.

CCM YAIPONGEZA SERIKALI KUANGALIA UPYA SUALA LA KODI YA TOZO YA LAINI ZA SIMU

Jul 31, 2013

NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza serikali, kwa uamuzi wake kurejesha bungeni kwa ajili ya mdajala zaidi, muswada wa sheria ulioanzisha kodi mpya ya tozo ya sh. 1,000 kwa laini ya simu.

Taarifa ya CCM iliyotolewa leo mjini Dodoma, na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye imesema uamuzi huo umedhihirisha kwamba serikali inawasikiliza na kuwajali wananchi wake.

Akiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari leo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amekaririwa akisema kwamba mjadala kuhusu muswada wa sheria ya kodi hiyo ya tozo hiyo utafanyika wakati wa mkutano wa Bunge unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Baada ya kupitishwa na bunge Juni mwaka huu, na utekelezwaji wake kuanza rasmi Julai mwaka huu, CCM ilikuwa miongoni mwa wadau waliopinga vikali kuanzishwa kwa kodi ya tozo hiyo, ikieleza kwamba ni mzigo na usumbufu usio wa lazima kwa watumiaji wa simu ambao wengi matumizi yao ni ya kawaida.

Katika taarifa hiyo, CCM imesema kwa kuwa wabunge wengi ni wa chama hicho, watumie fursa hiyo kuhakikisha sheria ya tozo hiyo inaondolewa na wakati huohuo watumie uwezo wao wote kuhakikisha wanaishauri serikali vizuri kupata njia mbadala itakayotumika kuziba nafasi itakayokuwa imeachwa kwa kuondolewa tozo hiyo.

"Kimsingi hatua hii imetupa faraja na hivyo CCM inaipongeza Serikali kwa kuamua kusitisha sheria ya kodi ya tozo hiyo ya sh. 1,000 kwa laini ya simu kwa kuwa ingesababisha usumbufu na adha isiyo ya lazima kwa wananchi", imesema CCM katika sehemu ya taarifa yake.

TCRA YAZINDUA KAMPENI YAKUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO YA MAWASILIANO

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza na wadau mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) juu ya kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano hapa nchini, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akifafanua jambo zaidi.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wadau mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) juu ya kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akibonyeza kitufe kwenye Kompyuta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Wimbo wa kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano hapa nchini.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo kwa wadau mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) juu ya kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kiasili,Mrisho Mpoto akisisitiza jambo juu ya umuhimu wa Mawasiliano Mazuri ya Mitandao wakati wa Warsha ya siku moja kwa wadau mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) juu ya kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wamiliki wa Magazeti tando hapa nchini (Blogger), John Bukuku kutoka Full Shangwe Blog akitoa shukrani zake za dhati kwa TCRA ikiwa ni kwa niaba ya Bloggers Wengine baada ya kutambuliwa kuwa ni sehemu ya vyombo ya Habari hapa nchini. TAARIFA KAMILI ILIYOTOLEWA NA TCRA KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI HIYO BOFYA HAPA

MAABARA YA KISASA YENYE UWEZO WA KUTAMBUA MAGONJWA MAPYA NA YALE YA HATARI SANA IKIWEMO EBOLA YAZINDULIWA BAGAMOYO

Bagamoyo 2
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid na Balozi wa Italia nchini Pierluigi Velardi wakizindua maabara ya kisasa kwenye majengo ya Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) huko Bagamoyo hivi karibuni. Maabara hiyo ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inajulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3, na ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI).
Bagamoyo 1
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Seif Rashid hivi karibuni amezindua maabara ya kisasa kabisa ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inayojulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3 ambayo ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) kwenye maabara zake za Bagamoyo. Pichani anaonekana Mratibu wa mradi wa maabara hiyo Bw.Francesco Vairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afyya (wa pili kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani ( WHO) Dr. Rufaro Chatora na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wakiwa ndani ya maabara hiyo.

WORLD BANK MOBILIZED RECORD SUPPORT FOR AFRICA'S ECONOMIC GROWTH AND DEVELOPMENT PROSEPECTS IN FY 13

Jul 30, 2013

WASHINGTON, July 29, 2013 
The World Bank Group committed a record US$14.7 billion in fiscal year 2013 (July 2012 to June 2013) to support economic growth and better development prospects in Africa despite uncertain economic conditions in the rest of the global economy.

