.

MIJIZI YAKOMBA HADI BASTOLA KATIKA OFISI YA DK. CHEGENI, MWANZA

Jul 31, 2012

Dk. Cheni

Habari tulizopata kutoka jijini Mwanza zinasema, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega wilayani Magu, Dk. Raphael Chegeni, ameibiwa bastola yake usiku wa kuamkia leo.
   Kwa mujibu wa habari kutoka jijini Mwanza, bastola ya Chegeni imeibwa baada ya majizi kuvunja ofisi yake na kwamba mbali na bastola majizi hayo yameondoka na kasha maalum la kuhifadhiwa fedha na laptop. 
  "Vitu vingine vinavyodaiwa kuibwa katika ofisi hiyo binafsi ya Chegeni iliyopo katika jengo la Benki ya Exim, barabara ya Kenyatta jijini Mwanza, ni pamoja na sefu ya fedha", kimesema chanzo chetu cha habari. 
   Ikithibitisha tukio hilo, polisi mkoani Mwanza, imesema wezi wamekomba sh. Milioni 5 za madafu na Dola 13 za Kimarekani zilizokuwa kwenye sefu hiyo.

USHIRIKI WA KUTOA MAONI KATIBA MPYA

Bw. Khamis Said Abdalla (47), mkazi wa Shehia ya Madungu, Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, ambae ni mlemavu, akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika Shehia hiyo hivi karibuni. (Picha na Othman Maulid)

DK ASHA ROSE MIGIRO AKUTAKA NA JAJI WARIOBA

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba wakati Dkt. Migiro alipotembelea ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Julai 31, 2012). (Picha na Ismail Ngayonga).

AJALI YA KUZAMA MELI ZANZIBAR: GRANDMALT NA ZIF WATOA POLE

Meneja masoko wa Kinywaji cha Grandmalt Fimbo Buttalah Kulia akimkabidhi makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy Fedha Shilingi milioni tano kama sehemu ya Rambirambi zilizotolewa kwa pamoja kati ya Grandmalt ambao ni wadhamini wa Ligi kuu ya Zanzibar na Chama cha Soko Zanzibar ZFA. Kushoto ni Makau wa rais wa Zfa Kassum Suleman. 
FULL STORY  INGIA TANZANIA VISION BLOG

MSHINDI WA TANZANIA DRIVER OF THE YEAR 2011 KUSHIRIKI BINGWA WA MABINGWA MASHINDANO YA DUNIA YA UDEREVA

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Kampuni ya Scania leo imeandaahaflafupikumuagamshindiwamashindanoyamaderevayanayojulikanakama“Tanzania Driver Of The Year” yaliyofanyikakatikaviwanjavya Biafra sikuyaJumamositarehe 19th November mwakajana.
     Mr. Erasmus Mtui, mwenyeumriwamiaka 44 iliyebukamshindibaadayakufaulukatikangazizotetatuzashindanohilomwakajanaameajiriwakamaderevakatikakampuniyausafirishajiya Super Star Forwarders iliyokobarabarayaNyerere, Dar Es Salaam. “Nimefanyamazoezinanimepatamafunzoyakutoshakabisa, kwasasanikotayarikukabiliananashindanolijalo, naahidikufanyajitihadazanguzoteiliniiwakilishevizurinchiyangu, benderaya Tanzania ipeperukevizurikwenyemashindanohaya!” AlijigambaBw. Mtui.

