.

CCM YAHITIMISHA KWA KISHINDO KAMEPNI ZAKE ARUMERU

Mar 31, 2012

 Umati wa watu ukiwa kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki, katika kijiji cha King'ori leo jioni
 Rais na Mweneyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa akimnadi mgombea wa CCM Sioi Sumari leo
Watu wakinyoosha mikono kuashirikia kuunga mkono CCM

MKAPA KATIKA KAMPENI ZA CCM ARUMERU, KUFUNGA KAMPENI LEO

 Rais na Mwwnyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa akiwasili kwenye viwanja vya Patandi, kuhutubia  mkutano wa kampeni za CCM, jana. Leo atapanda jukwaani kufunga kampeni za CCM. Kulia ni Mama Anna Mkapa.
 Mkapa akisalimia wananchi baada ya kuwasili
 Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wasira baada ya kuwaili kwenye mkutano huo. Katikati ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Asha Abdallah Juma.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimia wananchi kwenye mkutano huo
 Katibu wa NEC, Mahuaisiano ya Kimataifa, Januari Makamba akisalimia wananchi kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakimshangilia Mkapa 
 Wabunge wanane wa CCM wanaosaidia katika kampeni za CCM jimbo la Arumeru Mashariki, wakisalimia wananchi kwenye mkutano huo.
 Mkapa akienda kupanda jukwaani

 Mkapa akihutubia jukwaani
 Umati wa watu ukimsikiliza Mkapa
 Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Uchaguzi CCM, Matson Chizi akimpeleka jukwaani, mgombea wa CCM Sioi Sumari
 Mkapa akimnadi Sioi
 Vijana wakiwa wametulia katika Defender la Polisi baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kujaribu kufanya fujo kwenye mkutano huo
Baadhi ya watu wakisoma nakala za toleo maalum la uchaguzi Arumeru Mashariki la Uhuru, kwenye mkutano huo

UHURU PUBLICATIONS LTD YATOA MPIGAPICHA BORA TENA MWAKA HUU

Mar 30, 2012

Khamis Saidi Hamad ambaye ni Mpigapicha Mkuu wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani yanayochapishwa na kampuni ya Uhuru Publications Ltd, usiku huu ameibuka kuwa mshindi wa nafasi ya mpigapicha bora wa Tuzo ya Umahiri wa Waandishi wa habari (EJAAT).


Ushindi huo wa Hamadi umeifanya kampuni ya Uhuru Publications Ltd kupata fursa nyingine ya kutoa mpigapicha bora mfululizo baada ya mwaka jana kutoa pia mpigapicha bora, Bashir Nkoromo.

MKAPA ATUA ARUMERU KUFUNGA KAMPENI ZA CCM

Rais na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa (kushoto) akiwa kwenye chumba cha kufikia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kupokewa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (kushoto) leo asubuhi. Wa pili kulia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

NAPE ATIA TIMU ARUMERU, AMNADI SIOI LEO

Mar 29, 2012

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimnaadi mgombea wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, leo, eneo la Makumira ambapo idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu cha Makumira walihudhuria mkutano huo
 Nape akihutubia mkutano wa kampeni kumnadi mgombea wa CCM Sioi Sumari, jimbo la Arumeru mashariki wakati wa mkutano huo wa Makumira.
Wananchi ambao wengi wao ni kutoka Chuo Kikuu cha Makumira, wakimsikiliza kwa makini Nape alipohutubia mkutano huo.

NEC YASISITIZA KUWA NI KOSA WATU KURANDA-RANDA VITUONI BAADA YA KUPIGA KURA


WANASIASA WANAOJITAPA KUIGEUZA ARUMERU TUNISIA KUKIONA: POLISI

Mar 28, 2012

Kamishna Msaidizi wa Polisi Isaya Mngullu

* Yasema imejiandaa kisawasawa  kusambaratisha vyanzo vyote vya vurugu vitakavyojitokeza


* Watakaozianzisha kuwa wa kwanza kushukiwa

USA RIVER
Zikiwa zimebakia siku tatu ufanyike uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki,  Jeshi la Polisi limewaonya wanasiasa wanaojitapa kuwa jimbo hilo litageuka Tunisia kwa umwagaji damu, na kusema kwamba jeshi hilo limejiandaa kikamilifu kukabiliana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani tangu sasa hadi mwisho wa uchaguzi.


Limesema limeshasikia kauli za baadhi ya wanasiasa wakijitapa na kuwashawishi kwenye mikutano ya kampeni kwamba vyama vyao visipopata ushindi Arumeru Mashariki patachimbika na kuwa kama Tunisia, kauli ambayo limesema ni ya hatari sana kwa wapenda amani na utulivu.


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Operesheni Jimbo la Arumeru Mashariki, Kamishna Msaidizi wa Polisi Isaya Mngullu alisema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kila hatua moja kunakuwa na doria imara zikiwemo za askari waliovaa kiraia.


Akitoa taarifa ya hali ya hali ya ulinzi na usalama katika kipindi cha kampeni zinazoendelea, Mngullu alisema jumla ya matukio 36 ya uhalifu wa kisiasa yameripotiwa na kuendelea kuchukuliwa hatua mbalimbali. 


Mngull alisema  miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kwafikisha mahakani kwa hatua zaidi za kisheria na kuyataja matuki hayo kuwa ni ya kujeruhi, matumizi ya lugha za matusi, kuchana picha za wagombea, kushambulia mwili, kuchana bendera, kutishia kuua, kuchoma moto bendera, wizi wa bendera na kuharibu mali na kwamba matukio hayo yapo kwa idadi mbalimbali.

“Mpaka sasa kesi nne namba USR/IR718.2012 CC No. 227/2012 kuharibu mali, USR/IR/721/2012 CC No. 228/2012 shambulio, USR/IR/780/2012 CC No. 241/2012 shambulio ,USR/IR/749/2012 CC No. 230/2012 shambulio zimepelekwa mahakamani" alisema Mngullu na kuongeza.

