.

MTEMVU AMALIZA UBUNGE KWA KUZINDUA MRADI WA MAJI JIMBONI KWAKE LEO

Jul 31, 2010

Mbunge wa zamani wa Temeke, Abass Mtemvu akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Mtoni Relini, Hadija Mohamed, alipozindua kizima cha maji katika eneo hilo jana. Kisima hicho kimejengwa kwa mchango wa juhudi zake kwa gharama y ash. Milioni 19. (Na Mpigapicha wetu

MAOFISA MAUZO TIGO WAPATA MAFUNZO

Meneja wa Kanda wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo Brahim Gutierrez akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uuzaji wa bidhaa za kampuni hiyo, Jamal Balemba, katika sherehe ya kutunuku vyeti kwa maofisa mauzo waliohitimu mafunzo hayo, iliyofanyika katika Ofisi mpya za Tigo, Buguruni mjini Dar es Salaam. Kushoto ni mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Empower, iliyosimamia mafunzo hayo, Miranda Naiman.

CORPORATE GOLF DAY 2010

Jul 29, 2010

Hii ni kuwahabarisha kuwa, siku ya jumamosi ya tarehe 31 kutakuwa na Press conference itakayofanyika viwanja vya Gymkhana club,posta.

Press conference hii inahusu Corporate Golf Day, itakayofanyika tarehe 14 ya mwezi wa nane, palepale Gymkhana,ikiwahusisha wafanyakazi wa makampuni mbalimbali watakaoshindana katika mchezo wa golf.

Vilevile, Kutakuwa na zoezi la mnada wa vitu mbalimbali kama vyumba vya kulala pale Movenpick, Harbour View na Kempinski,...modem za internet, tiketi za ndege, na Live cooking BBQ itakayoandaliwa na Hillside Hotel, Bagamoyo. Mapato ya mnada huu yatapatiwa kwa Gymkhana Golf Club kwa ajili ya kuandaa mazoezi na mafunzo ya golf kwa watoto na vijana wanaocheza Golf.

Watakaoongea katika press conference hii ni Oscar Shelukindo-TBL, Emillian Rwejuna- Precision Air, Mr. Nyirabu- Mwenyekiti wa Dar Gymkhana Club, na Mariam Ndabagenga- Muandaaji wa shughuli hii kupitia Brand Image Ltd.

Wote mnakaribishwa,

Ahsante

Mariam Iddi Ndabagenger
Marketing Manager
Brand Image Ltd
+255 713 299 678
+255 787 028 658
mariam.ndaba@gmail.com

MWANDISHI WA HABARI AFARIKI DUNIA DAR

Jul 27, 2010

Aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Primtiva Pankrasi (Pichani), amefariki dunia.
Taarifa zilizofikia Blogu ya Chachandu Daily, zimethibitisha kwamba mwandishi huyo alifariki jana mchana katika hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lugali ya mjini Dar es Salaam, alikokwenda kwa ajili ya matibabu ya kawaida ‘Check up’. Imeelezwa kuwa baadaye alipatwa na presha ya ghafla na kupoteza kufariki muda si mrefu.

JK MEETS GADDAFI IN KAMPALA

President  Jakaya Mrisho Kikwete meets Libyan Leader Col.Muammar Gaddafi  at  Kampala Munyonyo international Conference centre during the on  going 15th African union summit yesterday evening (PHOTO BY FREDDY MARO)

MAMA JK NDANI YA KAMPALA

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  akizungumza na mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Mama Azeb Meefin Zenawi wakati  nwa kikao cha wake wa marais na wakuu wa nchi za Afrika kinachofanyika sambamba na kikao cha marais na wakuu wa nchi za Afrika huko Speke hotel, eneo la26.7.2010 Munyonyo, Kampala nchini Uganda tarehe 26.7.2010.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akichangia akichangia wakati wa kikao cha wake wa marais na wakuu wa nchi za Afrika kinachofanyika Kampala nchi Uganda.
Mama Salma Kikwete akifuatana na mke wa Rais wa Sierra Leone Mama Sia Nyama Koroma (katikati),na Kulia ni Mama Azeb Zenawi, mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia wakitoka nje kwa mapumziko mafupi tarehe 26.7.2010.PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI

PRESIDENT KIKWETE IN KAMPALA FOR THE 15th AU SUMMIT

Jul 26, 2010

President  Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete receive bouquet of flowers upon arrival in Kampala for the 15th African Union Summit this yesterday.