Akiongeanawaandishiwahabari, Bwana Mark Cameron MenejaUendeshajiwakampuniyaScania Tanzania alisemakwamba‘Derevandiokiungomuhimupekeekatikauchumi, mazingiranausalama. Maderevawenyeutaalamunawanaopendakaziyaohusaidiakuendeshakwausalamabarabarani, hutumiamafutakidogo, hiihusaidiakiwangokidogo cha uchafuziwamazingira”.AlisemakwambaScaniailianzishamashindanoyamaderevakwamaraya kwanza mwaka 2003 katikanchizaulaya. Mashindanohayayalieneanakuwayadunianzima, yakionyeshaumuhimuwautaalamukwamaderevapamojanakusisitizamafunzokwamaderevailikuboreshaufahamuwausalamabarabaraninauchafuziwamazingiraunaosababishwanamoshiwamagari. Mr. Cameron alimalizakwakusema “Maderevandioutiwamgongowasektayausafirishaji. Pamojanakutengenezamagarimakubwa bora, salamanayanayotumiamafutavizuriScaniamudawoteinamuangaliamtualiyekonyumayausukani. Kwamaraya kwanza tumewezakufanikishamashindanohayahapa Tanzania, tukonamshindiwetuMr.Mtuiambayeamejiandaavizuri, tunamuamininatunatarajiaatatusababishiasifakubwa, tunamtakiakila la kheri!.Naye Bi. Margaret Legga, afisamasokomsaidiziwakampuniyaScania Tanzania alisemakwambamashindanohayayaliyopewajina la “BingwawaMabingwa”yatafanyikakatikamjiwa Sun City hukoAfrikayaKusinimapemamweziujaokuanziatarehe 09 hadi 11. Mashindanohayayatajumuishamaderevakutokamabaramenginekamabara la Ulaya, Asia naAmerikayaKusini, kutokanchizaAfrikakunamaderevakutokanchiza Botswana, Lesotho, Malawi, Namibia nasisi Tanzania. WaandaajiwamashindanohayanikampuniyaSwiss organisation UICR Union Internationale Des ChaffeursRoutiersna The South African RTMC Road Traffic Management Corporation, Scanianimojawapoyawadhaminiwakuuwashindanohili. Shindanohilihufanywamarambilikilamwaka.Mwakahuujumlayamadereva 105 kutokanchi 17 kotedunianiwatachuanakatikangazitofauti 6 zashindano.Mr.Mtuiatashindanakatikakitengo cha “Semi truck and trailor” ambachoatapambanakikwelikwelikwanikiladerevaatatakiwakuonyeshaufundikwakuendeshanakupitavipimo 19 vyamchuano. Vipimohivinipamojanauendeshajiunaotumiamafutakidogo, namnayakubebamzigokiusalama, kulifahamugarianaloendesha, bilakusahauuendeshajimakinibarabarani. KufanyikakwashindanohilihapabaranikwetuAfrikakunatuongezeauwezekanowakufaulusisiwenyeji” Alimaliza Bi.Legga. 
Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Scania nchini Tanzania, Mark Cameron(kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa dereva, ErasmusMtui ambaye ni mshindi wa mwaka 2011nchini Tanzani anayekwenda kwenye mashindano ya Dunia ya Bingwa wa Mabingwa yanayotarajiwa kufanyika  Afrika Kusini.Makabidhiano hayo yalifanyika makao makuu ya ofisi za Scania Dar es Salaam.

CCM YAMSHUKIA TUNDU LISSU

*Yadai orodha ya Lisu inalenga kupotosha  tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge *Anataka kuwaokoa wa Chadema katika sakata hilo.
*Yasema tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe suala la kisiasa
Nape akizungumza na waandishi wa habari leo
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinalaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wana siasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.
    Akizungumza na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.
    "Mfano mzuri wa juhudi hizi ni kitendo cha Tundu Lissu, ambaye ni  mbunge wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kkambi ya upinzani Bungeni cha kutoa aliyoiita orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara na TANESCO na kwamba ndio watuhumiwa wa rushwa inayozungumziwa", Alisema Nape na kuongeza;
   "Cha kushangaza orodha yake ilikuwa na wabunge wa CCM peke yake wakati wote tunajua kuwa yapo majina ya baadhi ya wabunge wa vyama vingine hasa Chadema, yanayotajwa katika orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hii".
    Nape alisema juhudi hizo za Lissu na wenzake zinalengo la kuuficha ukweli na kujaribu kuwalinda watuhumiwa wa uhalifu wanaotokana na Chadema.
   "Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.
    Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.
    "Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.
     Nape alisema  CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri na umahiri wao mkubwa waliouonyesha kwa muda mfupi waliokaa kwenye wizara hiyo.
     "Tunaamini uzalendo walioonyesha katika kusimamia wizara hii,utaigwa na watumishi wengine wa umma katika kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali za nchi zinalindwa ili kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanatimia. Tunaunga mkono jitihada zao", alisema Nape.
     Alisema, pia CCM inalipongeza bunge kwa kuendelea kusimamia serikali na rasilimali za nchi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa ya maendeleo.
    "Tunawaomba waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.
                   HABARI HII INAPATIKANA PIA TANZANIA VISION BLOG

NAPE,SHIGELLA WANA PRESS FONFERENCE LEO

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye atakafanya mkutano saa 5 ASUBUHI,  katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, Wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Martine Shigella tafanya saa 4 asubuhi, makao makuu ya UVCCM, Dar es Salaam. Taarifa zilizopo ni kwamba viongozi hawa watazungumzia mambo tofauti.

RAIS AOMBOLEZA KIFO CHA MBUNGE WA ZAMANI WA KILOSA

Jul 29, 2012

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Joel Nkaya  Bendera kuomboleza kifo cha Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilosa, Alhaj Shaweji Abdallah, ambaye pia alipata kuwa mjumbe wa miaka mingi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi.
Katika salamu zake kufuatia hicho
INAENDELEA

POLISI WASTAAFU WAUNDA CHAMA, WAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI

NA FRANK GEOFREY, JESHI LA POLISI
Chama cha Askari Wastaafu wa Jeshi la Polisi (TAPOA) kimefanya Uchaguzi wake wa Viongozi katika nyadhifa mbalimbali ambao watakiongoza kufikia malengo yake ambayo nikuwaletea maendeleo wanachama wake.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo na nyazifa zao kwenye mabano ni pamoja na Hilary Rashid (Mwenyekiti), Mustapha Wangwi(Mwenyekiti Msaidizi),Chai Msugar (Katibu),Fadhili Walele (Katibu Msaidizi), SSP Mstaafu Galimanywa (Mweka Hazina), Moses Lyimo (Mwanasheria wa Chama), Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Na Wadhamini wa TAPOA.


Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TAPOA Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Bw.Hilary Rashid ametoa wito kwa Askari wastaafu wote wa Jeshi la Polisi kujiunga katika Chama hicho kwakuwa kitawasaidia katika kupata maendeleo na kudai stahiki zao.

Amesema hivi sasa ni wakati muafaka kwa wastaafu kujitokeza kwa wingi na kulisaidia Jeshi la Polisi katika kuimarisha dhana ya ulinzi shirikishi na Polisi Jamii ili kupunguza uhalifu hapa nchini.


Kwa upande wake Katibu wa TAPOA Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Polisi , Bw.Chai Msugar alisema umoja huo utawawezesha kukutana mara kwa mara nakubadilishana mawazo bila kusahau kushirikiana katika shughuli mbalimbali kwa hali na mali.

Aidha Bw Msugar alisema lengo la Chama hicho nikuhakikisha kinamfikia kila Mstaafu popote pale alipo ili kuweza kupata wanachama wengi ambao watakiimarisha kwakushirikiana na uongozi wa Jeshi la Polisi.

Naye Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Naibu Kamishna Mstaafu Abbas Mwamasoli alisema changamoto wanayokabilina nayo ni kuhakikisha wanafika kila mkoa na kufungua matawi ili iwe rahisi kuwafikia wanachama wote walioostaafu wakiwa na  vyeo mbalimbali bila ubaguzi wowote.

AIRTEL YAZINDUA MNARA WA MAWASILIANO ENEO LA MISUNGWI, MWANZA

 Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh Charles Kitwanga akikata utepe kuashira uzinduzi wa Mnara wa mawasiliano uliojengwa na Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ili kurahisisha
upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, wakwanza kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.
 Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh charles Kitwanga akikata utepe kuashira uzinduzi wa mawasiliano uliojengwa na Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, wakwanza kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.
Katikati ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh charles Kitwanga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Nyamayinza (kulia) na wakati kushoto ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania
kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi mnara wa mawasiliano wa  Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamayinza, Buhunda, Ishoke na Seke, . hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki
Katikati alivaa shati la bluu ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa RaisMMh charles Kitwanga meneja mauzo kanda ya ziwa Galus Mgawe na meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakishangilia na wananchi mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi wa mawasiliano wa  Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, . hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.
HABARI KAMILI HAMIA TANZANIA VISION BLOG

VODACOM FOUNDATION YAFANYA MAMBO

HABARI KATIKA PICHA
 BOFYA TANZANIA VISION BLOG

JK ATETA NA KIKONGWE

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bibi Antonia Mbagalla (85) katika kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki leo(Jumapili).(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bibi Antonia Mbagalla (85) katika kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki leo(Jumapili).(picha na Freddy Maro).

YANGA BINGWA TENA KOMBE LA KAGAME

Jul 28, 2012

 Yanga imefanikiwa kulitwaa tena Kombe la Kagame mwaka huu wa 2012,  na hivyo kuutetea ubingwa wa kombe hilo iliokuwa inaushikilia. Imefanikiwa kuutwaa ubingwa leo baada ya kuifunga Azama FC, katika mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Taifa, jijini  Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na Hamis Kiiza katika kipindi cha kwanza  na Saidi Bahanuzi kipindi cha pili.

