.

RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI TANGA LEO KUWA MGENI RASMI MEI MOSI KESHO

Apr 30, 2012

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa ka furaha na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyaakzi Tanzania (TUCTA) Bw Nicholaus Mgaya  leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi PICHA NA IKULU
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi

HABARI KAMILI HUKUMU YA KUVULIWA UBUNGE MBUNGE WA SUMBAWANGA MJINI


Sumbawanga
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga imemvua Ubunge mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hilal wa CCM, baada ya kufuta matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba 2010.
     Mahakama hiyo imeyafuta matokeo baada ya kuridhika kwamba kulikuwa na kukiukwa kwa baadhi ya taratibu za uchaguzi zilizoathiri matokeo ya uchaguzi huo.
    Habari kutoka Sumbawanga zimesema, hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Bethuel Mmila katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyowasilishwa mahakamani na CHADEMA kikilalamikia kukiukwa kwa baadhi ya taratibu za uchaguzi huo hivyo kusababisha matokeo yasiyo ya haki.
     Katika hukumu hiyo iliyochukua saa tatu na Jaji Mmila imeelezwa kuwa katika kusikiliza shauri hilo mahakama imepokea vielelezo na ushahidi ulioweza kuthibitisha kuwa baadhi ya taratibu za uchaguzi zilikiukwa na hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi huo.
 Baada ya matokeo hayo watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa CHADEMA kama kawaida yao wameonekana wakitamba mitaani na pikipiki huku wengine wakipaza sauti huko huko mitaani.
    Hata hivyo shamra shamra hizo hakuathiri hali ya usalama wa mji wa Sumbawanaga hasa baada ya polisi kuchukua tahadhari kudhibiti uwezekano wa vibaka kutumia fursa hiyo kufanya uporaji na wizi wa mali za watu.

SERENGETI BREWERIES LIMITED(SBL) ANNOUNCE MR STEVE GANNON AS MANAGING DIRECTOR


Mr. Steve Gannon

Serengeti Breweries Limited (SBL) is pleased to announce the appointment of  as Managing Director, effective 1 July 2012. Mr.

Steve Gannon joins SBL from Diageo Cameroon Hub where he has been Managing Director since 2009.

In this role at the helm of SBL, Mr. Gannon will be a member of the East African Breweries Ltd Executive committee.

Under Mr. Gannon’s leadership for three years, the Diageo Cameroun Hub business has delivered significant share growth in beer and established new businesses in premium spirits.

During Mr. Steve Gannon’s tenure leading the Diageo Cameroun Hub business he has led significant investment behind building capacity and expanding the businesses routes to market.

In addition, Mr. Gannon has been central in leading the development of the Business Coalition Against Corruption in Cameroon – an unprecedented initiative in partnership with the Cameroon government to create a private sector movement united against corruption.

Prior to his role within Diageo Cameroun Hub, Mr. Steve Gannon has had 30 years commercial experience in Diageo, including leading the Diageo Venture Africa Business, launching the Guinness brand in a number of African markets as well as doubling the Diageo Africa spirits business in the Diageo Venture Africa markets.

CCM YAPATA PIGO S'WANGA, MAHAKAMA YAMVUA UBUNGE AESHI

Mahakama imemvua ubunge, aliyekuwa mbunge wa Sungawanga mjini (CCM) Aeshi Hillary(pichani) mchana huu, kufuatia hukumu iliyotoka dhidi ya kesi ya kupinga matokeo iliyokuwa inamkabili Aeshi ambayo ilifunguliwa na Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema mjini Sumbawanga, ambaye alidai kuchakachuliwa matokeo katika uchaguzi huo.
    Katika mashitaka hayo mlalamikaji alidai pia kuwepo utoaji rushwa ikiwemo kutoa kinanda kwa kanisa katoliki.

HUKUMU KESI YA KUPINGA UBUNGE WA AISHA WA CCM LEO

Hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa mbunge wa

SIMBA YACHAPA AL AHLY SHANDY TATU BILA

Apr 29, 2012

Wachezaji wa Simba na kocha wao wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho kulia timu hiyo ikiwa imeitandika mabao 3-0 timu ya Al Ahly Shandy ya Sudan, katika mechi ya Kombe la Shirikisho, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo. Simba imepata mabao yote katika kipindi cha lala salama na kutoka kifua mbele katika mchezo huo wa kwanza kabla ya ule wa marudiano utakaopigwa Sudan, wiki mbili zijazo. Walioifungia mabao hayo Simba ni Patrick Mafisango, Uhuru Selemani na Emmanuel Okwi.

