.

BONANZA LAA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA BIA TANZANIA (TBL)

Jun 30, 2012

Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), pamoja na ndugu zao wakishindana katika mchezo wa kuvuta kamba kwenye bonanza la kufurahi pamoja na familia zao, katika ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi Beach,Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki. PICHA ZAIDI INGIA KATIKA UKURASA WA MATUKIO-BOFYA HAPA

ZANZIBAR KIDEDEA MICHUANO YA UMISETA

KIBAHA, TANZANIA
Timu ya Soka ya Kanda ya Zanzibar imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya 34 ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa kuifunga Kanda ya Kaskazini Mashariki kwa magoli 2-1.
         Fainali hiyo ambayo ilikuwa na msisimko tangu mwanzao wa mchezo na kushuhudiwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Anjela Kairuki, ilipigwa kwenye uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.
        Zanzibar walianza kuandika bao kwenye dakika ya 56 ya mchezo kupitia kwa Ibrahim Hamad ambaye aliongeza bao la pili kwenye dakika ya 61 ya mchezo huo ambao uliwavutia wakazi wa mji wa Kibaha na vitongoji vyake.
       Kaskazini Mashariki walijitahidi kuhakikisha wanarejesha magoli hayo lakini ukuta wa Zanzibar ulikuwa imara na kuondo hatari zote zilizoelekezwa langoni mwao kabla ya dakika ya 80 kupata bao kupitia kwa Obisa Joel.
       Kwa upande wa wasichana Kanda ya Dar es Salaam walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuifunga Kanda ya Mashariki kwa penati 3-1 baada ya dakika 90 kuisha timu hizo zikiwa sare ya goli 1-1.
     Kwenye mchezo wa Kikapu wavulana Dar es Salaam iliifunga Mashariki kwa vikapu 88-72. Kutokana na matokeo ya michezo mbalimbali Kanda ya Dar es Salaam wameteuliwa kuwa mabingwa wa jumla wakifuatiwa na wenyeji Mashariki na watatu ni kanda ya Kaskazini Magharibi.
    Michezo hiyo ya 34 iliwashirikisha wanamichezo 1,659 kutoka kanda 12 na walishindana kwenye michezo ya bao, soka, meza, kikapu, riadha, mikono na wavu.
 Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Anjelina Kairuki amesema kuwa kamati ya bunge ya sheria itafuatilia halmashauri ambazo zitashindwa kutekeleza agizo la serikali la kutenga bajeti za michezo.
       Akifungua mashindano   ya 34 ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) kwenye uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha,mkoa wa Pwani, alisema, serikali imekuwa ikitoa maelekezo kwa halmashauri kuweka mipango na kupanga bajeti kwa ajili ya kuendeleza michezo hasa ya vijana wadogo lakini utekelezaji imekuwa ni tatizo.
     “Kamati ya hseria na katiba ipo hivyo tungependa yaleyanayopendekezwa yafanywe kwa vitendo kwani tunaweza kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kupitia michezo,” alisema Kairuki.
     Alisema kuwa ili nchi iweze kufanikiwa kimichezo ni lazima iwekeze kwa vijana kwenye michezo kwa gharama yoyote kwani kizuri ni gharama.
   “Halmashauri zinapaswa kuhakikisha walimu wanapelekwa kwenye vyuo vya michezo na wanatumiwa ipasavyo na kuwe na viwanja vyenye ubora ili kuinua michezo nchini,” alisema Kairuki.
    Aliwataka wazazi kutowakatisha tamaa watoto wao ambao wana vipaji vya michezo bali wawaunge mkono ili waweze kufikia mafanikio yao na nchi kwa ujumla.

