.

MANGULA AKUTANA NA MSAIDIZI WA RAIS WA SUDAN LEO

Feb 28, 2013

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula (kushotio) akiagana na mgeni wake, Nafie Ali Nafie, Msaidizi wa Rais wa Sudan, baada ya mazungumzo yao leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

YANGA YAIKAMUA KAGERA SUGAR BAO 1-0 JIONI HII

Feb 27, 2013

PICHA ZA MECHI HIYO INGIA UKURASA WETU WA SPOTI AU BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE AKAGUA UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO WA KIMATAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Feb 26, 2013

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall' uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali (picha na Freddy Maro)

MeTL GROUP YAPATA TUZO


Mkurugenzi kutoka taasisi ya Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya Superbrands wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya tuzo za ubora na thamani ya nembo kwa makampuni bora 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki Jawad Jaffer akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Raha Aashiq Sharrif (Kulia) akiwa Mwakilishi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Raha Preetkamal Bansal ( wa pili kulia) wakati wa hafla fupi ya Superbrands kukabidhi vyeti kwa makampuni bora kwa mwaka 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhaville ( wa pili kulia) aliyembatana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP Bi. Joyce Luhanga ( wa tatu kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo iliyoendeshwa na Taasisi ya Superbrands.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.

RAIS KIKWETE AMTEUA JAJI MSUMI KUWA MWENYEKITI BARAZA LA MAADILI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji na Balozi Mstaafu Mheshimiwa Hamis Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa BARAZA LA MAADILI.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, 26 Februari, 2013 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Februari 18, mwaka huu, 2013.

WANNE WADAKWA TUKUYU,WAKIIBA KWENYE ATM ZA NMB

Benki ya NMB inazidi kuwa katika balaa baya na la kutia hofu kwa usalama wa fedha za wateja. Taarifa zinasema  Watu wanne wamekamatwa wakiwa na kadi za ATM 150 za NMB kwenye tawi la Tukuyu mkoani Mbeya. Inadaiwa tayari walishakwapua milioni sh. 20. Wenye account huko kuweni makini. Chanzo-Radio One breaking news

MISUMARI INAPOUZWA PAMOJA NA VYAKULA DUKANI

TEMBEA UONE! Wadau hivi karibu mwenzenu nilishangaa kukuta misumari (kushoto) ikiuzwa pamoja na bidhaa za kula kama haya maharage kwenye duka moja lililopo mji wa Kikwetu, wilaya ya Lindi mjini hivi karibuni. Je, hii si hatari? Maana mteja anaweza kutahamaki amepika mseto wa maharage na misumari iliyoingia kwa bahati mbaya wakati mwenye duka anampimia kwenye mzani!

BAADHI YA MAGAZETI LEO


 

JW WAWILI WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI ZA MABARANI MOROGORO

Feb 25, 2013


MOROGORO,Tanzania
ASKARI wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari mkoani Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Faustine Shilogile amesema leo kuwa tukio la kwanza la ajali ilitokea jana, saa 12 asubuhi katika eneo la Kambi ya Jeshi ya Mikumi iliyopo wilayani Kilosa.

Amesema ajali hiyo ilihusisha gari lisilofahamika namba wala dereva wake, kutokana na dereva kutimka na gari lake baada ya ajali hiyo wakati gari likitokea Ruaha kwenda Mikumi.

Kamanda amesema gari hilo lilimgonga askari MT 76810 Koplo Deogratius Lulakuze (37) ambaye alikuwa ni askari wa JWTZ kikosi namba SUUK-KJ mikumi na kufariki dunia papo hapo.

Katika tukio la pili askari wa JWTZ Boniface Nathaniel (29) mkazi wa jijini Dar es salaam, aligongwa na gari wakati akiendesha pikipiki kwenye barabara Mikumi iendayo Kilombero mkoani hapa.

Kamanda Shilogile amesema, ajali hiyo ilitokea juzi, saa 3 asubuhi katika daraja la Jeshi la wilaya ya Kilosa mkoani hapa.

Alisema kuwa askari huyo aligongwa na gari T 233 CDT lililokuwa na tela lenye namba T 687 CGE aina ya Scania lililokuwa likitokea Kilombero kwenda Mbeya likiendeshwa na Ismail Kunga (53) mkazi Tabata jijini DSM.

Alisema, gari hilo liligongana na pikipiki lenye namba T424 BYU aina ya Lantic lililokuwa likiendeshwa na askari huyo na kusababisha kifo chake papo hapo na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha pikipiki huyo kuzidi upande wa kulia zaidi wa barabara hiyo.

