.

KINANA AFANYA ZIARA YA KIBONDO KWA VITENDO ZAIDI

Jan 31, 2013

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo amedhihirisha kuwa ni mtu wa vitendo zadi kuliko maneno, baada ya kuonyesha uwezo wake wa kufanya kazi za kijamii kwa umahiri mkubwa, kwa kushiriki katika ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya Sekondari Kumwambo   na ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Bunyambo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, ambayo ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma. Pichani Kinana akishiriki ujenzi wa darasa katika shule ya sekondari Kumwambo, Kibondo
 Kinana akiongoza ujenzi wa chumba cha darasa kwenye shule ya sekondari Kumwambo. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Abdallah Bulembo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Walid Kaborou
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananfunzi wa shule hiyo baada ya kushiriki ujenzi huo. Baadaye Kinana alienda na msafara wake Kijiji cha Bunyambo ambako pia alishiriki ujenzi wa Ofisi ya tawi la CCM na kuahidi kuwapa sh. milioni 2 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi.
 Kinana akiongoza ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Bunyambo, wilayani Kibondo mkoani Kigoma
 Kinana akihakiki kwa kipimo wakati akiendelea na ujenzi kwenye ofisi hiyo ya CCM. Kulia ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Stanley Mkandawile
 Kinana akiendelea na ujenzi kwenye Ofisi hiyo ya CCM
 Kinana akitazama kama tofali limekaa sawa, wakati akishiriki kujenga Ofisi hiyo ya CCM

 LETE TOFALI: Anasema Kinana kumwabia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Kaborou wakati akiendelea kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM
Kisha Kinana akawaaga wananchi waliohudhuria kwenye Ujenzi wa Ofisi hiyo
Katibu Mkuu wa CCM (kushoto) na ujumbe wake wakichagua miwa kwa muuzaji waliyemkuta njiani wakati wakitemebea kwa mguu kiasi cha kilometa moja na nusu kwenda kwenye mkutano wa hadhara baada ya ujenzi huo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)

MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZI WA TFF NA TPL BOARD


Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi kama ifuatavyo:

1.                   Waombaji uongozi wa TPL Board


(a)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeid anayeomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na  Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:

(i)                   Si Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii)                 Si mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi  hiyo.


(b)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa  na  Ndg. Daniel T. Kamna na  Ndg. Juma Ally Magoma walioomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali Manji :

(i)                   Hana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) wa uendeshaji wa mpira wa miguu.
(ii)                 Hana sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(iii)                Hana elimu ya kidato cha nne
(iv)               Ameshindwa kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6), 18(1)b, 27 (2) na (5).

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma hazikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.  

(c)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg.  Hamad Yahya Juma, kwamba Ndg. Hamad Yahya Juma:

(i)                   Si Mwenyekiti wa Klabu ya Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii)                 Si mkweli na mwadilifu na amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa klabu.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi ya Ndg. Frank M. Mchaki kwa kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake haikukidhi matakwa  ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.

2.                   Waombaji uongozi wa TFF


(a)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani K. Kambi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi aliwekewa pingamizi kwamba amefanya Kampeni kabla ya muda uliopangwa.

Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi.


(b)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Eliud P. Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella aliwekewa pingamizi na Ndg. Said Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter Naminga, kwamba Ndg. Mvella:

(i)                   Akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa kuleta maendeleo ya soka katika ukanda huo.
(j)                   Ana kesi ya rushwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa

Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.

(c)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Epaphra Swai anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie Chalamila, kwamba Ndg. Epaphra Swai:

(i)                   Alifanya ubadhilifu wa fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA).
(ii)                 Alitumia madaraka yake vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.
(iii)                Alivunja Katiba ya MZFA na FIFA
(iv)               Anavuruga shughuli za uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa wawekaji pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na vielelezo vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya hila na udanganyifu (collusion) dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) na hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.

(d)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Vedastus F.K Lufano na Ndg. Mugisha Galibona wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg. Galibona waliwekewa pingamizi  na Ndg. Paul Mhangwa kwamba  hawana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu wa miaka mitano (5).

Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).


