.

INTERNATIONAL PHOTOGRAPHY COMPETITION - "JOBS IN THE WORLD"

Nov 29, 2012
WATANZANIA WAISHIO UJERUMANI KUMUAGA BALOZI AHMADA NGERERA DESEMBA 8, MWAKA HUU MJINI BERLIN


Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) unaheshima kubwa kutarifu na kuwaomba watanzania wote wanaoishi ujerumani na jirani ya Ujerumani kuwa umoja wetu tunatarajia kufanya afla ya kumuaga
Mheshimiwa balozi  Bw. Ahmada Ngemera ambaye anamaliza mda wake wa kufanya kazi,

Hafla hiyo itafanyika mjini Berlin siku ya Jumamosi tarehe 8.12.2012 .

Mhe.Balozi bwana Ahmada Ngemera  (pichani) amekua balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na watanzania wanaoishi ujerumani watamkumbuka daima Mheshimiwa Balozi Bw.Ahmada Ngemera kwa kuwa karibu sana na jamii ya watanzania,pia atakumbukwa kwa jitihada zake au kile ambacho watanzania wa ujerumani wanachokiita kuasisi Umoja na mshikamano wa watanzania nchi ujerumani, ambapo Mhe.Balozi Bw.Ngemera na msaidizi wake Mhe.Bw.Ali Siwa wahamua kuhamasisha watanzania waishio Ujerumani kuungana katika kila hali kuanzisha umoja wa mshikamano wa watanzania,kitu ambacho mabalozi wengi walishindwa kufanikiwa kufanya labda kwa sababu ya ukubwa wa nchi ya ujerumani wa watanzania wanaishi katika miji mbali mbali,lakini kazi hiyo ya kuwaungunganisha watanzania, Balozi Bw.Ahmada Ngemera na Msaidizi wake Bw.Ali Siwa walifanikiwa kuwafikia
 watanzania wote waishio Ujerumani na kuwashauri waanzishe umoja wa mshikimano, na matunda ya juhudi zao ndipo kukazaliwa Umoja wa waTanzania Ujerumani.(UTU)  Umoja ambao ni chombo cha watanzania wote ! chombo ambacho watanzania waishio ujerumani wanajivunia !

UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO MSINGI WETU IMARA!
OMBI:TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE ! NA MARAFIKI WOTE WA TANZANIA
AMBAO WANATAKA KUSHIRIKI KATIKA AFLA HII,TUNAOMBA MTOE MCHANGO WA EURO 20.00 NA KWA WANAFUNZI EURO 10.00 TU
 kwa kupitia Account : Union of Tanzania in German e.V.
VR Bank Rosenheim-Chiemsee AG
Konto-No.: 59641   BLZ: 71160161
Verwendungszweck: „Kumuaga Mhe. Balozi Ngemera

Pia unaweza kuwasiliana na kamati.utu@googlemail.com
simu namba +491734297997 au Katibu simu namba 01734744265 .

MWILI WA MSANII WA BONGO MOVIE JOHN MAGANGA WAZIKWA LEO

Nov 27, 2012

 Wasanii wa Bongo Movie wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyamala, Dar es Salaam. Maganga amefariki dunia Jumamosi hii, katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam, baada ya kuugua ghafla. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA KWENYE UKURASA WETU WA SPOTI

WIZARA YA FEDHA YASAINI MKATABA WA BILIONI 33 NA UHOLANZI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) na Balozi wa Uholanzi nchini Dr. Ad  Koekkoek (kulia) wakibadilishana hati  ya msaada wa shilingi bilioni 33 uliotolewa na Serikali ya Uholanzi kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali 37 hapa nchini. Tanzania nayo inatakiwa kuchangia kiasi kama hicho katika huduma hiyo ili  kuwa asilimia 50 kwa 50 kila pande yaani Tanzania na Uholanzi.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam

SHARO MILIONEA AFARIKI KWA AJALI YA GARI


JK AONGOZA HARAMBEE CHUO KIKUU CHA ST. JOHN

Nov 26, 2012

Mkurugenzi mkuu wa PPF Bwana William Eriyo akikabidhi hundi ya shilingi milioni kumi kama mchango wa shirika lake kwa ajili ujenzi  ya Hosteli ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na wasichana katika Chuo Kikuu cha St.John kilichopo mjini Dodoma, wakati wa harambee iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar ea Salaam leo.Katika Harambe hiyo jumla ya shilingi milioni 584/m zilikusanya ikiwa ni ahadi na fedha taslimu.Wapili kushoto ni Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Dr.Valentino Mokiwa na kulia ni Mkuu wa chuo hicho askofu mkuu mstaafu Dr.Donald Mtetemela (Picha na Freddy Maro)

