.

DK. BILAL KATIKA MKUTANO WA WAZAZI

Oct 31, 2012

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alipowasili kwenye Mkutano Mkuu wa Wazazi leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati

TAKUKURU SASA WALA SAHANI MOJA NA WAZAZI, WATANO WAKAMATWA KWA RUSHWA


*ZUNGU NAYE NDANI
Zungu
NA MWANDISHI  WETU, DODOMA
WATU watano akiwemo mbunge wa Ilala Musa Zungu wamekamatwa na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Dodoma wakidaiwa kutoa rushwa kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi ili wawachague.

Kamanda wa Taasisi hiyo Eunice Mmari alisema Zungu alikamatwa katika Hotel ya Golden Crown jana kati ya saa mbili na nusu na saa tatu usiku.

Eunice alisema baa ya taasisi yake kupata taarifa hizo walianza kumfatilia kwa karibu mgombea huyo na ndipo walipomsikia akitoa maagizo kupitia simu ya mkononi kuagia nani apewe kiasi gani.

Alisema baada ya hatua hiyo TAKUKURU walianza kumfatilia Zungu na ndipo waligundua kuwa yupo katika gari ndogo aina ya  Toyota Mark –II huku akifuatana na gari jingine aina ya Prado ambalo ndiko fedha na wapambe wake walikuwa wamepanda.

Alisema baa da kulisimamisha gari hilo alilokuwemo Zungu ghafla Prado hilo liliweza kutoroka na kumuacha Zungu na ndipo alipokamtwa na kuhojiwa.

Alisema hata hivyo TAKUKURU waliweza kufuatilia mitandao ya simu na kisha kubaini kuwa fedha hizo zilikuwa zikigawiwa na mmoja wa wakala wake ambaye naye kwa sasa wamekamtwa.

Kamanda huyo aliwataja wengine waliokamatwa  na Zungu ni pamoja na  Yahya Khamis Danga , Busulo Mohamed Pazi na Famik Joseph Mang’ati.

Alisema kwa sasa watuhumiwa hao wote wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi zaidi ukiendelea na watafikishwa mara baada ya kukamilika.

Aidha kamanda huyo alisema mwingine aliyekamtwa ni pamoja na Fatuma Kasenga  ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi kutoka Mkoa wa Mbeya.

Alisema mwenyekiti huyo alikamatwa usiku wa kuamkia leo, saa tisa usiku katika hoteli ya Kitoli mjini hapa akiwanunulia wajumbe wake chakula.

Kamanda huyo apia alisema kuna taarifa zaidi ambazo zinamtaja Alhaji Abdalah Bulembo kuwa naye amekuwa akitajwa sana katika utoaji huo wa rushwa.

Alisema hata hivyo wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma za Bulembo na wamepata taarifa za awali kuwa anatoa rushwa hizo nyumbani.

RAIS AFUNGFUA BARABARA TARAKEA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasin katika hafla ya ufunguzi rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea, leo kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MSIBA WA MTUNZA IKULU NDOGO YA ARUSHA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mtunza Ikulu ya Arusha (House Keeper), Lucy Samillah katika ibada ya mazishiliyfanyika nyumbani kwa marehemu, Arsha Mjini Oktoba 31, 2012. )Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZIARA YA RAIS KIKWETE KILIMANJARO

