.

JK KUHUTUBIA BARAZA LA EID LEO; HOTUBA HIYO NDIYO PIA YA MWEZI HUU

Aug 31, 2011

UNITED REPUBLIC OF TANZANIADIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539

Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alasiri ya leo, Jumatano, Agosti 31, 2011, atahutubia wananchi kupitia Baraza la Idd kutokea mjini Dodoma.
Rais Kikwete ameungana na mamilioni ya Waislamu duniani kote na katika Tanzania kusherehekea siku hii ya kumaliza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na atahitimisha Sikukuu ya Idd Mosi kwa hotuba ambayo ataitoa kwenye Baraza hilo.
Hotuba hiyo kwa wananchi pia itachukua nafasi ya Hotuba ya Mwisho ya Mwezi wa Agosti ambayo Mheshimiwa Rais angeitoa kwa wananchi kwa mujibu wa utaratibu wake wa kawaida wa kuwasiliana na wananchi kila mwisho wa mwezi kwa hotuba.
Hotuba hiyo ya Mheshimiwa Rais itatangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari mbali mbali nchini kuanzia saa 10 alasiri.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
 31 August, 2011

RAIS AONGOZA SWALA YA EID EL FITR DAR

 Eid Mubarakaaaaa! Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono waumini wa Kiislam kabla ya kuondoka Msikiti wa Kichangani, Magomeni Dar es Salaam, baada ya Swala ya Eid El Fitr leo asubuhi
Waumini wakiswali Swala ya Eid El Fitr leo katika msikiti huo wa Kichangani, Magomeni Dar es Salaam. (Picha zote na Freddy Maro).

WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WAUAWA DODOMA;WANANCHI WAPANGA FOLENI KUONA MAITI

Aug 30, 2011

 Kamanada wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen akionyesha  gamba lisilopenywa risasi lililonusuru maisha ya polisi wake katika mapambanao na majambazi katika pori la Goma, barabara ya manyoni-Singida nje kidogo ya mji wa Dodoma, wiki iliyopita. katika tukio hilo watuhumiwa wanne wa ujambazi waliuawa na polisi
 Wananchi wakijaribu kunyanyua ili kujua uzito wa gamba lisilopenya risasi ambalo lilinurusu maisha ya polisi yaliokuwa wakipambana na majambazi wa kurushiana risasi katika msitu wa Goama, nje kidogo ya mji wa Dodoma wiki iliyopita.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen  akionyesha bunduki iliyotengenezwa kienyeji inayosadikiwa walikamatwa nayo watuhumiwa wanne  wa ujambazi waliouawa mjini humo wiki iliyopita katika majibishano ya risasi na polisi nje kidogo ya mji wa Dodoma.
wananchi wakipanga foleni kuingia chumba cha maiti cha hospitali ya mjini Dodoma kutambua maiti za watu wanne waliouawa na polisi katika majibishano ya risasi wakituhumiwa kwa ujambazi wa kuteka mabasi katika barabara kuu ya Manyoni-Singida. 
Wananchi watazama maiti za watuhumiwa wa ujambazi iliyowekwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa Dodoma 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen na Mkuu wa mkoa wa  Dodoma Dk James Nsekela na Mganga Mkuu wa hospitali ya Dodoma, Dk. Godfrey Mtei wakitoka katika chumba cha maiti kwenye hospitali  hiyo (Picha zote na Emmanuel Ndege aliyekuwa Dodoma)

CCM YATANGAZA MGOMBEA WAKE IGUNGA

Aug 29, 2011

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kutangaza mgombea huyo wa CCM jimbo la Igunga. Kushoto ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba.

PRESS CONFERENCE YA NAPE

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, leo saa kumi na moja jioni hii anazungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo muhimu ya Chama.
Miongoni mwa atakayozungumzia ni yaliyojiri katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyilia leo chini ya Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwetwe. Dont Miss!
Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati (kushoto) wakibadilishana mawazo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar  es Salaam, kabla ya kwenda katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM leo. Kikao hicho kilichofanyika mjini Dar es Salaam kimefanyika chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

LOWASSA ALIMWAGIA KKKT MAMILIONI YA FEDHA

NA MWANDISHI WETU KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Mwenge, Dar es Salaam, limevuna zaidi ya sh. milioni 119 zikiwemo sh. milioni 30.7 zilizochangwa na Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa katika harambee ya  kuchangisha fedha za kumalizia ujenzi wa kanisa hilo.
   "Mimi sina cha kikubwa cha kuchangia hapa, niseme tu kwamba nimekuja kuwazindulia harambee hii nanyi mtachangia kwa kadri ya nguvu zetu, lakini kuongoza ni kuonyesha njia kwa hiyo mimi nikisaidiwa na familia na marafiki zangu nitachangia sh. milioni 30.7", alisema Lowassa.
          Baada ya kutamka hivyo na kukabidhi kibunda hicho cha minoti kwa Msaidizi wa Askofu wa Kanisa hilo Kanda ya Mashariki na Pwani, Geoge Fupe, harambee hiyo iliyofanyika kwa watu kuchangia papo hapo na kunadiwa vitu mbalimbali, ilmalizika kwa kuingiza sh. 119,562,300
.       Mapema katika risala, Mchungaji  Luhuvilo Sigala alisema, ili kumalizia ujenzi wa kanisa hilo zilikuwa zinahitajika sh. milioni 94 na kwamba hadi sasa kanisa hilo limeshajengwa kwa asilimia zaidi ya 80.
        Baadhi ya vitu vilivyonadiwa na Lowassa ambnaye alaifuatana na Mkewe, Regina Lowassa, ni mbuzi watano waliotolewa na waumini, mchele, sukari na mikungu ya ndizi.
        Akizungumza katika misa kabla ya harambee hiyo, Fupe aliwataka waumini wa Kikristo na hususan wa KKKT kuhakikisha wanawalea watoto wao katika mazingira ya kupenda dini ili kuweza kupatikana waumini wa baadae.
       Fupe alisema kujenga makanisa bora bila  kuwalea watoto katika malezi hayo hakutakuwa na faida yoyote kwa sababu baada ya miaka ijayo  yatabakia makanisa mengi yasiyo na waumini.
      "kuna nchi nilitembelea hivi karibuni nikashangaa kuona makanisa makubwa makubwa, nilipohudhuria misa na kuombwa kuiendesha nilishangaa kukuta kanisa kubwa lakini ndani mna waumini wachache mno" alisema Fupe na kuongeza.
       "Nikauliza mbona kanisa ni kubwa mno tena la ghorofa lakini waumini wachache? nikaambiwa siku hizi waumini hawaji kanisani na sababu kubwa ni kwamba vijana wamenyimwa utamaduni wa kuabudu walipokuwa watoto", alisema.

UBUNIFU!!! BAJAJ ZENYE 'CHARGER' YA SIMU ZASAKA SOKO BONGO

Meneja Biashara ya Kimataifa wa Kampuni  ya Bajaj nchini India  Pulkit Kapahi akizungumza na madereva wa pikipiki hizo wakati wa mafunzo ya maalum kwa madereva na wamiliki kuhusu toleo jipya la Bajaji zenye muundo wa kisasa na vifaa vya kuchajia simu.
Commercial Manager of the Bajaj International company Pulkit Kapahi from India speaks with Bajaj Drivers during a special training session held in Dar es Salaam over the weekend for owners and drivers of the Bajaj, on a new Bajaj make-up with a new and unique accessories and a phone-charger 

KAMATI KUU YA CCM KUWAJADILI KESHO WANACHAMA WAKE WALIOOMBA KUGOMBEA UBUNGE IGUNGA

Aug 28, 2011

NA MWANDISHI WETU
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, inakutana kesho mjini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa na CCM leo imesema kikao hicho kitafanyika mchana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, pale mtaa wea  Lumumba.

"Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama  agenda za mkutano huo ni kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo ya maandalizi ya uchaguzi mdogo jimbo la Igunga ambayo itaenda sambamba na kujadili mapendekezo ya wana CCM wanaoomba kuteuliwa na CCM kugombea jimbo hilo", imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema, pia  Kamati Kuu itapokea na kujadili mapendekezo ya wana CCM wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya meya wa manispaa ya Songea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  Mukama amesema Kamati Kuu haitaishia hapo, mbali na hayo itajipa uwanja wa kujadiliu na kuamua kuhusu masuala mengine mbalimbali ya ndani ya Chama.

VODACOM MISS TANZANIA WACHUANA KATIKA BONANZA LAO LA MICHEZO

Aug 27, 2011

Na Mwandishi Wetu
Washiriki 30 wa Vodacom Miss Tanzania leo (jana)  walichuana vikali katika siku ya michezo ya Miss Tanzania iliyofanyika kwenye ufukwe wa bahari  wa Hoteli ya Jangwani See Breeze iliyopo Mbezi Kilongawima jijini Dar es Salaam.
 Wakiadhimisha siku hiyo washiriki hao wa shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo nchini walichuana kwenye michezo mbalimbali ikiwemo Volleball, kuruka kamba, kukimbia na magunia, mbio za vijiti, kuvuta kamba na michezo mingine ya kuvutia.
Akizungumzia siku hiyo Meneja Uhusiano na Habari kwenye Mtandao Matina Nkrulu alisema lengo la siku hiyo ni kuwaunganisha warembo pamoja wakiwa tayari kuelekea kwenye hatua ya mwisho ya shindano hilo.
Akifafanua Nkurlu alisema kwamba mbali ya kuwaunganisha michezo pia imesaidia kuibua vipaji vya warembo hao mbali na fani ya urembo wanayojihusisha nayo.
“Tukiwa kwenye siku ya michezo ya Vodacom Miss Tanzania warembo wameonesha vipaji vyao vya kimichezo jambo lililowafanya pia kuendelea kuwa pamoja kama ilivyo tasnia hiyo kwamba inawaunganisha watu wote bila kujali dini rangi au kabila.
Kwa wake mrembo Glory Lory amesema siku hiyo ni ya faida kwao kwani wameweza kujifunza michezo mbalimbali ambayo walikuwa hawajawahi hata kuipitia.
Akifafanua Glory alisema mbali ya kujenga afya pia wamepanua mtazamo wa kiakili kwani ni moja ya fani zinazoenda kushindaniwa katika shindano la Miss World kwa atakayebahatika kuliwakilisha taifa.
“Michezo ni moja ya vipengele kwenye shindano la urembo la dunia, hivyo kwa atakayebahatika atafanya vizuri kwani mazoezi haya yamempika tayari kwa kwenda kushiriki michuano hiyo ya urembo ya dunia.
Nae Mkuu wa kitengo cha Itifaki wa Kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye alisema ari waliyonayo warembo inaonesha utayari wao katika kuliwakilisha taifa katika medani za kimataifa.
“Mmejionea wenyewe washiriki wetu walivyochuana katika michezo mbalimbali katika kuadhimisha siku ya michezo kwa warembo. Hili tu linadhihirisha kwamba shindano la mwaka huu litakuwa na changamoto kubwa ikilinganishwa na mengine yaliyopita,” alisema Makoye.
Tayari washiriki hao wanaoishi ndani ya jumba la Vodacom wameanza kupigiwa kura na watazamaji wa vituo vya televisheni  Star tv na Clouds TV baada ya maisha yao ndani ya nyumba kuoneshwa moja kwa moja na vituo hivyo.

NAPE:MAKANISA YANATOA MCHANGO MKUBWA MAADILI YA VIJANA


Nape Nnauye (wapili kulia) akikata keki maalum iliyoandaliwa katika sherehe ya
 kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne ambao ni wanachama wa  Jumuia
ya wanafunzi wakatoliki Tanzania (TYCS) Kanda ya Kimala, kuchangisha
 fedha za kuimarisha jumuia hiyo, leo Kimara, Dar es Salaam.
 Kulia ni Mlezi wa TYCS Kimala, Padri  Zengo. Watatu kulia ni Katibu wa
 Jumuia ya Wazazi Kinondonbu, Stanley Mkandawile
 Na Mwandishi Wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinatambua mchango wa Makanisa katika kujenga maadili ya vijana.

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne, wanachama wa Jumuia ya Wanafunzi Wakakatoliki Tanzania (TYCS) Kanda ya Kimara, Dar Salaam.

"Mchango unaotolewa na madhehebu ya dini mkiwemo Wakatoliki hapa nchini, kwa kweli ni mkubwa sana na ndio unaochangia kwa kiasi kikubwa kujenga uadilifu kwa vijana na Wananchi kwa jumla", alisena Nape na kuongeza. "Uadilifu unaotolewa na dini  huwajenga vijana na wananchi kwa jumla kumweka mbele Mungu wao katika kila jambo na hivyo kuwa sababu kubwa ya kuwa waadilifu kuliko wale wanaofanya mambo yao bila kutanguliza Mungu".

"Hata viongozi wetu wanapokuwa katika upokeaji rushwa hufanya hivyo kutokana na kutokuwa na hofu ya Mungu kwa kuwa wakati wakifanya hivyo kujiona yupo yeye na mtoa rushwa tu Mungu hayupo nao, tofauti na mwadilifu ambaye huogopa kupokea au kutoa rushwa kwa kuwa moja ya mambo yanayomzuia ni kutambua kuwa popote alipo Mungu yupo", alisema Nape.

Nape alisema hatua ya dini kuwapatia vijana malezi ya Kimungu kunawafanya kuwa binadamu wa kwa sababu binadamu asiye  na malezi ya Kimungu hahofii chochote anapotenda jambo na kwa hiyo huwa hana tofauti na mnyama yeyote kama simba au bweha.

Alisema, malezi ya kimungu huwafanya watu kuwa waadilifu zaidi ya wale ambao kufanya uadilifu kwa kuhofia sheria za serikali na kwamba hata yakiwepo magereza mengi kiasi gani bado wasio na uadilifu unaotokana na malezi ya Kimungu wengi hawaogopi.

Nape aliwataka wahitimu hao na vijana kwa jumla kuwa na malengo wanapotaka kufikia mafanikio mazuri katika maisha yao na baada ya kuweka malengo kuyalinda kwa kukwepa yale yanayoweza kusababisha wasifikie malengo hayo.

"Kwa mfano ukiweka lengo la kufaulu mtihani lazima ujitahidi kukwepa vishawishi vinavyoweza kukufanya usifikie lengo hilo kama utoro shuleni, kulala badala ya kujisomea na kupenda starehe", alisema.
Aliwataka kujiepusha na  mazungumzo mabaya akisema mazungumzo ya aina hiyo huwa chanzo cha kuharibu tabia njema ya kijana.

Nape aliwataka vijana kuwa makini wanapotembelea mitandao katika konpyuta na simu zao kwa kuwa licha ya ubora wa mawasiliano kwa njia hiyo lakini mna taarifa nyingi za uongo na upotoshaji wa maisha malisi.

Katika sherehe hiyo Nape alikabidhi vyeti kwa wanafunzi zaidi ya 300 na  kukata keki maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuendeleza Umoja wa TYCS Kanda ya Kimara ambapo kabla ya kuondoks zilikusanywa sh. 500,000 zikiwemo 100,000 alizochangia.

