.

SHAIRI MWANANA

Oct 31, 2013

YARABI MPE UZIMA HASIDI WA MOYO WANGU
 
Yaarabi mpe uzima, atukie kunipenda
kila akinitizama, huku wakiuma vyanda
yarabi mpe uzima, yule hasidi wangu
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
yakale tangu dahare, anijua namjua
nina moyo sina jiwe, hakika alinitesa
nyonda ufanye hima, moyo wangu wateketea
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
hidaya anishushie, hasidi ashuhudie
matozi yammwaike, yungali hali ayaone
haya hatukuoneana, anijua namjua
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
chakula niliona sumu, mapendo yaliniadhibu
mapendo aliyashika, mimi kaniadhibia
naleo nasadiki, kweli hayana dawa
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
takadiri siwezi kuepuka, tasubiri siku itafika
kunihasidi ndo yake kazi, usiku kwa mtana
wema wake wa mshumaa, sasa ateketea
yarabi mpe uzima,hasidi wa moyo wangu
 
yarabi mpe uzima,nimuone mwisho wake
njiani tukipishana,matozi yammwaike
jangili wa moyo wangu,hasidi aso hisani
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
kalamu naweka chini, karima akuangaze
dhulumu ulonitenda, kwako nimeyashiba
kunihusudu wazi, nikuone mwisho wako
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu.
 
Mshairi: Hemed I. Kivuyo

RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA LONDON

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete(Right), British Prime Minister David Cameron(left), Indonesia Vice President Boediono(second left) and Warren Krafchick during the opening plenary session of Open Government Partnership 2013v Summit held at Queen Elizabeth II Conference Centre in London today. (Photo by Freddy Maro).

TIMU YA SOKA YA UHURU FM YAPIGWA TAFU NA DIWANI MALEMBEKA

 Diwani wa Kata ya Msongola, Ukonga, Dar es Salaam, Angel Malembeka (kulia) ameipiga tafu timu ya soka ya Uhuru FM, kwa kuipatia jozi mbili za jezi na mipira miwili ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano baina ya timu hiyo na kata yake. Pichani, Diwani huyo akikabidhi vifaa kwa uongozi wa timu hiyo, Angel Alikimali na Furaha Luhende, katika hafla fupi iliyofanyika nje ya Jengo la CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo. Wakati Luhende ni Mwenyekiti wa timu hiyo,  Akilimali ambaye ni Kaimu Mkurugebzi Mtendaji wa Uhuru FM ni mlezi wa timu hiyo.
 Akilimali akimshukuru Masala Mabula ambaye ni mchezaji aliyeibuliwa kipaji chake katika michuano ya Malembeka Cup iliyomalizika hivi karibuni ambaye sasa anajiandaa kwenda Msumbiji kucheza soka la kulipwa. Masala alifuatrana na Diwani huyo (kulia)
Luhende na Akilimali wakifurahia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na diwani
 Diwani na Akilimali wakiwa na baadhi ya waandishi na watangazaji wa Uhuru baada ya makabidhiano hayo.
Mtangazaji wa Uhuru FM, Mhina Dungumalo akimhoji diwani huyo baada ya makabidhiano

ETI JAMANI HII NDIYO CHADEMA?

Oct 30, 2013

ARUSHA, Tanzania
SAKATA la kupigwa na kusimamishwa kwa uanachama kwa mwenyekiti wa Chadema Arusha Samson Mwigamba kwa tuhuma za usaliti wa chama limeendelea kuzua kizazaa baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Arusha Dominick Mboya kusema chama hicho kimejaa udikteta na kutaja orodha ya viongozi na wanachama waliowahi kufanyiwa umafya.

Mboya ambaye awali alikua mwenyekiti wa chama hicho kata ya Elerai amese leo kwamba tukio hilo lililomkuta Mwigamba liliwahi kumkumba hata yeye pale alipokua akiungana na Mwigamba katika kudai utekelezaji wa katiba ya chama kwa kudai kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi mkoa wa Arusha.

Alisema wakati huo Mwigamba alikua ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa yeye akiwa mwenyekiti wa kata hali iliyosababisha viongozi wakuu wa chama hicho kujaribu kuwanyamazisha hadi kufikia kupewa rushwa ya cheo cha uenyekiti wa wilaya bila kufanyika kwa uchaguzi.

Alisema siku chache kabla ya kuelezwa kuhusu uteuzi wake wa uenyekiti ambao ulikua kinyume na katiba alipigiwa simu na kiongozi mmoja akitaarifiwa kupewa nafasi hiyo na kutakiwa kuhudhuria mkutano uliofanyika katika hoteli ya Stereo ili atangaziwe rasmi yeye na wanachama wengine.

Alisema mara baada ya kufika katika mkutano huo alitamkiwa kuhusu uteuzi wake hali ambayo pia hakuifurahia kwakuona kama amekuwa msaliti wa wanachama na viongozi wenzake waliokuwa wakipambania kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi kama katiba inavyotaka.

Alisema baada kuona hilo alikata waziwazi uteuzi huo kwakua umekiuka katiba kwakua hakuna mwenyekiti wa kuteuliwa bali wa kuchaguliwa na pia atakua msaliti kwa kukubali rushwa ya cheo ili kufumbia macho ukiukwaji wa katiba.

Alisema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho viongozi wote wa kuteuliwa wanakaa madarakani kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja kisha uchaguzi kufanyika lakini kwasasa anashangaa kuona viongozi wa kuteuliwa wanakaa madarakani milele.

Aliongeza kuwa mara baada ya kukataa cheo hicho alitolewa katika ukumbi huo kwa vurugu chini ya ulinzi wa vijana wa ulinzi wa Red Briged ambapo pia walimpora mali zake mbalimbali zikiwemo simu mbili pamoja na fedha taslimu.

Alisema tukio la Mwigamba siyo la kwanza na wala halitakua la mwisho kwakua wapo wanachama na viongozi wengi tu waliofukuzwa,kutekwa na kuporwa pindi wanaposema ukweli au kukosoa uongozi wa juu wa chama hicho.

Aliwataja viongozi waliofanyiwa umafya kuwa ni Bakari Kasembe aliyekuwa katibu wa chama hicho wilaya ya Arusha na katibu mwingine aliyefuatia aliyemtaja kwa jina moja la Credo pamoja na Gerald Majengo aliyekua mwenyekiti wa chama hicho kata ya Terati.

Pia aliwataja vijana wawili wa Red Briged waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM baada ya kutekwa na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ambao ni Nicholaus Kiyeuyeu baada ya vijana hao kutofautiana kimawazo na viongozi wa chama hicho ngazi mbalimbali.

“huku Chadema bwana ukiwa msema ukweli na muwazi katika baadhi ya mambo yanayowahusu viongozi utapigwa tuu siyo kama vyama vingine vilivyokomaa kama CCM hakuna mambo haya wala hakuna udikteta”alisema Mboya.

Alisema kutokana na vitendo hivyo viongozi na wanachama wengi akiwemo yeye wameamua kujiweka pembeni ili kujionea vitendo viovu vinavyofanyika ambapo aliahidi kumpokea Mwigamba katika kambi yao ya waliojiengua kutoka Chadema.

KAMPUNI YA BRAVO YAWAPATIA KAZI DUBAI WATANZANIA WENGINE WAWILI


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bravo Job Centre, Jaffar Kingwande (kulia), akimkabidhi tiketi Amisa Ally (22), ya kwenda Dubai kufanya kazi ya ndani aliyotafutiwa na kampuni hiyo. Anayeshudia hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Mohamed Omar. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

 Jazira Rashid akipatiwa tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda Dubai kufanya kazi aliyotafutiwa na kampuni hiyo. Amisa na Jazira wakiwa na baadhi ya maofisa wa Bravo pamoja na wadhamini wao

Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Omar akifafanua jambo wakati wa kuwaaga wafanyakazi hao

