.

KARUME AFUNGUA MKUTANO WA MAJAJI NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KUHUSU MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI KATIKA UKANDA HUO NA UHALIFU WA KIMATAIFA, LEO KATIKA HOTELI YA GOLDEN TULIP DAR ES SALAAM

Aug 31, 2010

.JAJI Kiongozi, Fakih Jundu (kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar, Hamid Mahamoud Hamid na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dk. Stephen Bwana (kulia) wakijadili jambo nje ya ukumbi wakati wakimsubiri Rais wa Zanzibar, Dk. Abeid Amani Karume kuwasili kwa ajili ya kufungua mkutano wa majaji wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi katika ukanda huo na uhalifu wa kimataifa, jana uliofanyika jana katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam
RAIS wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, akifungua mkutano wa Majaji wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi katika ukanda huo na uhalifu wa kimataifa, jana, katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam. Kulia ni Jaji Mkuu, Augustine Ramadhani. .

MUFT WA ZANZIBAR AZIKWA LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,(wa tano kushoto)alijumuika na Viongozi wengine katika swala ya Maiti ya Marehemu Mufti Mkuu wa Zanzibar,Sheikh Harith Bin Helef,katika Msikiti wa Mwembeshauri leo.

DK KARUME AFUNGUA LEO MKUTANO WA KUPANBANA NA UGAIDI NA UHALIFU WA KIMATAIFA, GOLDEN TULIP, DAR ES SALAAM

BAADHI ya majai wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, wakimsubiri Rais wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, kufungua mkutano huo leo.

JK NDANI YA MPANDA

Aug 29, 2010


MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dk.Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwakiwaqpungia mikono waelfu ya wananchi walihudhuria mkutano wa kampeni ulifanyika katika mji wa Mpanda koani Rukwa juzi. (Picha na John Lukuwi).
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dr. Jakaya Kikwete akimbeba kwa bashasha mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, alipowasili katika Uwanja wa michezo wa mjini Mpanda ambako alihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni jana.
WAKAZI wa mji wa Mpanda, wakimkaribisha kwa mabango mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dr.Jakaya Kikwete, alipowasili mjini humo jana.(picha zote na Freddy Maro)

MAMA SALMA ATUA MBEYA KULONGA KWA KARIBU NA KINA MAMA WA UWT

MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, akifurahia vikundi vya ngoma za asili, alipowasili unwanja wa ndege mjini Mbeya, juzi kwa ajili ya kuzungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuhusu umuhimu wa Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) mkoa Mbeya, Fatma Tawfiq, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Mbeya, juzi. (katikati ni) ni mkuu wa mkoa huo, James Msekela.(Picha zote  na Mwankombo Jumaa-MAELEZO).

KAMPENI UCHAGUZI MKUU

Aug 28, 2010

CHADEMA wadaiwa kuzusha tafrani za kutaka kumdunda mtangazaji wa TBC 1.

Uzindunzi wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, umeingia
dosari baada ya wafuasi wa chama hicho kutaka kumpiga mtangazaji wa TBC1, Marin Hassan Marin.
   Habari kutoka viwanja vya Jangwani, zilisema kwamba, katika mkutano huo uliohutubiwa na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Dk. wilbroad Slaa (pichani akihutubia mkutano huo), wafuasi wa Chadema wanadaiwa ukumvamia mtangazaji huyo na kumtia msuokosuko baada ya kukatishwa ghafla matangazo ya mkutano huo yaliyokuwa yakirushwa moja akwa moja 'live' na kituo hicho.
     Akizungumzia katika taarifa ya habari saa saa 2 usiku huu, Mkurigenzi wa TBC, Tido Mhando alisema, kituo kililazimika kukatiza matangazo hayo kutokana na baadhi ya viongozi kuanza kutoa maneno ya kukashifu mtu binafsi badala ya kunadi sera.

