.

RAIS KIKWETE AMPONGEZA ASKOFU MPYA ALBERT RANDA WA KANISA LA MENONITE MWANZA

May 29, 2011

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Askofu Mpya wa  kanisa la Menonite Dayosisi ya Mwanza Mhashamu Albert Jella Randa katika sherehe za kimsimika askofu huyo mpya zilizofanyika huko Nyakato Mwanza leo mchana (picha na Freddy Maro)

SEKTRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA (NEC) KUANZA ZIARA RUKWA MEI 31, MWAKA HUU

 CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI  NDOGO YA MAKAO MAKUU  S.L.P. 9151 DAR ES SALAAM F2180108

 Barua zote zipelekwe kwa Katibu Mkuu                                               Fax: 255-022-2185245; 022-2184580

  
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa itafanya ziara ya siku nne (4) Mkoani Rukwa kuanzia tarehe 31 Mei, 2011.  Pamoja na mambo mengine ziara hiyo itakuwa na dhumuni la kukutana na wanaCCM na Wapenzi wa CCM na kufikisha maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa iliyofanyika tarehe 10-11 Aprili, 2011.

Katika ziara hiyo, ujumbe huo wa Sekretarieti utaongozwa na Ndugu Nape M. Nnauye, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa – Itikadi na Uenezi.  Kutokana na ziara hiyo, wanaCCM, Wakereketwa, wapenzi wa CCM na wananchi kwa ujumla wao wanaombwa kuhudhuria mikutano ya hadhara inayotarajiwa kufanywa katika maeneo mbalimbali kama ratiba inavyoonyesha.

Ratiba ya ziara hiyo ni kama ifuatavyo hapa chini:-


TAREHE
MUDA
SHUGHULI
MAHALI
MHUSIKA
31/5/2011
3.30-400
Mapokezi
Mji Mdogo wa Laela (Barabara Kuu)
Viongozi wa CCM Mkoa
4.00-6.00
Mkutano wa Hadhara
LAELA
Katibu wa Wilaya
6.00-7.30
Kuelekea Sumbawanga Mjini
Katibu wa Mkoa
8.00-12.00
Mkutano wa Hadhara
Uwanja wa Mandela
Katibu wa Wilaya
1/6/2011
4.00-6.00
Mkutano wa Hadhara
Namanyere (Wilaya ya Nkazi)
Katibu wa Wilaya
9.00-11.00
Mkutano wa Hadhara
Kabwe
Katibu wa Wilaya
11.00-12.30
KUELEKEA MAJIMOTO (KULALA)
2/6/2011
4.00-6.00
Mkutano wa Hadhara
Maji Moto
Katibu wa Wilaya
8.00-11.00
Mkutano wa Hadhara
Usevya
Katibu wa Wilaya
KULALA       MPANDA
3/6/2011
4.00-6.00
Mkutano wa Hadhara
Kakese
Katibu wa Wilaya
9.00-12.00
Mkutano wa Hadhara
Mpanda Mjini
Katibu wa Wilaya


Imetolewa na:


Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
29/5/2011

NELLY KAMWELU MISS UNIVERSE 2011

 Nelly Kamwelu (katikati) akiwa na Mshindi wa pili Neema Kilango (kulia) na mshindi wa tatu Yacoba Assenga baada ya kutwaa taji la Miss Universe, 2011, jana.

ISRAEL YATAKIWA KUWACHIA WAFUNGWA WA KIPALESTINA

Na Mwandishi Maalum

Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, 
 Mahadhi Juma Maalim akizungumza wakati wa Mkutano huo.

Mawaziri wa Mambo ya Nje  kutoka  nchi zisizofungamana na upande wowote   maarufu kama Non –Aligned Movement (NAM), wameitaka Israel kuwaachia huru wafungwa wa  kisiasa wa  Kipalestina.

Mawaziri hao ambao walikutana kwa siku nne katika mkutano wao wa 16 uliofanyika Bali, nchini Indonesia, wamesisitiza katika tamko lao kwamba   kitendo cha   Israel kuwaachia wafungwa  hao kitakuwa nikupiga  hatua moja muhimu kuelekea mchakato wa  amani ya kudumu.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umeongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  na  Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi Juma Maalim (MB). Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Tanzania katika  mkutano huo.

Mawaziri hao  katika tamko lao wameitaka  Israeli kuachia huru idadi kubwa ya wafungwa wa kisiasa  wa kipalestiana, kitendo ambacho kitatafisiriwa kama hatua sahihi inayolenga kujenga mazingira ya kuaminiana  na kufungua milango ya mazungumzo kati ya  pande hizo mbili zinazohasimiana.

