.

MATUKIO MBALIMBALI SAFARI YA MISS VODACOM TANZANIA 2011, SALHA ISRAEL KUELEKEA FAINALI ZA MREMBO WA DUNIA

Oct 31, 2011

Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa kwanza kushoto akiwa katika Vazi la Ufukweni na Wenzake katika maonesho ya Mavazi hayo hapo jana.
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Kumi kutoka kulia akiwa na wenzake katika Dina la nguvu Huko Scottish maeneo ya Scottish Hydro.
Miss Vodacom Tanzia 2011 Salha Israel  aliye vaa Nguo za Njano katika Mazoezi  ya nguvu kabisa wakati wa maandalizi ya shindano la Miss World Tanzania
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa pili kutoka kulia akiwa Edinburgh Castle hivi karibuni katika safari ya kuelekea katika mashindano ya kumsaka Mrembo wa Dunia.
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Pili kutoka kulia akiwa anapiga Chiazi  na wenzake .. katika safari  ya kuelekea kumtafuta Mrembo wa Dunia.
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa kwanza kushoto aliye simama akiwa katika picha ya pamoja na wenzake
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Tatu  kutoka kulia akifurahia kwa Shangwe wakati wa  Highland Games kuelekea kinyang'anyiro cha Mrembo wa Dunia (Kwa picha zaidi Tembelea: www.fredynjeje.blogspot.com )

MATUKIO KATIKA PICHA: MKUTANO NA WANAJUMUIA WA TANZANIA HOUSTON NA NAPE

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza katika mkutano na wanajumuia ya Watanzania mjini Houston, Marekani. Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu, Itikadi na Uenezi Sixtus Mapunda na wengine ni viongozi wa CCM tawi la Houston
Six akijitambulisha kwa wanajumuia hao

Wanajumuai wakiwa kwenye mkutano huo

Wanajumuia wakimskiliza Nape kwa makini alipozungumza nao

Nape na Six wakiwa na kiongozi wa wanajumuia hao

Nape akaiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM tawi la Houston na wanajumuia wengine waliohudhuria mkutano huo
Wkawa katika mapozi mbalimbali kama hivi

Nape akimbeba mtoto wa kiongozi wa tawi la CCM la Houston baada ya kupigapicha ya pamoja

Viongozi wa CCM wa tawi la HoustonMKUTANO WA CHOGM WAMALIZIKA AUSTRALIA, JK ALONGA