KAMPENI UCHAGUZI MKUU:

DK. SLAA  KUZINDUA KAMPENI ZA CHADEMA LEO 
Wafuasi wa CHADEMA wakiandamana kutoka katika viwanja vya Kidongo Chekundu, Dar es Salaam, mchana huu, kwenda kwenye viwanja vya Jangwani katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho utakaofanywa punde na mgombea wake, Dk. Wilbroad Slaa.
================================================
JK yupo Kigoma, mgombea mwenza wake Mtwara.
Kwa picha za kina bofya:- http://www.issamichuzi.blogspot.com/ na http://www.sufianimafoto.blogspot.com/ 

STARS YAONGEZA WAPYA

PULSEN ATEMA WAKONGWE WATANO STARS SAFARI YA ALGERIA

Aug 27, 2010

WACHEZAJI wakongwe watano na wawili wa timu ya taifa, Taifa Stars wameachwa na kocha Jan Paulsen katika kikosi kitakachokwenda Algeria katika mechi iliyopangwa kuchezwa septemba 3, mwaka huu nchini humo.

Walioachwa ni Kipa Juma Kaseja, Athumani Iddi na athumani Iddi kutokana na kuwa wagonjwa wakati wachezaji wengine akiwaachwa kocha huyo kwa kudaiwa kushuka viwango ambao nii Abdurahim Humudi, Kelvin Yondan, Juma Jabu, Uhuru Selemani na Jerrison Tegete.Kikosi cha Stars kitakachoondoka Agosti 31,mwaka huu kwenda Algeria kitakuwa na wachezaji 20.
KOCHA Pulsen timu yake ktakachokwenda Algeria.leo kwenye Ofusi za shirikisho la soka nchini (TFF). Kushoto ni Meneja wa timubya taifa Leopord Tasso.

KATIBA MPYA YAANZA KUFANYAKAZI KENYA

Ni baada ya kutiwa saini leo na Rais wa nchi hiyo, Mwai Kibai katika sherehe zilizofanyika mjini Nairobi.

DK BILAL ATINGA RUANGWA KUTAFUTA KURA ZA CCM

Aug 26, 2010

 Mgombea Mwenza Dk. Gharib Bilal, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa, wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika wilayani hapo leo Agost 26.

Akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili eneo hilo leo

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ILIYOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MANENO NILIYOYASEMA WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM MOSHI MJINI


Agosti 26, 2010

Taarifa kwa vyombo vya habari
Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa za kupotosha zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu uzinduzi wa kampeni za CCM Moshi Mjini, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Moshi Mjini Agosti 21, 2010 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, akiwemo Katibu wa Mkoa, Mzee Kazidi ambaye alikuwa mgeni rasmi. Pia alikuwepo Mgombea Ubunge (Moshi Mjini) kwa tiketi ya CCM, Bw. Justin Salakana, viongozi wa jumuiya mbalimbali za CCM, madiwani na wananchi.

Taarifa hizo zilizopotoshwa zilikuwa na nia kunichonganisha na chama changu na kumjenga Mbunge wa Moshi Mjini anayemaliza muda wake, Mh. Philemon Ndesamburo na kuonyesha kuwa mimi kada wa CCM, nina msimamo tofauti na Chama changu CCM.

Pamoja na mambo mengine, taarifa hizo ziliashiria kwamba katika mkutano huo wa hadhara, mimi, kada wa CCM, mbele ya viongozi wa CCM, katika mkutano wa kumnadi mgombea wa CCM, nilisema kuwa juhudi zilizofanywa na Ndesamburo zisibezwe na kwamba nilimjenga Ndesamburo wakati mimi nilikuwa nazungumzia mapungufu yake kwa kutaka kutofautisha kati ya uwezo wa mbunge anayetegemea nguvu zake binafsi na mbunge anayetokea kwenye chama tawala.

Ukweli ni kwamba nilimaanisha kuwa wananchi wa Moshi hawatapata maendeleo ya kweli bila serikali na nikatoa mifano nikasema, huenda Ndesamburo ameongeza madarasa matano katika shule tano lakini pengine mahitaji ya wilaya yalikuwa kupata shule tano kitu ambacho mbunge ambaye hayuko ndani ya chama tawala hawezi kufanya.