“Tunaitaka Israeli kuwaachia huru angalau wafungwa 300 ambao kati yao ni watoto walio chini ya miaka 18 wakiwamo pia wanawake. Tunasikitishwa sana na mwendelezo wa vitendo visivyo vya kibinadamu dhidi ya wapalestina” inasema sehemu  ya tamko hiko.

Inakadiriwa kwamba kuna wafungwa  wa kiasiasa wa Kipalestina wapatao 6,000 waliofungwa  nchini Israel.

Kupitia tamko hilo, Mawaziri wa NAM wanasema  licha ya kuitaka Israel kuwaachia huru wafungwa hao wa kisiasa, pia inaunga mkono  uwepo wa mataifa mawili yanayoishi sambamba kwa  kuzingatia mipaka ya  mwaka 1967.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Naibu Waziri Mahadhi Juma Maalim, amesema, wakati Tanzania  ikiridhishwa  na  kile ambacho NAM imefanikiwa  kukitekeleza katika kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, lakini bado inasikitishwa sana na kutopatikana kwa ufumbuzi wa suala zima la  matatizo ya Palestina.

  Tatizo la Palestina limesuasua kwa muda murefu sana, na kusababisha madhara makubwa. Ujumbe  wa Tanzania leo hii  ni  mfupi na ulio wazi,  nao ni kwamba, madhara na maumivu wanayoyapata wananchi wa palestina ni lazima  sasa yakomeshwe ” anasema  Naibu Waziri

Na kuongeza. “ Maeneo yanayokaliwa kimabavu na waisraeli lazima yarudishwe kwa wananchi wa Palestina. Na  ndoto iliyodumu kwa muda mrefu ya  wananchi wa  Palestina  ya kuwa na taifa lao huru na mji mkuu wao ukiwa ni  Mashariki ya Jerusalemu, wakiishi sambambana na kwa amani na usalama na taifa la  Israeli ni lazima itimie  sasa”.

Akabainisha kwamba,   Jumuia ya Kimataifa inaowajibu wa kutowaangusha wananchi wa Palestina,  halikadhalika NAM nayo haipashwi kuwaangusha  raia wa Palestina.

Akizungumzia wajibu wa NAM na hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto  mbalimbali, Naibu Waziri anasema  wanachama wa NAM wanatakiwa kuwa kitu kimoja na kushikamana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.

Anasema  Naibu Waziri , nchi wanachama wa  NAM ambazo hivi sasa wamefikia 120 baada ya kujiunga kwa FIJI na AZEBAIJAN wanatakiwa kushikamana na kuwa kitu kimoja katika kuzikabili changamoto za sasa na zile  mpya zitakazoimbuka.

“ Ni lazima na ni wajibu wetu kutumia nguvu na uwingi wetu, tupo wanachama 120 hivi sasa, idadi hii inatupa nguvu  ya kusukuma mbele  ajenda  zinazolenga  kuleta mabadiliko katika mfumo wa utendaji kazi wa Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa.” akasema

 Na kuongeza kuwa  idadi ya wanachama wa NAM inawawezesha    kuitisha mabadiliko katika utekelezaji wa ahadi za mipango ya maendeleo, kusisitiza upokonyaji wa silaha,  uwepo wa  mifumo  halali na sawa ya biashara  na itakayojielekeza katika uainishaji wa matakwa sahihi ya nchi maskini zaidi duniani.

“haya ni mambo ambayo tunaweza kuyasimamia kama tukiamua.” Anasema Naibu Waziri.

Akimnukuu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuhusu nguvu na wajibu wa   NAM katika masuala mbalimbali yakiwamo ya nguvu za kiuchumi.


Alisema hivi  miaka ya 1970 na hapa ninamnukuu “ Tunaweza kusaidiana kuimarisha uhuru wetu na kukataa kutaliwa kiuchumi kwa kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana kwa faida yetu pamoja. Kwa sababu hatutaweza kamwe kuwa  na uhuru wa kweli  kama tu wadhaifu kiuchumi, huku matarajio yetu kiuchumi  yakitulazimsiha kupiga makoti kama vile waokotezaji au  ombaomba kutoka kwa mataifa makubwa”.


Mkutano huo wa 16 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NAM licha  ya kujadili suala la Palestina, pia walijadiliana kwa kina na kubadilishana  mawazo kuhusu mwelekeo  na mchango wa  baadaye wa  NAM katika kipindi cha miaka 50 ijayo na hasa kwa kuzingiatia  mabadiliko makubwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia hivi sasa.

