.

TANGAZO LA KIFO CHA MAMA ROSE HEINRICH SANGIWA MATAJI, KILICHOTOKEA ROCHESTER, NEW YORK, MAREKANI

Sep 30, 2013

Familia ya Marehemu Chief Shaaban Mtengeti II, inasikitika kutangaza kifo cha shangazi yao mpendwa Mama Rose Heinrich Sangiwa Mataji, mama yake Robin, Henry na Robert, kilichotokea Jumamosi tarehe 28 September alasiri huko Rochester, New York, Marekani. Habari ziwafikie ukoo wote wa Mzee Heinrich Sangiwa, Bakari Sangiwa, Athumani Sangiwa, Mtengeti Sangiwa,  Kihama Sangiwa, Koshuma Sangiwa, Profesa Twalib Ngoma na ukoo  wote wa kina Ngoma,  na wa kwa Mdimu wote, na ukoo wa Rtd. Col. Julius Mataji wa Dodoma. Mipango ya mazishi inafanywa huko
 Rochester, New York. 
Kwa Dar es Salaam ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu watakutana nyumbani kwa Bi. Hajjat Mwatumu Jasmine Malale, 51 Mlingotini Close, Regent Estate, Dar es Salaam Jumatatu Septemba 30, jioni baada ya saa za kazi. Kwa mawasiliano simu 0713 317 254; 0752 345 602

SERIKALI YAFUNGIA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA

Sep 28, 2013

Serikali imeyafungia  kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013  kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala  za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne (14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice ) Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.
Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013”  kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri  haukupaswa kuchapishwa Magazetini.
Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI”  habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa  mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la  ukweli.
Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia  katika maeneo ya ibada.
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi  lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa  kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za  fani ya Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta  kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika  na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na  waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama  wavione kuwa haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.
Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani  nchini.
Imetolewa na
 MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

RAIS KIKWETE AHUTUBIA UMOJA WA MATAIFA


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban- Ki- Moon ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuhutubia kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani leo mchana(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kikao cha 68 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo jijini New York Marekani.

SEMINA YA KAMATA FURSA YAFANYIKA MWANZA

 
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Gold Crest.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini,aliyajipatia fursa mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya kusubiri Serikali iwafanyie ama iwaletee kila kitu hapo walipo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akizungumza kwenye mada yake iliyohusu masuala mbalimbali, kuhusiana na Fursa ya kuongeza thamani na kutengeneza jina,sambamba na fursa ya matumizi ya Teknolojia mbele ya maelfu ya vijana waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzzetu,iliyofanyika leo,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza.
 Sehemu ya wakazi wa mji wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzetu,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada mbalimbali zilikuwa zikizungumzwa. 
  Mmoja wa wasanii wa bongofleva,Nikki Wa Pili akizungumza kwenye semina ya kamata fursa twendzetu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max Malipo,Bwa.Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya Max Malipo inavyoweza kuisadia jamii kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi Washiriki wakifuatilia.
Mmoja wa waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael akijulikana zaidi kwa la kisanii kama Lulu akiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,ambapo pia atazungumzia mambo kadhaa mbalimbali kwenye semina hiyo,ambayo itawakutanisha Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba,Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini na watoa mada wengine mbalimbali. 

Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha alipokuwa akiwasili kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii.

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele (mwenye miwani) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha walipokuwa wakiwasili kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,pichani kati ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group,Bwa.Ruge Mutahaba.

Baadhi ya Wakazi wa mji wa Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii. 
 Baadhi ya viongozi walioketi meza kuu.

JAJI WARIOBA: MIKUTANO YA MABARAZA YA KATIBA TUMEIFANYA KWA UFANISI MKUBWA

Sep 26, 2013

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuelezea utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Agustino Ramadhani. Pamoja na mambo mengine Jaji Warioba amezungumzia namna mikutano ya mabaraza ya katiba iliyoendeshwa  kwa ufanisi.
     Amesema ili kuendesha mikutano ya katiba kwa ufanisi,Tume ilijigawa katika makundi 14, kila kundi likiwa na wajumbe kati ya wawili na watatu. Makundi haya yalizunguka nchi nzima na kufanya jumla ya mikutano 179 iliyohudhuriwa na wajumbe 19,337. Mikutano hii ilifanyika katika kila Halmashauri ya Wilaya, Halmashaurio ya Manispaa na Jiji na mkutano mmoja ulidumu kwa wastani wa siku tatu. Kati ya mikutano hii, jumla ya mukutano 116 ulifanyika Tanzania Bara na 13 ilifanyika Tanzania Zanzibar.

'CASH MONERY' WATOA MSAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA TEMEKE

Wana kikundi cha Cash Money wakiwa tayali kwa kutoa msaada katika hospitali ya Temeke
Mlezi wa Kikundi cha Cash Money ,Ratifa Masasi kulia akimkabibi muhuguzi wa wodi ya watoto bi, Nuswe Ambokile zawai mbalimbali walizoleta kwa ajili ya watoto waliolaza katika hospital ya Temeke
Baadhi ya wana kikundi cha Cash Money wakiwa katika picha ya pamoja na wahuguzi wa word ya watoto Hospitali ya temeke baada ya kukabidhi msaada


Na Mwandishi Wetu
MSANII nguli wa muziki wa dansi aliyestaafu, Muhidini Gurumo, atapanda
jukwaani leo kutumbuiza na mkewe, sambamba na kupewa zawadi za
heshima.

