.

RAIS KIKWETE KUFUNGUA MAONYESHO YA NANE NANE KESHO

Jul 31, 2011

Rais Kikwete
 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kesho, Agosti Mosi, 2011, atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Wiki ya Sherehe za Nane Nane na Maonyesho ya Kilimo mwaka huu kwenye Uwanja wa Maonyesho ya Kilimo wa Nzuguni, Dodoma.
Shughuli kuu za Mheshimiwa Rais katika ufunguzi huo itakuwa ni kufungua Maonyesho ya Kilimo ya Nane Nane kwa hotuba rasmi na baadaye kutembelea baadhi ya mabanda ya maonyesho hayo.
Hotuba hiyo ya kesho itakuwa badala ya Hotuba ya Mwisho wa Mwezi wa Julai ambayo ilikuwa itolewe jioni ya leo, Jumapili, Julai 31, 2011 lakini haitatolewa kwa sababu ujumbe na maudhi yake yatakuwemo katika hotuba ya kesho.
Mheshimiwa Rais tayari yuko mjini Dodoma tangu jana, Jumamosi, Julai 30, 2011 kwa vikao vya Chama cha Mapinduzi ambacho yeye ni Mwenyekiti wake wa taifa.
Mara baada ya kuwasili jana, Rais Kikwete aliendesha Kikao cha Kamati ya Maadili na leo amekuwa anaendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho.

RISALA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANDk. Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein, akisoma risala ya maalum ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuwatakia wananchi kheri kati mfungo huo kwa salama na amani, pia kuwataka wajitahidi katika kufanya ibada kwa wingi na kuzidisha imani katika jamii. Mwezi wa Ramadhani unatarajiwa kuandama leo, (Picha na Ramadhan Othman wa Ofisi ya Rais, Ikulu Zanzibar)

KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA DOM

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais, Dk Jakaya  Kikwete, akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM a leo katika ukumbi wa Makao Makuu ya Chama  Mjinji  Dodoma 
Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM ( Zanzibar), Vuai Ali Vuai, kabla ya kuanza  kikao  hicho.  
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, akisoma utaratibu wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM  kilichofanyika leo, katika ukumbi wa CCM Makao Makuu Dodoma, (wa pili kulia) Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Rais  Kikwete, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Amaan Abeid Karume, Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa  Kamatiu Kuu ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, wakisikiliza kwa makini,taarifa zilizotolewa katika kikao hicho.(Picha na Ramadhan Othman Dodoma )

VODACOM YATUMIA 'SUPERMAN' KUNADI HUDUMA YA M-PESA

KAMPUNI ya Mawasiliano  ya Vodacom Tanzania imeipatia huduma yake M-PESA muonekano mpya kuendana na kaulimbiu ya 'kazi ni kwako' ambapo kuanzia sasa 'Super Man' ambae ni kielelezo maarufu duniani cha ujasiri, uhodari, kasi na  usalama kitatumika kuitangaza sokoni huduma hiyo. Pichani, Ofisa Mkuu, Masoko na Mahusiano wa Vodacom, Mwamvita Makamba akizungumza katika uzinduzi wa muonekano huo,leo katika hoteli ya  Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Fedha, Jacques Voogt na Mwamvita Makamba wakishikana na 'midori' ya Superman' wakati wa uzinduzi huo 
Baadhi ya waalikwa katika hafla hiyo wakiwa wamevaa vinyango vya 'Superman'

JK AKUTANA NA MSHAURI WA KATIBU MKUU WA UN, PROF SACHS

Jul 30, 2011

Rais Dr.Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu, Prof. Jeffrey Sachs mshauri maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

VODACOM FAMILY DAY HII

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwashangilia watoto  walioshiriki katika michezo mbalimbali  siku ya “ Vodacom family day”inayofanyika katika Hotel ya Kunduchi Beach  jijini  Dares Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwashangilia watoto  walioshiriki katika michezo mbalimbali  siku ya “ Vodacom family day”inayofanyika katika Hotel ya Kunduchi Beach  jijini  Dares Salaam.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Imani Dominick wa kitengo kinachojihusisha na majengo na minara akimtoka mfanyakazi mwenzake katika mchezo wa beach soccer  siku ya Vodacom Family day inayofanyika Hotel ya Kunduchi Beach  jijini  Dares Salaam.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakichuana vikali kwenye mchezo wa Beach Soccer wakati wa siku ya Vodacom Family day inayofanyika katika Hotel ya Kunduchi Beach  jijini  Dares Salaam. 
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakichuana vikali katika mchezo wa Beach Volleyball  siku ya  Vodacom family day inayofanyika katika Hotel ya Kunduchi Beach  jijini  Dares Salaam. (Picha kwa hisani ya Vodacom)

