.

SEAMIC MEETING

May 28, 2010

Mwenyekiti wa SEAMIC, Waziri wa Madini na Nishati, William Ngeleja akizungumza wakati wa mkuatno huo, uliofanyika leo katika ukumbi wa kituo hicho, Kunduchi, Dar es Salaam 
Badhi ya wajumbe wakiwa kwenye mkutano huoBaadhi ya waandishi wa habari aakiwemo Mzee wa Chachandu-Daily (kushoto) wakiwa kwenye mkutano huo.Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huoWaandishi wa habari wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi baada ya ufunguzi wa mkutano huo, ksuhoto ni mtangazaji wa ITV Fatma Nyangasa na mwenzake ni raia wa Finland ambaye anafanya mazoezi kituo cha TBC1

MANOWARI UHOLANZI YA KUSAKA MAHARAMIA ILIPOTIA NANGA DAR

Waandishi wa habari kutoka Uhuru Publications na Nipashe ni miongoni mwa waandishi waliofika kushuhudia na kuchukua habari za meli hiyo kwa ajiri ya kuripoti kwenye vyombo vyao. 
Waandishi wa bahari akiwemo Mzee wa Chachandu-Daily hii (kulia) akiwa kwenye tukio hilo
Manowari ya Kivita ya HR Ms John Dewit ya Uholanzi ikishusha mapipa ya mafuta ya  dizeli,   petroli na vilainishi ya jumla ya lita 10,000, ambayo meli hiyo iliwanyang'amya maharamia iliowakamata wakati ikija Tanzania 
Mmoja wa maofisa wa Kijeshi katika manowari hiyo akiwapatia maelezo waandishi wa habari inavyofanya kazi na mfumo wake ulivyo sehemu ya uongozaji. 
Moja ya silala zilizomo kwenye manowari hiyo 
Suleiman Jongo wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani akiwa kwenye eneo la kutua helkopta za kivita katika meli hiyo. 
m
Askari katika meli hiyo akimsaidia mwandishi wa Chaane Ten Dina Ismail kupita katika moja aya maeneo magumu ndani ya meli. 
Askari katika meli hiyo akimsaidia  Fatma Almas Nyangassa wa ITV kupia kwenye moja ya vihunzi katika meli hiyo. 
Daktari akionyesha bonge ala hospitali yenye kila kitu na aina zote za tiba katika meli hiyo.

LINDI YATINGA NUSU FAINALI BAADA YA KUIKUNG'UTA ILALA 3-0

May 27, 2010

MCHEZAJI wa timu ya Ilala, Bao Bofu (kushoto)akipambana na Justin Philipo wa timu ya mkoa wa Lindi timu hizo zilipomenyana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup', jana.Lindi iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.MASHABIKI wa timu ya mkoa wa Lindi wakishangilia baada ya mechi kumalizika, timu hiyo ikiwa imeibuka na ushindi wa mabao 3-0, ilipomenyana na timu ya Ilala, katika nusu fainali ya Kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup', kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

KILI TAIFA CUP, SINGIDA YAING'OA ARUSHA; YATINGA FAINALI

May 26, 2010

*Yazisubiri Lindi au Ilala katika fainaliMSHAMBULIAJI wa timu ya Singida Kelvin Charlle (kulia) akimtoka beki wa Arusha, Saidi Mussa, timu hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika nusu fainali ya michuano ya Kili Taifa Cup. Singida imeibuka na ushindi wa mabao 3-1.