Mfano mwingine niliotoa ni kuwa huenda amefanikiwa kuongeza vyumba vitano katika zahanati tano za wilaya wakati mahitaji ya wilaya ni zahanati tano na sio vyumba vitano. Pia huenda aliweza kuchangia katika ujenzi wa kilomita moja ya lami lakini pengine mahitaji ya wilaya ni kilomita 31 za lami na ukizingatia kuwa kilomita moja inagharimu Shilingi Bilioni 1.5. Ni dhahiri kuwa bila mkono wa serikali, Ndesamburo anashindwa kukidhi mahitaji ya wananchi.

Nia na madhumuni ya ujumbe wangu ilikuwa kuwaeleza wananchi na wapiga kura wa manispaa ya Moshi kwamba ili tuondokane na umaskini na kukaribisha maendeleo na maisha bora kwa manufaa ya wananchi wa Moshi, ni vizuri wana CCM wa Moshi wawe wakweli na wajiepushe na kurubuniwa na wapinzani ili wauze kura ambayo ni sawasawa na kulia njaa na kulishwa pipi. Nawahisi wasifanye hivyo na badala yake wamchague Bw Justin Salakana kwa kumpa kura ili aweze kufanya kazi na serikali ya Chama tawala kinachoongozwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Niliwasihi wananchi wa Moshi kuwa wasipofanya hivyo, basi la maendeleo halitasimama Moshi na badala yake litaenda katika mikoa jirani kama vile Arusha, Tanga, Manyara, na mikoa mingine jirani.

Nimestushwa mno na taarifa potofu zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa mimi, Kada wa CCM, kwenye mkutano wa kuzindua kampeni na kumnadi mgombea wa CCM, mbele ya wana CCM, nimethubutu kusema kuwa jitihada za Ndesamburo zisibezwe wakati ni dhahiri kuwa Wilaya ya Moshi Mjini imerudi nyuma baada ya kushikiliwa na upinzania kwa miaka 15.

Ni wazi kuwa Ndesamburo ameshindwa kukidhi mahitaji ya wakazi Moshi na kuikosesha Moshi msukumo wa kiuchumi unaopatikana wakati kuna ushirikiano mzuri na serikali.

Nimesema nimestushwa na upotoshaji huu wa taarifa lakini sijashangaa maana naelewa mbinu zinazotumika sasa hivi Moshi Mjini kwani kuna watu maalumu waliopandikizwa wenye nia ya kumkashifu na kumharibia mgombea wetu Bw. Salakana. Watu hawa wamepandikizwa kwenye daladala, mabaa, viwanja vya michezo na vijiweni ili kueneza haya maneno yenye kashfa.

Yote haya ni kwa sababu ni wazi kuwa wananchi wa Moshi wamechoka na umaskini, ukosefu wa ajira na maendeleo kwa ujumla. Mwaka 2000 Ndesamburo alisema hatagombea mwaka 2005 lakini aliendelea na hata 2005 alisema hivyo kuhusu 2010. Wananchi wanalia njaa wanapewa pipi wakati haiuwi njaa.

Wapinzani walipewa miaka 15 ya kufufua uchumi wa Moshi na wameshindwa. Ni wazi kuwa bila kuwa na mbunge wa CCM Moshi Mjini wananchi wataendelea kukosa msukumo mkubwa wa kiuchumi kutoka kwa serikali.

Kuendelea kukalia kiti cha Jimbo la Moshi Mjini bila kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya wananchi ni sawa na mtu asiyekula nyama (vegeterian) kulinda friji lililojaa nyama na yeye mwenyewe hali na wala hataki wengine wale.

Muda umefika sasa wa wakazi wa Moshi Mjini kufanya maamuzi sahihi kwa kumchagua mgombea wa CCM, Bw. Justin Salakana. Wapinzani wamepewa dhamana kwa miaka 15. Wakazi wa Moshi wanasema, “Sasa mzee basi.”

Ahsanteni kwa kunisikiliza

Imetolewa na;

AGGREY MAREALLE

Kamanda UVCCM Moshi Mjini

DK. SHEIN ASAINI HATI YA KIAPO KUOMBA URAIS ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein kulia, akitia saini hati ya fomu ya kiapo ya kugombea Urais wa Zanzibar mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Hamid Mahamoud katikati, Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika leo Maisara mjini Zanzibar. Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mshibe Ali Bakari.