BALOZI WA MSUMBIJI KUJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN,LEO


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Msumbiji nchini Tanzania Dr.Vicente Mebunia Veloso,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili  ya kujitambulisha kwa Rais, leo.[Picha na Ramadhan Othman,IKulu.]

DHL EXPRESS TRIPLES ITS NETWORK IN SUB-SAHARAN AFRICA


DHL Express has expanded its network of DHL Service Points in Sub-Saharan Africa from the initial 300 to over 1000, in just a few short months
CAPE-TOWN, South-Africa, February 25, 2013/African Press Organization (APO)/ 
•    Express company expands footprint from 300 to more than 1,000 DHL Service Points within six months
•    DHL expands its role of connecting Africa with over 220 countries worldwide
DHL Express (http://www.dhl.com), the world’s leading international express services provider, has expanded its network of DHL Service Points in Sub-Saharan Africa from the initial 300 to over 1000, in just a few short months. The move is an aggressive expansion into the market which is aimed to further cement the company’s leading position in Africa but also to offer local consumers and small businesses an efficient, convenient way of shipping overseas.
The logistics and express company, which is present in 52 Sub-Saharan Africa markets, has been looking to improve access for cash and account customers, creating enhanced accessibility for customers and increasing connectivity between African markets and the over 220 countries that DHL currently serves worldwide.
“In our recent 2012 Global Connectedness Index, which measures the state of globalization around the world, Sub-Saharan Africa remained the globe’s least connected continent,” comments Charles Brewer, Managing Director for DHL Express Sub-Saharan Africa. “However, it did average the largest increase from 2010 to 2011 and boasted the top five ‘gainers’ – Mozambique, Togo, Ghana, Guinea and Zambia. This tells us that there is still major opportunity to improve connectivity across the continent, and access to logistics services and international markets are both key to this improvement.”
The logistics operator had also identified the need for increased convenience for small to medium enterprises (SMEs), as a recent study by global information and analytics company, IHS, showed that accessibility to international markets was a driver of small business success. “The SME is sector is growing at an amazing pace and this investment will help to connect African SME’s to the rest of the world,” notes Brewer.
The drive to increase consumer access points has been as a result of a multi-pronged retail strategy which looks at retail offerings from a small spaza shop in South Africa to a telecommunications company in Angola or a post office in Mauritius.
“Africa is a complex market to operate in but we’ve proven that, with a bit of creativity, you can expand your footprint and provide a way to service the continent’s growth,” concludes Brewer. “Ensuring the people within Africa can access global markets, and transfer skills, goods and information, means we are able to support and spur on the continued African resurgence. Expanding our retail presence is just the first step.”
Distributed by the African Press Organization on behalf of Deutsche Post DHL.
Media Contact:
Lee Nelson
Head: Advertising and Public Relations, Sub-Saharan Africa
DHL Express
Tel +27 21 409 3613 Mobile +27 72 361 0178
DHL – The Logistics company for the world
DHL (http://www.dhl.com) is the global market leader in the logistics industry and “The Logistics company for the world”. DHL commits its expertise in international express, air and ocean freight, road and rail transportation, contract logistics and international mail services to its customers. A global network composed of more than 220 countries and territories and about 275,000 employees worldwide offers customers superior service quality and local knowledge to satisfy their supply chain requirements. DHL accepts its social responsibility by supporting climate protection, disaster management and education.
DHL is part of Deutsche Post DHL. The Group generated revenue of 53 billion euros in 2011.
SOURCE
Deutsche Post DHL

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA BABA WA RAIS MUSEVENI WA UGANDA


 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akimpa pole Rais Yoweri Kaguta Museveni kutokana na kifo cha Baba yake Mzee Amos Kaguta, katika kijiji cha Rwakitura nchini humo.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akifariji mke wa Rais wa Uganda Mama Janet Museveni kufuatia kifo cha Baba wa Rais Museveni Mzee Amos Kaguta. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua juu ya jeneza la Marehemu Mzee Amos Kaguta(97),Baba Mzazi wa Rais Wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijiji Cha Rwakitura nchini Uganda.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiweka udongo kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta(97) wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura. PICHA ZOTE NA FREDDY MARO, IKULU

WAMCHOMA MWENZAO NDANI YA NYUMBA KISA UGOMVI WA ARDHI RORYA

Feb 24, 2013


RORYA, Tanzania
Mkazi wa Kijiji cha Ochuna Kata ya Nyathorogo tarafa ya Luo Imbo Wilayani Rorya Mkoani Mara ,Samson Jeremia (49) amefariki dunia baada ya kuchomewa ndani ya nyumba yake usiku na watu wanaosadikiwa kuwa na ugomvi naye kuhusu ardhi.

