.

tiGo YAZAWADIA MSHINDI

Nov 30, 2010

OFISA Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi zawadi ya hundi ya sh. milioni kumi kwa mshindi wa jumla wa promosheni ya Dunia ya Washindi, Farijala Athumani Iddi mkazi wa Singida, katika makabidhiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Miradi wa Huduma za Ziada (VAS) wa Tigo, Suleiman Bushagama.

STARS YAIKUNGUTA SOMALIA 3-0

MSHAMBULIAJI wa Kilimanjaro Stars, Thomas Ulimwengu (kulia), akimkabili Anwar Ibrahim wa Somalia, timu hizo zilipomenyana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya Kombe la Chalenji, leo

PEACOCK HOTEL KUADHIMISHA MIAKA KUMI YA USIKU WA MTANZANIA

Kiongozi wa bendi ya DDC Mliman Park, wana Sikinde ngoma ya ukae, Habibu Mgalusi akizungumza na waandishi wa habari jinsi bendi hiyo itakavyoshiriki Tamasha hilo. Kushoto ni mwanamuziki wa bendi hiyo, Rehani Bitchuka na wengine kutoka kulia ni Wakurugenzi wa Hoteli ya Peacock,  Joseph Mfugale na Damasi Mfugale
==================================
Habari Kamili
Peacock Hotel ni hoteli inayojali wateja wake kwa kiwango cha juu. Ili kudumisha na kuendeleza mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania, hoteli ilianzisha Usiku wa Mtanzania ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia. Ni hoteli pekee nchini Tanzania ambayo inadumisha menu halisi ya kitanzania.

Usiku huu unatimiza miaka kumi(10) mwaka huu tangu uanzishwe. Kila Jumatano usiku panakuwepo vyakula vya kitanzania vya aina mbalimbali na makabila mbalimbali. Mandhari ya hotel hugeuka kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huu.

Tarehe 3.12.2010 ni siku ya kusherehekea kutimiza miaka kumi ya Usiku wa Mtanzania katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku.

Shamrashamra hizo zitapambwa na ngoma za asili pamoja na muziki kutoka kwa Kidum-Kenya, Lady Jay Dee, Sikinde-Ngoma ya Ukae, na Waane Star.

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu wote ambao wanaendelea kuburudika kwa milo ya kitanzania pamoja na burudani za asili. Kwa kutambua uwepo wao na kuthamini usiku huu tunawaahidi huduma bora zaidi na siku ya sherehe tutawatambua rasmi baadhi yao kwa niaba yaw engine kwa kuwapa zawadi.

Washiriki wenzetu katika kuunga mkono Usiku wa Mtanzania kutimiza miaka kumi ni Benki ya Posta, Shear Illussion, Vayle Springs, na Precision Air. Hawa wanadhihirisha dhamira yao ya kuunga mkono mila na desturi za kitanzania.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr.Damas Mfugale kwa namba 0789-280112

KOMBE LA CHALENJI: MALAWI YAITUNGUA KENYA 3-2

Nov 29, 2010

MSHAMBULIAJI wa harambee stars akishambulia langoni mwa Malawi, timu hizo zilipomenyana leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo kwenye mtanange wa michuano la Kombe la Chalenji. Shambulio halikuzaa matunda kutokana na kuokolewa na mabeki ya Malawi. Hatimaye Harambee ilitoka uwanjani ikiwa imejiinamia kwa kutwangwa mabao 3-2

RAIS KIKWETEAKUTANA NA BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI

RAIS Jakaya Kikwete akizungumza na mawaziri wake, leo Ikulku mjini Dar es Salaam
Mawaziri wote wakiwa katika kikao hicho na rais Kikwete leo (Picha zote na Freddy Maro)

PROFESA ANNA TIBAIJUKA AKABIDHIWA OFISI NA CHILIGATI

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. John Zefania Chiligati (kushoto) akimkabidhi nyaraka mbalimbali za kutendea kazi Waziri mwenye dhamana hiyo Mh. Prof. Anna Tibaijuka. Makabidhiano hayo yalifanyika mara baada ya Mh. Tibaijuka kuingia ofisini jana tangu aapishwe. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara Mh. Patrick Rutabanzibwa. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Anna Tibaijuka, (wa Pili kutoka kulia, waliokaai) akiwa pamoja na Waziri aliyemaliza muda wake Mh. John Chiligati (kulia kwake), wakurugenzi na wakuu wa Vitengo, baada ya makabidhiano ya ofisi. Wengine (waliokaa) ni Naibu Waziri wa Wizara Hiyo Mh. Goodluck Ole Medeye (kulia kwa Mh. Chiligati), Katibu Mkuu Bw. Patrick Rutabanzibwa (wa kwanza kulia) na Naibu Katibu Mkuu Bibi Maria Bilia ( wa kwanza kushoto)

BAADA YA KIMUHEMUHE CHA MAWAZIRI KUPITA SASA NI WAKUU WA MIKOA, WILAYA

Wakuu wa mikoa wa sasa wakiwa kwenye maeneo yao. Mkoa wa dar es Salaam, weneyewe upo wazi kutokana na aliyekuwa mkuu wake, Wiliam LukuLukuvi sasa kuwa waziri.

