.

WASANII WA FILAMU WALALA 2-0 KWA WENZAO WA BONGO FLEVA

Feb 26, 2011

MCHEZAJI wa timu ya Wasanii wa filamu, John Mhuvile 'Joti'  wa kundi la Komendi Orijino (kushoto) akichuana na mcezaji wa timu ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Producer, timu hizo zilipomenyana leo kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, katika pambano la hisani kwa ajili ya walioathirika na milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto, wiki iliyopita. Bongo Fleva wameibuka na ushindi wa mabao 2-0

EVER BUJIKU AFUZU KIDATO CHA SITA, ST. ANTHONY, MBAGALA
















BARAZA LA PILI LA MAJADILIANO YA PAMOJA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Feb 25, 2011

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, akifungua Baraza la Pili la Majadiliano ya pamoja katika Utumishi wa Umma, katika ukumbi wa wizara hiyo, leo. Wengine kutoka kushoto ni Wajumbe wa Baraza hilo, Hamis Dihenga, Geonge Yambesi na Mathias Kabunduguru. 
Group photo

KUTOKA MAREKANI

UNACHANGAMOTO KUBWA YA KUTAFSIRI KWA VITENDO SERA NA MIPANGO INAYOHUSU JINSIA- NAIBU WAZIRI
NA MWANDISHI MAALUM, NEW YORK
Pamoja na ukweli kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuingiza masuala ya jinsi katika sera, mikakati na mipango yake, bado inakabiliwa na changamoto za kuzitafrisiri kwa vitendo, sera, mipango na mikakati hiyo.  Hayo yameelezwa Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii , jinsia na Watoto, Mhe. Ummi Alli Mwalimu (pichani), wakati alipokuwa akichangia majadiliano kuhusu fursa na ushiriki wa wanawake na watoto wa kike katika elimu, mafunzo, sayansi na teknolojia pamoja na fursa sawa katika ajira.
       Naibu Waziri Ummi Mwalimu , anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wa 55 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ujumbe huo pia unajumuisha washiriki kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
        Anazitaja changamoto hizo kuwa ni katika kufanya uchambuzi wa masuala ya jinsia na ufinyu wa takwimu za jinsia ambazo zingeweza kutoa ushawishi katika maandalizi na utekelezaji wa sera na mipango.
        Naibu Waziri Ummi Mwalimu amewaeleza washiriki wa mkutano huo, kwamba changamoto nyingine ni katika kubadilisha mawazo na mitizamo ya jamii kuhusu suala zima la maendeleo na ushiriki wa wanawake.
       Hata hivyo anasema pamoja na changamoto hizo, serikali inaendelea na kazi ya kuzikabili na kuzifanyia kazi kwa kuwa imejiweka misingi madhabuti. Na kubwa zaidi ni utashi mkubwa wa kisiasa ulioonyeshwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na serikali zima katika kuwapatia fursa sawa wanawake katika ngazi za maamuzi.
       Akizungumzia kuhusu ushiriki wa wasichana katika masomo ya Sayansi, Naibu Waziri anasema idadi ya wasichana wanaojiunga na Masomo ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imeongezeka maradufu.
        Anasema mafanikio hayo yametokana na uamuzi wa Serikali wa kuweka mpango mahsusi wa kuwasaidia wasichana kwa kuwapatia mafunzo ya awali yanayowaweza kujiandaa na kufanya vizuri katika mitihani ya usaili kabla ya kujiunga na masomo ya sayansi.
       Akaeleza kuwa kupitia utaratibu huo idadi ya wanafunzi wasichana wanaochukua masomo ya Sayani imepanda kutoka asilimia 7 mwaka 2003-2004 hadi kufikia asilimia 27 mwaka 2007-2008. Aidha idadi ya wasichana wanaojiunga na elimu ya juu imeongezeka kutoka asilimia 32.2 hadi kufikia asilimia 35.5.
      Kuhusu ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi, Mhe. Ummi Mwalimu anasema, Baada ya kutambua tatizo la ushii mdogo wa wanawake katika ngazi za maamu, iliamua kwa makusudi kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutoa mwanya wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika Bunge na mabaraza ya Serikali za Mitaa.
        Kutokana na marekebisho hayo, idadi ya wabunge wanawake ni asilimia 35 ya viti vyote kukiwa na ongezeko la wabunge wanawake kutoka 63 mwaka 2004 hadi 125 huku nafasi ya Spika wa bunge ikishikiliwa na mwamamke. Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi uwiano wa wanake katika baraza hilo ni asilima 30
       Kwa upande wa vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike, Naibu Waziri anasema kuwa serikali imepitisha sheria mbalimbali dhidi ya wale wanaokiuka haki za wanawake na watoto wa kike.
“tumejitahidi kutimiza wajibu wetu kwa kuendana na matakwa ya kimataifa kuhusu maendeleo, ulinzi na usawa wa wanawake. Aidha Serikali imeingia, imesaini au imeridhia mikataba ya kimataifa inayohusiana na maendeleo na ulinzi wa wanawake” anasisitiza Naibu Waziri Ummi Mwalimu.
       Ameihakikishia kamisheni hiyo ya Hali ya Wanawake kwamba Tanzania inaendelea na jukumu la kuhakikisha inaondoa mifumo yote inayomkandamiza mwanamke kwa kuzingatia malengo na maudhui ya mikataba na matamko ya kimataifa.