PRESIDENT/CCM MOVE ON CABINET

Dear Citizen Editor,
I have Read in your  26th, April The opinions of Mr Mtikila,Dr Bakari insinuating that CCM MPs by not signing the Motion of no Confidence Against the Premier,Means they are Hypocrites!
       To me these two Learned Fellows are not Truthful,CCM MPs infact are the Ones who Spearheaded this ATTACK against their Govt,We saw Chairmen of Parliamentary Sectoral Committees,Peter Serukamba,Deo Filikunjombe and Hordes of other Kangi Lugora,Luhaga Mpina etc Rising one after Another demanding Resignation of Ministers in very Strong Language one Even Even Calling Them WEZI(THIEVES)!! In Broad Daylight!
       Serukamba Rose and Urged his CCM FELLOW MPs to go in their Party Caucus to Take to Task the Government by Demanding RESIGNATION and Action Against Embezzlers!  They Convened this CCM Party Caucus And They Deliberated and Grilled the PM,and Finally a RESOLUTION to their Party Chairman/President was Issued To Take to Task these Officials.
      How on Earth Did anyone Expect them to Run Sign a NO CONFIDENCE VOTE against the Premier?? After all isnt the One to Take to Task the MINISTERS,so that would be not Just, They had the Right to Wait for their Party Caucus Resolution to see How the President Shall Work on it! 
       Politics of Cheap Popularity will Ruin this Nation. The President has Okayed their Resolution,Now Some people out of their Usual Political Timidity and Hatred Want to Water Down the Significance of his Move to show it Emanated from the Opposition this is HYPOCRISY ON THEM NOT CCM MPs whom they Accuse.                                                                                          History is Vindicative of my Assertion,3rd Phase Prof Mbilinyi,Kilontsi Mporogomyi,Idd Simba,Juma Ngasongwa all Ministers Resigned out of CCM MPs Pressure, RICHMOND
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania,
---Original Message-----
From: lugakingira@gmail.com
Date: Sun, 29 Apr 2012

VIJANA VYUO VYA ELIMU YA JUU WATINGA CCM KUFIKISHA UJUMBE WAO KUHUSU MAFISADI

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwapokea  Vijana wa Shirikisho la Vijana wa CCM walioko vyuo vya  Elimu ya Juu, walipofika kwenye ofisi za Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo kuonana naye ili  kufikisha msimamo wao kuhusu Mawaziri na Maofisa wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotevu wa fedha za umma. Vijana hao walookuwa na mabango yenye ujumbe mbali mbali pamoja na mambo mengine wamemuomba Rais Kikwete awachukulie hatua wahusika wote kwa kuwaondoa kabisa kwenye nafasi zao na si kuwahamishia kwingineko na kisha wachukuliwe hatua za kisheria, Kauli ambayo Nape aliwaunga mkono akiahidi kufikisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete.
 Nape akizungumza na Vijana hao
 Nape akisoma ujumbe kwenue moja ya mabango waliyofika nayo vijana hao
 Kisha akasoma na mango hili 
 Vijana wakionyesha moja ya mabango waliyofika nayo
 Na hili likieleza maana ya Mapinduzi
Hili likawataka 'magamba' wanaoondoka CCM wazidi kutimka

SIMBA LEO KAZI MOJA TU, USHINDI TAIFA


Kikosi cha Simba

Baada ya kusubiriwa kwa hamu mechi muhimu ya Kimataifa kati ya Simba na Al Ahly Shandy kutoka Sudan katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), leo ndio leo, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Kutokana na umuhimu uliopo ambao si kwa Simba tu ila kwa Watanzania wote, Uwanja wa Taifa unatarajiwa kufurika mashabiki kibao wa soka na bila shaka wale wenye tofauti za kiitikadi katika soka wataachana nazo kwanza na kuungana na wenzao kulishangilia Simba kuipa moyo ili iweze kuibuka na ushindi.
 Viingilio katika mechi hiyo ambavyo tiketi zake zilianza kuuzwa tangu juzi mpangilio wake ni hivi, Viti vya bluu na kijani itakuwa Sh. 5,000, Rangi ya Chungwa Sh, 10,000, VIP C 15,000, VIP B 20,000 na VIP A 30,000

VIONGOZI AFRIKA MASHARIKI WATIA SAINI MKTABA WA USHIRIKIANO KATIKA ULIZNI WA NCHI HIZO

 Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionesha hati baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha. Wengine kushoto ni Paul Kagame wa Rwanda, Mwai Kibaki wa Kenya na Yoweri Museven wa Uganda

