.

NAPE ATEMBELEA 'NEWSROOM' ZA MWANANCHI NA GLOBAL PUBLISHERS

Jun 30, 2011

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye(kulia) akikumbatiana kwa fraha na Mhariri Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Daniel Msacky,alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Ltd, Tabata, Dar es Salaam, 29/6/2011. Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Sixtus Mapunda.
Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, alipofaya ziara katika ofisi za kampuni hiyo, Tabata Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda na  Kshoto ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Theophil Makunga, Mhariri Mrendaji gazeti la Mwananchi Dennis Msacky, na Mhariri wa Mwanaspoti Frank Sanga.
Waandishi wa habari wakiwa kazini katika chumba cha habari cha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd.
                                       Mhariri wa Habari wa Mwananchi, yahya Charahani akiwa kazini.
Mwandishi wa habari mkongwe wa Lauden Mwambona wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, akifurahi Nape alipoingia chumba cha habari cha magazeti ya kampuni hiyo.
Nape akionyeshwa maandalizi ya gazeti la Mwananchi katika hatua ya mwisho kabla ya kwenda kuchapwa mtamboni. Anayempa maelezo ni Makunga.
Meneja uzalishaji katika mtambo wa  uchapaji magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Sameer Aher akimweleza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye sehemu ya mtambo huo inavyofanya kazi.Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa MCL Theophil Makunga.
===================================================
NDANI YA GLOBAL PUBLISHERS
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Kiu, Ijumaa na Champion, Abdallah Mrisho, baada ya kuwasili Ofisi za kampuni hiyo, Mwenge, Dar es Salaam. leo . Wapili kulia ni Mhariri Kiongozi wa kampuni hiyo    na Mhariri Kiongozi Oscar  Ndauka na Mwandishi wa kampuni hiyo Luqman Maloto na wapili kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.
Nape akiwa katika ofisi za Global Publishers. Kushoto ni  Abdallah Mrisho Wengine kutoka kulia ni, Sixtus Mapunda, Maloto,Ndauka na Mhariri kiongozi wa michezo wa Global Saleh Ally
Nape akizungumza na wafanyakazi wa Global Publishers katika chumba cha habari cha Global. Wengine ni Mrisho, Ndauka, Sixtus na Ally.
Waandishi wa habari wa kampuni ya Global Publishers wakiwa kazini wakati wa ziara hiyo ya Nape.
Kunfi la kwanza la wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja na Nape baada ya kuzungumza nao leo 
Kundi la pili la wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha nya pamoja na Nape

NAPE, ASHA 'MSHUA' WAMALIZA ZIARA MTWARA KWA KISHINDO, 154 WA CUF WATIMKIA CCM WAKATI WA MKUTANO MTWARA MJINI

Jun 28, 2011

Wazee wa kijiji cha Mpapura, Mtwara Vijijini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye katika kijiji hicho 28/6/2011 
Wanachama wa CCM wakishiriki kula kiapo katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika kijiji cha Mpapura, Mtwara Vijini mkutano huo ulihutubiwa na Nape. 
Mjumbe wa NEC, Oganaizesheni, CCM, Asha Abdallah Juma akimsaliia mtoto Hadija Juma,  wakati wa mkutano huo katika kijiji cha Mpapura. Asha pia alihutubia mkutano huo. 
Nape na Asha Abdallah Juma, wakitoka katika Ofisi ya Mbunge wa Lindi mjini 
Mamia ya wananchi wakishangilia katika mkutano wa hadhara aliohutubia Nape mjini Mtwara, 28/6/2011 
Nape akizungumza na mbunge wa Mtwara mjini, Hasnain Mohammed Murji wakati wa mkutano huo
Nape akipokea kadi ya CUF kutoka kwa mwanachana wa chama hicho, aliyeamua kuhamia CCM wakati wa mkutano huo wa Mtwara mjini. Kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma, akishuhdia. Jumla ya wanachama 154 wa CUF walihamia CCM wakati wa mkutano huo.