HII NAYO NI HUDUMA NYINGINE YA TTCL?

Baada ya husimduma  za 'Rafiki Simu ya Kadi'  ya Shirika la Simu Tanzanaaia (TTCL) kufa, baboksi ya huduma hiyo sasa yamebaki yakitumiwa na wateja wa aina nyingine, kama Chachandudaily Blog, ilivyomshuhdia mlinzi akipata huduma hiyo mpya kwenye moja ya boksi lililopo nje ya hospitali ya Aljumaa, Kariakoo, jijinni Dar es Salaam.

JK AREJEA NCHINI LEO

Feb 24, 2011

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika ,mazungumzo na Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal(watatu kushoto),Waziri mkuu Mizengo Pinda(wanne kushoto) pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  leo jioni akitokea nchini Ivory Coast ambapo alishiriki katika juhudi za kutatua mgogoro wa kisiasa nchini humo.(Picha na Freddy Maro)

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MITAMBO YA KUFUA UMEME YA DOWANS

WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakikagua mitambo ya umeme ya Dowans, Ubungo, Dar es Salaa, leo 
MKURUGENZI wa Fedha wa Kampuni ya Dowans,  Stanley Munai (kulia) akizungumza na waandishi wa habari, waliofuatana na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, leo, kwenye mitambo ya kampuni hiyo, Ubungo, Dar es Salaam.

KIBONZO CHA LEO

Kibonzo hiki ni kwa hisani ya gazeti la Majira la leo

Feb 23, 2011

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akifafanua jambo wakati wa semina ya wateule watakaoshiriki kinyang'anyiro hicho. Zifuatazo chini ni picha za wasanii wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Paradise, ndani ya jengo refu la Benjamin William Mkapa, katikati ya jiji la Dar es Salaam. (Picha zote na Chachandudaily.blogspot.com)










IDADI YA WANAWAKE WASIOJUA KUSOMA HAIJASHUKA-MIGIRO




NA MWANDISHI MAALUM,NEW YORK
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro

 Imeelezwa kuwa wanawake ni theruthi mbili ya watu wote wazima wasio jua kusoma. Na kwamba takwimu hizo hazijaonyesha dalili ya kushuka kwa takribani miaka ishirini sasa.


Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Ufunguzi wa mkutano huo wa wiki mbili umefanyika siku ya Jumanne hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York.


Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo, unaongozwa na Mhe. Ummi Ally Mwalimu (MB),Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.


Akiuhutubia umati wa wajumbe kutoka nchi wanachama 192 wa UM, Migiro anaeleza kuwa licha ya kwamba uwekezaji katika elimu hususani kwa wanawake na watoto wa kike ni jambo lisilo na ubishi, bado kundi hilo la jamii limeendelea kuachwa nyuma.


Anasema Migoro, “ wakati mkiwa mmechagua elimu kama dhima kuu la mkutano wenu. Na wakati tunajadili hali ya wanawake, ni vema mkatambua kwambaTheruthi mbili ya watu wazima wasio jua kusoma ni wanawake. Na takwimu hizi hazijabadilika kwa kipindi cha miaka 20.


Kwa hiyo anasema Naibu Katibu Mkuu, hakuna jambo jema kama uwekezaji katika elimu, manufaa yake ni makubwa na ni mengi. Elimu sit u kwamba ni ufunguo muhimu katika ukuaji wa uchumi. Lakini ni nyezo muhimu sana katika uwezeshaji wa mwanamke.