AJALI YA BASI MOSHI: RAIS KIWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

Jul 29, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
            Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani), amemtumia salamu za rambirambi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Meja Jenerali (Mst.) Saidi Saidi Kalembo kuomboleza vifo vya watu 10 vilivyotokana na ajali mbaya ya barabarani iliyotokea usiku wa tarehe 28 Julai, 2011 katika Barabara ya Moshi – Arusha maeneo ya Kibosho Road mkoani humo.
            Ajali hiyo ilihusisha magari manne. Katika ajali hiyo, gari aina ya Mitsubishi Fuso la Kampuni ya LIM Safari lililokuwa katika mwendo kasi likiwa limebeba wafanyakazi wa shamba la Kahawa la Kilimanjaro Plantation Limited, lilipoteza mwelekeo na kuligonga gari aina ya Toyota Land Cruiser Prado. 
Baada ya kuigonga Prado, gari hilo lilirudi tena barabarani na kuparuzana na basi la Scania la Kampuni ya Fresh Coach na baada ya kulipita basi hilo, ndipo Fuso hiyo ilipogongana ana kwa ana na lori jingine aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa limebeba shehena ya nyanya.  Lori hilo lilipinduka na kuliangukia basi na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo, akiwamo dereva wa gari lililosababisha ajali ambaye amefia hospitali. Watu wengine 24 kujeruhiwa katika ajali hiyo.
            “Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za vifo vya watu 10 vilivyosababishwa na ajali mbaya ya barabarani”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake hizo na kuongeza, “kwa mara nyingine ajali hii imeleta simanzi na huzuni kubwa isiyokuwa ya lazima kabisa kwa familia za wafiwa ambao ghafla wamejikuta wakipoteza ndugu zao.”
            Rais Kikwete amemuomba Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro kumfikishia salamu zake za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wote waliopotelewa na wapendwa wao katika ajali hiyo.
            Aidha amewaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi chote cha maombolezo huku akiwahakikishia kwamba yeye binafsi yuko pamoja nao katika msiba huo mkubwa.  Kwa upande wa watu 24 waliojeruhiwa, Rais Kikwete anawaombea kwa Mola wapone haraka, ili waungane tena na familia, ndugu, jamaa na marafiki zao na hivyo kuweza kuendelea na shughuli zao za kawaida za maisha yao.    
             Rais Kikwete amesema ni jambo la kusikitisha sana kuwa katika siku za hivi karibuni Taifa limeshuhudia kuongezeka kwa matukio ya ajali za barabarani, ambapo nyingi ya ajali hizo kama hii iliyotokea mkoani Kilimanjaro, zinasababishwa na uzembe wa madereva.  
Amezitaka mamlaka zote zinazohusika na utekelezaji wa Sheria ya Usalama Barabarani kutathmini upya utendaji wao wa kazi kwa lengo la kuongeza jitihada za kuisimamia kikamilifu Sheria hiyo, na kuimarisha mbinu za kukabiliana na ajali zinazotokea, ili wananchi wawe na uhakika na usalama wa maisha yao na mali zao wakati wote wanaposafiri.
            Rais Kikwete amemaliza rambirambi zake kwa kusisitiza: “Naelewa fika machungu ya watu wote waliopoteza wapendwa wao katika ajali hii. Naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aziweke mahali pema peponi roho za marehemu wote. Amina.”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

29 Julai, 2011

AJALI YA BASI MOSHI, CCM YATOA POLE KWA MAJERUHI


Katibu wa CCC mkoa wa Kilimanjaro,Steven
Kazidi (kulia), akipatamaelezo kutoka kwa muuguzi mkuu wa
Hospital ya Rufaa ya KCMC, Redempta Mamseri 
 kuhusu maendeleo  ya majeruhi waliolazwa katika hosiptal hiyo
 kufuatia ajali ya basi la LimSafari iliyotokea juzi joni nje
kidogo ya manispaa ya Moshi.
 CHAMA  cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Kilimanjaro,kimetoa pole kwa majeruhi wa ajali
ya  Basi iliyotokea juzi jioni katika bara bara ya kibosho road nje kidogo ya
Manispaa ya Moshi.