MICHUANO YA CHALENJI: ZANZIBAR HEROES YATAKATA , YAIBOFYA SUDAN 2-0

Nov 28, 2010

Ali Ahmed Salum Shibiri akishangilia baada ya kuipachikia bao la pili na la ushindi, timu yake ya Zanzibar Heroes, timu hiyo ilipomenyana na Timu ya Taifa ya Sudan, leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
MCHEZAJI Elrayan Abdallah wa timu ya Taifa ya Sudan (kushoto) akipambana na Sabri Ramadhani Mzee wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, wakati wa mechi hiyo.

JK AZINDUA MICHUANO YA KOMBE LA CHALENJI LA TUSKER; KILI STARS YALALA KWA ZAMBIA 1-0

Rais Kikwete akiongoza kusikiliza wimbo wa taifa kabla ya kuzindua rasmi michuano ya CECAFA ya Kombe la Chalenji la Tusker. pamoja naye ni, Waziri mwenye mamlaka ya michezo, John Nchini (watatu kulia) na viongozi wa soka wa TFF, CECAFA 
Rais Kikwete akipiga mpira kuzindua mashindano hayo 
JK akimsalimia Kipa wa Kili Stars, Juma Kaseja wakati akikagua kikosi cha Stars kabla ya mchuano na timu ya Zambia 
Kili Stars 
Zambia 
Rais Kikwete akikabidhiwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Richard Wells, Kombe la Tusker Challenge Cup 
Thomas Ulimwngu wa Kili Stars akichuana na Steven Kkabanga wa Zambia

JK AAPISHA MAWAZIRI WAKE WAPYA

RAIS Kikwete, akiwa na Mawaziri wapya baada ya kuwaapisha, Ikulu mjini Dar es Salaam. Pamoja naye ni Makamu wa Rais, Dk. Bilal na Waziri Mkuu Pinda. Picha. http://www.richard-waikenda.blogspot.com/

Nov 27, 2010

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodeger Tenga (picahni) anatarajiwa kuwania nafasi ya ujumbe katika Shirikisho la Soka la Soka Barani Afrika (CAF) katika uchaguzi utakaofanyika nchini Sudan mwezi Februari mwakani. Imetoka: http://www.mamapipiro.blogspot.com/

JK KUAPISHA BARAZA JIPYA ASUBUHI HII, IKUKU MJINI DAR ES SALAAM

Chuo Kikuu Cha Dodoma Jana kiliwatunuku  Shahada ya Heshima ya Udaktari (Doctor Honoris Causa), Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Marehemu Mzee Rashid  Mfaume Kawawa kwa  kutambua michango yao mbalimbali katika nyanja za siasa na  elimu nchini ikiwemo kuasisi ujenzi wa Chuo hicho. Pichani Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa akimtunuku shahada ya Heshima ya Udaktari Rais Dr.Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho iliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma jana.Katikati ni Makamu mkuu wa Chuo Profesa Idriss Kikula.   (Picha na Freddy Maro).

MAADHIMISHO YA MIAKA 5O YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) YAANZA

Huu ndio viongozi wa Chuo Kikii cha Dar es Salaam, hadi kufikia Rwekaza Mukandara wa sasa
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambaye pia ni Rais wa wanataaluma wa chuo hicho, Waziri Mkuu wa zamani, Jaji mstaafu, Joseph Sinde Warioba, alipowasili kwa ajili ya kuzindua rasmi maadhimisho hayo, katika ukumbi wa Nkrumah. Wengine kutoka wapili kushoto ni, Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa UDSM, Balozi Fulgence Kazaura. Kulia ni mmoja kati ya wanafunzi 14 wa kwanza kusoma kilipoanzishwa chuo hicho 1961, Mganda, Kakuba Gerald. 
Baadhi ya wanafunzi wa UDSM wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho hayo,huku wengine akiwa na bango la ujumbe waliotaka umfikie Pinda
Mwanamuziki mahiri wa kike, Karola Kinasha akiimba kwa hisia kali, wimbo maalum wa miaka 50 ya UDSM,
Mwanamuziki mahiri kwa mashairi, Mrisho Mpoto akiimba shairi maalum la kusherehesha uzinduzi huo akiwa na bendi yake ya Mjomba Band

CHUO KIKUU CHA DODOMA CHAZINDULIWA RASMI LEO

Nov 25, 2010


Rais.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin William Mkapa wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ndiye Mkuu wa chuo cha Dodoma, na Dr Biala ni Mwenyekiti wa kwanza wa Chuo hicho.(Picha na Freddy Maro)