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MAMA WA STEVEN WASSIRA

Jun 29, 2012

Rais Jakaya Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wakitoa salama zake za mwisho kwa mwili wa Mama wa Waziri Steven Wasirra, Masaki, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni  Waziri Wasira,

BAN KI MOON AMUAGA RASMI DK. ASHA-ROSE MIGIRO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizingumza wakati wa hafla maalum aliyoandaa kumuaga Naibu Katibu Mkuu wa UN, Dk. Asha-Rose Migiro kwenye Ofisi za UN mjini New York Picha zaidi BOFYA HAPA

NAIBU KAMANDA VIKOSI VYA AMANI DARFUR AKUTANA NA NAAFISA UBALOZI WA TANZANIA UN

 Meja Jenerali  Wynjones Kisamba, Naibu Kamanda wa Vikosi  vya kulinda amani katika Jimbo la Darfur akibadilishana mawazo na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, katika mazungumzo  yake na maafisa hao, Meja Jeneral amezungumza kwa kina fursa za uwekezaji zilizopo  katika nchi  ya Sudani ya Kusini namna gani Tanzania na watanzania  kama wakijipanga na wakithubutu watakavyoweza kunufaika na fursa hizo ambazo amesema kwa sasa zimechangamkiwa sana na majirani zetu ili hali Tanzania bado tukisuasua. Akazungumzia pia kuhusu operesheni ya kulinda amani huko darfur na changamoto zake, lakini pia  uwepo wa fursa ya Tanzania kupanua ushiriki  wake katika eneo hilo.
 Baadhi ya Maafisa wa Ubalozi wakiwa  katika picha ya pamoja na  Meja Jenerali Kisamba, ambapopia alitumia mazungumzo yake na maafisa hao  kuwashukuru na kwa kazi nzuri ya kuiwakilisha Tanzania katika Umoja wa Mataifa, huku akiwataka kuto legeza kamba katika kutetea maslahi ya nchi na vile vile kutoa ushauri endelevu katika masuala mbaliambali yanayohusika na utekelezaji wa majukumu yao.  HABARI KUHUSU TUKIO HILO BOFYA HAPA

RASILIMALI YA WANYAMAPORI MBUGA YA MIKUMI LIVE

Twiga akikatiza barabara katika mbunga ya Mikumi, Morogoro, juzi, Picha zaidi BOFYA HAPA

MGOMO WA MADAKTARI: MBEYA NA DODOMA WATIMULIWA

Jun 28, 2012

TANZANIA
BODI ya hospitali ya Rufani Mbeya, imewatimua kazi madaktari 54 waliokuwa katika mazoezi ya vitendo, na wengine 18 waliokuwa wameajiriwa ambao walikuwa wanaendelea na mgomo usio na kikomo.
    Kaimu mkuu wa mkoa wa Mbeya, Dk.Norman Sigalla, aliyasema hayo leo kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi hiyo, mjini hapa.
    Dk.Sigalla alisema Juni 25, mwaka huu Bodi ya hospitali ya Rufani Mbeya, ilifanya kikao cha dharula kujadiri hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini hapo.
   Alisema baada ya kikao hicho iliamuliwa Mwenyekiti wa Bodi (ambaye ni Mkuu wa mkoa), akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika kazini na kujadiri namna ya kumaliza matatizo hayo.
   Aidha, iliamuliwa madaktari wote ambao hawakufika kazini waandikiwe barua za kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali hiyo na pia kukiuka kanuni za utumishi wa umma toleo la 2009, kifungu namba F. 16-17 na F.27.
   Dk.Sigalla aliongeza kuwa hivyo leo, madaktari 54 wamepewa barua zao za kuwaeleza kuwa Bodi ya hospitali ya Rufani Mbeya imesitisha Internship yao hospitalini hapo na kuwarudisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi zinazostahili.
   "Madaktari 18 ambao ni waajiriwa nao wamekabidhiwa barua zao za kusimamishwa ajira yao hospitali ya Rufani Mbeya na kurudishwa Wizarani ya Afya kwa Katibu Mkuu kwa hatua stahiki za kinidhamu" alisema Dk.Sigalla.
   Aliongeza kuwa ni kwa mujibu wa mkataba waliokuwa wameingia nao madaktari hao wa mazoezi ya vitendo, walitakiwa kuwepo kazini kwa mwaka mzima, hivyo kwa kuwa wameshindwa kutekeleza hilo, Bodi ambayo ndio iliingia nao mkataba imeamua kuuvunja.
   Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa mkoa, ili kukabiriana na upungufu wa madaktari hospitalini hapo, tayari Bodi imefanikiwa kuazima madaktari wengine sita kutoka halmashauri ya jiji la Mbeya, ili kuongeza nguvu hospitali ya Rufani Mbeya.
   Kutoka Dodoma Inaripotiwa kwamba, Madaktari 11  wa mafunzo kwa vitendo katika Hospital ya Mkoa wa Dodoma wamesimamishwa kazi kutokana na kuendelea na mgomo.
   Mwenyekiti wa Kamati Jumuiya ya Madaktari Mkoa wa Dodoma Dk. Cassian Mkuwa tukio la kufukuzwa kwa madaktari hao ilitokea leo asubuhi wakati wakiwa hospitalini hapo wakiendelea na mgomo wao.
   Amesema baadaye Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk Ezeliel Mpuya aliwaita madaktari wote waliopo katika mafuunzo kwa nia ya kuzungumza nao kisha alitoa barua kwa madaktari 11 za kuwasimamisha kazi kuanzia leo kutokana na mgomo.
  Hata hivyo madaktari hao walikataa kupokea barua hizo lakini wakatakiwa kuondoka katika eneo la Hopsitali
Dk. Mkuwa akiwa mmoja kati ya waliofukuzwa, alisema anashindwa kuelewa ni vigezo gain vilitumika kuwapata madaktari hao 11 na kuwasimamisha kazi kwani walikuwa wakigoma ni zaidi ya madaktari 20.