Katika ajali hiyo iliyohusisha basi la Lim Safari lenye namba za usajili T489BJR
na roli la mizigo aina ya Bitisubishi Fuso lenye namba za usajili T884BFJ
likiendeshwa na dereva wake Sifael Kaaya,watu 11 walifariki papo hapo wakiwamo
madereva wote wa magari hayo mawili.

Wote waliofariki ukiondoa madereva hao,ni vibarua waliokuwa  wakirejea makwao
huko machame wilaya ya Hai wakitoka kuvuna kahawa katika shamba la kahawa la
Kilimanjaro Plantretion Ltd ambalo lipo eneo la Kibosho wilaya ya Moshi
Vijijini.

Mashuda wa ajli hiyo walisema dereva wa basi hilo,alikuwa amelewa na hakuweza
kusikia kilio cha abiria wake waliomtaka apunguze mwendo.

Akitoa pole jana katika Hosiptal ya rufaa ya KCMC baada ya kutembelea majeruhi
wa ajli hiyo,katibu wa CCm mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi,alisema ajali hiyo
inatoa funzo kwa mamlaka husika kuwajibika katika kusimamia sheria za usalama
barabarani.

Katibu huyo alisema kuwa,aajli nyingi zinatokea kutokana na uzembe wa madereva
na kutaka jitihada zifanywe na vyombo husika kutoa adhabu kali kwa madereva
wanaosababisha ajali.

Alisema Chama cha Mapindizi CCM kimeguswa na ajali hiyo na katika kuonesha kwa
vitendo,CCM ilitoa msaada wa sh,600,000 na kati ya hizo sh,300,000 zilitolewa na
Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Manispaa ya moshi .

Msaada huo aliutoa kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya uuguzi katika Hospital
hiyo ya KCMC Redempta Mamseri aliyepokea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospital
hiyo,Moshi Ntabae.

Kazidi ambaye alitembelea Idara ya upasuaji katika hospital hiyo na kuzungumza
na baadhi ya majeruhi ,alifuatana na katibu wake msaidizi,Habas Mwijuki, Kamanda
ya UVCCM Manispaa ya Moshi Agrrey Marealle  na Katibu wa CCM Manispaa ya
Moshi,Amos Shimba.

Kwa upande wake kamanda wa UVCCM Manispaa ya Moshi,Agrrey Marealle ,alitioa wito
kwa serikali kuona umhimu wa ajali za barabarani kuongezwa katika orodha ya
majanga ya kitaifa   pamoja na kuweka sheria kali za kudhibiti uzembe kwa
madereva.

Aidha Marealle alishauri serikali kuboresha elimu ya madereva kwa kutoa elimu
kila mara juu ya sheria za usalama barabarani,kudhibiti mianya ya rushwa ikiwamo
biashara ya leseni bandia na pia kuwa na utaratibu wa madereva kurudia majaribia
ya udereva(driving test) mara kwa mara .

alishauri pia kuweka mkazo katika kuwadhibiti madereva wanaoendesha vyombo vya
moto huku wakiwa wamelewa,kupunguza safari za usiku pamoja na kutoa muda wa
kupumzika kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo bila hivyo taifa
litaendelea kupoteza nguvu kazi hasa vijana.

"Bila hivyo tutaendelea kupoteza watu hususani vijana ambao ndiyo raslimali kuu
ya nchi,kampeni hii inahitaji ushirikiano kati ya polisi na serikali,vyama vya
siasa,vyombo vya habari,madhehebu ya dini na jamii kwa ujumla"alisema Marealle.

katibu wa ccm mkoa wa kilimanjaro,Steven Kazidi,akimpa pole Bi.Esimend Parimina
ambaye amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya KCMC baada ya kujeruhiwa jicho lake
la kulia katika ajali ya basi la Lim Safari iliyotokea juzi jioni eneo la
kibosho road nje  kidogo ya Manispa ya Moshi,watu 11 walipoteza maisha yao na
wengine 26 kujeruhiwa vibaya. 
Katibu wa CCC mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi(mwenye suti kulia)akipata
maelezo kutoka kwa muuguzi mkuu wa Hospital ya Rufaa ya KCMC,Redempta
Mamseri(kushoto  aliyevaa gauni la kijani) kuhusu maendeleo  ya majeruhi
waliolazwa katika hosiptal hiyo kufuatia ajali ya basi la LimSafari iliyotokea
juzi joni nje kidogo ya manispaa ya moshi.