Oct 30, 2011

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Afrika imeridhishwa na msimamo wa Jumuia ya Madola kuendelea kuhakikisha kuwa suala zima la maendeleo linabakia sehemu ya ajenda kuu ya Jumuia hiyo.
“Sisi wanachama wa Jumuia ya Madola kutoka Afrika, na kwa hakika Bara zima la Afrika, tumeridhishwa na yaliyojadiliwa na kukubaliwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola ya Madola (CHOGM) mwaka huu kuhusiana na umuhimu wa suala zima la maendeleo,” Rais Kikwete amesema kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kufunga mkutano wa CHOGM mwaka huu mjini Perth, Australia.
Rais Kikwete alikuwa mwakilishi na msemaji wa nchi wanachama wa Jumuia ya Madola kutoka Afrika kwenye mkutano huo wa waandishi wa habari ambako amejiunga na Waziri Mkuu wa Australia, Mama Julia Gillard ambaye alikuwa mwenyeji wa CHOGM mwaka huu na mwenyekiti mpya wa Jumuia hiyo.
Viongozi sita wamehutubia mkutano huo wa waandishi wa habari wengine wakiwa Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago Mheshimiwa Kamla Persad-Bissessar ambaye ndiye mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Waziri Mkuu wa Visiwa vya Samoa Mheshimiwa Tuilaepa Lupesoliai Sailele Malielegaoi, Rais wa Visiwa vya Maldives Mheshimiwa Mohamed Nasheed na Katibu Mkuu wa Jumuia, Mheshimiwa Kamaleshi Sharma ambaye ameongezewa kipindi kingine cha miaka minne cha kuongoza Jumuia hiyo kwenye CHOGM ya mwaka huu kuanzia Aprili mwakani.
Rais Kikwete amesema kuwa nchi za Afrika na zile zote zinazoendelea ndani ya Jumuia ya Madola zimeridhishwa na msimamo wa CHOGM wa kuibakiza ajenda ya maendeleo kwenye ajenda kuu ya Jumuia hiyo.
Rais Kikwete alikuwa ameulizwa kama nchi masikini zaidi na ndogo zaidi ndani ya Jumuia zimemeridhishwa na ajenda zilizowekewa mkazo katika CHOGM ya mwaka huu na hasa ajenda ya maendeleo.
Rais amesema kuwa ajenda ya maendeleo lazima iendelee kubakia ajenda kuu ya Jumuia ya Madola kwa sababu sehemu kubwa ya wanachama wa Jumuia hiyo ni nchi masikini na zinazoendelea.
Kwenye mkutano huo, viongozi hao wameelezea mambo makubwa yaliyokubaliwa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na kufanya mageuzi makubwa ndani ya Jumuia hiyo kuhakikisha kuwa Jumuia hiyo inabakia taasisi yenye nguvu, yenye kutumikia kiasi cha kuridhisha mahitaji ya nchi wanachama wake na yenye uwezo wa kupambana na changamoto za karne ya 21.
Moja ya mageuzi yaliyokubaliwa yafanyike ni pamoja na kuimarisha kundi la kusaidia utendaji ndani ya Jumuia ambalo linaundwa na mawaziri la Commonwealth Ministerial Action Group (CMAG) na Tanzania imeteuliwa kuwa katika kundi hilo kwa miaka miwili ijayo.
Mbali ya Tanzania, nchi nyingine zitakazounda CMAG kwa miaka miwili ijayo mpaka mkutano ujao wa CHOGM ni Australia, Bangladesh, Canada, Jamaica, Maldives, Sierra Leone, Trinidad na Tobago na Vanuatu.
Viongozi hao wamesema kuwa katika CHOGM ya mwaka huu viongozi wa Jumuia ya Madola wamekubaliana kuendelea kutetea, kulinda na kudumisha misingi mikuu ya Jumuia hiyo ambako viongozi wamepitisha ma kukubali mapendekezo 30 kati ya 105 yaliyopendekezwa na Kundi la Watu Maarufu (Eminent Persons Group) wa Jumuia hiyo.
Viongozi hao pia wamewaambia waandishi wa habari kuwa CHOGM imekubaliana kuelekeza nguvu zaidi kwenye mahitaji ya maendeleo ya nchi wanachama ambako suala la usalama wa chakula litatiliwa mkazo mkubwa.
Waziri Mkuu Gillard ambaye ameongoza mkutano huo wa waandishi wa habari amesema pia kuwa CHOGM imekubaliana  kushirikiana na washirika wa kimataifa wa Jumuia ya Madola katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo makubwa ya kiuchumi yanayoikabili dunia kwa sasa.
Mama Gillard pia amesema kuwa viongozi wamekubaliana kuongeza nguvu zao katika kutafuta usawa wa jinsia na kuwasaidia vijana kuwa na sauti kubwa zaidi ndani ya Jumuia hiyo.
Aidha, amesema kuwa viongozi wa Jumuia ya Madola wamekaribisha nia ya Sudan Kusini kutaka kujiunga na Jumuia na wametaka Makao Makuu ya Jumuia ya Madola kufuatilia suala hilo.
Pia, Mama huyo amesema kuwa wakuu wa CHOGM wameridhishwa na mazingira yanayojengeka kutaka kuikaribisha tena Zimbabwe kwenye Jumuia hiyo na wamezipata pande zote nchini humo kuendelea kutekeleza makubaliano ya kuleta maridhiano nchini humo ya Global Political Agreement (GPA).
Waziri Mkuu huyo pia amesema kuwa CHOGM imekubaliana kumpongeza Mkuu wa Jumuia ya Madola, Malkia Elizabeth wa Uingereza, kwa kufikisha miaka 50 ya uongozi wake wa Jumuia mwaka ujao. CHOGM imekaribisha wazo la kuanzisha taasisi iitwayo Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust ambayo kazi yake kuu itakuwa kugharibia miradi ya kibinadamu kama vile maradhi, kuendeleza elimu na utamaduni na shughuli nyingine za kipaumbele za Jumuia ya Madola.
Mama Gillard pia amewaambia waandishi wa habari kuwa CHOGM imeridhia kuwa mkutano wake ujao ufanyike Sri Lanka mwaka 2013,  unaofuata ufanyike Mauritius mwaka 2015, na unaofuata ufanyike Malaysia mwaka 2019.