Oct 29, 2012


KILIMANJARO, TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Oktoba 29, 2012 ameendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika siku ya pili ya ziara yake ya siku nne katika Mkoa wa Kilimanjaro ambako amesimamishwa mara tisa na wananchi waliokuwa na hamu ya kumwona na kumsikiliza.
Mradi wa kwanza ambao Rais Kikwete ameukagua ni ujenzi wa nyumba za kisasa kwa ajili ya wahanga wa maporomoko ya ardhi ya mwaka 2006 katika kijiji cha Goha kilichoko Mamba Miamba katika Jimbo la Same Mashariki, Wilaya ya Same.
Katika kijiji hicho, Rais Kikwete amezindua ujenzi wa nyumba nane kwa ajili ya wahanga hao ambazo aliahidi kuwa Serikali ingewajengea wahanga hao wakati alipotembelea eneo hilo Desemba 18, 2006, kuhami msiba wa waliofariki na kuwafariji wafiwa.
Katika maporomoko hayo, watu 24 walipoteza maisha baada ya kufukiwa na ardhi ya maporomoko na wengine 25 waliumia.
Kiasi cha sh. milioni 150 zinatumika katika ujenzi wa nyumba hizo ambazo imepangwa kukamilika na kukabidhiwa kwa wenyewe Februari 5, mwakani, 2013.
Miongoni mwa wafadhili waliochangia ujenzi huo na huduma nyingine kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo zenye vyumba vitatu, sebule na baraza ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotoa kiasi cha sh milioni 162, Kampuni ya Barrick Gold inagharimia uunganishaji wa maji kwa kiasi cha sh. milioni 38 na Benki ya National Micro-Finance Banki ilitoa sh milioni 9.7.
Mradi mwingine mkubwa wa maendeleo ambao Mhe Rais Kikwete amezindua ni Kiwanda cha Kisindika Tangawizi cha Mamba Miamba ambacho kinamilikiwa na Wana-Ushirika wa Wakulima wa Tangawizi katika Wilaya ya Same – Mamba Ginger Growers Cooperative ambacho ujenzi wake ulianza 2008.
Kiwanda hicho ambacho ujenzi wake na mitambo yake tayari imegharimu sh. milioni 348 kitakuwa na uwezo wa kuajiri watu 300, kitachangia kupunguza umasikini kwa kuongeza kipato cha wananchi na pia kitawapa wananchi zao la kudumu la biashara.
Kiwanda hicho ambacho michango ya ujenzi wake na kazi ya kukijenga ulisimamiwa kwa karibu na Mbunge wa Same Mashariki, Mheshimiwa Anna Kilango Malecela kina uwezo wa kusindika tani kati ya nane na 10 za tangawizi kwa siku na tani 2,220 kwa mwaka
  Rais Kikwete alitoa mchango wake katika ujenzi wa kiwanda hicho kwa kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kiwanga hicho uliofanyika Oktoba 16, mwaka 2009 kwenye Hoteli ya New Africa, mjini Dar es Salaam. Kiasi cha sh milioni 287 zilipatikana kwenye harambee hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara baada ya kuzindua kiwanda hicho, Rais Kikwete amesisitiza umuhimu wa uongezaji thamani kwenye mazao ya wakulima nchini. Aidha, Rais Kikwete ameitaka Benki ya Raslimali Tanzania (TIC) kuongeza kasi katika kushughulikia maombi ya kiwanda hicho kwa ajili ya fedha za kufanya kazi (working capital).
Rais Kikwete pia ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli kwenye shule ya wasichana ya Dkt. Asha Rose Migiro iliyoko mjini Mwanga katika Wilaya ya Mwanga.
Ujenzi wa Hosteli hiyo umegharimu kiasi cha sh.milioni 367 ambao umechangiwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotoa sh. milioni 130, wafadhili wa shule hiyo kutoka Canada ambao mpaka sasa wametoa kiasi cha dola za Canada 200,000 na Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ambayo mpaka sasa imetoa sh milioni 7.5.
Ujenzi wa shule hiyo ambayo ni wasichana na inafundisha masomo ya sayansi ulianza mwaka 2006 kama mradi uliobuniwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Mwanga lakini baadaye shule hiyo ilichukuliwa na Halmashauri ambayo iliendeleza ujenzi huo kama shule ya kata.
Shule hiyo ambayo ujenzi wake pia umekuwa unachangiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Cleopa Msuya tokea mwaka 2009 mpaka sasa imefikia kidato cha tatu na wanafunzi 232. Shule ina wanafunzi 13.
Rais Kikwete anaendelea na ziara yake Mkoani Kilimanjaro kwa kufungua Barabara ya Mkuu-Tarakea wilayani Rombo na baadaye atafungua Jengo la Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali.

PINDA AWASILI DODOMA LEO TAYARI KWA KIKAO CHA BUNGE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi baaada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ajili ya kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Oktoba 30, 2012. (Picha na Ofisi ya Wazieri Mkuu)

CCM YAIBWAGA CHADEMA BUGARAMA, KAHAMA

Oct 28, 2012


Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kuibwaga Chadema katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika katika Kata ya Bugarama wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zilizopatikana zimesema,  katika uchaguzi huo ulifanyika leo CCM imepata kura 1145
Chadema: 772 na TADEA: 156 wagombea wakiwa Nixon Igoko (CCM) Erasmus Francis (Chadema) na Clement Michael (TADEA) 
Pia habari zilizopatikana kutoka Kata ya Shinyanga mjini ambako pia uchaguzi mdogo wa Udiwani umefanbyika, zimasema CCM imeshinda. Hata hivyo hatukuweza kupata mizania ya ushindi huo kwa kura.

CHADEMA YABAKI YATIMA NJOMBE, IRIMBA NA MBEYA


*MLEZI KATIKA MIKOA HIYO AJIVUA UANACHAMA KUEPUKANA NA KINA  MBOWE NA DK. SLAA
MBEYA, TANZANIA
CHADEMA kimebaki yatima katika mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa kufuatia aliyekuwa mlezi wa chama hicho katika mikoa hiyo, Thomas Nyimbo, kujivua  rasmi uanachama.

Nyimbo ambaye alikuwa nguzo muhimu kwa uhai wa Chadema katika mikoa hiyo, katika kujivua uanachama amesema  ni kwa sababu ya kuchoshwa na ubabaishaji uliopo miongoni mwa viongozi wakuu wa chama hicho huku akiwavurumishia lawama, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.Willbroad Slaa kwamba wamekuwa wakitumia chadema kama SACCOS yao ya kujipantia manufaa binafsi.

Akizungumza leo katika ukumbi wa hoteli ya Mount Livingstone mjini Mbeya, Nyimbo alisema ameamua kujivua uanachama baada ya kuona CHADEMA kinakwenda kinyume na malengo yake kama kinavyojipambua mbele ya umma wa watanzania.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana nchini kupigania maslahi yao kwa mtazamo chanya wenye kuleta mustakabari mzuri kwa Taifa, badala ya kufikiri kuwa mabadiliko ni kuiondoa CCM madarakani na kuiweka CHADEMA

“Licha ya CHADEMA kujaribu kuwaaminisha watanzania hasa vijana kuwa ndio chama chenye kuleta mabadiliko ya kweli, lakini Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dk.Slaa wamekuwa wakikitumia kujinufaisha wao binafsi” alisema Nyimbo.

Aliongeza  viongozi hao wakuu pia wamekuwa siyo watu wa kushaurika ndani ya chama huku kikbaya zaidi wakiendesha siasa katika mfumo mbaya wa kushawishi na kuaminisha jamii bila ya kuwa na suluhisho.

Nyimbo aliongeza siasa za namna hiyo ni hatari kwa Taifa, kwani baada ya kuungwa mkono kwa kiwango cha juu na kundi la vijana kwa imani ya kukombolewa pale watakapofanikiwa kushika dola, na kushindwa kutimiza vurugu kubwa zitalipuka nchini.

HERIETH MAKOMBE AHITIMU SHAHADA YA UZAMILI

Jana ilikuwa siku ya furaha kwa Herieth Makombe alipohitimu na kutunukiwa Shahada ya uzamili ya uchumi na Maendeleo ya jamii kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, wakati wa mahafali yaliyofanyika Viwanja vya Kibaha mkoa wa Pwani pamoja na naye ni mhitimu mwenzake Caroline Henrich

NAPE , MAIGE NA MGEJA KATIKA KUFUNGA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI BUGARAMA, WILAYANI KAHAMA

Oct 27, 2012

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM za udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, jana Oktoba 27.(Picha na Bashir Nkoromo)
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia mkutano wa kampeni a uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakiwa na  watafiti wa madini  kutoka kampuni ya Majordrilling, katika kijiji cha Kakola wilayani Kahama mkoani Shinyanga
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa katika mapokezi ya wananchi alipowasili kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM za udiwani kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga
 Wananchi katika kata ya Bugarama , Kahama mkoani Shinyanga, wakishangilia wakati wa kufunga kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo
 Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (kushoto) akimlaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipowasili Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Bugarama, mkoani humo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama, Mabala Mlolwa.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana kw furaha na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja walipokutana katika Kata ya Kakola, kabla ya kwenda kwenye mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM kata ya Bugarama mkoani humo.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakishiriki kucheza ngoma ya Baswezi, katika kijiji cha Buyange, Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM kata ya Bugarama.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Sinyanga Hamis Mgeja wakishiriki kucheza ngoma ya Baswezi kwenye mkutano wa kampeni za udiwani kata ya Bugarama mkoani humo.
 Madiwani wa Kata za Kahama wakiwa na mgombea Udiwani wa CCM, Kata ya Bugarama katika wilaya hiyo Nixon Ikoko wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani katika kata hiyo, uliohutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Msalala,  Ezekiel Maige wakati akimuombea kura mgombea udiwani wa CCM Kata ya Bugarama, kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika mji mdogo wa Bugarama.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimnadi mgombea wa Udiwani kata ya Bugarama, Nixon Igogo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakiwa na  watafiti wa madini  kutoka kampuni ya Majordrilling, katika kijiji cha Kakola wilayani Kahama mkoani Shinyanga
  Wazee wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipohutubia mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM  Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga.
 Kina mama wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Kata ya Bugarama
 Mzee wa miaka 98, Nickson Toma akifuatilia kwa makini mkutano wa kampeni za udiwani Kata ya Bugarama mkoani Shinyanga uliohutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicharaza ngoma kwenye mkutano wa kampeni za udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa shinyanga, Hamis Mgeja baada ya mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM Kata ya Bugarama mkoani humo, jana, Oktoba 27, 2012. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

KATIBU WA BAKWATA AJERUHIWA KWA BOMU ARUSHA

Oct 26, 2012EID MUBARAK WOTEEEEEE!!!!


Kwa niaba ya timu yote, mmiliki wa Blog za Nkoromo Daily,
 na Tanzania Vision, Bashir Nkoromo, anakutakia Amani, Upendo, Kheri na Fanaka katika Sikukuu hii ya Eid El Hajj.
Eid Mubarak!!!! 

JERRY SILAA MGOMBEA ALIYEVUNJA REKODI YA KUPATA KURA NYINGI UCHAGZI UVCCM


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, amevunja rekodi kwa kuzoa kura nyingi zaidi kuliko wagombea wengine wote katika Uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) uliofanyika juzi mjini Dodoma, baada ya kutetea nafasi yake ya Ujumbe wa NEC kupitia UVCCM kwa kupata kura 501. Pichani, Silaa (aliyesimama) akizungumza baada ya uchaguzi huo.

KHAMIS SADIFA JUMA MWENYEKITI MPYA UVCCM

Oct 24, 2012

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni akimpongeza, Khamis Sadifa Juma baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM, leo mjini Dodoma, kufuatia uchaguzi uliofanyika jana. Picha na Bashir Nkoromo wa Daily Nkoromo Blog

TANGAZONAPE AWA KIVUTIO MKUTANO MKUU WA UVCCM

Oct 23, 2012

Katibu wa Halmashauri Kuu yabTaifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicharaza gita zito la besi wakati bendi ya Vijana Jazz ilipokuwa ikiimba wimbo maalum katika Mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM, kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, mkoani Dodoma leo. Habari Kamili BOFYA HAPA

UCHAGUZI MKUU UVCCM, MGOMBEA AJITOA WAKATI WA KUOMBA KURA

Lulu akitangaza kujitoa

NA BASHIR NKOROMO, DODOMA
Wakati ilitarajiwa kwamba uchaguzi wa kumpata Mweneyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM (Taifa) ungeweza kutoa ushindani zaidi kutokana na nafasi hiyo kuombwa na wagombea wa jinsia zote, hali ilibadilika ghafla baada ya mgombea pekee mwanamke, Lulu Abdalla Msham kuamua kujiondoa badala ya kuomba kura.

Kufuatia kujiondoa kwake  mwanamke huyo, nafasi hiyo ilibaki ikiwaniwa na madume wawili, 
Msaraka Rashid Simai na Khamis Sadifa Juma wote kutoka zanzibar.

Katika uchaguzi huo uliofanyika baada ya kufunguliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere mjini Dodoma, nafasi ya Makamu Mwenyekiti wamechuana Ally Salum Hapi, Paul Christian Makonda Mboni Mohamed Mhita.

Nafasi nyingine ni, Halmashauri Kuu ya Taifa Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22, Nafasi ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti vitano Zanzibar wagombea 14,  Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.

MARTHA: WANAOTUMIA FEDHA KUSAKA UONGOZI HAWAITAKII MEMA CCM

Oct 22, 2012

Martha Mlata

NA MWANDISHI WETU
MATUMIZI makubwa ya fedha katika uchaguzi ndani ya CCM na Jumuia zake yanayofanywa na baadhi ya wanachama wasio waaminifu, yameendelea kulalamikiwa ambapo, kwa sasa mikakati ya kuwadhoofisha wagombea wengine imebainika.

Miongoni mwa wagombea wanaodaiwa kuwa wako kwenye mtego wa kudhoofishwa ni Martha Mlata, ambaye anawania nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Taifa.

Habari zilizopatikana zinadai kuwa, baadhi ya vigogo wanaohusishwa na mbio za urais katika uchaguzi mkuu wa 2015, wametenga fungu kubwa la fedha kuhakikisha mgombea wao anachukua nafasi hiyo.

Pamoja na Mlata, wanaowania Uenyekiti wa Wazazi Taifa, ni John Barongo na Abdallah Bulembo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wajumbe walisema kuwa wanachama wanaotumia fedha kwa ajili ya kupanga safu ya uongozi hawana mapenzi mema na Chama na kwamba, wamelenga kukitumia kwa maslahi binafsi.

Hata hivyo, wamesema kuwa kamwe hawatakubali kuona hilo likifanyika na kwamba, wataingia kwenye chumba cha kupiga kura na kumchagua kiongozi bora na mwenye mapenzi mema na CCM.

"Mambo yanayoendelea ni machafu na hatutakubali yapite kama wanavyotaka, CCM ni ya Watanzania wote hivyo mambo ya watu wachache kupanga safu za uongozi hatutakubaliana nayo. Wameanza katika uchaguzi ngazi za wilaya, mikoa na sasa wanakuja taifa kwenye jumuia kuharibu," alisema mwanachama mmoja ambaye hakupenda kutajwa jina.

Mwana-CCM huyo alidokeza kuwa, uchaguzi wa UWT uligubikwa na vitendo vichafu na ukiukwaji wa taratibu ikiwa ni pamoja na matumizi makubwa ya fedha na kwamba, hata kuangushwa kwa Martha na Namelok Sokoine kulipangwa mapema.