(e)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Michael R. Wambura anayeomba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg. Josea Samuel Msengi kwamba Ndg. Wambura:

(i)                   Alikiuka Katiba ya TFF kwa kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu masuala ya uchaguzi.
(ii)                 Alikosa uadilifu kwa kutumia kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi aliyokuwa aniongoza akiwa Katibu Mkuu wa FAT.
(iii)                Amekuwa akijaribu kupotosha umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake kwa kutumia haki na kuviita ‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo Courts).
(iv)               Mwaka 2004 alikiri kwamba alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari kwa kuwa alikuwa akivipa pesa na kwamba vyombo vya habari vilimgeuka kwa sababu aliacha kuwapa waandishi pesa.
(v)                 Mwaka 2004 alikataa kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu Mkuu wa FAT iwe ya kuajiliwa.
(vi)               Alikosa uwezo wa kutekeleza wajibu na malengo ya TFF.

Ndg. Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg. Wambura. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Said Rubea Tamim kwa kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).

(f)                  Pingamizi dhidi ya Ndg. Jamal E. Malinzi anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF; Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape Fue kwamba:

(i)                   Alivunja Katiba ya TFF kwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa wanachama wa TFF kikiwemo Chama chake cha Mkoa wa Kagera haviheshimu wala kutekeleza maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na FIFA baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba kwa njia ya Waraka, ambayo yalihusisha pia  maagizo ya FIFA na CAF
(ii)                 Hana sifa ya uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
(iii)                Anakosa uadilifu na haiba ya kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.


Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Agape Fue kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi hilo.

(g)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na  Ndg. Mintanga Yusuph Gacha na Ndg. Medard Justiniani kwamba:

(i)                   Ni Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni mtumishi wa umma hivyo alikosa kigezo na sifa ya kugombea nafasi ya urais wa TFF.
(ii)                 Anakatazwa na Judicial Service Act, Public Service Act 2002 na Code of Conduct for Judicial Officers of Tanzania kugombea nafasi aliyoomba ya Rais wa TFF.
(iii)                Kutakuwa na Mgoganao wa kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais wa TFF.
(iv)               Amekosa umakini na uadilifu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha Akanunti za TFF kufungiwa na TRA.

Ndg. Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo halikujadiliwa na Kamati. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Medard Justiniani kwa kuwa alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa alikuwa na ufahamu wa kutosha wa pingamizi lake ikiwa ni pamoja na viambatanisho vyake, hali iliyotanabaisha kuwa pingamizi hilo lilikuwa na chembechembe nyingi za hila na udanganyifu.Angetile Osiah
KATIBU
KAMATI YA UCHAGUZI

KAMPUNI YA BE FORWARD YAKABIDHI ZAWADI YA GARI KWA MTEJA WAO ALIYESHINDA ‘PHOTO CONTEST’


Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya magari ya Be Forward Tanzania, Mashariki na Kati Oliver Philbert akizungumzia kuzinduliwa rasmi kwa Kampuni ya Be Forward hapa Tanzania na pia tukio la kampuni hiyo kukabidhi zawadi kubwa ya gari kwa mmoja wa wateja wake kutoka Uganda aliyeibuka mshindi wa shindano la photo contest..
Amesema Be Forward ni kampuni inayojihusisha na uuzaji magari nchini Japan kwa njia ya mtandao wa Internet, na ili kuongeza ufanisi na Imani kwa wateja wetu tumefungua kampuni Tanzania ambayo inajishughulisha na huduma kwa wateja.
Be forward Tanzania itatengeneza ajira zaidi ya 1,000 kwa watanzania hivyo kuipunguzia mzigo serikali na kuongeza kipato kwa watanzania.
Kampuni hiyo iliendesha ‘Photo Contest’ ambapo wateja wake walitakiwa kutuma picha za magari walionunua kutoka katika kampuni hiyo, na kisha ziliwekwa katika mtandao wa Be Forward na katika ‘Kurasa yao ya Facebook na watu kuzi’like’.

Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akizungumza machache ambapo amewataka watanzania kujisikia huru kufika na kufanya kazi na kampuni hiyo, pia amempongeza mteja wao kutoka Uganda aliyeibuka kuwa mshindi wa zawadi ya gari na kuahidi kuwa wanafanya maandalizi ya kuendesha kitu kingine tena kwa ajili ya wateja wao.

Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akimkabidhi mfano wa funguo ya gari Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan (kushoto).

Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan akitoa shukrani kwa washiriki wote wa nchi mbalimbali walioshiriki na hatimaye yeye kuwa 

Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa ( wa pili kulia) na baadhi ya wageni waalikwa wakimsikiliza mshindi wa shindano hilo Bw. Kakuru Adnan (hayupo pichani) wakati wakati akitoa shukrani zake kwa kampuni hiyo.