MAHAFALI YA TATU YA DARASA LA SABA SHULE YA AWALI NA CHEKECHEA YA SUNRISE

Waziri wa zamani wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta akiwa na wahitimu wa darasa la saba wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika katika shule hiyo katika, Kinondoni Morocco, Dar es Salaam. Kulia (nyuma) ni Mkurugenzi wa shule hiyo Mary Mushi. 
WAZIRI wa zamani wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta akiinama kuona vizuri kazi za mikono za wanafunzi wa shule ya Chekechea na Msingi Sunrise, alipohudhuria mahafali ya tatu ya darasa la saba ya shule hiyo, Kinondoni mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa shule hiyo Mary Mushi.  
WAZIRI wa zamani wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta  (kushoto) na Mkurugenzi wa shule ya chekechea na msingi ya Sunrise, Kinondoni Dar es Salaam, Mary Mushi, wakiwasili kwenye sherehe za mahafali ya tatu ya darasa la saba ya shule hiyo. Kulia ni wahitimu hao. 
Wanafunzi wa shule hiyo ambao ni Skauti wakifanya gwaride maalum wakati wa mahafali hayo. 
Wanafunzi wakipata burudani ya midori maalum  
Mdau wa shule hiyo, Furaha Luhende akiwa na Mama Sitta. 
Mama Sitta akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mahafali hayo

CCM DAR YALAANI WABUNGE KUDHARAU BUNGE

NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, kimelaani vitendo vya baadhi ya wabunge wa CHADEMA kuendeleza tabia ya kulikosea heshima bunge.
      Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa CCM wa mkoa huo, Kilumbe Ng'enda alisema, pamoja na vitendo vya wabunge hao kuaibisha taifa, lakini wanawaaibisha zaidi vyama vyao na wananchi waliowachagua.
       Kauli hiyo ya kulaani imetolewa na CCM mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni siku mbili baada ya baadhi ya wabunge wa CHADEMA wakiwemo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje, Tundu Lissu (Singida Mashariki),Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa kufukuzwa katika ukumbi wa Bunge na Naibu Spika Job Ndugai kwa kulikosea heshima bunge,juzi.
       "Hali ya vurugu, utovu wa nidhamu, jazba na ubabe vinavyojitokeza kwa baadhi ya wabunge katika kikao kinachoendelea mjini Dodoma, haionyeshi kuwa dhana ya kuwapata wabunge wenye sifa imezingatiwa. Hawa wanaofanya vitendo hivi bungeni wanatutia aibu wanasiasa wote ukiacha tofauti zetu za kiitikadi", alisema N'genda.
        Alisema, baada ya ushindani katika uchaguzi mkuu wa 2010,kuzaa wabunge 166 wa majimbo kutoka CCM, CUF (24), CHADEMA (23) NCCR-MAGEUZI (wanne) na TLP na UDP mbunge mmoja kila chama, ilitarajiwa kila chama kimetoa mchango wa wabunge wenye sifa za uongozi na Utumishi wa umma wenye hekima,busara na malezi ya Kitanzania yanayojali utu na heshima kwa wengine,kuheshimu mawazo ya wengine na utii katika sheria na taratibu, lakini kinachoonekana sasa kwa upande wa CHADEMA.
        "Ni imani yangu kuwa katika dunia watu wanatambulika katika makundi yao ya kazi, ukiacha namna nyingine ya kumtambua mtu mmoja mmoja, hivyo sisi kama wana siasa, wanasiasa wenzetu hawa wanatutia aibu! Lakini zaidi wanakitia aibu chama chao, na wananchi wa majimbo yao", alisema Ng'enda.
         Ng'enda alisema, hatua hiyo ya wabunge kukosa nidhamu ya kutofuata taratibu walizojiwekea ni kielelezo cha wazi kuwa vyama vyao havikuwachuja vizuri na wananchi hawakupata walichokusudia.
        Alisema, hapa shaka kuwa CCM na serikali yake inayo madhaifu yake kwa kuwa haiwezi kuyakosa ikiwa inaongozwa na binadamu ambao si malaika, lakini kutokana na yanayojitokeza bungeni ni dhahiri wengi wa viongozi wa CHADEMA na wabunge wao wana mapungufu yaliyopita kiwango cha ubinadamu wa kawaida.
        "Kwa kutazama Mawaziri wa serikali na wale Mawaziri Kivuli wa kambi ya upinzani, utakapota kuunda serikali yako unayotaka uwe makini, ukiletewa Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha na Waziri Kivuli wa wizara hiyo kambi ya upinzani Godbless Lema,unaweza kumfanya Lema awe waziri na mambo yakawa shwari kwa anavyoonekana kuweka mbele jazba, kiherehere na ubabe?" alihoji Ng'enda.
       Ng'enda alisema wanachofanya baadhi ya wabunge wa CHADEMA kuendekeza jazba, kiherehere na ubabe ni kusaka sifa na umaarufu ili waonekane bora, bila kukumbuka kwamba tabia hiyo ya kusatafuta heshima kwa nguvu itawapatia dharau kwa urahisi zaidi.
      Aliwapongeza wabunge wa CCM na viongozi wote wa Bunge, Spika, Naibu Spika na Wenyeviti kwamba wanajitahidi kutekeleza amajukumu yao bila woga na kumtaka Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akidhi hadhi yake ya kuwa kiongozi wa wapinzani kulaazni vitendo vya wabunge kukosa nidhamu.
      "Namkubusha mhe. Mbowe awe kweli kiongozi wa wapinzani na kuongoza maana yake kuonyesha njia, lazima alaani vitendo vya wabunge kukosa nidhamu", alisema Ng'enda.