TANZANIA YAOMBWA KUCHANGIA WAANGALIZI WA AMANI SYRIA

Apr 28, 2012


Baadhi ya walinzi wa amani wa UN walioko Syria wakizungukwa na wananchi 
Na Mwandishi Maalum,
New York
Mkuu Idara ya   Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa (DPKO) , Balozi Herve Ladsous, ameziomba nchi ambazo zimepelekewa maombi ya kutoa waangalizi wa amani  kwenda kuhudumu nchini Syria, kutoa waangalizi hao haraka na mapema iwezekanavyo.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni  kati ya mataifa  ambayo yameombwa kutoa wanajeshi wake.
 Balozi Ladsous ametoa wito huo   siku ya ijumaa wiki hii, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi  wa nchi ambazo zinashiriki katika Operesheni za ulinzi wa   kulinda amani za UN  maarufu kama TCC.
Ombi la  Balozi Ladsous kwa nchi hizo  linakuja ikiwa ni takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la Usalama kupitisha Azimio namba 2043 ( 2012)  linalotakamka pamoja na mambo mengine,  kuanzishwa kwa Misheni  ya Umoja wa Mataifa ya kusimamia amani Syria ( UNSMIS) itakayokuwa na waangalizi 300 wanaotakiwa kupelekwa nchi humo ndani ya kipindi cha siku 90 tangu kupitishwa kwa Azimio hilo.
 “ Ninawaomba sana  sana, tafadhali fanyeni hima, kutupatia waangalizi wa amani, wasilianeni na  Makao  Makuu ya Nchi zenu. Hatuna  muda na dunia inatuangalia”. Akasisitiza na kusihi   ombai alilokuwa akirudia mara kwa mara ,Mkuu huyo wa DPKO  aliyekuwa ameandama na maafisa waandamizi kutoka  Idara hiyo.
Kwa mujibu wa  Bw.  Herve Ladsous   ili   Azimio hilo liweze kutekelezwa kikamilifu,  waangalizi   wa amani 100 wanatakiwa  wawe wamewasili nchini Syria ndani ya siku 30 na idadi    itakayobakia  ya  waangalizi 200 iwe imekamilika  ndani ya siku 60.
Akasema kwamba ili malengo hayo yaweze kufikiwa  kama ilivyopangwa, ni vema na muhimu nchi zilizoombwa  zikawasilisha majina ya wanajeshi wanaowapendekeza  haraka na mapema iwezekanavyo ili taratibu za maandalizi ya kuwapeleka Syria  yaweze kutekelezwa.
Akifafanua zaidi kuhusu majukumu ya  waangalizi hao, ambao hawatakuwa na silaha  za aina yoyote ile ,  kuwa jukumu  lao kuu la  msingi litakuwa ni   kufuatilia na  kusimamia  kwa ukamilifu utekelezaji wa  ajenda Sita za mpango wa amani kama zilivyoainishwa      na  Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa  Nchi za Kiarabu, Bw. Kofi Annan.
Mapendekezo  hayo yanataka pande zote husika nchini humo kusitisha mapigano na vitendo vyovyote  vya uvunjifu wa amani,  kuondoa wanajeshi na  silaha katika makazi ya watu, kuruhusu mashirika ya misaada ya kibinadamu na hatimaye kuruhusu   kuanza  mchakato wa mazungumzo ya amani yatakayozingatia matakwa ya  watu wa Syria.
            Akabainisha kwamba waangalizi hao wa amani  300 watasambazwa katika maeneo 25 ambayo yameainishwa kama  maeneo tete  yanayohitaji uwepo wa maafisa hao.
            Hadi kufikia siku ya  ijumaa  wiki hii kulikuwa na waangalizi wa amani wapatao 14  ambao wapo  tayari  nchini Syria  kwa lengo la kusimamia mchakato huo wa  usitishswaji wa mapigano  na uondoaji wa silaha katika  makazi ya watu na pia kutoa taarifa ya kile kinachoendelea.
Hata hivyo idadi hiyo ya waangalizi hao imekuwa ikilalamikiwa na wananchi wa Syria kwamba haitoshi ikilinganishwa na ukubwa wat atizo.
Wakati huo huo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ametangaza uteuzi wa Meja Jenerali  Robert Mood raia  wa  Norway kuwa Mkuu wa  Misheni   ya Usimamizi  ya Umoja wa Mataifa nchini Syria (UNSMIS)

