.

UCHAGUZI WA CCM MKOANI KATAVI

Sep 30, 2012

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda ambaye ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM akifungua mkutano mkuu wa Uchaguzi wa  CCM  wilaya za Mlele na Mpanda mkoani Katavi kwenye Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Milala wilayani Mpanda, Septemba 30,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

NAGU AMGARAGAZA SUMAYE KATIKA U-NEC


MZEE MWINYI AWAKABIDHI KWADELO TANGI LA MAJI, KITANDA CHA KUJIFUNGULIA

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Ali Hassani Mwinyi leo
 Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omari Kariati akimsalimia Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwa Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi (kushoto), Mikocheni jijini Dar es Salaam. kabla ya hafla ya wananchi wa Kata hiyo kukabidhiwa tangi la maji na kidanda cha kujifungulia kina mama, iliyofanyika nyumbani hapo, leo.
 Diwani Kariati akiongozana na Mzee Mwinyi na Mama Sitti Mwinyi kwenda eneo la tukio
 UNAONA MAMBO YA KILIMO KWANZA? Akasema Omari Kariati wakati akitazama maembe yaliyopo kwenye mwembe wa kisasa uliopo nyumbani kwa Mzee Mwinyi.
 Kina mama wa Kwadelo wakiwa kwenye viwanja vya shughuli ya makabidhiano ya vifaa hivyo
 "Kwanza tunamshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mzee wetu  Ali Hassan Mwinyi kwa kutukaribisha nyumbani kwake kukamilisha hafla hii. Shughuli iliyotuleta hapa ni Mzee wetu kuwakabidhi wana-Kwadelo tangi kubwa la maji la sh. 650,000 na kitanda cha kujifungulia kina mama, kisha atamapatia sh. 200,000 kijana wetu aliyemuahidi kwa ajili ya kukamilisha masomo yake ya ualimu pale Ununio" akasema Diwani wa Kwadelo Omari Kariari kufungua shughuli. pembeni ni Mzee Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, wakimsikiliza.
 Kisha mzee Mwinyi na mkewe wakasongea pamoja na waalikwa pahala vilipokuwa vitu vya kukabidhi. Hapa anakabidhi kitanda
 Kwa furaha baada ya kukabidhiwa, mama mmoja wa Kwadelo akakifanyia majaribio kidogo kitanda hicho.
 Kisha Mzee Mwinyi akakabidhi tangi la lita 5000 kwa Mwadham Msami (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerereng'ombe, palepale Kwadelo. Naye Omari Kariati akishuhudia
 Baada ya kurejea meza kuu, Mzee Mwinyi akakabidhi sh. 200,000 kwa kijana, Kassim Omar kwa ajili ya kumalizia masomo yake ya ualimu Chuo cha Ununio, Bagamoyo.
 Kisha Mzee Mwinyi akaeleza yake ya moyoni kuwahusia wana Kwadelo na Watanzania kwa jumla akisema "wanaodhani maandamano yanaleta maendeleo wanapotea, maendeleo yanaletwa na kujituma na kutumia fursa zilizopo kufanya kazi kwa bidiii". Kushoto ni Mama Sitti Mwinyi.
 Picha za pamoja na Mzee mwinyi zikapigwa kwa makundi ya wananchi wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
 Hawa ni kina mama wa Kwadelo wakiwa na Mzee Mwinyi
 Na kina Baba wakachangamkia 
 Vijana wa Kwadelo wakiwa nyumna ya Mzee Mwinyi katika picha ya pamoja
 Hawa pia ni vijana wa Kwadelo kati ya 50 wanaofanya shughuli zao jijini Dar, waliojitolea kwenda kulima katika kata hiyo 
 Waandishi nao wakatumia fursa hiyoo adhimu kupigapicha na Mzee Mwinyi. Kulia kabisa ni Mimi
 Hapa pia ni waandishi wakichangamkia fursa hiyo.
 "Karibuni Chai" akasema Mama Sitti kuwakawakabisha wageni mwishoni mwa shughuli
Wageni wakachangamkia chai kama hivi: JE MZEE MWINYI ALISEMA NINI KWENYE HAFLA HII? TAFADHALI BOFYA HAPA 

NAPE: DK SLAA MWOGA WA KUSHINDWA

Sep 28, 2012

*Asema Dk. Slaa ameikimbia Mwanza mapema baada ya kunusa Chadema kugaragazwa
*Awapongeza madiwani wa CCM wa Nyamagana kwa kuwezesha ushindi wa Menya na Naibu Meya Nyamagana
NA MWANDISHI WETU, MWANZA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema  dalili za kubwagwa kwa CHADEMA ndizo zilizomkimbiza mapema jijini Mwanza, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroard Slaa.

Amesema kushindwa kwa Chadema katika kinyang’anyiro cha Meya na Naibu Meya, ni mavuno ya ubabe wa viongozi wa chama hicho ambao baadhi wanazeeka vibaya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Nape (pichani) alisema kwamba, Slaa alikimbia baada ya kuona maji yamezidi unga.

Nape aliyetumia fursa hiyo pia kuwapongeza Madiwani wa CCM wa wilaya ya Nyamagana na Chama kwa ushindi wa Viti vya Meya na Naibu wake, alisema Dk. Slaa anazeeka viba ndiyo maana naongoza chama hicho kwa ubabe na maandamano ya kila mara.

“Babu (akiwa na maana ya Dk Slaa) alisema CCM Mwanza itaondoka madarakani, imejidhihirisha wazi katika uchaguzi wa leo kuwa CCM bado ina nguvu na ni Chama kikongwe kisiasa, vingine vinaiga.”

“Chadema wameona mavuno ya ubabe wao japo kura za CCM ni ndogo…., Babu ajiulize kwa nini ameshindwa kwenye uchaguzi huo wa Meya na Naibu Meya.” Alisem Nape na kuongeza kwamba, kutokana na dalili za kushindwa zilizoonekana mapema, ndiyo maana Dk Slaa alikimbia Mwanza mapema.

Akiwapongeza madiwani hao kwa ushindi alisema kwamba wamefanya kazi kubwa na ya ziada kuhakikisha CCM inarejesha Halmashauri ya jiji hilo mikononi mwake baada ya kushikwa na Chadema kwa kipindi kifupi na hivyo kuwataka wana Mwanza wawe na mshikamano na kuwapa ushirikiano viuongozi wao.

“Nawasihi wananchi wa Mwanza wawe  na mshikamano na kuacha maandamano yasiyokuwa na msingi, badala yake wafanye maandeleo, waimamini CCM sasa inachokuja kufanya ni cha uhakika.” Alieleza Nape.

UCHAGUZI WAMEYA NA NAIBU MEYA, ILEMELA JIJINI MWANZA WAKWAA KISIKI


MEJA JENERALI MSTAAFU, ANATORY RUTA KAMAZIMA KUAGWA KESHO DAR


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa  Meja Jenerali Mstaafu, Anatory Ruta Kamazima (pichani), ambaye amefariki dunia mwanzoni mwa wiki hii, ataagwa rasmi katika Hospitali ya Lugalo tarehe 29 Septemba, 2012 saa saba mchana (7.00 mchana)  Nyumbani kwa marehemu eneo la Tegeta - Kibaoni baada ya soko la Nyuki Maruku Cottage.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk


    

AGNES KASANJA CHRISTOPHER YAMO KUZIKWA LEO


MDAUM USISUMBUKE!

Sep 27, 2012

KUMBUKA UNAWEZA KUPATA HABARI ZA SIASA, MICHEZO, JAMII NA NYINGINEZO KWA KUINGIA MOJA KWA MOJA KWENYE ENEO LA KURASA ZETU, KWENYE MKANDA HAPO JUU,  AU KWA MICHEZO TU-BOFYA HAPA NA KWA HABARI ZA SIASA TU BOFYA HAPA; TUNAKUPENDA SANA!