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA BALOZI SEPETU, ZANZIBAR

ZANZIBAR, Tanzania
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaongoza viongozi na mamia ya wananchi wa Zanzibar katika mazishi ya mwanasiasa na mwanadiplomasia mkongwe Balozi Issac Abraham Sepetu yaliyofanyika huko kijijini kwake Mbuzini, Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi unguja.  
Serikali katika salamu zake zilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed imesema kuwa Marehemu Balozi Sepetu atabaki katika nyoyo za wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla kutokana na mchango wake katika kulitumikia Taifa.  
Waziri Aboud alimuelezea Balozi Sepetu ambaye katika uhai wake alishika nafasi mbali mbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa mtu aliyeitumika nchi yake kwa uadilifu na uaminifu mkubwa hivyo msiba huo si wa familia tu bali kwa wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania.  
Alisema Serikali na wananchi wa Zanzibar wamepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa hayati Balozi Sepetu na kuwaomba wanafamilia kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezi.  
Akitoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mazishi hayo  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe alisema Rais Jakaya Mrisho wa Kikwete ameguswa sana na kifo cha Balozi Sepetu ambaye aliwahi kufanya nae kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje kwa miaka kumi.  
Alisema kifo chake ni pigo kwa taifa na daima watanzania watamkumbuka sana Balozi Sepetu na kubaki katika nyoyo zao kutokana na utumishi wake bora kwa taifa.  
Akisoma wasifu wa Balozi Sepetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitega Uchumi-ZIPA nchini Khamis Salum alieleza kuwa maraeehmu Balozi Sepetu alizaliwa tarehe 16 Oktoba, 1943 huko Tabora alipata elimu yake ya msingi na sekondari katika skuli ya Mtakatifu Joseph mjini Unguja ambayo sasa inaitwa Tumekuja.  
Mwaka 1966 alikwenda iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwa masomo hadi mwaka 1970 ambapo alihitimu shahada ya pili katika Uchumi na sayansi ya siasa. Aliporejea nyumbani aliteuliwa kushika nafasi ya Meneja Msaidizi Mkuu wa Shirika la Shirika la Biashara Zanzibar BIZANJE.  
Kabla ya kwenda masomoni nchini Ujerumani marehemu alifanyakazi katika Idara ya Habari na Utangazaji Zanzibar na aliwahi kuwa Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Kweupe ambalo llianzishwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume.    
Balozi wa Sepetu aliwahi kushika nyadhifa za Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Habari na Utalii katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi wa Tanzania katika Shirikisho la nchi za Kisoshalisti la Kisovieti wakati huo na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo wakati huo ikiitwa Zaire.  
Katika Serikali ya Zanzibar aliwahi kuwa Kamishna wa Tume ya Mipango, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mipango.Mwaka 2000 alichaguliwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki hadi mwaka 2005. Hadi anaaga dunia Balozi Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ZIPA.  
Marehemu Balozi Sepetu ameacha wajane wawili, watoto na wajukuu.    
Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi pamoja na wageni mbalibali kutoka Tanzania bara. 
wakati huo huo mamia ya wakaazi wa mji wa Zanzibar walitoa heshma zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu mapema asubuhi huko katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo mjini Unguja
Mwili wa marehemu uliwasili kwa boti mapema asubuhi ukitokea Dar es Salaam ambako Balozi Sepetu mauti yalimkuta.
Baadae mwili ulipelekwa katika Kanisa la Roma la Minara Miwili lililopo Shangani mjini hapa kwa misa.

PICHA ZAIDI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,  akiwa na viongozi wengine akiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Mohamed Gharib Bilali,katika Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu, yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo,  alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu, yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Padri wa Kanisa Katoliki la  Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, akiuombea mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu, ukitemshwa katika kaburi wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo.

DK. BILAL AGUNGUA KONGAMANO KUJADILI MTANDAO WA MAJI KWA NCHI ZA SADC, LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua rasmi kongamano la kujadili Mtandao wa maji kwa Nchi Wanachama wa SADC, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leoJijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua rasmi kongamano la kujadili Mtandao wa maji kwa Nchi Wanachama wa SADC, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leoJijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa 'local Organizing Commitee', Prof. Mtalo Felix, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
   Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
   Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya kufungua rasmi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bashir Mrindoko, wakati akiondoka baada ya picha ya pamoja na kufungua Kongamano la kujadili Mtandao wa maji kwa Nchi Wanachama wa SADC, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leoJijini dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Prof. Mtalo Felix, wakati akiondoka baada ya picha ya pamoja na kufungua Kongamano la kujadili Mtandao wa maji kwa Nchi Wanachama wa SADC, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leoJijini Dar es Salaam.