NAM ambayo imetimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1961 pamoja na kutoa mchango mkubwa sana katika kipindi cha uhai wake,  yakiwamo mafanikio ya kumalizwa kwa ukoloni.

Lakini baada ya kumalizika kwa  vita baridi ambayo  hasa ndiyo iliyopeleka kuanzishwa kwa  chombo hicho kisichofungamana na upande wowote. Sasa  NAM inalazimika kujitazama upya na kutafakari nafasi yake, nguvu yake na ushawishi wake katika dunia inayobadilika kwa kasi huku ikikabiliwa na changamoto  mbalimbali.

WANAHARAMU WAMTIA UMASIKINI MWAIKENDA; WAMPORA KAMERA, LAP TOP NA VITENDEA KAZI KIBAO

Na Mwandishi Wetu

MPIGAPICHA Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, ambaye pia ni Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda ameporwa begi lenye kamera na kompyuta na
vibaka waendesha pikipiki.

Vibaka hao waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki, walimpora begi hilo lililokuwa kiti cha mbele cha gari lake alilokuwa akiendesha, likiwa karibu na makutano ya barabara za  Kitunda na Nyerere, eneo la Banana, Ukonga, Dar es Salaam Jumamosi wiki iliyopita.

Aliyechukua begi kwenye gari ni kibaka aliyepakizwa nyuma na pikipiki hiyo kuondoka kwa kasi kuelekea
Ukonga na kumwia vigumu mpiga picha huyo kuachia usukani kuwafukuza kwani magari yalikuwa yameanza kutembea.

Alitaja vitu vingine vilivyokuwemo kwenye begi hilo kuwa ni, Modemu ya Vodacom, kifaa cha kutolea picha kutoka kamera ya digital kwenda katika kompyuta (Card reader),
Flash, vitambulisho vya kazi na nyaraka muhimu.

Akisimulia tukio hilo, Mwaikenda alisema , inaelekea vibaka hao walimfuatilia kutoka Kitunda ambapo
alisimamisha gari lake na  kuchukua kamera kwenye begi na kupiga picha mashimo makubwa barabarani karibu na Kituo Kidogo cha Polisi cha Kitunda.

Mwaikenda alikuwa anatokea nyumbani kwake, Kivule kwenda Pugu Kanisani  kuripoti tukio la Ibada ya misa ya shukrani kwa Hayati Papa John Paul wa Pili kutangazwa Mwenye Heri.

Nkoromo Daily Blog, inatumia fursa hii kumpa pole Kamanda wa Matukio. ikiamini kwamba za mwizi arobaini

WASHINDI TUZO ZA kILI TANZANIA MUSIC AWARS 2011 WAWASHA MOTO MJINI MOSHI

Waimbaji wa bendi ya Mapacha Watatu, Jose Mara na Khalid Chokoraa (kulia) akitumbuiza wakati wa tamasha la wanamuziki walioshinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2011, lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi (MUCCoBS) na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro 
Wanamuzi bora wa Hip Hop, Jacob Makala 'JCB' (kulia) na Daudi Bakari  wakitumbuiza wakati wa tamasha la wanamuzi walioshinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2011, lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Moshi (MUCCoBS) na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro.

NBC YACHANGIA SH. MILIONI TANO MBIO ZA MWENGE MBEYA

Mshauri wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, Bi. Robi Matiko-Simba (wa pili
kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni tano kwa Mkuu wa
Wilaya ya Mbeya, Bw. Evans Balama ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki
hiyo kwa ajili ya mbio za Mwenge wa Uhuru katika makabidhiano
yaliyofanyika Mbeya hivi karibuni. Wengine pichani kushoto ni Meneja
wa NBC Kanda ya Nyanda za Juu, Bw. Ramadhani Lesso, Meneja wa benki
hiyoTawi la Mbeya, Bw. Salema Kileo (wa pili kulia)  na Bw. Lazaro
Mwankenja, mmoja wa waratibu wa mbio hizo.

BAECELONA WAMALIZA UBISHI


Lionel Messi akishangilia  

LONDON, England
UBISHI wa nani zaidi umefikia tamati yake jana baada ya Barcelona kutwaa ubingwa wa ulaya kwa kuibugiza vibaya Manchester United mabao 3-1 katika pambano kali la fainali lililopigwa akwenye uwanja wa Wembley.
Matokeo hayo, yameendeleza ubabe wa Barca kwa Man United ambapo mwaka 2009, waliwafunga Mashetani Wekundu mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa, Rome nchini Italia.

