.

KIKWETE ATIMIZA AHADI YA KUJENGA DARAJA LA MWANHUZI WILAYANI MEATU

Nov 30, 2013


Picha: Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi John Magufuli kukagua daraja la Mwanhuzi lililoko Meatu Mkoani Simiyu.

SIMIYU, Tanzania
Ahadi ya ujenzi wa daraja la Mwanhuzi katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu imetimia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kulifungua rasmi daraja hilo ambalo ujenzi wake umekamilika na tayari limeanza hutumika.

Awali kabla ya kulifungua daraja hilo Rais Kikwete aliwaasa wananchi wa eneo hilo la Mwanhunzi pamoja na watumiaji wengine kulitunza daraja hilo ili liweze kudumu kwa muda uliokusudiwa na hivyo kuhakikisha panakuwepo huduma hiyo muhimu ya usafiri kati ya Wilaya ya Meatu na Mikoa ya jirani ya Arusha na Singida.

‘Ninawasihi mlitunze daraja hili na asije akatokea mtu kwenda kuanza kukata vyuma au kunyofoa vifaa vingine vya daraja kwani kwa kufanya hivyo mtalidhoofisha ubora wake na hatimaye kuharibika kabisa tukajikuta tunarusi katika kero ya usafiri katika eneo hili kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kujengwa kwa daraja” Alisisitiza Rais kikwete .

Aidha, Mhe. Rais aliongeza kuwa atahakikisha katika kipindi cha miaka miwili kilichobakia akishirikiana na Waziri Magufuli watahakikisha wanafikisha sehemu nzuri ahadi zote za miradi ya barabara katika wilaya hiyo na mkoa wa Simuyu kwa ujumla.

Daraja la hilo lenye urefu wa meta 40 ni kiungo muhimu cha usafiri kuvuka mto Mwanhuzi ambako barabara kuu inayo tokea Kolandoto mkoani Shinyanga kupitia Lalago katika mkoa wa Simiyu na kuelekea mikoa ya Singida na Arusha.

Awali wakati akimkaribisha Rais, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alielezea kuwa usanifu pamoja na usimamizi wa daraja hilo umefanywa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kwa gharama ya Shilingi milioni 13.45 na ujenzi wake umetekelezwa kwa awamu mbili.

”Kukamilika kwa mradi huu ni moja ya ushahidi unaothibitisha kuwa ahadi ulizotoa kwa wananchi zinakamilika popote bila kuangalia itikadi za vyama au watu” alisema Waziri Magufuli

Waziri Magufuli alifafanua kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa daraja hilo ilikamilika mwezi Agosti mwaka 2013 ikiwa imejengwa na Mkandarasi M/S Pet Cooperation kutoka Kahama kwa gharama ya Shilingi milioni 355.58.

Awamu ya pili ya mradi huu ambazo zilianza mwezi Agosti 2013 na kukamilika nwezi Oktoba 2013 zilijumuisha ujenzi wa kingo za daraja. Kazi hizo zillitekelezwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Meneja wa Tanroads mkoa wa Simiyu mara baada ya mkoa huo mpya kuanzishwa. Awamu hii ya pili ilitekelezwa na Kampuni ya Ms Tolerance Engineering Ltd ya Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi milioni 97.55.

Fedha hizo zote zilizotumika katika ujenzi wa awamu zote mbili pamoja na usimamizi ambazo ni jumla ya Shilingi milioni 455.58 zimetolewa na Mfuko wa Barabara (Roads Fund).

NAPE AMTAKA WAZIRI CHIZA KUANDAA MAJIBU KAMATI KUU, BADALA YA KUZUSHA MALUMBANO KWENYE MAGAZETI

NAPE NNAUYE

NA MWAMNDISHI WETU, MBOZI
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amemtaka Waziri wa Kilimo na Chakula, Christopher Chiza kuandaa majibu ya uhakika atakayotoa kwenye Kamati Kuu ya CCM, badala ya kuanzisha malumbano kwenye vyombo vya habari.

Amesema, kuzusha malumbano kwenye vyombo vya habari kulikoanza kufanywa na waziri huyo, hakuleti tija wala faida yoyote kwa Waziri huyo au kwa Watanzania, ila anachopaswa kuafanya ni kujiandaa kwa majibu yenye kuridhisha kwenye kikao cha Kamati Kuu hiyo mwezi ujao.

