.

UCHAGUZI MKUU TANZANIA WAFANYIKA LEO

Oct 31, 2010

Rais Jakaya Kikwete leo ameongoza Watanzania kuoiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Maadiwani na Rais Abeid Amani Karume akiongoza kwa upande wa Zanzibar. Pichani rais Kikwete akipiga kura yake kijiji cha Msoga, mkoa wa Pwani. 
Karume akipiga kura Kituo cha Kiembesamaki, ZanziRais bar. 
Dk. Gharib Bilal akipiga naye pia kura yake katika kituo hicho. Bilal ni mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM 
Mgombea Urais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, yeye alipiga kura yake katika kituo cha Skuli ya Mtopepo Wilaya ya Mjini 
Wananchi wakiwa wamefurika katika kituo cha kupiga kura cha Shule ya Mtoni, wilaya ya Mjini. 
Ilikuwa asiye na mwana abebe jiwe, kama  Zainabu Ngwadani mkazi wa Mtoni Kidalu, wilaya ya Magharibi, akipiga kura huku akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miezi mitano, katika kituo cha shule ya Mtoni
Amina Mohammed (80), liha ya uzee alio nao, akamuomba msaada kijana kumpeleka kituo cha kupiga kura cha Mwanakwerekwe, akapiga. 

Kisha Bibi huyu akabebwa kuingizwa katika gari kurudi nyumbani baada ya kupiga kura yake. 
Polisi nao wakawa na kazi ya ziada ambapo pamoja na ulizni lakini pia wakawa na jukumu la kusaidia wazee na wengine waliohitaji msaada. Pichani, polisi akimsaidia Bi , Swaumu Mbaraka Fumu ili aende kupiga kura yake katika kituo cha Ban Bella, Zanzibar.
Mvua nayo ilikuwa na kasherehe ya aina yake baada ya kudamka ikinyesha asubuhi na mapema, katika muda ule ambao wapigaakura wengi walitaraajiwa kujitokeza vituoni. pichani watu waliofika kituo cha Kimbe Sakmaki kupiga kura, wakijificha mvua hiyo. 
Musimu Hassani Ali akipiga kura yake mapemaaa kutuo cha Ben Bella

MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI CCM, ZANZIBAR

Oct 30, 2010

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume akimsalimia Dk. Sheni.
Rais Karume akimsalimia Komandoo, Dk. Salmin Amour. Katikati ni Shamsi Vuai Nahodha ambaye kwa sasa ni waziri Kiongozi na pia ni mgombea Ubunge jimbo la Mwanakwerekwe
Wana-CCM wakiserebuka muziki wa Taarab ulioporomoshwa

SALAM ZA WANA-CCM KISONGE ZANZIBAR HIZI HAPA

Hizi ndizo salam za wanakisonge

MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI WA CUF VIWANJA VYA MAISARA,ZANZIBAR

WAFUASI wa CUF wakisubiri kuhutubiwa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Seif Sharif Hamad (picha ya chini), katika mkutano wa kufunga kampeni viwanja vya Maisara mjini Zanzibar. 
Maalim Seif Sharif Hamad kwenye mkutano huo leo

VIJANA KAZINI KATIKA OFISI YA UENEZI AFISI KUU YA CCM KISIWANDUI

Mwandishi Mwandamizi wa Uhuru FM, Antar Sangali na mtaalam wa masuala ya IT, Haji Mrisho katika ofisi hiyo leo. 
Sangali wa  Uhuru FM (kushoto) na Yunus Sose na Suleiman Nzalro wa Habari Leo wakiwa katika ofisi hiyo. 
OFISA wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar, Juma Mohamed akiwa ofisini kwake leo hii mjini Zenzibar 
Mhariri wa Uhuru na Mzalendo, Noor Shija akielekezana jambo na mwakilishi wa Uhuru FM, Zanzibar, Mariam Mziwanda, katika ofisi hizo. 
Maraiam Mziwanda

JK AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI USIKU WA KUAMKIA LEO

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa tayari  kuzungumza na baadaye kujibu maswali, katika mkutano wake na  waandishi wa habari, katika ukumbi wa Arnatoublou, mjini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Press Conference hiyo iliyoratibiwa na,  Asha Mtwangi, ilihusisha vituo tisa vya televisheni vikiwemo ATN, Channel 10, East Africa TV, TBC, TV Milimani, Clouds TV, Star TV na ITV. kurushwa 'live'.
Akisikilizwa wakati akichambua masuala mbalimbali kuhusu kwa nini wananchi wanapaswa kumchagua tena yeye katika uchaguzi utakaofanyika kesho nchini kote. 
Baadhi ya Wahariri watendaji wa vyombo vya habari wakimsikiliza kwa makini 
Baadhi ya wananchi pia walipata fursa ya kuingia ukumbini kusikiliza 'live' 
Wadau wakifuatilia anachosema JK katika ukumbi 
JK akiagana na watu mbalimbali baada ya mkutano huo 
JK akitoka ukumbini na mgombea mwenza wake, Dk. Mohammed Gharib Bilal baada ya mkutano kumalizika salama (Picha  kwa Hisani ya Michuzi Blogspot).