MEMBE HOLDS BILATERAL TALKS WITH U.S., KOSOVO AND NEW ZEALAND TODAY


Bilateral talks with the United States of America   
Hon. Bernard K. Membe (MP) (right), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation in a photo with Mr. Johnnie Carson, U.S. Assistant Secretary of State for African Affairs after they held bilateral talks yesterday at the United Nations Headquarters in New York, U.S.A. MORE PHOTOS:- CLICK HERE

RAIS KIKWETE ATETA NA MKE WA BILL GATES

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati alipokuwa katika mazungumzo na  Mkurugenzi wa  Bill and Melinda Gates Foundation Bibi Melinda  Gates wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa “African Green Revolution Forum 2012,” uliofanyika mjini Arusha leo (picha na Freddy Maro)

UTEUZI WAGOMBEA CCM, PAUL KIRIGINI ACHOMOZA

NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza majina ya makada wake walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, ambapo vijana wameonekana kupewa nafasi kubwa zaidi za kuwania fursa ya kukiongoza Chama hicho kikongwe nchini.

Vijana wengi wameonekana kuchomoza katika nafasi za uenyekiti, makamu mwenyekiti, itikadi na uenezi, uchumi na fedha na zile za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Miongoni mwa vijana mahiri na wenye uwezo mkubwa katika uongozi walipata fursa ya kupitishwa na NEC ni pamoja na Paulo Herman Kirigini, ambaye ameteuliwa kuwania ujumbe wa NEC kupitia viti vitatu bara kwa kundi la Wazazi, ambako atachuana na wakongwe kadhaa wakiwemo mawaziri na wabunge.

Vijana wengine waliochomoza katika kuwania nafasi mbalimbali ni Christopher Pallangyo (Mwenyekiti wilaya ya Meru), Latifa Ganzel (Morogoro Mjini), Harold Lyimo (Arusha), Peter Mushao (Longido), Nanai Konina (NEC- Monduli), Patrick Myovela (Iringa Vijijini), Muhaji  Bushako, Alice Mjula (Muleba) na Asad Salum Kikule (Kilolo).

Wengine ni Murdhid Ngeze (Bukoba Vijijini), Revocatus Babeiya, Editha Kokutona Rwezaula, Alistides Mujwahusi, Lucas Zakaria, Janes  Darabe.

Vijana wengine ni Dk. Sebastian Ndege (NEC-K-ndoni), Thabiti Ntuyabaliwe (NEC-Kndoni), Saidi Omar (NEC-K-ndoni).

Wengine ni Issa Mangungu (31) Phares Magesa (33) NEC Temeke,  Leonard Bugomola (27),
Malugu Mwendesha (33) nafasi ya katibu uchumi mkoa wa Geita, Christian Sinkonde (31) NEC Kisarawe.

Vijana wengine waliochomoza kwenye nafasi ya NEC, Morogoro Vijijini Omari Mgumba (36)
Robert Selasela (28), Zuberi Mfaume (39) na Morogoro Mjini ni Robert  Makorere (32),Kelvin Mutatila Njuwa (33 na Amina  Mhina (36).

Kuteuliwa kwa idadi kubwa ya vijana kunaashiria kuwa CCM imeanza kutekeleza mikakati yake ya kuendelea kukisuka upya na kuingiza damu changa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kisiasa na kuwadhibiti wapinzani.

WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA CCM – MWAKA 2012

Yafuatayo ni majina ya walioteuliwa na NEC ya CCM mjini Dodoma, Septemba 25, 2012, kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa CCM utakaofanyika Novemba Mwaka huu. KUYAONA MAJINA HAYO BOFYA HAPA

JK AWAAPISHA MAOFISA WA JWTZ LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Sep 26, 2012

 Amirijeshi Mkuu, Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Ikulu jijini Dar es salaam
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu kutoka kushoto) na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa leo  mara baada ya hafla fupi ya kuwaapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) akimweleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati).
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa leo jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, mkuu wa Jeshi la Polisi (wa pili kutoka kulia) na Paul Chagonja kamishina wa Oparesheni. Kulia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Devis Mwamunyange.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa waandamizi wanawake wa JWTZ leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni Meja Jenerali Lilian Kingazi (Kulia) na Meja Jenerali Grace Mwakipunda (kulia). Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO. TUKIO HILI LIPO PIA TANZANIA VISION BLOG

TANGAZO KWA WADAU WA BLOGU HII

HABARI ZOTE ZA MICHEZO ZIKIWEMO ZA KILA SIKU NA ZILIZOPITA  ZINAPATIKANA KATIKA UKURASA WETU WA SPOTI, UNAWEZA KUBOFYA KWENYE UKURASA HUO SEHEMU YA KURASA ZETU, AU BOFYA HAPA

AGNES YAMO WA TANZANIA DAIMA AFARIKI DUNIA

Sep 25, 2012


JK AWAAGA WAJUMBE WA NEC WA SASA, DODOMA

JK:PICHA HII TUNAPIGA KWA SABABU TUNAAGANA.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kabla ya kikao cha NEC, leo mjini Dodoma. Wengine, waliokaa. Kutoka kushoto ni Mawaziri Wakuu wa zamani, John Malecela na Cleopa Msuya, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama,  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, Rais wa Zanzibar  Dk. Ali Mohamed Sheni, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Kulia ni Mawaziri wakuu wa zamani Frederick Sumaye na Edward Lowassa. Picha zaidi tafadhali BOFYA HAPA

KUAPISHWA KWA MNADHIMU MKUU WA JESHI (JWTZ) NA MKUU WA JKT


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atamuapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga, kesho Jumatano tarehe 26 Septemba, 2012, katika viwanja vya Ikulu, katika muda utakaotangazwa baadaye.

"Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie jina la mwandishi na mpigapicha ambao watafika Ikulu kwa ajili ya shughuli hii. Kwa umuhimu wa maandalizi ya shughuli hii, tunaomba majina ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu leo Jumanne 25, Septemba, 2012", imesema taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

 "Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika. Aidha, tunasisitiza mavazi yawe nadhifu na heshima, kwa kuwa hii ni shughuli ya Kitaifa. Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni", Taarifa hiyo imeongeza. 

KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA DODOMA, WAWANIA UONGOZI 'PRESHA' JUU

Sep 24, 2012


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama
 Katika Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akisoma utangulizi, mwanzoni wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya  Kikwete na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius  Msekwa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwaslimia wajumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, Mjumbe wa NEC Oganaizeshenu, Asha Abdallah Juma na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, (Zanzibar Vuai Ali Vuai) kabla ya kuanza kukao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo
Wajumbe wa Kamati Kuu, Maua Daftari na Simba wakijadili jambo taratibu, kabla ya Kikao cha kamati hiyo kuanza leo mjini Dodoma
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiwa kwenye kikao hicho
 Wajumbe wa Kamati Kuu, Shamsi Vuai Nahodha na Spika Pandu Ameir Kificho wakiwa kwenye kikao hicho na kulia ni Dk. Abdallah Kigoda.
Baadhi ya viongozi wa CCM wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi kwa awamu nyingine katika uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika Novemba mwaka huu, wakiwa nje ya ukumbi wakati kikao cha Kamati Kuu kikiendelea mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Azim Premji, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus-Rukwa, Wajumbe wa NEC Asha Baraka na Hkadija Kopa  
 Anthony Dialo (kulia) akijadili jambo na wenzake nje ya ukumbi
Kina William Lukuvi, Tyson (siyo wa ngumi) na Nchemba wakibadiloishana mawazo nje ya ukumbi kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza
ยช