MTAALAM WA KODI AMINA MKUMBA AOMBA KUWANIA UBUNGE KIBITI, RUFIJI MKOA WA PWANI: AKIPITA ATAKUWA MWANAMKE WA KWANZA KUTOKA ENEO HILO KUWA MBUNGE, BAADA YA BIBI TITI MOHAMMED

Jul 23, 2010

MSOMI wa masuala ya Usimamizi wa kodi, Kada wa CCM Amina Mussa Mkumba (29) akirejesha fomu yake ya kuwania Ubunge jimbo la Kibiti, wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani, jumatano wiki hii, kwa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Joseph Pandisha. Amina ambaye ni msomi mwenye Stashahada ya Uzamili ya usimamizi wa Kodi, akichaguliwa atakuwa mwanamke wa pili kuwa mbunge katika wilaya hiyo, baada ya aliyekuwa mwanasiasa mashuhuri nchini, marehemu Bibi Titi Mohammed aliyekuwa wa kwanza.


STORI

MSOMI wa masuala ya usimamizi wa kodi  Amina Mussa Mkumba (29), amejitosa kuwania ubunge jimbo la Kibiti, wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani,  kwa tiketi ya CCM.

Akizungumza na baada ya kurejesha fomu yake ya maombi kwa Katibu wa CCM Wilaya  hiyo, Joseph Pandisha, alisema, ameigia katika kinyang'anyiro hicho kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuweka rekodi ya kuwa mwanmke wa pili kuwa mbunge wa jimbo hilo, baada ya aliyekuwa mkongwe wa siasa nchini, Bibi Titi Mohammed aliyekuwa wa kwanza katika wilaya hiyo.

Msomi huyo mwenye stashahada ya juu (Advanced Diploma) na Stashahada ya Uzamili,(Post graduate Diploma) alizopata katika Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam, alisema, pia lengo lake ni kuitika mwito wa Rais Jakaya Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa kuwataka wanawake nchini kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

"Kimsingi nina malengo mengi, lakini baadhi yake ni la kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa pili kushina Ubunge hapa U-ndengerekoni, baada ya Mama yetu, Bibi Titi Mohammed aliyekuwa wa kwanza ambapo baada ya yeye hajatokea tena mwananamke mwingine kushika ubunge", alisema na kuongeza, "tena nafanya hivi kwa kuwa naunga mkono mwito wa Rais wetu, na Chama Cha Mapinduzi kwamba wanawake tujitokeze kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi'.


Amina alisema mwanamke anayeacha kujitokeza kuwania uongozi wakati anaona ana uwezo wa kufanya hizo, ni kama anapuuza mwito wa Rais Kikwete na Chama Cha Mapinduzi, jambo ambalo si sahihi.

Mbali na Amina, pia wamejitokeza wana-CCM kadhaa kuwania ubunge wa jimbo hilo akiwemo mbunge za zamani aliyemaliza muda wake, Abdul Marombwa anayetetea kurejea tena.

Chachandudaily Blog  inamtakia kila la kheri katika kusaka nafasi hiyo

VODACOM FOUNDATIONSYAFANYA MAMBO DAR

Jul 22, 2010

Pichani  kutoka kulia ni Afisa Habari   Kutoka  kampuni ya mwanamitindo  Mustafa Hassanali  ajulikanae Hamis Omary, Mbunifu Mustafa Hassaanali, Afisa Habari wa Mfuko kutoka VODACOM Yessaya Mwakifulefule, Afisa habari kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Joseph Ishengoma. Picha na Mwanakombo Jumaa (MAELEZO. )
Tanzania Information Services
P.O.Box 9142
Dar es salaam
Tel.+255 754 479 639

DUDUMA,MADEGA NA KAWAMBWA WAREJESHA FOMU ZA KUOMBA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM


KADA wa CCM, Nassoro Duduma (kulia) akimkabidhi fomu yake ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani, Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo Fikirini Masokola, aliupoirejesha jana katika Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, baada ya kukamilisha kuijaza.  Jumla ya wana-CCM tisa wamejitokeza kuomba nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Imani Madega (kulia) akimkabidhi fomu yake ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani, Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo Fikirini Masokola, aliupoirejesha jana katika Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, baada ya kukamilisha kuijaza.  Jumla ya wana-CCM tisa wamejitokeza kuomba nafasi hiyo.