VIONGOZI WA CHADEMA MBARONI KWA WIZI WA MILIONI 16 ZA KIJIJIGEITA, TANZANIA
Baada ya Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na upotevu wa sh. milioni 16.6, za Halmashauri ya Kijiji cha Katoro mkoani Geita,  wakamatwe haraka na kufikishwa mahakamani, viongozi watatu wa kijiji hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Joel Mazemule (CHADEMA), wamekamatwa na walitarajiwa kufikishwa mahakamni leo kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.

Mwanri alitoa agizo hilo  wakati wa ziara  ya Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, iliyongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Abdulrahman Kinana, baada ya wananchi kuelezwa kuwa, viongozi hao wametafuna kiasi hicho cha fedha lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao.


Kamanda wa polisi Mkoani Geita, Leonard Paulo, katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jana, aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Mazemule (42) kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katoro, Fundi Makanza(44) na kuwa mwingine ni Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho kupitia CHADEMA, Charles Malegi (34).

Kamanda huyo alisema “Ni kweli tunawashikilia hawa viongozi watatu toka jana kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. Milioni 116.6 ambazo ni mali ya umma.”

Alieleza kwamba, polisi limefuatilia vielelezo vyote ikiwemo nakala halisi zilizotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Alexander Lumelezi na kujiridhisha, ndio maana wakawakamata.

Alisema, fedha hizo zinazodaiwa kutafunwa na watuhumiwa hao, zilitokana na ukusanyaji ushuru, toka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo mashamba, visima na maduka yaliyopo kijijini hapo.

Alifafanua kuwa, kati ya mwaka 2010/2011 kiasi kilichokusanywa na watuhumiwa hao kilikuwa sh. mil 21.3 lakini sh. Milioni  l6.6 zilipotea na hadi sasa hazijulikani zilipokwenda.

Kamanda Paul alisema, watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zinazowakabili.

UNCTAD LAUNCHED ONLINE THE 2012 LEAST DEV. CONTTRIES REPORT (LDCs)


Dear colleagues,
 Today,26 November 2012,the United Nations Conference onTrade and Development(UNCTAD) launched online the 2012 Least Developed Countries Report. This is the only annual report in the United Nations system that exclusively addresses issues related to the 48 least developed countries (LDCs).

This year’s Report, which is subtitled Harnessing Remittances and Diaspora Knowledge to Build Productive Capacities, examines the potential role of migrants, or the diaspora, from LDCs as sources of development finance and channels of knowledge transfer to home countries. In many other developing countries, diasporas also serve as facilitators of trade and market access opportunities in the host countries. The Report assesses whether such opportunities are also open to LDCs that have nationals living and working abroadAttached please find a press release and some background info on the report for your use on your esteemed media channels. Otherwise, the Report itself and the translations of the Overview are available: CLICK HERE

WAANDISHI WALIOKUWA KATIKA ZIARA YA NDUGU KINANA WAREJEA DAR ES SALAAM

Nov 25, 2012

Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib, wakiwa na maofisa wa Chama na Waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuwasili kutoka jijini Arusha kwenye ziara ya kikazi ya  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana. Huyu wa upande wa kulia unamjua?

SHIA DAR WAADHIMISHA SIKU YA KIFO CHA MJUKUU WA MTUME MOHAMMAD (S.A.W).


Pichani Juu na Chini Waumini wa dhehebu la Shia wakiwasili na kukusanyika katika eneo la makaburi ya Washia Kisutu jijini Dar es Salaam wakijiandaa kuanza maandamano ya kuadhimisha siku ya Ashura kukumbuka kifo cha Mjukuu wa Mtume Mohammed (S.A.W) Imam Hussein yaliyofanyika jana.

Mwenyekiti wa Msikiti wa Jamaat Shia Ithna Asheri Bw. Azim Dewji akifafanua kwa waandishi wa habari amesema katika kuadhimisha siku hii Waislam wa dhehebu la Shia watafanya matembezi kutoka makaburi ya Shia Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia Ithna Asheri na wakati wa matembezi hayo ndani yake kutakuwa kunafanyika kumbukumbu kwa njia ya kuimba nyimbo za maombolezo tukikumbuka shujaa wetu namna alivyouwawa na vile vile sisi kujipa uhai kiroho katika kuonyesha namna kiongozi anaweza kujitolea kwa watu wake na kwamba ni funzo kwa kila mwanadamu ajitolee kwa ajili ya wenzake.