NATURE, SNURA, FIVE STARS, MWANAHAWA KUUPAMBA USIKU WA KUMTOA MALKIA KOPA DAR LIVE

WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KONYAGI WALIOKWENDA KUONA MECHI YA BARCELONA NA REAL MADRID,HISPANIA WAREJEA WAKIWA NA BASHASHA TELE


Mfanyakazi wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Khadija Madawili ambaye alikuwa kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa TDL waliokwenda kushuhudia pambano la Ligi ya La Liga ya Hispania kati ya Barcelona na Rael Madrid, akirejea jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Wafanyakazi watano wa TDL, waliteuliwa baada ya kampuni hiyo kushinda  Tuzo ya SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13)

 Joseph Chibehe (kushoto) akilakiwa na mkewe baada ya kuwasili

                                             Chibehe akiwa na furaha baada ya kulakiwa na mkewe


 Bavon Ndumbati (kushoto), akilakiwa na ndugu yake. Katikati ni Michael Mrema

                                                              Bavon akiwa na furaha

                                                                 Mwesiga Mchuruza.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (katikati), akiwa na mabosi wa kampuni mama ya SABMILLER AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya  MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13).KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd, (KONYAGI) ambayo ni miongoni mwa kampuni tanzu za Kampuni ya Sabmiller South Africa, imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13). Sabmiller inamiliki zaidi ya viwanda 60 vya bia na vinywaji vingine duniani.

Baada ya ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TDL, Mgwassa ambaye alipambana mpaka kupata ushindi huo, aliamua kuwazawadia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, kwenda Hispania kushuhudia pambano la timu kubwa za Barcelona na Real Madrid lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Wafanyakazi waliokwenda Hispania  na kurejea jana usiku kwa ndege ya Afrika Kusini ni; Joseph Chibehe, Khadija Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesiga Mchuruza.

Wafanyakazi hao, walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, walionekana kuwa na bashaha na kupokelewa na ndugu zao pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzie,Michael Mrema wa Kanda ya Kaskazini, alisema kuwa wanashukuru uongozi kuwapa zawadi hiyo, ambayo imewafanya kuwa na morari mpya wa kazi.

Pia anaseama walifurahi sana kushuhudia mechi hiyo kubwa ya timu za Barcelona na Real Madrid ambapo timu ya Barcelona waliyokuwa wanaishabikia kushinda mabao 2-1.

UNESCO CALL FOR STRENGTHENING EDUCATION ON SEXUAL REPRODUCTIVE HEALTH IN AFRICA

Oct 29, 2013

IMG_1618
Acting UNESCO Country Representative, Abdul Wahab Coulibaly speaks to invited dignitaries during the official launching of the “Young People Today. Time to Act Now” report which highlighted Reproductive Health Services (RHS) to young people in Africa for social well being of the African society across the continent.