Nape amesema hayo, jana, alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika, Vwawa, wilayani Mbozi mkoani Mbeya, ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye yupo mkoani hapa, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kutatua kero hizo.

"Baada ya kubaini kuwepo kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika sekta ya kilimo, ikiwemo malalamiko juu ya wakulima kulazimishwa kutumia mbolea ya minjingu ambayo inaonekana kuwa haiwasaidii, tulisema tutaiomba Kamati Kuu ya CCM imwite waziri mwenye dhamana ili atoe majibu
 yatakayosaidi kutoa ufumbuzi wa karo hii", alisema Nape na kuongeza;

"Lakini badala ya kuandaa majibu atakayoleta kwenye Kamati kuu, huyu Waziri tumemsikia kupitia vyombo vya habari akianzisha malumbano yasiyo na tija tena akionyesha kuambana na kejeli, hii siyo sawa".

Akizungumzia kuhusu baadhi ya mawaziri kuitwa kwenye Kamati Kuu, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema, kwenye mkutano huo kwamba, viongozi wa CCM wanapotoa tamko hilo huwa siyo matakwa yao binafsi bali ni utaratibu wa kisheria wa CHama, ambao kwa bahati mbaya ulikuwa umetelekezwa kwa miana mingi.

Alisema, kulingana na utaratibu na mamlaka ambayo CCM inayo kama chama kilichpewa na wananchi dhamana ya kuunda serikali, ni lazima pale kinapoona mambo hayaendi sawasawa kiwaite wahusika na kuwahoji ili kupata majawabu kwa manufaa ya wananchi au taifa kwa jumla.

"NInaposema, kwamba Waziri fulani tutaomba aitwe kwenye Makati Kuu, siyo mimi ninayetaka hivyo, bali ni Chama kinachowaita. Na Ndugu Wananchi suala la viongozi kuhojiwa ni utaratibu wa Chama kuisimamia serikali yake ambao kwa bahati mbaya ulitelekezwa kwa muda mrefu jambo ambalo ni kinyume kabisa", alisema Kinana.

Akiwa katika ziara ya zaidi ya siku 20 kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wanancho na kujadiliana nao njia za kutatua karo hizo katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya, Kinana alitangaza kuitwa kwa mawaziri kadhaa akiwemo Chiza, baada ya kupokea malalamiko mbalimbali zinazohusiana na wizara zao.

Akiwa mkoani Ruvuma, Kinana ambaye anaambatana na Nape na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, alikumbana na malalamiko ya wananchi kuhusu ubaya wa mbolea ya minjingu na pia wakulima hasa wa zao la korosho kukopwa au kucheleshewa malipo yao kwa muda mrefu.

Karika mkoa wa Mbeya ambako yupo sasa akiendelea na ziara hiyo, licha ya kuwepo kero mbalimbali, lakini iliyoonekana kuwanyong'onyesha zaidi wananchi hasa wakulima, ni mbolea ya aina ya minjingu ambayo imeonekana kutowafaa wakulima kiasi cha wengine kuamua kuachana nayo.

KINANA ALIPORNDIMA MBOZI Katibu Mkuu wa CCM  Abdulrahman Kinana akitoka katika nyumba ya mjumbe namba nane, eneo la Mtunduru, wilayani Mbozi, Hongera Myola, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishirki ujenzi wa nyumba ya mganga katika Hospitali ya Isansa, katika Kata ya Mtunduru, wilayani Mbozi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013. Nyuma yake ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishirki ujenzi wa nyumba ya mganga katika Hospitali ya Isansa, katika Kata ya Mtunduru, wilayani Mbozi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013. Nyuma yake ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akiongoza kupanda miti kwenye eneo la Mtundulu, wilayani Mbozi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013. Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(kulia), Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimartaifa, Dk. Asha-Rose Migiro,  Mbunge wa Mbozi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Kijana Huruma William, akimuonyesha 'machejo' ya sarakasi Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (watatu kushoto), alipofika katika kata ya Mtunduru, kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba ya mganga katika hospitali ya Kata hiyo, wilayani Mbozi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013.
 Wasichana na Kinamama wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipowasili katika Kata ya Mtundulu wilayani Mbozi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro, akihutubia wananchi, katika Kijiji cha Isansa, Kata ya Vwawa wilayani Mbozi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipozindua miradi ya maendeleo katika Kata hiyo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013.
 atibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Baraza katika Kata ya Vwawa, wilayani Mbozi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi katika Kata ya Vwawa, wilayani Mbozi, katika ziara ya katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013
 Wananchi hadi barabarani kumsikiliza Kinana
Mama wa Kinyiha, akiwa amejipamba usoni na kuwa kivutio cha aina yake, kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, aliofanya katika Kata ya Vwawa, wilayani Mbozi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wanannchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Mbeya, Nov 29, 2013.