Katika mchezo wa jana, Barcelona walianza kwa kasi huku wachezaji wake Lionel Messi, Javier Mascherano na David Villa wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Dakika ya kumi, Villa nusura aipatie bao Barcelona, lakini shuti alilopiga liliokolewa na Rio Ferdinand kabla ya kutoka nje.

Nao Man United walijibu shambulizi kupitia kwa Javier Hernandez 'Chicharito', lakini shuti lake lilikuwa butu.

Pedro Rodriguez aliiandikia Barca bao la kuongoza dakika ya 27 baada ya kuwalamba Nemanja Vidic na Ferdinand na kisha kuachia mkwaju uliotinga kimiani.

Man walicharuka na kujipanga kutafuta bao la kusawazisha ambapo Wayne Rooney aliachia kombora kali lililojaa kimiani dakika ya 34 na kufanya hadi mapumziko kuwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, lakini Barca ndio walionekana kutawala zaidi. Muda mwingi, walimiliki mpira asilimia 67 dhidi ya 33 za Man United.

Dakika ya 54, Messi anafanikiwa kufunga bao la pili kwa Barca akipiga shuti la mguu wa kushoto na kumuacha kipa wa Man United, Edwin van der Sar akiduwaa.

Licha ya Man U kuwaingiza Paul Scholes na Nani kuchukua nafasi za Fabio na Michael Carrick, bado walishindwa kuhimili mikikimikiki ya Barca.

Vijana wa Pep Guardiola walijihakikishia ubingwa wa ulaya dakika ya 70 baada ya David Villa kufunga bao la tatu.

Kuingia kwa bao hilo kulichanganya Man United ambao walianza kucheza rafu jambo lililomfanya mwamuzi Victor Kasai wa Hungary kuwaonyesha kadi za njano Antonio Valancia na Michael Carrick kwa mchezo mbaya.

May 27, 2011


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


TAARIFA KWA UMMA

UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TANAPA

Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Alan Kijazi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Bwana Kijazi anachukua nafasi ya Bwana Gerald Bigurube ambaye alistaafu kwa hiari.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Kijazi alikuwa mfanyakazi wa TANAPA kama Mkurugenzi wa Mipango, Miradi ya Maendeleo na Huduma za Utalii.

Bwana Kijazi alisoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika fani ya Uendelezaji wa Maliasili (MSc. Management of Natural Resources). Awali Bwana Kijazi alipata elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alihitimu Shahada ya Mipango ya Mazingira (BA. Environmental Planning).

Kabla ya kujiunga na TANAPA Bw. Kijazi alifanya kazi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, mwaka 1998 hadi 1999. Pia alikuwa Meneja wa  Mradi wa Kuendeleza Uhifadhi wa Wanyamapori (African Wildlife Foundation), mwaka 1999 hadi 2003.

                                      Uteuzi huo unaanza mara moja.

Tarishi M. K.
KATIBU MKUU
25 Mei 2011

MKE WA WAZIRI MKUU WA INDIA AIMWAGIA WAMA SH. MILIONI15

Mama Salma Kikwete akikabidhiwa hundi ya Sh. milioni 15 na MamaKaur


Ziara ya Waziri Mkuu wa India  Dk. Manmohan Sigh imeshusha neema kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) baada ya mkewe, Mama Gursharan Kaur kuipa WAMA msaada wa sh.  milioni 15 kwa ajili shughuli mbalimbali za kuwasaidia watanzania zinazofanywa na taasisi hiyo.

Mama Kauri  ameukabidhi msaada huo leo kwa Mwenyekiti wa  WAMA Mama Salma Kikwete, alipotembelea Ofisi za Taasisi hiyo, mjini Dar es Salaam.


Akikabidhi  hundi ya fedha hizo, Mama Kaur alisema kuwa ameguswa na kazi zinazofanywa na WAMA za kuisaidia jamii ya kitanzania, hivyo msaada huo utasaidia kutekeleza majukumu mbalimbali wanayoyafanya.

Kwa upande wake Mama Kikwete alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo yanayoikabili jamii ya kitanzania.

Alisema kuwa taasisi ya WAMA imekuwa ikipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa maendeleo wa ndani na wa nje ya nchi hivyo aliwaomba wananchi wenye moyo wa kusaidia wasisite kufanya hivyo bila ya kuangalia kama msaada watakaoutoa ni mdogo au mkubwa.

Mama Kikwete alisema kuwa Taasisi ya WAMA imekuwa ikifanya kazi mbalimbali za kuhakikisha kuwa inawasaidia wanawake kuinua maisha yao, kuisaidia jamii ya watanzania kuwa na afya bora, kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa vijana na kada tofauti, kushughulikia uzazi salama  na kuwawezesha watoto wa kike ambao ni yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu.

