.

JK KATIKA MKUTANO WA MARAIS NA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MJINI ADDIS ABABA LEO

Jan 30, 2011

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 21 wa Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika mjini  Addis Ababa leo 
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Ghana Mheshimiwa Jerry Rawlings wakati wa kikao cha Marais na Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Afrika kinachofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 30.1.2011. 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki wakati wa kikao cha Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika kinachofanyika Addis Ababa tarehe 30.1.2011 (Picha zote na John Lukuwi).

UVCCM BADO WAIKOMALIA BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU ING'OKE

Martine Shigella akizungua katika mkutano wa Shirikisho la matawi ya Umoja wa Vijana wa CCM, wa Elimu ya Juu, leo katika ukumbi wa Vijana, Kinondoni mjini Dar es Salaam. Katika mkutano huo Shirikisho hilo lilitosa tamko kuhusu mgogoro wa mikopo ya elimu ya juu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Chiristopher Ngulaigani  na katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Taifa, Beno Malissa.  
Viongozi na makada wa UVCCM kutoka vyuo vya elimu ya juu wakiwa kwenye mkutano huo 
WAKEREKETWA wa UVCCM wa zamani, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekile Maige (kushoto) na Mbunge wa Suvye, Richard Ndasa, wakimshauri jambo , Katibu Mkuu wa UVCCM, Shigella katika mkutano huo. 
KATIBU wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM ambaye pia ni Mbunge kwa tiketi ya Jumuia hiyo, Ester Bulaya na akifurahia jambo na mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UVCCM, Huseein Bashe, nje ya ukumbi baada ya kikao hicho cha kutoa tamko.

WARSHA YA WAHARIRI KUHUSU NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA YAFANYIKA DAR

Jan 28, 2011

JENERALI Umlimwengu akizungumza katika warsha ya wahariri kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika mchakato wa Katiba mpya, iliyofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Profesa Issa Shivji. 
BAADHI YA wahariri wakiwa katika warsha ya wahariri kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika mchakato wa Katiba mpya, iliyofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Profesa Issa Shivji. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), Mkubwa Ally na Mhariri Mtendaji wa Uhuru Publications Ltd, Josiah Mufungo.

MAHAFALI YA TATU CHUO CHA KODI KUFANYIKA KESHO

MKUU wa Chuo Cha  Kodi,  Patrick Mugoya, akizungumza na waandishi wa habari, jana mjini Dar es Salaam, kuhusu mahafali ya tatu ya chuo hicho yatakayofanyika kesho. Kulia ni Ofisa Mkuu Taluma wa Chuo hicho, Imelda Rwebangira.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA NSSF ARUSHA

Jan 27, 2011

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Ludovic Mrosso ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo, akizungumza na waandishi wa habari, leo mjini Dar es Salaam, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mkutano wa siku tatu wa wadau wa shirika hilo, utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa mjini Arusha (AICC), kuanzia Februari 2, mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT) wa NSSF, Said Masimango.
========================================
Stori
MAANDALIZI ya mkutano wa kwanza wa wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), yamekamilika ambapo hadi kufikia jana wadau 400 walikuwa wamejisajili kushiriki mkutano huo.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini, Dar es Salaam, leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ludovic Mrosso ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo, alisema, mkutabo huo wa siku tatu utafunbguliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Februari 2, mwaka huu.

Alisema mkutano huo ambao utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa mjini Arusha (AICC), unatarajiwa kuhudhuriwa na wadai 600 kutoka hapa nchini.

Mrosso alisema, mbali na wadau wa ndani, pia NSSF imewaalika wadau kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Malaysia na Omani ambao kati yao wamo wataalamu mahiri na wenye uzoefu katika masuala mbalimbali ya Hifadhi za jamii.
Alisema, Katika semina hiyo, wataalam kutoka Malaysia watatoa mada kuhusu uzoefu wao katika namna ya uenezaji makazi huku wale wa Oman walitoa funzo kuhusu uwekezaji katika masuala ya nishati.

Mrosso alisema, hakuna ada ya ushiriki katika mkutano huo, na wadau wanaolengwa ni waajiri, waajiriwa, wakuu wa vitengo vya Utawala na Fedha wa maofisi mbalimbali na Wataalam mbalimbali wa masuala ya hifadhi ya jamii.

Alisema, katika mkutano huo aliouita wa kipekee, kutakuwa na mada tatu kuu zitakazozungumziwa ambazo ni Uendeshaji na Uwekezaji katika NSSF, Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi na Mamlaka ya usimamizi wa mashirika hifadhi ya jamii.

"NSSF itahakikisha washiriki wanafaidika na mkutano huo hususan kupitia elimu itakayotolewa na pia watapewa nafasi y a kujadili kwa kina dukuduku zao kuhusu masuala na changamoto mbalimbali zikiwemo shughuli za NSSF kwa jumla," alisema.

MATOKEO KIDATO CHA IV, WASICHANA WAONGOZA KUMI BORA

Jan 26, 2011

*Ufaulu waporomoka kwa asilimia 22.11
* Baadhi ya watahiniwa waandika matusi badala ya majibu!
*Kituo cha Dar es Salaam, hafutwa.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa Bara za la Mitihani la Taifa, Dk. Joyce Ndalichako alipokuwa akitangaza matokeo ya kidato cha sita, mjini Dar es Salaam.
Kuona matokeo bofya Link hii chini:-
www.moe.go.tz/NectaResults/olevel.htm

AZAM MOTO; YAIKUNJA 5-1 ARUSHA FC

BEKI wa Arusha FC, Daudi Magige (kushoto), akipambana na mshambuliaji wa Azam FC, Salum Aboubakar, timu hizo zilipomenyana leo kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Azam FC iliinyuka Arusha FC 5-1.

