Breaking News

Your Ad Spot

May 14, 2010

MAKALA YA KILI TAIFA CUP, IRINGA

 JUMATANO wiki hii michuano ya Kombe la Taifa (Kili Taifa Cup), hatua ya makundi ilimalizika katika vituo vyote sita vilivyoshirikisha timu za mikoa  26 yote (ya kisoka kwa mujibu wa mashinsano hayo) Tanzania Bara.

Iringa ni miongoni ma vituo hivyo sita ambako michunao hiyo ilirindima ikizikutanisha timu za Mbeya (Mapinduzi Stars), Rukwa (Pinda Boys), Kinondoni Kombaini ya Kinondoni jijini  Dar es Salaam, na wenyeji Iringa (Ruaha Stars).

Vitui vingine ambako michuano hivyo ilipigwa ni Arusha, Dodoma, Mtwara, Mwanza na  Tanga na baada yakumalizika raundi hiyo tayari timu nane zimefuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo iliyopangwa kuanza  Mei 22, 2010 katika Uwanja a Uhuru mjini Dar es Salaam.

Timu zilizotinga robo fainali ni Iringa, Arusha, Mwanza, Singida, Temeke na mabingwa a mwaka jana wa kombe hilo Ilala ambayo bila shaka itajitutumua kufanya kila iwenzavyo kuweza kulitwaa tena kombe hilo pamoja na donge la sh. milioni 35 zilizotengwa na wadhamini wa michuano hiyo, Kampuni ya BIa Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager , kwa mshindi wa kwanza.

Na ikiwa itashindwa kutwaa ubingwa pengine ikijitahidi itazeza kushika walau nafasi ya pili yenye zawadi ya sh, milioni 20 au ya tatu ya sh. milioni tano ambayo bila shaka haitafurahiwa sana na timu hiyo kwa kuzingatia kuwa ndiyo bingwa mtetezi.

Kwa ajili ya knogesha michuano hiyo mbali na kwamba mshindi wa kwanza hadi wa tatu TBL imewatengea zawadi nono, pia kutoka timu hizo zilizofanikiwa mojawapo itakayoibika kuwa yeneye nidhamu itajipatia sh. milioni 2.

Kadhalika katika timu hizo watatokea kipa na mchezaji bora ambao kila mmoja atajinyakulia sh. milioni 2, huku mmoja kati ya makocha wa timu hizo atakayeonekana kuwa ni kiboko ya wote akipata pia sh. milioni hizo mbili na mwamuzi bora naye akitia kibondoni kisi kama hicho cha fedha.

Yapo mambo kadhaa yaliyojiri katika michuano hiyo katika vituo vyote, lakini mwandishi wetu ataungumzia zaidi kituo cha Iringa ambako alikuwa katika kipindi chote tangu michuano inaanza.

Moja ya mambo yaliyojitokeza ni kuonekana kwa vipaji vingi vipya vikionyesha ushindani na wachezaji wa siku nyingie waliocheza zamani Ligi Kuu ya Tanzania Bara na wale ambao hadi sasa wanaendelea kuchezea timu za ligi hiyo.

Moja ya timu zilizokuwa na wachezaji walioonyesha vipaji ni Rukwa (Pinda Boys) ingawa haikuweza kufanikiwa kuingia robo fainali na pia kuwa iliyoongoza kwa kufungwa mabao mengi huku ikimaliza miichuano bila kupata bao walau moja.

Wachezaji kama Onesmo Isaya na kipa Sood Fauz walionyesha uchezaji wa hali ya juu, kiasi kwamba Isaya aliweza kuibuka mchezaji bora, katika mechi ambayo timu hiyo ilicheza na Iringa na kujipatia sh. 50,000 zilizokuwa zikitokitolewa na TBL kwa kila mchezaji bora wa kila mechi.

Ni bahati mbaya tu kwamba timu hiyo licha ya kuwa na soka safi, ilikwama zaidi katika umaliziaji hivyo ikajikuta kila mechi inaondoka bila mabao, licha ya kushambulia lango la wapinzani ikiwemo kupata kona ambapo katika mechi yake na Iringa iliweza kupata kona tatu lakini zote ikala hola.

"Tumemaliza tukiwa tumefungwa.. huu ni mchezo lakini kwa kweli wachezaji wangu ni wazuri tu isipokuwa upande wa umaliziaji ndiyo tatizo, na hii ni changamoto hasa ukitazama kwamba timu tulizocheza nazo nyingi zilikuwa na wachezaji wazoefu waliocheza na wanaocheza Ligi Kuu", alisema kocha wa timu hiyo Heri Chibakasa baada ya mechi ya timu hiyo na Iringa iliyomalizika kwa kuchapwa mabao 6-0.

Wakati timu ya Mbeya ilikuwa na mchezaji aliyewahi kuchezea Ligi Kuu kama Mwaikimba aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga, Iringa ina wachezaji wa ligi hiyo watano, wawili kutoka Yanga kina Godfrey Bon na Athumani Idd 'Chuji' ambapo waliweza kuifanya timu hiyo kug'aa katika hatua hiyo ya makundi na kufuu kucheza robo fainalio ikiwa na poiti 7 kwa kufunga mechi mbili na kutoka suluhu mechi moja ambayo ilikuwa kati yake na Kinondoni.

Wengine katika timu hiyo ni Kipa Odo Nombo wa Manyema Rangers, Salum Swedi (Mtibwa Sugar) na Yona Ndabila wa Moro United, huku Kinondoni nayo ikiwa nao pia wengi akiwemo mchezaji wa zamani wa Simba Sunday Frank.

UBORA  

Kismngi michuano ilifanyika kwa maandalizi mazuri, lakini bila shaka ni kutokana na wadhamini kuwa na nia thabiti kuhakikisha michuano hiyo inafanyika katika upangilio uliopangwa na kwa ufanisi uliotarajiwa.

Hii inatokana na kwamba kwa mfano katika kituo cha Iringa TBL ilihakikisha mara tu timu zilipowasili zinapatiwa huduma zote ikiwemo usafiri , malazi na vifaa na hadi michuano inafikia tamati hakuna malalamiko yaliyokuwa yamejitokeza kuhusu masuala hayo.

Kadhalika malipo yote ikiwemo ya wachezaji bora kwa kila mechi ambayo ni sh. 50.000 alipata kila mchezaji tena kwa wakati.

Timu zilionekana nadhimu uwanjani kutokana na jezi zilizo bora ambazo zilionesha namba mgongoni na kifuani na pia katika bukta zilionekana namba kwa mbele jambo ambalo halijawahi kutokea kwa timu za hapa nchini hata katika Ligi Kuu na ikitokea ni mara chache sana.

Kwa upande wa jezi TBL bila shaka iliweza kugawa jezi zilizokamilika mahitaji kisi hicho kutokana na kusikiliza maoni ya wadau ambao yalitolewa wakati wa semina ya waandishi wa habari za micheza iliyofanyika Kigamboni mwanzoni mwa maandalizi ya michuano hiyo.

Sasa kilichosalia ni kusubiri ni nini au ubora gani utaonekana katika robo fainali na faina zenyewe zitakazorindima Dar es Salaam.

Bilashaka

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages