.

RAIS KIKWETE ATOA SALAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA HALIMA MCHUKA

Dec 29, 2011

Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana, kufiatia kifo cha mtangazaji maarufu wa siku nyingi wa  shirika hilo, Halima Mohammed Mchuka ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia leo, Alhamisi, Desemba 29, 2011 kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
“Nimepokea kwa huzuni habari za kifo cha Halima Mohammed Mchuka. Nakutumia wewe Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo hiki. Nakuomba, kupitia kwako, uniwasilishie salamu zangu kwa wafanyakazi wenzake katika TBC ambao wamempoteza mwenzao na rafiki yao.” Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam, imesema ikimkariri Rais.
“Aidha, nataka kupitia kwako niwatumie salamu zangu za rambirambi wana-familia, ndugu na jamaa wote za marehemu. Wajulishe kuwa niko nao katika wakati huu wa maombolezo na kwamba msiba wao ni msiba wangu pia. Nawaomba wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi ya Mungu. Naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amen.” amesema Rais.
 Rais amesema kuwa Mchuka ametoa mchango mkubwa katika nyanja ya utangazaji nchini. “Sote tutaendelea kukumbuka weledi wake, uzalendo wake na ujasiri wake katika utangazaji uliomsukuma kuwa Mwanamke wa Kwanza katika Tanzania kutangaza mechi za mpira wa miguu”.

Amesema ni dhahiri kuwa nyanja ya utangazaji imeondokewa na mtu muhimu na namna nzuri zaidi ya kumuenzi  Mchuka ni kwa watangazaji waliobakia kuendelea kuiga mfano wake katika ubora wa utangazaji nchini mwetu.

MAHAKAMA MISRI YAZUIA KUWAPIMA BIKIRA AMBAO HAWAJAOLEWA

Mahakama katika mji wa Cairo nchini Misri imepinga kitendo kilichofanywa na Baraza la Kijeshi la Misri cha kuwapima bikra wasichana saba waliokamatwa kwenye maandamano, ikisema ni kinyume cha sheria na inabidi wasichana hao walipwe fidia.

Jaji wa mahakama hiyo,  Aly Fekry ametoa uamuzi huo katika kesi iliyofunguliwa na msichana Samira Ibrahim (25), ambaye alisema yeye na wenzake  sita waliteswa na kudhalilishwa na wanajeshi hao baada ya kukamatwa kwenye Uwanja wa Tahrir wakati wa maandamano yaliyofanyika Machi 9, mwaka huu.

Semira alikuwa miongoni mwa waandamanaji 200 waliokamatwa siku hiyo 20 kati yao wakiwa ni wanawake.

Alisema siku iliyofuata  wanawake hao walitenganishwa makundi mawili kwa kuwaweka walioolewa kundi lao na ambao bado ambao walikuwa saba waliwekwa kundi la pili na kuamriwa wapimwe bikira na madaktari wanaume.

Walisalimika baada ya kukutwa na bikira zao, lakini kama wangekutwa hawana wangefunguliwa mashikata ya kufanya umalaya. 

KIM JONG IL AZIKWA

Dec 28, 2011

Alipozikwa Kim Jong Il
Korea Kaskazini inafanya maziko ya kitaifa ya kiongozi wake Kim Jong-il huku msafara mkubwa wa magari yaliyosindikiza jeneza la kiongozi huyo ukipitia mji mkuu Pyongyang.

Picha za runinga zimeonyesha maelfu ya wanajeshi wakitoa heshima za mwisho kwa picha ya kiongozi huyo iliyopitia kwenye barabara za mji.

Mridhi wa uwongozi ambaye ni mwanawe wa kiume Kim Jong-Un amezindikisha jeneza la babake lililokuwa juu la gari maalum. Kim Jong-il alifariki dunia Decemba 17 baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo akiwa na miaka 69.

Hakuna viongozi wa nje walioalikwa wala waandishi wa habari wa kimataifa. Wadadisi wanasema mazishi ya leo ni sambamba na ya mwasisi wa nchi hiyo Kim IL-Sung mwaka 1994 yalioandamana na gwaride kubwa ya kijeshi.

Kiongozi mtarajiwa Kim Jon-Un ameandamana na mjombake Chang Song-taek anayetarajiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika uwongozi mpya pia mkuu wa jeshi Ri Yong-ho, alionekana kando ya jeneza la Kim Jong-Il.

