.

JK AKUTANA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA IRAN NA MJUMBE WA RAIS WA BURUNDI IKULU DAR ES SALAAM LEO

May 30, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 Mjumbe maalumu kutoka serikali ya Burundi, Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo. Kati ni Balozi wa Burundi nchini Tanzania 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mjumbe maalumu kutoka serikali ya Burundi, Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo. Kushoto  ni Balozi wa Burundi nchini Tanzania
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe kutoka serikali ya Burundi alioletewa na Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi. Katikati yao ni mkalimani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi

WAZIRI ABOUD NA ASKOFU MOKIWA WAZUNGUMZIA VURUGU ZA ZANZIBAR


Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd akifafanua jambo alipozungumza na Maaskofu mbalimbali kufuatia kwa matatizo yaliotokezea Zanzibar ya kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
-Askofu Mkuu wa Anglican Tanzania Dk Valontine Mukiwa wakwanza kulia akizungumzia kuhusiana na matatizo yaliotokezea Zanzibar ya kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walipokutana  Maaskofu mbalimbali na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud Mohd kushoto akisalimiana na Askofu Mkuu wa Anglican Tanzania Dk Valontine Mokiwa baada ya kumaliza kwa mazungumzo yao pamoja na Maaskofu mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Askofu Mkuu  wa Anglican Tanzania Dk Valontine Mukiwa akifanya mahojiano na Muandishi wa BBC kuhusiana na  matatizo yaliotokezea Zanzibar ya kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR

CCM YATAKA WAZIRI WA KATIBA ZANZIBAR AJIUZULU

May 29, 2012

Abubakar Khamis Bakar

ZANZIBAR, Chama cha Mapinduzi kimetoa shindikizo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumtaka  Waziri wa Sheria na Katiba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Abubakar Khamis Bakar ajiuzulu kwa madai ya kushindwa kuishauri vizuri serikali katika suala la kudhibiti asasi za kiraia ikiwemo uamsho.
     Aidha chama cha mapinduzi kimetaka kufutwa mara moja kwa jumuiya ya uamsho kwa sababu imekwenda kinyume na malengo yake ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ambayo kazi yake kutoa elimu kuhusu mihadhara ya dini ya kiislamu tu.
     Akizungumza na waandishi wa habari hapo makao makuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema leo, kuwa  kikundi cha kutoa mihadhara ya dini ya kiislamu cha Uamsho kimesajiliwa kwa ajili ya kutoa mihadhara ya mambo ya dini tu na sio kujishungulisha na siasa za majukwaa ikiwemo kuwahoji wananchi kuhusu uhalali wa muungano na kuwakashifu viozngozi wa serikali ikiwemo waasisi wa taifa hili.
     Alisema kitendo cha Waziri wa katiba na sheria kushindwa kuishauri vizuri serikali kuhusu mwenendo wa kikundi hicho ndiyo kimesababisha maafa makubwa na kuiingiza nchi katika wasiwasi mkubwa kiasi kuvurugika kwa sekta ya biashara na utalii.
     'Chama Cha Mapinduzi, kinamtaka waziri wa sheria na katiba wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujiuzulu mara moja kwa sababu ameshindwa kumshauri vizuri rais pamoja na serikali kuhusu mwenendo wa kikundi cha uamsho ambacho kinafahamika kwamba kazi yake kutoa mihadhara ya kidini tu na siao siasa'alisema Vuai.
     Akifafanua zaidi Vuai alisema kwa mfano vyama vya hiari vyote vilivyopata usajili wa kudumu wa kufanya shunguli zao vinasajiliwa katika ofisi ya katiba na sheria ambayo ipo katika wizara yake.
    Aidha alisema mawaziri wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar walikutana pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa uamsho tarehe 25 Aprili na kutaka kikundi hicho kuacha kufanya mihadhara inayohusiana na mambo ya siasa au kitachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
      Kwa mfano alisema hivi karibuni jeshi la polisi lilizuwia utoaji wa vibali kwa viongozi wa chama hicho lakini vibali vilitolewa katika ofisi za mufti ambazo zipo chini ya wizara ya katiba na sheria.
     'Tulimtaka waziri wa katiba kulifanyia kazi suala hilo kuona kwamba kikundi hicho hakifanyi mihadhara inayohusiana na mambo ya siasa ikiwemo kuwakashifu viongozi na kuhoji uhalali wa muungano lakini hakufanya kazi hiyo'alisema Vuai.
    Vuai alisema hivi sasa chama cha mapinduzi kimetambuwa na kufahamu kwamba jumuiya ya uamsho ipo katika kivuli cha chama kimoja cha siasa na ndiyo maana kimekuwa kikifanya kiburi na jeuri kiasi ya kutamka kwamba hakuna mtu wa kukifuta.
     Aidha Vuai alisisitiza na kuitaka serikali kuifuta taasisi ya uamsho mara moja kwa sababu imekwenda kinyume na dhamira yake ya kuanzishwa.
      'Tunaitaka serikali kuifuta mara moja taasisi ya uamsho kwa sababu imekwenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo 'alisema Vuai.
     Aidha Vuai aliwataka wafuasi wa chama cha mapinduzi kuwa watulivu katika kipindi chote na kuacha kujishungulisha na vurugu hizo ambazo zinahatarisha amani na utulivu.
     Kwa mujibu wa katiba ya jumuiya ya uamsho,taasisi hiyo itakuwa na kazi ya kutoa mihadhara ya kidini kwa waumini na wafuasi wake na kulinda haki za binaadamu kwa makundi ya waislamu mbali mbali.
     Aidha jumuiya hiyo kazi yake kusaidia matatizo ya kijamii ikiwemo migogoto na majanga mbali mbali ikiwemo waathirika wa ugonjwa wa ukimwi.
     Katiba ya chama hicho inapiga marufuku taasisi hiyo kujishungulisha na mambo ya kisiasa ikiwemo viongozi wake.