Martha alikuwa akichuana na Namelok katika kuwania nafasi ya uwakilishi wa UWT katika Jumuia ya Wazazi, ambapo nguvu kubwa ya fedha ilitumika kumwagusha ili kutengeneza mazingira ya kumdhoofisha katika kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Taifa.

Kwa upande wake Martha alipoulizwa, alisema ni muda mrefu amekuwa akifanyiwa kampeni chafu kwa lengo la kumwangusha katika harakati zake za kuwania nafasi hiyo, lakini hatimaye wajumbe ndio watafanya maamuzi.

"Mimi namwachia Mungu na waamuzi wa mwisho ni wajumbe wa mkutano mkuu wa Wazazi, kila kukicha nafanyiwa kampeni chafu ili nishindwe. Nia yangu ni kuitumikia jumuia na CCM na watanzania ili kusukuma gurudumu la maendeleo, sasa kama wengine wanatumia fedha kuharibu basi viongozi wataamua la kufanya," alisema Martha.

UCHAGUZI MKUU UVCCM KUANZA KESHO DODOMA


*Shigela atamba rushwa kutopenya kwenye uchaguzi wao
* Awakamia watakaotafuta ushindi kwa njia hiyo na kampeni za majitaka
Shigela akizungumza mjini Dodoma leo
NA BASHIR NKOROMO, DODOMA, TANZANIA
WAKATI Uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umemalizika juzi, huku ukidaiwa kugubikwa na ubabe na rushwa, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umejitapa kwamba, utahakikisha vitendo hivyo havitokei katika uchaguzi wake mkuu utakaofanyika kuanzia kesho mjini Dodoma.

UVCCM imeapa kwamba mgombea au hata mpambe atakayebainika kujihusisha na kampeni zilizo nje ya utaratibu na kanuni za UVCCM au kujihusisha na vitendo vya rushwa atashughulikiwa mara moja ikiwemo kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM,Martine Shigela alisema, wameweka mtandao mpana wa kutosha kukabiliana na aina yoyote ya ukiukwaji wa tararibu, kanuni na sheria za uchaguzi wa UVCCM.

"Sisi hatuwezi kuzungumzia hayo mnayosema, yamejitokeza kwenye uchaguzi wa UWT,lakini kwa upande wetu tunawahakikishieni kwamba tutamkabili vilivyo tena bila mzaha,mgombea au mpambe yeyote atakayejaribu  kutumia mbinu chafu za kampeni ikiwemo kutoa rushwa", alisema Shigela.

Shigela alisema, taratibu za mkutano mkuu utakaoambatana na uchaguzi huo, zimekamilika na utafanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, uliopo Chuo Cha Mipango ambako ndiko ulikofanyika pia ule wa UWT.

Alisema, mkutano unaanza kesho, Oktoba 23, na utafunguliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete."Hadi sasa maandalizi yamekamilika, leo Oktoba 22, tunakazi kupokea wageni mbalimbali kutoka maeneo kadhaa wakiwemo wa kutoka nchi za nje amabao watahudhuria mkutano wetu. alisema Shigela.

Katika nafasi ya Mwenyekiti wanachuana wagombea watatu, Lulu Mushamu Abdallah,  Sadifu Juma Khamis na Rashid Simai Msaraka wakati katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ally Salum Hapi, Paul Christian Makonda Mboni Mohamed Mhita.

Nafasi zingine ni, Halmashauri Kuu ya Taifa Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22, Nafasi ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti vitano Zanzibar wagombea 14,  Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.

MATOKEO UCHAGUZI WA KINA SOPHIA SIMBA

Oct 21, 2012


DODOMA, TANZANIA
Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) jana ulikamilisha uchaguzi wake mkuu ambao Mwenyekiti wa zamani Sophia Simba akitangazwa kuwa mshindi kwa kura 716 huku Anne kilango aliyedhaniwa kutoa ushindani mkali akipata kura 310 tu. Akitangaza matokeo hayo jana saa 7.30 usiku...INAENDELEA.. BOFYA

SERIKALI: SMS ZINAZOSAMBAZWA KWAMBA MPAKANI MWA TANZANIA NA MALAWI KUNA MABOMU NI ZA UONGO


Kuna taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message za simu kwamba  kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100 na kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa waangalifu. Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake  haliwezi kuwa zuri kwa Watanzania.  Wananchi wanashauriwa kutotuma taarifa zozote kwenye namba hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.

Assah Mwambene
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.
Mobile +255782-553737,+255756887880

DK. BILAL KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE WAFANYABIASHARA KUTOKA NCHI ZA MASHARIKI MWA AFRIKA


NA TIGANYA VINCENT-MAELEZO
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal (PICHANI), anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya Mashariki mwa Afrika unaonza kesho  jijini Dar es salaam kwa lengo la kuimarisha mtandao wao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami wakati  akiongea na waandishi  wa habari  Ofisi kwake.