“The region has shown remarkable resilience in the face of a global recession and continues to grow strongly,” said Makhtar Diop, World Bank Vice President for the Africa Region. “Africa is at the center of the World Bank Group 2030 goals of ending extreme poverty and promoting shared prosperity, in an environmentally, socially, and fiscally sustainable manner.”

The World Bank Group continued its strong commitment to Africa approving $8.25 billion in new lending for nearly 100 projects this fiscal year (FY13). These commitments=>READ MORE

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA MKUTANO WA HIGH LEVEL GROUP-GABERONE -BOTSWANA

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea ua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Sir Seretse Khama jijini Gaberone nchini Botswana kutoka kwa binti Jessica Kissasi, anayesoma darasa la pili, Baobab International School  tarehe 29.7.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Bwana Christopher Castle,Mkuu wa Idara ya HIV and Health Education kutoka Makao Makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) yaliyoko Paris nchini Ufaransa wakati Mama Salma alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama huko Botswana tarehe  29.7.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipewa maelezo mafupi na Dr. Patricia Machawira, Mshauri Mkuu wa HIV and AIDS wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika muda mfipi kabla ya kuanza kwa  mkutano wa  “High Level Group-Action on comprehensive sexuality education and health services for adolescents and young people in Eastern and Southern Africa “ unaofanyika Gaberone nchini Botswana tarehe 30-31.7.2013.
  Wajumbe wakimsikiliza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia katika mkutano wa  sikuk mbili wa  “High Level Group”  kutoka  Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini Botswana.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa mkutano wa  sikuk mbili wa  “High Level Group”  kutoka  Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini Botswana.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa mkutano wa  sikuk mbili wa  “High Level Group”  kutoka  Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini Botswana.
 Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania  ( kulia kwenda kushoto) Dr. Kadija Mwamtemi, Mwanahamisi Kitogo, Mshauri wa Rais kuhusu masuala ya huduma za jamii, Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA foundation na Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini Mheshimiwa  Radhia Msuya Mtengeti wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma tarehe 30.7.2013.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipongezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Jesca Eriyo baada ya kufungua mkutano wa “High Level Group” huko Gaberone nchini Botswana terehe 30.7.2013. 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akichangia baadhi ya mambo wakati wa mkutano wa  “High Level Group” kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika nchini Botswana  tarehe 30.7.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI.

WAZIRI MKUU WA THAILAND AANZA ZIARA YA KIKAZI TANZANIA, AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS JAKAYA KIKWETE, IKULU


  Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akikagua gwaride la heshima la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo.
  Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya ngoma akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam.
 Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri mkuu wa Thailand ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Dr. Surapong Tovichakchaikul (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Tanzania Mh. William Mgimwa (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya kudumisha , kutunza na kuendeleza uwekezaji kati ya Tanzania na Thailand Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Tanzania na Thailand walioongozwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Yingluck Shinawatra ambapo Tanzania na Thailand zimesaini mikataba minne ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa, uendelezaji wa shughuli za uwekezaji, ushirikiano katika masuala ya Ufundi na ushirikiano katika sekta ya Nishati na Madini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