WAPIGAPICHA NA WAKUU WA VYOMBO VYA HABARI WA ENZI ZA MWALIMU NYERERE

.BAADHI YA WAPIGA PICHA TOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI NCHINI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BABA WA TAIFA MWL. NYERERE WAKATI WA KUMUAGA BAADA YA KUSTAAFU URAIS IKULU JIJINI DAR ES SALAAM 1985. WALIOSIMAMA TOKA KUSHOTO MAX MADEBE (MFANYAKAZI), SAM MMBANDO(SHIHATA), VINCENT URIO, (DAILY NEWS), JOHN MAKWAIA (MAELEZO), MZEE SILEN(AVI), JUMA DIHULE(SHIHATA), ADINAN MIHANJI (SHIHATA) NA KIYUNGI WA KIYUNGI (MAELEZO). WALIOCHUCHUMAA WAPILI TOKA KUSHOTO,CHARLES KAGONJI (MAELEZO), GERVCE MSILLO (DAILY NEWS), MWANAKOMBO JUMAA (MAELEZO), KHATIBU ALLY (UHURU) NA RAPHAEL HOKORORO (MAELEZO).
BAADHI YA VIONGOZI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MWL. NYERERE SIKU  YA KUMUAGA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA KUSTAAFU MWAKA 1985. KUSHOTO NI DAVID WAKATI (RTD),NYUMA YA MWL. NI MZEE SAILEN (AVI), GERVACE MSILO (DAILY NEWS, ADINAN MIHANJI (SHIHATA) NA KIYUNGI WA KIYUNGI (MAELEZO) Picha na: www.latestnewstz.blogspot.com

NAPE ATEMBELEA TAWI LA CCM HOUSTON-TEXAS

Oct 29, 2011

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (Katikati), akizungumza na viongozi wa CCM tawi la Houston, Texas alipotembelea tawi hilo akifuatana na Katibu Msaidizi Mkuu, Itikadi na Uenezi Sixtus Mapunda leo.
Nape na Sixtus wakiwa na viongozi wa CCM tawi hilo
Nape na Situs wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM ya tawi hilo la Houston-Texas leo, Nape na Six wapo nchini Marekani kwa ajili ya kozi fupi ya masomo ya uongozi katika chuo kimoja nchini humo

MATUMLA, MIYAYUSHO WAPIMA UZITO LEO KWA AJILI YA MPAMBANO KESHO

Na Mwandishi Wetu
Mabondia Mbwana Matumla 'Golden Boy' na Francis Miyayusho 'Chichi Mawe' leowamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Ubingwa utakaofanyikakatika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam kesho jumapili OKCTOBA30.

wakizungumzawachezaji hawo kwa wakati tofauti baada ya kupima wamesema wapo tayarikuonesha mchezo mzuri wa ngumi na kuwapa raha zisizo na kifani kwasababu akuna kisingizio chochote kile kwa kua tumejiandaa vya kutosha

Lichaya mabondia hawo kupima uzito pia wamepima vipimo mbalimbali ususaniUkimwi, Mkojo kwa ajili ya kuangalia kama mabondia hao kama wanatumiamadawa ya kuongeza nguvu.

Pambano hilo kubwa litakuwa la 12 la uzito wa Bantam, ambapo kabla ya mpambano kutakua na mapambano mengine ya utangulizi.