PINDA AMWAKILISHA JK SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA BURUNDI LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Spika wa Bunge la Burundi,Pie Ntavyohanyuma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura, ambako leo atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumwapisha Rais wa Nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Burundi waliofika kwenye uwanja wa ndege Bujumbura, ambako leo atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumwapisha Rais wa Burundi, Pierre Nkurnzinza. Kulia ni Spika wa Bunge la Nchi hiyo Pie Ntavyohanyuma na wapili kushoto ni mkewe Tunu.

VIAZI VIKUU: CHAKULA AMBACHO HUONEKANA ZAIDI MWEZI WA RAMADHANI

MFANYABIASHARA ya viazi vikuu, akimuuzia mteja, katika mtaa wa Lumumba , Dar es Salaam, jana. Viazi hivyo aliuza kati y ash. 2,500/ na sh. 5,000 kwa kiazi kimoja.

Dk.BILAL AANZA KUSAKA KURA KANDA YA KUSINI

Mgombea Mwenza wa Urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Wialaya ya Lindi Vijijini, Magagula Said, wakati alipokuwa akipokelewa mpakani mwa wilaya hiyo na Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya mikutano ya Kampeni jana, Agost 25. Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wialaya hiyo, Mohamed Rashid

JK ATINGA BUKOBA KUOMBA KURA ZAKE NA CCM

Aug 25, 2010

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Mji wa Bukoba katika siku yake ya kwanza ya ziara ya siku mbili mkoani Kagera kuomba ridhaa ya wananchi wa mkoa huo ili waweze kumchagua katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 31.10.2010. PICHA NA JOHN LUKUWI

MFANYABIASHARA SHABIKI WA PICHA ZA VIONGOZI

MFANYABIASHARA mmoja katika makutano ya mitaa ya Swahili na Mafia, Kaariakoo, Dar es Salaam, amejipatia umaarufu wa aina yake kutokana na kuhakikisha eneo lake la biashara linapambwa na picha mbalimbali za viongozi zikiwemo zinazoendana na wakati. Pichani, mfanyabiasha huyo, akiwa amebandika kwenye duka hilo picha mpya ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete (kushoto), kama ilivyoshuhudiwa na mpigapicha wetu, jana. Picha nyingine ni za viongozi wakuu wan chi na mashuhuri wakiwa katika amatukio mbalimbali.

UTOAJI HOLELA WA LESENI KUDHIBITIWA

Na Mohammed Mhina na Christina Mponji wa Jeshi la Polisi

Matatizo ya ajali za barabarani yanayosababishwa na uwezo duni wa madereva katika fani hiyo nchini sasa kupatiwa ufumbuzi baada ya kubuniwa kwa mfumo mpya wa utoaji wa leseni kwa madereva.

Akizindua mafunzo ya siku mbili kwa wakuu wa polisi mikoa na mameneja wa TRA mikoa yanayofanyika katika chuo cha usimamizi wa kodi, Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema amesema mfumo huo wa utoaji wa leseni utazingatia uwezo, ubora na kiwango kizuri alichonacho dereva kabla ya kupatiwa leseni.
“Dereva atapimwa uwezo wake ili kujua kama ana sifa zinazostahili kupata leseni na endapo atabainika kutokuwa na sifa zinazokidhi mahitaji basi dereva huyo hatapewa leseni”, alisema Bw. Said Mwema.

Akizungumzia Lengo la kuanzishwa kwa mpango huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini alisema ni kudhibiti utoaji holela wa leseni jambo linalochangia utoaji wa leseni kwa madereva wasio na viwango vinavyolingana na madaraja ya leseni wanazopewa pamoja na utengenezaji wa leseni feki.
Ameongeza kuwa leseni hizo zitasaidia kudhibiti madereva watakao fanya makosa katika mkoa mmoja na kukimbilia mkoa mwingine ili kupata leseni nyingine baada ya kufungiwa leseni zao kutokana na makosa yao.

Viongozi Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini wameanza kupatiwa mafunzo juu ya mchakato wa utoaji wa leseni mpya za udereva hapa nchini.