WAKUU WA EAC WAKUTANA ARUSHA LEO


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajiwa kukutana  Arusha, hii leo, katika mkutano maalum utakaojadili pamoja na mambo mengine, mapendekezo ya maombi ya nchi ya Sudan Kusini, kujiunga na jumuiya hiyo.
Nchi zote tano za Kenya, Uganda, Tanzania,Rwanda na Burundi zinatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa siku moja utakaofanyika katika hoteli ya Ngurdoto, nje kidogo ya mji wa Arusha.
Taarifa zilizopatikana toka ofisi ya EAC,Idara ya Mawasiliano na Masuala ya Umma imesema mkutano huo pia unatarajiwa kujadili agenda nyingine nne.
Maombi ya Sudani Kusini yatafikiriwa ikiwa ni miezi karibu mitano baada ya maombi ya Jamhuri ya Sudani kukataliwa kwa madai ya kutokidhi vigezo vilivyoanzisha mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkataba huo unaeleza wazi kwamba nchi yoyote inayotaka kujiunga na EAC, sharti iwe imepakana na moja kati ya nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo.
Hata hivyo maombi ya Sudani Kusini yanakuja wakati ambapo ipo katika hali ya uwezekano wa kuingia katika vita kamili na jirani yake, Sudani Kaskazini, hoja ambayo huenda pia itatupiwa jicho na kikao hicho cha Wakuu wa EAC.
Nchi hiyo mpya kabisa barani Afrika na duniani kwa ujumla, ilipatikana Julai 1, 2011 baada ya mwongo mmoja wa vita na Sudani Kaskazini.
Hoja nyingine ambazo zinatarajiwa pia kujadilia katika mkutano huo ni pamoja na uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu mpya wa EAC, atakayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, kuchukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Beatrice Kiraso wa Uganda ambaye kamaliza mkataba wake wa kazi na pia kufikiria kumwongezea mkataba wa kazi, Naibu Katibu Mkuu, anayeshughulikia Uzalishaji na Sekta ya Jamii, Jean Claude Nsengiyumva kutoka Burundi.
Mkutano huo wa Wakuu wa EAC, umetanguliwa na mkutano maalum wa 24 wa Baraza la Mawaziri wa EAC.

WANANCHI WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI MONDULI


Na Rose Jackson,Arusha
WANANCHI zaidi kutoka   kata ya Lepurko Wilayani Monduli Mkoani Arusha  wanaokabiliwa na ukosefu wa maji hivi sasa watanufaika na mradi wa maji ya bwawa la kisasa linalojengwa katika kijiji cha Nanja  Wilayani humo.
     Bwawa hilo pia litasadia mifugo zaidi ya   elfu ishirini kupata maji na kupunguza kuenea kwa magonjwa ya mifugo  katika maeneo hayo.
     Kwa mujibu wa wananchi hao walikuwa wakitembea mwendo wa kilomita zaidi ya kilomita zaidi ya kumi na tano  kutafuta bidhaa hiyo adimu katika eneo hilo la wafugaji wa kimasai.
     Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kijiji cha Nanja  eneo linakojengwa  bwawa hilo Tingide Shamburi  alisema kuwa  bwawa hilo linajengwa na kampuni  inayokarabati  barababara ya Arusha Minjingu ya Sogea Satom ya nchini Ufaransa.
    Alisema kuwa tatizo la kufuata  maji katika maeneo ya mbali pia limekuwa likichangia kuenea kwa magonjwa ya mifugo na kusababisha wafugaji kupoteza mifugo yao .
    Tingide aliongeza kuwa  wanawake wamekuwa wakijeruhiwa na wanyama nyakati za usiku wakati wakifuata maji katika vijiji vya jirani katika eneo hilo lililopo karibu na hifadhi taifa. 
    Aidha aliwashukuru wahisani hao kwa kuamua kuwasaidia kuondokana na tatizo hilo aambalo limekuwepo katika maeneo yao kwa miaka mingi.
    Alisema kuwa kwa mujibu wa wataalamu bwawa hilo litadumu kwa muda mrefu kutokana na kuwekewa kitambaa maalumu katika sakafu yake  ili kutoruhusu maji kupotelea ardhini.
    Kwa upande wake afisa uhusiano wa kampuni  SOGEA SATOM ya nchini Ufaransa   Jamal  Nassoro Addi alisema kuwa  bwawa hilo litagharimu shilingi miloni mia moja za kitanzania  na litakamilika katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
    Addi aliongeza kuwa  kampuni yake iliamua kutoa msaada kwa wananchi  kama sehemu ya kuonyesha utu.
    “Kimsingi sisi hatukuwa na wajibu wa kujenga bwawa hili katika mkataba wetu wa ukarabati wa barabara ya Arusha Minjingu lakini sisi kama kampuni tuna sera ya kujitoa kwa ajili ya matatizo ynayowakabili binadamu wenzetu”alisema Addi.
    Alisema zaidi ya msaada huo pia wananchi wa vijiji hivyo watapata hasa zile ambazo hazihitaji wataalamu kama sehemu ya kuwawezesha  kupata kipato.
     Aliongeza kuwa pia kampuni hiyo inaendesha pia mradi wa afya kwa kugharamia utoaji wa elimu ya ukimwi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na wananchi wa vijiji ambavyo barabara hiyo inapita.