Kabla ya kufariki kiongozi wa Korea Kaskazini alikuwa katika mchakato wa kumtayarisha mwanawe Kim Jong-Un kuchukua hatamu za uwongozi. Kifo chake cha ghafla cha Kim Jong Il kimepelekea hofu ya kuzuka mzozo wa uwongozi katika taifa hilo lenye msingi wa ujamaa.

KHADIJA MUSAA WA UHURU ANG'ARA SHINDANO LA AAJAT

Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dk. Fatma Mrisho (kushoto) akitao zawadi na cheti kwa Mwandishi wa Habari wa Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Hadija Mussa kwa kushinda kutokana na  kuandika makala za Ukimwi katika shindano lililoandaliwa na  Chama Cha Waandishi wa Habari za Ukiwmi Tanzania ( AJAAT), hafla ya uroaji zawadi  kwa washindi ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Dar es Salaam.. (Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO)

UDF YATOA MSAADA WA BAISKELI 30 ZA WALEMAVU


MRATIBU wa UDF Enock Bigaye akikabidhi baiskeli moja
 kati ya 30 za walemavu kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa
Dar es Salaam,  Eliya Ntandu, jana. Katikati ni Mbunge wa
Kinondoni, Iddi Azan akishuhudia.
NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Unit in Diversity Foundation (UDF), imekabidhi msaada wa baiskeli 30 za walemavu  zenye thamani ya sh. milioni tisa kusaidia waathirika wa mafuriko mkoani Dar es Salaam.

Msaada huo umelanga kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kambi za waathirika wakaoshi.

Akikabidhi msaada huo jana kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Eliya Utandu, Mratibu wa UDF Enock Bigaye, alisema baiskeli hizo zitagawiwa kwa walemavu wenye mahitaji katika halmashauri zote tatu za Kinondoni, Temeke na Ilala.

Alisema UDF ambao ni mdau mkubwa wa walemavu nchini, imeguswa na maafa hayo na kwamba, baiskeli hizo zitawawezesha kuwasaidia kutoka eneo moja kwenda jingine.

“Ni maafa makubwa kwa taifa na walemavu wengine wanaishi kwenye maeneo yaliyoathirika. UDF tumetoa msaada huu ili uwasaidie na tutaendelea kuwawezesha ili kuhakikisha wanakuwa salama daima,” alisema Bigaye.

Akipokea msaada huo Ntandu, aliishukuru UDF kwa kuwajali walemavu kwa kuwapatia misaada mara kwa mara na kwamba, huu wa baiskeli umekuja kwa wakati muafaka.

Alisema serikali itahakikisha msaada huo unawafikia walengwa na kutumika kama ilivyokusudiwa na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa taasisi hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan ambaye amesaidia kufikishwa kwa msaada huo, alisema jamii na serikali kwa ujumla haina budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na UDF.

Alisema katika jimbo lake kuna walemavu wengi walioathirika na mafuriko huku wengine wakiwa na mahitaji mbalimbali na kwamba, msaada huo utakuwa mkombozi.

“Kwangu kuna walemavu wengi wameathiriwa na mafuriko, msaada huu utawapa nafuu ya kuishi kwenye kambi ambako serikali imewahifadhi kwa sasa,” alisema Azzan.

Pia, alisema atakuwa bega kwa bega na UDF katika kuhakikisha walemavu nchini wanawezeshwa kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Katibu Mkuu wa Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA), Nicholaus Kihwelo, alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka wakati walemavu wengi wakihangaika kwenye kambi za waathirika.

“Walemavu ndiyo wenye nchi, vikitokea vita, mafuriko na maafa mengine hawawezi kujiokoa na wala hutawaona wakikimbia. Tunaendelea kuishukuru UDF kwa kutusaidia,” alisema.

WANA YANGA TABATA KUKUTANA 'BOXING DAY'

Dec 25, 2011

Na Mwandishi Wetu

WANACHAMA wa klabu ya Yanga tawi la Tabata wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa mwaka utakaofanyika kesho Jumatatu (26 Desemba, 2011) kwenye Ukumbi wa Afisa Mtendaji Kata huku ajenda kubwa ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa tawi hilo, Michael Warioba alisema, wanachama wa tawi hilo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mkutano huo utakaoudhuriwa na vingozi wa kitaifa wa timu hiyo.