MKATABA WA KUDHIBITI BIASHARA YA SILAHA DUNIANI WAKWAMA

Ujumbe wa Tanzania  ambazo kwa mwezi mzima umeshiriki kikamilifu  hadi usiku wa manane pale ilipobidi na kuhakikisha kwamba maslahi ya Tanzania katika  majadiliano ya kidiplomasia ya nchi wanachama kuhusu  Mkataba wa Kisheria wa Kudhibiti Bishaara ya  Silaha duniani yalikuwa yamezingatiwa. Hata hivyo mkutano huo ulioanza Julai Mbili na kumalizika Julai 27 umeshindwa kutoa Mkataba kutokana na  wajumbe kutokukubaliana kuhusu baadhi ya vipengere ambavyo wengine walikuwa wanataka viwe sehemu ya mkataba, huku  wengine wakikataa kata kata. Mkataba huo kama ungepatikana  ulitarajiwa kwamba ungeleta matumaini na unafuu kwa  mamilioni ya watu ambao maisha yao kila siku yamo hatarini kutokana na  matumizi mabaya ya silaha.  Inaelezwa kwamba biashara ya silaha duniani inashika nafasi ya pili baada ya biashara ya madawa ya binadamu. Kutoka kushoto  mstari wa mbele ni Bw. Theobald Kazora kutoka Ofisi ya Rais, Brigedia  Jenerali Dkt. Charles  Muzanila kutoka JWTZ ambaye pia alikuwa kiongozi wa ujumbe, Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere ambaye pia alikuwa kiongozi wa ujumbe akisaidia na  Brigedia Jenerali Muzanila na  Bw. John Kinuno ambaye ni wakili kutoka Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kutoka kulia mstari wa nyuma ni Bw. Peter Macomara kutoka  Taasisi ya Kiraia, Brigedia Jenerali Venance Mabeyo kutoka  JWTZ na Kamishna Esaka Mugasa kutoka Jeshi la Polisi na Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Meja Wilbert Ibuge ambaye hayupo pichani. 
HABARI ZAIDI BOFYA TANZANIA VISION BLOG

YANGA KUFANYWA KAMA SIMBA AU KUTETEA UBINGWA LEO?

Tafadhali toa Maoni yako bure hapa!

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU MGOMO WA WALIMU

Jul 27, 2012


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUSUDIO LA WALIMU KUGOMA
____________________________________________
SERIKALI kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi leo, Ijumaa, Julai 27, 2012 majira ya saa tisa alasiri, imepokea notisi ya saa arobaini na nane (48) ya kusudio la walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kugoma kuanzia Jumatatu tarehe 30 Julai 2012 saa moja na nusu asubuhi.
Kabla ya notisi hii kutolewa, Serikali imekuwa ikifanya jitihada nyingi za kujadiliana na viongozi wa CWT kuhusu jinsi ya kuboresha maslahi ya walimu kwa nia ya kumaliza suala hili kwa maelewano kwa kutumia vyombo na ngazi mbali mbali za kisheria.
Kwa sasa, shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na leo hii siku ya Ijumaa tarehe 27 Julai, 2012 majira ya saa sita mchana pande zote mbili zilifika Mahakamani, na Mahakama ikaamuru kwamba pande zote zikamilishe maelezo yao ifikapo siku ya Jumanne tarehe 31 Julai, 2012 saa sita mchana, ili kuiwezesha Mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kutoa uamuzi.
Kwa hiyo, Mgomo huu siyo halali kwa sababu shauri hili bado liko Mahakamani.
Kwa msingi huo hatua ya CWT kutoa notisi ya kuanza kwa mgomo kabla ya kukamilika kwa shauri hili ni kukiuka taratibu halali za Kimahakama ambazo kila mmoja anawajibika kuziheshimu.
Serikali inapenda kuwafahamisha walimu wote kuwa kujihusisha na mgomo huu ni kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi. Hivyo, walimu wanapaswa kupima madhara ya mgomo huu usiokuwa halali na Serikali inawataka walimu kupuuza mgomo huo na kutokujihusisha nao. Walimu wote wanatakiwa waendelee na kazi kama kawaida.

Peniel M. Lyimo
KAIMU KATIBU MKUU KIONGOZI

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
27 Julai, 2012

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINMGI UJENZI HANGA LA PRECISION AIR DAR

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi  hanga la Precision Air lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Precision Air Bwana Michael Shirima.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi hanga la Precisionair katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere leo asubuhi.Kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Precision air Bwana Michael Shirima.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya ndege za shirika la ndege la Precision ikifanyiwa matengenezo katika hanga jipya la shirika hilo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hanga la shirika hilo la ndege lililojengwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu  Julius Nyerere(picha na Freddy Maro) HABARI KUTOKA TANZANIA VISION BLOG

MEYA ANG'OLEWA MWANZA

Meya Halmashauri ya jiji la Mwanza, Japheth Manyerere, ameng’olewa kwa madai ya madiwani wa Halmashauri hiyo, kutokuwa na imani naye. Inaendelea TANZANIA VISION BLOG

JOHN KOMBA AREJEA NYUMBANI BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI INDIAj


Kampteni Komba akiwa na mkewe, Salome Komba
 nyumbani kwake Kawe leo
Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni mstaafu, John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa upasuaji kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu wake wa kulia.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo, Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi, Kawe,  Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini,  Juzi,  baada ya kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad nchini India tangu mwanzoni mwa wezi huu.

Alisema, aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu wa Bunge John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu hapa nchini kwa sababu ya mgomo wa madaktari.

"Siku napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya kwanza ya mgomo wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge na kisha nikamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa mamlaka yake akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda kutibiwa nje", alisema Komba.

Alisema, uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande wa mguu wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo 138 wakati wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa mwili wake ni kilo 90 au 100 tu.