SOKA: VIPAJI KWANZA

MCHEZAJI wa timu ya kituo cha kukuza  vipaji ya soka cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Abuu Moshi (kushoto) akipambana na mchezaji wa timu ya kituo cha Africa Youth Sports Academy (TAYOSA), Magomeni, Ali Saidi, katika mechi maalum iliyoandaaliwa kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya tano ya programu ya Benki ya NMB ya kugawa mipira kwa shule za msingi nchini,  kwenye Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam. Timu hizo zilitosa suluhu. 
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars Posen akipiga mpira kufunga bao, wakati wa uzinduzi wa programu hiyo. wapili kulia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa NMB,  Kees Verbeek

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Nov 24, 2010

 RAIS Jakaya Kikwete akitangaza Baraza lake jipya la
 Mawaziri (Picha na Freddy Maro)
1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora):- Mathias Chikawe
     Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu): Stephen Wassira

2.Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma):- Hawa Ghasia

3. Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano):- Samia Suluhu
     Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira):- Dk. Terezya Luoga Hovisa

4. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge):- William Lukuvi
* Uwekezaji na Uwezeshaji :- Dk. Mary Nagu

5. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI);- George Huruma Mkuchika
    Naibu:- Aggrey Mwanri
    Naibu:- Kassim Majaliwa

6. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo
     Naibu:- Gregory Teu
     Naibu:- Pereira Ame Silima

7. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi;- Shamsi Vuai Nahodha
    Naibu:- Balozi Khamis Suedi Kagasheki

8. Wizara ya Katiba na Sheria;-  Celina Kombani

9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Kimataifa;- Bernard K. Membe
     Naibu:- Mahadhi Juma Mahadhi

10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa;-       Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi

11. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi;-      Dk. Mathayo David Mathayo
      Naibu:- Benedict Ole Nangoro

12. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia;- Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
      Naibu:- Charles Kitwanga

13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka
       Naibu:- Goodluck Ole Madeye

14. Wizara ya Maliasili na Utalii;- Ezekiel Maige

15. Wizara ya Nishati na Madini;-  William Mganga Ngeleja
     Naibu;- Adam Kigoma Malima

16. Wizara ya Ujenzi;- Dk. John Pombe Magufuli
     Naibu:- Dk. Harrison Mwakyembe

17. Wizara ya Uchukuzi;- Omari Nundu
      Naibu:-  Athumani Mfutakamba

18. Wizara ya Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami
      Naibu:- Lazaro Nyalandu

19. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;- Dk. Shukuru Kawambwa
      Naibu:- Philipo Mulugo

20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii;- Dk. Haji Hussein Mpanda
      Naibu:- Dk. Lucy Nkya

21. Wizara ya Kazi na Ajira;- Gaudensia Kabaka
     Naibu;- Makongoro Mahanga

22. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto;- Sophia Simba Umi Ali Mwalimu

23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo;- Dk. Emmanuel John Nchimbi
      Naibu:Dk. Fenella Mukangara

24. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki;- Samuel John Sitta
      Naibu;- Dk. Abdallah Juma Abdallah

25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika;- Prof. Jumanne Maghembe
      Naibu: Christopher Chiza

26. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
      Naibu: Eng. Gerson Lwinge

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI KUTAJWA LEO

ILE kiu ya  kutaka kujua nani watakuwemo katika Baraza jipya la Mawaziri la awamu ya pili ya miaka mitano ijayo ya Rais Jakaya Kikwete, waliyokuwa nayo wengi hasa wafuatiliaji wa masuala ya siasa za Tanzania itakatika leo kwa kuwa ndiyo siku ambayo Rais Kikwete atatangaza Baraza lake jipya.
     Kulingana na taarifa zilizopo Rais Kikwete atatangaza baraza hilo leo saa nne asubuhi.

KILI STARS YAIFUNGA KABAO KAMOJA HARAMBEE STARS

Nov 23, 2010

 MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Mrisho Ngasa (kulia) akipambana na Stephen Ocholla wa timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars, timu hizo zilipemenyana katika mechi ya kirafiki ya Kimataifa, leo kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Kilimanjaro Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mwaikimba akipongezwana wachezaji wenzake baada ya kupachika bao la pekee katika mechi hiyo 
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Kenya, 'Harambee Stars',Jacob Mulee (kushoto) akimpongeza Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars'Jan Paulsen naada ya mechi

MATAKWA YA WANANCHI YAZINGATIWE KURA YA MAONI SUDANI KUSINI

KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA, BAN KI MOON AKIBADILISHANA MAWAZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UINGEREZA BW. WILLIAM HAGUE MUDA MFUPI KABLA YA KUANZA KWA MKUTANO WA BARAZA KUU LA USALAMA LILILOKUWA LIKIJADILI HALI YA SUDANI HUSUSANI MCHAKATO WA UPIGAJI KURA YA MAONI UTAKAOFANYIKA SUDANI YA KUSINI NA ENEO YA ABYEI JANUARI TISA MWAKANI.