Amesema kuwa Mkutano huo ambao ni wa saba(7) unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu walipoanzisha ushirikiano huo wa wanawake wafanyabiashara kwa nchi za  Afrika Mashariki.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa wajumbe wa Mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika Nchi za Kenya, Uganda, Rwanda , Burundi, Ethiopia , Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania.

Amesema kuwa  Mkutano huo utakuwa fursa nzuri kwa wajumbe kutoka nchi zote saba kubadilishana uzoefu katika kazi ya kuwainua kiuchumi wakimama na kuimarisha Mtandao wa Wafanyabiashara wanawake katika Nchi za Afrika Mashariki.

Ameongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kufanya soko la wafanyabiasha wanawake wa Afrika Mashariki kuwa kubwa na hivyo kuwainua kiuchumi wakimama.

Aidha Bibi Fatma Riyami amesema kuwa TWCC imeanzisha matawi katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Pwani, Dodoma, Mbeya, Dar es salaam na Arusha ikiwa na lengo la kutaka kuwa karibu na wafanfanyabiashara wanawake kwa nia kuimarisha Umoja wao.

Wakati huo Mwenyekiti huyo amewasisitiza wajumbe wa Mkutano huo kufika katika Hoteli hiyo ifikapo saa 1.30 Asubuhi , Mgeni rasmi atafungua mkutano huo saa 2.00 kamili

JE, WEWE NI MPENZI WA HABARI ZA KI-SPOTI?

TAFADHALI BOFYA KWENYE UKURASA WETU WA SPOTI KWENYE UTEPE HAPO JUU AU BOFYA HAPA UPATE HABARI ZA LEO LEO

ZIARA YA NAPE MKOANI KILIMANJARO

 Nape Nnauye, Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi akiweka jiwe la msingi katika ofisi mpya ya CCM ,Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro tarehe 20/10/2012
 Wananchi wa kata ya Nanjara Reha wakimpokea Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, tayari kwa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM kwa kiti cha Udiwani.
 Wanachama wakongwe wa chama cha mapinduzi wakionyesha kukubaliana na hotuba ya Katibu wa NEC,itikadi na Uenezi, Nape Moses Nnauye alipowahutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni za Diwani wa Kata ya Nanjara Reha, Rombo ,mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Madiwani wakiwa kwenye picha ya pamoja, Madiwani hawa ni kati ya Madiwani 21 ambao kwa pamoja wataweka nguvu zao kuhakikisha kata ya Nanjara Reha inarudi CCM. PICHA ZOTE NA ADAM MZEE

NI SOPHIA SIMBA TENA UWT

Oct 20, 2012

MWWENYEKITI wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo muhula uliopita, Waziri Sophia Simba amefanikiwa kukitetea  kiti hicho, kufuatia duru za uchaguzi mkuu wa Jumuia hiyo uliofanyika leo mjini Dodoma, kuonyesha kuwa ameshinda.

Habari zinasema, katika uchaguzi huo uliosimamiwa na viongozi mahiri akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Wilison Mukama na  Mjumbe wa NEC wa zamani Abdulrahman Kinana, Simba ametajwa kuongoza  kwa kura nyingi dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Anne Kilango Malecela. TUTAWALETEA MATOKEO KAMILI TUKIYAPATA

TANZANIA YAISHAURI ICC KUJIEPUSHA NA USHAWISHI WA KISIASA

Oct 19, 2012

 Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mjadala wa wazi ulioandaliwana Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Mjadala huo ulihusu uhusiano kati ya Amani na Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC)
Wajumbe wa Baraza Kuu la  Usalama la Umoja wa Mataifa wakiwa kwenye kikao chake cha wazi kujadili uhusiano kati ya  Amani, Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai. (ICC). HABARI KAMILI BOFYA HAPA

UWT YAAPA KUWAVUA USHINDI WAGOMBEA WATAKATAFUTA KURA KWA NJIA HARAMU

Amina Makillagi

DODOMA, TANZANIA
KITIMU timu cha Uchaguzi Mkuu wa Jumuia ya Wanawake Tanzania(UWT) kinaanza lesho Mkutano Mkuu wa Jumuia hiyo utakapoanza. 

Wakati joto likiwa limeshapanda miongoni mwa wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika Jumuia hiyo, UWT imeapa kumpoka mshindi mgombea yeyote atakayebainika kujihusisha na rushwa au kampeni za kupakana matope.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Makillagi amesema ingawa mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za kuwepo kwa vitendo vya rushwa miongoni mwa wagombea lakini, atayekegundulika atapokonywa ushindi bila kujali ameshinda kwa kura kiasi gani.

"Kama ilivyokawaida yetu na kanuni na maadili yetu yanavyosema kuwa yeyote atakayebainika kujihusisha na rushwa au kampeni za kupakana matope hatutasita kumpoka uongozi alioupata'' alisema.