"Amesema, baada ya matibabu amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 128 ambao hata hivyo ametakiwa kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi ambazo atalazimika kupumzika nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi Septemba mwaka huu kama alivyoelekezwa na madaktari.

Akizungumzia upasuaji ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa tano na kukamilika bila matatizo katika upasuaji huo ambao alisema sehemu iliyopasuliwa ni ya ukumbwa wa futi moja.

Alisema, hata hivyo baada ya upasuaji huo, hakuweza kurejea katika wodi ya kawaida, kwa sababu majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali, presha, hivyo akalazimika kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) kwa siku tano.

"Sasa nimerejea nikiwa mzima, kwa sasa natumia fimbo hii, ili kuwezesha uzito uzilemee upande wa kulia nilikopanyiwa upasuaji, lakini sijambo kabisa", alisema Komba.

Komba alilaani baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwamba katika kuugua kwake alikuwa mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.

"Jamani ninyi waandishi wa habari, jizoesheni kuandika habari zilizokamilika siyo kurashia-rashia tu na kuzusha uongo, mfano gazeti moja liliandika eti naugua figo nipo mahututi, wakati si kweli kabisa, ilikuwa jambo rahisi tu, kuja hapa nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke wangu lingepata kwa uhakika ninachoumwa", alisema Komba. HABARI HII INAPATIKANA PIA KATIKA BLOGU YETU YA TANZANIA VISION BLOG

FAINALI KAGAME CUP NI YANGA NA AZAM

Jul 26, 2012

Mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga ya Dar es Salaam, wametinga fainali baada ya kuibugiza APR ya Rwanda bao 1-0, kwa timu hizo kumenyana kwa dakika 120,  baada ya muda wa kawaida wa dakika 90 kumalizika zikiwa nguvu sawa ya bila kufungana. Kufuatia ushindi huo, sasa Yanaga inaingia katika fainali ya timu yenzake ya Tanzania, Azam FC ambayo imetinga pia fainali leo baada ya kuifunga As Vita 2-1

MELI TATU ZAFUTIWA USAJILI ZANZIBAR KWA KUWA HATARISHI

KWA HABARI HII TAFADHALI

ASKOFU MKUU RUGAMBWA AMTEMBELE RAIS KIKWETE IKULU

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Askofu Mkuu Protase Rugambwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedict wa XVI kuwa Katibu Mwambata wa Idara au Kongregasio ya Uenezaji wa Injili kwa ajili ya Mataifa na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari yenye makao yake, Roma. Wakati wa mazungumzo hayo Rais Kikwete kwa mara nyingine tena,amempongeza Askofu Rugambwa kwa uteuzi wake na kusema kuwa uteuzi huo ni kielelezo dhahiri cha imani kubwa aliyonayo Baba Mtakatifu kwa askofu huyo na kuwa ni heshima kubwa kwa Mtanzania kupata nafasi ya kushika wadhifa huo mkubwa. Kabla ya Uteuzi huo Askofu mkuu Rugambwa alikuwa askofu wa jimbo Katoliki Kigoma. Pichani, Rais Kikwete akiagana na Askofu Mkuu Rugambwa bada ya mazungumzo yao.(Picha na Freddy Maro) PICHA HII IPO PIATANZANIA VISION BLOG

AZAM YATINGA FAINALI

AZAM IMETINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA AS VITA MABAO 2-1. 
HABARI NA PICHA BOFYA

AJALI ZAUA WATATU DODOMA

NA LUPPY KUNG'ALO WA POLISI DODOMA
Watu watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti ya ajali za barabarani na wengine kujeruhiwa katika Mkoa wa Dodoma.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bw. Edmund Urio alisema tukio la kwanza lilihusisha mpanda pikipiki ambaye aligonga mkokoteni, jana, saa 6 usiku, katika Barabara Kuu ya Dodoma-Morogoro eneo la Kibaigwa Wilayani Kongwa

Akizungumzia tukio hili Bw. Edmund Urio alisema kwamba pikipiki yenye namba T202 BDH aina ya FERICON iliyokuwa ikiendeshwa na Joseph Hekela (27) Mkazi wa Kibaigwa iligonga mkokoteni kwa nyuma uliokuwa ukiendeshwa katikati ya babara na kusababisha kifo kwa mpanda pikipiki huyo.

Kamanda Edmund Urio alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mwendesha pikipiki kwa kutofuata sheria kwani hakupaswa kuwa katika mwendo wa kasi, na kwa mujibu taratibu taa zake zinapaswa kumulika umbali wa mita mia tatu hivyo alipaswa kuuona mkokoteni huo uliokuwa mbele yake.