IDDI SIMBA NA MWAKING'INDA WAFIKISHWA KIZIMBANI KWA 'KUIFILISI' UDA

Na Mwandishi Wetu
Iddi Simba akisindikizwa na Polisi kwenda kizimbani
Waziri wa Viwanda na Biashara wa zamani, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ,Iddi Simba, leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kujibu mashata ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kulisababishia hasara Shirika hilo zaidi ya Sh. bilioni 2.3
    Amefikishwa mahakamani pamoja na washtakiwa wengeni watatu, Mkurugenzi wa shirika hilo, Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi.
    Katika kesi hiyo, washitakiwa wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa na Said El Mamry na upande wa Serikali unawakilishwa na wakili wa Taasisis ya Kuzia na Kupambana na Rushwa,Ben Lincol.
     Mbele ya Hakimu Mfawidhi Ilivin Mugeta ,wakili Lincoln alisema katika mashtkama manane yanayowakabili, la kwanza kula njama ambalo linamkabili Simba na Milanzi ambao inadaiwa, kati ya Septemba 2 ,2009,  jijini Dar es salaam walikula njama na watu wasiofahamika na kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha namba 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa ya mwaka 2007.
     Shitaka la tatu ni la kuhamisha fedha kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya kupambana na Rushwa, kwamba Simba na Milanzi kwa tarehe hiyo Simba akiwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Milanzi akiwa Meneja Mkuu wa UDA, kwa pamoja walishirikiana kuhamisha fedha kwa faida yao binafsi sh milioni 320,ikiwa ni malipo ya awali na ni sehemu ya ya malipo ya hisa za UDA ambazo walizipokea wao binafsi kupitia nyadhifa zao .
     Washitakiwa wote wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti na Kesi hiyo imeairishwa hadi Juni 28 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.
Iddi Simba akiwa na wakili El Maamry (kushoto) mahakamani

Mwaking'inda  Picha kwa hisani ya BOFYA HAPA  

SPEECH BY HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, ON THE OCCASION OF THE NATIONAL LAUNCH OF GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP DIALOGUE, 29TH MAY, 2012

His Excellency Ali Hassan Mwinyi, Second President of the United Republic of Tanzania;
Honorable Bernard K. Membe, Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, 
Honourable Ministers and Deputy Ministers, 
Amb. Ombeni Sefue, Chief Secretary and Convener of the Global 2013 Dialogue,
Dr. Mihaela Smith, CEO of the Commonwealth Partnership for Technology Management and Co-Convener of the Global 2013 Dialogue,
Excellencies Members of the Diplomatic Corps,
Distinguished Smart Partners, 
Invited Guests, 
Ladies and Gentlemen,

It gives me great pleasure to join all the smart partners gathered here today to witness the launching of the official preparations for the Global 2013 Smart Partnership Dialogue. I take this opportunity to thank our distinguished guests and friends of the Smart way of life who have travelled many miles to be here with us at this solemn occasion.
It is the invaluable contributions of the people gathered here today that have made and are making the Smart Partnership Dialogue relevant and strong.  The dialogue is a result of collective effort and continuing legacy of many individuals from many countries across the world, to which I pay tribute. Indeed, it would be remiss of me not to recognize the singular efforts in particular of Dr. Mahathir Mohammed, Former Prime Minister of Malaysia, Dr. Mihaela Smith, current CEO of the Commonwealth Partnership for Technology Management, and our very own Professor Msangi among others. These individuals have pushed the movement from being confined to the realm of technology and a forum for the few, to the creative and respected platform for discussing serious issues of development on the global arena. And the good thing is, these issues are discussed, freely, without the limitations of borders, rank or file.

Excellencies, Ladies and gentlemen;
I agreed to host the next session of the Smart Partnership Dialogue here in Tanzania during the Langkawi International Dialogue that took place in Putrajaya, Malaysia in June 2011. My decision to host the Dialogue was not by accident. It was based on my conviction following my experience of participating in the Dialogue twice, first in Munyonyo, Uganda and then Malaysia in 2011. In both occasions, I found that the Dialogues provided a unique forum of interaction and equal opportunity for all participants. It did not matter whether you were a Head of State or  a  CEO of a growing company, everyone had an equal voice.
The dynamism of the Dialogue created a rare atmosphere of solidarity that crossed out status, political and ideological boundaries. This was the approach that I believe works, the approach that fostered friendships and bottom-to-top networking that produces international joint ventures based on rare and lasting political goodwill.
Excellencies,
Distinguished Smart Partners,
 Ladies and Gentlemen,
The Theme for the 2013 Smart Partnership Dialogue is “Leveraging Technology for Africa’s Socio Economic Development”. It is a wide theme, an ambitious theme, that I believe will provide sufficient sub-themes to cater for vibrant and fruitful discussions. We are branding the Dialogue the Global 2013 Smart Partnership Dialogue in recognition of the global scope of the theme.  We have chosen the theme simply because technology is quickly becoming a prerequisite for development. It is also a prerequisite for survival in the current socio economic environment in the global arena. In the present globalization era, one cannot shy away from technology and Africa needs it most.
The easiest way to illustrate this is by looking at how a farmer in Tanzania does business with a company in China, via a mobile phone and access to internet. This increasing interconnectivity made possible by advanced telecommunication and internet allows instant communication, reducing the cost in terms of time and money that distance previously imposed. Indeed, technology empowers farmers and allows them to cultivate without worrying about the vagaries of weather through irrigation and green house options. Governments are able to improve governance systems through IT solutions.
As a country we want to use the opportunity of hosting the Global 2013 Smart Partnership Dialogue to send out a clear message to all the technologically advanced countries that the continent has geared itself towards the discourse on technology. We are willing to accept partners and to incorporate technological change and advancement in all initiatives that are currently being conceived, designed and implemented in the continent. And it is our sincere hope that the forum will achieve that noble objective of engendering the technological change that is needed in the continent.


Excellencies,
Ladies and Gentlemen,
I am happy to announce that the Dialogue will be held here in Dar Es Salaam from 24th - 28th May next year. We are ready to host the event, and pleased to receive participants from all nations.  We count ourselves lucky that we have with us members of the Joint Executive Group of the Smart Partnership Movement, the Joint Secretariat Members from the CPTM in London, friends of the Movement and previous conveners of the Dialogue from different countries as well as Members of the Diplomatic Corps. We implore you to be the goodwill Ambassadors of this Dialogue back in your countries. We also request you to communicate our invitations to your leaders and your people. We are looking forward to seeing them next year!
 As part of technological change, a website that provides more information on the Dialogue, including registration and administrative details, programme, sub themes and side events, will also be officially launched. I would like to urge potential participants to use this technological tool as well.
Distinguished Smart Partners,
Excellencies,
Ladies and gentlemen,
Now it is my singular honor and pleasure to launch the national preparations and the official website of the Global 2013 Smart Partnership Dialogue.

Thank you for your kind attention.