PICHANI NI WAJUMBE WA BARAZA KUU LA USALAMA WA UMOJA WA MATAIFA WAKIWA KATIKA MKUTANO WA KUJADILI HALI YA SUDANI NA MCHAKATO WA UPIGAJI WA KURA ZA MAONI. MKUTANO HUO ULIOKUWA KATIKA NGAZI YA MAWAZIRI ULIHUDHURIWA PIA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI BI HILARY CLINTON NA WAWAKILISHI WA PANDE MBILI ZINAZOHUSIKA NA MCHAKATO HUO YAANI SERIKALI YA SUDANI KUSINI INAYOONGOZWA NA KIKUNDI CHA SPLM NA SERIKALI KUU YA KHARTOUM 
NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK
Wakati wananchi wa Sudani ya Kusini wakiendelea na zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura ya maoni itakayoamua mstakabali wao wa kujitenga, Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limezihimiza pande zote zinazohusika na mchakato huo kuheshimu matakwa ya wananchi.

Aidha Baraza hilo pia limezitaka pande zinazohusika kuchukua hatua muhimu na za haraka kuhakikisha kura hiyo inapigiwa katika muda waliokubaliana.

Wananchi wa Sudani ya Kusini watapiga kura Januari tisa mwakani kuamua kama wajitenge na serikali Kuu ya Khartoum. Ili hali wananchi wa eneo la Abyei wao lenye utajiri mkubwa wa mafuta wao watapiga kura ya kuamua waende upande upi.

Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika mkutano wake uliofanyika katika ngazi ya mawaziri, lilikutana siku ya jumanne chini ya Urais wa Uingereza kwa mwezi Novemba kujadili hali ya Sudani.

Katika taarifa yake kwa Baraza hilo, Waziri Uingereza anayehusika na Mambo ya Nje na masualaya Jumuia ya Madola, wa Mambo ya N Bw. William Hague amesema “ Baraza linazitaka pande zote zinazohusika na mkataba wa amani wa mwaka 2005 kuchukua hatua haraka , kuhakikisha kunakuwapo na amani, na kura ya maoni inapigwa kwa wakati na katika mazingira huru na kwa kuzingatia matakwa ya wananchi wa Sudani ya Kusini na Abyei.

Katika Mkutano huo, wajumbe walipokea taarifa za kuanza kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura. Zoezi hilo lilianza siku ya jumatatu na litaendelea hadi Desemba Mosi.

Wajumbe hao pia wamezungumzia haja ya kukamilishwa kwa baadhi ya vipengele vilivyomo katika Mkataba wa amani, baadhi ya vipengele hivyo ni suala la mipaka, mali asili, uraia, sarafu na suala zima la amani.

Aidha Baraza hilo pia limezitaka pande husika kushirikiana kwa karibu na jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Sudani ( UNAMIS) katika kipindi chote na utekelezaji wa majukumu yake.

Ushirikiano ambao pande hizo zinatakiwa kulipatia jeshi hilo ni pamoja na uhuru wa kwenda wanakotaka, uhuru wa kusafirisha vifaa na watu na usafirishaji wa vifaa vya kupigia kura.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, amesema ingawa jumuia ya kimataifa inatoa misaada na ushirikiano mkubwa kuhakikisha upigaji kura ya maoni unafanyika na kwa wakati. Lakini anabainisha kuwa wajibu huo hauwezi kuchukua nafasi au kuwa mbadala wa utayari wa pande zinazohusika kutimiza wajibu wao.

Amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa unafanya kazi na pande zote mbili ili kuhakikisha kwamba kunakuwa na hali ya amani na utulivu wakati wa kipindi cha upigaji kura na baada ya kupiga kura.’

Hata hivyo ametahadharisha kwamba majeshi ya Umoja wa Mataifa yanaweza yasiwe na uwezo wa kutosha wa kuzuia kurejea kwa vita endapo ghasia kati ya pande hizo mbili zitaibuka tena

Wakati huo huo timu ya watu watatu inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, tayari iko nchini Sudani kuangalia zoezi la uandikishaji wapiga kura linavyoendelea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolwa na Idara ya Habari ya Umoja wa Mataifa, Rais Mstaafu Mkapa na timu yake waliwasili nchini humo muda mfupi kabla ya zoezi hilo halijaanza.

Akiwa nchini humo, Mkapa amenukuliwa akisema kuwa uandikishwaji wa wapiga kura ni hatua moja muhimu sana ya kuelekea mchakato wa upigaji wa kura yenyewe

Akabinisha kuwa timu yake inalifuatilia kwa makini sana zoezi hilo wakati wote watakapo kuwapo nchi humo ili kuona linakwendaje.

Mkapa pia amesema ni matumaini ya timu yake kuwa wananchi wote wa Sudani ya Kusini kokote kule walipo watajitokea kwa amani na kujiandikisha.