“Muendesha mkokoteni naye ana makosa kwani muda wa chombo hicho kutumia barabara mwisho wake ni saa kumi na mbili jioni, sasa mpaka muda huo wa saa sita usiku kuwepo barabarani ni makosa” Alifafanua Kamanda Urio

Bw. Edmund Urio alisema Muendesha Mkokoteni huo  amekimbia na anatafutwa kwa kosa la kuendesha mkokoteni kwa muda usioruhusiwa na pindi atakapo kamatwa atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinavyotaka.

Katika ajali nyingine iliyohusisha mpanda pikipiki kuwagonga watembea kwa miguu na kusababisha kifo na majeruhi, Kamanda Edmund Urio, alisema ilitokea mnamo tarehe 25/07/2012 majira ya saa moja na dakika saba jioni (19:07hrs) katika eneo la Ipagara Kata ya Ipagara na Wilaya ya Dodoma kwenye Barabara kuu ya Dodoma/Morogoro.

Akizungumzia ajali hiyo alisema Pikipiki No. T. 662 BKC aina ya LIFAN iliyokuwa ikiendeshwa na mtu asiyefahamika  jina  iliwagonga watembea kwa miguu wawili na kusababisha kifo cha mmoja wao aliyejulikana kwa jina la Theresia Chansi mwenye umri wa miaka (37) mgogo na mkazi wa Ipagara amabaye alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

 “Katika Ajali hiyo kulikuwa na majeruhi wawili ambao ni Mpanda Piki Piki mwenyewe ambaye amepoteza fahamu na amelazwa wodi namba (1) pamoja na Magreth Daniel mwenye umri wa miaka (40) na mkazi wa Ilazo mjini Dodoma ambaye naye amelazwa katika hospitali hiyo ya mkoa wodi namba (10).” alieleza Bw. Edmund Urio.

Kaimu Kamanda huyo wa Mkoa wa Dodoma alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi aliokuwa akiendesha mpanda Pikipikki huyo, uliosababisha kushindwa kudhibiti Piki piki yake wakati wakinamama hao walipokuwa wakivuka barabara.

Aidha katika tukio la tatu Kamishna Msaidizi huyo wa Jeshi la Polisi Bw. Edmund Urio alisema gari No. T 668 AYQ aina ya FUSO lilokuwa likiendeshwa na Bw. Philipo Wami mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa Msanga liliacha njia na kupinduka kisha kusababisha kifo kwa mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Henry Wami mwenye umri wa miaka (19) na mkazi wa Msanga.

Alisema ajli hiyo lilitokea tarehe 25/07/2012 majira ya saa moja kamilia asubuhi (07:00 hrs) katika maeneo ya Kijiji cha Msanga Wilaya ya Chamwino.

Kamanda Edmund Urio alisema Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa usukani, uliosababisha gari hiyo kupoteza muelekeo na kupinduka.

Hata hivyo Kamanda Edmund Urio amewaasa watumiaji wote wa barabara kuwa makini na matumizi sahihi ya bararabara ikiwa pamoja na kufuata na kuheshimu sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

CONTACT:
POLISI MKOA WA DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
Phone:  0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)
Phone:  0712  360203, Silyvester Onesmo – Police  Konstebo  (PC0)

AZAM INAONGOZA KWA 2-1 DHIDI YA VITA YA DRC

Hadi nusu mechi ya Azam FC na Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inamalizika muda si mrefu, Azam inaongoza kwa mabao 2-1

DAU LAZAMA NA KUUA ZANZIBAR

SALMA SALIM HASSAN, ZANZIBAR
Dau lililokuwa limebaba abiria na mizigo limepinduka na kuzama katika pwani ya bahari ya Hindi, eneo la Mkoani Kisiwani Pemba.
     Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Hassan Nassir alisema Dau hilo limezama majira ya saa 11 alfajiri ya leo, ikitokea bandari bubu eneo la Mkoani kuelekea Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
     Katika tukio hilo mtoto mwenye umri wa miaka mitano amefariki dunia ambaye alikuwa pamoja na mama yake Sharifa Mohammed ambaye ameokolewa akiwa na mtoto wake mwengine mwenye umri wa miaka miwili.
     Watu wengine waliokuwamo kwenye  dau hilo hali zao sio nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Abdallah  Mzee Wilaya ya Mkoani Mkoa Kusini Pemba kwa matibabu.
    Waliolazwa ni pamoja na Salum Suluhu, Juma Siasa Abdallah, Ali Denge na Abdallah Omar Kombo ambaye hali yake ni mbaya. Majeruhi wengine walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
     Kamanda huyo wa Polisi alisema wanamshikilia Nahodha wa Dau hilo Omar Juma Ali(29) mkazi wa Kangani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini  Pemba na anatarajwia kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.
    Wakati tukio hilo likitokea, bado wananchi wamo katika maafa ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyokuwa ikitokea bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar . Watu 94 wamepoteza maisha na 146 waliokolewa wakiwa hai.
      Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 karibu na Kisiwa cha Chumbe umbali wa maili sita kuelekea Kusini mwa Kisiwa kidogo cha Yasin Zanzibar ikitokea Bandari ya Dar es Salaam ilikoanza safari saa 5:30 asubuhi.
      Meli hiyo inamilikiwa na Kampuni ya Sea Guall Sea Transport Ltd, Kampuni ambayo Meli yake nyengine ya Mv. Fatih ilizama ikiwa Bandarini Malindi Zanzibar na kufariki watu sita mwaka 2009. Habari hii inapatikana pia katika TANZANIA VISION BLOG