VODACOM YAJA NA SIMU YA WATU WENYE MATATIZO MACHO

Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom Tanzania Upendo Richard akionyesha simu maalum kwa waandishi wa habari ambayo kampuni hiyo imeizindua leo kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na kusikia,kushoto Meneja mawasiliano wa kampuni hiyo Nector Foya,kulia Msimamizi wa kitengo cha mauzo wa kampuni hiyo Mgope Kiwanga.
======================================================
STORI:

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua simu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na wenye matatizo ya kusikia.


Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nector Foya, alisema Jijini Dar es Salaam, simu hizo ni tofauti na nyingine kwa kuwa zitawawezesha wateja wao wenye matatizo ya kuona na kusikia kupata huduma ambazo hazipo katika simu za kawaida.

Alizitaja baadhi ya huduma hizo maalum zilizopo katika simu hiyo ni pamoja na maandishi makubwa katika Keypad zake, sauti kubwa katika spika zake na king'ora maalum nyuma ya simu kitakachowawezesha wateja wao kukibonyeza wakati wa dharura.

"Simu hizi za aina yake zitawawezesha wateja wetu wenye matatizo kama hayo kupata huduma ambazo hazipatikani katika simu nyingine za kawaida, natoa wito kwa watanzania wenye matatizo kama hayo kuzichangamkia simu hizi" Alisema.


Alizitaja aina hizo za simu kuwa ni S306 ZTE ambazo zitapatikana katika maduka mbalimbali maarufu kama Vodashop au kwa mawakala wa Vodacom waliopo nchi nzima.


"Tumeamua kuja na simu hizi baada ya kugundua kuwa kuna watanzania wengi wanapata matatizo na simu nyingi kutokana na maandishi madogo, sauti ndogo, na kadhalika. Lengo ni kuwasaidia na kuhakikisha ya kwamba wanaendelea kupata huduma za msingi kwa kutumia simu zao za mkononi bila vikwazo vyovyote vidogovidogo," Alisema.

Alisema kwamba simu hizo zinaweza kutumiwa hata na wasioona kwani ikibonyezwa herufi hutoa sauti inayo kujulisha umebonyeza herufi gani. Hivyo basi ni simu maalum kwa watu maalum katika jamii yetu.


Vodacom Tanzania imekuwa ya kwanza hapa nchini kubuni huduma mbalimbali kwani mbali na simu hiyo,Vodacom mapema mwaka jana ilizindua simu inayotumia mionzi ya jua ambayo imekuwa ikisaidia sana wananchi mbalimbali ambao wanapata matatizo ya miundo mbinu ya umeme.

Vodacom pia imewarahisishia mamillioni ya watanzania kupitia huduma ya Vodafone M-Pesa, huduma inayowawezesha wateja kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao za mkononi.

Mbali na kutuma pesa kwa ndugu na marafiki wanao tumia mtandano wa Vodacom. Wateja wana watumia jamaa walio katika mitandao mingine hapa nchini.

Alimalizia kwa kusema, leo tuna furaha kuwawezesha wateja wetu kuchati bure kwenye mitandao ya Face Book, the grid na Vodamail. Vodacom Tanzania itaendelea kuboresha huduma zetu mara kwa mara kwa ajili ya wateja wake na wananchi kwa ujumla

NGO ZINAZOJINUFAISHA KUPITIA MATATIZO YA WANAWAKE ZISIPEWE NAFASI-TANZANIA

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza wa Bodi ya Chombo kipya cha Umoja wa Matiafa kijulikanacho kama UN Women, chenye jukumu la kushughulikia matatizo ya wanawake katika nyanja mbalimbali zikiwemo za maendeleo, uwasa na jinsia, uwezeshwaji, Elimu, nafasi mbalimbali za uongozi, Ulinzi, Amani na Usalama na vitendo vya ukatili dhidi yao. Tanzania ni kati ya nchi kumi za Afrika ambazo ni wajumbe wa Bodi ya chombo hicho. Aliyekaa nyuma ya Balozi ni Meshacrk Ndaskoi, Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Maendeleo katika Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto.
====================================================================
HABARI KAMILI

Na Mwandishi Maalum, NEW YORK


Tanzania imeutaka Umoja wa Mataifa kutozikumbatia taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazolenga kujinufaisha kupitia matatizo ya wanawake.


Tanzania imetoa wito huo kupitia Balozi wake katika Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Bodi ya Chombo kipya cha Umoja wa Mataifa, kinachoshughulikia masuala ya wanawake maarufu kama UN-WOMEN.


Akizungumza katika mkutano huo wa siku tatu, ambao Tanzania ni kati ya nchi za kwanza zinazounda Bodi ya UN-WOMEN. Balozi Sefue anasema wakati Tanzania ikiunga mkono na kukaribisha ushirikiano wa wadau mbalimbali zikiwamo NGOs katika kuchagiza maendeleo na haki za wanawake, tahadhari ichukuliwe dhidi ya wale wanaotaka kujinufisha kupitia matatizo ya wanawake.


“tunakaribisha wazo hili la kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwamo NGOs, na hasa wale ambao kweli wamedhamiria kuonyesha kwa vitendo nia hiyo na si wale wanaolenga kujinufaisha wao” akasisitiza Balozi.


Aidha Mwakilishi huyo wa Tanzania katika UN, amekitaka Chombo hicho kipya katika ujumla wake, kuhakikisha kinakidhi kiu na matarajio ya nchi wanachama na hasa wanawake.