NDEGE YA MADAKTARI YAPATA AJALI ARUSHA, SITA WANUSURIKA KIFO

NA LILIAN JOEL, ARUSHA
Watu sita wamenusurika kifo baada ya ndege ndogo ya madaktari maalum (Flying doctors), wanaotoa huduma katika vijiji vya jamii ya wafugaji wa Kimaasai imeanguka leo katika eneo la kijiji cha Kipenjiro, wilayani Ngorongoro.
Habari zilizopatikana kutoka Ngorongoro na kuthibitishwa na Mbunge wa Ngorongoro, Saning’o Telele zimeeleza kuwa ndege hiyo iliyokuwa na abiria saba ilianguka kati ya Saa 9:00 na 10:00 alasiri.
“Ni kweli ndege ndogo ya Flying doctors wa Kanisa Katoliki inayotoa huduma za kitabibu katika vijiji kadhaa wilayani Ngorongoro imeanguka leo ila ni bahati nzuri hakuna taarifa ya vifo hadi hivi sasa,”alisema Mbunge Telele kwa njia ya simu.
Mbunge huyo alitaja baadhi ya vijiji ambavyo madaktari hao hutoa huduma kuwa ni Naiyobi, Ngarasero, Olitatiro na Endulen.
Kwa mujibu wa Telele, majeruhi wote waliokuwepo ndani ya ndege hiyo walikimbizwa hospitali ya Seliani Jijini Arusha kwa matibabu baada ya shirika linalomiliki ndege hiyo kutuma ndege nyingine kuwachukua kutoka eneo la ajali.
Taarifa zilizopatikana kutoka hospitali ya Endulen inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Arusha zinasema ndege hiyo ilikuwa na daktari mmoja na wauguzi wawili kutoka hospitali hiyo ambao majina yao hayakupatikana mara moja.
Pamoja na daktari na wauguzi, ndege hiyo pia ilikuwa na marubani wawili na wagonjwa wawili ambao ni mama na mtoto wake.
Vijiji ambavyo Flying doctors hufika kutoa huduma kwa ndege hiyo ni vile visivyokuwa na huduma ya kitatbibu na hazifikiki kirahisi kwa njia ya barabara.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo lakini hakuwa tayari kuizungumzia kwa undani kwa maelezo kuwa hajapokea taarifa rasmi za kutosha kutoka kwa maafisa wake walioko wilayani Ngorongoro kutokana na mazingira halisi ya jiografia ya wilaya hiyo kimawasiliano.

AIRTEL YAFUTURISHA BADHI YA WATEJA WAKE DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto) akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wao jijini Dar es Salaam jana.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akiwakaribisha baadhi  ya wateja wao katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya. PICHA ZAIDI>BOFYA HAPA

WAZEE WA KIMILA WAMPONGEZA MBUNGE NYAMBARI NYANGWINE

NYAMBARI NYANGINE
TARIME, Tanzania
SAISA chafu zinazodaiwa kuanza kushika kasi katika majimbo ya Tarime na Rorya, zimewaibua wanasiasa wakongwe na wazee wa kimila, ambao wametoa maonyo makali.

Pia, wamewataka wananchi kuendelea kuwaunga mkono wabunge Nyambari Nyangwine (Tarime) na Lameck Airo (Rorya), ili waendeleze kasi ya kuleta maendeleo.

Wamesema majimbo hayo kwa sasa yamekuwa mfano wa kuigwa nchini kutokana na maendeleo makubwa yaliyopatikana tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma, ambapo wamesema kamwe wanachama wanaoendesha siasa za makundi wasipewe..>>Inaendelea>BOFYA HAPA

YOUNG DEE AIBUKA NA 'KIJUKUU'

Jul 29, 2013


Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Young Dee anajipanga kuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kijukuu’ ikiwa ni muendelezo wa kuwashika mashabiki wa kazi zake.

Young Dee alishawahi kutamba na kazi ya ‘Dada anaolewa’ licha ya kuwa na kazi nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Young Dee alisema kazi hiyo kaitengeneza katika studio ya MJ rekodi chini ya mtayarishaji wake mahiri, Marco Chali.

Pia aliwataka wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri kutokana na mashairi yaliyomo ndani yake kubeba ujumbe katika jamnii.

“Naomba wapenzi wa kazi zangu wake mkao wa kula kwaajili yakuipokea kazi hii, naimani nitaisambaza hivi karibuni ikiwa ni pamoja na video yake ili niwape burudani iliyokamilika wapenzi wa kazi zangu,” alisema.

