.

JAZZ JAM SESSION@LIVINGSTONE WITH CARL WINTHERS AND HIS BAND THE GRAND BEAT

Nov 30, 2011

MAANDAMANO, FUJO NA VURUGU HAVIWEZI KUZALISHA AJIRA-CHEYO

                                                                                       Na Mwandishi Maalum, New York
Maandamano  yasiyokuwa na ukomo na yasiyozingatia utawala wa sheria, vurugu na fujo  zinazofanywa na vijana kwa kisingizo cha kutaka fursa sawa na uwajibikaji, hayawezi kujenga  mazingira ya uzalishaji wa ajira.

Kauli hiyo imetolewa na Mhe. John M. Cheyo  mbunge wa Bariadi Mashariki na mwenyekiti wa  UDP,  wakati alipokuwa akichangia majadiliano kuhusu    fursa na changamoto   za ushiriki wa vijana katika  demokrasia.

Mhe. Cheyo ni kati ya wabunge wawili wanaouhudhuria mkutano wa siku mbili unaoshirikisha  wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani, mkutano huo unafanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, ukiwa umeandaliwa na UN kwa kushirikiana na Chama cha Mabunge ( IPU). Mbunge mwingine kutoka Tanzania anayeshiriki mkutano huo ni Mhe. Betty Machunge

 Akafafanua zaidi  kwa kusema ingawa vijana  wanadai  uwajibikaji zaidi kutoka serikali zao pamoja na fursa za ajira, lakini ajira na fursa hizo haziwezi kupatikana katika mazingira ambayo yametawaliwa na vurugu na maandamano yasiyokuwa na kikomo.

“ Ni kweli wanayo haki ya kudai fursa sawa za kushiriki katika demokrasia na kupata ajira, lakini pia wanatakiwa kukumbuka kwamba wanaowajibu pia wa  kufuata utawala wa sheria na taratibu zilizopo katika kuwasilisha madai yao, kinyume na hapo wanachokifanya si demokrasia” akasititiza  Cheyo.

 Akizungumzia  ushiriki wa vijana katika siasa, Bw. Cheyo amesema bila ya kubadili mifumo ya uchaguzi   ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya makusudi  itakayoongeza idadi ya vijana mabungeni. Vijana wengi hususani  Barani Afrika watabaki kuwa wasindikizaji badala ya kuwa washiriki .

Akasema kuwa vurugu nyingi na maandamano yasiyokwisha na  yanayoendelea sehemu mbalimbali duniani na yakiwahusisha zaidi vijana,  yanatokana na sababu nyingi lakini kubwa ni kunyimwa kwao fursa za kushiriki siasa.

“ Vijana wengi hivi sasa wamekata tamaa na wamechoka kuendelea kuwa vipandio vya watu wengine kujipatia nafasi za uongozi wa kisiasa. Kama kweli tunataka na wao washiriki kikamilifu katika siasa  basi tunatakiwa kubadili mifumo yetu ya uchanguzi na hasa zile chaguzi ambazo zinatanguliza mbele fedha” akasisitiza  Bw. Cheyo.

Akaongeza kuwa  kila nchi inatakiwa kuweka mikakati ya makusudi itakayohakikisha  kunakuwapo na ongezeko la wabunge vijana katika mabunge yao.

 “ sisi katika  Tanzania   tumeweza kuongeza idadi ya wanawake bungeni maradufu kwa sababu tulijiweka malengo na mikakati ya kuhakikisha kwamba idadi ya wanawake inaongezeka. Kwa utaratibu huu ambao Tanzania imeutumia tunaweza pia kuutumia kwa vijana”. Akasema Cheyo.

Akizungumzia suala zima la vijana  na changamoto zinazowakabili. Mhe. Cheyo ametahadharisha kwamba, vijana wasipopatiwa  matumaini ni sawa na  silaha ya maangamizi inayosubiri kulipuka.

Akasema wanachokifanya  vijana hivi sasa katika maeneo mbalimbali duniani kama hakitaangaliwa katika umakini wake. Kuna hatari  kubwa ya kujirudia kwa tabia  ya kuwaondoa viongozi walioko madarakani kwa njia zisizo halali. Pamoja kurejea kwa matukio kama vile  mapinduzi ya kijeshi  yaliyotawala sana katika miaka ya 70 na 80.