VIDEO FUPI TAMKO LA CCM

Apr 27, 2012


KAMATI KUU YA CCM YAMRIDHIA RAIS KUVUNJA BARA ZA LA MAWAZIRI

Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012  chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya maamuzi kadhaa ikiwemo kumridhia Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri.

 Ifuatayo ni taarifa Kamili kama ilivyosomwa kwa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye.
       Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.
      Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na  taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
        1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.
           2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais   KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.
           Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
           Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.

A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;


Geita,Njombe,Simiyu,Katavi,MagharibiHivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu Katibu wa CCM wa Mikoa.

1. Ndg. Hilda Kapaya

2. Ndg. Shaibu Akwilombe

3. Ndg. Hosea Mpangile

4. Ndg. Alphonce Kinamhala

5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri


Imetolewa na

Nape Moses Nnauye

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi

MABONDIA CHEKA NA MAUGO WAPIMA UZITO LEO,KUMENYANA KESHO PTA


Na Mwandishi Wetu
Mabondia Francis Cheka na Mada Maugo leo wamewapima uzito kwa ajili ya pambano lao la uzito wa Kg 75, litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa PTA, mjini Dar es Salaam.


Waandaji wa pambano hilo, la ubingwa wa IBF, wamewapima mabondia hao leo na wamekutwa na KG.KG.76.5.


Pambano hilo linatarajiwa kuwa la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.


Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.


“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.


Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.


“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D 

KIMOON SENT A CONGRATULATION MESSAGE TO JK


Mr.  Ban Ki Moon, The   Secretary- General of the United Nations   has  sent a congratulation message  to  President Jakaya Mrisho Kikwete, on the occasion of the Union Day. In his massage, Ban Ki Moon said.
“It is my   great pleasure to extend to you and the Government and people of the United Republic of Tanzania my warmest congratulations on the occasion of the Union Day.
This is an opportunity to celebrate the proud culture and history of your country. It is also a chance to reflect on the role the United   Republic   of Tanzania is playing in our interconnected world. I appreciate your engagement at the United Nations, which is helping   to forge shared solutions to our common challenges.
Our global agenda includes five generational opportunities to create the future we want: promoting sustainable development, building   a safer and more secure world, preventing crises, helping countries in transition, and doing more for the world’s women and young people.
In order to rise to these challenges, I am conscious that we must strengthen   our Organization. A more mobile, efficient and effective United Nations is essential   to delivering for the world’s people.
In this effort, I welcome the   contribution, commitment and leadership of the United Republic of Tanzania in our quest to usher in a more just, peaceful and prosperous future for all people.
Please accept, Your Excellency,   the assurance of my highest consideration.”
Ban Ki Moon, Secretary-General of the United Nations
Issued by  Permanent Mission of the  United  Republic of Tanzania to  the United Nations 

MBICHI AU MBIVU UBUNGE WA TUNDU LISU LEO

Hukumu ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Tundu Lisu wa chama cha CHADEMA pale pande za Singida ni leo. Na habari zilizoufikia mtandao huu ni kwamba, hakimu alichelewa kuingia mahakamani na ndiye alikuwa akisubiriwa kwa hamu. Zaidi peruzi hapa baadaye

KKKT KUZINDUA JENGO LAKE LA KITEGAUCHUMI JUMAPILI HII

Apr 26, 2012


Kanisa la Kiinjili la Kilutehri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, imekamilisha ujenzi wa jengo lake la Kitegauchimi ambalo ujenzi wake umegharimu sh. bilioni 3.5.
     Jengo hilo lililoanza kujengwa mwaka 2009 katika eneo la Kijitonyama, Dar es Salaam, litazitazinduliwa Jumapili hii, Aprili 29, mwaka huu na litaitwa Kijitonyama Lutheran Centre (KLC).   Pichani, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi, wakiwa kwenye jengo hilo leo akiwemo Mchungaji wa Usharika wa wa Kijitonyama, Ernesti Kadiva.