DK.ULIMBOKA AZUNGUMZIA HALI YAKE HOSPITALI

Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka  ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya taifa Muhimbili, Dar es Salaam, tangu jana baada ya kupigwa na watekaji nyara, leo amezungumzia hali yake, ambapo ameeleza kwamba ni ya nafuu ikilinganishwa na alivyojuwa jana. Pia amesema kutokana na hali yake anaomba wanaomjulia hali kuacaha kwanza kwa sababu anahitaji kupumzika zaidi. KUONA VIDEO YAKE BOFYA HAPA

SAKATA LA DK. ULIMBOKA KUPIGWA NA WATU WASIOJULIKANA

Jun 27, 2012

Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, wakimwingiza kwenye gari la wagonjwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, Steven Ulimboka, kumpeleka kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) baada ya kufikishwa hospitali leo, baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kipigo na watu wasiojulikana, waliomteka usiku wa kuamkia leo, katika eneo la Mabwepande.             Picha zaidi za tukio hili BOFYA HAPA

DK ULIMBOKA WA MGOMO WA MADAKTARI APIGWA NA KUNDI LA WATU, ALAZWA MOI

Dokta Steven Ulimboka ambaye ni Kiongozi wa Jumuia ya Madaktari  Tanzania akiwa ameumia vibaya kutokana na majeraha ya kipigo alichopia na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA (MB), KUHUSU MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA 2012/2013

Jun 25, 2012

KUSOMA HOTUBA HII BOFYA HAPA

NAPE KATIKA MAHAFALI YA WANA-CCM TAWI LA CHUO KIKUU CHA TEKU, MBEYA

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na viongozi wa  CCM mkoa wa Mbeya baada ya kuwasili leo asubuhi kwa ajili ya ziara ya siku mbili mkoani humo.
 Nape akiongozwa na vijana wa Chipukizi wa CCM, baada ya kuwasili mjini Mbeya kuanza ziara hiyo.
 Nape akiwasalimia baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Mbeya alipokwenda hoteli ya Paradise kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya wana-CCM hao
 Nape akishiriki kucheza muziki wa kwaito na wana-CCM tawi hilo la TEKU
 Wana-CCM tawi la TEKU wakimshangilia Nape ukumbini
 Katibu wa Vijana wa UVCCM mkoa wa Mbeya Ramadhabi Kizinga akihamasiha wakati wa sherehe hiyo ya mahafali
 Katibu wa uchumi na Fedha tawi la CCM TEKU, Eliwasa Wawa akisoma taarifa ya tawi hilo
 Wana-CCM wakila kiapo pamoja na wanachama wapya kwenye mahafali hayo
 Nape akizungumza na wahitimu na wanachama hao
 Nape akimkabidhi kadi ya CCM, mmoja wa wanachama wapya waliopewa kadi wakati wa mahafali hayo
 Nape akiibusu picha yake baada ya kuzawadiwa na wana-CCM tawi la TEKU
 Kisha akaiangalia picha hiyo kwa makini
Hivi ndivyo walifanya kabla ya kumkabidhi picha hiyo.