Anaeleza kuwa ni vema watendaji wa Chombo hicho ambacho kimechukua majukumu ya taasisi nyingine nne za UN zilizokuwa zikihusika na masuala ya wanawake. Kwamba licha ya kuwa wabunifu na wanaojituma, lakini pia wanapashwa kuyatambua kwa kujielemisha mazingira watakayofanyia kazi.


Anafafanua kwa kusema. Kila nchi inachangamoto zake linapokuja suala la kushughulikia haki, usawa na maendeleo ya wanawake. Na kwamba kila nchi ina mila, desturi na tamaduni zake, hivyo ni vema watendaji wa Chombo hicho wakayajua na kuyazingatia hayo.


Balozi Sefue anaeleza kuwa ni vema pia Chombo hicho katika utekelezaji wa majukumu yake na hasa kwa kuzingatia kwamba kitalenga zaidi kufanya kazi ndani ya kila nchi husika, kwamba kikazingatia mipango mkakati ya kila nchi na vipaumbele ambavyo nchi hizo imevichagua.


“ Kila nchi inachangamoto zake, kila nchi ina mila na taratibu zake, na kila nchi imejipangia program zake na kuchagua vipaumbele vyake, kwa hiyo ni muhimu sana kwa Chombo hiki kufanya kazi kwa ukaribu sana na serikali husika ” akasisitiza Balozi.


Akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali za kisera, kisheria na kimipango ambazo zimefanywa na serikali ya Tanzania katika kutatua kero za wanawake.


Akasema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameonyesha utashi mkubwa wa kisiasa katika kushughulika haki za wanawake na kwamba utashi huo hauishi kwa Rais tu bali hata kwa viongozi wengine wa Serikali.


Pamoja na mambo mengine akasema Tanzania imejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za utoaji wa maamuzi.


Kwa mfano, akasema kupitia juhudi hizo za serikali, Tanzania hivi sasa Spika wake wa Bunge ni mwanamke, imeazisha Benki ya wanawake, pamoja na kutoa nafasi sawa za kielimu kwa watoto wa kike na wakiume.


Hata hivyo amesema pamoja na mafanikio hayo na mengine mengi Tanzania bado ina safari ndefu katika utekelezi wa mipango ya kuwasaidia wanawake.


Akasema ni matumaini ya Tanzania ya kufanya kazi kwa karibu na Chombo hicho katika kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo ya wanawake katika Nyanja mbalimbali.


Awali Mkurugenzi Mtendaji wa UN-WOMEN Madam Michelle Bachelete ambaye aliwahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Chile. Aliainisha mbele ya wajumbe wa Bodi vipaumbele vinavyotakiwa kutekelezwa katika siku mia moja pamoja na mipango kazi ya baadaye ya Chombo hicho.

MAADALIZI TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA MWAKA HUU YAIVA: KURINDIMA FEBRUARI 9-13 NDANI YA MJIMKONGWE ZENJI.

Jan 25, 2011

MKURUGENZI wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dar es Salaam, leo,  kuhusu maandalizi ya Tamasha la Sauti za Busara, ambalo mwaka huu litafanyika Februari 9-13 nadji ya Mjimkongwe,  Zanzibar. kushoto ni Brian Karokola wa Kampuni ya Zanztel inayodhamini tamasha hilo, na kulia ni Mwenyekiti wa maadalizi ya tamasha hilo, Waziri Ally.                                        ===================================

                               STORI
SAUTI za Busara ni moja ya matamasha yenye mvuto wa kipekee barani Afrika, mwaka huu litarindima tena ikiwa ni mara ya nane Visiwani Zanzibar katika Mji Mkongwe kuanzia tarehe 9-13 mwezi ujao.
        Tamasha hili hukutanisha watu wa tanaduni mbalimbali na kuwaweka pamoja, wakisherehekea na kufahamiana kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake wa ufunguzi wa lamasha la mwaka jana.
        'tukio hili ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa kwa wageni na wenyeji wa tanaduni mbalimbali kubadilishana mawazo, kuonyeshana upekee wao, utajiri na utofauti wa muziki wetu. kwa ujumla linachangia kuimarisha muingiliano wa atanaduni na urafiki," alisema Rais Kikwete.
        Sauti za Bisara huwakutanisha wakubwa wa muziki barani Afrika na kuibua vipaji vingine nchini. Mwaka huu vikundi 40 vitatumbuiza, baadhi ni Orchestre poly Ryhmo de Cotonou (Benin),, Blick Bassy (Cameroon), Otentikk Street Brothers (Mauritius), African Stars Band -Twanga Pepeta (Tanzania), Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Kwani Experience (Afrika Kusini) na Cultural Musical Club (Zanzibar).
       Nyingine ni Mohammed Ilyas &Nyota Zameremeta ft. Bi Kidude (Zanzibar), Jangwa Music(Tanzania), Bismilahi Garger (Kenya), Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar), Djeli Moussa Diawara (Guinea) Christine Salem (Reunion),  Yaaba Funk (UK), Muthoni The Drummer Queen (Kenya), jahazi Modern Taarab  (Tanzania),  Les Freres Sissoko (Senegal), Sukiafrika Sukiyaki Allstars (Pan Africa/Far East), GROOVE Lele (Re uinion),  Vusa Mkhaya & Band (Zimbabwe/Various), Djaaka (Musumbiji), Nomakanjani Arts (Zambia), Percussion Discussion Afrika (Uganda), Tunaweza Band (Tanzania), Staff Band namasabo (Tanzania) Lelelele Africa (Kenya), Atemi & The Ma3 band (Kenya) na Sauda (Tanzania).
         Kwa mujibu wa uongozi wa Busara Promotions, sherehe za mwaka huu zitafungwa na maonyesho mbalimbali ya kuvutia, muziki wenye nakshi mbalimbali ikiwemo nyimbo za kiswahili, madansa, maonyesho ya vipande vya filamu za muziki kutoka Tanzania, Uganda, DRC, Ivory Coast na Senegal.
       Wakati huohuo, tamasha litadhamini, Busara Xtra, yaani matukio ya nje ya tamasha yatakayoandakliwa ndani ya zanzibar na ambayo yatawavutia na kuwanufaisha wageni waalikwa.
      Hii itatoa fursa kwa wasanii wa ndani kuonyesha kazi zao, kuwahamasisha wageni kuendelea kutazama maeneo mengine ya visiwa na kuongezakipato kwa watu wengi.

