a Stars iliwasili jana salama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo saa
5.52 asubuhi (saa 6.52 kwa saa za nyumbani) kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea
Nairobi. Timu iko hapa kwa ajili ya mechi ya ufunguzi wa Uwanja wa Taifa. Uwanja
huo mpya ambao capacity yake ni watazamaji 40,000 umejengwa na Wachina na uko
nje kidogo ya Jiji la Maputo ambapo ni wastani wa saa moja kwa gari kutoka
mjini.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa uwanja huo ambao ndiyo utakaotumika kwa
michezo ya All Africa Games Septemba mwaka huu atakuwa Rais wa Msumbiji wakati
Rais Jakaya Kikwete anawakilishwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Emmanuel Nchimbi. Timu imefikia hoteli ya VIP Grand ambapo jana saa
12.30 kwa saa za hapa ilifanya mazoezi Uwanja wa Taifa kwa dakika 45.

Mechi itaanza saa 12.30 jioni kwa saa za hapa, na itachezeshwa na waamuzi kutoka
Swaziland. Mwamuzi ni Simanga Hhleko wakati wasaidizi wake ni Bhekisizwe
Mkhabela na Lybnah Sibiya. Fourth official ambaye ni wa hapa Msumbiji ni Estevao
Matsinhe.

Taifa Stars line up;
Shabani Dihile (1)
Shadrack Nsajigwa (14)- captain
Amir Maftah (3)
Aggrey Morris (6)
Nadir Haroub (13)
Nurdin Bakari (5)
Mohamed Banka (16)
Shabani Nditi (19)
John Boko (9)
Machaku Salum (11)
Mwinyi Kazimoto (22)

Substitutes:
Shabani Kado (18)
Kigi Makasi (7)
Julius Mrope (8)
Ramadhan Chombo (21)
Jabir Aziz (12)
Mbwana Samata (10)
Juma Nyoso (4)

Officials:
Jan Poulsen- Head Coach
Sylvester Marsh- Assistant Coach
Juma Pondamali- Goal keeping Coach
Leopold Tasso- Team Manager
Dr Mwanandi Mwankemwa- Team Physician
Alfred Chimela- Kit Manager

Timu itaondoka hapa kurejea nyumbani kesho April 24 saa 11.35 kwa Kenya Airways
hadi Nairobi ambapo itakaa kwa muda ikisubiri kubadili ndege kwa ajili ya safari
ya Dar es Salaam.
My contact in Maputo +258 767 310242
Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation