.

OPENING UP NEW ROUTES TO THE FAR EAST

Apr 30, 2013


OPENING UP NEW ROUTES TO THE FAR EAST
.

TANGAZO: JAHAZI MODERN TAARAB KUUPAMBA MKESHA WA MEI MOSI NDANI YA DAR LIVE LEO

MGEJA AWAASA VIJANA KUWAPUUZA WANASIASA WANAIOHUBIRI MAANDAMANO BADALA YA KUWALETEA MAENDELEO


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), Khamis Mgeja (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanachama wa Tawi la Wakereketwa la Pamba Road, katikati ya Jiji la Dar es Salaam jana. Aliyevaa koti ni Mwenyekiti wa tawi hilo, Ramadhan Makula ambaye alimwalika Mgeja kutembelea tawi lao. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)Na  Mwandishi WetuMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC), Khamis Mgeja, amewataka vijana wawapuuze wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaohubiri maandamano, badala yake wajikite katika kufanya kazi kwa bidii kwani ndiyo ni njia pekee ya kujiletea maendeleo.Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Shinyanga, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na vijana wa Tawi la Pamba Road, Dar es Salaam ambao  walimkaribisha kumweleza changamoto wanazokabiliana nazo.Alisema wanasiasa wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipandikiza chuki miongoni mwa wanajamii kwa kuwaambia kuwa eti Serikali inaweza kuwatafutia ajira wakati tatizo hilo ni la dunia nzima na kwamba suluhisho ni kufanya kazi kwa bidii."Wapuuzeni wanasiasa wanaopandikiza chuki. Matatizo haya ya ajira lazima tuyakabili kwa kufanya kazi kwa bidii,"alisema Mgeja.Aliongeza kuwa matatizo ya vijana yanazungumzika na si kauli za viongozi hao kuwaambia wananchi kuwa wanawashtakia viongozi kwao waamue cha kuwafanya hatua ambayo inaeneza taifa lenye manung'uniko.Alibainisha kuwa Serikali ya CCM inafahamu matatizo mbalimbali waliyonayo wananchi wake ndiyo maana inasisitiza watu wafanye kazi kwa bidii na kuhimiza mabenki yawakopeshe wafanyabiashara wadogo.Aliwasifu vijana wa tawi hilo kujikita katika kazi mbalimbali za ujasiliamali wakiwemo mafundi viatu.Aliwataka waendelee kujikita katika kazi za kujiongezea kipato badala ya kupanga uhalifu ambao hauleti taswira njema katika jamii.Aidha kiongozi huyo wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa Shinyanga, alitoa msaada wa sh. 100,000 kwa vijana hao ili ziwasaidie kununua rangi za kupaka katika viatu.


LADY JAYDEE KUADHIMISHA MIAKA 13 YA KUWA KATIKA FANI YA KUZIKI

Apr 29, 2013

JIDE

TANGAZO RASMI
Katika mwaka huu 2013, Inatimia miaka 13 tangu nianze kazi ya muziki.
Nashukuru MUNGU tuko pamoja na pia, nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea ku support muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki.
Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.
Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la NOTHING BUT THE TRUTH ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu awabariki

LEMA ATINGA KIZIMBANI LEO


Mbunge wa Arusha, Godbles Lema akiwa katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha na aliyekua katibu wa Chadema Arusha mjini Derick Magoma kabla ya kusomewa shitaka la uchochezi wa vurugu za wanafunzi wa chuo cha uhasibu jijini Arusha kufuatia  na kifo cha mwanafunzi mwenzao Henry Kago.

UDOM WAKUTANA NA SPIKA BUNGENI LEO


SPIKA wa Bunge Anna Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baadhi ya wanachuo hao walipotembelea bungeni leo

TUME: RASIMU ITAZINGATIA MAONI YA KATIBA YA WANANCHI, WALEMAVU KUHUSISHWA

JAJI WARIOBA

Na Hussein Makame na Genofeva Matemu-Maelezo
TUME ya Mabadiliko ya Katiba inajiandaa kutengeneza rasimu ya Katiba Mpya itakayozingatia maoni ya wananchi ambayo inatarajiwa kutolewa Juni mwaka huu.

 Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Joseph Warioba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mchakato wa uundwaji wa katiba mpya.

Aidha Jaji Warioba amesema wakati utakapofika anawaomba wananchi waipitie rasimu hiyo, waijadili na kutoa maoni bila ya woga kama walivyofanya wakati wa kukusanya maoni.

 Jaji Warioba alitoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa, jumuiya na taasisi nyingine kuwaachia wananchi watoe maoni yao kuhusu rasimu hiyo bila ya kuwaingilia.

Alisema, tume hiyo iko tayari kufanya maamuzi magumu ya kuainisha mambo muhimu yaliyopendekezwa katika mchakato wa kukusanya maoni, mfano masuala ya Muungano, Madaraka ya Rais na majimbo ambayo kila mwananchi amependekeza kwa jinsi anavyotaka yeye, lakini ni lazima tume ichague moja kati ya maoni hayo na kuyaacha mengine.

 “Tumefanya uchambuzi wa maoni ya wananchi, kwa kweli ni mengi sana, hivyo tume iko tayari kufanya maamuzi magumu ya kuweka maoni ambayo ni ya msingi, hivyo tunaomba wananchi wawe tayari kuyakubali kwa kuwa haiwezekani kila maoni ya mwananchi yakachukuliwa”, alisema Jaji Warioba.

Aliongeza kuwa baada ya rasimu hiyo kutengenezwa, tume hiyo itaunda mabaraza ya katiba ya watu wenye ulemavu ili kuwapa fursa walemavu kutoa maoni yao kuhusu rasimu hiyo.

“Walemavu hawakusahaulika, lakini tuliona tufanye utaratibu maalum wa kupata wawakilishi kutoka makundi 10 ya walemavu kupitia vyama vyao vya Tanzania Bara na Zanzibar”, alibainisha Jaji Warioba.

Akizungumzia uchaguzi wa wawakilishi wa mabaraza ya katiba ya kata na shehia, Jaji Warioba alisema jumla ya kata 3,331 kati ya kata 3,339 zimekamilisha vizuri mchakato wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya.

Alisema kwa upande wa Zanzibar, shehia 323 kati ya 335 zimekamilisha vizuri mchakato wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya.

“Hivyo kuna shehia 12 za Zanzibar na kata 3 za Tanzania hazijakamilisha uchaguzi wake kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mivutano ya kisiasa, kidini na rushwa” alifafanua Jaji Warioba.

BAISKELI INAPOJAZA MZIGO KUPITA KIASI

Mwananchi akikatiza barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro, eneo la Kibaha, huku akisukuma baiskeli iliyosheheni nyasi kiasi hata cha yeye mwenyewe kukaribia kufunikwa, kama alivyokutwa na mpigapicha wetu jioni hii.

HATARI, HATARI HATARI


Waya wa umeme ukitoapovu kutokana na kuwa na moto, baada ya kuangukia kwenye dimbwi la maji ya mvua, mtaani eneo la Mwenge, Dar es Salaam, leo mchana. Hapi mpigapicha wetu anaondika eneo hilo Tanesco walikuwa hawajafika kuondoa umeme huo ambao ulikatwa na lori la kubebea taka lilipita katika mtaa huo.