Mapambanohayo ya kati ya Juma Fundi na Fadshili Majia, Mohamed Matumla naRamadhani Mashudu, Issa Sewe atazidunda na Ramadhani Shauli wakati kwaupande wa ngumi za wanawake Asha Nzowa (Asha Ngedere) atazichapa naSalma Kihobwa (mwajuma Ndalandefu)

Katika Mchezo huo kutakua naDVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zakembalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo RajabuMhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbalimbinbu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super Dalisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanawezakutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja namashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambanokama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye,MOhamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zakeMarekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katikamchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi manazinafundisha mambo mengi '' alisema Super D;

Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
 Mob;+255787 406930
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

MALKIA WA UINGEREZA AMKARIBISHA MNUSO JK

Malkia Elizabeth II wa Uingereza na Mumewe Philip Wakiwakaribisha Rais Dkt.Jakaya Kikwete, Mama Salma na wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola katika dhifa aliyoiandaa kwaajili ya viongozi hao wanaohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Perth,Australia(picha na Freddy Maro)

JK AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA NA RAIS KIBAKI WA KENYA

Waziri Mkuu wa Australiua Julia Gillard mjini Perth wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Madola unaoendelea mjini Perth, Australia(picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Kenya Mwai Kibaki wakati wa mkutano wa wakuu wa Ncxhi za Jumuia ya Madola Perth, Australia,(photo by Freddty Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakisalimiana

MALIKIA AHUTUBIA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIA YA MADOLA LEO

Oct 28, 2011

Malkia Elizabeth II wa Uingereza akihutubia wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola jijini Perth, Australia leo asubuhi(picha na Freddy Maro)
Malikia akiwa katika picha ya pamoja na viongozi hao baada ya kuwahutubia

WAJIBU WA KULINDA AMANI NI WETU SOTE TUSIBAGUANE-TANZANIA

Walinzi wa amani wa UN wakiwa Darfur ya Kaskazini.