JK AONGOZA WATANZANIA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MUUNGANO Rais Dk. Jakaya Kikwete, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
 Rais Kikwete akikagua gwaride
 Rais Kikwete akimsalimia Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba
 Rais Kikwete akimsalimnia Mama Maria Nyerere. Kulia ni Spika wa Bunge Anna Makinda
 Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
 Rais Kikwete akimsalimia Makamu wake, Dk. Mohammed Gharib Bilal
 JWTZ wakionyesha ukakamavu wao wakati wa gwaride
 Nevi katika gwaride
 Vijana wa halaiki wakisherehesha maadhimisho hayo
Kikundi cha Sanaa cha JKT Oljoro, kikionyesha umahiri wake wa kuimba na kucheza 'Kiduku' wakati wa sherehe hizo. Picha: Freddy Maro na Muhidin Sufian

CHUNGA SANA UJUMBE KAMA HUU UNAPOKUFIKIA!


Greetings from spain


Hope you get this on time,sorry I didn't inform you about my trip in Spain for a program, I'm presently in Madrid and am having some difficulties here because i misplaced my wallet on my way to the hotel where my money and other valuable things were kept.I want  you to assist me with a loan of 2600 Euros to sort-out my hotel bills and  to get myself back home.

I have spoken to the embassy here but they are not responding to the matter effectively,I will appreciate whatever you can afford to assist me with,I'll Refund the money back to you as soon as i return, let me know if you can be of any help. I don't have a phone where i can be reached. Please let me know immediately.
    
     Thanks
       
Agnes

UNAIJUA HISTORIA YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR? HII HAPA

Apr 25, 2012


MKATABA, HATI NA MAMBO 11 YA MUUNGANO
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.
     Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.
    Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika,  kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.
     Msingi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za Mwaka 1964.
     Hati za Muungano zilitiwa saini na Nyerere na Karume, Aprili 22, 1964 na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
      Aprili 26, 1964, bunge la Tanganyika lilipitisha sheria za Muungano, ambazo baadayezilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
      Mnamo Aprili 27, 1964 waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai.
     Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianisha mambo 11 ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano ambayo ni; Katiba na Serikali ya Muungano, Mambo ya nchi za nje, Ulinzi, Polisi, Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na Biashara za nje, Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania unaosimamiwa na idara ya forodha, Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
      Katiba ya muda ya mwaka 1965 ilianisha utawala wa serikali ya mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP kwa Zanzibar. Katiba hii, ilizingatia misingi ya makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na sheria za Muungano wa Tangayika za Zanzibar.
      Katiba hiyo ilianisha serikali mbili, uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Muungano ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano kwa upande  wa Tanganyika. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
       Hata hivyo mambo ya Muungano yaliongezwa kutoka 11 hadi 22 kutokana na mahitaji ya ndani ya nchi pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwengini baada ya Muungano.
       Mwaka 1985, jambo la 12 linalohusu sarafu na fedha kwa ajili ya malipo na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na benki katika Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, liliingizwa.
     Kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, mambo matatu ya Muungano yaliyongezwa, ambayo ni leseni za viwanda na takwimu; elimu ya juu; na usafirishaji wa anga.
     Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya magari na ama ya petroli na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliyongezwa kwenye orodha hiyo.
Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi kufikia 21 kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa  Jumuiya ya Afrika Mashariki.
     Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa siasa nchini suala la 22 la uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha hiyo.
      MJADALA KUHUSU MUUNGANO
Katika miaka hivi karibuni kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusiana na muundo wa Muungano, baadhi wakitaka uwe wa zaidi ya serikali mbili, wengine serikali moja, wapo wanaotaka Tanganyika iwe kivyake na Zanzibar kivyake.
      Hata hivyo hekima inaonyesha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unabaki kuwa ni fahari ya Watanzania, kwani mwelekeo wa dunia katika nyanja mbalimbali, mataifa kuungana kwa ushirikiano wa aina mbalimbali ni muhimu kuliko taifa moja kupambana kivyake.
      Urejeaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuvunjika mwaka 1977, uwepo wa SADC, ECOWAS, COMESA, na jumuiya nyingine nyingi duniani kote, ni vielelezo kwamba ushirikiano baina ya mataifa ni suala lisilohitaji mjadala.
       Ieleweke kwamba hakuna ushirikiano usio kuwa na matatizo kama ilivyo kwa Muungano wa Tanzania, vivyo hivyo muungano mwingine kama vile ya United Kingdom (UK), Uingereza na United States of America (USA) kwa maana ya Marekani na United Arabs Emirate (UAE), nayo ina matatizo, lakini hata mara moja mjadala juu ya matatizo hayo siyo kuvunja ushirikiano bali kutatua na wale wanaotaka kuvunja hushughulikiwa ipasavyo.
      "Matatizo ya Muungano kama wa UK ni mabaya zaidi, na hata UAE hawana ahueni, ila wanajua kwamba Muungano wao ni lazima. Wamarekani wanapambana na watu wenye mawazo haya ya kuvunja miungano kwenye majimbo ya Alaska, Hawaii na Texas na mwishowe wameamua kuweka kambi kubwa ya jeshi la nchi kavu Texas; utitiri wa kambi za anga Alaska; na vituo vikubwa kupindukia vya majini kule Hawaii. Hivi, hawa mabingwa wa demokrasia wanapoamua kulinda nchi yao namna hii, unafikiri ni wajinga? Walimwaga damu na waliyanunua majimbo haya na wamepitia shida kubwa, ndiyo maana leo wanajidai," anaandika mchangiaji katika mjadala kuhusu Muungano.
        Ni vyema Watanzania wakati huu wa kusheherekea miaka 48 ya Muungano, kila mmoja akajisikia ufahari wa kuwa na kitu kizuri kilichoasisiwa na Waafrika wenyewe na kudumu kwa umri huo.         Mawazo ya kubaguana kwa sababu zisizo na msingi, pengine kukidhi matakwa na wakati kama vile ya kibinafsi na kisiasa, yasipewe nafasi kuisambaratisha nchi. Chambilecho wahenga, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

