuru Kawambwa na Mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone.WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda akikata utepe kuzindua barabara ya Dodoma-Manyoni, katika sherehe zilizofanyika juzi, mjini Manyoni. Kulia kwake ni Waziri wa Miundombini, Dk. Shukuru Kawambwa na kushoto kwake ni mke wake, Tunu Pinda.Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 126 uegharimu sh. bilioni 143 WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda na mke wake, Tunu Pinda,wakiagana na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Betty Mkwasa baada ya kuzindua barabara hiyo.Betty ni Mkuu wa wilaya ya Bahi mkoani humo. Kina mama wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Mizengo Ponda kuzinfua barabara hiyo.WAZIRI Mkuu akiondoka na msafara wake baada ya uzinduzi huo
WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya Manyoni wakifutahia barabara hiyo mpya kwa kuendesha baiskeli zao baada ya kuzinduzi huoMOJA ya maeneo yaliyozingatiwa katika ujenzi wa barabara hiyo nikuwekwa  njia za wanedesha baiskeli kama hawa waliokuwa wakiendesha baiskeli zao katika barabara hiyo.Moja ya madaraja yaliyopo kwenye barabara hiyo.Barabara ikiwa na moja ya mabango au alama za barabarani ambazo hasipswi kunyofolewa na wezi kama ilivyoelezwa kufanyika katika eneo la ChikuyuPOLISI wa usalama barabarani akiwa amelisimamisha lori katika eneo inakoishia lami ya barabara hiyo ya Dodoma-Manyoni. eneo hilo ni la kilometa 55 kutoka Manyoni hadi Isuna ambalo nalo litakamilika kuwekwa lami mapema mwakahuu.

AJALI YA TRENI NA GARI LA MIZIGO YAUA WANNE NA KUJERUHI WATANO DODOMA

Apr 26, 2010

WATU wanne wamekufa na watano kujeruhiwa baada ya gari la mizigo kugonga kichwa cha treni mjini Dodoma leo.
  Ajali hiyo imetokea leo katika eneo la Hazina baada ya gari aina ya Landrover kukwama kwenye makutano ya reli na treni wakati ikitaka kuvuka na hatimaye kukutwa na kichwa na treni.

BARABARA YA DODOMA-MANYONI KUZINDULIWA KESHO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Mhandisi Omari Chambo akizungumzia uzinduzi wa barabara ya Dodoma -Manyoni, leo baada ya kukagua barabara hiyo ambayo itazinduliwa kesho na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.MAFUUNDI wakikamilisha jiwe la msingi lauzinduzi wa barabara hiyo ya Dodoma-Manyoni utakaofanywa kesho na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika eneo la Tambuka reli mjini Manyoni.

KATIBU Mkuu Nhandisi Omari Chambo akikagua barabara ya Dodoma-Manyoni katika eneo la Manyoni leo. wengine ni maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na wa Wizara hiyo
Ofisa Habari wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Aisha Malima akifurahia jambo na Ufoo Saro wa ITV kwenye eneo la uzinduzi wa barabara hiyo mjini Manyoni leo

Katibu Mkuu Chambo akibadilishana mawazo na watendaji wa TANROADS na wa wizara hiyo baada ya ukaguzi


MUUNGANO KESHO

Apr 24, 2010

BABA wa taifa Hayari, Mwalimu Julius Nyerere akichanganya mchanga wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe za kuuasisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

TAJI LAMISS UNIVERSE 2010/11 LAENDA ARUSHA

MWANADADA Hellen Dausen kutoka jiji la Arusha, nwenye umri wa miaka 23, akipinga mkono baada ya kulitwaa taji la Miss Universe 2010/11  nchini katika shindano lililofanyika katika  ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,  usiku wa kuamkia leo.


RAIS KIKWETE AMJULIA HALI MBUNGE KIMARO MUHIMBILI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza leo asubuhi na Mbunge wa Vunjo(CCM) Aloyce Kimaro alyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kuugua shinikizo la damu juzi akiwa bungeni mjini Dodoma(Picha na Freddy Maro)

MKUTANO WA KIMA TAIFA WA HALI YA UCHUMI BARANI AFRIKA (WEF) WAIVA

*Utafanyika Dar es Salaam, 05-7 Mei 2010
*Vyombo vya habari vyaombwa kuupa shavu
*Hadi sasa 959 wamejiandikisha kushiriki mkutano huo.KATIBU Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akizungumza na waandishi wa habari leokuhusu mkutano huo waKimataifa.KATIBU Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akizungumza na waandishi wa habari, jana mjini Dar es Salaam, kuhusu mkutano wa Kimataifa wa uchumi katika bara la Afrika utakaofanyika hapa nchini mwezi ujao. Kulia ni Mshauri wa Rais masuala ya Uchumi, Elsie Kanza na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO,Clement Mshana. MIKONOZ wa Ikulu, Freddy Maro na Kaka Kengengere wakifurahia jambo wakati wa Press Conference hiyo.MIKONOZ wa Chachandu-Daily na Kaka Freddy baada ya Press Conference hiyo.