Mama Kaur ameambatana na mumewe waziri Mkuu wa India Dr. Manmohan Singh aliyeko nchini katika ziara ya kikazi ya siku tatu.

VIJANA CCM ARUSHA WAMSHUKIA LOWASSA

May 25, 2011

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM MKOA WA ARUSHA
Tarehe 25/05/2011

Edward Lowassa

Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuweze kutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi na Jumuiya yetu ya Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha.

Tumewaita hapa kwa malengo makuu Sita:-
Kuunga mkono Halimashauri kuu ya CCM Taifa kwa kuona umuhimu wa kuifanyia kazi kwa vitendo falsafa ya kujivua gamba. Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa watanzania. Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa kifisadi ambao ni Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania. Pia tunasisitiza kuwa Andrew
Chenge aondolewe kwenye kamati ya maadili ya CCM mara moja na wakati huohuo Edward afukuzwe kwenye kwenye ya uwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya umoja wa vijana wa CCM Taifa haraka iwezekanavyo.

Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunamtaka kuwa James Millya ambaye ni kibaraka mkuu wa mafisadi mkoa wa Arusha ajiuzulu mara moja na tunatamka rasmi kumfukuza kwenye UVCCM mkoa wa Arusha ili apate fursa ya kwenda kuwa tumikia mafisadi.

Tunamtaka James Millya aache kufikiria kwa kutumia tumbo na badala yake atumie kichwa.

Pia tumeshaandika barua yenye kumbukumbu namba kumb. Ars/Malalamiko/01 kwenye Chama kuelezea namna alivyo mnafiki, mfitini,mwongo na namna asivyo jali maslahi ya vijana wa UVCCM mkoa wa Arusha.

Vilevile tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa Ally Bananga anaetumiwa na Millya pamoja na mafisadi hana nafasi yoyote ndani ya Umoja wa vijana wa CCM kuanzia kwenye tawi hadi Taifa.

 Kwamantiki hiyo Ally Bananga aache mara moja kuganga njaa kwa kutumia jina la UVCCM. Pia tunampa onyo kali Catherine Magige  aache mara moja kutumia fedha za mafisadi kuwagawa vijana wa Arusha kabla hatujatumia haki yetu ya kikanuni ya kumsimamisha Ubunge. Tunajua kuwa amepata ubunge kwa nguvu za kifisadi kupitia UVCCM.

Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunakiomba chama cha cha mapinduzi kiwafukuze mara moja makatibu wa UVCCM kutoka wilaya za Monduli, Arumeru, Longido na Karatu kwa kushiriki mandalizi ya maandamo haramu na kwa kukataa wito wa chama wa kwenda kutoa ushahidi wa malamiko yao kuhusu mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa. Kitendo hicho cha kukataa wito wa Chama ni dharau na ukosefu wa maadili.

Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunatamka kwamba ili kulinda hadhi ya CCM mkoa wa Arusha tunamtaka Onesmo Nangole ajiuzulu mara moja kwa kuwa anafanya kazi ya Fisadi Edward Lowasa na si ya CCM. Kitendo chake yeye cha kufanya kazi ya mafisadi na si ya CCM kimetupelekea kupoteza majimbo mawili kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.

Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunatamka kwamba Mhe. Mary Chatanda (MB) ambaye ni katibu wa CCM Mkoa wa Arusha ni mpiganaji na ni lulu ya CCM mkoa wa Arusha. Amefanya mengi ya maana na wa-CCM makini, wazalendo na wanaojali maslahi ya chama chetu wanatambua hilo.

Pia tunawaomba CCM Taifa waendelee kumwacha hapa Arusha ili aendelee kukijenga chama na kukomesha mafisadi pamoja na dagaa wao.

Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha
tunatamka rasmi kumtambua Ndugu. Mrisho Gambo kuwa ni mjumbe halali wa baraza kuu la UVCCM Taifa kuwakilisha mkoa wa Arusha.

Tunamuunga mkono kwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana na ufisadi ndani ya chama na Tanzania kwa ujumla. Na huo ndiyo msimamo wetu kwa kuwa una tija kwa vijana wa Tanzania.

 Tunashauri CCM Taifa kuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge) kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa na kisha kuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chamatawala katika nchi hii.
TUTASEMA KWELI DAIMA FITINA KWETU MWIKO
KAULI YETU: KULINDA NA KUJENGA UJAMAA
KITADUMU CHAMA CHA MAPINDUZI BILA MAFISADI
ยช