By Staff Writer
The United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO) calls for strengthened sexuality education and sexual reproductive health services for young people in Eastern and Southern Africa and Tanzania in general.
Speaking at the launch to invited dignitaries from all UN agencies, government officials and reporters, UNESCO’s Regional Aids Advisor, Dr Patricia Machawira said the poor status of sexuality education and Sexual Reproductive Health (SRH) is evidenced by the high rates of teenage pregnancies in the region.
“For instance, by age 17, at least 20 percent of young women in six of the 21countries in the region have started childbearing, early childbearing often contributes to school dropout and may lead to maternal mortality,’ Dr Machawira
A UNESCO report was disseminated recent urging ministers from Eastern and Southern Africa to respond to continuing high levels of HIV infection, unintended pregnancy and low HIV prevention knowledge impacting on the region’s 158m adolescents and young people.
IMG_1687
Assistant Director from the Ministry of Education and Vocational Training(Diversity Unity) Dr. Laetitia Sayi speaks to invited guests and reporters on behalf of the government on the importance of sexual and reproductive health education to young people in Tanzania and Africa at large.
The 21-country report, “Young People Today. Time for Action NOW” BY UNESCO, UNAIDS, UNFPA, WHO and other bi-lateral partners demonstrates that adolescents and young people especially young women –face a wide range of challenges that compromises their life chances.
Currently, every hour, an estimated 50 young people, again mostly women, become infected with HIV. This makes Eastern and Southern Africa the world’s most affected region.
The report said with 430,000 new infections annually among young people aged 15-24 and an estimated 2.6 million other young people living with HIV in the region.
IMG_1638
UNESCO National Program Officer – HIV & Sexuality Education Mathias Herman who present the progress made by the Eastern Southern Africa Commitment process and snap shot in the region and country summary report.
The report presents findings from 21 countries in the ESA region, covering the health and the social status of adolescents and young people, access to education, HIV knowledge, HIV and unintended pregnancy prevalence and key gender and human rights indicators.
Other key findings in the report include, less than 40 percent of young people know basis information about HIV; key health services are often withheld from adolescents and young people due to their age, marital and legal status and sexual or gender based violence is a reality for up to 35 percent of young women.
The report added that getting education and health ministers to commit to good quality comprehensive sexuality education and access to sexual and reproductive health services is one of the most effective solutions to address the issues affecting young people, whose numbers are expected to increase to 281m by 2050.
As Professor Sheila Tlou, Director of UNAIDS Regional Support, states “it is time for urgent action by our governments, young people and civil society to re-affirm the re-affirm the rights of young people to a better future.
IMG_1610
Acting UNESCO Country Representative, Abdul Wahab Coulibaly display a New Report on adolescents and young people in Eastern and Southern Africa.
IMG_1675
Representative from Pan-African Youth Leaders Network for the UN Jacqueline Maeda gives an overview of the African Focal Point of Youth Ambassadors on HIV/ AIDS issues.
IMG_1710
Udak Bassey-Duke, Youth Sexual Reproductive Healthy and Development Expert from UNFPA, she highlighted that the report recommendations and information focuses on Youth Services in Reproductive Healthy which is their focus.
She added that UNFPA also focuses on Youth who are not in Schools and Unemployed where by the programs empowered them to know the Pros and Cons of sexual education.
IMG_1615
Some of the participants following up the launching ceremony held at UNESCO headquarters in Dar es Salaam.
IMG_1735
Mussa Kalinga from Azania Secondary School contributing a point during the launching of the report in which he said that still teachers in most schools in Tanzania are not widely open about HIV/Aids pandemic and sexual reproductive healthy.
IMG_1627
Session going on.
IMG_1758
UN staff and Youth with the guest of honour pose for a group photo.

WADAU WA WANYAPORI WAKUTANA MKOANI KILIMANJARO LEO KUJADILI MBINU ZA KUKABILI UJANGILI DUNIANI

Kaimu Mkuu wa Chuo cha uhifadhi na usimamizi wa Wanyama Pori mkoani Kilimanjaro (MWEKA), Dkt. Freddy Manongi alkitoa maelezo katika Kongamano la kujadili changamoto na mbinu za kukabili ujangili duniani, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho leo kama ssehemu ya Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Mweka.
Wadau wa Uhifadhi wa Wanyapori kutoka katika nchi 20 duniani, wakifuatilia mafunzo katika Kongamano la kujadili changamoto na mbinu za kukabili ujangili duniani, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho leo kama sehemu ya Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Mweka.

Wadau wa Uhifadhi wa Wanyapori kutoka katika nchi 20 duniani, wakifuatilia mafunzo katika Kongamano la kujadili changamoto na mbinu za kukabili ujangili duniani, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho leo kama sehemu ya Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Mweka.
Mmoja wa Wawezeshaji akiwasilisha mada katika Kongamano la kujadili changamoto na mbinu za kukabili ujangili duniani, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho leo kama sehemu ya Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Mweka.

 
Sehemu ya wadau wa Uhifadhi wa Wanyapori kutoka katika nchi 20 duniani, wakifuatilia mafunzo katika Kongamano la kujadili changamoto na mbinu za kukabili ujangili duniani, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho leo kama sehemu ya Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Mweka.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha uhifadhi na usimamizi wa Wanyama Pori mkoani Kilimanjaro (MWEKA), Dkt. Freddy Manongi alkitoa maelezo katika Kongamano la kujadili changamoto na mbinu za kukabili ujangili duniani, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho leo kama ssehemu ya Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Mweka.
Sehemu ya wadau wa Uhifadhi wa Wanyapori kutoka katika nchi 20 duniani, wakifuatilia mafunzo katika Kongamano la kujadili changamoto na mbinu za kukabili ujangili duniani, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho leo kama sehemu ya Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Mweka.
ยช