Akongeza kuwa timu yake iliyoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mwezi Septemba, inatambua wazi kwamba uratibu mzima wa maandalizi ya daftari la wapiga kura halikuwa jambo rahisi na hasa kwa kuzingatia ukubwa wa eneo lenyewe na kasi ya maandalizi lakini wana matumaini kwamba kazi hiyo itamalizika kwa mafanikio.============================================================

JK KUTANGAZA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI KESHO JUMATANO

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atatangaza Baraza la Mawaziri jipya kesho, Jumatano, Novemba 24, 2010.
     Rais kikwete atatangaza Baraza la Mawaziri hilo jipya kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 31, mwaka huu, 2010.
   Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
23 Novemba, 2010

JK AMTUMIA SALAM ZA RAMBIRAMBI UVCCM

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Ndugu Martin Shigela, kufuatia kifo cha ghafla cha Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Wilaya ya Musoma Mjini, Ndugu Wilfred Peter Muga.

Ndugu Muga (32) alipoteza maisha yake wakati basi alimokuwa akisafiria kwenda Kigoma kushambuliwa na majambazi jana, Jumapili, Novemba 21, 2010. Ndugu Muga amezikwa mjini Kigoma leo, Jumatatu, Novemba 22, 2010.

Katika salamu zake, Mwenyekiti Kikwete amemwelezea Muga “kama kijana ambaye alikuwa ameufanyia mengi Umoja wa Vijana katika kipindi alipoajiriwa na Umoja huo.”

Muga aliajiriwa kama Katibu wa Vijana wa CCM wa Wilaya Oktoba mosi, mwaka 2006, na katika miaka yake minne ya utumishi wa Vijana amekuwa Katibu wa Wilaya wa Chato na Bukoba Mjini, Mkoani Kagera kabla ya kuhamishiwa Musoma Mjini mwanzoni mwa mwaka jana.

Ameongeza Mheshimiwa Kikwete: “Umoja wa Vijana umepoteza kijana hodari, mwenye kujituma na mwenye mapenzi makubwa na Umoja wa Vijana na Chama cha Mapinduzi. Tumempoteza katika mazingira ya kusikitisha sana wakati tulipokuwa bado tunamhitaji na kuhitaji utumishi wake.”

“Kupitia kwako, Katibu Mkuu wa UVCCM, napenda pia kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya Ndugu Muga. Nawaomba subira katika kipindi hiki kigumu. Nataka wajue kuwa tuko nao katika kipindi hiki cha huzuni na maumivu makubwa lakini yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Novemba, 2010BURIANI 'JENERALI' JUMA MKAMBI

JENEZA  lenye mwili wa marehemu 'Jenerali' Juma Mkambi ukifikishwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, tayari kwa mazishi ambapo mamia ya wapenzi wa soka, ndugu jamaa na marafiki walijitokeza kumzikaMkambi aliyekuwa  kiungo huyo nyota wa Taifa Stars na Yanga aliyefariki dunia Jumapili alfajiri. Juma Mkambi atakumbukwa kuwa kwa mengi ikiwemo kuwa mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa waliokuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichoshiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la Afrika huko Nigeria mwaka 1984 na alifunga bao.

RAIS WA COMORO AMTEMBELEA JK IKULU LEO

Nov 22, 2010

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam , Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Ahmed Abdallah Mohamed Sambi leo mchana.Viongozi hao wawili baadaye walifanya mazungumzo(picha na Freddy Maro)

MBIO ZA UMEYA: WALIOCHUKUA FOMU ILALA WAKAMILISHA KUZIJAZA NA KUZIAREJESHA

JUMLA la madiwani wateule wanne waliochukua fomu za kugombea umeya katika manispaa ya Ilala wamerudisha fomu hizo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala Ernest Chale alisema wagombea wote waliochukua fomu kwake wamerudisha isipokuwa Hashim Sagafu. Chale alisema hayo leo alipokuwa akizungumza na Chachandu Daily, mjini Dar es Salaam .

Alisema kuwa waliomba nafasi ya unaibu meya ni wawili ambao ni diwani wa Kisutu, Kherry Kessy na Abdulkarim Masamaki wa Kariakoo na tayari wamesharudisha fomu zao.

Chale aliwataja wengine waliochukua fomu na kurudisha ambapo kata zao zipo katika mabano kuwa ni Jerry Silaa (Gongo la Mboto), Salum Bisakala (Gerezani) na Dk. Didas Masaburi (Kivukoni)


Alisema uchukuaji wa fomu hizo ulianza Novemba 20 na ulimalizika jana saa 10 jioni ambapo alisema baada ya kumalizika kwa mchakato huo majina hayo yatapelekwa katika kikao cha utendaji cha kamati ya siasa ya wilaya kwa ajili ya kujadiliwa.

MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA MBEA AJIUZULUMWENYEKITI wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya,Sambwee Shitambala (pichani), ambaye pia alikuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini amejiuzuru nafasi hiyo kutokana na kutuhumiwa kuwa amehogwa Sh. Milioni 600 na Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kusababisha ashindwe kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.
          Ametangaza uamuzi huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea tathimini ya uchaguzi mkuu wa uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu mbela ya Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya,Eddo Makata na Kaimu Mwenyekiti wa Vijana Chadema mkoa,Exavery Mwalembe.
         Shitambala alisema amechukua uamuzi wa kujiuzuru nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Chadema mkoa ili kupisha uchunguzi uweze kufanyika ndani ya chama kufuatia tuhuma zambazo zinaelekezwa kwake kwamba kushindwa kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini kumetokana na kuhongwa fedha na CCM.
       Alisema shutuma zinazoelekezwa kwake ambazo pia zinatolewa na wanachama wa Chadema na viongozi zimemshushia hadhi mbele ya jamii na utendaji wake wa kazi ya uwakili kama mwanasheria hivyo njia pekee aliyoamua kuchukua ni kujiuzuru nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya kwa lengo la kupisha uchunguzi uweze kufanyika kubaini kama kuna ukweli wa tuhuma hizo. 
      “Maneno yanayozungumzwa kwamba nimehongwa fedha yamepunguza imani kubwa sana kwa wananchi ambapo sasa wamesahau hata mambo mazuri niliyofanya ya kukijenga chama mkoa wa Mbeya,kutokana na hali hiyo nimeona ni bora niachie ngazi na nitabaki kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya chama,”alisema Shitambala.
     Alisema tangu kumezuka uvumi huo ndani ya chama,amejaribu kumpigia simu Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe, lakini bahati mbaya hapokei simu jambo ambalo linanisikitisha na kutoamini kama ni kweli muda wote anakuwa bize kiasi kwamba ashindwe kupokea simu yangu.
     Alisema kinachompa mashaka ni kwanini tuhuma za kuhongwa fedha na CCM zinaelekezwa katika jimbo la Mbeya vijijini wakati yapo majimbo kama Songea, Njombe, Segerea, kilombero, Arumeru, Kiteto, Busanda, Bukoba na Tarime ambayo Chadema ilikuwa na uhakika wa kuibuka na ushindi lakini wagombea wake wameshindwa na hakuna tuhuma kama hizo.
    Shitambala alisema kutokana na kuwepo kwa tuhuma hizo zinazoelekezwa kwake tu anaamini kuwa kuna jambo limejificha ndani yake hasa ikizingatia kuwa hii ni mara ya pili kutuhumiwa hivyo ambapo mara ya kwanza ilikuwa wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini uliofanyika mwezi Januria 2008.
    Katika uchaguzi huo mdogo Shitamba aliondolewa kugombea ubunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kukosea mashariti ya kiapo ambapo badala ya kuapa mahakamani aliapa kwa wakili kitu ambacho kinapingana na kanuni za viapo vya uchaguzi na hivyo kukaibuka maneno kwamba alihongwa fedha na CCM ili afanye makosa hayo hasa ikizingatia kuwa ni mwanasheria anayefahamu sheria.
    Shitambala alisema kimsingi yapo mambo mengi yaliyosababisha ashindwe kwenye kinyang’anyiro cha ubunge uchaguzi wa mwaka huu ikiwemo jiografia ya jimbo la Mbeya vijijini na pia baadhi ya mawakala wake hususani wa kata ya Inyala ambao walikimbia na hawajulikani waliko hadi sasa.
    “Mambo yaliyochangia nijitoe ni kutuhumiwa kwa mara ya pili hivyo nadhani watu wa Mkoa wa Mbeya ni wapenda majungu hivyo hakuna haja ya kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa ,tuhuma ya kwamba sikuweka mawakala siyo za kweli niweka mawakala kila kituo na nikawalipa japo wapo waliokimbia na mpaka leo hii tunaendelea kuwatafuta,”alisema Shitambala.
    Alisema wakati umefika kwa wanachama wa Chadema wawe wanajenga imani kwa viomngozi wao kwa kutambue kuwa nguvu ya mgombea wao ikoje kwa mpinzani wake badala ya kuwa wepesi wa kupokea propaganda na wepesi wa kumeza ndoani.
    Aliongeza kuwa kwa hali iliyojitokeza Mbeya inawezekana propaganda hii ya kwamba amehongwa fedha ili kuuza jimbo ilienezwa na mtu mmoja tu lakini wanachama wengi wamechukulia kama ni jambo la kweli hali ambayo ni hatari kubwa kwa chama.
    Shitambala alisema wana Chadema wafahamu kuwa kamwe hawezi kuuza heshima yake kwa pesa maana yeye si Malaya wa siasa kwani anategemea busara zangu si kwa pesa.
    Alisema pamoja na kujiuzuru kwake hana mpango wa kuhamia chama chochote cha siasa na kwamba kama ataamua kuhamia chama kingine cha siasa itakuwa ni maamuzi yake hayatakuwa maamuzi ya kununuliwa.
   “Sina wasiwasi na maisha kiasi kwamba mpaka nikubali kununuliwa kirahisi.iwe CCM, TLP au chama chochote cha siasa wakinitaka sitawakubalia nitabaki kuwa mwanachama wa Chadema japo vyama vingi vimekuwa vikinitaka lakini sina mpango wa kwenda chama chochote ikitokea ni maamuzi yangu,”alisema Shitambala.
     Hata hivyo kujiuzuru kwa Shitambala kumeelezwa na wachambuzi wa masuala ya kiasia kwamba itakuwa ni pigo jingine kwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Mr. Sugu ambaye kimsingi kuchaguliwa kwake kumetokana na msaada wake mkubwa.
     Pia uamuzi huo wa Mwenyekiti wa Chadema mkoa ni pigo na athali kwa chama hicho mkoa wa Mbeya kwani katika kipindi cha mwaka huu viongozi wawili wamejiuzuru na kufukuzwa ambapo wa kwanza alikuwa ni Ipyana Seme ambaye aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbeya Vijijini ambaye alifukuzwa na viongozi wa makao makuu ya chama .
     Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu uliomalizika Oktoba 31 mwaka mgombea wa CCM, Mchungaji Luckison Mwanjale aliibuka kidedea wakati nafasi ya pili ilishikiliwa na Sambwee Shitambala wa Chadema