Wachangiaji wengine waliochangia ajenda hiyo, walisema kwamba pengine vijana si  wakulaumiwa sana bali wakulaumiwa ni  wale wanaowatumia vijana  kwa manufaa  na malengo yao.

Aidha baadhi ya wachangiaji, walitaka kuwepo na tafsiri sahihi ya nani ni kijana. Kutokana na kile kilichoelezwa kwamba kumekuwa na  tafrisi zinazochanganya ni umri gani unaoweza kutajwa kwamba ni umri halali wa kijana kushiriki siasa na hata uchaguzi.

“ tumezungumza  sana kuhusu haki na fursa za vijana, wote tunakubaliana kwamba vijana wanahasira  na wanataka mgawanyo sawa wa  raslimali. Lakini hebu tuanzie humu humu  katika ukumbi tuliomo, je kati yetu ni nani mbunge kijana? Hakuna. Nadhani tuna mengi ya kufanya”. Akasema mbunge mmoja kutoka Bunge la  Uingereza na kuwafanya washiriki wengine kuangua kicheko.

Ajenda  hiyo ambayo ilikuwa kivutio kwa wachangiaji wengi lakini pia kila mmoja akitoa maoni  tofauti, na hisia tofauti katika matumizi ya vyombo vya habari vya kijamii kama vile face book na tweeter kama eneo mbadala la mawasiliano kwa vijana.

Lakini kauli za wazungumzaji wengi  ilijidhirisha wazi kwamba kila aliyeichangia  hakusita kusema vijana wengi si katika nchi zinazoendelea  bali hata zile zilizoendelea wamechoka, wamekata tamaa  na  hawana matumaini ya  maisha yao ya baadaye.

Naye Mhe. Betty Machunge akichangia majadiliano kuhusu dhana  ya uwajibikaji, uhusiano kati ya UM na Mabunge na ushiriki wa wanawake katika siasa na demokrasia kwa ujumla. Yeye alitaka kuimarishwa  na kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya Umoja wa Mataifa na  Mabunge.

Akasema kuwa maamuzi mengi yanayofanywa na Umoja wa Mataifa  hayawafiki wabunge na kama yanawafikia basi yanachelewa mno.

Akapendekeza kuwapo na mfumo au utaratibu utakao wawezesha wabunge kupitia mabunge yao kutoa taarifa za utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa hasa yale ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na wabunge.

Aisha akasema kuwa kama ushirikiano kati ya UM na wabunge utaratibiwa vizuri, utasaidia pia katika kubadilishana mawazo na mbinu mbadala za kuongeza idadi ya wanawake wabunge.

John Cheyo akibadilishana mawazo na  Bw. Oscar Fernandez-Taranco aliyewahi kuwa Mwakilishi  Mkazi wa Shirika la  Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP) nchini Tanzania. muda mfupi kabla ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa wabunge kutoka mabunge mbalimbali. Bw. Taranco ambaye kwa sasa ni Msadizi wa Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akisimamia  Idara ya masuala ya Siasa alikuwa miongoni mwa watoa mada.Mhe. Cheyo anahudhuria mkutano huo akiliwakilisha  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

MIGIRO ATAKA WABUNGE WAWAJIBIKE KWA WANANCHI

Na Mwandishi Maalum, New York
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro amewahimiza wabunge  kuweka mbele maslahi ya wananchi wanaowawakilisha.

 Ameyasema  hayo jana Jumatatu, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili unaowakutanisha  wabunge  kutoka mabunge mbalimbali duniani, ufunguzi uliomshirikisha pia Rais wa Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, Nassir Abdulaziz Al-Nasser.

Katika mkutano huo ambao umeandaliwa na Umoja wa Mataifa na  Muungano wa Mabunge ( IPU),Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linawakilishwa   na wabunge wawili, Mhe. John M. Cheyo na Mhe. Betty Machangu.

“ Mkiwa ni  wabunge  kazi yenu si kupitisha sheria tu na kusimamia utendaji wa serikali. Bali mnatakiwa kuwajibika kisiasa kwa kuwasikiliza wananchi na kuelezea matakwa yao”, Akasisitiza Migiro.

Naibu Katibu Mkuu amewaambia wabunge hao, wakiwamo pia baadhi ya maspika , kwamba, uwajibikaji wa kisiasa na utawala wa kidemokrasia haviwezi kutengenishwa kwa kuwa vyote ni muhimu katika kuchagiza  maendeleo ya binadamu,  haki na amani.