BREEKING NYUUUUUUUUZZZZZ

Jul 28, 2011

MAHAKAMA YAMWACHA HURU MSHITAKIWA KESI YA RICHMOND


Gire akitoka
makamani leo
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.

Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hata kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali  kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.

"....Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa  kuridhisha kumuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu...kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu  Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema.

MAREALLE AONYA JUU YA MAKUNDI CCM MOSHI


Kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi mjini  Aggrey Marealle
akihutubia  katika uzinduzi wa baraza kuu  la CM  Manispaa ya
Moshi  kuzindua rasmi baraza hilo mjini Moshi. Kulia ni Katibu
wa  CCM wilaya ya Moshi mjini  Amosi Shimba na kushoto ni
Mwenyekiti  wa Makamanda wa Vijana Moshi Mjini
Alhaji Omari Shamba.

MFUMO rika , makundi ndani ya chama  na baadhi ya viongozi kushindwa kusimamia serikali kwa kutatua kero za wananchi ni miongoni mwa sababu kuu zilizochangia  Chama cha Mapinduzi (CCM) kushindwa  nafasi ya ubunge katika jimbo la Moshi Mjini katika  uchaguzi mkuu uliopita.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Vijana wa moshi mjini  kupitia CCM Aggrey Marealle katika hafla ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa baraza la vijana wa jimbo hilo uliofanyika katika chuo cha maendeleo ya wananchi Msinga kilichopo kata ya Kibosho wilayani Moshi vijijini.

Marealle alisema pamoja na chama chao kufanya kampeni na maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanakomboa jimbo la moshi bado jimbo hilo lilibaki mikononi mwa wapinzani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mfumo rika ambao vijana wengi walipigia kura chama cha CHADEMA wakiamini watapata maisha bora zaidi.

Alisema sababu nyingine ni baadhi ya viongozi kushindwa kuwajibika katika nafasi zao na hivyo wananchi kuona serikali haiwajali na kuamua kupiga kura kwa chama kingine wakiamini watapata maendeleo bora zaidi.

Kwa mujibu wa kamanda huyo wa vijana rushwa ndani ya chama na nje ya chama ni sababu nyingine iliyochangia chama hicho kushindwa kwani baadhi ya wananchama walikua CCM mchana na usiku kuwa chama cha upinzani huku wakitoa siri za chama ili wapewe kitu kidogo.