SECURITY COUNCIL PRESS STATEMENT ON SYRIA

UNITED NATIONS INFORMATION CENTRE – DAR ES SALAAM
May 27, 2012 UNIC 2012/03/16
                           
The members of the Security Council condemned in the strongest possible terms the killings, confirmed by United Nations observers, of dozens of men, women and children and the wounding of hundreds more in the village of El-Houleh, near Homs, in attacks that involved a series of government artillery and tank shellings on a residential neighbourhood. The members of the Security Council also condemned the killing of civilians by shooting at close range and by severe physical abuse. The members of the Security Council extended their profound sympathies and sincere condolences to the families of the victims, and underscored their grave concern about the situation of civilians in Syria. 
Such outrageous use of force against civilian population constitutes a violation of applicable international law and of the commitments of the Syrian Government under United Nations Security Council Resolutions 2042 and 2043 to cease violence in all its forms, including the cessation of use of heavy weapons in population centres. The members of the Security Council reiterated that all violence in all its forms by all parties must cease. Those responsible for acts of violence must be held accountable. The members of the Security Council requested the Secretary-General, with the involvement of UNSMIS, to continue to investigate these attacks and report the findings to the Security Council. 

 The members of the Security Council demanded that the Government of Syria immediately cease the use of heavy weapons in population centres and immediately pullback its troops and its heavy weapons from in and around population centres and return them to their barracks. 
The members of the Security Council reaffirmed their strong commitment to the sovereignty, independence, unity and territorial integrity of Syria, and to the purposes and principles of the Charter. 
The members of the Security Council reiterated their full support to the efforts of the Joint Special Envoy for the implementation of his six point plan in its entirety and requested him to convey in the clearest terms to the Syrian parties, and in particular the Syrian Government, the demands of the Security Council.

WAZIRI WA MAENDELEO FINLAND ATETA NA MAKAMU WA RAIS DK. BILAL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wa Waziri wa Maendeleo wa Finland, Heidi Hautala (wa pili kushoto kwa Makamu) aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo asubuhi, Mei 29, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

UNATAKA KUJUA SHERIA ZA MCHEZO WA MASUMBWI?

BOFYA HAPA SASA

WASHENZI WACHINJA MTU KAMA KUKU ARUSHA

Na Rose Jackson,Arusha
MTU mmoja aliyetambukika kwa jina Israe Ngonda(45) mkazi wa Kijenge juu jiijini Arusha amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa nyumbani.
   Walioshuhudia wamesema baada ya kujinjwa kinyama watu hao wameuacha mwili kitandani ukiwa umepiga magoti na kichwa kulalia kitandani.
   Kwa muijbu wa Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas ,mwili wa marehemu ulikutwa asubuhi baada ya majirani kupita eneo hilo na kukuta mlango wa nyumbani kwa marehemu ukiwa wazi ndipo walipojaribu kuingia ndani huku wakimwita jina lake bila  majibu.
    Alisema polisi walipata taarifa na kufika eneo la tukio ambapo walimkuta marehemu huyo akiwa amepiga magoti huku sehemu kubwa ya mwili ukiwa umelazwa kitandani   na sehemu  ya shingo ikiwa imekatwa na kitu chenye ncha kali.
    Aidha Sabas aliongeza kuwa hakuna mtu yoyote anayeshikiliwa hadi sasa kuhusiana na tukio hilo na polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
     Taarifa zaidi kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zimedai kuwa kabla ya tukio hilo marehemu alichomewa nyumba yake na watu wasiojulikana na baadae wanakijiji walifanikiwa kuuzima moto huo.
     Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa akiishi pekee baada ya familia yake kusafiri na kwamba tukio hilo linahusishwa na ulipizaji wa visasi.
     Tukio kama hilo liliwahi kutokea hivi karibuni wilayani Arumeru, baada ya Mwenyekiti wa Chadema , Kata ya Usariver, Msafiri Mbwambo, kuuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulika.

ECO BENKI/ PIC WAWEKEZA DOLA MILIONI 250 KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

Na Rose Jackson ,Arusha

Benki ya Eco kwa kushirikiana na shirika la uwekezaji wa sekta ya umma la Afrika ya Kusini(PIC) imetia saini mkataba ambayo imegarimu kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 250 kwa ajili ya kukuza na kuimarisha shuguli mbalimbali za Miradi ndani ya nchi za bara la Afrika.
     Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwekeana saini ya mkataba huo Mkurugenzi wa Eco Benki Bw Anolrd Ekpe alisema kuwa kuanzia sasa zoezi la kuwekeza miradi mbalimbali kwa nchi za bara la afrika zinaanza rasmi.
     Alifafanua kuwa mpango huo ambao unaanza kwa nchi za bara la Afrika utakuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kuruhusu uwekezaji wa hali ya juu sana huku hata baadhi ya benki ikiwemo hiyo ya Eco Benki kuweza kukua na uimarika kiuchumi
      Pia alisema kuwa kupitia makubaliano hayo baina ya benki hiyo na PIC pia kutaweza kuongezeka sana kwa shuguli mbalimbali za uwekazaji katika bara la Afrika hali ambayo nayo itachangia sana kukua kwa uchumi ambapo ndilo lengo halisi la makubaliano hayo
     “huu mpango ambao utaenda kwenye nchi 32 za bara la Afrika zitaweza kutumia vema mkataba huo ambapo kupitia hata mpango huo uchumi nao utaaimarika sana na hata kiwango cha uwekezaji nacho kitapanda tofauti na sasa ndani ya nchi hizo”aliongeza Bw Anorld
     Awali alifafanua kuwa kupitia mchakato huo wa nchi 32 za bara la Afrika nayo Eco Benki itaweza kunufaika sana kwa kuwa mapato yake nayo yataweza kuongezeka kwa kiwango cha asilimia 19.58 hali ambayo nayo ni nzuri kwa ajili ya shuguli mbalimbali za uwekezaji wa bara la Afrika.
      Bw Anorld alisema kuwa ili kuweza kuimarisha hata uchumi wa nchi mbalimbali za bara la Afrika wamejiwekea Mikakati maalumu wa kuhakikisha kuwa kila jamii inafikiwa na huduma muhimu kwa ajili ya kukuza na kuimarisha uchumi ambao ndio lengo halisi la Benki hiyo
      Alitaja Mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa benki hiyo inajikita zaidi kwenye kila kona ya nchi ambapo kupitia kona hizo wataweza kuwekeza kwa kiwango cha hali ya juu sana hali ambayo nayo itachangia kukua na kuimarika kwa uchumi barani Afrika.