“Kesi mbili USR/IR/687/2012  shambulio la kudhuru mwili na USR/IR/694/2012  shambulio  la kudhuru mwili zimepelekwa ofisi ya mwanasheria kwa hatua za utendaji na zilizobakia zipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.".


Mbali na taarifa hiyo jeshi hilo pia limebainisha kwamba linaendelea kufanyia kazi matamko yaliyotolewa na baadhi ya vyama vya siasa vinavyoshiriki kufanya kampeni kwa kutumia lugha za matusi, kudhalilishana, uchochezi na vitisho kwa vyombo vya dola kuwa ushindi usipopatikana  Arumeru patachimbika na kuwa mfano wa Tunisia.

Mngullu alisena Jeshi la polisi limestushwa sana na kauli hizo kutolewa na wanasiasa wawapo majukwaani huku Asasi za kiraia zinazopigania haki za binadamu na utawala bora hususani wanaharakati wakiwa wamekaa kimya na kushindwa kujitokeza na kukemea vitendo hivyo badala yake kusubiri kutoa matamko ya kulaumu polisi pale linapoingilia kati na kuchukua hatua za kurudisha hali ya utulivu na amani kutokana na vitendo vya uvunjifu amani vinavyosababishwa na kuchochewa na viongozi.


Mbali na kuonyesha kusikitishwa, jeshi hilo limekemea na kuvitaka vyama vya siasa vinavyojifanya maandamano na misafara batili mara baada ya kumaliza mikutanio yao ya kampeni kuacha mara moja kwani kuendelea kufanya hivyo ni kuvunja sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.

Mngullu alisema, zipo taarifa kwamba moja ya vyama ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa kufanya maandamano ni CHADEMA na kutoa mfano kwamba  baada ya mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Jumatatu mjini Usa River, walionekana wakiongoza misarafa ya wanedesha pikipiki kuzunguka mitaani wakiandamana na malori yao Fuso ya chama hicho jambo ambalo lingeweza  kuhatarisha amani.


Kamishna Msaidizi Mngulu aliwataka wanasiasa wanaohamasisha wafuasi wao, wakereketwa na wanachama kulinda kura za mgombea wao kuacha mara moja kitendo hicho kwani kila Chama kimeweza kutoa wakala ambaye kimemuamini kwa kazi hiyo. 


“Wanachama hawana sababu ya kuhamasishana kulinda kura kwani kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 80 (2) (G) cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ya Mwaka 2010 inabainisha wazi kuwa kila Chama kitakuwa na wakala wake wa kuhakiki na kulinda kura za mgombea ndani ya kila chumba cha kupigia kura,” alisema Kamishna Msaidizi Mngulu. 


Kamishna Msaidizi Mngulu alivitaka vyama vya siasa kujipanga baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo, ambapo alikitaka Chama kitakachokuwa kimeshinda kuainisha mapema sehemu, muda na taratibu za kusherehekea ushindi wao bila kuathiri na kubughudhi shughuli au mali za watu wengine. 


Uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki, utafanyika Aprili Mosi mwaka huu, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Jeremiah Sumari mapema mwaka huu ambapo jumla ya vyama vinane vimeweka wagombea.

NI KOSA KURANDA RANDA VITUONI BAADA YA KUPIGA KURA:JAJI LUBUVA


Jaji Mstaafu Damian Lubuva

 USA RIVER
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeonya kuwa ni kosa kisheria watu kuranda randa au kukaa makundi kwenye vituo vya uchaguzi baada ya kupiga kura.


Onyo hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, katika mkutano wake na viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki.


"Tumekuwa tukisisitiza kila mara kwamba ni kosa kisheria mtu au kundi la watu kuzagaa kwenye vituo baada ya kupiga kura. Ndugu viongozi sisitizieni sana wananchi kwamba ni vema baada ya kupiga kura kila mmoja arudi nyumbani kusubiri matokeo", alisema Jaji Lubuva.


Alisema, ni kufanya kosa lisilo la lazima wapiga kura kubaki vituoni au kuranda randa au kuweka vikundi kwenye vituo, kwa sababu wapo mawakala waliowekwa na vyama vyao ambao ndiyo wenye dhamana ya kulinda kura.


Jaji Lubuva alisema, vyama vyote vinapaswa kutaja mawakala wao mapema badala ya kuwaweka katika hatua za mwisho jambo ambalo alisema linaweza kusababisha uwezekano wa chama kukosa wakala.


Alisema, kila chama kina wajibu wa kuweka wakala wake ambaye kitamgharamia na kwamba kutokuwepo wakala kwa chama chochote hakutaathiri mwenendo wa upigaji kura au kuathiri kutangazwa matokeo.


Jaji Lubuva alisema, maandalizi ya uchaguzi huo ambao utafanyika Aprili Mosi mwaka huu, yamekamilika na TUme hiyo imejitahidi kuhakikisha hazitokei kasoro zisizo za lazima.


Katika uchaguzi huo, vyama vinane vimeweka wagombea kama ifuatavyo, majina ya vyama vyao yakiwa kwenye mabano,Mazengo Abdallah Adam (AFP),Sumari Sion Solomon (CCM),Nassari Joshua (CHADEMA), Muhammad Abdalla Mohammed (DP), Hamis Juma Kiemi(NRA),Kirita Shabani Moyo (SAU),Chipaka Abraham Moova (TLP) na Charles Mosses Msuya( UDP).


Uchaguzi huo unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Jeremia Sumari kufariki dunia mapema mwaka huu.