DORIS KASAKA (KAPINGA) AMEREMETA KWENYE KITCHEN PARTY YAKE ILIYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA TBS - UBUNGO JANA

Doris Kasaka (Kapinga) jana alifanyiwa Kitchen Paty ya nguvu kwenye ukumbi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Hii ndiyo keki iliyokuwa moja ya vivutio kwenye mnuso huo. Picha zaidi zimo kwenye Ukurasa Maalum wa mambo ya Kijamii na Minuso, sasa BOFYA HAPA

MIJAMBAZI YAMPORA SH. MILIONI 12 MSIMAMIZI WA KUNDI LA MUZIKI, ARUSHA

Na Rose Jackson, ARUSHA,TANZANIA
MSIMAMIZI wa kundi la muziki la Contagious lenye makazi yake jijini Arusha,Njara Rasolomanana maarufu kama Dady amevamiwa na kundi la majambazi nyumbani kwake Kimandulo jijini hapa ambapo alijeruhiwa na kisha  kuporwa vitu mbalimbali vyevye  thamani ya zaidi ya sh, milioni 12.  HABARI ZAIDI INGIA UKURASA WA MICHEZO BOFYA HAPA

WAJASILIAMALI 16 DAR WAKABIDDHIWA RUZUKU ZA ZAFARI WEZESHWA.

Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya Ilala, Raymond Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amewakabidhi ruzuku wajasiliamali 16 katika viwanja vya Leaders, kufuatia program ya Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager ambayo inainua wajasiliamali kwa kuwapa vitendea kazi vya kupanua biashara zao.
     Mushi aliwazkabidhi vitendeakazi mbalimbali kwa kila mtu kutokana na alivyoomba wenyewe ikiwa ni pamoja na mshine za kuranda mbao,friji,viti vya bar,meza,compresar za kupakia rangi,Cheranani za kisasa na  vingine vingi.
  Kampuni ya Bia ya TBL kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kufikiri jambo zuri kama hilo ambalo liko kwenye sera ya Taifa kwa kuinua kipato kwa wananchi hasa wanajishugulisha ambao wataisaidia majirani zao,jamii inayo wazunguka kwa kuwaajili na Serikali pia ambayo itafaidika kupitia kodi Mushi alisema.
   Alisema Mushi ni kazi kwenu sasa wajasiliamali mliowezeshwa kuwa mabalozi wazuri wa TBL haswa katika bia hiyo ya Safari Lager kuitangaza na kuinywa ili kurudisha walipotoa na kesho wawezeshwe na wenzenu.
   Jumla ya watu 9638 waliomba kuwezeshwa lakini waliobahatika kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni 16 hivyo aliwataka waliokosa nafasi hiyo wasikate tama awamu nyingine waombe tena.
    Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema mkataba wa ruzuku hizo ni wa miaka mitano hivyo watakuwa wakiwafuatilia wajasiliamali hao kujua maendeleo yao katika kipindi hicho chote wakiwasaidia wanapokwama na kuwaendeleza kuhakikisha wanainuka na kuinua jamii inyowazunguka.
    Vifaa vilivyogawiwa kwa wajasiliamali wote vinathamaniya zaidi ya shilingi milioni 200. PICHA ZA TUKIO HILO BOFYA HAPA