VURUGU ZANZIBAR,CUF YATOA TAMKO

Umma unashuhudia hali tete ya machafuko ambayo hayakutarajiwa yakiibukia tena Zanzibar ,wakati ambapo Nchi ilishaanza kunawiri matunda ya utulivu na maridhiano, chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
     Pamoja na sababu au visingizio mbali mbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwamo hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hikma, matumizi ya nguvu za dola, na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutopendelea Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar.
    Kwa thamani yoyote hakuna asiyeweza kubaini umuhimu wa hali ya amani na utulivu, na madhara ya kukosekana kwake, hasa katika Visiwa hivi vya Unguja na Pemba ambavyo vimewahi kuelemezewa athari kubwa ya machafuko kwa muda mrefu.
     Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania, hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo, kwa maslahi binafsi, na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa.
     Chama cha CUF, kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao .
     Vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na Utamaduni wa Kizanzibari; uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria, bila uonevu wala upendeleo.
     Tahadhari iwepo ya kuepuka matumizi ya mabavu yanayoweza kuleta hamasa kwa wananchi, hatimaye ikachochea vitendo vya hujuma dhidi ya watu na mali zao, na pia kuepuka tabia isiyokuwa ya haki, ya kuwabambikizia kesi wananchi.
      Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.

HAKI SAWA KWA WOTE
Salim  A Bimani
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari na
Uenezi na Mahusiano na Umma

SEMINA YA WAPIGAPICHA ZA HABARI WAANDAMIZI YAFANYIKA LEO

May 28, 2012

 Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari-Tanzania Media Fund (TMF) , Ernest Sungura akifunghiua semina ya wapigapicha za habari waandamizi, leo kwenye ukumbi za Msimbazi Centre, Dar es Salaam. Kushoto ni mratibu wa semina hiyo Selemani Mpochi na watatu kushoto ni OfisaMawasiliano wa Airtel Dagio Kaniki.
Wapigapicha wakiwa kwenye semina hiyo
Mkufunzi kutoka Frem Tree, Mwanzo Milinga akitoa mafunzo kuhusiana na kazi ya kupiga picha za habari, wakati wa semina hiyo

MA-DC NA MA-RC WATEMBELEA CHUO KIKUU CHA DODOMA

May 27, 2012

Wakuu wa mikoa na wa Wilaya wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo jipya la Utawala la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walipotembelea chuo hicho leo. Picha kutoka HABARI MSETO BLOGU

MAMBO YA YANGA

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Mei 26 mwaka huu ili kutoa mwongozo wa nini kifanyike ndani ya Yanga baada ya wajumbe wake kudhaa kujiuzulu. Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ilikuwa imeomba mwongozo huo TFF.
      Baada ya kupata taarifa rasmi kutoka Yanga, Kamati imebaini kuwa Kamati ya Utendaji ya Yanga imekosa akidi baada ya wajumbe wake wengi kujiuzulu hivyo kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi kwa mujibu wa Ibara ya 32(1) ya Katiba ya klabu hiyo.
      Hivyo, Kamati imetoa mwongozo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambayo ndiyo msimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuwa ili Kamati ya Utendaji ya Yanga iwe na nguvu za kikatiba kufanya shughuli zake ikiwemo uamuzi wa masuala mbalimbali ndani ya klabu hiyo ni lazima iwe na akidi.
      Kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) ya Katiba ya Yanga nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zinatakiwa kujazwa katika Mkutano Mkuu wa Kawaida ujao.
      Pia Kamati imebaini uteuzi wa kujaza nafasi zilizo wazi za wajumbe uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mei 21 mwaka huu ni batili kwa vile Kamati ya Utendaji iliyofanya uteuzi huo haikuwa na akidi.
      Ili kupata akidi na kufanya uamuzi Kamati ya Utendaji ya Yanga yenye wajumbe 13 inatakiwa kuwa na asilimia 50 ya wajumbe wote, hivyo ili wafanye uamuzi halali hawatakiwi kupungua saba.
      Kwa wajumbe ambao hawajajiuzulu; Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro na Salim Rupia kwa sasa hawawezi kufanya shughuli zozote za Yanga hadi nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zitakapojazwa.
      Kama inavyoelekeza Katiba ya Yanga, shughuli za kila siku za klabu hiyo zitaendelea kufanywa na Sekretarieti ya Yanga ambayo kiongozi wake ni Katibu Mkuu.
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji

ARUSHA WAFUNIKA RUAHA HALF MARATHON 2012

IRINGA
WAKAZI wa mjini Iringa mwishoni mwa wiki walishuhudia kwa mara ya kwanza wanariadha zaidi ya 320 wakichuana katika mbio za barabarani za Ruaha Half Marathon huku wanariadha kutoka mkoani Arusha wakitawala.
       Katika mbio hizo, zilizoanzia mnara wa saa karibu na ofisi za Manispaa ya Iringa na kuelekea njia ya kwenda Ruaha National Park na kurudi hadi uwanja wa Samora  ambako zilihitimishwa, kwa upande wanaume Alphonce Felix kutoka sekondari ya Winning Spirit alishika nafasi ya kwanza akitumia saa 1:03.09 huku kwa wanawake, Mary Naali kutoka klabu ya Skytel akishinda kwa saa 1:13.01.
      Alphonce alifuatiwa na Dickson Marwa wa klabu ya Mbui ya jijini Dar es Salaam 1:03.29 huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Saidi Makula wa Winnig Spirit 1:03:29 mshindi wa nne Getuni Tsekeway pia wa Arusha 1:04.06 wakati aliyefunga tano bora alikuwa ni mwenyeji, Moses Mwadeni aliyetumia saa 1:11:18.
      Naali ambaye kwa muda huo kaweka rekodi kwa wanawake hapa nchini, alifuatiwa kwa mbali na Stephancy Perkins kutoka Australia aliyetumia saa 1:32.55, Natali Struble wa Marekani alishika nafasi ya tatu kwa saa 1:38.50 huku nafasi ya nne ikienda kwa Yoko Imamura wa Japan 1:59.00 wakati Mia Mjengwa wa Iringa alifunga tano bora akitumia saa 2:03.00.
       Mbio hizo, ambazo zimepangwa kufanyika kila mwaka Jumamosi ya mwisho wa Mei, kwa mwaka huu wa kwanza zilishirikisha wanariadha chipukizi wengi kutoka Iringa na mikoa za jirani na baadhi wa kimataifa wa hapa nchini na kutoka nje. Ruaha Half Marathon, iliratibiwa na kudhaminiwa na shirika lisilo la kiserikali
la Mindset Empowerment (ME), lenye makao yake makuu mjini Iringa, zikiwa na ujumbe wa kulinda na kuboresha mazingira, ambako kauli mbiu yake ikiwa ni 'Mazingira bora kwa utalii endelevu, Okoa mto Ruaha’.

