.

PINDA AKUTANA NA MWALIMU WAKE WA 'LOG TIME'

Aug 31, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwalimu wake, John Kasalamimba wakati walipokutana Mjini Mpanda jana, Agust 30,2012.Mwalimu Kasalamimba alimfundisha Waziri Mkuu  kuanzia mwaka 1960darasa la tatu katika Shule ya Msingi ya Kibaoni wilayani Mlele, Mpanda. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KATIBU MKUU WA CCM MKUTANONI NJE YA NCHI

KATIBU MKUU WA CCM MHE. WILSON MUKAMA (WAPILI KULIA) AKIFUATILIA MKUTANO MKUU WA 24 WA SOCIALIST INTERNATIONAL UNAOFANYIKA, CAPE TOWN, AFRIKA YA KUSINI. MKUTANO HUO ULIFUNGULIWA NA RAIS WA AFRIKA KUSINI, MHE. JACOB ZUMA, NA UTAMALIZIKA TAREHE 1/09/2012. PICHA NA EDWARD MPOGOLO WA OFISI YA KATIBU MKUU.

MFUMO WA MAWAKALA WA BENKI KUU KUNUNUA DHAMA NA HATI FUNGANI KWA ONLINE WAZINDULIWA

 GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu akiongea na waandishi wa habari jana  (leo) jijini Dar es salaam kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mfumo wa mawakala wa Benki hiyo wa kununua dhamana za Serikali na hati fungani kwa njia ya mtandano(online) kwenye mnada na hivyo kupunguza ule utaratibu wa dhamana wa kupeleka karatasi katika Benki ili kupata huduma hiyo, (kulia) ni Naibu Gavana wa BoT, Dk Natu Mwamba.

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu akizungumza jijini Dar es salaam, katika uzinduzi rasmi wa mfumo wa mawakala wa Benki hiyo wa kununua dhamana na hati fungani kwa njia ya mtandano(online) kwenye mnada na hivyo kupunguza ule utaratibu wa dhamana wa kupeleka karatasi katika Benki ili kupata huduma hiyo. PICHA NA TIGANYA VINCENT- MAELEZO-DAR ES SALAAM

BAADHI YA MAGAZETI YA LEO TANZANIA


MBUYU TWITE ATUA DAR, YANGA WAMPOKEA NA ULINZI WA POLISI

Aug 30, 2012

Mchezaji nyota wa  Rwanda Mbuyu Twite akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, alipowasili leo kukipiga katika  timu ya Yanga.

TBL YAFANYA MKUTANO WA MWAKA NA WANAHISA WAKE

 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Waziri Mkuu wa zamani Cleopa Msuya akizungumza, baada ya mkutano mkuu wa 39 wa mwaka Agosti 30, 2012, katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Kempinski Regency jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TBL,  Raphael Mollel, Mkurugenzi wa Mahusiano na Sheria TBL Steve Kilindo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,   Robin  Goetzsche.
 MWENYEKITI wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Waziri Mkuu wa zamani Cleopa Msuya akikifafanua jambo wakati wa mkutano mkuu wa 39 wa mwaka Agosti 30, 2012, katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Kempinski Regency jijini Dar es Salaam. Wengine, kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TBL,  Raphael Mollel, Mkurugenzi wa Mahusiano na Sheria TBL Steve Kilindo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,  Robin  Goetzsche na kulia ni Mjumbe wa Bodi Arnold Kilewo na Mkurugenzi wa Fedha TBL,  Kelvin O'Flaherty
Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Cleopa Msuya akitoka ukumbini baada ya mkutano huo
 Mwenkiti wa Bodi ya TBL Cleopa Msuya akimweleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Goetzsche nje ya ukumbi baada ya mkutano huo
 Meneja Uhusiano wa TBL  Editha Mushi akimshauri mmoja wa mabosi wa TBL
Mwenyekiti wa Bodi ya TBL Cleopa Msuya na Viongozi wa TBL wakiwa katika picha na Wanahisa wa kampuni hiyo baada ya mkutano huo.

DC WA ZAMANI HAWA NGURUME AFARIKI DUNIA


ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DK. RASHID WILAYANI RUFIJI

 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid  (Kulia)  akisalimiana na akina mama wa Kijiji cha Mtanza baada ya kumalizika kwa mkutano na wananchi wa eneo hilo wakati wa  ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Dk Rashid akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtanza jimboni humo juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mwaseni, Athuman Mbange (CUF) na kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtanza.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid  (wa pili kukushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa Kata ya Mwaseni, akikagua maendeleo ya ujenzi wa chumba cha darasa wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Bibi Fatuma Mazengo akiangua kilio mbele ya waziri alipokuwa akieleza jinsi mkwe wake na mjuu wake walivyouawa kinyama na Askari wa Wanyapori katika Hifadhi ya Mbuga ya Selou mpakani mwa kiji cha Mloka, Rufiji. Watu hao waliuawa walipokwenda kuvua samaki katika ziwa la Mzizizmia kwa ajili ya kitoweo
Akina mama wa Kijiji cha Mibuyu Saba  wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri

Mkazi wa Kijiji cha Mtanza, Yusufu Nyamgumi, akihoji kwenye mkutano kitendo cha Diwani wao, Athuman Mbange (CUF) kutokuwa na tabia ya kuwatembelea kujua matatizo yao, (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

WADAU WA TBL

Baadhi ya wadau wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiwa na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo, Editha Mushi  (katikati) wakati wa mkutano wa Wanahisa wa TBL unaoendelea mida hii kwenye Hotel Hyatt Kempinski, Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa Masoko ya Nje wa Kampuni ya Konyagi Bavon Ndumbali na kulia ni Mwandishi wa Tanzania Daima Edna Bondo.