Na Mwandishi Maalum
New York

Tanzania imeitaka Idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya ulinzi wa amani (UNDPKO), kutoendekeza dhana inayotaka kuota mizizi ya kuwa, kuna nchi ambazo jukumu lake  ni kutoa walinzi wa amani kwa upande mmoja, na kuna nchi ambazo jukumu lake ni kutoa raslimali fedha na vifaa kwa upande mwingine.
Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa,   Ombeni Sefue, wakati wa mkutano wa Kamati Maalum ya 34 ya Opereshani za Ulinzi wa Amani (C34).  kamati  hiyo  ni sehemu ya   Kamati  ya Nne ya Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa. Mkutano huo ulikuwa ukijadili   ajenda namba 54 inayohusu dhana nzima ya ulinzi wa amani.
Kamati ya nne ni kati ya kamati sita za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kamati hiyo inahusika   pamoja na mambo mengine, masuala ya siasa na umalizaji ukoloni  na operesheni za ulinzi wa amani na vilevile masuala ya Habari.
 Balozi Sefue amesema, kuna   kila dalili ndani  Umoja wa Mataifa, za kutaka  kujengeka kwa mazingira ya  kubaguana kati ya nchi  zile zinazojiita wachangiaji wakubwa wa askari na zile zinazojiita wachangia wakubwa wa raslimali zikwamo fedha.
“Ningependa kusisitiza mambo kadhaa, ambayo ujumbe wangu unaamini ni ya msingi  na yanatakiwa kuzingatiwa. Kwanza tunahitaji kupanua wigo wa kuchangia   walinzi wa amani. Na tuachane na dhana inayotaka kujengekea ya kwamba kuna nchi ambazo jukumu lao ni kuchangia askari,kwa upande na wengine  jukumu lao ni kuchangia raslimali.  Hii ni dhana potofu na si sahihi.   Jukumu hili adhimu ni  wajibu wetu sote”. Akasisitiza Balozi Ombeni Sefue.
Takwimu zinaonyesha kuna walinzi wa amani  120.000 wanaume na wanawake, wanaotekeleza majukumu  yao katika misheni mbalimbali. Idadi kubwa ya wanajeshi hao wakiwamo askari polisi wanatoka katika   nchi za Afrika ,  Asia na baadhi ya nchi za   Mashariki ya Kati.
 Tanzania   inashika nafasi  ishirini  miongoni mwa katika kundi la nchi zinazotambuliwa kama wachangiaji wakubwa. Aidha Naibu Kamanda wa vikosi vya kulinda amani huko Darfur ni Mtanzania, Meja Jenerali Wynejones Kisamba. 
Aidha  Balozi Ombeni Sefue ameitaka pia  Idara hiyo ,  kutoa tafsiri sahihi kuhusu baadhi ya majukumu  wanayopewa  walinzi wa amani.
Akatoa mfano kwa kusema,  jukumu lijulikanayo kama ya Robust Peacekeeping ni moja ya  jukumu jipya  ambalo  licha ya kwamba utekelezaji wake ni tata lakini hata  tafsri yake yaijaeleweka miongoni  mwa walinzi wa amani.
Akasema   kama hapatolewa tafsiri sahihi  ya jukumu hilo na namna ya kulitekeza, inaweza kujenga mazingira ya mkanganyiko na hivyo kuhatarisha mfumo mzima wa utekelezaji wa  amri  na udhibiti katika eneo la  husika. “ kwa kweli hili ni jambo la mwisho  kutarajiwa na walinzi wa amani na makanda wao  ” akasisitiza Balozi.
Suala lingine ambalo Tanzania imetaka lipewe umuhimu ni usalama wa walinzi wa amani.
Akasema   usalama wa walinzi hao   ambao wanatekeleza majukumu yako katika mazingira magumu na hatari, unatakiwa kuratibiwa ipasavyo.
“ Lazima tuhakikishe walinzi wetu wa amani kwanza,  wanakuwa salama wao wenyewe ,wanapewa vifaa  zikiwamo Helkopta. Na kwamba  majukumu yako yanatambulika na  yameratibiwa vizuri ” akasitiza Sefue.
Taarifa kutoka Idara hiyo ya Operesheni za Ulinzi wa Amani, zinaonyesha kwamba jumla ya walinzi wa amani  86 wamepoteza maisha kwa mwaka huu peke yake  na  kati  hao  29 ni raia.
Kuhusu marejesho ya malipo kwa nchi zinazochangia walinzi wa amani pamoja na vifaa, Balozi Ombeni Sefue amesema, Tanzania  inakaribisha wazo la kuundwa kwa Jopo la washauri ambao watalifanyia kazi suala la marejesho ya malipo.
Hata hivyo akasema ni matarajio ya Tanzania kwamba, ushauri wowote utakaotolewa na  Jopo hilo utakuwa jumuishi.
Suala jingine ambalo pia lilichangiwa na wazungumzaji wengi. Lilihusu jukumu la kulinda raia wakati wa machafuko  (Protection of Civilians).
Akiizungumzia jukumu hilo,   Balozi wa Zimbabwe katika Umoja wa Mataifa,Chitsaka Chipaziwa. Amesema kama iliyokuwa kwa  jukumu la Robust Peacekeeping.  Jukumu ulinzi  wa rais pia bado lina utata na utekelezaji wake pia .
“ Hivi tunapozungumzia jukumu la ulinzi wa raia,  je ni kweli walinzi wetu wanaelewa vema namna ya utekelezaji wake?. Ni wiki iliyopita tu tulionyeshwa hapa namna gani jukumu hilo linatakiwa kuingizwa katika mitaala ya ufundishaji. Lakini tayari walinzi wetu walishaanza kulitekeleza jukumu hili.  Kwa hiyo ni nini kinachoanza, mafunzo kwanza au utekelezaji kwanza mafunzo baadaye”. Akahoji Balozi wa Zimnbabwe.
Akafafanua zaidi kwa kusema pale ambapo jukumu hilo la kulinda raia lisipotekelezwa ipasavyo wanaolaumiwa ni nchi zinazochangia walinzi wake . Ili hali hapakuwa na muda wa kutosha kwa walinzi wetu kujifunza na kulielewa vema jukumu hilo.
mwisho   