RAZA AAPISHWA LEO


ZANZIBAR
Mohammedraza Dharamsi aliyekuwa mwakilishi mteule jimbo la Uzini, leo ameapishwa rasmi na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho tayari kushika mikoba ya kuongoza jimbo hilo.


Mohammedraza maarufu kama Raza aliapishwa leo asubuhi mida ya saa nne asubuhi, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi.


Raza ametinga Barazani baada ya kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwezi uliopita ambapo alipata ushindi wa asilimia 61.


Akizungumza  baada ya kuapishwa Raza amewashukuru wananchi wa Uzini kwa kumwamini na hatimaye kumchagua kuwa mwakilishi wao.


"Sina cha kusema zaidi lakini nawashukuru wananchi wa Uzini kwa kuniamini na kunipa dhamana hii kubwa ya kuwaongoza hivyo naamini sitawaangusha,''alisema.


Alisema wakati wa mchakato wa kupata jina la moja la mgombea ndani ya chama walikuwa  14 huku kati yao 13 wakiwa wazawa wa jimbo hilo na mmoja(yeye) akiwa si mzawa.
  
"Licha ya kuwepo na wazawa wa jimbo hilo, bado wanachama na baadae wananchi wa Uzini walinihitaji mimi kuwa mwakilishi wao kwa kuwa naweza kuwatumikia kwa moyo mkunjufu,''alisema.


Katika kudhihirisha furaha yake, Raza amesema mshahara wake wa kila mwezi atautoa kwa wananchi wa jimbo hilo kutekeleza miradi ya maendeleo akisema anafanya hivyo kwa sababu hakuihitaji nafasi hiyo kwa ajili ya kuganga njaa bali kusaidia wananchi.

KAMATI KUU YA CCM YAKETI LEO DAR

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, leo Ikulu mjini Dar es Salaam. Kushoto ni wajumbe wa Kamati hiyo wakimsikiliza. Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilitarajiwa kujadili wagombea wa ubunge Afrika Mashariki. (Picha na Freddy Maro)

TANGAZO RASMI KABISA


RAIS WA KAMPUNI YA UJERUMANI YA UTAFITI WA MAFUTA AKUTANA NA PINDA DAR


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana Rais wa kampuni ya utafiti wa mafuta ya  Europe and Africa Schlumberger Seaco Inc ya Ujerumani, Bw. Sherif Foda  kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 27,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAZA KUPISHWA LEO BARAZANI

MOHAMMED RAZA
MWAKILISHI  mteule wa Baraza la Wawakilishi jimbo la Uzini, Mohammed Raza Daramsi ataapishwa leo katika kikao cha Barza la Wawakilishi kitakachoanza leo mjini Zanzibar.


Raza ataapishwa kufuatia kuibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, uliofanyika mapema mwaka huu na Raza kuibuka na ushindi wa asilimia 61.

MRADI WA MAJI WA VODACOM KUNUFAISHA WANAKIJIJI 4,000 DODOMA

Mar 27, 2012

Mwanamke akitishwa ndoo ya maji wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia Jamii (Vodacom Foundation) imekabidhi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 40 katika kijiji cha Inyumbu ikiwa ni mwendelezo wa azma yake ya kusaidia jamii hapa nchini.

Kukabidhiwa kwa mradi huo kunapunguza shida ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi zaidi ya 4,000 wa kijiji cha Inyumbu na maeneo jirani.

Akipokea mradi huo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Yona Ngobito aliishukuru kampuni ya Vodacom  kwa kuwekeza shilingi Milioni 40 ili kuokoa maisha ya wananchi ikifahamika wazi kuwa maji ni bidhaa muhimu na  nyeti katika maisha ya binadamu.

"Kila msaada ni muhimu kwa walengwa husika ila tunapozungumzia maji tunagusa moja kwa moja uhai wa binadamu, hili ni jambo jema kwenu wanakijiji wa Inyumbu ambao sasa wanawake na wasichana wanaweza kutumia muda mfupi kupata bidhaa hiyo na kutumia muda wa ziada kufanya shughuli nyengine za kifamilia"Alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa kijiji ametumia pia fursa hiyo kuwasihi wanakijiji kuona thamani ya mradi huo na njia pekee ya kurudisha shukrani kwa Vodacom ni kuutunza mradi huo ili uwasidie kwa muda mrefu zaidi.

"Ndugu zangu hasa wakina mama tukitambua shida ambayo tulikuwa nayo hapo kabla ya kuletewa mradi huu na Vodacom ni wazi tutaona thamani yake na kila mmoja atakuwa mlinzi wa mradi huu dhidi ya aina yoyote ya uharibifu, hiyo si tu kwamba itatusaidia kuwa na uhakika wa maji bali tutawapa nguvu Vodacom kurudi tena kuangalia eneo jingine la kutusaidia"Aliongeza Ngobito.

Nae Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,alisema Vodacom Foundation imekua ikithamini maisha ya watanzania wengi na hivyo kujitolea katika kusaidia na kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii hapa nchini.

Aliongeza kuwa kutokana na kwamba Mkoa wa Dodoma una ukame katika baadhi ya maeneo yake na hivyo kuleta changamoto katika upatikanaji wa maji safi na salama kwamatumizi ya binadamu hasa maeneo ya vijijini jambo lililoigusa kampuni ya Vodacom kupitia mfuko huo na kufikia uamuzi wa kufadhili mradi huo wa maji kupitia teknolojia ya upepo.
.
"Katika jitihada zetu za kuboresha ustawi wa jamii za watanzania kwa kuwa washirika wa huduma za kijamii nchini zimetufikisha hapa katika kijiji cha Inyumbu kukabidhi mradi huu, ni matumaini yangu kwamba sasa mama zangu wa hapa kijijini wamefurahi kwa kupunguziwa hali iliyokwepo hapo  awali ya kutumia muda mrefu kusaka maji kwa shughuli mbalimbali za kifamilia"Alisema Mwakifulefule.