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA YAFANA, LONDON-UINGEREZA

 Mheshimiwa Balozi wa Uganda, Mama Joan Rwabyomere, akifungua Maadhimisho ya siku ya Afrika hapa nchini Uingereza, katika sherehe ambazozilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, London.
 Mheshimiwa Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika.
 Kutoka kulia, Dada Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, Bwana Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Dada Jestina George, maarufu kama Queen wa Blog hapa Uingereza.
 Mabalozi ,Maafisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
 Dada Jestina George na dada Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao katika sherehe hizo za siku ya Afrika                                                                                                                                                          

Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, wakitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika hapa London

MISS DAR INTER COLLEGE KURINDIMA JUNI 8 CLUB SUNCIRO


SHINDANO la kumsaka Miss Dar Intercollege 2012 linatarajiwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Sunciro, ulipo Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam, imefahamika.
     Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba warembo watakaoshiriki shindano hilo wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.
    Alisema mpaka sasa warembo 12 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamesharipoti kambini.
    Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus,Jane Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.
    Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.
    “Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano letu…mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na Clouds Fm.

VITABU VYA MZEE MAKAMBA VYAZINDULIWA LEO NA MAKAMU WA RAIS

 Vitabu 'Binadamu na Kazi' na Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kurani Tukufu, Suna za Mtume Muhammad (SAW) na Sheria za Nchi vilivyozinduliwa leo na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, kwenye ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais akionyesha kitabu cha kwanza baada ya kuzindua. Kulia ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Kushoto ni Mama Januari, mke wa Mzee Makamba.
Dk. Bilal akionyesha kitabu cha pili  baada ya kuzindua

YANGA NA SIMBA WASHIRIKI UZINDUZI RASMI WA 100 TZ FLAVA YA BIA YA KILIMANJARO

May 26, 2012

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe akizindua rasmi Kampeni ya 100% TZ Flava inayoendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager huku akiwa  na Wachezaji wa Vilabu vya Simba na Yanga, wasanii wa Bongo Movie na Bongo Flava. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Nyumbani Lounge Jijini Dar es Salaam juzi.

Kilimanjaro Premium Lager Brand Manager George Kavishe officially launches the 100%TZ Flava Campaign  that is being run by Kilimanjaro Premium Lager as he is flanked by players of Simba and Yanga clubs, Bongo Movie stars and Bongo Flava Artistes. The launch took place at Nyumbani Laounge in Dar es Salaam on Thursday evening.

TASWA WAMPONGEZA MHARIRI WA MICHEZO TANZANIA DAIMA

Tullo Chambo

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimatoa pongezi kwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Tanzania Daima, Tullo Chambo kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Tanzania (RT).

Taarifa ya Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando imesema, Chambo alitwaa nafasi hiyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa RT uliofanyika Jumapili mjini Morogoro, ambapo ni miongoni mwa wajumbe wapya walioingia kwenye chama hicho.

Wengine walioshinda ni Anthony Mtaka ambaye anakuwa Rais mpya wa RT, wakati Makamu wa Rais Utawala ni William Kallaghe, Makamu wa Rais Ufundi, Dk. Ahmed Ndee, Katibu Mkuu, Suleiman Nyambui, Katibu Msaidizi, Ombeni Zavalla, Mhazini, Is-Haq Suleiman.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mwinga Mwanjala, Meta Petro, Peter Mwita, Rehema Killo, Lwiza John, Zakaria Barrie, Zakaria Gwanda, Robert Kalyahe na Christian Matembo.

TASWA inatambua Chambo ni mwanahabari mzoefu, ambaye kwa muda mrefu amekuwa mhariri wa habari za michezo na ni mtu mwenye kujua mambo mengi yanayohusu riadha, hivyo atakuwa kiungo muhimu kwa watu wa riadha, pia atakuwa kiongo kizuri kwa waandishi wa habari za michezo kuhusiana na mambo ya riadha.

TASWA inaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kadri itakavyoweza na inamtakia kila la heri, huku ikiamini hatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa RT waliomuamini wakamchagua kushika wadhifa huo.

Pia Taswa inawapongeza viongozi wote wa RT walioingia madarakani Jumapili, ikiamini watakuwa chachu ya mafanikio ya riadha hapa nchini.

MKE WA MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA NA WATANZANIA BOTSWANA

Mke wa  Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi nchini Botswana baada ya kuzungumza nao jana jioni mjini Gaborone Botswana. PICHA NA VPO

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS WA ANGOLA

Mjumbe maalum wa Rais wa Angola Dr.Andre de Oliveira Sango akiwasilisha ujumbe maalum kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

LLYOD NCHUNGA AACHIA NGAZI YANGA

May 24, 2012

Baada ya vuta ni kuvute iliyogubika Klabu ya Yanga baada ya kukumbwa na mnikasa mingi ikiwemo kukumbwa na madeni na kufanya vibaya katika michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyomalizika, aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Llyod Nchunga ameachia ngazi.
     Habari zilizoufikia mtandao huu zimesema Nchunga ametangaza uamuzi huo leo baada ya kinachoonekana maji kumfika shingoni.
    Hatua hiyo, Nchunga ameichukua baada ya wiki iliyopita, Wanachama wa Yanga wakiongozwa na Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa timu hiyo kukutana klabuni hapo na kutangaza kumfukuza.
Hata hivyo baada ya hatua ya wanachama hao ilipingwa na baadhi ya wadau wa michezi ikiwemo TFF kwamba hawakufuata taratibu.

TIMU YA MALAWI YATUA LEO NCHINI

Dar es Salaam, Tanzania
Timu ya Taifa ya Malawi-The Flames (pichani) inatarajiwa kuwasili nchini leo jioni kwa ndege ya Air Malawi kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayofanyika Jumamosi (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
        Mechi hiyo ni kwa ajili ya kujipima nguvu Taifa Stars kabla ya mechi yake ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini chini ya Kocha Kim Poulsen.
       Malawi itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu ambapo Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
       Malawi ambayo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu baada ya mechi hiyo itakwenda Zanzibar ambapo Mei 28 mwaka huu itacheza na Zanzibar Heroes.
      Makocha wa timu zote mbili Taifa Stars na The Flames kesho (Mei 25 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF.

KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA AFRIKA KUSINI

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akizungumza na ujumbe wa wafanyabisahara kutoka Afrika Kusini, ulipokwenda ofisinbi kwake, Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni kiongozi wa msafara huo, Dumisan Sooi

BIA YA KILIMANJARO YAZINDUA KAMPENI MPYA YA KILI-100% TZ FLAVA

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza katika semina ya waandishi wa habari za michezo kuitambulisha kampeni mpya ya '100% Tz Flava' inayoendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo kwenye hoteli ya New Africa, jijini Dar es Salaam.

MNYIKA ASHINDA KESI YA UBUNGE MAHAKAMA KUU LEO


Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika akiwa na aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi Mkuu 2010,Hawa Nghumbi, wakati wakisubiri hukumu, katika Mashakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuhusu kesi  ya kupiga matokeo yaliyompa ushindi Mnyika iliyofunguliwa na Nghumbi kwenye mahakama hiyo.