Katika tukio hilo Prisca Samson (35) ambaye ni mke wa marehemu,alinusurika kwa kuokolewa na majirani akiwa hoi baada ya kuvunja milango ambapo kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Kowak Wilayani Rorya akiwa na majeraha ya kuungua kwa moto mwili mzima.

Kamanda wa Polisi Tarime-Rorya, Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha alisema leo kuwa  tukio hilo limetokea  jana, Februari 23 Usiku nyumbani kwa Samson Jeremia, ambapo ilidaiwa kundi la Watu wanaosadikiwa kuwa na uhasama wa kugombea mashamba walifika na kufanya uhalifu huo wa kuchoma nyumba wakati Samson akiwa amelala na mke wake Prisca.

Alisema, watu hao walifunga milango kwa nje ili wasiweze kutoka nje wauungulie ndani wote, lakini moto ulipokolea mke alipiga Kelele za kuomba msaada huku moshi ukiwa umejaa ndani ya nyumba.

Kamanda Kamugisha alisema kuwa  polisi wamewakamata watu wawili kuhusiana na tukio hilo na kuwataja kuwa ni  Silveri  Abela Anundu (75) na ndugu yake Ezekia Kachula Anundu ( 80) na kwamba polisi waendelea na msako wa kuwapata wengine waliohusika katika Tukio.

AJALI INAPOGEUKA MAAJABU!!!!!!!! Naibu meya  wa Manispaa ya Iringa Gravas Ndaki akishangaa ajali ya karne yenye maajabu makubwa kwa mkoa  wa Iringa  ,ajali  iliyotokea  usiku wa leo eneo la Hoteli ya kati (makosa) au CRDB ya  zamani katika barabara ya Iringa -Dodoma,hakuna majeruhi  wala aliyepoteza maisha 
 Askari  wa usalama barabara  nao  washangaa kuona ajali  kama hii katikati ya mji 
 Mmiliki  wa  gari  aina ya  RAV 4 iliyogonga gari na kulipanda juu akiwa haamini  kilichotokea 
 
 Huyu ndie mmiliki wa RAV4 inasadikika ni mfanyakazi  wa Tanroads mkoa  wa Iringa 
 Dereva  wa Taxi yenye namba  za usajili T 510 AYUKelvin Kaduma akiwa  salama kabisa 
Wazungu ambao  ndio  wanatengeneza magari nao  wakifika  kushangaa ajali  hiyo ya maajabu CHANZO: FRANCIS GODWIN BLOG

STATEMENT BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AT THE SIGNING CEREMONY OF THE PEACE, SECURITY AND COOPERATION FRAMEWORK FOR THE DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO (DRC) AND THE REGION, 24TH FEBRUARY 2013, ADDIS ABABA, ETHIOPIA.

H.E PRESIDENT JAKAYA KIKWETE

Your Excellency Haillemariam Desalegn, Prime Minister of the Federal Democratic Republic Ethiopia and Chairperson of the African Union;
Excellencies Heads of State and Government;
Your Excellency Ban Ki-moon, Secretary General of the United Nations;
Your Excellency Dr. Nkosazan Dlamin Zuma, Chairperson of the African Union Commission;
Invited Guests;
Ladies and Gentlemen.
This is a very auspicious and historic day for the people of the Democratic Republic of Congo, her neighbours and the entire Great Lakes Region. It is a momentous day for the Southern African Development Community (SADC), Africa, the African Union, United Nations and the entire international community.
  The people of the DRC have suffered for too long. They deserve a break. They deserve to live a better life; a life where their safety and security is assured and guaranteed; a life where they pre-occupy themselves with more important things for improving their living conditions. 
The signatures we have just appended to the Framework is a solemn undertaking and commitment to deliver on the aspirations of the people of DRC and the Great Lakes Region for peace, security, stability and cooperation.
On behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania I promise that we will play our part accordingly.
        In conclusion, I commend the Secretary General of the United Nations, H.E. Ban Ki-Moon for this great initiative. I thank the AU Commission Chairperson, H.E. Nkosazana Dlamini Zuma for the Leadership which made this event possible. 
        Last but not least, I thank the Prime Minister of Ethiopia and Chairperson of the African Union, H.E. Hailemariam Desalegn for his wise leadership and warm reception and gracious hospitality accorded to us.

I thank you for your kind attention.