“ uwajibikaji wa kisiasa ni muhimu sana katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa.  Baadhi ya Changamato  hizo ni  pamoja na   umaskini,  vurugu, na uhalifu wa kupangwa mambo ambayo yanashamiri  katika nchi ambazo hakuna uwajibikaji” akabainisha Migiro.

Akasema kuwa  taarifa ya Bank ya  Dunia imeonesha kuwa  vita vya wenyewe kwa wenyewe,  makosa ya jinai, vurugu na hata ugaidi na  uhalifu wa kupangwa ni mambo yanayoota mizizi na kukua   katika nchi ambazo ama utawala wa sheria ni dhaifu au taasisi zake zimeghubikwa na  ufisadi.

Hata hivyo Migiro amewaeleza wabunge hao kwamba hakuhitajiki   utafiti  kama huo ulioofanywa na  Bank ya Dunia,kufahamu kwamba  kuongezeka   kwa vitendo vya halifu kunasababishwa na  serikali kandamizi.

Akatoa mfano kwa kutaja vunguvungu la kisiasa linaloendelea  hivi sasa  Mashariki ya Kati maarufu kama Arab Spring, ambako anasema vuguvugu hilo limeamsha hamasa  hususani kwa vijana, hamasa ya kutaka kuwepo na serikali za kidemokrasia, zinazowajibika na zenye kuheshimu misingi ya haki za  binadamu.

Akasema anafahamu vema changamoto wanazokabiliana nazo wabunge kwa sababu hata yeye aliwahi kuwa mbunge.

Hata hivyo akasema  yapo mambo kadhaa ambayo wabunge kwa kushirikiana na serikali zao yanaweza  saidia kuzuia au kupunguza mitafaruku ya kisiasa na  vitendo vya  uhalifu. 

Ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kujenga mazoea ya uwajibikaji, kufanya uchanguzi wa mara kwa mara na unaozingatia utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kukusanyika na kutoa mawazo na kuongeza idadi ya wanawake mabungeni.

“ Lakini uwajibikaji unakwenda mbali zaidi ya hapo” anasema Migiro. “ Ni kwa kuhakikisha  ushiriki wa  wananchi  na hasa vijana katika mambo ya  siku hadi siku, kwa kutimiza hayo na mambo  mengine wabunge mnaweza kujenga daraja imara kati ya wananchi na serikali zao” akasisitiza Migiro.

Aidha  Migiro ameyataka mabunge yote   duniani yawajibike katika kuzuia vitendo  vya rushwa.

Ajenda  muhimu zinazojadiliwa  na wabunge hao  katika  mkutano huo wa siku mbili ni    pamoja na, uhusiano kati  ya Umoja wa Mataifa na Mabunge , nafasi ya Umoja wa Mataifa katika kusimamia na kuimarisha dhana  ya uwajibikaji, na     fursa na changamoto  zinazowakabili vijana katika ushiriki wao katika demokrasia.

Nyingine ni  uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma na uimarishaji wa  uhusiano kati ya taasisi za kitaifa na asasi zisizo za kuserikali  ili kujenga jamii yenye uwazi.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro akifungua siku ya jumatatu mkutano wa siku mbili wa wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani mkutano huo unafanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, kushoto kwake ni Rais wa Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, Bw. Nassir Abdulazizi Al-Nasser na kulia ni Katibu Mkuu wa IPU Bw. Anders B. Johson.

 
Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro akibadilishana mawazo na  Waheshimiwa  Wabunge John M. Cheyo na Betty Machunge wakati alipowakaribisha Ofisini kwake Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.Wabunge hao wapo hapa wakihudhuria mkutano wa wabunge  ambao Naibu Katibu Mkuu aliufungua. Wabunge hao wanaliwakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo .

KATIBA MPYA : RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA

Nov 28, 2011

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539

Fax: 255-22-2113425PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Serikali yake, Jumapili, Novemba 27, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania.  Serikali imepokea mapendekezo hayo.

Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena asubuhi ya kesho, Jumatatu, Novemba 28, 2011, ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.

Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani,  utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.

Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba Mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za mwaka mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.

Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.  