HUKUMU UBUNGE WA MNYIKA LEO

Mnyika
Hukumu ya kuendelea kuwa mbunge au kutenguliwa Ubunge wa mbunge wa Ubungo John Mnyika ni leo kuanzia mida ya saa nne asubuhi hii.
   Kesi hiyo namba 107 ya mwaka 2010 ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa 2010, Hawa Nghumbi.

IVITATION TO THE LAUNCH OF THE FIRST AFRICA HUMAN DEVELOPMENT REPORT 2012

May 23, 2012

The United Nations Development Programme (UNDP) cordially invites the media to the launch of the first Africa Human Development Report 2012 (AHDR) titled “Towards a Food Secure Future” to be held on Friday 25th May 2012, at National College of Tourism, Bustani Campus Conference room, Shaban Robert Street, Adjacent to International House, at 0900am.

The report will be launched by the Deputy Minister of Finance, Hon. Janeth Mbene. Invited guests includes members of diplomatic corps, academicians, government officials and the media.

UNDP's Africa Human Development Report 2012 argues that human development in sub-Saharan Africa can only be fully realized when there is food security for all. Noting that this is an issue that goes beyond agriculture, the report explores the interlocking themes of agricultural productivity, nutrition, resilience and empowerment through the powerful prism of human development.

The report shows that food security and human development reinforce each other. To accelerate food security, countries in sub-Saharan Africa must boost agricultural productivity and enhance nutrition to improve availability, access and use of food.

The Africa Human Development Report is an editorially independent publication of the United Nations Development Programme (UNDP).

EVENT:  
         LAUNCH OF AFRICA HUMAN DEVELOPMENT REPORT
                         
DATE: 
    25 MAY, 2012

TIME:
 0900 AM

VENUE:
         NATIONAL COLLEGE OF TOURISM, BUSTANI CAMPUS CONFERENCE 

ROOM, SHABAN ROBERT STREET,ADJACENT TO INTERNATIONAL      HOUSE

PROFESA MWANDOSYA AAPISHWA LEO

May 22, 2012


Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum Profesa Mark Mwandosya akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Na watatu kulia ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.

BALOZI MPYA WA RWANDA HAPA NCHINI AWASILISHA HATI ZAKE KWA RAIS KIKWETE

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho wa balozi mpya wa Rwanda nchini Tanzania Mhe.Benjamin Ruganguzi wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana. Katikati ni Mkuu wa itifaki Balozi Antony Itatiro(picha na Freddy Maro).

WATATU WAUAWA KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI ARUSHA

Na Rose Jackson,Arusha
Watu watatu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wameuwawa na wananchi  wenye hasira kali  katika eneo la Ngusero mjini hapa  kwa silaha za jadi mara baada ya majambazi hayo kubainika kuwa wanapanga mbinu mbalimbali za kuvamia  nyumba
      Hayo yalielezwa mjini hapa na  kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo  alisema kuwa tukio hilo lilitokea alfajiri ya saa kumi za asubui ambapo majambazi hayo yalifika katika eneo hilo huku yakiwa ndani ya gari
      Alisema kuwa mara baaada ya majambazi hayo kufika katika eneo hilo la tukio wakiwa na gari aina ya Corola lenye namba T830 AHU walianza kuzunguka zunguka katika eneo hilo ili kupanga nyumba ambayo wanaingia hali ambayo iliwashitua wananchi
      Alifafanua kuwa mara baada ya wananchi kutilia shaka gari hilo ambalo lilikuwa na majambazi hao waliamua kuwaweka chini ya ulinzi na kukagua gari hilo ambapo walikutana na Silaha za jadi  pamoja na silaha nyingine ambazo ni za kuvunjia  nyumba hali ambayo ilisababisha waweze kupigwa sana na wananchi hao
      “inavyosemekana ni kwamba hawa majambazi walikuwa wameshazunguka san a na gari lao kwa muda mrefu sana na sasa mara baada ya kuhisiwa wananachi waliamua kujichukulia sheria mkononi na kisha kuanza kuwapiga sana hali ambayo ilisababisha Mauti yao hapo hapo”alisema kamanda Andengenye.
      Aliongeza kuwa mara baada ya Jeshi la Polisi kufika katika eneo hilo waliweza kugundua kuwa kati ya majambazi hayo matatu mawili yalikuwa yanatafutwa na jeshi hilo bila mafanikio kwa kuwa walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha ndani ya maeneo mbalimbali ya Mji wa Arusha
      Pia alisema kuwa majambazi hayo yalifajhamika  kwa majina ya Philipho Naftari,huku jambazi mmoja amejulikana kwa jina la Utani ambalo ni shidaa na mwingine hajajulikana jina lake huku jitiada za kuwatafuta ndugu zake zikiwa zinaendelea.
      Hataivyo kamanda huyo alisema kuwa pamoja na kuwa waliowawa walikuwa ni majambazi lakiniPolisi inatafuta chanzo halisi cha aliyeanzisha kipigo na kusababisha wengine kuwauwa majambazi hayo kwa kuwa wengeweza kusaidiasana  polisi katika upelelezi wao lakini kwa kuwa wameshawauwa hakuna upelelezi  tena
      Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia mkazi mmoja wa longido kwa kosa la kumsukuma Rafiki yake na kisha  kudondoka na kupoteza maisha papo hapo katika baa moja iliyojulikana kwa jina laZebra.
        Kamanda Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea  May 20 majira ya saa kumi za jioni ambapo mtu mmoja liyefhamika kwa jina la Abuu Msema alifariki dunia mara baada ya kusukumwa na rafiki yake ambaye aliyejulikana kwa majina ya Frank Mmasi  mkazi wa Longido mjini hapa
        Alisema kuwa katika siku hiyo ya tukio  Marehemu akiwa na rafiki yake wakiwa ndani jya baa ya Zebra walikunywa pombe sana linaendelea na upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo huku mtuhumiwa naye akiendelea kuhojiwa juu ya mauaji hayo na atafikishwa mahakamani upeleezi utakapokamilika.
     lakini marehemu alikataa kuondoka huku rafiki yake akimtraka aondoke hali ambayo ilimfanya amnyanyue kwa nguvu huku akiwa amelewa na badaye alidondoka chini na kufariki dunia papo hapo

MWANAME ATESEKA NA UJAUZITO WA MIAKA MINNE, ARUSHA

Rose Jakson- Arumeru
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja a julikanae  kwa jina la Chausiku Selemani(48) mkazi wa maji ya chai mkoani hapa yuko katika hali ya sintofahamu baada ya  kubeba mimba ya miaka minne ambayo ni ya mtoto wa 17  na hadi sasa  hajui siku ya kujifungua , hali ambayo imemfanya kuwaomba watu wenye mapenzi mema kujitokeza kumsaidia ili aweze kufanyiwa upasuaji.