ZANZIBAR HEROES NA DAR ALL STAR ZASHINDWA KUTAMBIANA

Nov 21, 2010

MCHEZAJI wa timy ya Kombaini ya 'Dar All Star' Rashidi Gumbo 'kushoto' akipambana na mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes),Othman Ally, timu hizo zilipomenyana leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika mechi ya kirafiki. Timu hizo zilitoka suluhu.

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LANUKIA

Wakati wengine wamekwisha jihakikishia kutorudi kutokana na kuanguka ubunge. kwa kutochaguliwa au kuteuliwa na Rais katika viti vyake kumi, je ni nani wataingia tena ndani ya Baraza la mawaziri kutoka katika hawa wa zamani?
Hawa ndio walikuwa mawaziri kamili
======================================== 
Naibu Mawaziri waliopita ambao kati yao, Balozi Seiff Ali Idd yeye ameshapenya kwa kuwa sasa ni Makamu wa pili wa Rais Zanzibar  na Mohammed Abooud  na Omar Yussuf Mzee ambao tayari wamo katika baraza jipya la mawaziri la Zanzibar

JK NA MWANDOSYA ENZI HIZO

Nov 20, 2010

Kwa sababu ninaelewa wapenzi watembeleaji wa Blogu hii mtakuwa na maoni mbalimbali kuhusu picha hii, sitaweka maelezo yanayoishusu lakini kwa kudokeza tu ni kwamba hapa Rais Jakaya Kikwete yupo safarini katika ndege na Profesa Mark Mwandosya enzi kabla ya Kikwete kuwa Rais na Mwandosya  akiwa hajawahi kushika nafasi yoyote ya uwaziri ambapo hadi unafanyika uchaguzi mkuu uliomalizika alikuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji OLD IS GOLD!!

MAHAFALI YA 45 YA CBE DAR ES SALAAM

JAMILLAH Kunenge ambaye ni miongoni mwa wahitimu 1824 waliokuwa kwenye mahafali hayo ya 45 ya Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE), akiwa mwenye furaha ya aina yake, alipokuwa katika mahafali hayo leo. yeye amehitimu Diploma ya Uhasibu. 
BAADHI ya wahitimu wakiwa katika mahafali ya 45 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), leo katika chuo hicho mjini mjini Dar es Salaam. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1824 wa fani mbalimbali walitunukiwa vyeti. Waliokaa mbele wapili kulia ni  Jamillah Kunenge. 
MHITIMU wa Diploma ya Uhasibu katika Chuo cha Biashara (CBE), Judith Limbanga, akimnyonyesha mtoto wake mwenye umri wa mwezi mmoja Ernest Limbanga, katika mahafali ya 45 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini Dar es Salaam, leo.

JK ASAKATA MUZIKI NA MREMA, ASALIMIWA KWA HESHIMA NA SHIBUDA DODOMA

Nov 19, 2010

"Hongera Mheshimiwa Rais" Mbunge wa Maswa Magharibi(CHADEMA) Mh.John Shibuda akimsalimia Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kuwapongeza wabunge iliyofanyika katika viwanja vya bunge mjini Dodoma jana usiku.(Picha na Freddy Maro) 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dr.Jakaya mrisho Kikwete akilisakata rumba na Mwenyekiti wa TLP ambaye pia ni mbunge wa Vunjo Agustine Mrema wakati wa hafla ya kuwapongeza wabunge iliyofanyika katika viwanja vya bunge mjini Dodoma jana usiku. Kulia ni Mwimbaji wa Kundi la Jahazi Modern Taarab,Mzee Yussuf. (picha na Freddy Maro)