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI KUHUSU UCHAGUZI MKUU

Oct 29, 2010

RAIS Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini baada ya kuwa na mazungumzo nao leo jioni, Ikulu mjini Dar es Salaam, kuhusu mustakabali wa nchi katika suala la amani na utulivu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili hii. (Picha na Freddy Maro).

MAMA MWINYI AMNADI MWANAWE JIMBO

Mke wa Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi, Mama Siti, akimuombea kura kwa wananchi, mtoto wake, Hussein Mwinyi jimbo la Kwahani, Zanzibar,leo,  katika mkutano wa kuwatambulisha wagombea wa jimbo hilo kwa nafasi mbalimbali kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi utakaofanyika keshokutwa, Jumapili.

KINA mama wa CCM jimbo la Kwahani, Zanzibar wakishangilia kwa raha zao, wakati Mama Siti Mwinyi akizungumza katika mkutano huo.

HUSENI Mwinyi (Kulia) na  akinadiwa na  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini, Borafya Silima Juma.

WAGOMBEA URAIS ZANZIBAR HAWA

Chachandu Daily Blog inawatakia uchaguzi wenye kheri, amani na utulivu wapiga kura wa Zanzibar, katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili hii. Kila mmoja ajitahidi kufikiri kwa busara zake zote ili aweze kuchagua kiongozi makini. Mtayarishaji

JK AKUTANA NA WAANGALIZI WA UCHAGUZI WA EU

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya Bwana David Martin ambaye alimtembelea Rais Kikwete huko Ikulu tarehe 28.10.2010.


Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na ujumbe wa waangalizi kutoka Jumuia ya Ulaya ulioongozwa na David Martin (Wa pili kushoto) na Naibu Mwangalizi wa Uchaguzi mkuu Bwana Tonny Risse tarehe 28.10.2010.(PICHA NA JOHN LUKUWI)

JAMAA AKIMSHABIKIA MGOMBEA WA CCM RAIS KIKWETE HUKU AKIWA NDANI YA FULANA YA CUF

Oct 28, 2010

JK dole tu, hakuna mwingine!  hivi ndivyo alikuwa akisema, jamaa huyo, huku akiwa ameegemea picha ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete, eneo la  Soko la Darajani, ambalo ni moja ya maeneo yenye msisimko wa masuala ya siasa za Zanzibar, cha kuvutia zaidi huyu jamaa alikuwa ametinga t-shirt ya CUF.

YALIYOJIRI LEO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, JUMAPILI HII

Waangalizi wa ndani na nje ya nchi wa uchaguzi mkuu wakiwa katika mkutano na Tume ya Uchaguzi zanzibar (ZEC), leo katika ukumbi uliopo Hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar.  
Waangalizi wa uchaguzi mkuu wakitumia kompyuta kutuma taarifa zao kwa mtandao wa internet uliowekwa katika ukumbi maalum utakaotumika kutangaza matokeo na shughuli nyingine za uchaguzi huo, uliopo hoteli ya Bwawani, Zanzibar. 
Ukumbi huu ndio utatumika kutangaza matokeo ya Uchaguzi Zanzibar, una uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 100. 
MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi, Zanzibar (ZEC), Khatib Mwinchande, akizungumza, wakati wa mkutano wake na waangalizi wa uchaguzi mkuu, Zanzibar, leo katika ukumbi maalum uliopo hoteli ya Bwawani, Zanzibar 
Waangalizi wa uchaguzi mkuu waliopo Zanzibar, si tu wanafuatilia uchaguzi huo ila pia wanafanya utalii katika kisiwa hicho. Pichani, wakitembelea soko la Darajani. leo. 
Picha za wagombea Rais Kikwete (CCM-urais), Dk. Shein (Urais zanzibar-CCM), Profesa Lipumba (Urais-CUF) na Seif Sharif Hamad (urais zanzibar (CUF) ndizo pekee zinatawaka katika viunga mbalimbali vyenye vuguvugu la mambo ya siasa Zanzibar, huku mgombea wa Chadema anayechacharika Bara Dk. Wilibrod Slaa picha zake zikiwa hazipo kabisa katika maeneo hayo. Pichani, ni eneo la soko la Darajani. 
ยช