MAANDALIZI MPAMBANO WA SIMBA NA AL AHLY YAKAMILIKA, AL AHLY KUTUA KESHO DAR


Maandalizi ya timu ya soka ya Simba kwa ajili ya kukutana na klabu ya Al Ahly Shandy kutoka Sudan katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), Jumapili hii, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, yamekamilika.
       Taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga, imesema kutokana na kwamba mechi hiyo itakuwa ya kimataifa, Simba imepanga viingilio ambavyo kila mwananchi ataweza kuvimudu.
       Kamwaga amevijana viingilio hivyo kuwa vitakuwa kama ifuatavyo;-
 Viti vya bluu na kijani itakuwa Sh. 5,000, Rangi ya Chungwa Sh, 10,000, VIP C 15,000, VIP B 20,000 na VIP A 30,000. 
     Amesema tiketi zitauzwa siku ya Ijumaa, katika maeneo yafuatayo, Big Bon, Benjamin Mkapa, Stears Mjini, Mbagala Dar Live, OilCom Buguruni, Tandika Mwembeyanga, Ubungo Oilcom, Mwenge Bus Stand, BP Mwananyamala na Gapco Ukonga
     Kwa mujibu wa Kamwaga klabu imepokea maombi mengi kutoka kwa wanachama na wapenzi wake kutoka mikoani na ingeomba kwamba wale wanaotaka kuja kutazama mechi hii kwa makundi kutoka mikoani, wawasiliane mapema na uongozi ili wanunuliwe tiketi zao mapema na kuongeza kuwa Simba SC imechapa tiketi za kutosha na ingependa wapenzi na wanachama wake kujitokeza kwa wingi kwenye pambano hilo.
     "Wana Simba wote wanaombwa kuja uwanjani wakiwa wamevalia mavazi yao ya rangi Nyekundu na Nyeupe ili uwanja mzima upendeze kwa rangi hizo", alisema Kamwaga. 
      Pia Kamwaga alitoa mwito kwa vyombo vya habari kuisaidia Simba na Tanzania kwa kuelekeza nguvu zao katika uandishi wa taarifa ambazo zitaisaidia timu hiyo kusonga mbele na si kuondoa morali au kusababisha watu wasiende uwanjani.
       "Simba ni timu pekee kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyobaki katika michuano yote ya kimataifa inayosimamiwa na CAF na kubwa zaidi ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa na hivyo wanabeba bendera ya taifa kokote kule waliko", alisema.  
     Alisema Al Ahly wanatarajiwa kuwasili kesho saa saba mchana kwa ndege ya Ethiopia Airlines. 
      Kwa mujibu wa Kamwaga ,waamuzi na Kamishina wa mchezo wamepangwa kuwasili Ijumaa (keshokutwa) wakitokea nchini Swaziland na Rwanda.
       Pia Simba wametoa shukurani walizoziita za namna ya kipekee kabisa, kwa serikali kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu Wekundu wa Msimbazi kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa kujiandaa na mechi hii muhimu.