KILI TAIFA CUP: BAADA YA KUONDOLEWA KATIKA HATUA YA ROBO FAINALI, TEMEKE YAIJATIA RUFANI SINGIDA aka SINGAPORE

May 25, 2010

BARUA YAO YA KULALAMIKA

KILI TAIFA CUP, IRINGA YALALA KWA ILALA, KILIMANJARO IKIPANDWA NA LINDI LEO

TIMU za Ilala na Lindi zimefuzu kuingia nusu fainali za Kombe la Taifa, Kili Taifa Cup, baada ya kufanikiwa kuzizaba mabao timu zilizochuana nazo katika robo fainali, zilizorindima leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
     Katika mechi ya kwanza Ilala iliinyuka Iringa mabao 6-4 kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya bao 1-1.
Na Lundi imefuzu baada ya kuizaba kiuhakika timu ya Kilimanjaro mabao safi 3-1.
NCHEZAJI Shabani Sunza wa Ilala (kushoto) wakichuana na Brighton Mponzi wa Iringa, timu hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika roboi fainali ya michuano ya Kili Taifa Cup. KOCHA wa timu ya Ilala  Jamhuri Kihwelo akikunbatiana na kocha wa Itinga Freddyu Felix Minziro baada ya mechi ya timu zao
BAADA ya kuwa nyumbani kwao Congo DRC alikokwenda kwa ajili ya kuona familia yake kwa zaidi ya mwezi mmoja, Kiongozi nwa bendi ya Akudo Impact Christian Bella ametua nchini na kuungana na bendi yake akiwa na wanenguaji wapya wanne aliokuja nao
Akiwatambulisha leo kwa waandishi wa habari, katika baa ya Stereo Kinondoni, Dar es Salaam, kiongozi wa bendo hiyo Bella, aliwataaja wanenguaji hao kuwa ni Framcina Pesabiloko kutoka kwa Werason Ngiama, Patricia RG 512 aliyekuwa na Fally Pupa, Raussa Sangwa aliyekuwa na Bozi Boziana na mnenguaji wa zamani wa bendi hiyo, Faniu Bosawa ambaye naye alikuwa nchini Congo.
Bella akiwa na wanenguaji haoWanenguaji hao wakioinyesha umahiri wao walipotambulishwa kwa waandishi wa habari leo.


KILI TAIFA CUP, ARUSHA NA SINGIDA ZAFUZU NUSU FAINALI

May 24, 2010

JACOB Masau wa timu ya Mwanza (kulia), akikabiliana na Nafu Sanane wa timu ya Arusha, timu hizo zilipomenyana leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, mechi ya robo fainali ya michuano ya Kili Taifa Cup.Mwanza ililala kwa mabao 6-4.

LIYUMBA AFUNGWA MIEZI 24 JELA


BAADA ya kusota mwaka mmoja rumande, wakati kesi yake kuhusu matumizi mabaya ya ofisi na kuitia hasara serikali, aliyekuwa Meneja Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, Amatus Liyumba, leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, sawa na miezi 24.
  Kulingana na taratibu wa vifungo hapa nchini, miezi hiyo 24 itahesabiwa kwa usiku na mchana, hivyo atatumikia jela hadi Mei Mwakani, huku uwezekano wa kutoka mapema kwa msamaha wa rais ukiwa wazi kwa kuwa kosa lililomtia hatiani si katika makosa ambayo hayaruhusu kupata msamaha wa Rais yakiwemo ya ubakaji, uhujumu uchumi na kupatikana na dawa za kulevya.
 Baada ya kuhukumiwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Wakili wa Liyumba , Magafu amesema atakata rufani.

Habari katika Picha
 
Basi la magereza likiwasili na Liyumba mahakama ya KisutuLiyumba akishukaAkisindikizwa na askari magereza kwenda kizimbaniLiyumba akiingia chumba cha mahakamaAkiwa katika benchi kabla ya kupanda kizimbaniLiyumba akipewa ufafanuzi na wakili wake Majira  Magafu (kushoto) baada ya hakimu kumtia hatiani na kutoa mapumziko ya nusu saa kabla ya kutoa adhabu.Liyumba akisindikizwa na askari magereza baada ya hukumuMTU mmoja mwenye nywele za kusokotwa maarufu kama rasta, akijifatagua kwa kuonyesha alama ya vodole viwili mbele ya Liyumba aliyekuwa akipelekwa rumande ya mahakama kabla ya kwenda jela.Mahakama ikiwa imefurika watu, wengi wao wakiwa ni ndugu na jamaa.Liyumba akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza baada ya hukumu 
Liyumba akipanda gari la magereza kuanza safari ya kwenda kutumikia kifungo jela miaka mwili.Asjariu Magereza wakiwa wameimarishja ulinzi

TRAFIKI NA 'LIFT' YA BAJAJI

May 22, 2010

POLISI wa Usalama barabarani al maarufu, Trafiki, akiisogelea bajaji na kuzungumza jambo fulani na derevaHaralafu akanyanyua mguu wa kulia kuingiza ndani ya bajaji hiyoHalafu akaingiza kichwaHalafu mwili woteSafari ikaanza.....
Hata hivyo blog yako ya jamii haikuweza kujua kama hii ilikuwa ni lifti tu au mambo mengine!