Mbali na rushwa pia tatizo la utoaji kadi kiholela kwa kuamini wote
wanaochukua kadi ni wananchama ilikigarimu kwa watu wasiofaa kupiga ura wakati wa kura za maoni na hivyo kusababisha makundi ndani ya chama hususan kipindi cha uchaguzi mkuu.

Alisema uratibu wa kura za maoni katika jimbo la moshi mjini uligawa chama kwa kiasi kikubwa na kuwafanya wagombea wengine kuwa upande wa pili licha ya wao kuonyesha kuwa chuki za kura zimeisha.

Kutokana na hali hiyo Marealle alishauri uongozi wa chama hicho ngazi za juu kuona umuhimu wa kuacha nafasi kati ya muda wa kura za maoni na uchaguzi ili wale watakaoshindwa kwenye kura za maoni wawe wamevunja makundi kukinusuru chama.

Katika hatua nyingine Marealle aliwataka vijana wa chama hicho kufuata kanuni na taratibu za chama na kuhakikisha wanatangaza chama hicho kwa vijana wenzao ili nao waweze kujiunga na kuinua upya chama hicho.

Alisema chama hicho kina ugonjwa wa woga,kwa kila mmoja kuogopa kumkemea mwenzake hata kama atamwona akikisaliti chama jambo ambalo limeendelea kukitafuna chama kama mchwa ambapo aliwataka vijana kuhakikisha wanakua mstari wa mbele kupinga tabia hiyo.
 

CHE MUNDUGWAO KUIBUKA UPYA

Jul 27, 2011

Baada ya ukimya wa takribani mwaka mmoja bila kuonekana jukwaani nchi Tanzania, mwanamuziki mahiri wa muziki wenye viongo vya kiasili ya Tanzania Che Mundugwao na bendi yake ya Chemundu & Mbega Arts ataanza kufanya vitu vyeke tena.

Kwa kuanzia, leo Che Mundugwao atapanda jukwaani na bendi hiyo katika Tamasha la Yakale Yanapokutana na Sasa linaloendelea katika ukumbi wa Kijiji Cha Makumbusho, Dar es Salaam. ambapo bendi ya Che Mundugwao ni mmoja wa washiri wa tamasha hilo.

ZIARA YA RAIS KIKWETE MTWARA

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwika ndoo ya maji bi.Zainab Yusuf Lidandi wakati Rais alipokagua na kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nyundo wilaya ya Mtwara vijijini jana jioni.Rais Kikwete yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kukaguana kuzindua shughuli mbalimbali za maendeleo.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyundo Mtwara vijijini jana jioni muda mfupi baada ya kukagua na kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.Mradi huo unafadhiliwa na shirika la AMREF.
Mtafiti wa zao la Korosho katika kituo cha utafiti wa Mazao na mafunzo cha Naliendele Mtwara, Dr.Peter Masawe akimpa maelezo Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais kikwete alipokitembelea kituo hicho jana mchana kukagua maendeleo ya tafiti za mazao mbalimbali.Baadaye Rais kikwete alikutana na uongozi wa kituo hicho na kujadili namna ya kuboresha shughuli za kituo hicho muhimu.
Mtafiti wa Muhogo na jamii ya viazi Dr.Geofrey Mkamilo(kulia) akimwonesha Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muhogo ulozalishwa kwa kutumia mbegu bora ya Naliendele wakati Rais alipotembelea kituo cha Mafunzo na utafiti wa mazao huko Naliendele,mkoani Mtwara jana mchana. 4---7048—Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyundo Mtwara vijijini jana jioni muda mfupi baada ya kukagua na kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.Mradi huo unafadhiliwa na shirika la AMREF (PICHA ZOTE NA FREDDY MARO)

JK AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA KIKRISTO

Jul 22, 2011

 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu ya Kikristo Tanzania baada ya kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee mjini Dar tarehe 22.7.2011.