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

27 Novemba, 2011


KIRUMBE NG'ENDA AKIWA DODOMA BAADA YA KUVULIWA UKATIBU WA MKOA WA DAR

Nov 26, 2011

"Hakuna tatizo..sikuzaliwa na ukatibu,,,tena nimeshajenga...nikimpisha katibu mpya kwenye nyumba pale Dar nahamia kwenye nyumba yangu... usafiri pia ninao..isipokuwa mimi CCM ipo kwenye moyo wangu sikuipenda sababu ya kazi" alisema aliyekuwa Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kirumbe Ng'enda (katika) wakati akipozi picha na wadau wa CCM alipokutana nao mjini Dodoma jana akiwa katika mitikasi yake mtaani

LOWASSA YUPO SINGIDA LEO

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa akiwa na viongozi wa mkoa wa Singida baada ya kuwasili mkoani humo jioni hii kwa ajili ya ziara ya kikazi ua siku mbili. (Picha na Godwin Challie)

SEMINA YA WATENDAJI WA CCM NCHI NZIMA INAYOENDELEA DODOMA

 Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati na Naibu (Zanzibar) Vuai Ali  wakati wa semina wa watendaji wa inayoendelea mjini Dodoma
 Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akitoa mada katika semina hiyo
Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba akitoa mada kwenye  semina hiyo.

MAHAFALI YA CHUO CHA MIPANGO DODOMA, TEU AAGIZA WANAOFANYA VIZURI WAAJIRIWE NA CHUO

 
Na Mwandishi wetu, DODOMA

Naibu waziri wa Fedha Mh Gregory Teu ameutaka uongozi wa chuo cha Mipango na Bodi yake kuangalia uwezekano wa kuwaajiri wahitimu wanaofaulu vizuri masomo yao ili kutumia raslimali zilizoandaliwa chuoni hapo kusaidia wenzao badala ya kusubiri kuajiri kutoka nje.

Ameyazungumza hayo jioni ya leo kwenye mahafali ya 25 ya chuo cha Mipango Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Amesema ni vyema chuo kikaanza kutumia vijana waliofaulu vyema kwenye shahada zao za kwanza kama inavyofanyika kwa vyuo vingine na hatimaye kuwaendeleza kwa ngazi za juu hatua ambayo itasaidia kupunguza pengo la wahadhiri  wasaidizi.
Mapema katika taarifa yake mkuu wa chuo hicho Costantine Lifurilo amesema,chuo hicho ambacho kimeanza mwaka 1979 kikiwa na wanafunzi 22, kimeendelea kukua ambapo hadi kufikia mahafali ya leo kimehitimisha wanafunzi 1477 kiwango ambacho amesema kimesaidia kupunguza pengo la wataalamu wa mipango katika ngazi mbalimbali za serikali na hasa serikali za mitaa.

Amesema pamoja na hatua hizo, chuo kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa miundombinu ya kufundishia na kuiomba wizara kuangalia uwezekano wa kuwezesha ukamilishaji wa jengo la ghorofa saba ambalo litatumika kwaajili ya mihadhara, ofisi na kumbi za kusomea.

Mapema katika salam zake Mwenyekiti wa bodi ya chuo Dr Razack Lokina amesema kwa sehemu kubwa chuo kimeweza kutekeleza malengo yake  ya mpango mkakati unaoishia 2014 na kwamba hatua inayokusudiwa sasa ni kuanzisha shahada mbili za uzamili baada ya kukamilisha kwa miundombinu muhimu ya uendeshaji mafunzo hayo.

Amesema hayo yote yamefikiwa kutokana na ushirikiano baina ya chuo hicho, wizara ya fedha ambamo chuo hicho ni sehemu yake, na baadhi ya wadau wahisani kutoka nje.
N

JOSE CHAMELEONE WA UGANDA APAGAWISHA WAKAZI DMV, MAREKANI


Mwana muziki wa kizazi kimpya ndani ya Washington DC, AJ Ubao wa kwanza (kushoto) pamoja mzee wa kuwachanganya Dmk global Dickson Mkama. wa kwanza( kulia) wakiwanyumba ya jukwa na mwana muzingi aliekuwa anasubiriwa kwa hamu siku ya jana Jumatano Nov23, 2011 katika sherehe za Thanksgiving Muimba Jose Chameleone katikati, akisubiriwa kwa hamu na wapenzi wake
Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone akifanya vituz vyake ndani ya Rendezvous Hall mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.S