MTOTO WA JK APIGA GOZI NA TIMU YA TAIFA YA VIJANA YA U17

Aug 26, 2011

Khalfan Kikwete, mtoto wa Rais Jakaya Kikwete(kushoto) akijaribu kuumiliki mpira aliposhiriki katika mazoezi ya timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, kwenye Uwanja wa Karume Dar es Saalm, jana 
Khalfan (kushoto) akiumiliki pia mpira wakati wa mazoezi hayo 
Kipa wa timu hiyo Mwangata, akidaka mpira pamoja na mguu wa  Khalfan kuepusha bao 
Baada ya kunusrika kudakwa mguu Khalfan akaruka kuepusha 'ajali' 
Kocha Julio wa tomu hiyo akitoa somo kwa wacheza wakati wa mazoezi hayo, watatu kushoto ni Khalfan 
Hussein Ibrahim wa shule ya sekondari Usagara ya Tanga ambaye ni mchezaji wa timu hiyo, akipeana mkono baada ya mazoezi kuhu kocha mkuu wa timu hiyo, Kim Polsen akiwacheki kwa bashasha 
Kocha msaidi wa timu hiyo, Julio akitoa nasaha baada ya mazoezi. Kushoto ni Khalfani

VODACOM YATOA FURSA WATANZANIA KUWAPIGIA KURA WASHIRIKI WA SHINDANO LA VODACOM MIISS TANZANIA

Aug 24, 2011

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetoa fursa kwa Watanzania kuweza kupiga kura na kuchagua mrembo anaevutia zaidi kati ya warembo 30 wanaoshiriki katika shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2011.
         Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Bw. George Rwehumbiza amesema ili kupiga kura Watanzania watatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na namba ya mshiriki kwenda 15550 ambapo gharama kwa kila ujumbe ni shilingi 150 tu .
       Aidha Bw, Rwehumbiza aliongeza kuwa kila ujumbe mfupi utakaotumwa utampatia Mtanzania pointi 10 ambapo wateja 20 watakaobahatika kuwa na pointi nyingi zaidi kila mmoja atajipatia TIKETI mbili za VIP zitakazomwezesha kwenda kushuhudia fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011 itakayofanyika tarehe 10 mwezi septemba katika ukumbi wa  Mlimani city jijini Dares salaam.
        Pia kwa wale watakaohitaji kutoa maoni au mitazamo yao mbalimbali kuhusu Vodacom Miss Tanzania watapata fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na maoni kwenda namba 15550.
        Akisisitiza hili Bw. Rwehumbiza alisema ili kuwafahamu warembo wanaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 Watanzania wote wanaweza kuangalia kituo cha STAR TV leo kuanzia muda wa saa moja jioni pamoja na CLOUDS TV muda wa saa tatu usiku kila siku pia soma magazeti ya Mtanzania, The African,Dimba,Rai na Bingwa.. 
   Vodacom kazi ni kwako

MBUNGE SILIMA AFARIKI KUFUATIA AJALI YA GARI ILIYOTANGULIA KUMUUA MKEWE

Aug 23, 2011

Silima
Mbunge Mussa Hamisi Silima, aliyejeruhiwa baada ya kupata ajali jana mjini hapa,
amefariki dunia.
      Silima alifariki dunia leo saa tano asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako alihamishiwa na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu
zaidi.
        Taarifa za kifo cha Silima zilitangazwa jana saa 5.50 asubuhi na Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati wabunge wakiendelea kuchangia makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2011/2012.
       "Waheshimiwa wabunge, kama mtakumbuka jana niliwatangazia kwamba,
mheshimiwa Mussa Hamisi Silima, alipata ajali mbaya eneo la Nzuguni, ambapo
mke wake, Mwanaheri Twalib alifariki dunia hapo hapo.
    "Aidha niliwaarifu kuwa, mheshimiwa Silima na dereva wake walipata majeraha makubwa na wamepelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Leo asubuhi kabla ya maswali,nimetoa taarifa kwenu kwamba nimeongea na mheshimiwa Silima akiwa anaendelea kupata matibabu. Ni kweli nimeongea naye.
          "Kwa masikitiko makubwa, nawatangazieni kuwa, nimepokea taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwamba, mheshimiwa Mussa Hamisi Silima amefariki dunia muda mfupi tu uliopita.
        "Kwa mujibu wa kanuni ya 149 ya kanuni za bunge, toleo la mwaka 2007, ninaahirisha shughuli za bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi," alisema.
         Kufuatia msiba huo, Spika Anne aliwataka wabunge wasimame kwa dakika moja kwa heshima ya mbunge huyo.
Spika alisema kwa kipindi cha siku tatu, familia ya Silima imekumbwa na matatizo makubwa, kufuatia kutanguliwa na msiba wa kaka wa mkewe kabla ya mkewe naye kufariki dunia.
  Katika ajali iliyotokea jana eneo la Nzuguni, mke wa mbunge huyo, Mwanaheri
alikufa papo hapo eneo la ajali wakati dereva wake, Chizali Sembonga, aliyekuwa
akiendesha gari aina ya Toyota Corolla, lenye namba za usajili T 509 AGC
alijeruhuwa.
Silima na mkewe walipatwa na ajali hiyo walipokuwa wakirejea Dodoma. Mbunge
huyo alikuwa amekwenda Zanzibar kuhudhuria maziko ya kaka wa mkewe,
Mwanaheri.
Mbunge huyo na dereva wake walisafirishwa kwa ndege juzi kwenda Dar es
Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Mwili wa Mwanaheri ulizikwa juzi alasiri

TAARIFA KIBAO KUTOKA TFF

Release No. 80
RATIBA YA LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA
Baada ya Serikali kuufunga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa ajili ya marekebisho, Yanga na Simba ambazo awali zilikuwa zimeruhusiwa kutumia uwanja huo kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zililazimika kutafuta viwanja vipya. Simba imehamia Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Yango iko Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

Licha ya timu hizo kupata viwanja vipya ratiba itabaki kama ilivyotolewa awali. Mechi za Simba zilizokuwa zichezwe Uwanja wa Taifa sasa zitachezwa Mkwakwani wakati za Yanga zitachezwa Jamhuri. Kutokana na mabadiliko hayo ratiba inasomeka kuwa Septemba 7 mwaka huu Coastal Union v Moro United (Mkwakwani) na pia Simba v Villa Squad (Mkwakwani). Mechi ya Simba v Villa Squad imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo sasa itachezwa Septemba 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

MCHEZAJI CASTORY MUMBARA
TFF imeshindwa kumpa leseni Castory Mumbara ambaye ameombewa usajili katika timu ya Toto Africans kutokana na kutokuwa na Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) ambayo inatakiwa kutolewa kupitia mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS).

Ikumbukwe kuwa Mumbara alikuwa akichezea timu ya Himalayan Sharpa ya Nepal ambapo alikwenda huko baada ya TFF kumpatia ITC. Hivyo ili aichezee Toto Africans, klabu hiyo ilipaswa kumuombea hati hiyo kupitia mtandao wa TMS baada ya kufanya mawasiliano na Himalayan Sharpa.

Muda wa usajili ulimalizika Julai 31 mwaka huu, hivyo Toto Africans kwa sasa haiwezi kumtumia mchezaji huyo badala yake inatakiwa kusubiri dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa tena Novemba mwaka huu. TFF iliendesha mafunzo ya kutumia mfumo wa TMS kwa watendaji wote wa klabu za Ligi Kuu ikiwemo Toto Africans.

MECHI YA STARS v ALGERIA
Mechi hiyo namba 103 ya mchujo kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani Equatorial Guinea na Gabon itachezwa nchini Septemba 3 mwaka huu.

Bado tunasubiri majibu ya ombi letu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo la kuturuhusu kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo.

ALL AFRICA GAMES
Mwamuzi msaidizi John Kanyenye wa Tanzania ni miongoni mwa waamuzi 32 (waamuzi wa kati na wasaidizi) walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha michezo ya All Africa Games itakayofanyika Maputo, Msumbiji kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu. Kati ya hao, 16 ni wanaume na 16 ni wanawake.