BANC ABC YATAHAMINI MICHUANO

Mkurugenzi wa masoko na matukio wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jimmy Kabwe akisaini mkataba wa makubaliano ya udhamini wa michuano ya Banc ABC SUP8R Soccer Tournament 2012 inayodhaminiwa na banc ABC kulia kwake ni katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Boni Nyoni na Mkuu wa Idara ya fedha ya benki hiyo, Mwalimu Zubery. Haflya hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam makao makuu ya TFF ambapo michuano hiyo itaanza Agosti 4-18. Picha na DINA ISMAIL BLOG

KATA YA KWADELO, KONDOA WATEKELEZA KILIMO KWANZA KWA KASI

 Diwani wa Kata ya Kwadelo,Kondoa mkoa wa Dodoma,  Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto) akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani (kushoto), Gabriel Galahenga, baada ya kuwakabidhi wakulima hao matrekta maane, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja  ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa  zilizobaki katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo.
 Diwani Kariati akikabidhi funguo ya trekta kwa mmoja wa wakulima  wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani. Wengine ni wakulima wa Kata hiyo, Alifa Hulufya (kulia), Chundu Damiani (wapili kushoto) na Gabriel Halahenga (watatu kushoto) na kati yao ni Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan.
 Diwani Kariati akikabidhiwa barua na mkulima wa Kwadelo,  Gabriel Halahenga, wakati wa hafla ya diwani huyo kukabidhi matrekta maane kwa wakulima wa kijiji hicho leo, Ofisi za Suma KJT, Mwenge, Dar es Salaam.  Wengine ni,  Alifa Hulufya (kulia), Chundu Damiani (wapili kushoto) na Gabriel Halahenga (watatu kushoto) na kati yao ni Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan. Barua hiyo ni kwa ajili ya Dhukurani kwa Mkuu wa JKT kutokana na Suma JKT kukubali kuwapa matrekta wakulima wa Kwadelo, kwa malipo ya nusu ya gharama na kumalizia deni katika kipindi cha miaka minne baadaye.
 Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan akifurahia jambo na Diwani Kariati wakati wa makabidhiano ya trekta hizo.
 Diwani Kariati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi trekta nne kwa wakulima wa kata yake leo. Habari hii inapatikana pia kwenye Blogu yetu ya Tanzania Vision Blog..BONYEZA HAPA UONE

MAANDALIZI YAIVA MKUTANO WA CCM KIGOMA JUMAPILI HII

Jul 21, 2012

 Bendera za CCM ziliwa zimepambwa jioni hii kwenye Uwanja wa Community Cetre, Mwanga mkoani Kigoma tayari kwa mkutano wa hadhara wa CCM utakaofanyika kwenye Uwanja huo Jumapili hii
Vijana wakiwa katika maandalizi ya Jukwaa kuu kwa ajili ya mkutano huo ambao umepangwa kuhutubiwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri KWA HABARI KAMILI:-BOFYA HAPA

UN YAOMBOLEZA MAAFA YA KUZAMA MELI ZANZIBAR

 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akisaini kitabu cha Maombolezo ambacho kimefunguliwa katika Ubalozi  wa  Kudumu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania katika Umoja wa  Mataifa.  Katika Salamu zake, Naibu Katibu Mkuu ameelezea kuguswa kwake na tukio la ajali  ya kuzama kwa meli  na  hasara iliyotokana na ajari hiyo ikihusisha pia kupotea kwa maisha ya watu. Mhe. Jan Eliasson ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika kutoa salamu zao za pole na kuungana na watanzania katika kipindi hiki cha majonzi.
Naibu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akizungumza na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu cha  maombolezo ambapo   alielezea  namna gani anavyoifahamu Tanzani na mapenzi yake makubwa kwa nchi hiyo  na kwamba ni kama miaka miwili tu iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar.   Katika salamu zake za pole  Mhe.  Elliasson amesema sala na dua zake anazielekeza kwa wahanga wa tukio hilo,  Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja na watanzania katika  kipindi hiki kigumu.