Mamia ya watu jana walifurika kuja kumuangali Msanii kutoka Nchini Uganda  kwa jina maarufu la Jose Chameleone, ana nyimba zake, ikiwemo mama roda, Jamalila analia, na nyingi nyenginezo.
 Warembo akiserebuka ukumbini

Mamia ya watu jana walifurika kuja kumuangali Msanii kutoka Nchini Uganda  kwa jina maarufu la Jose Chameleone, ana nyimba zake, ikiwemo mama roda, Jamalila analia, na nyingi nyenginezo.
 Wakati mwingine mashabiki walitulia ukumbini kusikiliza kwa makini nyimbo mbalimbali za mwanamuziki huyo
Wengine kama hawa hawakuvumilia , wakaamua kusakata muziki vilivyo
Picha zaidi peruzi http://swahilivilla.blogspot.com/

WATANZANIA WAWILI KUCHEZA LIGI DARAJA LA PILI SWEDEN

Nov 25, 2011

Wapiga gozi wawili wa Kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) naWilliam John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio (Trials).
       Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya 30 ambapo watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor(KIF)
 William John
Joseph Kaniki (Golota ) Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/

TAARIFA KAMILI YA MAAMUZI NA MAAZIMIO YA KIKAO CHA NEC YA CCM DODOMA


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mwishoni kwa kikao hicho mjini Dodoma jana. Wengine upande wa Mwenyekiti huyo ni Mwenyekiti mstaafu Benjamin Mkapa, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.

IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI YA MAAMUZI NA MAAZIMIO YA KIKAO HICHO KAMA YALIVYOWASILISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO NA KATIBU MKUU WA CCM WILSON MUKAMA.
 
 Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana kwa siku mbili kuanzia tarehe 23-24 Novemba, 2011 mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mambo mengine imeazimia yafuatayo:
UNUNUZI WA MAHINDI
     I.         Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Serikali kwa kuwa na mkakati wa kutafuta fedha haraka kwa kuamua kuuza mahindi tani 80,000 kwa UNFP na nchini Kenya ili kwanza, kulipa madeni ya wakulima, na pili, kununua mahindi ya wakulima yaliyopo majumbani na kwenye vituo vya ununuzi kabla ya upandaji wa msimu mpya haujaanza.

   II.         Imeipongeza pia Serikali kwa kuruhusu uuzaji wa mahindi nje ya nchi, hali ambayo itasaidia mahindi yaliyobaki kwa wakulima kupata soko. Hata hivyo, imesisitiza kuwepo na tahadhari sasa na siku zijazo, ili chakula chote kisiuzwe nje ya nchi na kusababisha tatizo la njaa nchini.

   III.         Imeitaka Serikali iimarishe Wakala wa Chakula wa Taifa kwa kuuwezesha kwa fedha zaidi na kujenga maghala mengi na makubwa zaidi ili uweze kununua kiasi kikubwa cha mazao.


  IV.         imeiagiza Serikali ihimize kuundwa kwa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Chakula, ambavyo navyo viwezeshwe kujenga maghala ya kuhifadhi nafaka katika maeneo yao pamoja na kuanzisha mfumo wa ununuzi wa mazao wa stakabadhi ghalani.

MJADALA WA KATIBA
  1. Halmashauri Kuu ya Taifa imewataka wananchi na wanachama wa CCM kuelewa, kutambua, na kuamini kwamba Katiba mpya pamoja na mchakato wa kuipata, ni kwa manufaa ya nchi. Imewataka Wabunge na viongozi wengine wa ngazi zote nchi nzima kuwaelewesha wananchi si tu maudhui yake, bali hata faida zake.

  1. Imeiagiza Serikali, pamoja na/au kupitia Tume ya Kukusanya Maoni, iweke msukumo wa kutoa elimu kwa umma wakati wote kuhusu jambo hili na mchakato mzima ili kuzuia upotoshaji unaofanywa kwa wananchi kuhusu mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.

  1. Imeitaka Serikali ihakikishe hakuna Chama chochote cha siasa, mtu, kikundi cha watu au taasisi yoyote ikayotumia mchakato wa kupata Katiba mpya kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani. Vyombo vya Usalama viwe imara katika kuhakikisha kwamba Sheria za nchi zinafuatwa na wanaochochea vurugu wanachukuliwa hatua kali bila kujali nafasi zao.