Imamu wa Msikiti wa Imam Ali wa Magomeni Mapipa Msabaha Shaaban Ali Mapinga akizungumza na waandishi wa habari amesema siku hii ni siku ya kukumbuka na kuadhimisha miaka 1473 ambapo katika nchi ya Iraq kwenye mji wa Karbala aliuwawa mjukuu wa Mtume Mohammed (S.A.W) aliyekuwa akijulikana kwa jina la Imam Hussein Bin Ali Bin Abutwalib.
Amesema katika nyakati hizo alitokea mtawala dhalim aliyekuwa akitetea dhulma na kukiuka haki za binadamu kitendo ambacho mjukuu wa Mtume Imam Hussein hakukubaliana nacho na kuunda jeshi lake dogo kutetea haki na kupinga Batili.
Kwakuwa Imam Hussein alikuwa na dhamana ya kutetea haki alikataa kuwa chini ya mtawala huo ndipo alipotumiwa jeshi la watu kama 30,000 naye akiwa na jeshi la watu 72 walipambana katika mji huo na mjukuu wa Mtume aliuwawa kifo cha kikatili cha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.

Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema siku hii ni muhimu sana kwa Waislam kote duniani kwa sababu tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo chake kilikuwa ni kifo cha kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso wa ardhi.
Amesema kifo cha Imam Hussein kinamgusa kila Muislam kwa sababu ilikuwa ni siku ambayo haki ilizimwa na dhuluma, maadui wa haki walijaribu kuitaka batil isimame , kwa hiyo siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.
Aidha Sheikh Salum amesema kwa Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni mtetezi wa haki, alikuwa anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba kutetea haki na kutetea uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha ya leo, kutetea wanyonge, kupiga vita Dhuluma na ukandamizaji wa namna yoyote ile ndio lililokuwa jambo alilolipenda Imam Hussein.

Waumini hao wakiwa wamejipanga tayari kuanza maadamano kutoka makaburi ya Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia.

Pichani juu na chini msafara wa waumini wa Shia umeanza.

Hisia na Majonzi vilionekana.

Ni jambo jema watoto kujua dini mapema, kama inavyoonekana pichani mtoto akiwa ameambatana na mzazi wake katika maandamano ya siku ya Ashura.
Bango lenye Ujumbe maalum wa siku ya Ashura.

KINANA AHUTUBIAMAELFU YA WATU GEITA JIONI HII

Nov 23, 2012

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa mpira mjini Geita, akiwa katika ziara ya mikoa minne kwa ajili kujitambulisha kama Katibu Mkuu mpya, kukagua uhai wa chama. Katika ziara hiyo, Kinana ambaye juzi alikuwa Mtwara, jana akawa Rukwa na leo mkoani Geita, kesho atamaliza ziara yake mkoani Arusha.

ZIARA YA DK. SHEIN VIETNAM

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto)m akizungumza na Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi Nguyen Thi Doan,alipofika Ikulu kwa Mazungumzo ya Uhusiano na Mashirikiano baina pande mbili hizo,Rais akiwa katika ziara maalum ya kiserikali nchini humo,[Picha na Ramadhan Othman Vietnam.]

KINANA ATUA TABORA KWA MUDA AKITOKEA RUKWA KWENDA GEITA ASUBUHI HII

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikaribishwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa baada ya kutua kwa muda mkoani hapo akiwa njiani kutoka Rukwa kwenda Geita asubuhi hii. pamoja naye ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu wa  NEC Oganaizesheni Muhammed Seif Khatib na Naibu Waziri TAMISEMI Aggrey Mwanri
 Kinana akimsalimia Mkuu wa wilaya ya Uyui Lucy Mayenga baada ya kutua kwa muda mkoani Tabora. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwasa
Mwassa bakitoa maelezo kwa Katibu Mkuu kwenye chumba cha mapumziko. Kinana akipumzika hapo kwa dakika 30 kabla ya kuondoka kwenda Geita kuendelea na ziara ya kikazi

KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TU


TFF itakuwa na mkutano na waandishi wa habari LEO siku ya Ijumaa (Novemba 23, 2012)
Muda: Saa 7.30 mchana
Mahali: Ukumbi wa Mikutano TFF

ZIARA YA KINANA MKOANI RUKWA

Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Chipukuizi wa CCM, wakati wa mapokezi yake kwenye Uwanja wa Ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa,jana. Wengine ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa Aggry Mwanri ambao wapo katika ziara hiyo.