        Vipe vile watu 25 wanatarajiwa kunufaika kwa kupata mafunzo ya kitaaluma ya sauti (live sound engineeing), jukwaa na sanaa ya habari.

*Kwa habari zaidi peruzi katika www.busaramusic.org

YANGA YATIA PINGU 2-0 POLISI DODOMA FC JIONI HII

Jan 24, 2011

MSHAMBULIAJI wa Yanga Davies Mwape (kushoto), akichuana na beki wa Polisi Dodoma FC Nahoda Haji, timu hizo zilipomenyana  leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vdacom. Yanga ilishinda bao 2-0
"Nimechinja", Mwape akishangilia baada ya kupachika bao la pili langoni mwa Polisi 
==============
MINZIRO AANZA KAZI YA UKOCHA MSAIDIZI YANGA
Minziro akiwa kwenye benchi la Yanga, leo timu hiyo ilipomenyana na Polisi. Kulia ni Kocha Mkuu Kostadic Papic.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI HAPA NCHINI

Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha na baadaye kufanya naye mazungumzo Balozi wa Marekani hapa nchini Mheshimiwa Alfonso Lenhardt huko ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 24.1.2011 (PICHA NA JOHN LUKUWI)

SIMBA YALA MWELEKA KWA AZAM FC

Jan 23, 2011

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Jamal Mnyate, akimtoka beki wa Simba, Meshack Abel, timu hizo zilipomenyana leo kwenye Uwanja, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom. Simba imelala kwa mabao 3-1.

JK AHUDHURIA KIKAO SEMINA YA WABUNGE WA CCM LEO

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiingia katika ukumbi wa Blue Peal Hotel jijini Dar es Salaam, kuhudhuria semina hiyo, iliyoanza jana katika ukumbi huo mjini Dar es Salaam, nyuma yake ni Spila wa Bunge, Anna Makinda

SHUJAA WA SAFARI LAGER APATIKANA KUTOKA SINZA KWA WAJANJA

Jan 22, 2011

PAUL Luvinga,  mkazi wa Sinza E, kwa wajanja jijini  Dar es Salaam, ameibuka mshindi wa tuzo ya 'Shujaa wa Safari Lager' na kuondoka na kitita cha sh. milioni 7.

Mbali na kitita hicho, bia ya Safari Lager imetoa pia sh. milioni 3 kwa ajili ya mradi wa kijamii eneo anakoishi.

Luvinga, alitangazwa kutwaa ushindi huo, na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk.  Makongoro Mahanga, katika katika hafla ya kuwazawadia washindi wa tuzo hiyo, katika ukumbi wa hotel ya City Paradise, iliyopo katika jengo la Benjamin William Mkapa, jijini Dar es Salaam, jana.


Mercy Shayo mkazi wa Bomang'ombe mkoani Kilimanjaro na Leonard Mtepa wa Mwananyamala A, Dar es Salaam, ambao waliingia na Luvinga katika fainali ya shindano hilo nao walizawadiwa sh. milioni moja kila mmoja.


Hadi matokeo yanatangazwa wote watatu walioingia fainali walikuwa ukumbini wakiwa hawajui nani mshindi kati yao, kabla ya Dk. Mahanga kufungua bahasha maalum na kumtangaza Luvinga kuwa ameibuka mshindi kwa kupata kura 1555 katika jumla ya kura 1855.

Mercy aliyepata kura 605, aliingia fainali kwa sifa za kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu na kikundi cha kina mama waishio na virusi vya ukimwi wakati, Mtepa ambaye naye alipata kura 135, alimsaidia mjane asidhulumiwe nyumba kwa kumuongoza katika vyombo vya sheria hadi kupata haki yake huku Luvinga akitamba kwa sifa ya kuanzisha maktaba ya mtaani yake iitwayo 'Udzungwa Street Library' inayoendelea kusaidia watu wa rika zote kujisomea bure.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bila yake ya Safari lager, ilianza mchakato wa kumpata Shujaa huyo Novemba 24, mwaka jana, kwa lengo la kuweza kutambua juhudi za watu katika jamii ambao wamekuwa wakijitolea kusaidia makundi yenye uhitaji bila kusukumwa na vyeo au fedha walizo nazo.

Baadaye mchakato huo uliendelea kwa wananchi kutuma majina ya wale ambao walidhani wanafaa kuingia kwenye kinyang'anyiro, ambapo baadaye waliingia fainali hao watatu ambao nao walipigiwa kura kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu.

YANGA YAICHAKAZA ARUSHA FC 6-1 JIONI HII

Jan 21, 2011

Shadrack Nsajigwa wa Yanga akichuana na Emmanuel Panju wa  Arusha FC, timu hizo zilipomenyana leo kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom, na Arusha kuondoka na kapu la mabao 6-1.