MABONDIA JAPHET KASEBA, ALIBABA KUZIPIGA DESEMBA 21 FRIENDS CORNER HOTEL DAR

Mabondia Japhet Kaseba wa jijini Dar es Salaam, na Alibaba Ramadhan wa jijini Arusha, wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21 Decemba, mwaka huu katika ukumbi wa friends corner hotel,kuzichapa katika pambano la ubingwa wa pst

Pambano hilo liloandaliwa na Promota Ibrahim Kamwe chini ya  BigRight Promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia kama Karage Suba na Fadhil Awadh, watakaozichapa kuwania ubingwa wa Mkoa katika uzito wa wealter Kg66 pambano la raundi kumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe, alisema kuwa  zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa, pia mahasimu wawili wa uzito wa juu Lusekelo Daudi atazipiga na  Mbaruku Kheri (ndota) ikiwa ni marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi.

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni pamoja na Bondia Adam Yahaya (Baby Edo) atazipiga na Harman Richard, mkongwe Enerst Bujiku (Tyson) atacheza na Shah Kassim,  kukumbushia Enzi za akina Stanley Mabesi , Jocky Hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena Rajabu.

Wengine ni Issa Omar  atazipiga na Haji Juma wa Tanga, Moro Best atapigana na Shafii Ramadhan, huku Shaban Bodykitongoji akizipiga na Mwinyi Mzengera.

Mabondia wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huo na wameshaingia kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.

kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi kutoka Kampuni ya Kiwango Security na jeshi la polisi amblo limeahidi kutoa mchango mkubwa ili kufanikisha pambano hilo.

MWANA WA MANGULA AZIKWA

Nov 29, 2013
PIKI PIKI YA MABONDIA NASSIBU RAMADHANI NA MOHAMED MATUMLA YAONESHWA

Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25 katika ukumbi wa friends corner wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mratibu wa mpambano wa ndondi Kaike Siraju akiojiwa akiwa juu ya pikipiki itakayogombaniwa na mabondia Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani siku ya Desemba 25 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

KINANA AWASILI MBOZI ASUBUHI HII

 Vijana wa CCM wa Tawi la Mpemba, wilayani Momba, Mbeya, wakiwa na hamu ya kumsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye na msafara wake walikuwa wanakwenda wilayani Mbozi kuendelea na ziara ya kuimarisha chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kusikiliza kero za wananchi.

 Wafuasi wa CCM wakishangilia wakati Katibu wa NEC wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza nao aliposimama kwa muda katika shina la Vijana wa CCM la Mpemba akiwa njiani kwenda wilayani Mbozi, akitokea wilayani Momba.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wafuasi wa CCM katika Tawi la CCM la Mpemba, wilayani Momba.

 Kinana akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alipowasili mjini Mbozi leo.

 Msanii wa kikundi cha ngoma cha Hakuna Kulala, Catherine Kapessa akipuliza baragumu wakati wa mapokezi ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Ofisi za CCM

 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimia baadhi ya viongozi wa CCM msafara wa Kinana ulipowasili Ofisi ya CCM Mbozi leo

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma iliyokuwa ikipigwa na wasanii kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya leo