Kwa habari zaidi kushu mkutano huo piga hodi katika www.weforum.org


WAJANE KAWE WAANZISHA CHAMA KUJIKWAMUA

Apr 23, 2010

MEYA wa Manispaa ya Kinondoni Saidi Londa akifungua mkutano wa Umoja wa Wanawake Wajane wa Mbezi A, leo katika ukumbi wa Ian Pub, Kawe, Dar es Salaam. Kushoto niu Katibu wa Umoja huo, Zaidani Mwamba na katikati ni Mwenyekiti wa umoja huo Ellen Newa. BAADHI ya wanachama wa Umoja wa Wanawake Wajane wa Mbezi A, Kawe, Dar es salaam, wakiwa kwenye mkuitano wao uliofanyika jana, Ian Pub Kawe.

ASHANTI KURINDIMISHA NGUMI ZA KUJIPIMA NGUVU MAXI

KLABU mpya ya Mchezo wa Ngumi ya Ashanti inayokuja kwa kasi kuleta mabadiliko ya mchezo huo watacheza mchezo wa kujipima nguvu na zingine za mchezo huo Ijumaa katika ukumbi wa Max Ilala Bungoni Dar es Salaam.
   Kocha mkuu wa klabu hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema Dar es Salaam jana kuwa klabu hiyo yenye mabondia 16 itapigana na klabu zingine itambulike kuwa ni miongoni mwa klabu zinazoendeleza mchezo wa ngumi Tanzania.
   Alisema kabla ya kushiriki michezo ya klabu bigwa yanayotarajia kufanyika mapema mwaka uhu ambapo klabu zote zipo katika maandalizi ya kushiliki mashindano hayo,
   Super D alisema katika kujipima huko kutakuwa na Klabu za Ashanti ya Ilala, Mtakuja ya Vingunguti, Sifa ya Manzese na Mkumwena ya Buguruni, na wenyeji Ashanti ambapo kila klabu aliwataja mambondia watakaopanda na klabu wanazotoka

KGS (LIGHT FLY WEIGHT)

1. RAJABU HAMISI ‘ROJA MJESHI’ (ASHANTI) Vs HUSSEIN SAID (SIFA)
2. BADRU HASSAN ‘MUHINDI MWEUSI’ (ASHANTI) Vs SALUMU IDDI (MTAKUJA)
3. SHABAN MADILU ‘TYSON’ (ASHANTI) Vs ASHRAF JUMA (MTAKUJA)
4. HASSAN SAID (ASHANTI) Vs SAID ALLY (MTAKUJA)

54 KGS (BANTAM WEIGHT)
1. JOSEPH RICHARD ‘MNYAMA’ (ASHANTI) Vs HUSSEIN KASSIM (SIFA)
2. HUSSEIN ABDALLAH (MTAKUJA) Vs HASSAN SHARI (SIFA)
3. MATIKU MAGESA (ASHANTI) Vs OMAR ABDALLAH (SIFA)
4. HASEN SAID ‘MNGONI’ (ASHANTI) Vs RASHID ABDALLAH (MTAKUJA)
5. IDDI RAMADHAN (ASHANTI) Vs KULWA KILIANI (MTAKUJA)

64 KGS (LIGHT WEIGHT)
1.MOHAMMED RAJAB ‘BONGE’ (ASHANTI) Vs IDDI PIALALI (MTAKUJA)
2. ABJERINA KADRI (ASHANTI) Vs HAMISI ABDI (ASHANTI)
3. JUMA CHAMBALA (ASHANTI) Vs ABDALLAH MSHINDO (MTAKUJA)
4. OMAR KANESA (MTAKUJA) Vs KOBA KITEA (MTAKUJA)
5. SAKO MWAISEJE (ASHANTI) Vs SHARIF MZEZELE (SIFA)
6. HANS JOHN (SIFA) Vs MOHAMMED MUSSA (MTAKUJA)

RAJABU MHAMILA “Super D” TEAM COACH
ASHANTI BOXING CLUB
Mobile Numbers:- 0713/0754/0787/0774-406938

WE ARE HERE TO SUPPORT THE GROWTH OF BOXING TALENT
Mchezaji mkongwe wa mchezo wa Ngumi Iraki Hudu (kushoto) akiwaelekeza mabondia wa Klabu ya Ashanti ya Ilala Dar es salaa wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano ya kirafiki yatakayofanyika siku ya 30/4/2010 katika ukumbi wa Max bungoni kulia ni Katibu wa Ashanti FC, Haji Bechina

WIZARA YA MIUNDOMBINU YAKAGUA FARAJA LA UMOJA, LITAZINDULIWA RASMI MWEZI UJAO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo (kulia0 na msafara wake wakikagua daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji ambalo litazinduliwa mwezi ujao. (Picha na Aaron Msingwa-MAELEZO).
ยช