Kila mwaka tunatenga fedha kusaidia maeneo mbalimbali ya kijamii hasa elimu,afya, maji,mazingira na ujasiriamali, tunafanya hivyi tukitambua kuwa biashara kwetu ni sehemu moja ila namna tunavyokuwa karibu kusaidia wale wanaotuzunguka katika baishara zetu ni jambo moja muhimu sana katika shughuli zetu, tutaendelea kufanya hivyo tukiamini kwamba azma yetu ya kubadili maisha ya wananchi inatekelezeka"Aliongeza Mwakifulefule.

Vodacom kupitia Vodacom Foundation iliufandhili mradi huo kwa shilingi Milioni 40 kupitia Mamlaka ya maji ya kijiji cha Inyumbu kwa kushirikiana na mradi wa maji wa C.P.P.S,

BARAZA KUU LA USALAMA LA LAANI MAPINDUZI YA KIJESHI NCHI MALI


Na Mwandishi Maalum
New York
Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa  Mataifa, limelaani vikali mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na askari wa chache dhidi ya serikali ya kidemokrasia nchini Mali. Na limewataka wanajeshi hao kuachana na vitendo vya kihalifu na fujo na kurejea katika makambi yao.

 Taarifa  iliyotolewa na  Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Marchi  Balozi wa  Uingereza Bw. Mark Lyall Grant (pichani) amesema. “  Baraza la Usalama linalaani mapinduzi hayo na linawataka wanajeshi kurudi katika makambi yao na  linatoa wito  wa kurejeshwa kwa  utaratibu wa Katiba  na kufanyika kwa uchaguzi kama  ilivyokuwa imepangwa.

Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana siku ya jumatatu ambapo lilijadili kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika Kanda ya Afrika ya Sahel, ambapo lilisema kwamba kuongezeka kwa makundi  yenye silaha na magaidi pamoja na kuzagaa kwa silaha kumeongeza hali ya wasiwasi katika kanda hiyo.

 Wiki iliyopita baadhi ya wanajeshi wa nchi  Mali  wakiongozwa  Kapteni Amadou Haya Sanogo walitangaza kuipindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure ambaye mpaka sasa hajulikano aliko.

Katika mkutano huo ambao uliwahusisha wajumbe 15 wanaounda Baraza   Kuu la Usalama,  Baraza hilo pia limelaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya makundi ya waasi ya kuvivamia vikosi vya serikali na kuwataka waasi hao kusitisha  aina zote za vurugu na kutafuta  ufumbuzi wa amani kwa njia ya mazungumzo ya kisiasa. Aidha   Baraza hilo  limesisitiza haja ya  kuzingatia na kuheshimu uhuru, umoja na mipaka ya nchi.

Tayari Umoja wa Afrika ( AU) umekwisha kutanga kutoyatambua mapinduzi hayo, huku  baadhi ya nchi  ikiwamo  Marekani  ikitangaza  kusudio la kusitisha misaada   kw anchi hiyo , nchi  ambayo uchumi wake kwa asilimia kubwa  unategemea sana misaada kutoka nchi wahisani.

Kuhusu hali tete ya kanda ya Sahel, Baraza limebainisha kuwa hali ya ukame , uhaba wa chakula na kurudi kwa  maelfu ya watu kutoka Libya kumeongeza hali ugumu wa maisha kwa watu wa eneo hilo. Hali ambayo imesababisha  maelfu ya   wananchi wa eneo hilo kukimbilia  katika nchi za jirani kutafuta hali bora ya maisha.

Kutokana na hali hiyo, Baraza  Kuu la  Usalama la Umoja wa Mataifa,  limetoa wito kwa  mamlaka za kitaifa na kimataifa, kikanda na masharika ya  misaada ya  kibinadamu  kuchukua hatua za haraka kuimarisha juhudi za kuwasaidia wananchi wa eneo hilo.

TUWE MACHO NA ONGEZKO LA AINA MPYA YA UTUMWA NA UBAGUZI WA RANGI- MIGIRO

Kikundi cha Utamaduni cha Cameroon kilitumbuiza katika maadhimisho hayo, kwenye Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa  Baraza kuu la  Umoja wa Mataifa

Na Mwandishi Maalum
New York
Ikiwa ni zaidi ya miaka 200 imepita tangu biashara ya utumwa na utumwa ulipokomeshwa. Jumuiya ya Kimataifa, imetakiwa kuwa macho  dhidi  ongezeko kubwa la   aina mpya ya utumwa unaojikita katika misingi ya  ubaguzi wa rangi, biashara haramu ya binadamu, utumwa wa madeni, unyanyasaji  na udhalilishaji wa kijinsia, ndoa za utotoni  na utumiaji wa watoto katika vita.

Tahadhari hiyo imetolewa  siku ya jumatatu wiki hii na   Naibu   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha- Rose  Migoro wakati Umoja wa Mataifa ulipoadhimisha siku ya kimataifa ya  ukomeshaji wa biashara ya utumwa na utumwa, maadhimisho ambayo hufanyika   Marchi 25 ya kila mwaka.

Kauli mbiu ya mwaka  huu katika maadhimisho hayo ni “kuwaenzi  mashujaa , wapinzani  na waathirika wa  biashara ya   utumwa”. Pamoja   hotuba  maadhimisho hayo  yalipambwa  na kikundi cha utamaduni kutoka nchini Cameroon.

Migiro amesema, licha ya kwamba  kumekuwapo na sheria mpya na mbinu mpya  na bora za kukabiliana na vitendo vya   ukiukwaji wa haki za binadamu. Hata hivyo anasema. “  Ni lazima tukubali kwamba   kunaongezeko la vitendo vinavyoashiria wazi kuwapo kwa ubaguzi kwa misingi ya rangi katika maeneo mengi duniani”.