CCM YAFANYA KUFURU TUNDUMA JIONI HII, MAELFU WAFURIKA MKUTANONI, WAMBEBA NAPE JUU KWA JUU

Nov 28, 2013

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutumia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, mjini Tunduma, wilayani Momba, jioni hii, Nov 28, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza nao njia ya kuzitatua, katika mkoa wa Mbeya.
 Wananchi wakiwa wamembeba Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye 'akihutoa dozi' alipohutubia katika mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa 'dozi' katika mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano uliofanyika  Uanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma,leo
Baadhi ya vijana wakiwa juu ya miti kuhakikisha wanaowaona viongozi wakati wa mkutano huo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati mwenye  miwani) akiselebuka na wananchi kwenye mkutano, Uwanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma leo
Kinana akizungumza na Kijana Martin Thomas (38) mjini Tunduru, aliyezaliwa bila mikono, mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na mbunge wa Mbozi Ndugu Zambi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiondoka Uwanjani baada ya mkutano huo kumalizika akiwa ametawazwa kuwa chifu wa moja ya makabila  maarufu ya Mbeya

WAANDISHI WA HABARI WA ZAMANI UHURU/MZALENDO WAKUMBUKA ENZI ZAO

Waandishi wa habari wa zamani wa Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani Abihudi Saideya (kushoto) na Laudem Mwambona waakionyesha furaha walipokutana leo, kwenye ukumbi wa  Uwanji, kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, katika wilaya ya Momba mkoani Mbeya. Wakati Saideya kwa sasa ni Mkuu wa wilaya ya Momba, Mwambona amehamia katika magazeti ya Mwananchi.

USAFI WA MITARO ENEO LA MAKUMBUSHO IMEKUWA TATIZO KUBWA,MAGONJWA YA MLIPUKO YANAWEZA KUTOKEA

Huu ni mtaro ambao umeziba na maji hayaendi,na watu kutupa uchafu ndani yake kama unavyoonekana.
Juu ya huo mtaro kuna mgahawa wa chakula,ambao watu wanautumia kwa mahitaji ya chakula.
Kama picha inavyoonesha maji machafu yakiwa yametuama,na uchafu ukiwa umetupwa ndani yake.
Ikifika mchan watu hukaaa hapo juu na kupata chakula hii ni hatari kwa afya ya binadamu.

Ukifika maeneo ya makumbusho nyuma ya Jengo la Tigo maarufu mtaa wa kwa bwela kwa wauza viatu maarufu kwa wakina dada,hali ya usafi katika mitaro ya eneo hili ni ya kutisha ingawa imezungukwa na maofisi makubwa kama kampuni za simu na mabenki mengi.Dj sek blog ilifanya utafiti makini na kujione hali ya mitaro hiyo ikiwa katika hali mbaya kiusafi,Kwanza mitaro hiyo imeziba hivyo kusababisha maji kutuama na kupelekea maji hayo kuvunda na kuwa rangi ya njano.


Kingine cha kushangaza zaidi ndani ya mitaro hiyo watu hutumia kama sehemu ya kutupia uchafu kama mifuko ya rambo,makopo n,k.Jambo lingine ambalo ni la hatari zaidi ni eneo la juu ya mitaro hiyo kuna mgahawa ambao unauza chakula kwa ajili ya matumizi ya binadamu.Jambo la kujiuliza je watoa huduma katika mgahawa huo hawaoni hali hiyo ya uchafu ambao upo kwenye eneo lao?na je hawaoni kwamba ni hatari kwa afya za binadamu wanaokula eneo hilo?Tulipojaribu kuwauliza walikuwa hawana majibu ya kutoa.Tunaomba serikali ya mtaa wa makumbusho walione hili na kulishughulikia na sio kukaa ofisini mpaka magonjwa yatokee ndipo tuanze kuhangaika. PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DJ SEK BLOG

DUNIA MZOBORA KUZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU, DAR ES SALAAM

DUNIA MZOBORA
DAR ES SALAAM, Tanzania
MHARIRI Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Dunia Mzobora, ambaye amefariki dunia jana, anazikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam

Habari zimesema Mzobora (49), ambaye alifariki dunia ghafla jana saa 12 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi, akitokea Hospitali ya Aga Khan pia ya Dar es Salaam, anazikwa leo saa 7 mchana katika makaburi hayo

Mussa, mdogo wa marehemu, alisema jana kuwa Mzobora alianza kujisikia vibaya juzi usiku  nyumbani kwake,Tabata Mawenzi na kupelekwa Aga Khan, lakini hali ilizidi kuwa mbaya na ndipo alipopelekwa Muhimbili. Alifariki muda mfupi baadaye wakati madaktari wakiwa katika harakati za kuokoa maisha yake.