VODACOM YAICHANGIA HOSPITALI YA CCBRT SH. BILIONI NANE

Nov 20, 2012

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikweteakionesha cheki ya Shilingi bilioni Nane iliyotolewa na Kampuni ya VODACOM kwa ajili ya ujenzi wa hospitali maalumu itakayo shughulika kutibu wanawake walioathirika na Ugonjwa wa Fistula pamoja na ulemavu mwingine.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe.Janet Mbene,Mkurugenzi Mtendaji VODACOM Tanzania Bwana Rene Meza,Ofisa mtendaji Mkuu Hospitali ya CCBRT Bwana Telemans  Erwin na kulia ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik(picha na Freddy Maro)

MAONYESHO YA VIFAA VYA UJENZI NA SAMANI ZA NDANI YAFUNGWA RASMI JIJINI DAR

Afisa uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile (wa pili kushoto) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko (wa pili kulia) kugawa vyeti kwa washiriki sambambamba na kufunga Maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za ndani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Building and Home Improvement EXPO 2012 Bw. Zakaria Malcom ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko akizungumza na washiriki wa maonyesho hayo kabla ya kugawa vyeti na kisha kuyafunga rasmi ambapo amewataka washiriki kuwasilisha Profile za makampuni yao katika mamlaka husika pamoja na kushiriki maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Saba saba yatakayofanyika mwakani. Pia amewataka washiriki kujijengea utamaduni wa kuzunguka katika maduka mbalimbali yanayouza vifaa vya ujenzi na samani za ndani kuangalia ubora wa bidhaa ili kugundua iwapo zinachakachuliwa na wafanyabiashara wa kigeni na kuwaasa kuongeza ubora wa bidhaa wanazozitengeneza kuwa na kiwango cha kimataifa ili kwa kushirikiana na mamlaka yake waweze kupata soko nje ya nchi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Alredha Lighting wanaopatikana Mkabala na Shoppers Plaza Mikocheni Bw. Riyaz Jetha akipokea cheti cha ushiriki bora katika maonyesho hayo kutoka kwa Bi. Jacqueline Mneney Maleko.
Pichani Juu na Chini baadhi ya washiriki wa maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za ndani wakipokea vyeti vyao vya ushiriki bora.
Mwakilishi wa Kampuni ya Masoko na Matangazo ya Advent Promotions Nassara Peter akipokea cheti.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa maoneysho hayo. Kulia ni Meneja Mauzo Afrika Mashariki wa Kampuni ya Alredha Lighting Bw. Mohammed Mustafa na Katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Masoko na Matangazo ya Advent Promotions Nassara Peter.
Meneja Mauzo Afrika Mashariki wa Kampuni ya Alredha Lighting Bw. Mohammed Mustafa akionyesha uimara wa moja ya bidhaa zinazopatikana katika duka la Alredha Lighting.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wa Maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za Ndani yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kufungwa jana. Maonyesho hayo yaliyodumu kwa siku tatu yaliandaliwa na Kampuni ya Tanzania Building and Home Improvement EXPO 2012.

TUME YA AJALI YA MELI YA SKAGIT YATOKA LEO

Nov 19, 2012


ZANZIBAR, TANZANIA
Tume iliyoundwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuchunguza ajali ya meli ya MV. Skagit iliyotokea tarehe 18.7.2012 ilipokuwa ikitokea Dare s Salaam kwenda Zanzibar imependekeza kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu watu saba kwa makosa mbali mbali yaliyochangia kutokea kwa ajali hiyo ili kuhakikisha kunakuwepo uwajibikaji kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa baharini na watendaji wa Taasisi zinazosimamia suala hilo na kuepusha ajali za mara kwa mara.

Akitoa taarifa ya Tume hiyo kwa Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Mnazimmoja, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee amewataja watu waliopendekezwa kuchukuliwa hatua za kisheria ni mmiliki wa MV.Skagit ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa  Kampuni ya Seagull Sea Transport Said Abdul-rahman Juma, Nahodha wa meli hiyo Makame Mussa Makame na Meneja wa Kampuni hiyo tawi la Dar es salaam Omar Hassan Mkonje.