KATIBU WA NEC OGANAIZESHENI ASHA ABDALLAH JUMA AJULIA HALI MAJERUHI WA BASI LA HOOD NA KUKAGUA UHAI WA CHAMA MOROGORO

Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma akimpa pole Beatrice Mjenga ambaye ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya basi Mikumi, Morogoro 
Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma, akisalimia viongozi na wanachama wa CCM mkoa wa Morogoro kabla ya kuwahtubia katika ukumbi wa Vijana kwa ajili ya kuimarisha uhai wa Chama 
Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akihutubia viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro mjini Fikiri Juma.

LILIAN TIMBUKA KATIBU MPYA SHINA LA CCM UPL

Msanifu wa kurasa wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd,
Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani,
Lilian Timbuka  amechaguliwa kuwa Katibu  wa CCM 
 shina la kampuni hiyo katika uchaguzi uliofanyika asubuhi
hii katika mkutano wa Chama. Nafasi hiyo ilibaki wazi
kutokana na  aliyekuwa akishika nafasi hiyo kuondoka.
Mwenyekiti wa sasa ni Yassin Kayobo.

NGASA NA FABIO DA SILVA

Kwa habari zaidi za mechi hiyo soma Uhuru
 la leo au peruzi  www.uhurupublications.com

SHARAMA: NIMEKUJA TZ KUWASHIKA

Ramadhani Chambo
Msanii mkali wa hip hop kutoka nchini Kenya Ramadhani Chambo anaejulikana kwa jina la Sharama amesema ameamua kuja kufanya uzinduzi wa albamu yake ya vunja winga hapa Tanzania kutokana na kuona ana mashabiki wengi hapa nchini halaf u hawajapata kile wanachostahili kutoka kwake
Akizungumza na mwandishi wetu Sharama alikuwa na haya ya kusema “unajua nilikaa na kuona kuwa watanzania ni miongoni mwa mashabiki wangu na ninawapenda sana ndio maana nimeamua kiuja kuwapa kile wanachokihitaji kutoka kwangu”
Sharama ambae kwa sasa yupo hapa bongo akiwa na baadhi ya wasanii wenzake kutoka katika lile kundi la Ukoo Flani Maumau wote kwa pamoja wakiwa wamepiga kambi pale katika studio za Mzuka Record wakipata madini tofauti kutoka kwa mtu mzima Benjamini wa mambojambo
Aliendelea sharama kwa kuwaomba mashabiki wake wote kuhudhuria kwa wingi pale Diamond jubilee siku ya tarehe 23/07 ambapo ndipo atakuwa akizindua albamu yake ya VUNJA WINGA. “mimi ninachowaomba mashabiki wangu wa Tanzania ni kuibuka kwa wingi pale Diamond ili kuona nimewaandalia nini kama zawadi yao maana nina imani kuwa kuna kitu kikubwa mashabiki wangu wanakihitaji kutoka kwangu hivyo na mimi nitawapa siku hiyo”
Sharama pia ameishukuru taasisi isiyo ya kiserikali ya Art In Tanzania kwa kuwezesha mpango mzima wa uzinduzi wake.
Katika uzinduzi huu pia kutakuwa na uzinduzi wa albamu ya HAIELEWEKI yak wake Totoo ze bingwa ambao nao kwa kiasi kikubwa umewezeshwa na kuletwa kwenu na Art In Tanzania
Katika shoo hii watu wazima hawa watasindikizwa na kundi zima la ukoo flani maumau, Abasi kutoka nchini Kenya na kutoka tanzanina watakuwepo 20%, Benjamini wa mambojambo, Zolla D, Sana asana Band na bendi ya Akudo Impact.

BREEKING NYUUUUUUUUZZZZZ

Jul 21, 2011

SAKATA LA BARUA: JAIRO ASIMAMISHWA KAZI


Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo
akizungumza na waandishi wa habari leo
mjini Dodoma.

Taarifa zilizopatikana kutoka mjini Dodoma zimesema, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo amesimamishwa kazi kuanzia leo. Hatua hiyo imetangazwa leo mjini Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi  Philemon Luhanjo katika mkutano na Waandishi wa habari. Jairo aliingia matatani baada ya kudaiwa kuandika barua ya kuchangisha sh. milioni 50 kila taasisi zilizopo chini ya wizara ya Nishati  na Madini.