Akifungua mafunzo hayo, mkuu wa jeshi la polisi nchini inspekta jenerali Said Mwema, amesema mafunzo hayo ya pamoja ni mchakato wa kuelekea kwenye utoaji wa leseni za kisasa ambao utaanza kutekelezwa kwa awamu kwenye mikoa tisa ya Tanzania bara.

IGP amesema leseni hizo zitasaidia kuwatambua madereva watakaofanya makosa katika mkoa mmoja na kukimbilia mkoa mwingine kupata leseni. Leseni hizo bado gharama zake hazijafahamika na imeelezwa kuwa zina alama nyingi za kiusalama na itatumia mfumo wa TEKNOHAMA ambayo inahifadhi kumbukumbu zote za muhusika zitakazosaidia kumtambua kama amefanya kosa.

Nae Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Kamishna Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mohammed Mpinga wameelezea mambo yatakayozingatiwa katika utoaji wa leseni hizo mpya.
Kwa upande wake Kamishna wa idara ya kodi za ndani wa TRA Bw. Patrick Kassera alisema leseni ya kwanza inatarajiwa kutolewa septemba 15, mwaka huu.

Alisema pia utoaji wa leseni hizo utatoa kipaumbele kwa wale wenye leseni za zamani na ambao watafanyiwa majaribio upya ili kuangalia uwezo walionao kabla ya kupatiwa leseni hizo mpya na kuwataka wenye leseni za zamani kuendelea kutumia leseni zao hadi hapo watakapopatiwa leseni mpya.

Utoaji wa leseni mpya utahusisha mikoa tisa katika awamu ya kwanza ambayo ni Tanga, Arusha, Kilimajaro, Mwanza, Mbeya, Dodoma na mikoa mitatu ya kanda maalum ya kipolisi ambayo ni Kinondoni, Temeke, na Ilala

Viongozi wanaoshiriki kwenye mafunzo hayo ni Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini pamoja na Wakuu wa TRA wa mikoa tisa inayolengwa kuanzishwa kwa utuaji wa leseni hizo

Akifungua mafunzo hayo, mkuu wa jeshi la polisi nchini inspekta jenerali Said Mwema, amesema mafunzo hayo ya pamoja ni mchakato wa kuelekea kwenye utoaji wa leseni za kisasa ambao utaanza kutekelezwa kwa awamu kwenye mikoa tisa ya Tanzania bara.

IGP amesema leseni hizo zitasaidia kuwatambua madereva watakaofanya makosa katika mkoa mmoja na kukimbilia mkoa mwingine kupata leseni. Leseni hizo bado gharama zake hazijafahamika na imeelezwa kuwa zina alama nyingi za kiusalama na itatumia mfumo wa TEKNOHAMA ambayo inahifadhi kumbukumbu zote za muhusika zitakazosaidia kumtambua kama amefanya kosa.

Nae Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Kamishna Paul Chagonja, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mohammed Mpinga na Kamishna wa kodi za ndani wa TRA Bw. Patrick Kassera, wameelezea mambo yatakayozingatiwa katika utoaji wa leseni hizo mpya.

Naye Mtaalam mshauri wa Mradi wa Taifa wa Leseni za Udereva nchini Bw. Alnoor Nkya, ameelezea muuondo na sifa za leseni hizo.

Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yanafanyika kwenye Chuo cha Usimamizi wa Kodi Jijini Dar es Salaam, pia yanahudhuriwa na Makamanda wa polisi wa mikoa.

ikoa itakayohusika na mchakato huo wa utoaji wa leseni mpya ni Arusha , Dodoma, Kilimanjaro, Tanga,Mwanza,, Mbeya, na mikoa mitatu ya kanda maalum ambayo ni Ilala, Kindoni, na Temeke ambayo makamanda wake wote wamehudhuria.

MATUKIO KATIKA PICHA LEO

WANAFUNZI wakidandia lori aina ya Center leo enbeo la Kawe, Dar es Salaam, wakati wanarejea nyumbani.