Mzobora, ambaye hadi anafariki dunia alikuwa Naibu Msanifu Mkuu wa Uhuru, alifanya kazi hadi kumalizika kwa gazeti la Uhuru toleo la jana, akikaimu nafasi ya msanifu mkuu, akiwa buheri wa afya.

Taarifa zilizopatikana jana kutoka kwa ndugu wa familia, zilisema maziko ya marehemu yatafanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mzobora, ambaye alizaliwa Aprili 6, 1964 Mwandiga mkoani Kigoma, alijiunga na Uhuru Publications Limited mwaka 1989, akiwa mwandishi wa habari mwanafunzi, baada ya kumaliza masomo ya ualimu ngazi ya cheti kutoka chuo cha Kasulu, mkoani Kigoma.
Kutokana na uwezo wake na kujituma kazini, mwaka uliofuata alithibitishwa kazini na kupandishwa cheo kuwa mwandishi kamili wa habari.

Mwaka 1992, alipandishwa cheo na kuwa msanifu kurasa wa Mzalendo na Burudani chini ya Msanifu Mkuu wa magazeti hayo kwa wakati huo, Hamisi Mkwinda, kabla ya kupandishwa na kuwa mwandishi wa habari daraja la pili mwaka 1994.

Mwaka 1995, alijiunga na kilichokuwa Chuo cha Uandishi wa habari cha Nyegezi (sasa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine), Mwanza na kuhitimu stashahada ya juu ya uandishi wa habari mwaka 1998.

Baada ya kurejea kazini, alipandishwa vyeo ngazi mbalimbali kuanzia mwandishi mwandamizi daraja la pili na hadi kufariki dunia kwake, alikuwa Mhariri Daraja la Pili.

Miongoni mwa nyadhifa alizoshika ni pamoja na Kaimu Msanifu Mkuu wa Uhuru, Kaimu Mhariri wa Mzalendo na Kaimu Mhariri wa Makala.

Kutokana na kiu yake ya kupenda elimu, mwaka 2006, Mzobora alijiunga tena na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Mwanza kwa masomo ya shahada ya uzamili katika mawasiliano ya umma na uandishi wa habari. Marehemu ameacha mke na watoto.

Wakati huo huo; Rais Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za pole Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, kufuatia kifo hicho.

“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha mmoja wa Waandishi wa habari shupavu na mchapakazi, Dunia Mzobora aliyekuwa akilitumikia Gazeti la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la UHURU,” alisema Rais Kikwete.

Alisema alimfahamu Mzobora, enzi za uhai wake, kama Mwandishi wa Habari aliyejituma katika kazi zake za kuuhabarisha, kuuelimisha na kuuburudisha Umma kwa kutumia vyema kalamu yake.

Katika salam hizo, Rais Kikwete ametoa pole pia kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Uhuru na Waandishi wote wa habari nchini, kwa kumpoteza mwenzao waliyekuwa wakifanya naye kazi kila siku.

“Aidha, kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu Dunia Mzobora kwa kumpoteza baba, kiongozi na mhimili wa familia,” alisema Rais Kikwete.

Amewahakikishia wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba wa mpendwa wao, na anamuomba  Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu, Amina.

Amewataka wawe na moyo wa uvumilivu, utulivu na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia baada ya kumpoteza mtu muhimu aliyekuwa kiungo cha familia yao, kwani yote ni mapenzi yake Mola.

RAIS KIKWETE AKAGUA NA KUZINDUA MIRADI MKOA MPYA WA SIMIYU

 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(watatu kushoto),Mbunge wa Bariadi  Mhe. Andrew Chenge(kushoto)pamoja na viongozi wengine w akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko enelo la Old Maswa mkoa mpya wa Simiyu jana.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Old Maswa muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya kilometa ya Bariadi-Lamadi 71.8 huko eneo la old Maswa, Mkoani Simiyu.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Umeme katika kijiji cha Nkololo wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu leo.Weninge katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. Steven Masele, Mbunge wa Bariadi Mhe.Andrew Chenge(wapili kushoto),Paroko wa Nkololo Padri Paulo Fegan(wanne kushoto) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bwana Saguda Kasili mlemavu ambaye pia ni mtendaji wa kijiji cha Ng’wang’wali leo wakati aliposimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi wa eneo hilo
ยช