RAIS JAKAYA KIKWETE AMKARIBISHA IKULU RAIS MOHAMED ABDEAZIZ WA SAHARAWI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimuonesha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya  Kiarabu ya Saharawi  Mhe.Mohamed Abdelaziz picha ya waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Hayati Mwalimu Julius Nyerere na  Hayati  Abeid Karume wakibadilishana hati za muungano muda mfupi baada ya Rais Kikwete na mgeni wake kumaliza mazungumzo rasmi  ikulu jijini Dar es Salaam leo.Mhe.Mohamed Abdelaziz  Rais wa Jamhuri ya kiarabu ya Saharawi aliwasili nchini jana jioni kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi Mhe.Mohamed Abdelaziz leo asubuhi.(picha na Freddy Maro)

MIYEYUSHO AMTWANGA MMALAWI KWA 'KO'

Jun 23, 2012

John Masamba kutoka Malawi akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana. PICHA ZAIDI ZA MWANGANO HUU INGIA UKURAA WA SPOTI BONYEZA HAPA

MCHEZA SINEMA WA MAREKANI DEIDRE LORENZ ATINGA KITUO CHA YATIMA CHA UPENDO

Kusoma habari hii nzuri tafadhali TIFUA HAPA

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA ALIYEKUWA MKUU WA UTAWALA MAKAO MAKUU YA CCM

 Mwenyekiti wa CCM,Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Mkuu wa Utawala CCM Makao Makao Makuu mjii Dodoma,  marehemu Mwangunza  Kinyamagoha,  nyumbani kwa marehemu  mjini Dodoma jana. Marehemu amefariki dunia hivi karibuni.
Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Kinyamagoha nyumbani kwake mjini Dodoma jana kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam. (Picha na Freddy Maro)

KUUA KATIKA UGOMVI KWENYE MCHEZO WA POOL KWA MPELEKA JELA MIAKA TISA

TARIME, TANZANIA
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, mjini ya Jaji Amir  Mruma imemuhukumu Mkazi wa Tarime  Chomete John Wambura kwenda jela miaka tisa baada ya kupatikana na hatia ya kuuwa bila kukusudia.
Katika kesi hiyo, Wambura amepatikana na hatia ya kumuua Chacha Ryoba Mkono kwa kumchoma kisu wakati wa ugomvi wakati  wakicheza  mchezo wa Pool.
Akitoa Hukumu hiyo Jumanne Wiki hii Jaji Mruma alidai kuwa amelidhika na Ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo bila Shaka yoyote na Mtuhumiwa kuiomba Mahakama imsamehe kwani kosa lake la Kwanza na walikuwa wakigombea sh 200/= wakati wakicheza Pool ,
Ambapo ilidaiwa na  Mwanasheria wa Serikali Varence Mayega kuwa Mtuhumiwa Chomete alifanya Mauaji hayo  Agost 19/2009  Mchana katika Kijiji cha Genkuru tarafa ya Ingwe alipomchoma Mwenzake Chacha Ryoba Kisu wakati wakigombana na Kusababisha Kifo kwa Ryoba , mbali na Mtuhumiwa  kuiomba Mahakama  imusamehe kwa kuwa amekaa Mahabusu kwa mda mrefu Jaji Mruma alimuhukumu Kwenda Jela Miaka 9 ili iwe Fundisho kwa watu wengine wanaoondoa Roho za Watu bila Sababu za Msingi ,
Katika kesi nyingine katika Mahakama hiyo Kuu ya Jaji Mruma imemuhukumu Marwa Magembe naye kwenda Jela miaka 9 kwa kuuwa bila kukusudia , ambapo Mwanasheria wa Serikali Mayega alidai kuwa Matuhumiwa Magembe alimuuwa Murian Chacha Tugara usiku Agost 19 /2010 katika Kijiji cha Nyantira Tarafa ya Ingwe

MAHAKAMA KUU YATOA AMRI KUSITISHA MGOMO WA MADAKTARI

Jun 22, 2012

Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
·        Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;
·        Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k

·         Wajibu maombi,ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.
Masharti hayo ni
·        Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
·        Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.
Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATIMULIWA KWA ULAFI, WENGINE WABURUZWA MAHAKAMANI