EDGAR DAVIS MOSHA NDANI YA VOICE OF AMERICA (VOA)

Edgar Davis Mosha mtoto wa mfanyabiashara tajiri na maarufu boss wa kampuni ya DELINA  Bwana Davis Mosha ahojiwa na VOA (Voice of America). Edgar na baba yake wametua kwa kishindo nchini Marekani wakitokea Uingereza ambapo Edgar amepeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuitwa  kufanya majaribio na klabu ya Chelsea ya Uingereza. Swahili TV itakuletea Exclusive video karibuni.
 Davis Mosha "The Boss" akifanya mahojiano na kituo cha VOA jijini Washington DC, kulia ni mwanae Edgar Mosha mwanafunzi mwenye kipaji cha masomo na soka.
 Davis Mosha "The Boss" akifurahia jambo katikati ya mahojiano na kituo cha VOA jijini Washington DC.
Kutoka kushoto; Juliet , Sunday Shomary, Edgar Mosha, Davis Mosha "The Boss" na Chief wa VOA Idhaa ya Kiswahili Dkt. Hamza Mwamoyo.
Davis Mosha "The Boss" na Edgar Davis wakipata picha ya kumbukumbu baada ya kuteta na VOA, Jijini jijini Washington DC
Edgar Davis, Davis Mosha "The Boss" na mtangazaji mahiri bwana Sunday Shomary
Juliet, Alex Kassuwi, Edgar na The Boss wakipata picha ya ukumbusho VOA.

MDAU: PROMOSHENI KAMA ZILE ZILIZOKUWA ZIKIFANYWA NA KINA BISHANGA BISHAIJA ZIMEISHIA WAPI?

Jul 28, 2013

Serikali  inahimiza  mashirika makampuni  wafanyabiashara  kutumia  wasanii wa nyumbani  katika  matangazo  na  promtion  mbalimbali          Pichani  anaonekana  msanii wa  kucheza  na  Nyoka  mama Salima  Moshi ( mama  nyoka)  akiwa  Promoter enzi  hizo  wa Kampuni  ya  Bia Tanzania   Akitangaza   vinywaji  vinavyozalishwa  na  TBL zikiwemo   Kilimanjaro  Ndovu    Bingwa na nyingine  nyingi  akiwa  amevaa  fulana  ya  Ndovu  ya TBL  akishirikiana  na  Wasanii  maarufu  Nchini  kwenye   Promotion  hiyo  ya  TBL   enzi  hizo   akina  Bishanga Bishaija, Rich  Rich   Waridi  kutoka kundi la mambo hayo wengine  ni ZIpompapompa, Majengo, Pangu Pakavu     Mama Shunda  Mzee Pembe, Mzee Sumaku    Wanne Star  na  kundi  lake   je? sasa  hivi  Promotion   kama  hizi  zimeishia  wapi ?    Na  je   kama zinafanyika  wasanii wanalipwa inavyostaili?

WANACHAMA WA MFUKO WA MAENDELEO YA MTANDAO WA WANAMBWEWE WAISHIO DAR ES SALAAM, WAKUTANA NA MBUNGE WAO

 MBUNGE wa Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Saidi Mwanamdogo, akizungumza na wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanambwewe waishio Dar es Salaam (MNDF), leo katika ukumbi wa Shule ya Msingi Ali Hassani Mwinyi, mjini Dar es Salaam. Wanachama hao walimwalika kwenye kikao chao cha kujadili jinsi ya kuuendesha mfuko huo kwa manufaa ya wananchi wengi
 MBUNGE huyo akisisitiza jambo
 Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Katibu wa wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya wanamtandao wa Mbwewe waishio Dar  es Salaam, Hassani Msonde akizungumza mwanzoni mwa kikao
 Mwenyekiti wa Umoja huo, Rajabu Papa akifungua kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati ya Umoja huo, Fatuma Kikwappe akisoma risala huku viongozi wakimsikiliza kwa makini akiwemo Mbunge Bwanamdogo
 Fatuma akiendelea kusoma risala hiyo
Kisha akaikabidhi risala hiyo kwa Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo
 Mbunge Saidi Mwanamdogo akiwakabidhi dola za Marekani, viongozi wa umoja huo, ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kufanikisha usajili.
 Mwenyekiti akimkabidi Mbunge Katiba ya Umoja
 Fatuma na mjumbe mwenzake wa Kamati katika Umoja huo wakipitia makabrasha kwa makini
 Mbunge wa Chalinze Saidi Mwanamdogo akiagana na viongozi wa Umoja huo baada ya kushiriki kikao>IMETAYARISHWA NA theNkoromo Blog
ยช