Alisema ni vyema wagombea wote wakafuata kanuni katika uchaguzi huo kwa kujiepusha kwa vitendo vya rushwa wasipokee wala kutoa rushwa kwa wagombea.

Akizungumzia matayarisho ya mkutano huo Katibu Makilagi alisema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal na kufungwa kesho na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema baada ya ufunguzi huo Mkutano huo utapokea salaamu toka vyama marafiki kikiwemo ANC,Zanu PF, Angola, Namimbia Rwanda,Burundi na Kenya.

Katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM Dodoma wapambe wa wagombea walionekana wakigawa vipeperushi huku kila mmoja akimnadi mgombea wake.

Katika Mkutano huo nafasi mbalimbali zitagombewa ikiwemo nafasi ya mwenyekiti wa UWT ambayo inagombewa na wagombea watatu ambao ni Sophia Simba, Mayrose Majige na Ane Kilango Malecela, huku nafasi ya Makamu wakichuana Asha Abdallah Juma na Asha Bakar Makame.  

'WAISLAM' WACHAFUA TENA HALI YA HEWA DAR

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Kama hali ilivyokuwa baada ya Sala ya Ijumaa iliyopita, leo baadhi ya waislam wanaotaka kujitambulisha kuwe wenye msimamo mkali hapa nchini wazua tafrrani katika maeneo mbali mbali ya jijini la Dar es Salaam na kusababisha hali ya amani kuwa ya wasi wasi.

Kufuatia tafrani hilo Daily Nkoromo Blog imeshuhudia maduka yakifungwa hasa  katika maeneo ya Kariakoo, ambako kwa kawaida huwa na pilikapilika nyingi za wafanya biashara kuliko maeneo mengi jijini Dar es Salaam.

Ilibidi polisi wa kikosin cha kuzuia ghasia kupambana na 'waislam' hao ambao awalifanya maandamano ya aina yake, kwa kuanza kukusanyika makundi madogo na maandaye kuwa makubwa ambapo polisi wamelazimika kutumia nguvu kuwatawanya.

Hadi sasa bado hali yaijarejea  kuwa shwari katika maeneo mbalimbali na polisi wanaonekana kuendelea kuimarisha ulinzi.

Yakijiri  zaidi tutawaletea baadaye

DIALLO AMPIGA MABINA: AWA MWENYEKITI MPYA CCM MWANZA

Oct 16, 2012


MANONGI:TUACHE MALUMBANO TUJADILI HALI HALISI

Balozi wa  Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Tuvako  Manongi, akizungumza  siku ya  Jumatatu,wakati wa Uzinduzi wa Tathmini ya Miaka  Minne ya Shughuli za Maendeleo za Umoja wa Mataifa ( QCPR). Uzinduzi ambao umefanyika  wakati wa Mkutano wa Baraza la Uchumi na Fedha  ( ECOSOC)la Baraza Kuu la 67 la  Umoja wa Mataifa. Tanzania ni Makamu Mwenyekiti wa  Baraza hilo.   Katika mchango wake Balozi aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili hali halisi ya  matatizo ya kiuchumi , kuongezeka kwa umaskini na upunguaji wa misaada ya  kimaendeleo  kwa nchi  hasa  zinazoendelea na  nafasi ya  Umoja wa Mataifa katika  ufadhili na usimamiaji wa miradi ya mendeleo  badala ya nchi wanachama kutumia muda mwingi kujitafutia uhalali na umaarufu. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Katibu  Mkuu, Bw. Jan Eliasson. HABARI KAMILI..BOFYA HAPA