Na kuongeza kwamba  kauli zinazoashiria ubaguzi wa rangi  zimekuwa zikiongezeka kupitia  majukwaa  ya kisiasa, katika baadhi ya vyombo vya sheria, mashirika na katika matumizi ya teknolojia za kisasa za mawasiliano ambapo  vyombo hivyo vimekuwa vikitumika kueneza dhana hasi ya kwamba rangi moja ni bora dhidi ya rangi nyingine.

 Naibu Katibu Mkuu amesema kuwa  kila mtu anao wajibu wa pamoja  wa kuwa macho juu ya ongezeko la vitendo hivyo vya  ubaguzi wa rangi na aina mpya ya utumwa.

Akabainisha kwamba maadhimisho hayo licha ya kuwakumbuka mamilioni ya waafrika walioathiriwa na  janga  la kutisha la biashara ya utumwa na utumwa. Maadhimisho  hayo ni  lazima pia yatumike kama sehemu kujifunza sababu na matokeo ya biashara ya utumwa, ukandamizaji na  ubaguzi wa rangi. ubaguzi ambao uliifanya  rangi  moja ya  binadamu kujiona kuwa ni bora zaidi dhidi ya rangi nyingine.

Akamaliza kwa kusema “ kwa kupitia  siku hii basi sote tuonyeshe dhamira ya kukabiliana na kupambana na ubaguzi wa rangi na kujenga jamii bora kwa kuzingatia usawa , haki na mshikamano”.

Pamoja na   Naibu Katibu Mkuu  kuzungumza katika maadhimisho hayo, Rais wa  Baraza  Kuu la 66 la  Umoja wa Mataifa, Bw. Nassir Abdulaziz Al-Nasser naye alizungumza ambapo kama ilivyo kuwa kwa Naibu Katibu Mkuu, alisisitiza haja na umuhimu wa  Jumuia ya Kimataifa kuunganisha nguvu dhidi ya aina mpya ya utumwa.

Akasema  jumuia ya kimataifa inapashwa kujifunza  kutoka yale yaliyojitokeza katika biashara ya utumwa na utumwa na kuhakikisha  matukio yale ya kutisha yalioathiri na kuudhalilisha utu  na hadhi ya Mwafrika  hayajirudi   kwa namna  moja ama nyingine au katika mfumo wowote ule.

Akabainisha kwamba mwaka 2007 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  liliitenga  Marchi 25 ya kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya kuwakumbuka  wa Wafrika zaidi ya milioni 28 walioathirika na  janga kubwa la  biashara ya utumwa na utumwa kupitia  bahari ya  Atlantik.

Aidha Bw. Al- Nasser amezikumbusha nchi wanachama ambazo   hazijachangia mfuko wa ujenzi wa mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya utumwa kufanya hivyo.

Mbali ya Rais wa Baraza   Kuu la Umoja wa Mataifa, wazungumzaji wengine katika maadhimisho hayo walikuwa ni  Balozi Chitsaka Chipaziwa  wa  Zimbabwe aliyezungumza kwa niaba ya nchi za Afrika,  Balozi Jane Chigiyai  wa Micronesia aliyezungumza kwa niaba ya nchi za Asia na Pacific, Balozi Petrika Jorgji wa Albania aliyezumgumza kwa  niaba ya nchi za  Ulaya  Mashariki na Balozi Dessima Williams ambaye alizungumza kwa niabya ya  nchi za  America ya Latini na Visiwa vya  Caribbean.

Wengine waliozungumza ni Balozi Daniele Bodini wa San Marino aliyezungumza kwa niaba ya nchi za Ulaya Magharibi na nchi nyingine, na Balozi Rosemary DiCarlo aliyezungumza kwa niaba ya Marekani. Wakati  Dkt. Rick kittles  ambaye ni Mkurugenzi wa African Ancestry,Inc yeye alitoa mada kuhusu historia ya utumwa na madhira yake kwa mtu  mweusi na matumizi ya vinasaba katika  kuwasaidia wamarekani  wenye asili ya Afrika  kutambua asili ya kule walikotoka.
Maadhimisho  hayo ya  kumbukumbu  ya  biashara ya utumwa na utumwa yanafanyika kwa juma zima  yakihusiaha pia, midahalo ya wanafunzi, asasi zisizo za kiserikali, maonyesho ya sanaa mbalimbali zinazohusiana na utumwa, filamu makala mbalimbali  pamoja na vyakula vya asili ya Afrika.

TAMASHA LA NANI MKALI ROMA VS IZZO NDANI YA DAR LIVE

THOMAS MASHALA AJIFUA KUMKABILI DELEMAN GALILE MWEZI UJAO

Kocha wa  wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

MICHUZI BLOG YAANZISHA HUDUMA YA 'WIFI HOTSPOTS' KWA DAR

Muhidini Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi. Kwa kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote.

Akikaririwa katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”.

Akiwa ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii zinatakiwa kuwafikia wanajamii kwa urahisi. Tovuti nyingi zinatembelewa na Watanzania waliopo nchi za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii siyo haki. Kama nina uwezo kupata taarifa kwenye tovuti ya Michuzi ni jukumu letu kama kampuni kuwawezesha watanzania waliopo nchini pia kupata huduma. Watanzania tunatakiwa kuwa na utamaduni wa kusaidiana na kupeana moyo na hii itasaidia kukuza uchumi wetu sio tu kununua na kuuza bidhaa kutoka nje.

Kwa pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo tu na wanaamini kwamba hili wazo litafuatwa na wengine. Kwa msisitizo Bwana Michuzi aliongea “Lazima tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu. Tumechukua hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga kwenye mapinduzi haya na kufanikisha”.

Kutembelea tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye Ipad, Tablet, Simu au Laptop. Tafuta Michuzi blog Wifi, Unganisha ,fungua browser yako uipendayo mfano Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na nenda kwa Issa Michuzi.blogspot.com.