Chausiku aliyasema hayo nyumbani kwake alipokuwa akiongea na mtandao huu, kuhusiana na hali aliyonayo ambayo imemfanya asijue la kufanya huku akiwa anakabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Alisema kuwa  katika maisha yake uzazi wake umekuwa wa shida kwa kuwa kila anapozaa mtoto ni lazima tumboni kibakie kiumbe cha miezi miwili hali inayompelekea kuzaa kila mwaka hadi kufanya kufikia  watoto 16 ambapo kati ya hao watatu walishafariki dunia  .

“Mimi mara ya mwisho kujifungua ilikuwa mwaka 2008 ambapo mara tu baada ya kujifungua nilimwambia daktari aniangalie kuna kitu kimebaki tumboni ,alivyoangalia aliniambia ni uvimbe upo hivyo nahitajika laki tatu na nusu ili nifanyiwe upasuaji lakini kutokana na hali niliyokuwa nayo sikupata fedha hizo hali iliyopeleka kiumbe hicho kukua hadi leo hii ni mtoto  namsikia kabisa akichezal akini kila nikipimwa haonekani”alisema chausiku

Aliongeza kuwa ilimlazimu  aenda katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro (KCMC)   na ndipo  madaktari wa kafanikiwa kumkata mirija ya uzazi ili kuthibiti hali hiyo lakini cha kushangaza uvimbe huo uliendelaea kukua hadi leo hii   ambapo  ameeleza kuwa kukatwa kwa mirija hiyo huenda ndio chanzo cha ujauzito huo ku kaa tumboni kwa miaka minne.

Kupitia hali hii mama huyo amewaomba watu wenye mapenzi mema wa msaidie kwa lolotelile ikiwa ni pamoja na maombi ili kumwezesha  kwenda kufanyiwa upasuaji ili aweze kutolewa kiumbe hicho ambapo kimemfanya hata kushindwa  kuwahudumia watoto waliopo kwani ni wadogo na kipato cha mume wake hakitoshelezi.

“Hapa kwangu hali ni mbaya sana kwani hata watoto hawana hata sehemu ya kulala na wengine wanasoma shule hawana hata sare za shule hivyo naombeni hata mkinisaidia kwa maombi naamini mungu atanisaidia “aliongeza

Kwa upande wake diwani wa kata ya maji ya chai Loth Nnko alikiri kuwepo kwa tatizo la  mama huyo na kusema kuwa yuko tayari kuangalia namna ya kuwasaidia kuwalipia ada za shule kwa wale watoto wa  watakaofaulu darasa la saba.

Amesema mama chausiku anahitaji msaada wa hali na mali hivyo amewataka watanzania wenye mapenzi mema na mama huyo kumsaidia ili aweze kufanyiwa upasuaji hospitali ambapo awali ilitakiwa jumla ya shilingi laki tatu na nusu  hivyo huenda kiasi hicho huenda kikawa kimeongezeka

Wasamaria wema wanaweza kutuma mchango wao wa m-pesa kupitia nambari ya simu ya mume wake ambaye ni Elidaima Kimoso 0764-65 02 88

WASHIRIKI DAR INTERCOLLEGE 2012 KUANZA KUJIFUA LAMADA

Na Mwandishi Wetu
WAREMBO watakaoshiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 leo wanatarajiwa kuanza mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo kwenye hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba warembo hao watatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, pamoja na  Ustawi wa Jamii.

“Kesho (leo) tutaanza mazoezi yetu pale Lamada ambapo warembo kutoka vyuo vinne wataanza kujinoa…wiki ijayo huenda tukaongeza washiriki wengine ambao watatoa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambao wanafanya shindano lao mwishoni mwa wiki hii,”alisema.

Alisema kuwa warembo hao watakuwa chini ya ukufunzi wa  mrembo aliyepata kushiriki shindano hilo, Rose John, huku kwa upande wa shoo watanolewa na Bob Rich.

Dina aliwataja wadhamini waliojitokeza mpaka sasa ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, na  Dodoma Wine, huku akiomba makampuni mengine kujitokeza kudhamini shindano hilo litakalofanyika mwezi ujao.

SHIBUDA AZIDI KUKOMALIA MSIMAMO WAKE KUGOMBEA URAIS 2015

May 21, 2012

 Awaomba wanachama wa Chadema wamuunge mkono
SHINYANGA
SHIBUDA
MBUNGE wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Magalle Shibuda, ameendelea kusisitiza nia na msimamo wake wa kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
      Amewaomba kwa dhati wanachama wenzake wa CHADEMA kumwunga mkono katika nia yake hiyo na pia katika harakati zake za kukosoa  tabia hasi ya baadhi ya viongozi wa chama hicho ya kuwanyima wanachama uhuru wa kutoa maoni kinyume na matakwa ya demokrasia.
       Aliyasema hayo juzi wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Shinyanga waliotaka kufahamu mustakabali wake na CHADEMA kufuatia tangazo lake la nia ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho lililozua mlolongo wa lawama kutoka kwa baadhi ya viongozi hususan Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Bw. Ezekiel Wenje.
      "Nasisitiza nia yangu kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama changu cha CHADEMA katikas uchaguzi mkuu ujao", alisisitiza nia yake.
       Shibuda alisema tatizo lililopo na linalozidi kupanuka katika chama hicho ni baadhi ya wanachama na viongozi kuwa na fikra hafifu na kutokuheshimu demokrasia katika vyama vya kisiasa
KWA HABARI ZA KINA ZA HABARI HII PATA GAZETI LA UHURU KESHO

RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI MAHAKAMA YA RUFANI

RAIS KIKWETE
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
     Taarifa iliyotolewa jioni hii na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imewataja walioteuliwa ni Jaji Semistodes S. Kaijage na Jaji Kipenka M. Musa.
  "Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Mei 21, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi wao ulianza tokea Machi 15, mwaka huu, 2012", taarifa hiyo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema.
     Imesema kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kaijage (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tangu Mei 17, 2007. Aliteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu Novemba 28, mwaka 2000.
    Naye Jaji Musa (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
     Pia amewahi kuwa Wakili wa Serikali, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Septemba 13, 2004.

BALAA DUNIANI!!!. 93 WAUAWA NA 300 KUJERUHIWA KWA BOMU YEMEN

Askari akiwa  katika  uokoaji
WATU 90 wamekufa na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa vibaya katika shambulio la kigaidi lililotokea leo nchini Yemen.
    Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha  Aljazira, shambulio hilo lililenga wanajeshi nchini humo.
    Taarifa zinasema mlipuko huo umetokea baada ya askari mmoja wa Yemen aliyekuwa amesheheni mabomu kujilipua katika eneo la kijeshi.