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
DODOMA, TANZANIA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amewavua madaraka wakurugenzi wanane wa Halmashauri  huku wawili kesi zao zikifikisha mahakamani.
   Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Serikali Hawa Ghasia alisema wengine watatu wamepumzishwa kazi na kuongeza kuwa maamuzi ya kufuta kazi wakurugenzi hao yalifanyika katika kipindi cha mwaka 2011/12.
    Alisema kufuatia tuhuma mbalimbali za ubadhilifu wakurugenzi wawili ambao ni Harold Senyagwa ( Kyela) na Rhoda Nsemwa (Bagamoyo) kesi zao zipo mahakamani na kwamba wakati hayo yakijiri Waziri Mkuu ameteuwa wakurugenzi wengine wapya 14 kujaza nafazi zilizokuwa wazi na wengine 22 wamwehamishwa vituo huku 11 wakipewa onyo kali.
   Waziri Ghasia alisema sababu ya kuwavua madaraka  wakurugenzi wanane ni kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao na kwamba wakurugenzi hao kwa sasa wamepewa kazi zingine katika halmashauri hizo .
    Aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni pamoja na Consolata Kamuhambwa (Karagwe), Ephraim Kalimalwendo (Kilosa), Elly Mlaki (Babati), Eustach Temu (Muheza) na Jacob Kayange ( Ngorongoro).
   Wengine ni Hamida Kikwega (Chato), Majuto Mbuguyu ( Jiji la Tanga) ma Raphael  Mbunda (Arusha Manispaa ).
     Waziri Ghasia alisema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kujaza wakurugenzi katika Halmahsuari ambazo hazina watendaji hao.
    Alisema orodha ya wakurugenzi hao imeshapelekwa kwa Rasi Jakaya Kikwete na inatarajiwa hadi Julai Halmashauri nyingi zitakuwa na wakurugezni wake.

RAIS AKAGUA SHAMBA LA MFANO DODOMA

Jun 21, 2012

Jakaya Mrisho Kikwete akikagua  nyanya  na mazo mengine ya mboga pamoja na mizabibu katika shamba linalomilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade huko katika kijiji cha Chikopelo,wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma  leo asubuhi.Kushoto ni mmoja wa wamiliki wa Shamba hilo Bwana Alon Hoven anayeshirikiana na Bwana Dunstan Mrutu(hayupo pichani).shamba hilo linamwagiliwa kwa kutumia teknolojia ya  matone(Drip irrigation system).

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAZINGIRA ENDELEVU JIJINI RIO DE JANEIRO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mkutanano wa Mazingira Endelevu jijini Rio De Janeiro unaofanyika jijini hapa ikiwa ni miaka 20 baada ya mkutano kama huo kufanyika mwaka 1992. Katika mkutano wa mwaka 1992, ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Rais wa wakati huo Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Mkutano wa mwaka huu unajadili kuhusu maazimio ya mwaka 1992 na namna yalivyotekelezwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wapatao 182 huku washiriki katika mkutano huu wakikadiriwa kutoka katika nchi 135. Sambamba na hilo mkutano huu unapitisha maamuzi mapya kuhusu kuiweka dunia na mazingira yake katika hali ya usalama ili yaweze kusaidia vizazi vijavyo. Mkutano huu unafanyika ikiwa ni siku chache tangu kufanyika mkutano wa G-20 uliokuwa ukifanyika nchini Mexico na matokeo ya mkutano huo wa G-20 kwa namna moja ama nyingine yameongeza hamasa ya mkutano huu wa Rio +20. Hamasa kubwa kwa mataifa inabaki juu ya kutazama namna uchumi wa kijani utakavyoweza kusaidia kukuza maendeleo ya maisha ya watu duniani huku maendeleo hayo yakiiacha dunia katika hali ya kawaida katika mazingira yake ya asili. Pia hoja ya kuhusu uzalishaji mkubwa wa gesi joto imepata mjadala mkubwa katika mkutano huu. Maeneo mengine ambayo yanajadiliwa ni kuhusu hali ya chakula duniani huku msukumo ukiwa kutoa uhuru kwa nchi kuzalisha chakula ili kutosheleza wananchi wa kila nchi husika.