Kanyenye ni mmoja kati ya waamuzi watatu kutoka  ukanda wa CECAFA- Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati walioteuliwa kuchezesha michezo hiyo. Wengine ni mwamuzi wa kati wa kike kutoka Uganda, Nabikko Ssemambo na mwamuzi msaidizi wa kike kutoka Ethiopia, Trhas Gebreyohanis.
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

TANGAZO LA AJAAT

1.0 WAZO: Chama cha Waandishi wa Habari za Ukimwi Tanzania (AJAAT), kupitia ufadhili wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kinatangaza shindano la miezi mitatu kwa wandishi wa habari ya kuandika kuhusu UPATIKANAJI WA HUDUMA ZOTE MUHIMU ZA UKIMWI KWA MAKUNDI YA WATU WALIONYIMWA FURSA NA WALE WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI ZAIDI NCHINI. Kilele cha shindano hilo litakalohusisha waandishi wa habari za magazetini,  majarida, vituo vya runinga, redio, wachora vikaragosi (katuni)  na mitandao ya blogu nchini, kitakuwa wakati wa maadhimisho  ya Siku ya Ukimwi Duniani, – Desemba 1, 2011. Washindi wa shindano watazawadiwa fedha taslimu, ngao na vyeti vya ushiriki.
2.0 TAARIFA YA MSINGI: Programu shirikishi ya Umoja wa Mataifa kuhusu virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI (UNAIDS) inatafsiri upatikanaji huduma kwa wote kuwa ni dhamira ya dunia katika kupanua upatikanaji wa matibabu, kinga, matunzo na misaada kwa waathirika wa Ukimwi. Inahusisha jamii ambapo kila mtu anaweza kupata taarifa sahihi kuhusu UKIMWI na huduma za matunzo ya kiafya.
Lakini je, kila mtu katika yamii zetu wanapata huduma za kiafya? Kila mtu anapata elimu kuhusu UKIMWI kupitia vyombo vya habari na hivyo kumwezesha kufanya uamuzi mzuri kuhusu afya zao? Bahati mbaya majibu kwa aina hii ya maswali ni hapana. Pamoja na uwepo wa huduma nyingi za afya, siyo kila mtu katika jamii yetu ana uwezo sawa wa kupata huduma hii hata kama angehitaji na kuipata.
Nchini Tanzania, kwa mfano, makundi kama ya wanaouza miili (changudoa), wanaoishi na virusi vya ukimwi, walemavu,  wanaojidunga dawa za kulevya, ombaomba , wafungwa na mashoga wanahisi kunyanyapaliwa na kubaguliwa kila siku kutokana na hisia hasi dhidi ya watu wa jamii hiyo. Hali inaweza kuwa mbaya zaidi na unyanyapaa unaohusisha Ukimwi hasa kwa wanaoishi na VVU na UKIMWI na kufanya kuwa ngumu zaidi kwa watu wa makundi hayo kupata haki za msingi na kupata huduma bora za kiafya.
Wakati huduma za UKIMWI nchini Tanzania na kwingineko inaongezeka katika baadhi ya vitengo, makundi ya waliomo kwenye mazingira hatarishi zaidi ya kuambukizwa VVU na UKIMWI yanazidi kupambana na vikwazo vya kiufundi, kisheria na vya kiutamaduni katika kupata huduma ya matunzo ya kiafya.
Zaidi ya hapo, kuna mambo yanayohusu usiri ambayo ni ya msingi kwa huduma ya Ukimwi katika visiwa vidogovidogo ambapo kila mtu anamfahamu mwenzake. Na hii inajitokeza katika maswali yanayoulizwa mara kwa mara na watu wanaohitaji huduma ya matunzo na matibabu, kwamba ‘Je, nikipata huduma hii kila mtu atajua shughuli yangu?’ Kwa hiyo changamoto ya kufanikisha upatikanaji huduma kwa wote haihusiani tu na upatikanaji wa huduma ya matunzo na matibabu, bali masuala kama unyanyapaa, ubaguzi na usiri.
Kwa hiyo, lengo la shindano hili ni kuwahamasisha waandishi wa habari wa magazeti na vyombo vya elektroniki kuandika makala na programu zitakazowawezesha watu wa makundi hayo kupata huduma bure na bora za UKIMWI na kuwawezesha kupata na kufurahia maisha chanya ambayo ni haki ya msingi kama Mtanzania mwingine yeyote.
Kimsingi, shindano hili halitawataka waandishi wa habari kuandika, kupiga picha, kuandika programu za redio na runinga tu kuhusu masuala ya haki kwa wote na yanavyohusishwa na janga la UKIMWI,  bali  litawataka waandishi kuibua mambo ya kisera na mipango ya serikali na mamlaka zake katika kushughulikia tatizo hili. Aidha, wataitaka sekta binafsi kuonyesha wanavyoweza kufanya kuueleza umma wa Watanzania ukweli kwamba upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI kwa wote hasa kwa walio katika hali hatarishi zaidi unaweza kupunguza kusambaa kwa VVU nchini.
3.0 UTANGULIZI: Takwimu na taarifa zilizopo za mpango wa sekta mtambuka wa kinga ya VVU na UKIMWI wa 2009 – 2012 (National Multisectoral HIV Prevention Strategy of 2009-2012) unaelezea kuwa kipaumbele katika hatua za kuchukua katika jitihada za kuzuia kasi ya maambukizi ya virusi ni kupanua huduma   kwa makundi yaliyomo katika mazingira hatarishi zaidi.
Makundi ya wanaouza miili yao (changudoa), wanaoishi na VVU na UKIMWI, walemavu,  wanaojidunga dawa za kulevya, ombaomba, wafungwa, mashoga na kadhalika, wanatengwa katika kupata huduma za VVU na UKIMWI kwa sababu mbalimbali pamoja na ukosefu wa huduma katika baadhi ya sehemu  na unyanyapaa, ubaguzi na kutokuwepo na usiri.
Kwa hiyo masuala hayo yanatakiwa kushughulikiwa mara kwa mara kwa njia ya uhamasishaji na kusambaza taarifa  kwa usahihi  kusudi taifa lifanikishe upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI hususani kwa kundi lililo katika mazingira hatarishi.
4.0 SHINDANO LENYEWE: Nia ya shindano hili ni kuwahamasisha waandishi wa habari, wapiga picha za habari, wachoraji wa vikaragosi, waandishi wa makala, makala maalum, watayarishaji vipindi na watangazaji wa vyombo vya habari kufanya uchambuzi na utafiti wa kina na kutoa makala zenye uelewa mpana na kuonyesha uhusiano kati ya haki ya kupata huduma za VVU na UKIMWI. Waandishi pia watatakiwa kuonyesha athari za kisera na kijamii kama makundi yaliyo katika mazingira hatarishi hayatapata huduma za VVU na UKIMWI, na kushauri mwelekeo sahihi na bora zaidi unaopaswa kuchukuliwa.
5.0 MALENGO: Shindano pia litakuwa na malengo yafuatayo:
i.          Kuhamasisha waandishi wa habari wa vyombo vyao kuandika kwa upana kuhusu uhusiano kati ya upatikanaji huduma za VVU na UKIMWI kwa wote wanaoishi katika mazingira hatarishi na uwezekano wa kuongezeka zaidi kwa maambukizi ya VVU kama watanyimwa huduma hizo.
ii.         Kuoanisha masuala ya jinsia katika taarifa zao ili kuzuia/kupunguza maambukizi zaidi ya VVU katika jamii ya Tanzania.
iii.        Kujaribu na kuthubutu kuibua vizuizi vya kisheria, kijamii na kitamaduni kwa makundi  hayo kupata huduma za UKIMWI zinazokubalika kimataifa na kutafuta ufumbuzi wake.
iv.        Kuziweka habari za UKIMWI katika hali ya kuvutia kwa kutumia mtindo wa uandishi wa habari unaohamasisha upatikanaji huduma za UKIMWI kwa wote nchini.
6.0 MATOKEO: Baada ya miezi mitatu ya shindano, waandishi wa habari wa vyombo vya elektoniki – redio, runinga; wapigapicha, waandishi wa makala, makala maalum na wa mtandao wa blogu watakuwa wameandika makala za kutosha kuhusu upatikanaji wa huduma za UKIMWI kwa wote na jinsi zinavyohusiana na kuongezeka kwa maambukizi ya VVU.
6.1 MATARAJIO: Kupungua kwa maambukizi ya VVU na UKIMWI katika jamii ya Kitanzania na kufikia mpango wa Tanzania bila UKIMWI inawezeka.
7.0 MWONGOZO WA MAUDHUI: Maswali yafuatayo yanaweza kuwaongoza waandishi wa habari katika juhudi zao za kutafuta mambo ya kuandika katika makala zao/programu zao/picha zao au vikaragosi vyao:
i.          Je, ni namna/jinsi upatikanaji mbovu wa huduma za UKIMWI kwa wote na uliokubalika kimataifa unaoweza kuongeza maambukizi ya virusi nchini.
ii.         Je, Matatizo gani yanayomkabili mtu aliye katika mazingira hatarishi katika kupata huduma za UKIMWI?
iii.        Nani na kwa namna gani serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi   anachangia/zinavyochangia katika upatikanaji wa huduma mbovu au bora za UKIMWI kwa wote.
iv.        Je, mtu anapogundua amenyimwa huduma za UKIMWI zinazokubalika kimataifa afanye nini kuepuka kuchochea maambukizi mapya ya virusi?
v.         Je, kuna njia yoyote ya kisheria inayomlinda mtu asinyimwe kupata   huduma za UKIMWI na kama kuna uwezekano wa utekelezaji wa sheria hizo.
vi.        Je, taifa linaweza kunufaika vipi kiuchumi na kijamii kama watu walio katika mazingira hatarishi watapata huduma zote kwa urahisi bila unyanyapaa au ubaguzi?
vii.       8.0 KUNDI LENGWA: Shindano lipo wazi kwa waandishi wote wa habari na makala maalum wa Tanzania kutoka vyombo vyote vya habari.  Ni vyombo vya habari vya Kitanzania tu vinaruhusiwa kushiriki na waandishi watakaoleta kazi zao lazima wawe wnafanya kazi katika vyombo vya Tanzania.
  