MATUKIO ZIARA YA RAIS KIKWETE AFRIKA KUSINI

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Zuma kwa heshima yake wakati wa kilele cha Ziara Rasmi ya siku mbili . 
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya mshujaa waliopigania uhuru wa Afrika ya Kusini nje kidogo ya jiji la Pretoria jana. Wapili kushoto ni Mama Salma Kikwete na watatu kulia ni mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini.Rais Kikwete yupo nchini Afrika ya Kusini kwa Ziara rasmi ya Kitaifa ya Siku mbili.  
Waziri wa Habari,Utamaduni na michezo Dr.Emmanuel Nchimbi na Mwenyeji wake Waziri wa Utamaduni wa Afrika ya Kusini Paul Mashatile wakisaini mkataba wa kuanzishwa rasmi ushirikiano katika Nyanja ya utamaduni kati ya Afrika ya kusini na Tanzania jana jijini Pretoria huku Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Afrika ya kusini Jackob Zuma wakishuhudia.

MWILI WA NAIBU MKURUGENZI WA MAELEZO WAAGWA DAR, KUZIKWA KESHO MTO WA MBU ARUSHA

Mwili wa Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Sozzy Mahmoud aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana umesafirishwa leo kwenda Mto wa Mbu Arusha kwa ajili ya Mazishi. Msafara wa kuuplele Mto wa Mbu mwili wa Sozzy ambaye alikuwa mke wa Mkurugenzi wa Uhuru FM,
Mikidadi Mahmoud ulianzia nyumbani kwao, Karakata, Kipawa Dar es Salaam.
Waombolezaji wakishusha jeneza kutoka kwenye gari. 
Marehemu Sozzy 
Waombolezaji wakiangua vilio baada ya mwili wa marehemu Sozzy kufikishwa nyumbani. 
Waandishi wa habari waandamizi waliokuwa karibu na Sozzy wakiwa katika majonzi mazito wakati wa kuagwa mwili wa marehemu. 
Baadhi ya waombolezaji wakisoma kisomo maalum 
Mhariri Mtendaji wa Uhuru Publications Ltd, Josiah Mufungo na maofisa wa kampuni hiyo wakiwa kwenye msiba. 
Waombolezaji kadhaa wa kadhaa wakiwepo msibani 
Waombolezaji wengi walikuwa kutoka Idara ya Habari (MAELEZO), Uhuru FM na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ukitazama kwa makini picha hii utawaona wanaotoka ofisi hizo. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi akitia saini kitabu cha maombolezo ya Souzzy. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Seth Kamuhanda. 
Waziri Nchimbi (kushoto) akimpa pole mume wa marehemu. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na watatu ni Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru 
Mahmoud (kulia) akimweleza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye jinsi kifo kilivyomfika marehemu Sozzy 
"Marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika sekta ya habari " pengine ndivyo Nape na Waziri Nchimbi walivyokuwa wakisema hapa, wakati wa kuangwa marehemu Sozzy 
"Sana Waziri,  huyu alikuwa kamanda katika wapiganaji kwenye eneo moja wapo la wizara yako," pengine hapa napo Nape alisema hivyo kwa Waziri Nchimbi.
Mahhoud akimshukuru Waziri Nchimbi baada ya kutoa salamu za  rambirambi. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Kushoto ni Nape 
Wadau kibao walihudhuria kuagwa kwa Sozzy. Kulia ni aliyekuwa Mkurugezi wa TBC, Datsun Tido Mhando 
Wafanyakazi katika Ofisi Ndogo ya Makau Makuu ya CCM 
Wadau wengine kama wanavyoonekana pichani.  
Jeneza lenye mwili wa Sozzy likitolewa ndani tayari kwa safari 

Likawekwa nje na kuswaliwa na waombolezaji 
Katibu Mkuu wa CCM ni miongoni mwa waliotoa salamu za rambirambi. 
Waziri Nchimbi alihitimisha kwa kutoa salamu za rambi rambi kabla ya safari ya kuupeleke mwili Sozzy kuanza.
Mzee Madanga Shaaban Madanga (aliyeshika tama) ni miongoni mwa waombolezaji walifika msibani hapo. 
Basi likiondoka nyumbani kwa Mzee Mikidadi Mahmoud kwa safari ya Mto wa Mbu, Arusha, likiwa na mwili wa marehemu Sozzy.
ยช