JK ATINGA BUKOBA

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Mji wa Bukoba katika siku yake ya kwanza ya ziara ya siku mbili mkoani Kagera kuomba ridhaa ya wananchi wa mkoa huo ili waweze kumchagua katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 31.10.2010.

PICHA NA JOHN LUKUWI

JK AMALIZA ZIARA YA KAMPENI MWANZA

RAIS Jakaya Kikwete akiagana na wananchi wenye shauku ya kusalimiana naye mara tu
baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Katoro, wilayani Geita

JK ATINGA SENGEREMA, SIKU YA PILI YA KAMPENI ZA CCM

Aug 23, 2010

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Nyehunge, wilayni Sengerema jana mchana (picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kumfariji msichana mwenye ulemavu wa ngozi aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Mahaluko muda mfupi baada ya kuhutubia katika mkutano wa hadhara huko Nyehunge, wilayni Sengerema jana mchana(picha na Freddy Maro)

KUMBUKUMBU

Familia ya Halima S. Kaubanika ya Ilala Dar es salaam, wanakumbuka kifo cha baba yao Mzazi Mzee Suleiman M. Kaubanika kilichotokea  24/8/2009 Kigogo Dar es salaam.
Sasa ni mwaka mmoja tangu ututoke wake zako, watoto,marafiki zako na majirani wanakukumbuka sana hasa kwa ucheshi na mawazo uliokuwanayo mungu allaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina

DK. SHEIN ZIARANI PEMBA LEO

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM MH. DK. ALI  MOHAMED SHEIN, AKIPATA MAELEZO JUU YA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA INAYOTOKA WETE HADI GANDO MKOA WA KASKAZINI PEMBA KUTOKA KWA MKANDARASI WA BARABARA HIYO, WAKATI ALIPOFANYA ZIARA FUPI KUANGALIAMAENDELEO YA UJENZI HUO LEO.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM MHE. DK. ALI MOHAMED SHEIN, AKILA FUTARI PAMOJA NA WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA, ALIYOIYANDAA KWA AJILI YA WANANCHI WA MKOA HUO HUKO IKULU WETE PEMBA JANA.
MKE WA MAKAMU WA RAIS NA MGOMBEA URAIS WA

ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM MH. MAMA MWANAMWEMA SHEIN, AKIHUTUBIA WANACHAMA WA JUMUIYA YA UMOJA WA WANAWAKE UWT PAMOJA NA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI PEMBA KWENYE MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA UMOJA NI NGUVU MKOANI PEMBA LEO. Picha na Amour Nassor VPO

KAMPUNI MPYA YA SIMU ZA MKONONI YA HITS YAZINDUA NEMBO YAKE

Hits Tanzania kuzinduliwa Januari 2011

Kampuni ya ExcellentCom inayoendesha shughuli zake kama Hits Tanzania imefanya uzinduzi wa chapa na nembo yake ya “hits” siku ya Jumatatu, tarehe 23 August 2010 kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam. Hits Tanzania ni kampuni inayoendesha mtandao wa mawasiliano ya simu ambayo imepewa leseni ya kutoa huduma za Sauti, ujumbe mfupi na huduma za Mtandao (Data).

Wakati wa uzinduzi wa nembo yake, mwenyekiti wa Excellentcom Tanzania Ltd, Mhe. Abdullah Mwinyi alisema “Hits Tanzania sasa imeanza rasmi shughuli zake na iko kwenye hatua za mwisho kuwasha mitambo yake, kwa hiyo tutaanza ujenzi na upanuzi wa mtandao ili kuwa na uwezo wa kutoa huduma zetu nchi nzima mapema mwakani".

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mtendaji Mkuu wa ExcellentCom, David Charles alisema kwamba kwa mujibu wa taarifa ya TCRA (Tanzania Communications Regulatory Authority) ya Machi 2010, soko la huduma za simu za mkononi kwa sasa zinapatikana kwa kuwafikia zaidi ya asilimia 40 ya wananchi wa Tanzania. Aliongeza kwamba na kwa mujibu wa taarifa ya BMI (British Market Index) ya awamu ya pili ya mwaka 2010, matarajio ni kwamba huduma hizo zitawafikia zaidi ya asilimia 60 ya wananchi ifikapo 2012.