Aidha, imempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwa wazee wa Dar es Salaam kwa ufafanuzi na maelezo fasaha kwa mambo makubwa na ya msingi yanayolikabili taifa letu.

Nishati ya Umeme na Mafuta Nchini

I.             Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Serikali kwa kutengeneza mpango wa umeme wa          dharura, licha ya gharama kubwa, lakini umesaidia kuleta nafuu katika uzalishaji umeme na kupunguza kero kwa wananchi. imeitaka Serikali kutoa taarifa sahihi kwa wakati kuhusu mgao wa umeme na maeneo yanayoathirika ili kupunguza lawama kwa Serikali.

II.           Aidha imeitaka Serikali kuongeza jitihada za kuzalisha umeme kwa vyanzo vingine, hasa makaa ya mawe ambayo yapo nchini na umeme wake ni nafuu.

III.         Halmashauri Kuu ya Taifa imepongeza pia jitihada za Serikali kusambaza umeme nchini, ambapo sasa karibu kila Makao Makuu ya Wilaya yana umeme. Hata hivyo, imeitaka Serikali, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), iongeze kasi ya usambazaji umeme vijijini ili kufikia lengo la Ilani ya Uchaguzi ya CCM la asilimia 30 ya kaya zote nchini kuwa na umeme ifikapo mwaka 2015.

IV.          Imepongeza jitihada za Serikali za kutafuta fedha (dola za Kimarekani takriban bilioni 1) za ujenzi wa bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambalo litawezesha kuongeza uzalishaji wa umeme na kuondokana na matumizi ya mafuta kuzalisha umeme. Aidha, Serikali iharakishe taratibu zote za upatikanaji wa fedha hizo ili utekelezaji wa mradi huo uanze mara moja.   

UPANGAJI WA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA.
     I.        Kutokana na umuhimu wa nishati ya mafuta kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu, Halmashauri Kuu ya Taifa imeitaka Serikali kuhakikisha kwamba EWURA inao uwezo, utaalamu na weledi wa kuisimamia sekta hii ipasavyo. Aidha imeipongeza Serikali kwa uamuzi wa kuwa na hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta, na wa kuanzisha Kampuni ya Mafuta ya Taifa kwa sababu itasaidia kuziba pengo pale linapotokea tatizo la hujuma kwa waagizaji wa sekta binafsi. 

UCHANGISHAJI FEDHA KWA AJILI YA KUPITISHA BAJETI
Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kuipokea taarifa ya Kamati Teule ya Bunge na kuahidi kuifanyia kazi.

Vurugu Katika MIji NA MAENEO MENGINE NCHINI.

  1. Kumejitokeza wimbi la vurugu katika maeneo mbalimbali hapa nchini hasa katika majiji yetu. Majiji ambayo hivi karibuni yameripotiwa kutokea vurugu zikifanywa zaidi na vijana ni Mwanza, Mbeya na Arusha. Kutokana na hali hiyo, Halmashauri Kuu ya Taifa, imeitaka dola kuchukua hatua thabiti na za haraka kudhibiti vitendo vya hujuma na uharibifu kwa mali za Watanzania. Imesisitiza kuwa Kusiwepo kabisa na uvumilivu kwenye uvunjaji wa amani kwa kisingizio cha kudai haki. Viongozi wa vyama vya siasa wanaojihusisha na vitendo vya uchochezi na hujuma wachukuliwe hatua za kisheria bila kuogopwa.

  1. Hata hivyo, Halamshauri Kuu ya Taifa imeitaka Serikali kuharakisha kutatua matatizo yanayowakabili vijana wa mijini, hususan tatizo la ajira na maeneo ya kufanyia biashara zao ndogo ndogo. Imeitaka kuuangalia upya mfumo wa elimu nchini ili vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne wawe na stadi za ufundi zitakazowapa uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa. Vile vile, mpango wa kujenga shule za ufundi kwenye kila wilaya uliomo kwenye llani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010-2015 utekelezwe haraka.

MIGOGORO VYUO VIKUU NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU
I.                Halmashauri Kuu ya Taifa imeitaka Serikali ihimize utawala bora katika menejimenti za baadhi ya vyuo vikuu vya umma kama moja ya jawabu la kupunguza malalamiko, migogoro, migomo na vurugu katika baadhi ya vyuo.