NGASA ATUA RASMI AZAM FC

MWENYEKITI wa Azam FC Said Muhammad Said Abeid akimkabidhi jezi namba 16, Mrisho Ngasa wakati akimtambulisha rasmi mchezaji huyo ambaye Azam imemsajili kutoka Yanga kwa sh. milioni 58, katika sherehe iliyofanyika mjini Dar es Salaam, leo
UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI: DAR WACHANGAMKIA

WAT U wakiwa katika foleni ya kuandikishwa au kuhakiki majina yao au ya jamaa zao katika kituo cha Jangwani.KARANI akiandikisha wananchi katika kituo cha Jangwani, Dar es Salaam, leo.Al amin Mohammed (13), wa pili kushoto, akiwa kwenye foleni kwa niaba ya babu yake, katika kituo chga Jangwani, leo.OMAR Mabalanga (61) aliyekuwa mkazi wa Morogoro, akiingia katika kituo cha kujiandikisha kuwa mpiga kura leo latika  kituo cha Madenge, Buguruni mjini Dar es Salaam, ambako amehamia kuwa mkazi sasa.MKAZI wa Buguruni Madenge, akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura leo

KILI TAIFA CUP, TBL HAIHUSIKI NA MASUALA YA KIUFUNDI

NI TAMKO LA EXECUTIVE SOLUTIONS LTD

TAARIFA KAMILI
Ndugu wanahabari wenzangu,
    Napenda kutumia nafasi hii kwanza kuwapa pole kwa kazi. Najua mnayo majukumu mengi kuhakikisha Watanzania hasa wapenda michezo wanapata habari kwa wakati unaostahili.
    Pia natoa shukrani za dhati kwa ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka kwenu katika shughuli zetu za kila siku hususani kwenye mashindano yanayoendelea ya Kili Taifa Cup.
   Japokuwa mashindano ya mwaka huu yamefana kuna mambo kadhaa yamejitokeza kama vile baadhi ya timu za mikoa ya Mara na Ruvuma kukata rufaa baada ya kutoridhika na uamuzi uliotolewa na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kutokana na timu ya Mara kudaiwa kuchezesha mchezaji ambaye hakukidhi masharti ya mashindano na Ruvuma kudai kuwa Lindi ilichezesha wachezaji wa aina hiyo pia. Rufaa hizi zinasikilizwa na TFF.
   Baadhi ya magazeti yanaandika kuhusu suala hilo na pia vituo vya redio na TV vinarusha habari zinazohusiana na suala hilo na baadhi kumhusisha mdhamini wa mashindano hayo na masuala ya kiufundi ya mashindano hayo.
   Executive Solutions, tukiwa wakala wa TBL kuratibu masuala ya habari katika mashindano haya, tunapenda kufafanua kwamba Kilimanjaro Premium Lager haihusiki kabisa na masuala ya kiufundi ya mashindano haya. Mashindano yanaratibiwa na TFF kwa asilimia mia moja.
  Kama kuna jambo lolote munahitaji kufahamu zaidi, nawaomba wanahabari wenzangu musisite kuwasiliana na TFF au Executive Solutions kwa ufafanuzi zaidi.
   Nitawatumia taarifa kamili kuhusu mashindano haya mara baada ya TFF kutoa uamuzi kuhusu rufaa mbili zilizotolewa. Bado wanaendelea na kikao.

Natanguliza shukrani,

Michael Mukunza
Media Manager
Executive Solutions Ltd
P.O. Box 1601, Dar es Salaam
Mobile: 0784/0776/0767978302 or 0714683451

MAKAMBA AZUNGUMZIA MASAUNI KUJIUZULI UVCCM, AKUTANA NA BALOZI WA ZIMBABWE HAPA NCHINI

May 21, 2010

KATIBU Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba akizungumza na waandishi wa habari, katika ukumbi wa sekretarieti, Ofisi Ndido ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Francis Mwonga. Pamoja na mambo mengine amezungumzia kuhusu kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Sauani hamad Masauni na CCM ilivyojipanga katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.BALOZI wa Zimbabwe hapanchini, Meja Jenerali, Edzai Chimonyo akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, baada ya mazungumzo yao, Ofisi kwa Katibu Mkuu, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumba Dar es Salaam.
ยช