Gurumo atatoa  burudani hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaaga mashabiki,
ambapo shughuli hiyo itaambatana na uzinduzi wa kundi la Cash Money,
la Tandika mjini Dar es Salaam.

"Tumeandaa zawadi kwa mzee Gurumo kutokana na heshima kubwa aliyonayo
katika tasnia ya muziki na kujenga maadili kwa taifa kutokana na
nyimbo zake.

Hivyo zawadi zetu zitaenda sambamba na uzinduzi, ambapo tumepanga
hivyo, ili lee mwenye chochote ampe mzee wetu,"Aliongeza Latifa Masasi
mlezi wa kundi hilo.

Uzinduzi huo unafanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Aziz
Ali, Dar es Salaam na utapambwa na bendi mbalimbali za taarabu
zikiwemo Coast na G Five.

Kundi la Cash Money ambalo lilianzishwa mwaka 2011, pia limetoa vitu
mbalimbali kwa wodi ya watoto, na vituo vya watoto yatima jana, ikiwa
ni sehemu ya uzinduzi huo
Mlezi wa kikundi cha Cash Money akimfaliji mama Samir Nassoro, Naomi Ramadhani walipokutana wakati kundi hilo likitoa msaada kwa wagojwa katika hod ya watoto
Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Cash Money wakimfariji Bi Naomi Ramadhani
Msanii wa bendi ya Msondo ngoma Saddy Ally katikati akisalimiana na wanakikundi cha cash money walipokutana katika hospitali ya Temeke wakitokea kutoa msaada
Wana kikundi wa chass money kushoto Amina Uredi 'Mmanyema ' na Zulfa Kasongo
Mlezi wa kikundi cha cash money bi, Ratifa Masasa akimfariji mtoto Salimu Ally wakati walipokwenda kutoa msaada katika hospitali ya temeke dar es salaam mwingine ni mama mtoto Tabu Salumu mkadhi wa Tandika

BAADHI YA MAGAZETI LEO, SEPTEMBA 26, 2013








©2013 theNkoromo Blog

MAPAMBANO YA MAISHA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, akiwa amebeba mzigo wa mihogo na ndizi kichwani kutafuta wateja, katika mtaa wa Lumumba jijini, kama alivyonaswa na kamera ya theNkoromo Blog leo

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MARA KWA KISHINDO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya sanamu ya mfano wake kutoka kwa Ndugu Elia Bugurilo Kamoga.

Josephat Amon Muruga akiwa na wenzake sita baada ya kujiunga na CCM wakitokea Chadema.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa anavuka na kivuko cha MV Musoma kutoka Kinesi kuelekea Musoma mjini,Kivuko hicho ambacho kimekuwa  mkombozi  wa usafiri kinauwezo wa kubeba abiria 330.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu vazi la kujiokoa wakati wa hatari wakati wa kuvuka  na kivuko cha MV Musoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Balozi wa shina namba 6 Tabitha Edgar wa kata ya Kitagi.
Balozi wa nyumba kumi Tabitha Edgar wa shina namba 6 kata ya Kitagi akitoa shurani zake za kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abbulrahman Kinana.
Katibu Mkuu akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria uliopo eneo la Bukanga(Makoko) mradi huo utakamilika katikati ya mwaka ujao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akikagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji huku akipatiwa maelezo na mhandisi Jairos Chilema ,mradi huo utakuwa na bomba kubwa la kilomita tisini na ukikamilika utaondoa kabisa tatizo la maji Musoma Mjini.

KAMA UNAKUMBUKA ENZI ZA REDIO TANZANIA DAR ES SALAAM,

Sep 25, 2013

Mdau unaweza kuzungumzia nini kuhusu watangazi hawa wa enzi za Redio Tanzania Dar es Salaam?

BAADHI YA MAGAZETI LEO, SEPTEMBA 25, 2013

MDAU KAMA UNATAKA KUONA VICHWA VYA HABARI KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO, TAZAMA SLIDE YA MAGAZETI HAYO, HAPO JUU YA COLUNMS UPANDE WA KULIA NA KAMA UNA MAONI TAFADHALI TUPIA KWENYE ENEO LA MAONI CHINI YA MAELEZO HAYA.
Mtayarishaji Mkuu, TheNkoromo Blog

THE LEGEND IS BACK 1ST ANNIVERSARY

Siku tunayoisubiri kwa hamu inawadia J'mosi hii. The Legend is Back first anniversary. Project ilianza kwa support yenu na ni mwaka sasa tunatimiza kwa sapport yenu. Tulianza pamoja karibu tujumuike tutimize mwaka tukiwa pamoja. Siku hii muhimu itaambatana na shindano kali la disco dancing toka kwa mabingwa wa zamani kuiwakilisha Morogoro Maneno Ngedere na toka DSM Athuman Diga Diga. Vile vile wakali wa chacha Africa Mashariki Moddy Jazz B na Sunday Boy watachuana vikali. Utakuwa vilevile na special moment of silence kuwakumbuka malegendari wa disco waliotutangulia mbele ya haki. Usikose mwana!, Ni J'mosi hii ya 28/9/2013 ndani ya Isumba Lounge. Wote mnakaribishwa
ยช