.

RAIS KIKWETE AHUZUNISHWA NA MAAFA YA KUPOROMOKA KWA GHOROFA DAR

Mar 29, 2013


*ATOA TAMKO ZITO NA MAELEKEZO MAHSUSI KWA MKOA
*AWAPA POLE WAFIWA NA WALIOFIKWA NA MAAFA HAYO

RAIS KIKWETE
IKULU, DAR ES SALAAM,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa leo, Ijumaa, Machi 29, 2013, ametembelea jengo  lililoporomoka na kusababisha vifo vya watu na majeruhi kwenye Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro mjini Dar es Salaam na amesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa yaliyotokana na kuporomoka kwa jengo hilo.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi wafiwa, anawapa pole nyingi walioumia na wanaoendelea kupatiwa matibabu baada ya kubanwa katika kifusi, wakiwamo watoto wadogo ambao walikuwa wanacheza chini ya jengo hilo la ghorofa 16 wakati lilipoporomoka asubuhi ya leo huku likiendelea kujengwa.
Rais Kikwete amewapongeza na kuwashukuru wananchi wote walioshiriki na wanaendelea kushiriki katika zoezi la uokoaji pamoja na vyombo na taasisi za umma na Serikali zinazoshiriki katika zoezi na kazi hiyo ya uokoaji.
Amewataka waendelee na jitihada hizo ili kama kuna watu ambao bado wamebanwa kwenye kifusi waweze kuokolewa ili wapatiwe matibabu, na kama watakuwa wamepoteza maisha basi miili yao ipatikane na iweze kupewa mazishi ya heshima yanayostahili mwanadamu.
Wakati alipotembelea eneo la tukio hilo, Rais Kikwete ametoa maelekezo mahsusi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mheshimiwa Saidi Mecky Sadik pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova.
Rais amewataka kuhakikisha kuwa Mjenzi wa jengo hilo ambaye ndiye anakuwa anajenga jengo hilo, Mhandisi Mshauri aliyekuwa anasimamia ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam  ambaye alitoa kibali cha ujenzi na ndiye Mkaguzi wa ujenzi pamoja na mwenye Jengo wanapatikana haraka na kuwajibishwa ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete amezitaka taasisi za kitaaluma zinazohusina na shughuli za ujenzi – Wachoraji Majengo, Wakadiriaji Majengo, Wajenzi, Wakandarasi na Wahandisi nazo zichunguze tukio hilo kwa haraka na kwa karibu, ili zibaini yapi yalikuwa ni matatizo na zichukue hatua kwa mujibu madaraka na mamlaka ya taasisi hizo kwa sababu zinayo madaraka na mamlaka hayo.
Rais pia amesema kuwa wakati umefika kwa taasisi hizo sasa kujihusisha kwa karibu zaidi na matatizo yanayojitokeza katika shughuli za ujenzi kwa sababu kila yanapoporoka majengo inakuwa heshima mbaya kwa taasisi hizo. Hivyo ni muhimu kwa taasisi hizo kufanya uchunguzi wa kubaini nini chanzo cha kila tukio kuanzia na lile la leo – kama ilikuwa ni udhaifu katika uchoraji, kama ilikuwa ni udhaifu katika ukandarasi, kama ilikuwa udhaifu na Ushauri ili hatua stahiki zichukuliwe.

PICHA, RAIS ALIPOTEMBELEA ENEO LA TUKIO
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la  jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam  asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUUAGA MWILI WA MBUNGE WA CHAMBANI DAR ES SALAAM LEO

 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika Anne Makinda alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais Kikwete akiwafariji wafiwa
 Rais Jakaya Kikwete akiwafariji wafiwa
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongzi wa kitaifa na wabunge katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambako aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na Spika wa Bunge Anna Makinda na baadhi yawaombolezaji
 Waombolezaji mbalimbali wakiwa ukumbini wakati wa shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu
 Wabunge Anne Kilango Malecela na Magreth Sitta wakiwa na waombolezaji wengine kwenye msiba huo

BALAAAAAAA! JENGO LA GHOROFA 16 LILILOKUWA LINAJENGWA LAPOROMOKA DAR ES SALAAM

 Mtoto Maisamali Karim (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat iliyoangukiwa na jengo hilo katika mtaa wa Indira Gandhi.)
 Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.
 Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo.
 Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
 Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Waokoaji.
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Waokoaji wakiwa kazini.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio. Kulia ni Mbunge wa viti maalum (NCCR-Mageuzi James Mbatia.

TAASISI YA CATHERINE FOUNDATION DEVELOPMENT YATOA MISAADA YA KIJAMII KWA WAGONJWA NA WATOTO YATIMA ARUSHA

 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
 Taasisi ya Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine Foundation ya jijini Arusha leo imetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo viwili vya Yatima vya Faraja na Lohada Moshono vyopte vya jijini humo.
 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akisoma taarifa yake na kuzungumza na watu mbalimbali wakiwapo wafanyakazi wa Hospitali ya Mount Meru.
 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali. 
 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwa amewapakata watoto wawili mapacha waliozaliwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha

BARABARA HATARINI KUTOPITIKA LINDI


Barabara kuu ya kutoka lindi kwenda Ruangwa mkoani Lindi ipo hatarini
kujifunga ikiwa jitihada za haraka hazitachukuliwa na Wakala wa
Barabara mkoa wa Lindi Tanroads kurekebisha hali hiyo(Picha na
Abdulaziz,Lindi)


SALAM KUTOKA KWA WATANZANIA WAISHIO UJERUMANI


Umoja wa Watanzania waishio Ujerumani,
Unawatakia kila la heri ya Sikuu ya Pasaka
watanzania wote popote mlipo,
Upendo na Amani katika jamii
ndio msingi imra wa watanzania.
Pasaka Njema

Mfundo. P.Mfundo
Mwenyekiti (UTU) Ujerumani

NUTRITION CLINIC-AGA KHAN HOSPITAL


Nutrition Clinic at The Aga Khan Hospital, Dar es Salaam
Monday - Friday: 11:00 AM - 1:30 PM
To book your appointment, or for more information:
022 2115151-53 | 0654 444404 | 0784 550100/200 | 0756 886620
For numbers above, dial extension #5611

_________________________________________________

You are currently subscribed to the HapoPapo Tanzania Mailing List as nkoromo@gmail.com 
To Unsubscribe from this Mailing List, kindly reply to admin@hapopapo.com with the subject "Unsubscribe"
To Subscribe to this Mailing List, kindly email admin@hapopapo.com with the subject "Subscribe"For Inquiries Contact:HapoPapo Tanzania9 - 92/94 Lugalo Street, Dar Es Salaam, Tanzania+255715500730 | admin@hapopapo.com | www.hapopapo.com

MATUKIO YA MIMBA KWA WANAFUNZI YAPUNGUA HANDENI

MUHINGO RWEYEMAMU

Na Thehabari.com, Handeni
Matukio ya kesi za kuwatia mimba/kuwabaka wanafunzi yaliokuwa yameshamiri katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Handeni sasa yameanza kupungua tofauti na ilivyokuwa awali. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 na Machi 2013 matukio ya mimba yanapungua.

Akizungumzia hali hiyo juzi Wilayani Handeni, Ofisa Elimu wa Wilaya, Mgaza Muchiwa alisema matukio ya mimba kwa wanafunzi yanapungua tofauti na miaka ya nyuma ambapo matukio ya utoro wa mimba kwa wanafunzi yalikuwa mengi.
“Picha ya mwaka jana niliiona na tulikuwa tukifuatilia kwa karibu matukio ya kesi za mimba kwa wanafunzi…huwezi kufananisha na ilivyo sasa kunamabadiliko kwani matukio haya yamepungua,” alisema Muchiwa akizungumza na mwandishi ofisini kwake Handeni juzi.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera alithibitisha pia kupungua kwa kesi za mimba zinazofikishwa katika vituo vya Polisi ukilinganisha na hapo nyuma. Akifafanua zaidi kupitia taarifa za Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Handeni, alisema hadi Novemba 2012 walipokea kesi 66 za matukio hayo lakini tangu hapo hadi Machi mwaka huu kesi hizo zimepungua kwa kiasi kikubwa.

Uchunguzi uliofanywa na www.thehabari hivi karibuni katika shule za sekondari Komnyang’anyo, Kileleni na Kivesa zote za wilayani Handeni umeonesha kupungua kwa matukio ya mimba kwa wanafunzi, huku walimu wakidai hali hiyo imechangiwa na kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya, Muhingo Rweyemamu.