Kama hautaona tovuti ya Michuzi Wifi, tafadhali wasiliana na Uhuruone kwa email ifuatayo, issa.michuzi@uhuruone.com au piga simu namba 255779477477 ili uweze kuunganishwa.

MKUTANO WA CCM KATIKA MJI MDOGO WA USA RIVER WAITIA KIHORO CHADEMA

Mar 26, 2012

*Yalazimika kuufanyia doria kwa helkopta na baadaye kuzusha maandamano ya pikipiki na fuso zao mitaani wakiimba 'peoples power yao' kufariji mashabiki wake.
Mgombea wa CCM Sioi  akisalimia maelfu ya watu kwenye mkutano huo
Mkutano wa CCM wa kampeni iliofanya leo jioni, umeonekana kuwatia kiwewe CHADEMA ambapo wamelazimika kuufanyia doria kwa helkopta na kama haitoshi ikabidhi wafanye maandamano ya pikipiki na fuso zao moitaani kuwafariki mashabiki wake ambao walijikunyata baada ya kishindo cha mkutano huo wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa mpira wa Ngarasero na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.

Mkutano huo ulipata wananchi wengi baada ya kuhudhuriwa hata na wananchi wa kawaida ukiachilia mbali wana-CCM waliokuwa wamejipambanua kwa kuvaa sare za chama kama Tshits, kofia au vitambaa.

Kutokana na wingi wa watu eneo la kusakatia kambumbu la uwanja huo lilifurika hadi watu wengine kuwa nje kabisa ya uwanja.

Katika hali inayoonyesha kwamba kulikuwa na mawasiliano na kati ya viongozi wa CHADEMA waliokuwa wakifanya kampeni kwa helkopta na watu waliokuwa pembeni mwa mkutano huo, baada ya mgombea wa CCM Sioi Sumari kupanda jukwaani, kiasi cha dakika mbili hivi helkopta ya CHADEMA ilipita eneo la mkutano kujaribu kushawishi watu waishangilie.

Lakini kutokana na mvuto mkubwa uliokuwa kwenye mkutano huo wengi waliendelea kumshangilia mgombea wa CCM, huku watu kadhaa waliokuwa pembeni wakijaribu kushangilia helkopta hiyo.

"Tunatisha. Hao wamepantwa presha waliposikia kwamba uwanja huu walimokuwa juzi, sisi tumefunika ndiyo maana imebidi sijui ni Mbowe au Slaa waje kujionea wenyewe" alisema Mratibu wa kampeni za CCM Mwigulu Nchemba baada ya helkopta hiyo kupita.

Juzi CHADEMA walipofanya mkutano kwenye Uwanja huo, ingawa walipata watu, lakini hawakuweza kufikisha idadi ya wale waliohudhuria mkutano wa leo wa CCM. 
Mgombea wa CCM Sioi Sumari akiwapungia mikono wananchi alipowasili kwenye mkutano huo. Mbele yake (kushoto) ni Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde

DK SHEIN AWAAPISHA KATIBU MPYA WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA MKUU WA KIKOSI CHA VALANTIA LEO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Yahya Khamis Hamad,kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,jana baada ya kumteuwa kushika nafasi hiyo,hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Luteni Kanali Mohamed Mwinjuma Kombo,kuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia  Zanzibar,jana baada ya kumteuwa kushika nafasi hiyo,hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM ZANZIBAR CHAFANYIKA JANA

Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,alipowasili viwanja
vya Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar jana kuhudhuria katika cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa,ya Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa mikutamo wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.  

Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM   Zanzibar, wakipitia makabrasha yenye agenda kabla ya kuanza kwa kikao hicho jana katika ukumbi wa mikutamo wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar


Mjumbe wa Kikao cha  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM  Zanzibar, Asha Abdallah Juma, akiwasalimia wajumbe wenzake  kabla ya kuanza kwa kikao hicho jana katika ukumbi wa mikutamo wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.   {Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu}

PINDA KUPOKEA KOMBEA LA MICHUANO YA UEFA KESHO

Mar 25, 2012

Kombe la Michuano ya UEFA kesho Jumatatu, litatua nchini na kukabidhiwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye atalipokea kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.

Kombe hilo litatua nchini likiwa katika safari yake ya kuzungushwa nchi mbalimbali Duniani.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam, imesema shughuli ya makabidhiano hayo itaanza saa 1.30 asubuhi na kuwaomba waandishi wa habari na wapigapicha za habari  watakaokuwa wametumwa na vyombo vyao vya habari kuwa wamewasili kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, eneo la Magogoni, mida hiyo.

MKUTANO CLIMATE CHANGE

Mar 23, 2012

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng Ngosi Mwihava akiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Mkutano wa wadau Kupitia na kujadili Mwongozo wa ujumuishaji wa Masuala ya kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi inayofanyika Hotel ya Giraffe Ocean View Mjini Dar es Salaam (Picha na Ali Meja)

TMK WANAUMEFAMILY KUKAMUA MEDIA DAY

Kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Family la jijini Dar es Salaam ni miongozi mwa burudani zitakazokuwepo kwenye bonanza la vyombo vya habari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Bonanza hilo litafanyika  Machi 24 mwaka huu ukumbi wa Msasani Beach Club, Dar es Salaam, huku TASWA ikiamini litakuwa bora na la uhakika.

Licha ya Wanaume Family, burudani  nyingine itakuwa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, ambapo wadhamini ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia burudani, michezo na mambo mengine yawe ya aina yake.

Bonanza litaanza saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku, ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na michezo.

Mgeni rasmi katika bonanza hilo atakuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta.