JK AKUTANA NA MKUU WA BARAZA LA COMMONWEALTH

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Commonwealth Council Dr.Mohan Kaul(kushoto) pamoja na Mweyekiti wa Makampuni ya IPP Bwana Reginald Mengi(kulia) mara baaada ya kufanya mazungumzo na Dr.Mohan pamoja na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Dr.Mary Nagu(wapili kushoto), Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu(wanne kushoto) na kulia Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Emmanuel Ole Naiko(picha na Freddy Maro).

PRECISIAN WATOA OFA NAULI ZA NDEGE ZAKE

Sasa Zanzibar-Dar, Sh. 35,000 kwa ndege za kudamka asubuhi tu.
MENEJA Masoko wa Precision Air, Emillius  Rwejura, akitangaza ofa ya nauli ya sh. 35,000 kwa safari za asubuhi za ndege zake kati ya Zanziba na Dar es Salaam, katika kipindi cha  miezi mitano, kuanzia mwezi ujao. Rwejura aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, leo, alisema, Ofa hiyo ni tofauti na nauli ya sasa ya  sh. 42,000 inayotozwa  kwa safari za kawaida ambayo itaendelea kuwepo. Kulia ni  Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Phil Mwakitawa

SAFARI YA SIMBA KWENDA BRAZIL YAOTA MBAWA

Jan 20, 2011

Ni baada ya kushindwa sharti la kuifunga Atletico Paranaens ambalo mmiliki wa timu ya African Lyon aliyeileta Atletico hapa nchini. yatoka sare ya bao 1-1, katika mechi iliochezwa na timu hizo leo kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es  Salaam.

JK AONGOZA KUAGA/MAZISHI YA JAJI MSTAAFU, DAN MAPIGANO

Jan 19, 2011

RAIS Kikwete ameungana na mamia ya waombolezaji wakiwemo ndugu, majaji, mawakili na wafanyakazi mbalimbali wa tasnia ya sheria katika mazishi ya Jaji Mstaafu Dan Mapigano, leo jijini Dar es Salaam.
        Kabla ya mazishi hayo yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni, asubuhi, kwanza  Rais Kikwete aliungana na waombolezaji hao, kuaga mwili, nyumbani kwa marehemu, eneo la Mwenge.
        Baada ya shughuli ya kuaga nyumbani, mwili ulipelekwa katika Kanaisa la Wadventista wa Sabato, Magomeni Mwembechai kwa ajili ya ibada, iliyofanyika kuanzia saa 2.30 hadi saa 3.00 asubuhi.
        Baada ya ibada hiyo, mwili wa marehemu Mapigano ulipelekwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, ambako pia zilifanyika shughuli za kuuaga, kwa waombolezaji kuongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi na Jaji Mkuu Mohammed Chande Othman.
        Shughuli za kuagwa mwili kwenye viwanja hivyo zilitangukiwa na kusomwa wasifu wa marehemu ambao ambao Jaji Kiongozi, Fakih Jundu kwa niaba ya jaji Mkuu Othmani.
        Akisoma wasifu huo, pamojana na sifa kadhaa, Jaji Jundu alisema, Marehemu Jaji mstaafu, Mapigano, aliyezaliwa mwaka 1939, katika kitongoji cha Murangi wilaya ya Musoma Vijijini, baada ya masomo yake ya msingi na sekondari, alijiunga Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, mwaka 1961 kuchukua shahada ya kwanza ya biashara, lakini mwaka 1963 alisitisha masomo hayo ili kusoma shahada ya sheria.

        Mwaka 1963 alijiunga na kitivo cha sheria cha University of London/Dar es Salaam College (Lumumba) na kuhitimu masomo ya shahada ya kwanza ya sheria mwaka 1965.

        Alisema, mwaka 1966 Marehemu Mapigano, aliajiriwa na idara ya Mahakama kuwa Hakimu Mkazi na kwamba katika utumishi wake katika wadhifa huo, alifanya kazi katika maeneo mbalombali ikiwemo mikoa ya Kilimanjaro, Unguja, Pemba, Dar es Salaam.
       Mwaka 1974 aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wadhifa amabao alifanya nao kazi katika mikoa mbalimbali kabla ya kustaafu kazi mwaka 1999.
        Mbali ya Rais mstaafu, Ali Hassani Mwinyi, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Mapigano ambaye alifariki dunia, Jumamosi iliyopita, walikuwepo pia viongozi mashuhuri wakiwemo Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, Mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye.

YANGA YALALA 3-2 KWA ATLETICO

Jan 18, 2011

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Job Ibrahim akipambana na beki wa Gabliel Lima de Oliveira wa Altatico ya Brazil, timu hizo zilipomenyana leo kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, katika mechi ya kirafiki ya Kimataifa.

JK AWAAPISHA KAMISHNA NA KATIBU WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU

RAIS Jakaya Kikwete, akimwaapisha Ali Hassan Rajabu kuwa Kamishna wa T ume ya Haki za Binadamu, Ikulu mjini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Chrescent Massay alipokuwa akisubiri kuapishwa kuwa Katibu wa Tume hiyo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo. 

BAADA YA KIPIGO CHA ZANZIBAR, PAPIC USO KWA USO NA PHIRI

Jan 17, 2011

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri na Kocha wa Yanga Costadin Papic, waki-chati nje ya  hoteli ya Movenpick mjini Dar es Salaam, leo wakati wa mkutano wa timu hizo kucheza kwa nyakati tofauti na timu ya Atletico, Yanga itacheza kesho na Simba keshokutwa. Picha kutokaBlogu ya  Fullshangwe

MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI AATEMBELEA OFISI ZA UHURU /MZALENDO DAR

Mpigachapa Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo akifurahia jambo na Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, baada ya kutembelea Makao makuu ya kampuni hiyo, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mhariri wa Mzalendo, Bakari Mnkondo. 