WANACHUO WAPORWA NA MAJAMBAZI ARUSHA, WALIACHA GETI WAZI

NA ROSE, ARUSHA 
WANAFUNZI  wa Chuo cha Uhasibu, Njiro jijini hapa, wamevamiwa usiku na watu wanaoaminika kuwa ni majambazi na kuporwa vitu mbalimbali vvenye thamani ya zaidi ya Milioni 10. 
       Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye amesema tukio hilo lilitokea juzi, musa wa  saa 2 usiku katika eneo la chuo hicho. 
        Kamanda Andenyenye alisema kuwa siku ya tukio katika nyumba inayomilikiwa  na Bw Frank Maungo ambayo inatumikia na wanafunzi hao kama bweni la wavulana  lilivamiwa na kundi la vijana ambao wanasadikika kuwa ni majambazi 
       Aliendelea kusema kuwa  mara baada ya kuvamia  nyumba hiyo ambayo inatumika kama bweni  majambazi hayo yalivunja Milango ya Vyumba vitano na kupora vitu mbalimbali ambavyo vilikuwa vinatumiwa na wanafunzi hao katika shuguli mbalimbali za masomo 
      Alitaja vitu ambavyo vimeorwa na majambazi hao kuwa ni pamoja simu za aina mbalimbali za mikononi,Laptop za aina mbalimbali  sita zenye thamani tofauti tofauti,kadi za benki ambazo zilikuwa zinatumiwa na wanafunzi hao,pamoja na Fedha taslimu ambazo zote zinakamilisha idadi ya zaidi ya Milioni kumi.
      “ walipoingia ndani waliiba vitu hivi vyote na baada ya hapo watu hao ambao walikuwa wanadhaniwa ni majambazi walitoweka na vitu hivyo bila ya wanafunzi hao na watu wengine kujua kuwa wametokomea wapi”alisema Kamanda Andengenye 
       Mbali mna hayo alisema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa majambazi hayo yaliingia katika bweni hilo la wanafunzi wakiwa na silaha  za jadi kama vile Mapanga,na Marungu  ambapo  mara baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya Bweni hilo na wakazingira kila chumba  na kisha kuwaamuru  wanafunzi  watoe kila kitu walichonacho 
       Kamanda Andengenye aliongeza kuwa  hata kwa upande wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa wanafunzi hao ndani ya siku ya tukio walikuwa wametoka kuangalia mpira wa Fainali ya Kombe la Mabingwa ya Ulaya kati ya Chelsea na Bayern Munich uliomalizika muda wa saa 6;30 usiku na waliporudi  wakaingia kulala katika vyumba vyao bila kufunga lango kuu na njia hiyo ikawa ni rahisi sana kwa majambazi hayo kuingia ndani 
     Awali kamanda huyo alisema kuwa katiika tukio hilo hakuna mtu yeyote ambaye amejuriliwa na bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini Majambazi hayo ambayo yamefanya uhalifu huo

IFM MABINGWA SAFARI HIGHER LEARNING DAR

Nahodha wa timu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Charles Evance, akikabidhiwa Sh.500,000 na Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mlimi, baada ya timu yake kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Pool Safari Higher Learning yaliyomalizika, jana, jijini Dar es Salaam.

HABARI KAMILI:

CHUO cha usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam(IFM) wametetea ubingwa wao juzi katika mashindano ya Pool Safari Lager Higher Learning yaliyomalizika kwenye Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
       IFM waliutwaa ubingwa huo kwa kuwachapa majirani zao chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) 4-0,hivyo kujitwalia tena ubingwa kwa mara ya pili kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kuibuka na zawadi ya kitita cha Shilingi laki tano
       Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni CBE ambao walizawadiwa laki tatu,wapili ni Chuo cha Ardhi ambao walipata laki mbili na wanne ni Chuo cha DIT ambao walipata laki moja.
        Wachezaji wa singles(mmoja mmoja) wanaume alishinda Peter Patrick kutoka chuo cha IFM alinyakua ubingwa akifuatiwa na Goodhope Mamkwe kutoka IFM pia,wakati upande wa Wanawake bingwa alikuwa Modesta David kutoka IFM akifuatiwa na Lilian Meiri kutoka chuo cha CBE.


VYUO VINANE VYAFUZU KUSHIRIKI FAINALI ZA SAFARI POOL.
 Katika hatua nyingine, vyuo vinane vimefaulu kuingia katika fainali za mashindano ya Pool Safari Higher Learning yatakayofanyika Mkoani Iringa May 26 mwaka huu kutoka katika Mikoa minane.
       Akizungumza mratibu wa mashindano hayo, Michael Machellah vyuo vilivyofaulu kuingia katika fainali hizo ni Morogoro ni Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kilimanjaro ni  Chuo cha Ushirika Moshi(MUCCOBS), Dodoma ni St.John,Arusha ni Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Mwanza ni St.Augustine,Iringa ni Ruaha(RUCO),Mbeya ni  Chuo cha Uhasibu(TAA) na  Dar es Salaam ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
       Wachezaji wa singles(mmoja mmoja) wanaume na wanawake kila mkoa watawakilishwa na mabingwa wa kila mkoa ambapo Morogoro ni Moyo Hamza kutoka Chuo cha Ardhi na Fotunate Shija kutoka chuo cha SUA,Kilimanjaro ni Alphael Jackson kutoka MUCCOBS na Suche Anastasia kutoka KCMUCO ,Dodoma ni justace Mhando kutoka MIPANGO na Lemi Jackson kutoka U-DOM na Waku ,Arusha ni Vicent Katiyega kutoka chuo kikuu cha Arusha(UOA) na Violeth Silas kutoka IAA ,Iringa ni Said Mohamed kutoka RUCO na Beatrice kutoka RUCO, Mwanza ni Joachim Mushi kutoka CBE na Agnes Mtalika wa chuo cha Bugando,Mbeya ni na Dar es Salaam ni Feter Patrick kutoka chuo cha IFM na Modesta David kutoka IFM.

WAZIRI DK TEREZYA AKUTANA NA BALOZI WA BRAZIL

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira Dk. Terezya Huvisa. Akizungumza na Balozi wa Brazil, Nchini Tanzania, Comoro na Seychelles Bw. Francisco Carlos Joares Luz. Ofisini kwake mjini Dar es Salaam, leo. Mazungumzo hayo yalihusu maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Rio +20. Picha na Ali Meja.
ยช