II.                Imeitaka Serikali kutekeleza Sheria yake ya kupiga marufuku harakati za siasa na uvaaji wa sare za vyama katika maeneo ya vyuo (Campuses). Wafanyakazi wa vyuo na wanavyuo wanaopenda kujihusisha na harakati za siasa basi wafanye hivyo nje ya maeneo ya vyuo.  Hii itawafanya jamii ya wanavyuo kutoingilia shughuli za masomo na mipango ya vyuo.


III.                Imeiagiza Serikali kuendelea kufuatilia kwa karibu hali ya migogoro na malalamiko hasa katika Chuo Kikuu cha Dodoma na ichukue hatua muafaka kurekebisha hali hiyo.

MIGOGORO YA ARDHI
     I.        Halmashauri Kuu ya Taifa imeitaka Serikali ihakikishe kwamba katika uwekezaji unaohusisha umiliki wa maeneo makubwa ya ardhi, wananchi wasiporwe au kudhulumiwa au kushurutishwa kuhama kwenye ardhi yao bila fidia stahiki.

   II.        Iwahamasishe pia wawekezaji waliopewa maeneo ya kulima mashamba makubwa kusaidia wakulima wadogo walio karibu na mashamba hayo makubwa kuinua kilimo chao.

 III.        Kuhakikisha uongozi wa Serikali katika ngazi zote kushughulikia kwa haraka migogoro ya ardhi nchini ili kupunguza kero kwa wananchi.  

  IV.        Imeipongeza Serikali kwa kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima, ambayo kwa sasa imepungua kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo imesisitiza jitihada ziendelezwe serikali katika kupanga matumizi ya ardhi, hasa kutenga maeneo maalum ya wakulima na wafugaji ili kuepusha muingiliano ambao husababisha migogoro.

KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDER I TAREHE 10/09/2011
             I.        Kutokana na maafa yaliyotokea tarehe 10 Septemba, 2011 ya kuzama kwa meli ya Spice Islander I, Halmashauri Kuu ya Taifa imezipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa hatua thabiti na za haraka ilizochukua katika kipindi chote cha maafa na msiba huo na hata baada.

           II.        Imewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dr. Ali Mohammed Shein kwa kutoa uongozi thabiti na kuongoza katika kuwafariji na kuwatuliza wananchi wa visiwa vya Zanzibari na Watanzania kwa jumla katika kipindi chote cha msiba huu. 

         III.        Halmashauri Kuu ya Taifa, pia imewashukuru watu binafsi na taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwenye zoezi la uokoaji na zilizochangia kwa hali na mali, kwa fedha na vifaa, katika msiba huu. Vilevile, imewashukuru na kuwapongeza wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba waliojitolea kushiriki kwenye zoezi la uokoaji.  

          IV.        Kwa kuwa tayari Tume imeundwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi, Halmashauri Kuu ya Taifa imewataka wananchi wasubiri na waiache  ifanye kazi  yake kwa uadilifu na kwa muda uliopangwa na kuhakikisha kuwa mapendekezo ya tume hiyo yanafanyiwa kazi.

            V.        Imeiagiza pia Serikali kuendelea na jitihada zake za kurahisisha usafiri wa abiria kati ya Unguja na Pemba na kati ya visiwa hivyo na Tanzania Bara ikiwemo nia yake ya kununua meli zake.

UTEKELEZAJI WA MAAMUZI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA KUHUSU VIONGOZI WANAOTUHUMIWA.

Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kuyatafsiri maazimio yake 27 ya tarehe 10-11 Aprili 2011, na kupokea taarifa ya utekelezaji wa azimio la “Viongozi wa CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari, wajipime na kuchukua hatua wenyewe kwa maslahi ya chama, wasipofanya hivyo, chama kiwawajibishe bila kuchelewa”.

Katika kutekeleza sehemu ya pili ya uamuzi huo, Halmashauri Kuu ya Taifa imeiagiza Kamati Kuu pamoja na kamati za siasa za ngazi zote za chama chetu, kupitia kamati za usalama na maadili za ngazi zao, kuanza mara moja mchakato wa kutekeleza azimio  hilo kwa mujibu wa kanuni na taratibu zinazohusika za chama, na kwamba zoezi hilo lifanyike bila kuchelewa.

Baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, taarifa za utekelezaji zipelekwe kwenye vikao vya kikatiba vya chama.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Wilson C. Mukama
KATIBU MKUU WA CCM
ยช