.

VIJANA MWANZA WAJINOA KWA AJILI YA GWARIDE LA 'KUFA MTU' KWENYE SHEREHE ZA KILELE CHA MIAKA 35 YA CCM

Jan 31, 2012

Vijana wa CCM kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza , wakiwa katika siku ya pili ya mazoezi ya gwaride maalum la sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, sherehe hizo pia zitafanyika Kitaifa katika Uwanja huo ambapo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
 Vijana wa CCM wakionyesha ukakamavu wao wakati wa mazoezi hayo leo
 Vijana wa CCM wakifanya mazoezi jisni watakavyokuwa wakitoa saluti kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa gwaride maalum watakalocheza siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, Jumapili ijayo, Februari 5, 2012
 Makamanda wa gwaride hilo nao wakifanya mazoezi kuhakikisha kwamba watakuwa hodari siku hiyo
 Kama kawaida hakuna gwaride bila brass band. Hawa vi vijana waliokuwa wakifanya mazoezi leo kwa ajili ya gwaride hilo la Februari 5, yaani Jumapili ijayo.
 Vikosi vya vijana hao vikiwa katika mazoezi ya kutembea katika gwaride leo
Kutokana na vijana hao kuweka kambi kwenye Uwanja huo ili kufanikisha maandaloizi yao hupata chakula na chai humo humo uwanjani. Hapa msosi unaandaliwa na vijana wenzao kwa ajili yao.

KATIBU WA NEC YA CCM, OGANAIZESHENI CCM ASHA ABDALLAH JUMA KATIKA MATIBABU INDIA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma 'Mshua'  akiwa na wauguzi wa Hospitali ya MIOT nchini India baada ya kufanyiwa matibabu ya mguu kwenye hospitali hiyo, Kiongozi huyo wa CCM ambaye alienda nchini India mwishoni mwa mwaka jana hali yake inaendelea vizuri.
  Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma akiwa na  Profesa Mohandas, Mkuu wa Hospitali hiyo ya MIOT ( PICHA KWA HISANI YA  ASHA ABDALLA JUMA, INDIA).

SAMWEL DANIEL NA KAINDI TARATIBU WAMEREMETA

Wakiwa na nyuso za furaha bwana harusi Samwel  Daniel  na mkewak e Kaindi  Taratibu wakiw a kwenye pozi la  picha baada ya kufunga ndoa yao katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kibaha hivi karibuni na kufuiatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbio wa Mbezi   Luxiry jijini Dar es Salaam.
 Bwana Harusi Samwel  Daniel  na mkewak e Kaindi  Taratibu wakiwa katika pozi la upendo 
Samwel  Daniel  na mkewak e Kaindi  Taratibu wakipozi mbele ya gari lao la harusi la kifahari
.  Bibi harusi akipita juu ya migongo ya wakwe zake wakati wa kuingia ukumbini ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika familia, kabila la Wayao .
Bwana harusi akipita juu ya migongo ya wazazi wake wakati wa kuingia ukumbini wakati wa harusi yake iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Luxiry jijini ,Dar es Salaam.utamaduni huu hufanywa na watu wa lindi kabaila la wayao. 
Makaka wa bwana harusi wakiwa katika picha ya pamoja wakisherehekea harusi ya mdogo wao .
Siwa wili tena ni mwili mmoja ,bwana harusi  Samwel akiwa na mkewa Kaindi wakishuka kutoka katika mlima kilimanjaro  uliopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, walipokwenda kufanya utalii wa ndani.baada  ya kufunga ndoa yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Januari 28. (picha zote na Albert)
ยช