Ujumbe wa Tanzania unaotolewa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal unalenga kuonesha namna Tanzania ilivyo na mikakati sadifu katika utunzaji wa mazingira yake sambamba na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kikubwa yanachangiwa na nchi kubwa zenye viwanda. Ujumbe huu pia unaakisi nafasi ya nchi za Afrika katika kulinda mazingira pamoja na mikakati ya baadaye inayozingatia uzalishaji bila kuathiri mazingira kwa kiasi kikubwa. Katika hotuba yake katika mkutano huu, Mheshimiwa Makamu wa Rais anazungumzia umuhimu wa nchi duniani kuzidi kushikamana katika kuhakikisha dunia inabakia kuwa sehemu bora ya kuishi kwa wanadamu wa sasa na wajao. Kufuatia mantiki hii, Mheshimiwa Makamu wa Rais anayakumbusha mataifa yote kuhakikisha yanazingatia maazimio ya mkutano huu wa Rio +20 ili uwe na mafanikio zaidi ya ule wa mwaka 1992.
Waliombatana na Mheshimiwa Makamu wa Rais na ambao wanashiriki mikutano ya kisekta ni pamoja na Mheshimiwa Terezya Huvisa, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Fatma Fereji, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais SMZ pamoja na Mheshimiwa Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kundi la Wabunge linawakilishwa na Mheshimiwa James Lembeli, Salehe Pamba na Magdalena Sakaya. Mkutano huu ulioanza Juni 20, 2012 unatarajiwa kumalizika Juni 22, 2012.

Imetolewa na: Boniphace Makene
        Press Secretary to the Vice President
                  June 21, 2012

BALOZI WA SAN MARINO AMSHUKURU MIGIRO KWA USHIRIKIANO

Pichani: Naibu Katibu Mkuu akiwa pamoja na mwenyeji wake na waalikwa wengine walioshiriki chakula cha mchana kilichoandaliwa na Balozi  Daniel Bodini wa San Marino. kutoka kushoto ni Bw. Parfait Onanga Anyanga, Mkurugenzi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu, Balozi wa Mongolia, Bi. Enkhtsetseg Ochir, Balozi wa Nigeria, Bibi. Joy Ogwu,  Balozi Bodini, Dkt. Asha- Rose Migiro na Bw. Vijay Nambier aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa Ofisi ya Katibu Mkuu  na  ambaye sasa ameteuliwa  kuwa Mwakilishi Maalum  wa Ban Ki Moon huko  Myanmar 

HABARI KAMILI

Balozi wa  Jamhuri ya San Marino katika Umoja wa Mataifa, Bw. Daniele Bodini amemuelezea Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro kama kiongozi ambaye katika  uongozi wake daima aliweka mbele maslahi ya nchi zote bila ya kujali ukubwa au udogo wa nchi.

Balozi Bodini ametao kauli hiyo siku ya jumatano wakati alipomuandalia chakula cha  mchana Dkt. Asha-Rose Migiro kumshukuru kwa mchango wake na ushirikiano aliouonyesha wakati wa uongozi wake.

 Chakula hicho cha mchana kiliandaliwa katika makazi ya  Balozi Bodini na kuwashirikisha pia Balozi wa Nigeria katika Umoja wa Mataifa Bibi Joy Ogwu,  na Balozi wa Mongolia Bi. Enkhtsetseg Ochir. Aidha  Balozi huyo wa San Marino   Akasema yeye binafsi anashukuru kwa kupata nafasi ya kufanyakazi kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu katika maeneo mbalimbali  yakiwamo  utekelezaji  wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia, uanzishwaji wa UN -Women,  masuala ya Ulinzi na Usalama na  System wide Coherence. 