Pichani Juu na Chini ni Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akikabidhi zawadi kwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa (wa pili kushoto waliochuchuma) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ofisi ya Tanzania na wageni waalikwa.

Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akimkabidhi rasmi mshindi wa shindano la picha ambaye pia ni mteja wa kampuni hiyo gari aina ya Toyota Corolla Bw. Kakuru Adnan kutoka nchini Uganda.

Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni hiyo pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo na idara mbalimbali za kampuni hiyo kutoka nchini Japan.
Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ofisi za Tanzania na wa makao makuu nchini Japan.

Bw. Kakuru Adnan akitoa tabasamu bashasha baada ya kuliwasha gari hilo.

Hili ndio gari aina ya Toyota Corolla alilozawadiwa mshindi huyo Bw. Kakuru Adnan.

TAASISI YA THE JOHN MASHAKA YAWAKUTANISHA WAANDISHI NA WATU WENYE ULEMAVU KUJADILI CHANGAMOTO MBALIMBALI


Katibu wa Taasisi ya The john mashaka Bi, Rabia Bakari akiungumza kwa ajili ya kufungua mkutano wa waandishi wa habari na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu ili kujadili kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa wenye ulemavu na wengine wasiojiweza.

Baadhi ya watu wanaotafsili lugha za alama wakiendelea na kazi hiyo wakati wa mkutano

Baadhi ya wawakilishi wakisikiliza kwa makini

Mwenyekiti wa TUSPO Bw. E LLEZER Mdakima kushoto akizungumza wakati wa mkutano huo wengine kulia ni Mjumbe wa Taasisi ya The John Mashaka Bi, Latifa Masasi na Katibu wa taasisi hiyo Bi, Rabia Bakari picha na www.burudan.blogspot.com

KINANA AINGIA KIBONDO KWA KISHINDO

 Wananchi wa Kijiji cha Kilemba wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wakiserebuka kwa ngoma mbele ya Katibu Mkuu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake, alipoowasili kwenye kijiji hicho nje kidogo ya mji mdogo wa Kibondo leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Bulembo na watatu ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou.
 Msafara wa Kinana ukiingia mjini Kibondo kwa shamrashamra za aina yake. (PICHA NA BASHIR NKOROMO)

MATUKIO KIGOMA

 Mtoto akitafuta wateja wa miwa kwenye stesheni ya Kazutramimba mkoani Kigoma, hivi karibuni
 Ally Bikulako mkazi wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, akiwa katika kazi ya ufundi wa kuchora bango la shule ya sekondari ya Nguruka, hivi karibuni.
 Mamalishe wakiwa kazini katika kijiji cha Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma hivi karibuni.
 Mafundi wakiwa katika ujenzi wa nyumba ya kisasa katika Kijiji cha Kasanda, wilayani Kakonko mkoani Kigoma juzi.
 Watoto wakichota maji safi ya bomba kwenye kijiji cha Nyabibuye, Kakonko mkoani Kigoma jana.
 Belitha Anthoy wa Kijiji cha Lumashi, Kata ya Nyabibuye, Kakonko mkoani Kigoma akichoma mahindi, nyumbani kwao, jana. Huu ni msimu wa mahindi mabichi Kigoma
 Mtoto akiswaga mbuzi aliokuwa anachunga katika kijiji cha Malagarasi, wilayani Uvinza mkoani Kigoma, juzi.

PINDA: MTWARA CORRIDOR KUPEWA UZITO WA PEKEE


DODOMA, TANZANIA 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda (pichani) amesema Serikali italipa uzito wa kipekee suala la uendelezaji wa Ukanda wa Kiuchumi wa Mtwara (Mtwara Corridor) kama ilivyo kwa Ukanda wa Kilimo wa Nyanda za Juu Kusini Tanzania (SAGCOT).

Amesema Serikali itachukua hatua hiyo ili kuiendeleza kiuchumi mikoa ya kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Ametoa kauli hiyo Jumanne, Januari 30, 2013) mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ili kutoa ufafanuzi juu ya suala alilokwenda kufuatilia mkoani Mtwara kufuatia vurugu zilizozuka hivi karibuni kuhusiana na suala la uchimbaji gesi mkoani humo.

Mbali na hilo, Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha Wizara ambazo zinawajibika kutoa maelezo kuhusu uwekezaji na uendelezwaji wa miradi mkoani Mtwara zinaweka ratiba maalum ya kwenda huko na kutoa maelezo ya kina kwa wananchi.