JAJI WARIOBA: HUU SIO WAKATI WA KUPIGA KURA, TUNATAFUTA HOJA


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (pichani), amesisitiza umumihu wa wananchi kutoa maoni maoni yao kuhusu Katiba Mpya badala ya kukimbilia kuwasilisha maoni waliyolishwa na viongozi wa vyama vya siasa, asasi za kiraia na kidini.
Jaji Warioba ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 16, 2012) katika mkutano kati ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na uongozi wa Tume hiyo uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Mstaafu huyo baadhi ya viongozi hao na wadau wengine wanadhani maamuzi ya kazi ya kukusanya maoni inayofanywa kwa sasa na Tume yatamuliwa kwa kura na hivyo kuwalisha wananchi maoni ili wayatoa kwa Tume kwa wingi.
“Wengine wanafikiri huu ni wakati wa kupiga kura…hapana, sisi tunatafuta hoja,” alisema Mwenyekiti huyo na kuwataka wadau mbalimbali kuwaacha wananchi watoe maoni yao binafsi.
Awali akiongea katika mkutano huo, Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Muhambwe, Bw. Felix Mkosamali alipendekeza Tume iwe inagawa kwa wananchi fomu maalum za kujaza maoni yao siku kadhaa kabla ya Tume kufika ili kuwapa wananchi fursa ya kuandika maoni kwa kina tofauti na sasa ambapo Tume hutoa karatasi hizo kabla ya kuanza mkutano.
Akifafanua kuhusu hilo, Jaji Warioba amesema uamuzi wa Tume kugawa fomu hizo mkutanoni unalenga kupata maoni binafsi ya wananchi na kuongeza kuwa fomu hizo zikigawiwa mapema kuna uwezekano mkubwa kwa wananchi kujaziwa maoni na watu wengine.
“Uzoefu wetu umeonyesha hili la watu kuelekezwa nini cha kusema ambacho kwa kwli hawavijui kwa kina,” alisema katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki, Katibu wa Tume hiyo Bw. Assaa Rashid na Naibu Katibu Bw. Casmir Kyuki.
Pamoja na ufafanuzi kuhusu utoaji maoni binafsi ya wananchi, Mwenyekiti huyo pia aliwaeleza Wajumbe wa Kamati hiyo  kuwa lengo la Tume ni kuhakikisha kuwa mchakato wote wa uandikaji wa katiba unakuwa wazi na wananchi wanashiriki kikamilifu.
“Tukimaliza kukusanya maoni, tutaingia hatua ya pili ya Mabaraza ya Katiba katika kila wilaya na baadhi ya taasisi ambapo tunataka wananchi wenyewe katika maeneo husika wachague nani awawakilishe katika mabaraza hayo,” alisema Mwenyekiti huyo.
Ufafanuzi huu ulifuatia swali la Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee aliyeomba ufafanuzi kuhusu upatikanaji wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ambayo yanapitia rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Tume.
Akifafanua zaidi, Jaji Warioba alisema Tume imepanga kufanya mikutano miwili katika kila wilaya ambapo wawakilishi wa wananchi watajadili rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Tume baada ya kukusanya maoni yao katika awamu ya kwanza.
“Ni hatua ambayo tunadhani itahitaji fedha nyingi hasa katika kuwasafirisha hao wawakilishi wa wananchi kuja katika mikutano…hatutaki kuona wananchi wanapata sababu ya kutoshiriki hatua hii muhimu,” alisema na kuwaomba Wajumbe wa Kamati kuzingatia hoja hizo pale Tume itakapoomba fedha zaidi.
Pamoja na maoni hayo, Wajumbe hao pia waliieleza Tume umuhimu wa kuongeza utoaji elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Tume na Katiba.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Kairuki alisema Serikali itaendelea kuipa Tume hiyo kila aina ya ushirikiano ili itekeleze majukumu yake kwa ufanisi na kuwaomba Wabunge hao kuendeleza ushirikiano wanaoipa Tume hiyo.

JE WEWE NI MTUMIAJI TUMBAKU? FAIDA ZAKE HIZI HAPA


RAIS KIKWETE AZUNGUMZA NA MFALME QABOOS NCHINI OMAN


Tanzania na Oman zina mahusiano ya kidamu na kindugu ambayo ni  maalum sana yanayopaswa kudumishwa, kuthaminiwa na kuenziwa kwa dhati.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemuambia Mfalme Qaboos Bin Said katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika katika nyumba ya kifalme ya Al -Alam mara baada ya kuwasili katika Taifa la Kifalme la Oman jana  tarehe 15.Octoba, kuanza ziara ya kiserikali ya siku 4. 

"Tanzania na Oman zina mashirikiano maalum kuliko nchi nyingine yeyote duniani  kwa sababu ya undugu wa damu uliopo baina ya watanzania na wa Oman, hivyo hii ni ziara  maalum sana  katika nchi zetu." Rais amemuambia Mfalme. 

Mfalme Qaboos amekubaliana na Rais Kikwete na kumueleza kuwa ni muhimu mahusiano haya yakadumishwa zaidi kwa njia ya uwekezaji katika nyanja mbalimbali, hasa katika Viwanda. 

Rais Kikwete amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula maalum cha usiku ambapo Rais na ujumbe wake wamehudhuria.

Katika ujumbe wake Rais amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof Sospeter Muhongo, Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe. Dr. Abdallah Kigoda, Waziri wa Kazi, Ushirika  na Uwezeshaji , Zanzibar Mhe. Haroun  Ali Suleiman na Naibu Waziri Fedha wa Tanzania Mhe. Janet Mbene.

Katika Ziara hii, Rais amefuatana na wafanyibiashara kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambapo leo tarehe 16 Octoba,2012 atakuwa na kikao na wafanyabiashara wa Tanzania na Oman na hatimaye kutia saini makubaliano ya kibiashara na kiuchumi baina ya nchi mbili hizi. 

Mbali na kufanya mkutano na wafanyibiashara, leo Rais  atatembelea makumbusho ya jeshi na jioni  atakutana tena na Mfalme kwa ajili ya chakula binafsi cha usiku.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                      
ยช