 "Vitu vingi tutavizungumzia kama vilivyoorodheshwa katika ajenda zetu, lakini kubwa ni maandalizi ya timu katika mzunguko wa pili wa ligi kuu, pia mchezo wetu na Zamalekh (Kombe la Shirikisho Afrika).

 "Tunaomba wanachama wajitokeze kwa wingi saa 4:00 asubuhi katika mkutano huo ili tuweze kuijenga klabu yetu na kutetea ubingwa wa Bara," alisema Warioba.

 Pia Warioba amewataka wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza kuchukua kadi za uanachama wa Yanga ili waweze kupata nafasi ya kutoa mchango wa hali na mali katika kuhakikisha timu inafanya vizuri kwenye michuano mbalimbali

DK. SHEIN AMTUNUKU SHAHADA DK. KARUME

Dec 24, 2011

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed  Shein,akimtunuku shahada ya uzamivu  ya  heshima ya chuo kikuu cha Taifa SUZA Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume,wakati wa sherehe za mahafali ya saba  ya chuo hicho katika viwanja vya Mnazi mmoja Mjini Unguja leo. (Picha na Ramadhan Othman IKULU).

NG'ENDA AKABIDHI OFISI LEO

Aliyekuwa Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Shaaban Kilumbe Ng'enda (kulia) leo amekabidhi rasmi Ofisi kwa Katibu mpya wa mkoa huo aliyerithi mikoba yake, Abilahi Mihewa aliyekuwa Biharamulo. Pichani, Ng'enda akimkabidhi  Mihewa nyaraka za ofisi, katika Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam.

RAIS AMTEUA LUBUVA KUWA MWENYEKITI TUME YATAIFA YA UCHAGUZI

Dec 22, 2011

Jaji Mstaafu Damian Lubuva
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.
Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011.
Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.
Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.

MAAFA YA MVUA DAR: JK AOMBOLEZA VIFO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu 13 ambao wamepoteza maisha katika mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua ambazo zimekuwa zinanyesha tokea jana, Jumanne, Desemba 20, 2011.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema aidha Rais Kikwete amempa pole Mkuu huyo wa Mkoa kutokana na uharibifu mkubwa wa nyumba, makazi na mali nyingine za wananchi uliosababishwa na mvua hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu wa miundombinu.

Rais Kikwete ameuelekeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusaidiana na taasisi na vyombo vyenye uzoefu wa maafa kushirikiana katika kuendelea kuokoa maisha ya watu, kusaidia waliozingirwa na mafuriko na
kuwahifadhi na kuwasaidia wale wote waliopoteza nyumba na makazi kutokana na mafuriko hayo.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Sadiq: “Nimepokea kwa masikitiko habari za vifo vya wenzetu 13 ilivyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo sote tumeishuhudia katika Mkoa wa Dar es Salaam tokea jana. 

Amesema: “Nakutumia wewe rambirambi zangu kutokana na vifo hivyo, na kupitia kwako kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika balaa hili la mafuriko. Wajulishe kuwa msiba wao ni msiba wangu, naelewa machungu yao na niko nao katika hali ya sasa ya maombolezo. Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote.” 

Ameongeza Rais Kikwete: “Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wote walioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu.

“Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo.”

MAJAJI WATANZANIA WAPETA UCHAGUZI UMOJA WA MATAIFA

Jaji William Hussein Sekule (pichani) na Jaji Joseph Chiondo Masanche wote kutoka Tanzania  wameingia katika orodha ya majaji wa Mfumo mpya wa Kimataifa wa kushughulikia kesi za Mashauri ya Masalia ya Mahakama za Makosa ya Jinai ( International Residual  Mechanism for Criminal Tribunals) majaji hao wameingia katika orodha hiyo wakiwa ni kati  ya majaji 25 walioshinda baada ya kupingiwa kura ya siri miongoni mwa majaji 36 walioomba nafasi hiyo. Upigaji kura huo ulifanywa na Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa na umekamilika siku ya Jumanne wiki hii.

MVUA NOMA DAR!