NAPE ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape  Nnauye akimsalimia Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mwanaidi Maajar, alipofika katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Washington, DC. Kulia ni Ofisa Ubalozi huo Suleiman Saleh na Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu, Itikadi na uenezi CCM, Sixtus Mapunda.
Kisha Nape na Sixtus wakawa na mazungumzo na balozi Majaar
Nape akisalimiana na Ofisa Ubalizi Kitengo cha Uhamiaji Abbas Misana
 Sixtus Mapunda akisalimiana na Ofisa huyo
Nape akimsalimia Ofisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, Edward Masanja baada ya kusalimiana na Balozi msaidizi Marekani na Mexico Mama Mnanka (katikati).
Nape akimsalimia Ofisa Ubalozi Agnes Lusinde (Source: Issamichuzi Blogspot.com)

NAPE AND SIXTUS AT LEADERSHIP INSTITUTE WASHINGTON DC

Oct 27, 2011
NOW VODACOM ( T) BRINGS YOU AN INTERNET ACCESS IN YOUR LIVING ROOM

Dear Tanzanians,                                                                                                  
Now Vodacom Tanzania brings you an internet access in your living room, a reality with Vodafone WebBox. “The 21st century is all about science and technology, anyone not connected to the internet is left behind. However here at Vodacom, we are at the forefront of enabling people to get connected to the world of internet in a manner which is smart and very affordable. This initiative will greatly increase opportunities for people to communicate and even enhance the way they do business” said Nector Foya Head of Corporate Affairs-Vodacom Tanzania. The Vodafone WebBox is specifically developed for customers in the emerging markets in which technology and high costs of equipment restrict many from enjoying affordable and reliable internet access.
It’s a great relaxed service, convenient… Vodafone WebBox is plug-n-play keyboard with a built-in EDGE modem and memory card that simply plugs into a television, turning your TV into a computer screen, allowing user to access emails, listen to radio, and open documents and social media in the comfort of your sofa.
All you need is an active SIM with data services activated and ANY TELEVISION SET (old or new, hunch back screen, plasma or LCD, 18 inch to 48 inch) so long as it has an RCA inputs.

KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI

Oct 25, 2011

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini, Liu Xinsheng,  Balozi huyo alipomtembelea Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,  Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.

DK. SHEIN AZINDUA KILIMO CHA MPUNGA 2011-2012

Oct 17, 2011

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwasha Trekta kama ishara ya uzinduzi wa kilimo cha Mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya katika  Mkoa wa  kusini Unguja.(17/10/2011)

WAREMBO WA CHUO KIKUU KUTOANA JASHO JUMAMOSI HII

 Shindano la kumsaka mrembo wa chuo kiu cha Kmpala International University 2011 litarajiwa kufanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Savanna Lounge (quality center) uliopo barabara ya Pugu,jumla ya warembo 12 wamejitokeza kuwania taji hilo siku ya tarehe 22 octoba.
Shindano litapambwa na wasanii wa kizazi kipya kipya Dully sykes,D-nob,Ngoma za asili na vijana wa kutikisika(shers),mabali ya burudani hizo kutakuwa na suprize ya majai pamoja masupastaa wa movie.
Miss Kampala Internationa 2011 imeandaliwa na serikali ya wanafunzi ikishirikana na wadau maarufu wa mabo ya urembo na mitindo nchini Tanzania,tiketi za fainali hizi zinapatikana CLOUDS fM,CHUONI KWAO,JB BELMONT HOTEL,SAVANNA LOUNGE(quality center)kitchen hut (mlimani city) kwa iasi cha 10,000/= (regular) na V.I.P 30,000/=
 Shindano hili limedhaniwa na Savanna Lounge hotel,Belmont hotel,clouds fm,Air Uganda na uniqueentertz blogspot.

WAZIRI NYALANDU ATEMBELEA KIWANDA CHA BAKHRESA KUONA UZALISHAJI CHAKULA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu akizungumza alipotembela kiwanda cha nafaka cha Buguruni Flour Mills, cha Kampuni ya Said Salim Bakhresa & Co Ltd, leo. Kulia ni Meneja Mkuu Msaidizi Saidi Salim Bakhresa & Co Ltd hussein Ally
Nyaladu akionyeshwa moja ya hatua za uzalishaji unga wa ngano katika kiwanda hicho leo. Anayemuonyesha ni Msimamizi wa uzalishaji  wa Kiwanda hicho, Patrick Muriuki.

