.

RAIS KIKWETE AZINDUA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI ILIYOFANYIKA TANZANIA MAPEMA MWAKA 2012

Dec 31, 2012

Hii ndiyo idadi ambayo imetangazwa na Rais Jakaya Kikwete leo kwenye uzinduzi matokeo ya Sensa iliyofanyika nchini kote mapema mwaka huu (2012)
 Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya kutangaza rasmi uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Rais Jakaya, alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12, 313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama hiyo ilifanyika tena mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012, ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44, 929,002. 
 Baadhi ya Madiwani na viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo leo.
 Kikundi cha Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kilichokuwa kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
 Bendi ya THT, kutoka (kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
 Wananchi wakisebeneka kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya Sensa.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi matokeo ya Sensa ya watu na makazi.

DK. SHEIN ATOA SALAM ZA MWAKA MPYA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk Ali Mohamed Shein, akitoa salamu za kuukaribisha Mwaka mpya wa 2013,kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote kwa ujumla,pia aliwasihi wananchi kuendela kushirikiana   na Serikali yao katika kuendeleza mipango mbali mbali ya maendeleo,na kuwataka kuwa walinzi wa rasilimali pia kuzingatia taratibu za kisheria, kwa kuwa na elimu bora ya rasilimali hizo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

HABARI KATIKA MAGAZETI LEO SIKU YA KUFUNGA MWAKA WA 2012

BABA WA PINDA ALAZWA MUHIMBILI

POLE BABA: Waziri Mkuu Mizengo Pinda akmjulia hali jana jioni, Baba yake mzazi Mzee Savere Kayanza Pinda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili   kitengo cha Moi, Dar es Salaam. Mzee Mizengo yupo hospitalini hapo baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo la nyonga. Kulia kwa waziri mkuu ni Muguzi wa zamu, Edna Mhina  na kushoto kwa waziri mkuu ni  Donatila Kwelukila ambaye ni Ofisa uguzi chumba cha wagonjwa mahututi  MOI, (Picha na Chris Mfinanga)

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MZEE MOHAMED ABOUD MOHAMED

Dec 30, 2012

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib  Bilali, Makamu wa Pili wa Rais Wa Znzibar Balozi Seif Iddi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 30, 2012.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 20, 2012. PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AMJULIA HALI PADRI MKENDA

POLE SANA:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsalimia Padri Ambrose Mkenda, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, leo Desemba 30, 2012 aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kujeruhiwa na risasi na watu wasiojulikana wakati akiwa getini akisubiri kuingia nyumbani kwake mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia ni Muuguzi mwangalizi wa mgonjwa huyo, Namsifu Fue. Picha na OMR

MSAMA ASAIDIA YATIMA

 Baadhi ya watoto wanaolelewa katika Kituo cha Mwendaliwa. 
  Baadhi ya watoto wanaolelewa katika Kituo cha Mwendaliwa. 
Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani  akizungumza waandishi wa habari kuhusu historia ya kituo chake.
 Kituo cha Mwendaliwa
  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani. Mbali ya kukabidhi vyakula hivyo, Msama pia alikabidhi hundi ya sh milioni 1.5 kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Msaada huo  umetokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
 Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
 Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
 Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
 Baadhi ya watoto wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 1.5 Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Mbali ya kukabidhi hundi, Msama alikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vikiwa na thamani ya sh milioni 3 zilizotokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani akimuonesha moja ya vyumba vinavyotumiwa na watoto hao.
 Alex Msama akipata maelezo katika chumba maalum kwa ajili ya watoto kujifunza kushona. 
Dua ya kumshukuru mungu ikisomwa.

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI PADRI AMBROS MKENDA ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR

 POLE SANA: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali  Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.
TUKIO LENYEWE LILIKUWA HIVI: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka. PICHA NA IKULU

KUTOKA BAADHI YA MAGAZETI JUMAPILI YA LEO YA MWISHO KWA MWAKA WA 2012
ยช