MAMA SALMA JK AKABIDHI AKABISHI VIFAA VYA TIBA VYA SH. MILIONI 20 NYAMISATI


PWANI, Tanzania
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, mama Salma Kikwete, amekabidhi msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20, kwenye Kituo cha Afya cha Nyamsati, mkoani Pwani.

Msaada huo umetolewana Mfuko wa Huduma za Jamii wa Vodacom Tanzania (Vodacom Foundation) na hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo, katika Kituo cha Afya cha Nyamsati mkoani hapa, ambapo pamoja na mambo mengine, mama Kikwete ameishukuru Vodacom Foundation kwa msaada huo, nakutoa rai kwa wadau wengine kujitokeza na kuunganisha Nguvu katika kukabiliana na matatizo ya kijamii,hasa eneo la afya ya mama na mtoto.

"Idadi ya vifo vya mama na mtoto, mapambano dhidi ya Malaria na UKIMWI, chanjo kwa watoto ikiwemo ya ugonjwa wa Nimonia, mimba kwawanafunzi wa kike pamoja na kuwawezesha wajasiriamaliwa kike ni mambo muhimu ambayo jamii inapaswa kuyatazama kama changamoto na kuangalia namna ya kukabiliana nayo," amesema.

Mama Kikwete amesema upungufu wadawa na vifaa tiba kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini bado ni changamoto, na kwamba msaada uliotolewa utasaidia kuunga mkono jitihada za Serikali zenye lengo la kuleta ustawi wa huduma za  Afya kwa manufaa ya watu wa Nyamsati na mkoa wa Pwani kwa ujumla.

Akipokea msaada huo, Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyamsati wilaya ya rufiji mkoa wa pwani Bw.Haruna Mhina alisema Kituo hicho cha afya  ambacho kinahudumia wastani ya wagonjwa 2000 kwa mwezi kinakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa madawa na vifaa tiba lakini kupitia msaada huo, kwa kiasi kikubwa utasaidia kutatua ukubwa watatizo hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mfuko wa Kusaidia Jamii wa Vodacom,Bw. Yessaya Mwakifulefule, amesema kuwa mfuko huo siku zote umekuwa mstari wa mbele kushirikiana na taasisi na vituo kadhaa vya afya nchini katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini kupitia misaada mbalimbali wanayoitoa.

"Azma ya Vodacom nikuhakikisha tunaifikia jamii na kushirikiana nayo katika kukabiliana na changamoto zinazoizunguka kwenye maeneo yote,hususani afya na elimu, na tutaendelea kuisaidia Nyamsati kadiri itakavyowezekana ili kuleta ustawi mzuri kwa afya ya watu wake," amesema Mwakifulefule.

TCRA KANDA YA MASHARIKI WASHEREHEKEA SIKU YA FAMILIA

PICHA ZA TUKIO HILI INGIA KWENYE UKURASA WETU WA SPOTI AU BOFYA HAPA

MAONYESHO YA SHANGAA-ART OF TANZANIA YATIA FORA JIJINI NEW YORK

Queense Community Collage ambacho ni sehemu ya mtandao wa Vyuo vikuu vya Jiji la New   York  ( City University of New York )  mwishoni wa wiki kiliandaa maonesho   sanaa za kitanzania. Maonesho    hayo  yaliyofanyika katika Chuo hicho  yanaelezwa na   waandaji  ni ya kwanza kufanyika nje ya Tanzania na Ujerumani,  yalipewa  jina  la  SHANGAA-Art of Tanzania likihusisha mkusanyiko  sanaa zaidi ya  112 lakini  kila moja ikibeba maudhui yake. Kwa kweli kama lilivyo  jina la maonesho hayo, ziliwashagaza wageni mbalimbali waliohudhuria maonesho hayo.  Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (pichani akifungua maonyesho hayo), ndiye aliyepamba maonesho hayo  kama mgeni wa heshima, akiambatana  na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Nchi Marekani, Bi. Lily Munanka.  Sanaa zilizopamba maonyesho hayo  zilikuwa ni za kuchonga nyingi kati yake zikitoka katika Mikoa ya  Usukumani na Umakondeni. Laini pia kulikuwa na video zilizokuwa zikionyesha aina mbalimbali za ngoma zikionyesha mila na utamaduni wa mtanzania katika uhalisia wake.  Jumla ya  sanaa 121 zilikusanywa kutoka wa wadau mbalimbali lakini ni 112 tu zilizoweza kuoneshwa kutokana na uhaba wa nafasi. Kwa kutambua umuhimu wa maonyesho hayo  Halmashauri ya Jiji la New York ilitoa Hati kwa waandaaji wa maonesho hayo.   


ยช