Oct 16, 2011

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,akiangalia maonesho ya bidhaa mbali mbali za vikundi vya ushirika vya akinamama,katika viwanja vya Salama Bwawani Hoteli,ikiwa ni njia moja ya kuvitangaza vikundi hivi katika mkutano wa Baraza la Biashara la Zanzibar,ZBC uliomalizika jana (Picha na Ikulu Zanzibar)

JAJI MKUU AMFAGILIA JK NEW YORK

* NI KWA KUONGEZA MAJAJI
 Jaji Mkuu, Mhe. Mohamed Chande Othman amempongeza na kumshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa  kuongeza Majaji.


Jaji Mkuu (watano kutoka kushoto katika picha) ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki, wakati alipoutembelea Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na maafisa wa Ubalozi huo (pichani).
Jaji Mkuu Mhe. Chande amesema, uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa kuteua majaji wengi katika Mahakama Kuu ni kielelezo cha namna gani anavyojali utawala wa sheria na anastahili kushukuriwa.
Aidha Jaji Mkuu, amesema uamuzi wa serikali wa kuanzisha Mfuko wa Mahakama kama ilivyo kwa muhimili mwingine wa dola yaani Bunge, ni jambo jema kwa kuwa mfuko huo utasaidia sana katika si, tu uboreshaji wa kazi za mahakama lakini pia katika suala zima la kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kupungunza mrundikano wa kesi.
“Mhe. Rais ametusaidia sana, ameteua majaji wengi katika Mahakama Kuu tena wengi wao wakiwa vijana, hawa watadumu kwa muda mrefu. Tunamshukuru sana kwa hili na ni matumaini yangu kuwa ataendelea na hatua hii ya kutuongeza majaji wengi zaidi” amesema.
Katika mazungumzo yake na maafisa hao, mazungumzo ambayo pia yaliwahusisha maafisa kutoka wizara mbalimbali ambao wapo hapa New York kuhudhuria mikutano ya Kamati za Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, Jaji Mkuu amebainisha kuwa mahakama nchini bado zinakabiliwa na changamoto nyingi.
Amezitaja baadhi ya changamoto hizo ambazo pia zina kwamisha ufanisi na ambazo baadhi zimeanza kufanyiwa kazi, ni pamoja na ile ya kujaribu kutenganisha kazi za kisheria na kazi za kiutawala.
“Kama nilivyosema, tunakabiliwa na changamoto nyingi, zikiwamo hizo za upungufu wa majaji na mlundikano wa kesi,lakini kuna hili la mahakimu kufanya kazi za utawala hasa huko mikoani, hili pia ni tatizo kubwa tumeanza kulifanyia kazi”
Amefafanua kwa kusema , mahakimu wengi wamekuwa wakifanya kazi za utawala kwa mazoea tu, na kwamba hiyo si sahihi na inawapunguzia muda wa kushughulikia kesi.
Akasisitiza kwamba kazi za utawala, za mipango, uhasibu, au uratibu wa raslimali watu ni kazi ambazo zina mafunzo yake, ni kazi za kitaalam.
“ Katika hili mahakimu wetu wanafanya kazi kwa mazoea tu ni mfumo ambao tumeurithi. Tumejipanga kuubadili utaratibu huu, ili mahakimu wafanye kazi za kisheria na watawala wafanye kazi za utawala na mengineyo.
Aidha ameongeza kuwa uongozi wake wake umejipanga pia katika kuboresha utendaji kazi katika mahakama za mwanzo ambako amesema asilimia zaidi ya 75 ya kesi ndiko ziliko
Akizungumzia kuhusu mlundikano wa kesi, Mhe. Jaji Mkuu amesema ingawa kumekuwapo na uboreshaji katika usikilizaji wa kesi na utoaji wa hukumu. Lakini bado kuna mlundikano mkubwa wa kesi ambazo hazijapata hata nafasi ya kusikilizwa .
Akatoa mfano wa Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi ambako amesema kuna kesi nyingi sana ikilinganishwa na majaji waliopo ambao ni wanne tu.
“ Matatizo ya ardhi ni moja ya tatizo kubwa na lenye mlundikano mkubwa wa kesi. Ni kweli kwamba Wizara husika imejitahidi sana katika kupunguza baadhi ya matatizo yakiwamo ugawaji wa viwanja kwa mtu zaidi ya mmoja . Lakini bado mfumo wa wizara hiyo kushughulikia matatizo ya ardhi si mzuri sana. ”
Akasema mfumo wa kushughulikia matatizo ya ardhi unatatiza kwa kuwa matatizo hayo yanaanzia katika ngazi za chini kama vile ngazi za vijiji na kuendelea hadi wizarani. Lakini utatuzi wake wa kisheria unaishia mahakamani.