 Mkazi wa bonde la Jangwani Dar es Salaam, akihamisha vyombo baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko jana, kufuatia mvua zilizonyesha tangu juzi.
  Mkazi wa Jwangwani akiogelea kwenye godoro kujiokoa baada eneo hilo kukumbwa na mafuriko.
 Barabara ya Morogoro, ikiwa imefunikwa na maji eneo la bonde la Jangwani Dar es Salaam, jana kufuatia mafuriko yaliyolikumba eneo hilo kutokana na mvua zilizoanza junyesha juzi.
 Nyumba na daladala vikiwa vimezingirwa na maji huku baadhi ya watu wakiwa juu ya paa za nyumba kujinusuru, baada ya eneo la bonde la Jangwani kukumbwa na mafuriko jana.
 Watu wakitembea kwa miguu baada ya magari walimokuwa wakisafiria kwenda Kariakoo na Posta kushindwa kuvuka eneo la daraja la jangwani kutokana na mafuriko jana.
 Eneo la Jangwani karibu na Ofisi za Kajima likiwa limefurika maji
 Barabara Bagamoyo ikiwa imemomonyoka karibu na daraja la Kawe, kutokana na mvua zilizonyesha jana. Hali hiyo imesababisha barabara kufungwa katika eneo hilo na hivyo magari kati ya Tegeta na
Mwenge ambayo hupita eneo hilo kulazimika kuishia hapo.
 Bajaji na pikipiki zisafirisha abiria waliolazimika kutafuta usafiri huo baada ya daladala  walizokuwa wamepanda kushindwa kuvuka eneo la Kawe-darajani, barabara ya Bagamoyo, kufuatia sehemu ya barabara hiyo kuharibiwa na mafuriko katika eneo hilo, jana.
 Wananchi wakisaidiana kunasua gari la mkazi wa Kawe-Darajani, baada ya gari hilo kuzolewa na mafuriko baada eneo hilo kukumbwa na mafuriko jana.
 Ofisi za Makao Makuu ya TLP zilizopo Magomeni Usalama, zikiwa zimekubwa na mafuriko.

MREMBO WA VENEZUELA AFARIKI DUNIA

Dec 20, 2011

Eva Ekvall
CARACAS, Venezuela
Miss Venezuela wa zamani, Eva Ekvall, amefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani ya matiti, akiwa na umri wa miaka 28.

Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo, familia yake imesema Ekvall amefariki Jumamosi katika hospitali ya Houston.

Ekvall alitwaa taji la urembo wa  Venezuela  mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 17 na mwaka uliofuata alitwaa nafasi ya tatu katika shindano la Miss Universe lililofanyika mjini Puerto Rico. Aliendelea kufanya kazi ya uanamitindo, mwigizaji wa filamu na mtangazaji wa habari katika televisheni.

Mrembo huyo amewahi kuandika kitabu "Fuera de Foco" ("Out of Focus"), kuhusu mapambano ya saratasni ambacho kilitumia picha za mpigapicha wa Venezuela Roberto Mata.

MAHAFALI YA MZUMBE KAMPASI YA DAR

Mahafali hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki yalikuwa ya aina yake, hasa kwa wahitimu kumeremeta katika majoho kama hawa ndugu waliojipatia shahada ya pili ya sayansi katika Menejimenti ya Ununuzi.  Kama unayafahamu majina yao nitajie kweneye  maoni hapo dauni.
 Hawa wao walipata  "Master Of Business Asdministration (MBA) Corporate Management.
 Nawa pia wanaopiga pozi usawa wangu wa kamera wamepata shahada hiyo hiyo ya MBA....
 Hawa bila shaka ungependa kujua majina yao kwa jinsi wanavyoonekana wenye furaha. Tafadhali anayewafahamu atuwekee hayo majina yao kwenye maoni chini ya ukurasa huu.
 Maandalizi ya kila aina yalihitajikamuda mfupi kabla ya wahitimu kutunukiwa shahada zao, Huyu ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwekwa sawa kofia yake na Mama yake mzazi mbaye kwa heshima nitamwita 'Mama Nape' basi. Kulia anayeshuhudia ni  Mkuu wa Kitengo wa Mahusiano na Umma katika Idara ya Itikadi na Uenezi Makao Makuu ya Chama, Comrade Chongolo.
 Kutokana na kuwa siku ya kipelee wahitimu karibu wote walisindikizwa na familia zao, huyu ni Ofisa Makao Makuu ya CCM pale Lumumba, Ndugu Mpelemba akipozi picha pamoja na wanafamilia yake.
Dada Emiliana wa Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani akimpongeza ndugu wake aliyepiga nondozzz hapo hapo Mzumbe. Bila Shaka Dada Emmy atatuwekea jina la huyu ndugu yake kwenye maoni chini ya ukurasa huu.