9.0 MUDA: Shindano litaendelea kwa miezi mitatu (kuanzia Agosti 18 hadi Novemba 18, 2011).
  
10.0 MASHARITI NA VIGEZO: Yafuatayo ni masharti na vigezo vya ushiriki.
  
i.    Waandishi wanaopenda kushiriki katika shindano ni lazima wawe wanaishi na kufanya kazi nchini Tanzania.
ii.   Makala/habari na programu zitakazowasilishwa lazima zilenge makundi yaliyomo katika mazingira  hatarishi zaidi Tanzania.
iii.  Kazi zitakazowasilishwa lazima zionyeshe ubunifu na si zilizonakiliwa kutoka machapisho mengine. Ziwe zimetangazwa au kuchapishwa katika kipindi cha miezi mitatu ya shindano, yaani kutoka Agosti 18 mpaka Novemba 18, 2011.
iv.  Ziwe zimechapishwa  au kutangazwa kwenye magazeti, majarida, runinga au redio.
v.   Zinaweza kuchapishwa au kutangazwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
vi.  Kazi halisi tu zitakubaliwa.
vii. Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha itakuwa Novemba 22, 2011.
viii.            Zawadi za fedha taslimu kuanzia 300,000/= hadi 700,000/= zitatolewa kwa washindi 15 wa kwanza watakaochaguliwa na jopo la majaji kutoka wadau mbalimbali Siku ya Ukimwi Duniani. Waandishi wote watakaoshiriki watapewa vyeti vya ushiriki.
  
11.0 UWASILISHAJI: Washiriki wanaruhusiwa kuwasilisha hadi makala/vipindi/machapisho matatu kwa ajili ya shindano na kupeleka kwa anuwani zifuatazo:

i.          AJAAT Media Writing Competition-2011, Bahari Motors Building, Plot No. 43, Kameroun Street, Kijitonyama, P O Box 33237, tel. 0713 640520/0786 300219, DAR ES SALAAM-TANZANIA
ii.         Ms Jovina Bujulu, MAELEZO/Information Auditorium Services Centre, Samora, Avenue, DAR ES SALAAM, TANZANIA

TASWA YAIPONGEZA TIMU YA TAIFA YA GOFU YA WANAWAKE, KUTANGAZA JUMATANO KAMATI YA KUSIMAIA TAMASHA LA MICHEZO MIAKA 50 YA UHURU

Aug 22, 2011


Katibu Mkuu wa TASWA,
 Amir Mhando
 (A)      TIMU YA TAIFA YA GOFU WANAWAKE
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pongezi kwa timu ya Taifa ya gofu ya wanawake ya Tanzania ‘Tanzanite Stars’ ilitwaa ubingwa wa mashindano ya gofu ya Kombe la Challenge kwa wanawake katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
          Mashindano hayo yalianza Agosti 16 hadi Agosti 18, mwaka huu kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Dar es Salaam.          TASWA imekunwa na mafanikio hayo na inatoa pongezi za dhati kwa timu hiyo kuweza kutetea ubingwa wake katika mashindano ambayo yanafanyika kila baada ya miaka miwili ambpo yalikuwa ya pili na ya viwanja 54.
      Tunasema vijana wetu wanastahili pongezi kwani nchi zote nne kutoka zilizoshiriki ambazo ni Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania zipo juu katika mchezo huo kwa wanawake. 
        Nchi za Rwanda, Burundi, Malawi, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zilishindwa kushiriki, lakini tatizo kubwa ni kukosa timu za wanawake.
       Tanzania ambao walikuwa mabingwa watetezi wa Kombe hilo ambalo kwa mara ya kwanza walitwaa mwaka 2009 Kampala, Uganda walitetea vema kwa kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Hayo ni mafanikio makubwa katika uongozi mpya wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) chini ya Rais, Mbonile Burton tangu kuingia madarakani Juni mwaka jana. Mafanikio haya yanafuatia yale ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Afrika ya gofu kwa wanawake Abuja, Nigeria mwaka jana.
       Pia TLGU imeweza kutangaza vema gofu ya wanawake na kuweka historia ya kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa kwa mara ya kwanza.
        Mwaka huu Tanzania wameibuka mabingwa kwa kishindo zaidi wakiwaacha wapinzani wao Zambia walioshika nafasi ya pili kwa tofauti ya mikwaju (strokes) 31. Mwaka 2009 ugenini walishinda kwa tofauti ya mikwaju 20.
        Tunaomba wachezaji wa Tanzanite Stars wakiongozwa na  nahodha Madina Iddi, Ayne Magombe, Angel Eaton na Hawa Wanyeche waone mafanikio haya waliyoyapata Watanzania wote tunayajali.
(B)  TAMASHA LA MICHEZO MIAKA 50 YA UHURU
Uongozi wa TASWA Jumatano Agosti 24, 2011 saa tano asubuhi utatangaza majina ya Kamati ya Kusimamia Tamasha la Michezo Miaka 50 ya Uhuru.
         Mkutano huo utafanyika hosteli za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam , hivyo ni imani yetu waandishi wengi watajitokeza. Pia tutazungumzia kuhusiana na semina mbalimbali ambazo chama kipo katika maandalizi ya kuzifanya.

Nawasilisha.

Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

FAINALI KUHIFADHI QUR-AN YAFANYIKA LEO DAR

Aug 21, 2011

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa  fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo  katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 21. Picha na Muhidin Sufiani-OM

UTAALAMU WA MFUGAJI KUKU WA ILALA DAR

Mkazi wa Ilala, Dar es Salaam, Sabri Ali Omari akiwalisha kuku majani kuwakinga ugonjwa wa mdondo badala ya dawa za kawaiada. Sabri ambaye pia ni mfanya biashara anafuga kuku zaidi ya 100 nyumbani kwake.(Picha na Emmanuel Ndege).

RAIS AKAGUA CHANZO CHA MAJI LINDI

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikagua chanzo cha maji ya Minispaa ya Lindi, Kitunda kata ya Msinjahili manispaa hiy leo mchana kwenye siku ya pili ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Lindi(picha na Freddy Maro).