“Tumejipanga kulitatua tatizo hilo, jambo moja tunalotaka kufanya ni kuifanya Mahakama Kuu kitendo cha Ardhi, mfumo wake uwe kama Mahakama ya Biashara. Kwa kutumia mfumo wa Makahama ya Biashara tunaamini kwamba kasi ya kushughulia kesi za ardhi utaboreka na ufanisi utaongezeka”. Amesisitiza.
Akijibu swali kuhusu mchakato wa maandalizi ya Katiba mpya pamoja na hukumu ya kuyonga.
Jaji Mkuu alikuwa na haya ya kusema. Kuhusu Katiba, kazi ya maandalizi ikiwamo ya kuratibu ukusanyaji wa maoni, pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi inaendelea vizuri na kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pia imeshirikishwa kwa asilimia 100.
Akasisitiza kwamba licha ya mkanganyiko uliojitokeza mwanzoni mwa zoezi hilo, ana imani kubwa na serikali kwa kile alichosema imejipanga vizuri.
Kuhusu hukumu ya kunyonga, Jaji Mkuu amesema kwa Tanzania, kuendelea kuwepo au kutokuwapo kwa hukumu ya kunyoga bado ni mjadala unaoendelea.
Akasema huko nyuma iliwahi kufanyika kura ya maoni kuhusu suala hilo. Matokeo ya kura hiyo yalidhihirisha kwamba bado wananchi walio wengi wanataka hukumu hiyo iendelee , huku idadi kubwa pia ikitaka hukumu hiyo ifutwe.
“kwa upande wa Tanzania, uamuzi wa kuwapo au kuto kuwapo kwa hukumu ya kunyonga bado lina mjadala wa aina yake. Na kwa kweli si kazi ya mahakama kuifuta adhabu hiyo, ni jukumu la chombo kingine ambacho ni Bunge. Lakini pia bado kuna mawazo tofauti miongoni mwa wananchi” akasema Jaji Mkuu.
Hata hivyo akasema kutokana na namna ambavyo mwenendo wa kimataifa umekuwa ukiichukulia hukumu hii ya kunyonga kama utoa kipaumbele  uboreshaji na utendaji kazi wa Mahakama nchini Tanzania

ukiukwaji wa haki za binadamu.Ana uhakika kwamba baada ya miaka kadhaa  nchi nyingi zitakuwa zimeondokana na adhabu hii.
Akasema kuwa ingawa Tanzania inayo na   hii ya kunyonga, lakini utekelezaji wake ni mdogo sana. Kwa mfano akasema Rais wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa na Rais wa awamu ya nne  Jakaya Kikwete hawajawahi kusaini hati za watu kunyongwa.  
Katika hatua nyingine Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Othman Chande amesifu uhusiano mzuri uliopo baina ya mihimili mitatu yaani, serikali, Bunge na Sheria na kwamba angalau hakuna muingiliano kati ya vyombo hivyo.
Katika  mazungumgo yake na Maofisa hao, Mhe. Jaji Mkuu amewapongeza maofisa hao wa Ubalozi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kupeperusha bendera ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, na kwamba utendaji wao wa kazi umeijenga  sifa kubwa Tanzania mbele ya  Jumuia ya Kimataifa.
ยช