 Vile vile  akasema  Migiro amekuwa mfano wa kuigwa  na wanawake, wasichana na watoto wa kike ambao wanamchukulia yeye kama kielelezo cha mafanikio ya wanawake  na kwamba ameatia moyo wengi. Akabainisha kwamba yako mambo mengi ambayo Migiro ameyafanya wakati wa uongozi wake na kwamba hapana shaka yataendelea kukumbukwa katika Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu akamshukuru kwa heshima hiyo na  kwa ushirikiano aliompatia  katika, pamoja na mambo mengine  kutekeleza majukumu aliyokuwa amekabidhiwa ya kumsaidia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Akasema daima ataienzi heshima hiyo na kuwashukuru wale wote ambao wameshirikiana  naye kwa karibu katika  utekelezaji wa masuala mengi na muhimu kwa maendeleo ya mwanadamu.

SBL YAZINDUA MRADI WA UVUNAJI MAJI YA MVUA IRINGA

 Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akizindua rasmi mradi wa uvunaji maji ya mvua uliopo Hospitali ya Wilaya ya Iringa iliyopo Frelimo mjini hapa jana. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na kugharimu zaidi ya Shilingi Milioni 50 na unataraji kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo zaidi ya 100,000. Wengine kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu, V Mushi.
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akimshukuru Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda kwa kampuni yake kufadhili mradi huo muhimu wa maji Hospitalini hapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akifungua maji kutoka katika tanki moja wapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akimtwisha ndoo ya Maji Augusta Mtemi ambaye ni Diwani wa Viti Maalum Iringa ikiwa ni ishara ya uzinduzi huo.
 Tanki litakalo tumika kusambaza maji katika mradi huo.

Hii ndio Hopspitali ya Frelimo iliyopo Manipaa ya Iringa ambayo itafaidika na mradi huo.

MCHEZASINEMA MAARUFU WA MAREKANI ATUA NCHINI


Mcheza sinema toka Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zinazofanyika Jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka. Pichani, Deidre Lorenz na Rais wa IBF-USBA bala la Africa, Masharini ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi. 
Kwa Habari zaidi BOFYA HAPA


MISS DAR INTERCOLLEGE YAIVA; KUFANYIKA KESHO DAR

Kamati ya Miss Tanzania, ikiwafunda washiriki wa shindano hilo, jana
KAMATI ya Miss TAnzania jana imetembelea kambi ya Miss Dar Intercollege iliyopo kwenye hoteli ya The Grand Villa, Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwafunda.
       Shindano hilo linatarajiwa kufanyika kesho, Ijumaa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na chuo cha Usmiamizi wa Fedha (IFM).
       Akizungumza na warembo hao, mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye aliwataka warembo hao kufuata miongozi na kanuni za shindano hilo ikiwemo kuwa na nidhamu.
       Alisema urembo si sura na umbo zuri bali unahusisha pia nidhamu katika jamii hivyo amewataka warembo hao kuzingatia hayo.
     "Nafahamu ninyi ni wasomi wazuri hivyo mmeyapokea vema mafunzo tuliyowapa...hatutarajii kusikia mmoja wenu anachafua hali ya hewa katika siku za usoni na mambo ya skendo skendo,"Alisema Makoye.
      Dina alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa uziki wa kizazi kipya nchini Nasib Addul ‘Diamond’ sambamba na bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
      “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
      Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
     Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan

KUTOKA IRINGA MJINI

 Mji wa Iringa ukiwa eneo la Posta
 Mama akiwa amebeba mzigo wa kuni alizoshuka nazo kwenye basi mjini Iringa. Kuni za kupikia Mamalishe
 Kondakta akiwa amemkalia binti kwenye daladala akati likitoka eneo la Ilula kwenda katikati ya mji
 Kituo Kikuu cha mabasi mjini Iringa kipo bizee
Blogger mkazi wa mjini Iringa, Francis Godwin akinunua gazeti

PAMBANO LA NGUMI LA MIYEYUSHO LAYEYUKA

Jun 20, 2012

Pambano la masumbwi kati ya bondia Francis Miyeyusho na  mmalawi John Massamba lililokuwa lifanyike ijumaa. limeahirishwa mpaka hapo tarehe itakapotajwa tena kuwa Miyayusho atacheza na nani, lini na wapi.Habari zaidi BOFYA HAPA
ยช