MAMA SALMA KIKWETE AWAPA CHANGAMOTO WALIMU

Mwalimu  Mama Salma Kikwete
Na Anna Nkinda – Maelezo
Ili kuboresha elimu na kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hapa nchini walimu wametakiwa kuwa karibu na wanafunzi wao na kuwapenda kwa kufanya hivyo wanafunzi watayapenda masomo wanayoyafudhisha na kuwaheshimu.
Wito huo umetolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiwaaga walimu wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino tawi la Mtwara waliokuwa wanafanya mazoezi ya kufundisha katika shule za Sekondari za WAMA – NAKAYAMA na Nyamisati zilizopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Hafla hiyo fupi ya kuwaaga wanafunzi hao ilifanyika jana katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) zilizopo ikulu jijini Dar es Salaam.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa WAMA alisema kuwa kama mwalimu hatakuwa karibu na wanafunzi wake ni vigumu kwa wanafunzi  kuyapenda masomo anayoyafundisha pamoja na kumpenda mwalimu huyo.
“Ninyi hapa ni walimu wanafunzi ipo siku mtakuwa walimu kamili na mtakuwa  walimu wa darasa au walimu wa zamu hivyo basi ni lazima muwe karibu na wanafunzi , msikae nao mbali na kuwachukia kwa kufanya hivyo hawatawapenda hata kama  mtakuwa mnafundisha vizuri kiasi gani”, alisema.
Aidha Mama Kikwete  aliwataka walimu hao kufuata maadili yao ya kazi  ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya heshima jambo ambalo litawafanya wafanye kazi zao vizuri huku wakipata heshima kutoka kwa wanafunzi pamoja na jamii inayowazunguka.
Wakiongea kwa niaba ya wenzao Hango Tatu na Magoa Kaiza walisema kuwa licha ya wao kwenda kujifunza kufundisha katika shule hizo pia wamejifunza mambo mengi zaidi ambayo yatawasaidia katika kazi yao ya ualimu na maisha yao kwa ujumla.
Walisema, “Tumeona jinsi walimu wanavyofundishana namna ya kuwafundhisha wanafunzi jambo ambalo hatujawahi  kuliona , wanaandaa program, namna ya kuandaa somo na kutengeneza skimu ya kazi hakika inapendeza.
Sisi kama walimu shida kubwa inayotusumbua ni lugha ya kiingereza na somo la hesabu tulipata bahati ya kuhudhuria mafunzo ya Peaceful start ambayo yametusaidia sana,  tunahakika kuwa mafunzo haya licha ya kutusaidia katika kazi yetu ya ualimu pia yatatusaidia katika maisha yetu ya baadaye”.
Kwa upande wa wanafunzi waliokuwa wanawafundisha walisema kuwa wanafunzi hao wananidhamu , hawahitaji kusukumwa huku wakifuata ratiba wanayopangiwa  ukilinganisha na wanafunzi wa shule zingine ambazo wamewahi kufundisha kwani mwanafunzi bila kuwa na nidhamu hawezi kusoma vizuri.
Kutokana na utaratibu wa vyuo kuwapa fursa wanafunzi wake kwenda kufundisha kwa vitendo katika shule mbalimbali hapa nchini shule hizo zilipokea walimu wanafunzi saba kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Mtwara  ambao walifundisha  kwa kipindi cha mwezi mmoja.

VODACOM MISS TANZANIA WAMALIZA ZIARA KANDA YA KASKAZINI

Washiriki waVodacom Miss Tanzania wakiwa mbele ya Vodacom House
Na Mwandishi Wetu.
Washiriki 30 wa shindano la Vodacom Miss Tanzania waliokuwa kwenye ziara ndefu ya kimafunzo mikoa ya Morogoro, Kilimanjaro na Arusha wamemaliza ziara hiyo na wamerejea ndani ya jumba lao 'Vodacom House'.
          Ziara hiyo ya mafunzo iliyochukua takribani siku kumi iliwafikisha walimbwende hao kwenye Hifadhi za Taifa za Mikumi, Ngorongoro,Tarangire na shule ya wasichana ya Maasai iliyopo wilayani Mbonduli.  
          Meneja Uhusiano na Habari za  Mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu aliyataja maeneo mengine waliyotembelea kuwa ni shule ya watoto wa kimaasai Monduli, Kaburi la hayati Moringe Sokoine, kiwanda cha Bia TBL tawi la Arusha na mitambo ya simu ya Kampuni ya Vodacom ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo.
           Akiielezea ziara hiyo ya mafunzo aliyoiita ya mafanikio, Nkurlu amesema warembo hao wamepata fursa ya kujifunza mengi hususani kuhusiana na utalii wa ndani.
           “Tumemaliza salama ziara hii ya mafunzo iliyowapa zaidi ufahamu walimbwende hawa kuhusiana na historia na rasilimali zilizopo nchini. Washiriki wamejionea maeneo mbalimbali ya kitalii ikiwemo Ngorongoro Crater ambapo wanyama pori na binadamu  wanaishi katika eneo moja,” alisema.
            Nae Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency ambao ndio waandaaji wa shindano hilo Hashim Lundenga alisema, baada ya kuwasili washiriki hao 30 walipata fursa ya kukutana na ndugu, jamaa na
marafiki katika siku ya familia iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo.
            “Baada ya ziara ndefu Morogoro na kanda ya kaskazini, warembo wamekutana na jamaa zao kwa mazungumzo kabla hatujaingia kwenye hatua ya mwisho ya kumtafuta mshindi. Ni matarajio yetu wataitumia elimu waliyoipata katika kuvitangaza vema vitutio vya utalii vilivyopo nchini huko waendako,” alisema Lundenga.
            Kwa upande wake mrembo Jennifer Kakolaki alisema anajivunia kuwa mmoja wa washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kwani hata baada ya  kumalizika kwa shindano hilo anaweza kutumia elimu waliyoipata kujitafutia ajira kupitia sekta hiyo ya utalii.
            “Kiukweli tumejifunza mengi kwenye ziara yetu, nawashukuru waandaaji na Kampuni ya Vodacom kwa kuona umuhimu wa kutuandalia ziara hii ikiwemo kutupatia muda wa kukutana na familia zetu. Kwa niaba ya wenzangu naahidi hatutawaangusha na tutafanya tulichojifunza,” alisema Kakolaki.
            Mwaka huu warembo hao wameingia kambini kwa mfumo  tofauti na uliozoeleka kwani wanaishi kwenye jumba maalum la Vodacom  ambapo matukio yao yatakuwa yakioneshwa kupitia Startv na Clouds TV na watazamaji watapata fursa ya kupiga kura kuchagua mrembo watakayemuona anafaa.

MTOTO WANYOKA NI NYOKA?

 Mtoto wa kocha wa ngumi, Rajabu Mhamila, Zainabu Mhamila 'Ikota' akimtupia ngumi, Bondia Yohana Robert katika mazoezi ya kukuza vipaji vya mchezo huo yanayoendelea  katika Klab ya Ashanti, Ilala, Dar es Salaam.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/ ).