NAPE AMALIZA ZIARA LINDI SASA YUPO MTWARA

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimjulia hali Somoye Ismaili (70) aliyekuwa akisubiri matibabu kwenye chumba maalum cha kuhudumia wazee, katika hospitali ya Wilaya ya Lindi mjini, juzi. Nape alitembelea hospitali hiyo, mwishoni kwa ziara yake ya siku mbili mkoani Lindi. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah juma. 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa (kushoto) akiuaga msafara wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati msafara huo ulipokuwa tayari kuingia mkoani Mtwara kuendelea na ziara yake Juni 27, 2011. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara, Alhaji Dadi Mbulu. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara walipoupokea msafara wake akiwa njiani kwenda Mjini Liwale. Juni 27, 2011 
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma akizungumza na wananchi wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara walipoupokea msafara wake na Nape, wakiwa njiani kwenda Mjini Liwale. Juni 27, 2011 
Wasanii wa kikundi cha hamasa cha Newala mkoani Mtwara wakitumbuiza baada ya kupokea msafara wa Katibu Nape ulipokuwa njiani kwenda Mjini Liwale. Juni 27, 2011 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki kucheza ngoma ya kikundi cha uhamasihaji cha vijana wa Newala, baada ya msafara wake kuwasili mjini Newala, Juni 27, 2011 
Katibu wa Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma (kushoto) akishiriki kucheza ngoma ya kikundi cha uhamasihaji cha vijana wa Newala, baada ya msafara wake na Nape kuwasili mjini Newala, Juni 27, 2011
Nape akisalimia wazee wa Newala alipokwenda kufanya mkutano wa ndani na  viongozi wa mashina na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM kwenye ukumbi wa Chama Cha Akiba na Mikopo (SACCOS) mjini Newala mkoani Mtwara. Juni 27.
Viongozi wa mashina na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wao wa ndani na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwenye ukumbi wa Chama Cha Akiba na Mikopo (SACCOS) mjini Newala mkoani Mtwara. Juni 27. 
Nape akicharaza ngoma baada ya kuwasili katika Tandahimba mkoani Mtwara kwa ajili ya mkutano wa hadhara, Juni 27. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa CUF, Rukia Panyota, aliyeamua kurejea CCM wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara. Juni27. 
Mashabiki wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara, Juni 27.

NAPE ALIVYOTIKISA LINDI MJINI

Jun 27, 2011

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi kabrasha la kuorodhesha wanachama, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mtanda, wilaya ya Lindi Mjini, Issa Malocho,alipofanya mkutano wa wajumbe wa mashina, leo katika ukumbi wa oceanic View, mjini Lindi. Jumla ya Kata 18 zilipewa fomu hizo kwa ajili ya kuorodhesha wanachama wa CCM katika maeneo yao. 
Wajumbe wa mashina kutoka kata 18 za Wilaya ya Lindi mjini, wakiwa katika mkutano wao na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  kwenye ukumbi wa Ocenic View mjini Lindi. 
Nape akisakata muziki na vijana wa kikundi cha sanaa cha mjini Lindi katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika leo, kwenye uwanja wa Fisi mjini Lindi. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia umati wa watu katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Uwanja wa Fisi mjini Lindi leo. 
Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma akihutubia umati wa watu katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Uwanja wa Fisi mjini Lindi leo. 
Nape akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye mkutano huo kwenye uwanja wa fisi 
Mmoja kati ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Fisi mjini Lindi akifurahia hotuba. 
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Fisi mjini Lindi leo. 
Nape na Asha Abdaallah Juma wakiaga wananchi baada ya mkutano huo

ZIARA YA NAPE NA ASHA ABDALLAH JUMA, LINDI

Jun 26, 2011

Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF) Selemani Bungara maarufu kwa jina la Bwege, (kulia) akishangilia wakati Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape  Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara, Kilwa Masoko mkoani  Lindi
Katibu wa NEC, Oganaizesheni,  Asha Abdallah Juma, akimnyamanzisha Asha Likalangala, alileangua kilio baada ya kuingiwa na maneno, Nape alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, Kilwa Masoko mko Itikadi. 
Nape akipokea kadi ya aliyekuwa katibu wa CUF kata ya Njinjo, Kilwa Mohamed Likalangala katika mkuttano wa  Kilwa Masoko  .
Nape akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mkapa Garden, Kilwa Masoko, Lindi 
Nape akishauriana jambo na Asha Abdallah Juma baada ya kupokewa na viongozi wa mkoa wa Lindi 
Nape akiwa amezungukwa na umati wa wananchi baada ya kuhutubia mkutano kwenye uwanja wa Mkapa Garden, Kilwa Masoko 
Nape na Asha Abdallah Juma wakisindikizwa na wananchi baada ya mkutano wa Kilwa Masoko 
Nape akishauriana jambo na Mzee Mtopa, Katibu wa CCM mkoa wa Lindi  
Nape akisakata muziki na vijana wasanii wa muziki wa kizazi kipya, kwenye mkutano wa Kilwa Masoko
ยช