CHIBUKU YAIBUKA KIVINGINE DAR ES SALAAM


 Wakala wa Uuzaji kinywaji cha asili cha Kibuku kinachozalishwa na Kiwanda cha Dar Brew, Samwel Marwa akinywa kinywaji hicho wakati wa semina ya siku moja ya kuboresha biashara ya kinywaji hicho mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Double View, Sinza, Dar es Salaam. Marwa anamiliki baa iitwayo Samwel Saccos iliyopo Nyantira, Jimbo la Ukonga. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Baadhi ya mawakala wakifaidi kinywaji hicho

 Mkurugenzi wa Bia za Asili za Kampuni ya Bia Tanzania, Kirowi Suma akitoa maelezo kwa baadhi ya mawakala jinsi ya kuboresha biashara ya kinywaji cha Kibuku. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Baadhi ya mawakala wakinywa Kibuku na Bia baada ya semina kumalizika
                                                    Mawakala wakipata mlo
                             Sasa ni wakati wa msosi na hatimaye kushushia na Kibuku na Bia. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mkurugenzi wa Bia za Asili za Kampuni ya Bia Tanzania, Kirowi Suma (katikati), akimsikiliza Meneja Mipango na Fedha wa Kiwanda cha Dar Brew, Andrew Asalile (kulia) walipokuwa wakijadiliana jambo wakati wa semina hiyo. Kushoto ni Sichilima Kazonda ambaye ni Meneja wa Operesheni. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Kibuku na bia zinayweka pamoja
                                                                  Makreti ya Kibuku
                            Mmoja wa mawakala akimimina Kibuku kwenye glasi tayari kwa kunywa
Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Double View, Venance Msaky akinywa Kibuku baada ya semina ya kuboresha biashara ya kinywaji kumalizika  mwishoni mwa wiki kwenye hoteli hiyo. Kulia ni Reginald Mosha ambaye ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Dar Brew kinachonunuliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)Machi 15, mwaka huu. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

CRDB YAKABIDHI JENGO LA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO

Apr 28, 2013

 Jengo la Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ikionekana ikiwa katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati na Benki ya CRDB na kugharimu kiasi cha sh. milioni 50.
 Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo (kushoto) akifurahjia jambo na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kati) na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey. 
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa wameshika miche ya miti tayari kwa kuanza zoezi la upandaji miti kuzunguka katika maeneo ya hospitali ya Mkoa wa Morogoro. 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akipanda mti wa kumbukumbu baada ya uongozi wa benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro lililofanyiwa ukarabati pamoja na kuwekewa vifaa
muhimu katika wodi hiyo. Jumla ya Sh. Milioni 50 zimetumika katika ukarabati huo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati), akishiriki kufanya usafi katika jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki ya CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Dk. Charles Kimei akishiriki katika zoezi la kufanya usafi. Hafla hiyo ilifanyika mjini Morogoro juzi. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiteta jambo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Mashishanga.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati) akipokea mfano wa ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakati wa kukabidhi jengo la wodi ya watoto ya Hospitali ya Mkoa wa  Morogoro,  ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika mjini Morogoro juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid  akizindua wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
 Kutembelea wodi ya watoto.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akitandika kitanda baada ya uongozi wa Benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto lililofanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitandika kitanda baada ya uongozi wa Benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto lililofanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. 
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakiweka chandarua katika kitanda wakati walipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya uongozi wa benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi hiyo ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. Kulia aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Juma Ngasongwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kufanyiwa ukarabati na Benki ya CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei.
Picha ya pamoja. 
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akiingia ukumbini wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wao. 
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wadau wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na wadau wa benki hiyo katika ukumbi wa Nashera mjini Morogoro. 
 MC wa hafla hiyo akiwa kazini.
 Msanii Mrisho Mpoto wa Mjomba Band akiimba kwa hisia. Kulia ni mwimbaji wa benki hiyo, Ismail Kipira.
 Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Juma Ngasongwa ambaye kwa sasa ni mkulima wa Mpunga akiwa na wadau kataika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akikata keki na Mkurugenzi wa tawi la Morogoro,  Pendo Assey. 
 Mdau wa benki ya CRDB, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo akipata keki.
 Wateja mbalimbali wakipa keki.
 Vinywaji kama kawa.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kushoto) akiwa na maofisa wa benki hiyo.
 Muziki ulishika kasi
ยช