VODACOM TANZANIA YAWAKABIDHI MAGARI YAO LEO WASHINDI 100 WA SHINDA MKOKO NA VODACOM

Miongoni mwa mikoko 100 waliyokabidhiwa washindi leo 
Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa kampeni ya kuuza magari ya Hyundai, Irene Kwimbere akimkabidhi hati ya shukurani, Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, Dietlof Mare kabla ya kukabidhi magari 100 kwa washindi 100 wa 'shinda mkoko na vodacom', leo kwenye viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof akiwa na Mwamvita Makamba wa Vodacom 
Dietlof na Ofisa wa Masuala ya habari wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu wakimpongeza mmona wa washindi,  Maijo Hamisi (28) baada ya Dietlof kumkabidhi funguo ya gari lake la ushindi. 
Hamisi akishangilia kwa furaha baada aya kukabidhiwa funguo za gari lake aina ya Hyundai i10 
Hamisi ambaye ni msimamizi wa meza ya mchezo wa pool akifurahia gari lake baada ya kuingia ndani 
Mjasiriamali Theonestina Kyagala mkazi wa Kigamboni akiwa katika gari lake, akiwa ni miongoni mwa washindi 100 waliokabidhiwa gari zao leo 
Meneja Mkuu wa Dodoma Hotel, Wellingtone Maleya, naye ni miongoni mwa washindi 100 walioshinda mikoko ya Vodacom. Pichani, akiwa katika gari lake baada ya kukabidhiwa leo katika sherehe hiyo. 
Na huyu Dada wa benki ya NBC , Yolanda Aloyce pia alikabidhiwa mkoko kati ya hao 100, ndiyo hapa anaujaribu baada ya kukabidhiwa katika sherehe hiyo leo. 
BAADHI ya washindi 100 wa 'shinda mkoko na Vodacom' wakiwa kwenye sherehe hiyo, huku wakipata 'bite' kidogo kidogo kabla ya kukabidhiwa mikoko yao.
=======================================
HABARI KAMILI
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya 'Shinda Mkoko' leo imekabidhi magari 100 aina ya Hyundai i10 kwa washindi wake ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa shindano hilo lilianza rasmi Agosti 2 mwaka huu.

Katika promosheni hii iliyochukua takribani siku 100 kila siku mteja mmoja wa Vodacom Tanzania alizawadiwa gari ambapo hadi bahati nasibu hii inafikia mwisho wake ikiwa ni maadhimisho ya miaka kumi ya utoaji huduma wa kampuni hiyo nchini tayari jumla ya washindi 100 walikwishapatikana.

 Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare alisema kwa kutambua umuhimu wa jamii inayofanya nayo biashara kampuni yake iliona irudishe kiasi cha faida wanayoipata kwa wananchi ili kiwasaidie.

        "Katika kusherehekea maadhimisho haya ya utoaji huduma zenye mafanikio kwa wateja wetu na jamii kwa ujumla, tumeona tutumie fursa hii ya kumbukumbu ya miaka kumi ya utendaji wa Vodacom Tanzania kwa kurudisha faida iliyopatikana kwa wateja wetu," alisema Mare.

Akifafanua alibainisha kuwa katika kipindi cha miaka 10 ya utoaji huduma nchini Vodacom imejiwekea utaratibu wa kutoa huduma bora tena za kipekee na uanzishwaji wa promosheni mbalimbali kwa lengo la kuiwezesha na kuinua kichumi jamii ya Watanzania.

"Licha ya kuwazawadia magari 100 wateja wetu mbalimbali, pia mtandao wetu una wateja takribani milioni 6 waliojiunga kwenye huduma ya kutuma na kupokea fedha ya M-Pesa iliyoenea kote nchini," alisema.

Naye Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru alisema shindano hilo liliwahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini waliofika kutoka maeneo tofauti nchini kupokea magari yao.

Aidha aliongeza kwamba washindi katika promosheni hiyo walipatikana baada ya kuwa na pointi nyingi walizojikusanyia ambazo zilichezeshwa kwenye droo ili kumpata mshindi wa promosheni hiyo kila ilipochezeshwa.

"Wakati promosheni inaendelea baadhi ya watu walidai tusingeweza kugawa magari haya 100 kwa kuwa ni wababaishaji, lakini kupitia bodi ya michezo ya kubahatisha nchini (TGB) leo tumetimiza lengo letu na kuwazawadia washindi magari yao," alisema Mafuru.

Kwa upande wake Meneja Mtendaji wa New Dodoma Hoteli Wellingtone Maleya alisema hafla hiyo imeondoa dhana kwamba wateja walikuwa wanapeleka fedha Vodacom ili watangazwe washindi hali ambayo imedhihirika kwamba ni uzushi.

"Leo tunashuhudia wateja wa matabaka tofauti wakikabidhiwa magari yao, wengine ni mameneja, akina mama wa nyumbani na hata shamba boy. Kama ingekuwa kupeleka hela Vodacom ndio kushinda leo tungekutana tunaojiweza watupu hapa," alisema Maleya.

Hyundai i10 ni gari inayohimili mazingira ya mijini (hatchback) ambayo imetengenezwa na Kampuni ya magari na mitambo ya Hyundai Motor Company, na lilizinduliwa rasmi nchini Oktoba 31, mwaka 2007.

Gari hiyo ya gharama nafuu ni rahisi kuihudumia kwani inatumia kiwango kidogo cha mafuta ikiwa pia tofauti na magari mengine ambayo unapoyatumia unajisikia raha na kukuweka huru.
ยช