KADA wa CCM, Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) akimkabidhi fomu yake ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Bagamoyo  mkoa wa Pwani, Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo Fikirini Masokola, aliupoirejesha jana katika Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, baada ya kukamilisha kuijaza.  Wanachama wengine wawili, Emmanuel Patuka na Andrew Kasambala wameomba nafasi hiyo.

PROFESA MWAIKUSA AZIKWA LEO

Jul 17, 2010

LOFEA Mwaikusa (wapili kushoto) akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mumewe, Profesa Jwani Mwaikusa, kabla ya maziko yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Mbezi Salasala, Dar es Salaam,jana. Profesa Mwaikusa aliyekuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliuwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake na watu wanaoaminika kuwa ni majambazi, Jumanne wiki hii. (Picha na Bashir Nkoromo).

MHADHIRI MWANDAMIZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KITIVO CHA SHERIA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI DAR

Jul 14, 2010

MESSAGE OF CONDOLENCE
Late Prof. Jwani Mwaikusa

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwa majozi kuhusu msiba huo  Nyumbani kwa marehemu Profesa Mwaikusa, Salasala, Dar es Salaam. Mbele ni gari alimopigiwa risasi na  wauaji, mara alipowasili nyumbani hapo saa nne usiku, jana. Polisi wakifanya uchunguzi eneo la tukio, nyumbani kwa marehemu leo Kiatu cha marehemu, Profesa Mwaikusa kilichobaki eneo la tukio baada ya kuuawa. Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu leo asubuhi. POLISI wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakipata maelezo nyumbani kwa mfanyabiashara aliyeuawa wakati akienda kutoa msaada nyumbani kwa Profesa Mwaikusa.


The Vice Chancellor Professor Rwekaza Mukandala expresses shock and deep grief at the sudden and untimely death of Prof. Jwani Mwaikusa of the University of Dar es Salaam School of Law (formerly Faculty of Law), which occurred reportedly after he had been assaulted by an armed gang at his residence in SalaSala, late on July 14th, 2010. He is survived by his widow and their four children.
   On behalf of the Management, the Vice Chancellor sends solemn condolences to the spouse of the late Prof. Mwaikusa, his entire family and friends, the Dean of the University of Dar es Salaam School of Law, colleagues and the University of Dar es Salaam family in its entirety. Prof. Mukandala prays for strength and calm at this moment of deep grief.
     Prof. Jwani Mwaikusa joined the University of Dar es Salaam in July, 1986 as Assistant Lecturer in the then Faculty of Law. Before that date he had been a State Attorney and Assistant Lecturer at the IDM, Mzumbe. In subsequent years and decades the late Mwaikusa rose through the ranks, and was in July 1999 promoted to the status of Associate Professor of Law.
     His distinguished services at the University of Dar es Salaam include Headship of the Department of Constitutional and Administrative Law (three different triennia including the current one), membership of the University of Dar es Salaam Legal Aid Committee (1988-1992), and Chairmanship of the same committee (1992). He has also been the Lead Counsel for the Defence, UN-International Criminal Tribunal for Rwanda (2007 to-date) and Chairman of the Centre for Media Studies, Research and Networking (2002 to-date). The late Prof. Mwaikusa has published numerous articles and book chapters on a wide range of subjects. He has also been a good poet.