MRADI WA MCHUCHUMA KUANZA KAZI KABLA YA JK KUMALIZA MUHULA WAKE

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC) linalosimamia mradi huo, Dk. Clisant Mzindakaya, akimtanabahisha jambo kwa undani, Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya China ya  Sichuan Hondga, Liu Canglong, kabla ya kuanza mazungumzo ya maafikiano kuhusu kuanza kwa mradi wa Mawe wa Mchucghuma na wa Chuma wa Liganga, jana mjini Dar es Salaam. 
Wawakilishi wa NDC (kushoto), wakiwa tayari kufanya majadiliao na wawakilkishi wa kampuni ya China ya  Sichuan Hondga, leo katika ukumbi wa DICC mjini Dar es Salaam.
=============================
Akizungumza na waandishi wa Habari, leo kabla ya mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa NDC,  Gideon Nasari alisema, mazungumzo hayo yatachukua siku nne, na taarifa kuhusu hatma ya mazungumzo ya maafikiano hayo  itatolewa baadaye.
Lakini akadokeza kwamba mradi wa makaa ya mawe unatarajiwa kuanza miezi sita baada ya maafikiano kufikiwa lakini zaidi ya hilo utakamilika kabla ya Rais wa awamu ya nne, Dk. jakaya Kikwete kumaliza muda wake.
DMI-St. Joseph College of Engineering and Technology

Run by Sisters of Daughters of Mary Immaculate and Collaborators & Accredited by NACTE 

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES

St. Joseph College of Engineering and Technology is a unit of internationally renowned DMI- ST. JOSEPH GROUP of Institutions which runs Colleges and Universities in India and in various African countries. The college is fully accredited by NACTE and is offering various Degrees and Diplomas. The college is well known for its discipline and quality of education that is imparted on its students. The College believes on setting standards in education and grooming students to meet the expectations of the world. To meet its expansion plans the college is in need of the following personnel, who are dedicated and committed for the development of Tanzanian Youth.The College is looking out for academicians in the following discipline on full time basis.

• Civil Engineering

• Mechanical Engineering

• Electrical and Electronics Engineering

• Electronics and Telecommunication Engineering

• Computer Science Engineering

• Information TechnologyNature of the posts: Professors/Associate Professors/ Assistant Professors.

Qualifications: PhD in relevant Engineering subject with experience.

Salary: Salary will range between Tsh 2,200,000 and 3,300,000 depending on experience. Exemptions in SALARY SCALE can be considered for deserving candidates.Duties and Responsibilities:

He/she should teach the students, as per the stipulated norms and conduct research, consultancies, extension services as recommended. He/ she should promote publications, and organize seminars and workshops. He should be ready to do any other duties assigned by the management

Interested candidates are requested to apply with their detailed CV and photograph within 2 weeks from the date of this advertisement. Send your applications toThe Registrar,

DMI- St Joseph Group of Institutions,

P O Box 11007, Dar es Salaam.

Email: jobs@dmi.co.tz

Only shortlisted candidates will be contacted. Successful candidates will be expected to join the post immediately.

BONANZA LA VODA KWA VYUO VIKUU DAR

Jan 16, 2011

Mshambuliaji wa timu ya Chuo Kikuu cha Tiba cha kumbukumbu ya Hurbert Kairuki, Joseph Mtombabali (kushoto) akimtoka mchezaji wa Chuo Kikuu cha IMTU, Edwin Alphage wakati wa mchezo wa bonanza lililofanyika katika shule ya Msingi, Mikocheni Dar es Salaam jana. Bonanza hilo liliandaliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.

BAN KI MOON ATAJA VIPAUMBELE VYA 2011

• AFRIKA KUPEWA UMUHIMU
• ATAHADHARISHA KUWA MWAKA MGUMU

Na Mwandishi Maalum
New York-Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoendelea kulikabili Bara la Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anasema bara hilo litaendelea kuwa moja ya kipaumbele chake katika mwaka huu wa 2011.

Ban Ki Moon ameyasema hayo wakati alipokuwa akivitaja vipaumbele vyake vya mwaka huu wa 2011 huku akitahadharisha kwamba kama ilivyokuwa katika mwaka uliopita mwaka huu pia utakuwa na changamoto zake.

“ Afrika bado itaendelea kuwa sehemu muhimu katika vipaumbele vyangu na vipaumbele vya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu, hasa kutokana na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara hili” akasema Katibu Mkuu.

Akivitaja vipaumbele hivyo mbele ya Mabalozi 192 wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja huo, Ban Ki Moon akiwa na Naibu wake Dkt. Asha-Rose Migiro anasema. “ Kama mwaka 2010 ulikuwa ni mwaka uliokuwa na changamoto nyingi kwa Umoja wa Mataifa, basi mwaka 2011 utakuwa zaidi”

Akaeleza kuwa kazi ya kukabiliana na changamoto hizo si ya mtu mmoja mmoja bali ni kazi inayowakabili watu wote katika ujumla wao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anakitaja kipaumbele cha kwanza kuwa ni juhudi mjumuisho za kukabiliana na suala zima la maendeleo endelevu katika dunia yenye kukabiliwa na mkwamo wa uchumi

Anasema kutokana na mkwamo wa uchumi bado watu wanahofu kubwa kuhusu ajira zao, kuhusu usalama wao na kuhusu maisha ya baadaye ya watoto wao. akaunganisha kipaumbele hicho na mkutano wa nchi maskini kuliko zote duniani utakaofanyika mwezi mei huko Uturuki.