CHAKA AJIFUA KUMKABILI MAUGO JUMAMOSI HII

Kocha wa mchezo wa Masumbwi Abdalah Ilamba 'Komandoo' akimfanyisha mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo bondia Francis Cheka, Dar es salaam jana Chaka anajiandaa na mpambano wake na Mada Maugo utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo mshindi atakuwa bingwa wa Mkanda wa I.B.F na atanyakua Zawadi ya gari.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAJIPANGA KUKUSANYA ZAIDI YA SH. BILIONI 56 2012/13


Na Rose Jackson,Arusha
Halmashauri ya Manispaa ya jiji la Arusha imepitisha bajeti ya kukusanya  zaidi ya shilingi  bilioni  56  kwa mwaka wa fedha 2012 -2013.
     Akisoma bajeti hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya arusha Estomih Chang’a alisema kuwa bajeti hiyon itatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato vilivyopo ndani ya manispaa hiyo.
    Chang’a alisema kuwa mapato ya vyanzo vya ndani ni sh.8,496,078,520,ruzuku toka serikali kuu sh.25,268,023,468,wafadhili sh.22,190,498,099,pamoja na fidia ya vyanzo vilivyofutwa sh.518,610,000.
     Alitaja vyanzo vingine kuwa ni pamoja na matumizi ya mishahara ambapo ni sh.27,316,260,154,matumizi ya uendeshaji sh.4,017,191,792,na miradi y a sh.25,139,758,141.
      Aidha aliongeza kuwa jambo la muhimu katika bajeti ya halmashauri hiyo ni kuelekeza asilimia hamsini ya fedha katika miradi ya maendeleo inayoendelea ikiwemo madarasa ya ghorofa yanayojengwa katika shule ya sekondari ya Felex Mrema,Themi na Sekondari ya Ngarenaro.
     Pia alisema kuwa bajeti hiyo itaelekezwa katika uendelezaji wa shule mpya ya sekondari Suye ili iweze kutoa elimu ya kidato cha tano na sita sanjari na kuanzisha chuo cha ufundi stadi shuleni hapo.
      Vilevile  halmashauri hiyo itakamilisha miradi ya  visima vya maji  maeneo ya kame kama vile kata ya Terrat,Sokoni One na Mushono ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kukarabati barabara za kata zote ikiwemo madaraja na kalavat.
     “hii bajeti sio kwa ajili ya kuendeleza maendeleo tu bali hata katika huduma za kijamii kama vile kutoa mikopo kwa akina mama na vijana ambapo kupitia mikopo hii itawasaidia kujikwamua kiuchumi"alisema Chang'a.

MISS ARUSHA CITY CENTRE 2012 YAIVA

 Washiriki wa kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,tayari kuchuana vikali Mei  5,  2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo katikati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/=
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo. PICHA NA AHMED MICHUZI

SAFARI LAGER YATANGAZA KUKAMILIKA KWA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WA “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”.Oscar Shelukindo akizungumza leo
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi kukamilika kwa mafunzo ya wajasiriamali waliopatikana katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”. 
        Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema mafunzo kwa wajasiriamali wa“Wezeshwa na Safari Lager” yalikamilika rasmi mwishoni mwa wiki katika mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.
        Aliwapongeza wajasiriamali wote waliofaulu na kupatiwa mafunzo haya yanayolenga kuwawezeshwa kupanua na kukuza biashara zao. Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hawa Bwana Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa.
        Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo.
        Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea nk.
        Shelukindo alisema “Ni jambo jema kwamba wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano nk”.
        Bwana Shelukindo aliwataja wajasiriamali waliomaliza mafunzo na watapatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali walifaulu ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Martin Richard Tupilike, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.
       Aliendelea kuwataja wajasiriamali waliofaulu katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa. 
        Bwana Shelukindo aliendelea kusema “Safari Lager tunayofuraha kubwa kuwasaidia wajasiriamali hawa, tunawapa pongezi kwa uvumilivu wao na jitihada kubwa waliyo nayo. Tutawakabidhi vitendeakazi vyao katika hafla maalumu kuanzia wiki mbili zijazo”. 
        Akielezea mafunzo yalivyoendeshwa Bw. Joseph Migunda wa taasisi ya TAPBDS alisema wajasiriamali katika mikoa yote wameonyesha uelewa kwa kiwango cha juu na wote walifaulu mtihani wa kuhitimisha mafunzo hayo. Alisema “Tuna imani wajasiriamali watatumia elimu na ruzuku wanayopatiwa ili kupiga hatua zaidi kufikia ndoto zao”.
       Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano hili, aliendelea “Shukrani nyingi sana ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na Safari Lager baadae mwaka huu.
______________________________________________________________________
Kuhusu Wezeshwa na Safari Lager;
Ni shindano linaloendeshwa na bia ya Safari Lager, likiwa na lengo la kuwainua wajasiriamali wadogowadogo kwa kuwapa msaada wa ruzuku ya vitendea kazi. Kwa maelezo zaidi tembelea www.wezeshwa.co.tz

Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Oscar Shelukindo, Safari Lager Brand Manager, simu;  +255 767 266 833, [Oscar.Shelukindo@tz.sabmiller.com].
Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.

Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.

Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.

Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India. SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.


ยช