MAY HIS SOUL REST IN ETERNAL PEACE

ZIF MOTOMOTO Z'BAR

Jul 12, 2010

DK. MOHAMMED GHARIB BILAL MGOMBEA MWENZA WA JK

MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Waziri Kiongozi mstaafu, Dk.Mohammed Gharib Bilal baada ya kumtangaza kuwa mgombea mwenza wake wa urais, jana katika ukumbi wa Kizota mjini Dodoma. Hiyo ilikuwa ni baada ya yeye (JK) kuthibitishwa na kutano mkuu wa CCM kwa  kura 1,893 kati ya 1,909 zilizopigwa.
   Awali Dk. Bilal alikuwa akiwania nafasi ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, lakini yeye na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha wakashindwa na Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Sheni.

HISPANIA YABEBA KOMBE LA DUNIA

Ni baada ya kuifunga Uholanzi 1-0 katika mechi ya fainali
Wachezaji wa Hispania wakishangilia baada ya timu yaoa kutwaa Ubingwa Kombe la Dunia 2010

JK APITA KUWA MGOMBEA WA URAIS KWA TIKETI YA CCM

Jul 11, 2010

Habari zilizopatikana dakika mbili zilizopita, zilizotangazwa na makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Amani Abeid Karume, Rais Kikwete aameshinda kwa asilimia 99.16 ya kura  za ndiyo na za hapana ni asilimia 0.84

UCHAGUZI KUMTHIBITISHA JK KWA MGOMBEA WAFANYIKA MCHANA HUU

 
MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha mkutano mkuu leo asubuhi katika ukumbi wa Kizota mjini Dodoma 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Mzee Makamba na Mzee Kingune Ngombale-Mwiru katika ukumbi wa Kizota wakati wa mkutano huo mjini Dodoma.
Rais Kikwete akijipigia kura, wakati wa uchaguzi uliofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM kumthibitisha au kumkataa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM leo. Wengine ni Waziri Kiongozi Shamsi Vuai nahodha, Mgombea mteule wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Makamu wa Rais Dk. Sheni na waziri Mkuu, Mizengo Pinda. (Picha zote na Freddy Maro)

MGOMBEA MWENZA KUJUKLIKANA LEO BAADA YA JK KUPITISHWA

KITENDAWILI cha nani kuwa mgombea mwenza wa Rais Jakaya Kikwete kinateguliwa leo hatua itakayofuata baada ya Jk kupitishwa rasmi na kikao cha NEC ya CCM mjini Dodoma.Dodosa za vyombo vya habari zinawapa shavu mmoja kati ya Waziri wa fedha wa zamani Zakia Meghji, Waziri Kiongozi aliyekuwa anawanaia kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar, Nahodha au Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais, anayeshughulikia Muungano Mohammed Seif Khatib.

KINONDONI YATWAA UBINGWA COPA COCACOLA

Jul 10, 2010

NAIBU Waziri wa habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Kinondoni, Habibu Khalfan, kufuatia timu hiyo kuibuka bingwa wa michuano ya Copa Cocacola ya vijana chini ya miaka 17, baada ya kuinyukaa mabao 2-0 timu ya Temeke, katika mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, jana. (Picha na Emmanuel Ndege).

RASHID MATUMLA KUNG'UTANA NA MADA MAUGO, JULAI 18, 2010

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Eng. Dr. James Alex Msekela kutokana na ajali mbaya ya barabarani iliyotokea tarehe 9 Julai, 2010 na kusababisha, vifo vya watu 15 na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa katika kata ya Mnenia baada ya lori walilokuwa wakisafiria kwenda mnadani kupinduka.

“Ni kwa majonzi na huzuni kuu, kupitia kwako wewe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ninawapa pole za dhati kabisa familia zilizopotelewa na ndugu zao katika ajali hiyo mbaya. Ninawahakikishia kuwa nipo pamoja nao katika msiba huu mkubwa na namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema aziweke mahali pema peponi roho za marehemu wote, Amina”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake hizo.

Aidha, Rais Kikwete amesema anamuomba Mwenyezi Mungu awawezeshe watu wote waliojeruhiwa katika ajalai hiyo kupona haraka ili waungane tena na ndugu, jamaa na marafiki zao na kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Rais Kikwete ameendelea kuzisisitizia mamlaka zinazohusika na masuala ya usalama barabarani kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao, kwani mojawapo ya sifa nzuri za mamlaka hizo ni uwezo wao wa kupunguza kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani au ikiwezekana kuondokana nazo kabisa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,


DAR ES SALAAM.