Bw. Charles alisema kwamba tayari kuna uwekezaji endelevu wa miundombinu kadhaa ya mawasiliano ambayo inashawishi kuwapo kwa mikakati ya ubia endelevu. “Kusema kweli, imeonekana dhahiri kwamba hakuna wakati muafaka kwa kampuni ya Hits Tanzania kusambaza mtandao wake kama sasa,” alisema.

Kampuni itaendelea na harakati za kuwekeana mikataba na wabia muhimu ambao wataiwezesha kampuni hiyo kuwapa wateja wa Hits na wateja wa wabia huduma maalum hapo ifikapo mwakani. Kwa mtazamo huo, kampeni hiyo itaitwa "a life time subscription" ambayo itatoa thamani na ubora kwa wabia wa Hits pamoja na wateja wake.

Hits Tanzania itazindua kampeni ya kutenga namba ya simu baadae mwaka huu, ambapo wateja wataweza kutengewa namba zao kupitia kianzishi namba cha Hits, ambacho ni 0741 mpaka 8.

English vesion

Hits Tanzania to launch in January 2011

Dar Es Salaam, August 23rd, 2010:

ExcellentCom trading as Hits Tanzania revealed its brand and logo “hits” to the public on Monday the 23rd August 2010 at the Movenpick Hotel. Hits Tanzania is a telecommunication network operator with a license to offer Voice, SMS and Data Services.

During the unveiling of the brand, the Chairman of Excellentcom Tanzania Ltd, Hons. Abdullah Mwinyi said that “Hits Tanzania operation is now in the final stages to go live and we will roll out a nationwide coverage by early next year.

Speaking to the media, ExcellentCom CEO David Charles said that according to TCRA (Tanzania Communications Regulatory Authority) 2010 March report, the cellular market in Tanzania currently has a penetration of over 40%. And according to BMI (British Market Index Q2 report, 2010) the projection is expected to reach over 60% in 2012.

He added that there are a number of network infrastructures in place that encourage synergies and strategic partnership. “Clearly there is never been a better time for Hits Tanzania to rollout its’ network than now,” He said.

The company will embark in signing partnership deals with a number of potential partners that will see them offer their customers and Hits customers with bundling packages comes next year. The campaign will be called “a life time subscription” that will create value to Hits partners and its customers.

Hits Tanzania will launch the reserve a number campaign later this year, where customers will be able to reserve their numbers on the Hits prefix which will be the 0741- 8.

REAL PICTURES OF HAZRAT BIBI FATUMA (S.A) HOUSE IN MADINA MUNAWARA


Photos forwaded by Khalfan Said

CCM YATIKISA MWANZA, JK AUNGURUMA

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete akihutubia wananchi katika viwanja vya Nyamagana.

CCM YAZINDUA KAMPENI ZAKE JANGWANI LEO

Aug 21, 2010

 Maelfu ya wana-CCM wakiwa wamefuriuka katuika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, wakatii wa mkutano huo leo

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wana-CCM na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni hizo katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.
MHESHIMIWATemba na Chege wakitumbuiza wakati wa mkutano huo
Marlow akitumbuiza na kundi lakwe
Mwanamuziki Zahir Ally 'Zorro na mtoto wake, Baba Zorro wakitumuiza katika mkutano huo'
NYOSHI El Saadat, akishambuliwa jukwaa na wanamuziki wa bendi ya fm Academia
Joti wa Orijino Komedi akibebwa na Wana-CCM kwenye mkutano huo baada ya kuwafanyia vijimambo
Jk akiondoka baada ya mkutano huo

KUMEKUCHA: CCM KUZINDUA KAMPENI ZAKE LEO MCHANA JANGWANI, JIJINI DAR ES SALAAM

MGOMBEA wa CCM Rais Jakaya Kikwete ataunguruma kwenye viwanja vya Jangwani wakati uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31.

MAAANDALIZI jukwaa yakikamilishwa leo asubuhi
Sehemu watakayoketi wageni waalikwa Vyoo maalum vilivyowekwa kwenye viwanja hivyo
 SHUGHULI zote zitakuwa live
ยช