Alitumi fursa hiyo kuwasihi wakazi wa mkoa huo kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinaimarishwa kama kweli wanataka mkoa huo uendelezwe.

“Ninawasihi wakazi wa Mtwara waimarishe amani na utulivu sababu fursa walizonazo ni kubwa sana. Ni vizuri viongozi na wananchi wa mkoa huo wakajipanga vizuri ili waangalie namna watakavyonufaika na uwekezaji huo,” alisema.

Akifafanua kuhusu mgogoro uliosababisha vurugu hizo, Waziri alisema katika muda wa siku mbili alizokuwa Mtwara aliweza kukutana na vikundi tisa vilivyojumuisha viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, madiwani, wafanyabiashara na vyombo vya dola.

Alisema baada ya kusikiliza pande zote, Waziri Mkuu aliwaita mawaziri wa Elimu, Uchukuzi, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Viwanda na Biashara na Kaimu Mkurugenzi wa TIC ili watoe ufafanuzi kwenye kikao cha majumuisho ambacho kilifanyika jana (Jumanne, Januari 29, 2013) mjini Mtwara.

“Ni bahati mbaya hali ilikuwa hivyo. Ni jambo ambalo lisingetakiwa kufika hapo. Ni bahati mbaya kwamba elimu kuhusu uwekezaji mkoani Mtwara haikuwa imefika kwa wananchi walio wengi, ni wananchi wachache waliofikiwa wakati wa kutoa taarifa. Wabunge walijua jambo hili na walikuwa na wajibu wa kuwaelimisha wananchi…,” alisema.

Waziri Mkuu alisema hoja kuu iliyotolewa na wakazi hao ni kwamba walikuwa hawapingi gesi kwenda Dar es Salaam isipokuwa walikuwa wakitaka kijengwe kiwanda cha kusafisha gesi pale Mtwara ili mabaki yanayotokana na usafishaji huo yatumike palepale mkoani kutengenezea bidhaa nyingine kama vile mbolea na vifaa vya plastiki.

Akielezea kuhusu hasara zilizosababishwa na vurugu hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi alisema nyumba, ofisi na magari vilichomwa moto katika sakata hilo lililohusisha wilaya za Mtwara na Masasi Januari 25 na 26 mwaka huu.

Alibainisha kwamba kwa wilaya ya Masasi pekee gharama za kurekebisha uharibifu huo zinafikia sh. bilioni 1.5/-. Hata hivyo, alisema gharama halisi za uharibifu uliotokea kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara pamoja na Manispaa ya Mtwara hazikuweza kupatikana kwa haraka.

RAIS KIKWETE AMTEUA NYAMBACHA KUWA KAMISHNA JENERALI WA ZIMAMOTO TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini.

Taarifa iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.                                      

RAIS KABILA YUPO TANZANIA, AKUTANA NA RAIS KIKWETE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jioni  ya Januari 30. 2013

ZIARA YA KINANA WILAYANI KAKONKO, KIGOMA

Jan 30, 2013

 Wananchi wa rika zote wa Kijiji cha Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilayani Kakonko, Kigoma wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahma Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Januari 30, 2013,katika  kijiji hicho, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilaya ya Kakonko mkoani  Kigoma, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua soko la Kata ya Nyabibuye, Kakonko leo Januari 30, 2013, ikiwa ni ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma. Kushoto ni diwani wa kata hiyo Steven Mnigakiko na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kakonko Peter Toima.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa daraja la Umoja linalounganisha Kata ya Nyabibuye, Kakonko na vijiji jirani vya Burundi. alipokuwa katika ziara wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Januari 30, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
 Kinana na ujumbe wake wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa daraja hilo
 Ujenzi wa daraja hilo umefikia hapa
 Maelezo ya mradi wa ujenzi wa daraja hilo
 Kinana akipanda mti kwenye shule ya sekondari ya Nyamtukuza, katika Kata ya Nyabibuye wilayani  Kakonko mkoani Kigoma. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Amani Ntibakiza
 Wanafunzi wa shule hiyo wakisomba mawe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo, alipofika kwa ajili ya kushiriki ujenzi wa nyumba ya walimu. Pia Kinana ameahidi kuipa shule, Mashine mbili za umeme wa Solar na kompyuta.
 Kinana akiwasalimia wanafunzi wa shule hiyoKinana akishiriki kusomba mawe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu katika shule hiyo
ยช