10 Julai, 2010
Telephone: 255-22-2114512, 2116898, E-mail: press@ikulu.go.tz, Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,


DAR ES SALAAM.
Tanzania.

GENEVIVA ATWAA TAJI MISS TEMEKE 2010

Miss Temeke 2010 Geneviva Emmanuel akiwa na mshindi wa pili Anna Daudi (kulia) na Pendo Urassa mshindi wa tatu

DK SHENI APITA KUWA MGOMBEA URAIS Z'BAR KWA TIKETI YA CCM

Hatimaye Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Sheni amepita kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu baada ya kuchaguliwa kwa kura 117  na kuaacha mbali waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal aliyepata kura 54 na waziri Kiongozi wa sasa,  Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 33, katika uchaguzi wa kinyang'anyiro hicho uliofanywa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa taifa (NEC) ya CCM  jana usiku katika ukumbi wa Kizota mjini Dodoma.

Dk. Sheni amepenya baada ya kuingia wakiwa watatu waliopenya awali katika mchujo wa Kamati Kuu wa CCM lakini akiwa pia katika wale watano waliokuwaa wamependekezwa na Kamati maalum Zanzibar, kati ya jumla ya makada 11 waliochukua fomu na kuzirejesha kuwania nafasi hiyo inayoachwa ana rais wa sasa Amani Abeid Karume.Dk Ali Mohammed Sheni akizungumza baada ya kuchaguliwa
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Dk. Shein baada ya ushindi wake. Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Dk. Gharib Bilal kwa kukubali matokeoBaadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao cha NEC. Kushoto ni Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha aliyekuwa akiwania nafasi hiyo.

KUTOKA KIZOTA

Jul 9, 2010

MWENYEKITI wa CCM Rais jakaya Kikwete akiongoza kikao cha kamati kuu ya CCM
Wawaniaji wa Urais wa Zanzibar, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai nahodha na makamu wa Rais Dk Sheni wakisalimiana nje ya ukumbi wa Kizota

URAIS Z'BAR: MCHUANO SASA NI DK. SHENI, DK. BILAL NA NAHODHA

Habari ilizotua bloguni hapa midamida hii, ni kwamba majina ya wana-CCM hao kati ya wale 11 waliokuwa wamechukua fomu kuwania 'ulaji' huo kwa ridhaa ya CCM wamebaki Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, Waziri Kiongozi, Kaka Shamsi Vuai Nahodha na Waziri Kiongozi mstaafu Mzee, Dk. Gharib Bilal.
  Awali kamati maalum ya CCM Zanzibar, ilipeleka majina ya watano pale Dodoma, lakini kikao cha leo asubuhi cha Kamati Kubwa kabisa yaani CC ya CCM  kilichukua yote kuyashughulikia.
DK. SHENI
 
DK. BILAL
NAHODHA
    *****Hivi sasa kikao cha NEC ya CCM ndiyo kipo shughulini kuchagua mmoja tu kati ya hao watatu waliopenya katika mchujo wa Kamati Kuu ya CCM.

KIZOTA SASA KWAIVA

Jul 8, 2010

KATIBU Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba (kushoto)m akimwelekez kitu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Uchumi na Fedha, Amos Makalla, walipokagua ukumbi wa Kizota, mjini Dodoma utakaotumika kwa mkutano mkuu wa CCM, leo

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiakagua ukumbi wa Kizota mjini Dodoma, jana Kulia ni Makamba na wapili kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Abduklrahman Kinana.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto), akisalimiana na Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Uchumi na Fedha, Amos Makalla, alipowasili ukumbi wa Kizota, jana. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba na watatu kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Oganaizesheni, Kidawa Hamid
VIJANA wa CCM wakibandika picha za Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwenye uzio kuzunguka ukumbi wa Kizota,leo.

MAELFU WAKOSA FIESTA MORO BAADA YA TIKETI KUISHA

*Waandaaji walikadiriwa tiketi 20,000, lakini zikaisha
*Wakauza hadi vishina lakini watu wakawa bado nyomi nje
TAMASHA la Fiesta mwaka huu limeanza kwa kishindo baada ya onyesho lake la kwanza lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kufurika maelfu ya watu huku mamie wengine washindwa kuingia kutokana na kumalizika tiketi.