Anasema mkutano huo pamoja na mambo mengine utalenga katika kutangaza mpango wa utekelezaji wa miaka kumi utakaoboresha hali ya usalama wa chakula, ajira, kupunguza matukio hatarishi, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na matumizi ya nishati mbadala na salama kwaajili ya nchi zinazoendelea.

Aidha suala zima la mabadiliko ya tabia nchi, ni kipaumbele cha pili kwa Katibu Mkuu huyo. Akisisitiza kwamba pamoja na mafanikio yaliyopatika katika mkutano uliofanyika Cancun, Mexico, bado kuna kazi kubwa mbele.

Uwezeshaji wa wanawake ni kipaumbele cha tatu, katika kipaumbele hicho, Ban Ki Moon anaahidi ushiriki na fursa sawa za kijinsia, kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za juu za uongonzi ndani ya Umoja wa mataifa.

Akisisitiza kuhusu nafasi ya wanawake, Ban Ki Moona anabainisha kwa kusema. “ Chukua jambo lolote lile, kuanzia mabadiliko ya tabia nchi, maendeleo, amani na usalama. Pale ambapo wanawake wanakuwa ni sehemu ya utekelezaji wa masuala hayo, basi dunia hushuhudia matokeo yanayoridhisha”.

Kuifanya dunia kuwa mahali salama ni kipaumbele cha nne, anakifafanua kipaumbele hicho kwa kuelezea pamoja na mambo mengine,juhudi za UN katika kuhakikisha demokrasia inachukua mkondo wake huko Ivory Cost, juhudi za kuleta amani ya kudumu katika Sudan pamoja na kura ya maoni ya Sudani ya Kusini.

Kwa upande wa kipaumbele cha Tano na cha Sita, Ban Ki Moon anavitaja kuwa ni kuboresha haki za binadamu pamoja na uharaka wa kushughulikia misaada ya kibinadamu kwa kujifunza kwa majanga yaliyotokea Haiti na Pakistani mwaka uliopita.

Akasema kuwa Umoja wa mataifa unaendelea na mikakati ya kujipanga vizuri katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuunganisha nguvu , uratibu na matumizi ya raslimali zilizopo ili Umoja wa Mataifa uweze kushughulikia kwa haraka na kwa ufanisi mara tu pale majanga yanapotokea.

Kuhusu upunguzaji wa silaha zikiwamo silaha kali na za maangamizi, ambacho ni kipaumbele cha saba, Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, anasema kuwa jitihada zitaendelea za kukabiliana na changamoto hizo, huku akielezea kuridhishwa kwake na hatua ya hivi karibuni ambapo Marekani na Urusi zilifikia maridhiano ya kupunguza malimbikizo ya silaha za nyukilia.

“Umoja wa Mataifa utahakikisha kwamba unaendelea na kazi kubwa ya kuhakikisha mkataba wa kupiga marukufu kabisa majaribio ya silaha za kinyukila unafanyika, na tutaongeza jitihada za kukabliana na tishio la usalama wa nyukilia na ugaidi wa kinyukilia.

Akitaja kipaumbele cha nane, Katibu Mkuu anakieleza kuwa ni mwendelezo wa mchakato wa kujisafisha, kujipanga na kuboresha mfumo wa kiutendaji, utoaji wa maamumi, uwazi, uwajibikaji zaidi ndani ya sekretarieti ya chombo hicho cha kimataifa.

Anasema kutokana na dunia kukabiliwa na changamoto nyingi na ngumu, mafanikio hayaji mara moja, lakini jambo la msingi ni kuendelea mbele kwa kujituma na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

Akazitaka nchi hizo 192 kuwa na imani naye na kwamba hapana shaka dunia inauhitaji Umoja wa Mataifa wenye nvugu na kuwajibika zaidi.

KATIBU  MKUU WA UMOJA WA MATAIFA, BAN KI MOON AKIVITAJA VIPAUMBELE VYAKE NANE  VYA MWAKA 2011 MBELE YA MABALOZI 192 WANAOZIWAKILISHA NCHI ZAO KATIKA UMOJA WA MATAIFA. KUSHOTO KWAKE NI NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA DKT. ASHA-ROSE  MIGIRO NA KULIA NA RAIS WA BARAZA KUU LA  65 LA UMOJA WA MATAIFA, BW. JOSEPH DEISS

JK APOKEA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS KIBAKI LEO, AKUTANA NA BALOZI KALAGHE JANA

Jan 14, 2011

Mjumbe maalum wa Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Mhe.Robinson Njeru Githae akimkabidhi RaisDr.Jakaya Mrisho Kikwete ujumbe kutoka kwa Rais Kibaki ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Bwana Githae ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya jiji la Nairobi aliambatana na maofisa waandamizi kutoka ubalozi wa Kenya nchini Tanzania 
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh.Peter Kallage Ikulu jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Freddy Maro

MABONDIA FRANCIS MIYEYUSHO NA JUMA FUNDI KUZIPIGA MWEZI HUU

MABONDIA Juma Fundi (kushoto) na Francis Miyeyusho (kulia),  wakitunishiana misuli, wakati likitangazwa pambano hilo leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mjini Dar es Salaam. Katikati ni mratibu wa mpambano huo, Khalifa Kipao wa Kipao Entertainment.

MUUNGANO WA WANAJESHI WASTAAFU TANZANIA WAANZISHWA

MWENYEKITI wa  Muungano wa wanajeshi  Wastaafu Tanzania, Assed Mayuggi, akionyesha hati ya usajili wa chama hicho, leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) mjini Dar es Salaam. 