Lengo la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa mwaka, likiandaliwa na TASWA

George John
Mwenyekiti Kamati ya Bonanza
23/03/2012

POLISI ASHINDA MILIONI KUMI ZA M-PESA

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imemkabidhi hundi mshindi wa zawadi ya kitita cha Shilingi Milioni Kumi wa droo ya mwezi ya promosheni ya M-PESA Bw Peter James Kilalo.

Bw. Kilalo (kushoto) amekabidhiwa hundi hiyo jijini Dra es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacoim Tanzania Bw. Rene Meza Kushoto)  katika hafla fupi iliyohudhuriwa pia na waandishi wa habari.

Akipokea hundi yake Bw. Kilalo ambae ni Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Dar es salaam ameshukuru kw akuibuka mshindi jambo ambalo amesema hakulitegemea.

"Kwa kweli mimi ni mteja mzuri sana wa M-PESA lakini kweli sikutegemea kwamba ningeibuka mshindi, ila sasa ninapopokea hundi hii naamini kwamba nimeshinda na fedha hizi Milioni kumi ni zangu"Alibainisha Bw. Kilalo.

Alipoulizwa namna alivyojipanga kutumia pesa hizo Bw Kialalo alijibu" Jamani mimi ni masikini na sikuwahi kuota kwamba ipo siku nitashinda kiasi kikubwa cha fedha namna hii hivyo jambo kubwa kwangu kwa wakati huu ni kwanza kuacha akili yangu itulie kabisa ndio niamue niziwekeze wapi ili zinikwamue kimaisha"Alisema

"Nina mawazo kadhaa ya biashara ambayo nimekuwa nikiyawaza kama njia ya kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha hivyo hizi pesa nitazielekeza huko ila baada ya akili yangu kwanza kutulia kutoka katika hali ya furaha niliyonayo sasa."Aliongeza

Mshindi huyo ametumia pia fursa hiyo kuwashauri watanzania kutumia huduma ya M-PESA kwa kuwa mbali na kwamba imerahisisha maisha katika utumaji na upokeaji fedha mijini na vijijini bado wanaweza kuwa katika nafasi ya kushinda kama yeye

Awali  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema promosheni hiyo imelenga kuwawezesha wateja wa M-PESA kubadili masiha kutokana na wanavyotumia huduma hiyo.

"Promosheni hii tulizindua mwezi uliopita tukilenga kuwawezesha wateja wetu kujishindia zawadi za fedha taslimu, kiasi cha Shilingi Milioni 480 kinashindaniwa ambapo hadi sasa wateja zaidi ya 4,000 wameshajinyakulia zaidi ya Shilingi Milioni 120" Alisema Bw. Rene

AmesemaVodacom inatambua umuhimu wa huduma ya M-PESA katika maisha ya kila siku ya wananchi na hivyo wakati wote imekuwepo mikakati imara ya kuiwezesha huduma hiyo kuendelea kuwa bora zaidi,salama na ya kuaminika sokoni.

"Matumizi ya huduma ya M-PESA hapa nchini yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana, kiwango cha wananchi kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo ya bidhaa mbalimbali kupitia M-PESA ni kikubwa jambo ambalo linakuwa rahisi zaidi kutokana na mtandao mpana tulionao wa mawakala wanaofikia 20,000 mijini na vijijini." Aliongeza Bw Rene

Promosheni hiyo itadumu kwa siku tisini kutoka Februari 13, 2012 hadi May 13, 2012. Mbali na kutoa mshindi mmoja wa shilingi milioni kumi kila mwezi pia kila siku washindi mia moja hujishindia Shilingi 50,000 kila mmoja. 

CHEKA VS MAUGO WAONESHWA MKANDA WA UBINGWANa Mwandishi Wetu
Waandaji wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo (pichani) jana walionyeshwa rasmi mkanda huo ambao wataushindanaia Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.


Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.


Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju alisema kuanikwa kwa mkanda huo kutaashiria kupamba moto kwa ambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.


"Tunauanika mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda," alisema Kaike.


Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.


Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.


Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.


"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D.SEKONDARI YA ACTAS DAR YASITISHA KWA WIKI MBILI HUDUMA YA BWENI KWA BAADHI YA WANAFUNZI

Na mwandishi wetu
UONGOZI wa Sekondari ya Actas iliyopo Mbezi Jogoo mjini Dar es Salaam, umesitisha huduma ya bweni kwa baadhi ya wanafunzi wake kwa muda wa wiki mbili.

Wanafunzi hao ni wale wanaoishi jijini Dar es Salaam huku kwa wale wanaotoka nje ya jiji wataendelea kupatiwa huduma hiyo kamakawaida.

Hatua hiyo inatokana na ukarabati wa baadhi ya mabweni na uhaba wa maji shuleni hapo na maeneo jirani, kufuatia kuharibika kwa miundombinu ya usambazaji.

Akizungumza na waandishi wa habari mjiniDar es Salaam, jana Meneja wa Shule hiyo Chacha Mghituti, alisema huduma za chai na chakula cha mchana kwa wanafunzi hao zitaendelea kutolewa kama kawaida.

Alisema huduma ya bweni kwa wanafunzi hao itasitishwa kwa wiki mbili ili kutoa fursa kwa shule kufanya marekebisho kwa lengo ili kuboresha mazingira na kuendelea kutoa huduma bora zenye viwango vya juu.

Alisema huduma ya bweni imesitishwa kuanzia juzi na kwamba, itarejea tena Aprili 16, mwaka huu.

“Tumesitisha huduma ya bweni kwa baadhi ya wanafunzi waishio hapa Dar ili tupate fursa ya kufanyia ukarabati baadhi ya majengo na kuboresha huduma za maji. Kuna tatizo la maji katika maeneo ya shule na jirani hivyo, ni lazima tuchukue hatua ili kudhibiti hatari inayoweza kutokea,” alisema Mghituti.