BURIANI ASKOFU KIKOTI


CRDB BANK KUMEKUCHA TABATA, TAWI LAKE JIPYA LAHUDUMIA WASTANI WA WATEJA 300 KWA SIKU

 Jengo la Benki ya CRDB Tabata Magengeni ndiyo hili
 Meneja wa Benki ya CRDB PCL  tawi la Tabata, Dar es Salaam, Hawa Sasya akiwa ofisini kwake jana.
 Meneja wa  Benki ya CRDB PCL tawi  la Tabata, Dar es Salaam, Hawa Sasya akiwa ofisini kwake katika benki hiyo jana 
 Mmoja wa Maofisa wa Benki hiyo  akiwa kazini
 Mmoja wa maofisa wa benki hiyo akiwa kazini katika tawi hilo
 Meneja wa Benki ya CRDB PCL tawi la Tabata, Dar es Salaam, Hawa Sasya ( watatu kushoto)  akiwasaidia wateja kupata huduma wanazotaka, kwenye tawi hilo, jana. Tawi hilo jipya limefunguliwa mapema mwaka huu ikiwa CRDB ndiyo benki pekee inayotoa huduma za kibenki katika eneo hilo. Kwa Mujibu wa Meneja huyo tawi hilo huhudumia wastani wa wateja 300 kwa siku. 
Eneo la Huduma kwa wateja ndani ya tawi la benki hiyo, Tabata.  Habari zaidi BOFYA HAPA

NAPE AIKOMALIA CHADEMA

Aug 27, 2012

* Agoma kuomba raidhi, asema tuhuma atazithibitisha mahakamani
* Amtaka Dk. Slaa kuandaa bilioni 3 na shilingi moja
* Ni kwa kudai CCM inaingiza siala nchini.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amewataka Chadema kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa radhi kama walivyotaka ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama chao kupewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri...INAENDELEA:-TANZANIA VISION BLOG

RAIS KIKWETE AHESABIWA KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Aug 26, 2012Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na familia yao, wakati Rais Kikwete akihojiwa na  kujibu maswali kutoka kwa karani wa sensa ya watu na makazi, Clement Ngalaba,  Rais alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililoanza kufanyika leo Agosti 26, 2012, nchi nzima.
PICHA NA IKULU

DIWANI KWADELO MKOANI DODOMA, AHAMASISHA MAENDELEO

 Mkazi wa Kijiji cha Makirinyi, Khadija Mussa, akikabidhi  kiroba cha alizeti kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati kuchangia ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho, wakati wa harambee ya kutafuta fedha za ujenzi wa zahanati, uliondeshwa na diwani huyo, jana. Jumla ya magunia 17 yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, na sh. milioni 9.2 vilipatikana, ikiwa ni pamoja na sh. milioni 7 zilizochangwa na  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki
 Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati akiendesha trekta wakati akiwasili kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji katika kata hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis
Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kushoto ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo
 Trekta 64 za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, ambazo wamezipata kwa jitihada za diwani wa kata hiyo, Omary Kariati kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa ajili ya harambee ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kufufua mradi wa maji wa kata hiyo, jana. Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa mstari wa mbele kuchangia mradi huo wa maji.  Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
 Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati, akionyesha mtaro anaosema uliochimbwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake mwaka 1973, kwa ajili ya mradi wa maji katika Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, jana. Hata hivyo mradi huo ambao ulikuwa ukihudumia watu 1,200 wakati huo, umekufa miaka 20 iliyopita na sasa diwani huyo anaunganisha nguvu za pamoja za wananchi na serikali ya CCM kuufufua. Kwadelo sasa ina watu 11,800.
 Wananchi wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wakiwa kwenye mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji, katika kata hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa
na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
 Wazee wa Kata ya Kwadelo, wakipungua mikono kumuaga Diwani wa Kata
 Msichana katika kijiji cha Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma akitumia baiskeli kutafuta maji, katika kijiji cha Makiranya, jana
 Kariati akikaribisha nyumbani kwake waandishi wa habari aliofuatana nao kwenye ziara hiyo ya kuhamasisha maendeleo
 Trekta nyumbani kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati

MKUU WA WILAYA YA SERENGETI AFARIKI DUNIA

Aug 22, 2012


MKUU wa wilaya ya Serengeti Kepteni mstaafu, James Lyamungu amefariki dunia katika hospitali ya Taifa Mhimbili  Dar es Salaam, baada yakupelekwa  kupata matibabu.