POLISI KIGOMA YANASA MWIZI ZA VOCHA ZA SIMU ZA MAMILIONI YA FEDHA

Na Pardon Mbwate wa Jeshi la Polisi, Kigoma.
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu 52 kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ujambazi wa kutumia silaha na wizi wa vocha za simu za mkononi zenye thamani ya karibu shilingi milioni 63.2.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amesema kuwa watuhumiwa 21 wamekamatwa katika wilaya ya Kigoma mjini, watuhumiwa 18 wamekamatwa katika wilaya ya Kasulu na wengine 13 katika wilaya ya Kibondo.
Amesema watuhumiwa wote hao wamekamatwa katika Operesheni maalum inayoendelea katika wilaya zote za mkoa huo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupambana na vitendo vya kihalifu vikiwemo vya ujambazi wa kutumia silaha, utekaji wa magari na uporaji wa mizigo na fedha za abiria.
Kuhusiana na wizi wa vocha za simu, Kamanda Kashai amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Itochiman Sebeha (27), mkazi wa Katubuka mjini Kigoma ambaye alikuwa ni msimamizi na mfanyakazi wa Kampuni ya Shivacom iliyopo chini ya Kampuni ya Simu za mkononi ya VODACOM mkoani humo.
Amesema kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na taarifa zilizokuwa zikikusanywa na Makachero wa Polisi mkoani humo waliokuwa wakifuatilia nyendo za mfanyakazi huyo ambapo mara baada ya kumtia nguvuni, Polisi waliwasiliana na uongozi wa Kampuni ya Shivacom Jijini Da es Salaam ambapo walitumwa wakaguzi wa mahesabu mkoani humo na kubaini kuwa fedha za vocha za milioni 63,199,000 za kampuni hiyo zilikuwa hazijapelekwa benki na hazijulikani zilipo.
Hata hivyo Kamanda Kashai amesema kuwa wakati wa ufuatiliaji wa nyendo za mtuhumiwa huyo, Makachero wa Polisi mkoani Kigoma wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Kigoma mjini ASP Mohammed Kilonzo, walifanikiwa kupata maboksi mawili yaliyojaa vocha za Vodacom yakiwa yamefichwa porini jambo ambalo limewaongezea mashaka katika ufuatiliaji wa nyendo za mtuhumiwa huyo.
Baada ya kuyafanyia ukaguzi maboksi hayo, Makachero hao walibaini kuwa yalikuwa na vocha mchanganyiko za Kampuni ya Simu za Mkononi ya VODACOM zikiwemo za shilingi 5,000 kwa kila moja, shilingi 2,000 shilingi 1000 na shilingi 500.
Baada ya kuwasili kwa maafisa wa Kampuni ya Shivacom mkoani Kigoma wakitoka Makao Makuu ya Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam, walibaini kuwa maboksi hayo pamoja na vocha hizo, zilikua ni sehemu ya zile alizopewa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya kuwasambazia wauzaji wa vocha za jumla mkoani Kigoma.
Kamanda huyo amesema bado Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba pamoja na mambo mengine, pia wanashirikiana na wenzao wa Uhamiaji ili kubaini uhalali wa uraia wa mtuhumiwa huyo.
Kamanda Kashai amesema kuwa watuhumiwa wengine 18 walikamatwa Wilayani Kasulu kwa tuhuma mbalimbali na wengine wawili, mmoja alikamatwa na kiasi kikubwa cha pombe haramu ya gongo na Bangi na mwingine anashikiliwa kwa tuhuma za kuingia nchini isivyo halali.
Katika Wilaya ya Kibondo Polisi wamekamata watuhumiwa 13 kwa makosa mbalimbali ambapo watatu kati yao wanatuhumiwa kwa kuingia nchini isivyo halali na wengine kumi wanashikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya unyang’anyi  wa kutumia silaha na utekaji wa magari ya abiria.
Bangi iliyokamatwa
Kamanda Fraisser Kashai, amewambia waandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Upelelezi wa matukio hayo unaendelea na kwamba baadhi ya washtakiwa hao wanaweza kufikishwa mahakamani Jumatatu kujibu tuhuma zao.
Hata hivyo Kamanda Kashai amewaomba wananchi kuendelea na juhudi za kutoa taarifa Polisi kila wanapobaini kuwepo kwa vitendo vya kihalifu ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu hutuma zinazowakabili.
        
Mhina Zanzibar 0784 886488/ 0715 886488/ 0767 886488

KINYWAJI BORA CHA GRAND MALT SASA KATIKA CHUPA

Aug 18, 2011Na Mwandishi Wetu
Kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt kinachotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambacho kimekuwa kikipatikana katika kopo, sasa kitapatikana pia katika chupa la  mililita 330.
      Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt imezindua chupa mpya ya aina yake yenye ujazo wa mililita 330 katika kiwanda chake cha Dar es Salaam leo.
      Grand Malt imekuwa ikiuzwa kwenye kopo zenye ujazo wa mililita 330 lakini kuanzia jana, itapatikana pia kwenye chupa mpya itakayouzwa sh 1000 kwa chupa na sh 20,000 kwa katoni kwa bei ya reja reja.
      “Chupa hii mpya itaziba pengo katika soko na kukifanya kinywaji hiki kupatikana kwa urahisi,” alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TBL  David Minja huku akisisitiza kuwa kinwaji hicho bado kitapatikana kwenye kopo pia.
       Alisema Grand Malt ilizinduliwa Aprili mwaka jana lakini kwa sasa ni kinywaji namba moja kisichokuwa na kilevi Tanzania. “Tunawashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kukikubali kinywaji hiki na kukifanya kiwe namba moja. Tunawahakikishia kuwa kitakuwepo sokoni muda wote ili kuendelea kuwaburudisha watanzania,” alisema Minja.
      “Tunapozindua kinywaji hiki leo, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa kinywaji kitakachouzwa kwenye chupa ni sawa na kile ambacho kinauzwa kwenye kopo, ambacho kina vitamini na mchanganyiko wa maziwa ya aina yake,” alisema Minja.
      Meneja wa Grand Malt Consolata Adam alisema, “Grand Malt ilizinduliwa Tanzania mwaka jana na leo tunapozindua chupa hii mpya, tunawashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono.”
       Alisema kinywaji hicho kimetokea kuwa bora kwa sababu ya ladha yake nzuri inayoifanya inyweke kirahisi kwa kuwa ina vitamini, laktosi yenye ladha nzuri, inayoitofautisha na malt zingine sokoni.
      “Kinywaji hiki kinawafaa wafanyakazi wenye shughuli nyingi lakini pia kinafaa kwa matumizi ya nyumbani, wafanyakazi wa usiku, wanafunzi, vikao vya kibiashara na sherehe nyinginezo,” alisema Consolata.
         Alisema TBL itaendelea kukitangaza na kusambaza kinwaji hiki na kuhakikisha kinawafikia watanzania wengi zaidi popote walipo.
Viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakigonganisha chupa za Grand Malt katika uzinduzi wa kinywaji hicho leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Editha Mushi, Meneja wa Grand Malt Consolata Adam na Meneja Masoko wa kinywaji hicho, Fimbo Butala

SIMBA YAIFANYA MBAYA YANGA: YAICHAPA MBILI KAVU

Aug 17, 2011

Nahodha wa Simba, Juma Kaseja na wachezaji wengine wa timu hioyo wakifurahia Ngao ya Hisani, iliyotwaliwa na timu hiyo baada ya kuixchapa Yanga 2-0, katuika mechi iliyomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