“Kweli kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya imesaidia sana maana watu wameanza kuogopa kuwarubuni wanafunzi…hata wazazi na wanafunzi nao wanaogopa kuhusishwa katika kesi hizo hii imesaidia kupunguza matukio ya mimba,” alisema Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo Nadhiru Kinyama.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Rweyemamu Agosti 2012 alianzisha kampeni ya kupambana na watu waliyokuwa wakiwakatisha masomo wanafunzi kwa kuwatia mimba na kuwaozesha kwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii juu ya umuhimu wa elimu wilayani humo.
*IMEANDALIWA NA WWW.THEHABARI.COM KWA KUSHIRIKIANA NA TAMWA

UZINDUZI WA CRDB CHINA DESK

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei (kushoto) akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu na  Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa CRDB China Desk.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa CRDB China Desk
 Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing akizungumza wakati wa uzinduzi wa CRDB Chine Desk.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu akizungumza katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa.

DAR ES SALAAM, Tanzania

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei, amewataka wajasiriamali na wawekezaji wanaofanya biashara zao kati ya Tanzania na China, kuchangamkia fursa pana ya ukuzaji mitaji yao na pato kwa kutumia huduma mpya ya CRDB China Desk.

Dk Kimei aliyasema hayo jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa China Desk, inayotolewa na CRDB, itakayo wahudumia wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji wanaofanyakazi zao baina ya mataifa hayo rafiki.
“China Desk, ni huduma yenye fursa inayoweza sio tu kusaidia kukuza mitaji na kutanua wigo wa maendeleo, bali kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo baina ya China na Tanzania, ambao uliasisiwa karibia nusu karne iliyopita,” alisema Dk Kimei katika hafla hiyo.

Aidha, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, aliiomba CRDB kuboresha utoaji wa mikopo ya riba nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, ili kuharakisha ukuaji wa pato la Mtanzania na Taifa kwa ujumla.

Dk Nagu alibainisha kuwa, taasisi za kipesa nchini zina mchango mkubwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kukuza pato lao, kama zitakuwa tayari kuwapa mikopo yenye masharti nafuu na riba ndogo, ili kusaidia harakati zao za kujikwamua na kukuza uchumi wa taifa.

“CRDB mnastahili pongezi kwa huduma hii, inayokuja wakati ambao Tanzania kama Taifa, lilimpokea rais mpya wa China, Xi Jinping katika ziara ya kikazi. Taasisi nyingine za kifedha zitambue umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa haya na kubuni huduma kama hizi,” alisema Dk Nagu.

Aliongeza kwamba, kwa kuwa harakati za kumkomboa Mtanzania zimeshika kasi, huku China ikijitoa kadri iwezavyo kuisaidia Tanzania, kuna haja huduma kama hizo za China Desk zikaambatana na mikakati endelevu ya kimandeleo, na taasisi nyingine nazo zinastahili kuiga.

Kwa upande wake, Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing, aliipongeza CRDB kwa kufuata nyayo za waasisi wa China na Tanzania, kiasi cha kubuni na kuzindua China Desk – dawati litakalowanufaisha wajasiriamali na wafanyabiara wa kila upande.

“Huduma hii ni harakati chanya inayofuata nyayo za waasisi wa ushirikiano baina ya China, Rais Mao Tse Tung na Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Vizazi na vizazi vitabaki kujivunia na kila mmoja atajisikia yu nyumbani anapokuwa katika moja ya nchi hizo,” alisisitiza Youqing. 

WIZARA YA AFYA YALISHUKURU SHIRIKA LA WHO KWA MSAADA WA MAMILIONI YA FEDHA

Mar 28, 2013

  Naibu Katibu  Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Regina   Kikuli akimshukuru    kwa WHO  baada ya kutoa  magari saba  yaliyotolewa leo (jana) ,na vifaa vingine vyenye thamani ya sh. bilioni 2.4  katika hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam. katika hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam. Katika msaada huo magari mengine 22 yatatolewa baade.
Naibu Katibu  Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Regina   Kikuli akitoa hotuba yake ya kushukuru Mwakilishi Mkazi wa Shirika la  Afya Duniani (WHO), Dk. Rufaro Chatora baada ya kutoa  magari saba  yaliyotolewa leo (jana) ,na vifaa vingine vyenye thamani ya sh. bilioni 2.4  katika hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam. katika hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam. Katika msaada huo magari mengine 22 yatatolewa baade.
ª