KUTOKA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

                                                                                                                              
 CHAPISHO LA PATO LA MKOA WA IRINGA 
 
Utayarishaji wa Pato la Mkoa wa Iringa umekamilika.
Kazi hii imefanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.

Kazi kubwa ilikuwa ni ukusanyaji wa taarifa ya uzalishaji wa bidhaa na huduma katika Mkoa wa Iringa kwa miaka iliyokusudiwa ambayo  ni mwaka 2006, 2007 na 2008.

Dhumuni kuu ni kutoa viashiria vya Pato la Mkoa, Pato la Wilaya ya Wastani wa Pato kwa Mkazi ambayo vitatumika katika kutathmini sera mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya umaskini katika Mkoa wa Iringa.

Matokeo haya yatatangazwa rasmi 20 Desemba, 2011 katika mkutano wa wataalamu wa Mkoa wa Iringa (RCC) tarehe 20 Desemba, 2011 mnakaribishwa.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu inahimiza wote kuwa kutoa Pato la Mkoa wa Iringa itakuwa ni chachu kwa Mikoa mingine ambayo haijafanya zoezi hili.

 TAKWIMU KWA MAENDELEO
 ASANTENI
Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu
S. L. P. 796 Dar es Salaam.
Simu +255 22 2122724, +255 22 2122722/3
Fax:  +255 22 2130852
Barua pepe: dg@nbs.go.tz
Tovuti: www.nbs.go.tz

KIBONZO

 
Meseji Sent!

TANZANIA: EDITOR QUESTIONED OVER OPINION ARTICLE

The Police on Friday questioned the Managing Editor of a Swahili daily Newspaper, Tanzania Daima, Absalom Kibanda, over an opinion article recently published by the paper.

Mr. Kibanda, who is also a Chairman of the Tanzania Editors Forum, was questioned on Friday December 16, 2011 for over three hours at police headquarters in Dar es Salaam over the article, which the police claimed was “seditious”.

According to Tanzania Union of Journalists (TUJ), Kibanda was later released on Tanzanian Shs. 5 millions bond (about 3125 US dollors) but was required to report back to the police today, apparently for further questioning.

The opinion piece in question was written by Samson Mwigamba, a columnist with the daily, and was published in the November 30, 2011 issue, apparently as an open letter to members of the security forces. Mwigamba, is out on bail after being charged with sedition in a Dar es Salaam court.

Police claimed the article had the motive of stirring up discontent among junior police officers so that they refuse to obey orders from their superiors if they seemed to be serving political interests.

According to Mr. Kibanda, the article was from a contributor who expressed his personal opinion and did not reflect the editorial views of the paper.

“I don’t agree with the police’s interpretation of the article. I have fears that the police may use the article in question to undermine press freedom in the country” Said Kibanda.

Reacting to the report, Eastern Africa Journalists Association (EAJA) Secretary General Omar Faruk Osman termed the move to summon and question the editor, “an attempt to stifle press freedom” in Tanzania.

“We urge the Tanzanian authorities to stop any acts of intimidation against journalists and even individuals who choose to use the press to express their opinions,” added Osman.

AFRIKA YATAJA VIPAUMBELE MKUTANO WA RIO+20

 Mhe. Ombeni Sefue,

Na Mwandishi Maalum, New York
Wakati maandalizi ya mkutano wa kimataifa  kuhusu  Maendeleo Endelevu ( United Nations Conference on Sustainable Development) maarufu kama  RIO+20   yakiwa yanaendelea, Afrika imetoa vipaumbele vyake ambavyo inataka vizingatiwe wakati wa  mkutano  huo  unaotarajiwa kufanyika mwezi Juni,2012, Rio de Janairo,  Brazil.

Balozi  wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe.Ombeni Sefue (pichani) akizungumza kwa niaba ya kundi la nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa. Amesema vipaumbele hivyo vinapashwa kuzingatiwa kwa kuwa ni muhimu katika kufikia malengo ya kuondoa umaskini hasa kwa   Afrika kupitia mkakati mpya wa  uchumi wa kijani.

 Anavitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na,   uboreshaji wa uzalishaji wa kilimo na usalama wa chakula,  kupambana na kudhibiti  kuenea kwa jangwa na uharibifu wa ardhi,  usimamizi wa mazingira ya  bahari, uimarishaji wa matumizi endelevu ya maliasili ikiwa ni pamoja na  maji safi, misitu na viumbe hai. 

Vipaumbele vingine ni  kukuza matumizi  na uzalishaji  endelevu na maendeleo ya viwandani na kuhakikisha usimamiaji wa kemikali taka, kukuza utalii  endelevu na kuhakikisha upatikanaji wa nishati  salama na endelevu.

Kwa siku mbili wadau mbalimbali wakiwamo mabalozi walikutana katika majadiliano ya  ya siku mbili  hapa Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo mengine, walijadili maandalizi ya mkutano  huo muhimu  na ambao utawakutanisha wadau mbalimbali kutoka duniani kote, wakiwamo wakuu wa nchi na serikali,  wanadiplomasia, wanasiasa, wataalamu wa masuala ya maendeleo endelevu,   mazingira , tasisi binafsi na za kiraia.

Balozi Sefue anasema   ni matarajio ya Afrika kwamba, washiriki wa mkutano huo siyo tu watajituma bali pia wataonyesha utashi wa kisiasa katika kuhakikisha kwamba mkutano huo unafanikiwa na kutoka na malengo yanayotekelezeka na ambayo yatakuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo.

“Kundi la afrika linatoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuonyesha dhamira  na utashi wa kisiasa ili  katika mkutano  huo wa RIO+20 tuwezwe  kutoka na  habari yenye matumaini kwa vizazi vijavyo . 

Afrika pia  inapenda kukaribisha kuanzishwa kwa  mfumo ambao utasimamia na kufuatilia  makubaliano yatakayofikiwa na, pamoja na utekelezaje wake kama suala la dharura” akasema Balozi Sefue.

Akitilia mkazo wa vipaumbele vya Afrika katika suala zima la maendeleo endelevu, Balozi Ombeni  Sefue ambaye kwa  miezi miwili mfululizo, Tanzania   imekuwa Mwenyekiti wa Kundi la  Nchi za Afrika.

Anasema  mtizamo wa  Afrika ni kutaka kuona kwamba nguzo kuu tatu muhimu kwa  maendeleo endelevu zinapewa umuhimu unaolingana bila ya mmoja kupewa uzito wa kipekee.

Anasema “ Afrika inapenda kutoa  wito  na kusisitiza  umuhimu wa ushirikiano wa uwiano katika nguzo hizo tatu  hasa nguzo ya kuondoa umaskini, bila ya kuongeza mzigo wa ziada kwa nchi zinazoendelea au  kuwekwa vikwazo au kuhoji kuhusu matarajio yetu ya maendeleo”

Akaongeza  Afrika ingepeda kuona  pia kwamba harakati zozote za kubadili mifumo ya kiutendaji ya taasisi za Umoja wa Mataifa ikiwamo ile ya mazingira  UNEP inazingatia maslahi ya  Afrika. 

Wakati maandalizi ya mkutano huo yakiendelea, kumejitokeza   dalili za  waziwazi ambapo nchi zilizoendelea zimekuwa zikilipa uzito wa aina yake nguzo ya  mazingira na kutoa mkazo kidogo katika nguzo ya kuondoa umaskini na hasa ikizingatiwa kwamba nguzo ya mazingira inalenga kuwanufaisha zaidi  nchi zilizoendelea kuliko nchi zinazoendelea ambazo kwao nguzo ya muhimu zaidi  ni kuondokana na umaskini.

Nembo ya mkutano wa Rio+20
Mkutano wa RIO+20 utafanyika ikiwa ni miaka 20 kupita tangu mkutano mwingine kama huo  uliobeba ajenda ya Mazingira na Maendeleo maaruku kama  (Earth Summit) ulipofayika mwaka 1992 huko huko  Rio de Janairo.  Mkutano wa mwakani utatoa fursa ya kufanya tathmini ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka 1992, kipi kimefanyika, wapi pameshindikana na kwa nini na hali kadhalika kutoa mwekeleo wa miaka 20 ijayo.

ยช