MKUTANO WA MAJAJI WANAWAKE WAFANYIKA LEO DAR

Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, aifunfua mkutano wa Majaji wanawake, leo katika ukumbi wa mikutabo wa kimataifa mjini Dar es Salaam (DICC) 
Washiriki wakiwa katika mkutano huo

ABS LANUSURIKA KUPINDUKA

ABIRIA waliokuwa katika basi hili la kampuni ya ABS iliyokuwa ikisafiri kutoka Iringa kwenda Dar es Salaam, wakiwa nje ya basi hulo baada ya kuacha barabara katika harakati za kujinusuru kugongana na lori moja, jana, eneo la Misugusugu, Barabara ya Morogoro, Kibaha mkoa wa Pwani. (Picha kwa hisani ya Diwani wa Kibaha, Mheshimiwa, Selina Wilson).

MZEE WA CHACAHANDU DAILY NA RAFIKI YAKE FRANCIS DANDE WA BLOGU YA JAMII WAKIVUKA BAHARI KUTOKA ZENJI KWENDA DAR LEO

Jan 13, 2011

Wakiwa katika boti ya kilimanjaro, kutoka Zanzibar kurejea Dar baada ya kushuhudia mtanange wa Simba na Yanga, ambapo yanga iklinyukwa mabao 2-0

YANGA YALALA KWA SIMBA ZANZIBAR; YATUNGULIWA 2-0


TIMU ya Yanga imeshindwa kufurukuta kwa Simba, baada ya kutandikwa mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi, kwenye Uwanja wa Aaman mjini Zanzibar.
Ni bao lililofungwa na Shija Mkina lililoiwezesha Simba kuibuka na ubingwa. Kutokana na matokeo hayo, Simba imeanza mwaka kwa kuwafunga watani wao na kulipiza kisasi cha kufungwa na timu hiyo zilipokutana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka jana mjini Zanzibar.

Yanga ndiyo iliyoanza mchezo kwa kasi huku ikitandaza kandanda safi na wachezaji wake kucheza kwa kuelewana kwa kugongeana pasi fupifupi ambazo wachezaji wa Simba walishindwa kuzidhibiti takribani dakika tano za mwanzo za mchezo huo.,


Dakika ya tisa, Yanga ilipata nafasi ya wazi kwa Idd Mbaga kumtoka beki wa Simba Jerry Santo lakini akaachia shuti lililoishia mikononi wa kipa wa Simba Ally Mustapha.

Simba ilijibu shambulizi hilo dakika ya 12 kupitia kwa Patrick Ochan aliyepiga shuti ambalo kipa wa Yanga Yaw Berko alitema kabla ya mabeki kuondosha mpira huo katika eneo la hatari.

Dakika moja baadae Simba iligfanya shambulizi jingine kupitia kwa Hiraly Echesa aliyepiga shuti kali baada ya kupata nafasi ya wazi lakini mabeki wa Yanga walizuia hatari hiyo na kuokoa mpira golini kwao.

Simba iliendelea kufanya mashambulizi makali langoni mwa wapinzani wao huku ikitafuta mabao ya kufunga na dakika ya 20 Mussa Hassan 'Mgosi' alipata nafasi baada ya kubaki na kipa lakini shuti hafifu alilopiga lilijaa mikononi mwa Berko.

Dakika ya 33 Mussa Hassan 'Mgosi' aliipatia Simba bao la kwanza baada ya kupokea pasi safi iliyopigwa kutoka wingi ya kulia na kuachia shuti kali lililomshinda kipa Yaw Berko wa Yanga na kujaa moja kwa moja wavuni.


Kipindi cha kwanza kilimalizika kw Simba kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa nbao 1-0, na kipindi cha pili kilipoanza Simba ilianza mchezo kwa kasi huku ikitafuta mabao mengine lakini mabeki wa Yanga walikaa imara na kuzuia hatari zilizojitokeza katika lango lao.


Hata hivyo mabeki wa Yanga hawakufua dafu kwa watoto wa Msimbazi ambao kila dakika zilivyozidi kuyoyoma ndivyo walivyozidisha mashambulizi huku wachezaji wa Yanga wakionekana kupoteana.

Yanga nao walifanya mashambulizi ya kushitukiza langoni mwa Simba kila walipopata nafasi lakini umaliziaji mbovu na shuti hafifu alizopigiwa kipa Ally Mustapha ziliifanya timu hiyo kushindwa kupata walau bao moja.

Laiti kama Simba ingetumia vyema nafasi nyingine ilizopata dakika ya 49, 52 na 66 kupitia kwa Jerry Santo, Mgosi na Echesa ingeweza kupata mabao mengi zaidi lakini umaliziaji uliifanya timu hiyo kushindwa kufunga mabao mengine.

Kutokana na ushindi huo Simba wamepata kombe lenye thamani ya sh. milioni 3 na fedha taslim sh. milioni 5.

Kwa mara ya kwanza Simba  iliifunga Yanga mjini Zanzibar kwa ambapo mwaka 1992, katika fainali ya kombe la Kagame ilishinda kwa mikwaju ya penalti 6-5.

Vikosi: Simba:- Ally Mustapha, Haruna Shamte, Meshack Abel, Jerry Santo, Abdulrahim Humoud, Mohamed Banka, Hirally Echesa, Mussa Hassan 'Mgosi' Patrick Ochan na Nico Nyagawa.


Yanga:Yaw Berko, SalumNtelela, Abuu Ubwa, Isack Boakye, Job Ibrahim, Ernest Boakye, Godfrey Bonny, Juma Seif, Razack Halfan/Kigi Makasi, Idd Mbaga na Davis Mwape.
ยช