Alisema tayari wamewasiliana na wazazi, ambao wameafiki na kupongeza uamuzi huo wenye lengo la kulinda afya za wanafunzi.

Alisema ukarabati huo unaendelea kufanyika kwa kasi ili wanafunzi waweze kurejea kwa muda uliopangwa.

“Tunajali afya za wanafunzi na walimu wetu, kuna tatizo la maji kutokana na miundombinu kuharibika, hivyo wanafunzi waishio hapa mjini watakuwa wakitoka nyumbani kuja shuleni, lakini huduma za chakula zitaendelea kamakawaida,” alisema.

Baadhi ya wazazi na majirani wanaozunguka shule hiyo, wamesema kumekuwepo na tatizo kubwa la maji katika maeneo hayo na kwamba, uamuzi wa shule ni muafaka.

“Hawa wanajali afya za wanafunzi, wamechukua uamuzi mzuri na hawana budi kupongezwa kwani, ingekuwa wengine wangeendelea kuwajaza wanafunzi ili wapate fedha wakati kuna matatizo,” alisema Benson John, mkazi wa Mbezi.

MAJIMAREFU AWAKA KUUNGANISHWA NA NASSARI WA CHADEMA KATIKA PICHA ANAYODAI NI FEKI

Mar 21, 2012

'Picha hii nilipigwa nikiwa na huyu mbunge mwenzangu, Vicent Nyerere (kulia), lakini huyu wa kushoto (Joshua Nassari) hakuwepo karibu yangu kabisa! Yeye alikuwa mbali akiamrisha vijana wanichome moto tena akiwa na hasira, tofauti na anavyocheka katika picha hii. Huu ni mchezo mchafu wa kuunganisha picha kwenye kompyuta uliofanywa na CHADEMA na kwa makusudi gazeti hili likaichapisha, baada ya kuona kwamba hatua aliyofanya Nassari ya kutaka niuawe jana ni mbaya sana. Nitalishitaki gazeti hili". Analalamika Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani wakati akionyesha picha inayomuonyesha akiwa katika furaha ya hali ya juu yeye, Nyerere na Nassari. Picha hiyo imechapishwa leo ukurasa wa kwanza gazeti la Mwananchi.
Picha yenyewe anayolalamikia Profesa Majimarefu ndiyo hii kama tulivyojaribu kuinakili kutoka gazeti la mwananchi. Mdau hebu itazame kwa makini, je ni halisi au feki,  hasa ukitazama vizuri kwenye kwapa la Nassari lililokutana na Ngonyani? Pia tunamkaribisha mpigapicha wa picha hii, Edwin Mjwahuzi kama hatajali atupe picha 'orijino' ya hii tuliyonakili kwa ajili ya kuthibitisha ukweli.

MEDIA ADVISORY

Journalists are invited to cover the NEPAD Colloquium and Congress live via webcast on 28th Wednesday, March 2012

ADDIS ABABA, Ethiopia, March 20, 2012/ -- Journalists are invited to cover the NEPAD Colloquium and Congress live via webcast on 28th Wednesday, March 2012.
The Colloquium will provide a platform for candid exchange on NEPAD as the African-owned development strategy adopted in 2001 to drive the Continent’s political and socio-economic transformation.


When:
28th Wednesday, March 2012
7:00 GMT to 17:00 GMT 
Time converter: http://bit.ly/GBMB5Z       

Programme:

10h00 – 10h15           Official Opening Session

Opening remarks by:

•          Executive Secretary (UNECA) as host institution
•          CEO, NEPAD Agency
•          President of the Pan African Parliament
•          AUC Chairperson
•          AU Chairperson (President of Equatorial Guinea)

10h15 – 10h30           Key note address by:

•          H.E. Meles Zenawi, Prime Minister of Ethiopia and Chairperson of the NEPAD Heads of State and Government Orientation Committee (HSGOC)

10h30 – 10h45           Introduction of high level panel of African eminent persons

11h00 – 12h45           Plenary I: High level panel discussion

Theme: ‘NEPAD Journey so far – Challenges, Gaps and Prospects’
                       
Open Discussion

12h45 – 13h00           Presentation by John Zogby on People’s voices on NEPAD

14h00 – 16h30           Plenary II: High level panel discussion

Theme: ‘NEPAD in the next decade’

Open Discussion


16h30 – 16h45           Launch of NEPAD related publications 

-          ‘NEPAD - A continental thrust’ – by NEPAD Agency
-          ‘The Role of the Private sector in NEPAD implementation’ (by NEPAD Agency and UNECA)
-          ‘Newsroom guide for reporting NEPAD’
-          ‘The New Harvest. Agricultural Innovation in Africa’ by Calestous Juma

16h45 – 17h00           Governing the NEPAD Programme – Chairperson, NEPAD Steering Committee
Representative of REC
Representative of AU Member States
Representative of Partner institution
Representative of Women’s groups
Representative of African Youth

17h00 – 17h15           Summary of highlights – Way ahead for the NEPAD Programme

AUC Commissioner for Economic Affairs and NEPAD CEO

17h15 – 17h45           Closing remarks

AUC Chairperson

17h45 – 19h00           NEPAD Agency exhibition

Background: 
2011 was NEPAD’s 10th Anniversary since its foundation. Over the past ten years, major developments have taken place to advance the NEPAD agenda including the recent integration of NEPAD into the African Union (AU) structures and processes.  As part of its celebrations, NEPAD agency has planned a number of activities and events to reach out to different stakeholder groups. The Congress and Colloquium is part of the NEPAD 10th anniversary celebrations.

Journalists are invited to cover the NEPAD Colloquium and Congress live via webcast on 28th Wednesday, March 2012.


Technical contact: +41 22 534 96 97  - sec.sg@apo-opa.org

SOURCE 
New Partnership for Africa's Development (NEPAD)

ยช