Amesema kutokana na matendo yao ya kuwa karibu mno na sababu zilizopelekea kutokea kwa ajali hiyo, Tume imependekeza watu hao washtakiwe kwa kosa la kusababisha vifo kutokana na uzembe.

Mmiliki wa kampuni hiyo amefanya kosa la  kufanya biashara ya usafiri wa baharini kwa kutumia chombo ambacho hakikusajiliwa kwa mujibu wa sheria na kutumia chombo ambacho hakikutimiza masharti ya ukaguzi kwa mujibu wa sheria ya usafiri wa baharini Zanzibar namba 5 ya mwaka 2006, kumuajiri nahodha bila ya kuwa na cheti cha umahiri cha daraja la tano  na kuruhusu meli kupakia idadi kubwa ya abiria kinyume na uwezo wake.

Abdulhamid amesema taarifa hiyo imesema Nahodha Makame Mussa ametenda kosa la kuendesha meli akiwa hana cheti, kushindwa kuwaandaa abiria  kujiokoa wala kutoa taarifa ya dharura, kuendesha meli hali ya kuwa si salama na kuruhusu kupakia abiria 431 badala ya 250 iliyoainishwa kwenye cheti cha abiria.

Watu  waliopendekezwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni  aliekuwa Mkaguzi wa meli na Kaimu Mrajisi wa meli kutoka Mamlaka ya usafiri wa baharini Zanzibar Juma Seif Juma, Mkaguzi wa kujitegemea Capt. Saad Shafi Adam na Maafisa wa usalama wa bandari ya Dar es Salaam Johari Mikidadi  Ndumbati na Peter Ndimbwa Mwasi kwa kushindwa kudhibiti uingizaji wa abiria katika meli ya MV. Skagit siku iliyopata ajali ikiwa ni kinyume na majukumu yao ya kazi.

Taarifa hiyo imetoa mapendekezo ya kuimarisha Sheria na kanuni za usafiri wa baharini namba 5 ya 2006 kwa kuvifanyia marekebisho baadhi ya vifungu ikiwemo kuweka utaratibu wa kisheria utakaowalazimisha wafanyabiashara wa usafiri wa baharini kuwa na utaratibu wa kuuza tiket za safari pamoja na kutengeneza urodha ya wasafiri kwa njia ya electroniki na kuweka utaratibu wa kisheria unaowalazimisha uongozi wa kampuni unaoendesha biashara ya usafiri wa baharini kuwa na taaluma ya masuala ya usafiri wa baharini.

Aidha Abdulhamid amesema Tume hiyo imependekeza Kampuni kuwalipa fidia abiria wote waliokuwemo ndani ya meli.  Kwa  waliofariki walipwe thamani ya kiwango cha mshahara wa chini cha muda wa miezi 80 na walionusurika na kupata ulemavu walipwe asilima 75 ya kiwango cha waliofariki na watu wengine walionusurika bila ya kupata majeraha yoyote walipwe asilimia 50 ya kiwango   walicholipwa waliofariki.

Katika ajali hiyo watu 81 wakiwemo raia watatu wa kigeni walifariki na maiti zao zilipatikana na kuzikwa,  212 walipotea na 154 waliokolewa wakiwa hai wakiwemo raia 15 wa kigeni.

Katibu Mkuu Kiongozi amesema Tume imeeleza sababu za kutokea ajali hiyo kuwa ni upepo mkali, muundo wa meli ilioruhusu abiria wengi kukaa juu, mwendo wa kasi, nahodha kukosa ujuzi na umahiri na abiria kuwa wengi kupita kiwango chake.

Amesmea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekubaliana na mapendekezo yote yaliyotolewa na Tume hiyo iliyokuwa na wajumbe 10 chini ya mwenyekiti wake Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Abdulhakim Ameir Issa.

VIJANA NCHINI WATAKIWA KUJIFUNZA ELIMU YA UJASIRIAMALI ILI KUONGEZA THAMANI KATIKA KAZI NA BIASHARA


Wahitimu wa Global Entreprenuership Week Tanzania katika picha  pamoja na mgeni rasmi na wawezeshaji. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU JACKSON MAKWETA

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo ya marehemu Jackson Makweta, nyumbanikwa marehemu, Boko jijini Dar es salaam Novemba 19, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole mjane wa marehemu Jackson Makweta,Mwhuvila Makweta, nyumbani kwa Marehemu, Boko jijini Dar es salaam Novemba 19, 2012.
ยช