Akabainisha kuwa nchi nyingi zimejidhatiti sana katika kuhakikisha kwamba zinafikia lengo la kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule na bila ya kujali jinsia yake anapata fursa hiyo.


Hata hivyo anasema kuwa pamoja na jitihada hizo kumnufaisha mtoto wa kike, lakini bado kunachangamoto kubwa wenye ubora wa elimu inayotolewa.


“ Bado ubora wa elimu inayotolewa hususani katika nchi zinazoendelea haujaendana na kasi ya kuandikishaji wa watoto. Watoto wengi wanamaliza shule wakiwa hawana ujuzi na maarifa ya kusoma wala kuhesabu” anabainisha Migiro.


Kama hiyo haitoshi, Naibu Katibu Mkuu anaeleza zaidi kwa kusema, uwakilishi wa wanawake katika Nyanja za sayansi, teknolojia ,elimu na ajira bado ni wa kiwango cha chini.


“ kwa ufupi ni kwamba hawapati ujuzi na maarifa yatakayowawezsha kushindana katika soko la ajira la dunia ya leo: anasisitiza Naibu Katibu Mkuu.


Akawataka wajumbe wa mkutano huo, kuutumia mkutano huu kujadiliana na kubadilishana mawazo na hatimaye kutoka na majibu ya mambo ya msingi ambayo bado yanaendelea kuwa kikwazo kwa maisha bora na maendeleo ya mwanamke.


Aidha amewataka wajumbe hao kuendeleza harakati za kumkomboa mtoto wa kike na vilevile kupinga ukatili dhidi ya mwanamke.

MABOMU GONGOLAMBOTO: KAMATI YA BUNGE MAMBO YA NJE NA SPIKA WATEMBELEA MAENEO YA TUKIO; MISAADA YAZIDI KUMIMINIKA, YANGA UPANDE WA TIMU ZA SOKA, TWANGA UPANDE WA BENDI ZA MUZIKI

Feb 22, 2011

SPIKA wa Bunge Anna Makinda akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, hundi ya Sh. milioni 37.80,  leo, kweye kituo cha uratibu na kupokea misaada kwa ajili ya waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, kilichopo, Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ukonga.Fedha hizo zimetolewa na wabunge kwa kusaidia wananchi walioathirika ma mabomu hayo. Kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecky Sadiki.
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Edward Lowassa, akikaribishwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, yeye na kamati hiyo walipotembelea leo, kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzaniani, Gongo la Mboto, Dar es Salaam, kufahamu mazingira na hasara ya milipuko ya mabomu iliyotokea katika ghala la silaha la JWTZ katika kambi hiyo, Jumatano iliyopita. 
MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa mkoa huo, Saidi Mecky Sadiki (kushoto), akitoa taarifa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kuhusu  mwenendo na hatua zilizochukuliwa na serikali ya mkoa huo, dhidi ya maafa ya milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto,Waziri Nahodha alipotembelea kituo cha  tathmini na kupokea misaada kwa waathirika wa mabomu hayo, kilichopo Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ukonga, leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inpekta Jenerali, Saidi Mwema

Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha akiwaachia maelekezo , Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inpekta Jenerali, Saidi Mwema na Kova


Mwenyekiti wa CUF, Prof, Ibrahim Lipumba akibeba kiroba cha unga uliotolewa msaada na chama chake kwa ahili ya waathiriwa wa mambomu 
Wachezaji wa Yanaga wakimkabidi msaada wao Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Anayekabidhi ni Fred Mbuna.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,  Victor Kimesela akikabidhi msaada wa shuka 166 kweneye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Ukonga.
Wafanyakazi wa TiGo wakikabidhi msaada wao kituo cha kupokela misaada cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ukonga.

TBL YATANGAZA WATAKAOSHINDANA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARD MWAKA HUU

Feb 21, 2011

Mwakilishi wa Lloyd Zhungu (kulia), akimkabidhi Mratibu wa Shindano la Kilimanjaro Tanzania Music Awards kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Angelo Luhala, bahasha yenye lakili , yenye nyimbo na wasanii waliopitishwa kuwania tuzo hizo leo. 
Luhala akitangaza nyimbo na majina ya wasanii hao. Kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe
Baadhi ya waandishi wa habari za Michezo na burudani waliohudhuria mkutano huo



ยช