YANGA NA SIMBA KATIKA VITA VYA NGAO YA HISANI LEO TAIFA

NA MWANDISHI WETU
Miamba ya soka yenye mashabiki wengi hapa nchini, Yanga na Simba  leo wanaingia vitani  tena kusaka heshima zao zitakapovaana katika mchezo wa maalumu wa Ngao ya Jamii uliopangwa kuchezwa kuanzia saa 2 usiku kwenye Uwanja wa kisasa wa Taifa, Dar es Salaam.
       Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa pazia la michuano ya Ligi Kuu soka Tanzania lililopangwa kufunguliwa Agosti 20, ambapo timu 14 za Tanzania Bara zitachuana kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Yanga iliyotwaa msimu uliopita.
       Pambano hilo la kukata na shoka, limepangwa kuanza saa 2.00 usiku ili kutoa fursa kwa waumini wa dini ya kiislamu waliopo katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kupata muda mzuri wa kufuturu kabla ya kwenda uwanjani kushuhudia mtanange huo.
      Msimu uliopita Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Simba mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti mchezo uliopigwa Agosti 18, kwenye uwanja huo baada ya miamba hiyo kutoka suluhu katika muda wa kawaida.
      Mbali na kupata matokeo hayo mazuri, Yanga itashuka uwanjani ikiwa na morari kubwa ya kuendeleza ubabe kwa mahasimu wao baada ya kushinda mchezo uliozikutanisha mara ya mwisho katika mechi ya fainali ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) Julai 10, walioshinda bao 1-0 lililofungwa na Kenneth Asamoah dakika 108.
     Mchezo wa Ngao ya Jamii utakuwa na changamoto kubwa, Yanga itashuka dimbani ikiwa na nia ya kuendeleza furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo kutoka makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani na 'Wekundu wa Msimbazi' bila shaka hawawezi kukubali kulala mapema kwa kupoteza mchezo huo ambao kocha Moses Basena, ameapa vijana wake watafia uwanjani.
      Timu zitakazoshiriki Ligi hiyo  ni Yanga, Simba, Azam FC, African Lyon, Villa Squad, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Toto African, Polisi Dodoma, Coastal Union, Moro United na JKT Oljoro. Jumla ya sh. bilioni 1.2 zinazotolewa na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom zinatarajiwa kutumika.
     Macho na masikio ya mashabiki wa klabu hizo zenye utani wa jadi, ni kushuhudia nyota wa kimataifa wakiwemo wapya watakavyoonyesha uhodari wa kucheza soka baada ya kusajiliwa kwa mamilioni ya fedha kutoka katika klabu zinazotamba katika medani ya soka barani Afrika.
     Yanga ilifanya kufuru baada ya kumng'oa kwa nguvu nahodha na 'injini' ya APR ya Rwanda, Haruna Niyonzima 'Fabregas' na mfungaji bora wa ligi ya Uganda, Hamis Kiiza kutoka URA na Asamoah ambao viwango vyao vya uchezaji vimekuwa gumzo nchini. 'Mapro' wengine ni kipa Yaw Berko na Davies Mwape.
       Kocha Mganda kama alivyo Basena, Sam Timbe anatambia vijana wengine waliopo kwenye viwango bora akiwemo kiungo aliyecheza vizuri msimu uliopita, Nurdin Bakari, Nadir Haroub 'Cannavaro', Chacha Marwa, Godfrey Taita, Julius Mrope, John Tegete na nahodha Shadrack Nsajigwa.
      Hata hivyo, Yanga huenda ikamkosa Kiiza aliyetimkia nyumbani kwao Uganda kwa madai kuwa ana matatizo ya kifamilia ingawa uongozi wa klabu hiyo umemkana na kudai mchezaji huyo anasumbuliwa na utoto.
     Kukosekana kwa Kiiza ni pigo kwa Yanga katika safu ya ushambuliaji kwani mchezaji huyo amekuwa kipenzi cha mashabiki kutokana na uhodari wake uwanjani kulinganisha na Mwape au Asamoah.
    Simba kwa upande wao walijibu mapigo kwa kumsajili mfungaji mabao wa kimataifa Mzambia, Felix Sunzu, Gervas Kago (Jamhuri ya Afrika ya Kati), Jerry Santo na Emmanuel Okwi ambao kimsingi wameonyesha uwezo mkubwa tangu walipojiunga na kigogo hicho.
     Timu hiyo imemrejesha beki wa kati hodari aliyekuwa akicheza soka ya kulipwa nchini Msumbiji Victor Costa 'Nyumba' na winga msumbufu uwanjani Ulimboka Mwakingwe na beki Said Nassoro 'Cholo'. Nyota wa zamani ni kipa Juma Kaseja, Kevin Yondan, Salum Kanoni na Juma Said 'Nyoso'. 
     Mchezo huo utakuwa wa kihistoria kwa Yanga na Simba ambazo muda mrefu zimekuwa zikitambiana kwa kila mmoja kuvutia upande wake akijinadi kuwa amefanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha anawapa raha mashabiki wake kwa kutoka uwanjani kifua mbele dhidi ya mpinzani wake.
   Miamba hiyo inavaana ikiwa imetokea katika maumivu baada ya kuboronga katika mechi zao za mwisho za maandalizi. Yanga ilikuwa Khartoum, Sudan ambapo ilichapwa jumla ya mabao 6-2, ilifungwa mabao 3-1 kwa kila mchezo katika mechi mbili ilizocheza na El Hilal inayonolewa na kocha wa zamani wa timu hiyo, Sredojevic Milutin 'Micho'.
       Simba ilionja shubiri na kuliona tamasha la 'Simba Day' kuwa chungu baada ya kulazwa bao 1-0 na Victors ya Uganda katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha kabla ya kulazimishwa suluhu na AFC Leopards ya Kenya.
        Matokeo hayo yametia shaka kwa mashabiki wa klabu hizo, ingawa ukweli unabaki pale pake kwamba zinapocheza timu hizo, mtoto hatumwi dukani kwani kila mmoja anacheza kwa nguvu zote ili kuhakikisha anapata matokeo mazuri ili kulinda heshima.
       Tayari hofu imetanda kwa mashabiki wa klabu zote mbili kutokana na historia ya timu hizo zinapocheza ambapo bendera za rangi ya njano na kijani kwa upande wa Yanga, nyeupe na nyekundu kwa Simba zinatawala sehemu kubwa mitaani.
Kumbukumbu muhimu
Rekodi za Yanga na Simba kuanzia mwaka 2000. Agosti 5, Yanga ilishinda mabao 2-0 yote yakifungwa na Iddi Moshi, aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza tangu ametoka kwenye fungate la ndoa yake.
Mechi iliyofuata Septemba 1, 2001, bao pekee la Joseph Kaniki ‘Golota’ alilofunga dakika 76 liliwalaza mapema Yanga.
Sekilojo Chambua, aliinusuru Yanga kulala tena mbele ya Simba Septemba 30, 2001 baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika 86, Kaniki alifunga kwa upande wa Simba dakika 65 na timu hizo zilitoka sare bao 1-1.
Agosti 18, 2002, Chambua aliikoa Yanga baada ya mwamuzi Victor Mwandike kutoa penalti dakika 89 na miamba hiyo kutoka sare bao 1-1 baada ya Madaraka Selemani Mzee wa Kiminyio kutangulia kufunga dakika 65. Novemba 10, 2002 timu hizo hazikufungana. 
Septemba 28, 2003 mabao ya Kudra Omary na Herry Morris yaliinusuru Yanga kulala 2-0 mbele ya Simba, kufuatia Emmanuel Gabriel kufunga dakika za 27 na 36. Novemba 2, 2003 hazikufungana.
Agosti 7, 2004, Shaaban Kisiga alitangulia kuifungia Simba dakika 64, kabla ya Pitchou Kongo kusawazisha dakika 48 na Mwakingwe alifunga la ushindi 76. Simba ilishinda mabao 2-1.
Simba iliifunga Yanga bao 1-1 Septemba 18, 2004 kwa bao pekee la Athumani Machupa dakika 82.
Aprili 17, 2005 Aaron Nyanda alitangulia kuifungia Yanga dakika 39, kabla ya Nurdin Msiga kusawazisha dakika 44 na Machupa kufunga la pili dakika 64. Simba ilishinda mabao 2-1.
Agosti 21, 2005, Nicodemus Nyagawa alikuwa nyota wa mchezo kwa kufunga mabao yote mawili yaliyoipa Simba ushindi wa 2-0. Mwaka 2006, timu hizo hazikufungana katika mechi zote mbili za ligi.
Mwishoni mwa mwaka 2006 katika fainali ya Ligi Ndogo Tanzania Bara, Moses Odhiambo alitangulia kuifungia Simba kwa mkwaju wa penalti dakika ya pili ya mchezo kabla ya Said Maulid ‘SMG’ kusawazisha dakika 55. Simba ilishinda kwa penalti 5-4.
Oktoba 24, 2007 ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Mwakingwe dakika 23.
Aprili 27, 2008 zilitoka suluhu, lakini Oktoba 26, 2008, Ben Mwalala alifunga bao dakika 15. Yanga ilishinda bao 1-0. Aprili, 2009 zilitoka sare mabao 2-2. Katika mchezo wa ligi msimu 2009/2010 Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Musa Hassan 'Mgosi' na ziliporudiana Aprili ilishinda 4-3.
ยช