KAMERA YE2 KIGOMA

Jul 20, 2012

 Stesheni Kuu ya Usafiri wa treni kwa njia ya reli kutoka mkoani Kigoma
 Moja ya majengo ya kisasa yanayobadili taswira ya mkoa wa Kigoma kimaendeleo. Jengo hili ni la Shirika la Nyumba Tanzania, mjini Kigoma, barabar Kuu ya kwenda nje ya mji huo kutoka eneo la Stesheni Kuu ya  reli
 Usafiri wa reli bado ndiyo usafiri unaotegemewa sana kutoka mkoani Kigoma kwenda mikoa mingine na baadhi ya maeneo ya pembezoni mwa mkoa. Pichani, abiria waliokuwa wakitaka kusafiri kwa treni jana kutoka stesheni kuu ya reli mkoani humo wakiwa katika foleni ya kukata tiketi
 Baadhi ya abiria wanaotoka vijijini hulazimika kulala stesheni kama hawa,
 Trafiki ni Tanzania nzima! askari wa kikosi hicho akimhoji jambo mwendesha pikipiki mjini Kigoma leo
 Ujasiriamali muhimu: Kina mama wakiwa katika biashara ndogo ndogo mjini Kigoma
 Kina Baba na Kina mama wakiwa katika biashara ya dagaa mjini Kigoma.
Wachuuzi wa vitunguu na mazao mengine katika Kijiji cha Bugaga, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakishindana kukimbilia wateja, waliokuwa wanapita na magari katika kijiji hicho, juzi. (INARUHUSIWA PICHA HIZI KUTUMIKA KWENYE VYOMBO VINGINE VYA HABARI KWA HISANI YA DAILY NKOROMO BLOG)

RAIS KIKWETE AZURU ZANZIBAR KUFARIJI WALIOPATWA NA AJALI YA MELI

PICHA ZA RAIS KIKWETE KWENYE MAAFA YA AJALI YA MELI ZANZIBAR INGIA KWENYE HUU MTABDAO WETU MWINGINE TANZANIA VISIO BLOG:-BONYEZA HAPA 

CCM YATOA POLE AJALI YA MELI ZANZIBAR

Jul 19, 2012

Nape

DODOMA, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa wale wote ambao wamepatwa na msiba katika ajali ya meli iliyotokea jana, Zanzibar.
Pamoja na pole, CCM  imeitaka serikali kuipitia upya taarifa ya Tume iliyoundwa kuchunguza ajali ya kwanza ya meli ya Mv. Spice Islander na kuitaka  serikali kuchukua hatua za haraka pale itakapobainika kuwepo kwa uzembe kwa watendaji wowote bila kujali nyadhifa zao.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM,  Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa leo kuhusu ajali hiyo.
Nape alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuipitia upya kwa taarifa hiyo kwani inawezekana kuna baadhi ya mambo hayakufuatiliwa kwa kina na au kuna uzembe unafanyika.
Alisema endapo kutabainika kuwepo kwa uzembe basi wale wote wanaohusika na uzembe huo wawajibike wenyewe kwani haiwezekani watumie fedha za wananchi lakini hakuna linalofanyika.
“Ni Muhimu tufike wakati wewe kama kiongozi unapoona jambo limekushinda au limetokea kutokana na uzembe na wewe kiongozi upo tujenge tabia ya kujudhuru hii itasaidia kuleta heshima zaidi’’ alisema Nape.
Alisema hali hiyo inatokana na ukweli kuwa mara kwa mara tukio la kuzama kwa meli au ajali mambo mbalimbali hujitokeza ikiwemo uzito wa mizigo au idadi kubwa kuliko uwezo wa meli au uchakavu.
Nape alisema vyombo vinavyohusika ni lazima kuwa makini na watendaji wake kama wameshindwa kufanya kazi ni bora wawajibike wenyewe au wawajibishwe na mamlaka  za juu.
“Sasa meli inaondokaje bandarini ikiwa imebeba abiria zaidi au mizigo zaidi ya uwezo wake wakati kuna watu wanaohusika na kazi hiyo, hii inatia shaka kidogo na huko ni kuwaibia wananchi kwa kutowajibika ’’
Kwa mujibu wa Katibu huyo alisema hivi sasa inaonekana kuwa usafiri wa ndege umekuwa ni wa uhakika zaidi lakini hilo linatokana na ukweli kuwa watendaji wake wamekuwa makini kila wakati.
Aidha Nape alisema kutokana na msiba huo ulitokea CCM imehairisha Mkutano wake wa hadhara ambao walipanga kufanyika Kigoma jana .
Alisema sasa mkutano huo utafanyika siku ya Jumapili  baada ya kumalizika kwa siku za maombolezo zilizowekwa na serikali.
“Tunatoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba na kwa wale ambao bado wanaugua kutokana na jail hiyo tunamuomba Mungu awaeze kuwasaidia waweze kupona haraka.
ยช