      Hadi kufikia saa 12 jioni uwanja ulikuwa umefurika maelfu ya watu wengi wao wakiwa ni vijana na watoto, na mamia ya watu wengine walibaki wakisikilizia nje baada ya kushindwa kuingia licha ya kwamba walikuwa na fedha za kiingilio.
      Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Ruge Mtahaba alisema, idadi ya tiketi zilizokuwa zimekadiriwa zilimalizika, hadi wakalazimika kuuza hadi vishina vya tiketi walizouza awali lakini bado mamia ya watu waliendelea kujazana mlangoni wakitaka tiketi.
      Onyesho lilianza saa 8 mchana kwa wasanii mbalimbali wa mjini Morogoro, kutoa burudani, hadai saa 1.30 onyesho lilipoanza rasmi kwa kupaanda wasanii mahiri waliopagawisha mashabiki vilivyo.
      Wasanii hao ni Joe makini, Fid Q, kundi la Tip Top Connection kutoka Manzese, Mwana FA, kundi zima la THT, Kalapina, Diamond, B elle 9, Mwasiti, Hussein Machozi Godzila, Jcb, Juma Nature, Chege na Temba.
      THT ndiyo walionyesha kukonga zaidi nyoyo za mashabiki, baada ya kuonyesha umahiri wao walipopanda jukwaani na kulisakata vilivyo sebene linalotamaba katika anga la muziki hapa nchini la 'Ala G'.
     "sasa hapa kiingilio chetu kimekwenda kihalali, maana vijana hawa wanajituma si mchezo", alisikika shabiki mmoja aliyekuwa miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliokuwa wakaishangilia THT walipomaliza 'kukamua'.
     Baada ya fungua dimba kwa onyesho hilo, maonyesho mengine la Fiesta inaroratibiwa na kampuni ya Prime Time Ptomotions na kudhaminiwa na bia ya Serengeti, yatarindima katika mikoa mingine ikiwemo ya Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.
 
Logo ya FIESTA 2010
Jukwaa likiwa limefurika mashabiki saa nane mchana kabla ya shoo kuanza
Tangazo la Vitamalt Plus, moja ya matangazo ya kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wadhamini wa Fiesta, likiwa katika uwanja huo wa Jamhuri.
Wadau wakiendelea kumiminika kuingia uwanjani
Wadau wakiwa katika foleni ya tiketi

Maelfu ya wadau ndani ya 'nyumba'
Mmoja wa mashabiki akiwa amembeba mtoto wake apate naye kuona uhondo uliokuwa ukiendelea
Watu mzukaaaaa
Mama huyu mwenye mtoto akiingia na mwanae kufaidi mambo
Jamaa akajifanya mjuaji akakutana na ulinzi mkali wa polisi uliokuwepo 
"Kaka hii kamera kiboko" inaelekea ndivyo alivyokuwa anasema huyu jamaa wa Clouds tv alipoijaribu kamera ya Michuzi Jr (kushoto)
Mzee wa Mabagala (mwenye tai) akiwa na baadhi ya wasanii kabla ya kuanza ' ukamuaji'
MMOJA wa mashabiki waliohudhuria onyesho la Fiesta lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Cuthbert Aloyce, akionyesha umahiri wake wa kucheza 'sebene' aliposhindanishwa na wenzake wanne kusakata muziki jukwaani. Aloyce aliwashinda wenzake na kupata zawadi ya sh. 20,000 na kugharamiwa kila kitu na waandaaji kwenda katika Fiesta itakayofanyika dar es Salaam. Maonyesho ya Fiesta yanaratibiwa na Prime Times Promotions kwa udhamini wa bia aya Serengeti inatotengenezwa na kampuni ya bia hiyo hapa nchini (SBL).
Vijana wa Offside trick wakikamaua na 'pole samaki'
Wakamuaji kutoka Tip Top Connection wakiwajibika
Ma-repoter nao muhimu, walikuwepo tele ndani ya nyumba!  
ยช