Awali Mkuu huyo aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuhamishiwa katika hospitali ya mhimbili baada ya hali yakekuzidi kubadilika.

Marehemu Lyamungu amefariki dunia leo asubuhi  wakati akipewa matibabu katika hospitali  hiyo ya mhimbili na mwili wake umehifadhiwa .

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa amesema  kuwa taarifa za msiba  wa mkuu aliyekuwa  mkuu wa wilaya ya Serengeti amezipokea na kwamba wasemaji wakuu juu ya msiba huo ni Makao Makuu.

“Taarifa za Kifo cha marehemu tumeishazituma makao makuu sisi kama mkoa sio wasemaji kwani sio kila mtu atoe taarfa hizi tusubiri zitatolewa na makao makuu kwa vyombo vya habari”,alisema Tuppa.

CHADEMA WADAIWA KUWAPA RUSHWA VIONGOZI JUMUIA YA WATANZANIA WAISHIO WAHINGTON DC KUFANIKISHISHA MNUSO, JUMAMOSI HII

UONGOZI DMV 
WASHINGTON DC
MWENYEKITI, Katibu na Mweka  hazina, wa Jumuia ya Watanzania waishio Marekani, wanashutumiwa na wanajumuia wa Washignton kuwa wamepokea rushwa kutoka kwa Chadema kwa ajili ya kufanyia pickic na party ya usiku, vitakavyofanyika Jumamosi hii, Agosti 25, 2012.

Habari za madai za shutuma hizo zinasema kuwa Jumuia ilikuwa na  fedha taslim zisizozidi  Dola 2000 za Marekani zinazotosha kufanya party ya mchana ya picnic peke yake, lakini kwa cha kushangaza wakati wanajumuia wakiwa wanahoji kwa nini party ya usiku ifanyike wakati Jumuia haina fedha za kutosha, Viongozi hao wameweza kuja na fungu  kubwa la fedha ambazo watazitumia kufanya party zote mbili kubwa na za kifahari zitakazoambatana na chakula na vinywaji  mchana na usiku bure.

Kama haitoshi kutokana na fungu hilo, pombe zitakuwa za bure  hadi saa nane usiku, wakati ukumbi na  muziki vikiwa vimelipiwa kwa Cash siyo mkopo.

"Habari za kuaminika na ushahidi upo zinasema kuwa Katibu wa Jumuia Bwana Amosi Cherehani ni Mweka hazina wa Chadema Washigton na ndiye ambaye ameweza kuhamasisha fedha hizo kutoka Chadema iliziweze kufanya hafla hiyo", Imsema taarifa iliyotumwa kwa mtandao kutoka Marekani.

"Wananchi wanahoji kwa nini Mwenyekiti ambaye alichaguliwa  kwa kishindo ameweza kukubali kadia hii wkati Jumuia haifungamani na chama chochote cha siasa?" Imehojiwa katika taarifa hiyo.

"Kutokana na kadhia hiyo, wakereketwa wa Jumuia wameipa Mamlaka Kampuni ya ERNEST & YOUNG kufanya  "INDEPENDENCE AUDITING" ya Jumuia ili kujua "INCOME AND EXPENDITURE za Jumuia yao zometoka wapi na zimetumika vipi kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa", Taarifa imesema.

Tarrifa imesema wanajumuia wanaomba kuitisha mkutano ili kupiga kura a maoni ya kutokuwa na imani  na uongozi kwakuwa bado mchanga. .."Na tuliuchagua kwa imani, hatutaki vyama vya siasa vituingile...Rushwa ni adui wa Haki"

CCM KUKATA RUFANI HUKUMU YA KESI YA UCHAGUZI IGUNGA


DAR ES SALAAM, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga, Peter Dalally Kafumu.

Taarifa iliyolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye mchana leo, imeseme kufuatia kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali,  kitakata rufani.

"Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora. Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter Kafumu.Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo". imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Nape.

Jana Jaji  Mary Shangali katika hukumu yake, alisema ametengua ushindi wa Dk. Kafumu baada ya kurishishwa na madai saba kati ya 17 yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo na Mlalamilikaji, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Chadema, Joseph Kashindye.

Dk. Kafumu wa CCM alitangazwa kushinda kiti na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Igunga, katika uchaguzi mdogo uliofanyika, Septemba mwaka jana, baada ya kujiuzulu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Rostam Aziz.

RAIS KIKWETE AFURAHIA MAVUNO YA MAHINDI SHAMBANI KWAKERais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma, wakiwa na mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze, Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ambaye ni mkulima na mfugaji katika kijijini hicho, ameelezea  kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi aliyopata shambani kwake. PICHA NA IKULU

DK. MALECELA NA DK. MENGI ENZI HIZO

Picha kwa hisani ya Maktaba ya UHURU

UHURU LEO


ยช