.

KUELEKEA KATIBA MPYA: TAASISI ZA KIJAMII, VYAMA VYA SIASA NA VYA KITALUUMA VYAPELEKA MAJINA 50 KWA RAIS KWA AJILI YA MCHAKATO WA BUNGE LA KATIBA

Dec 31, 2013

IKULU, DARES SALAAM
Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba 31, 2013, vimewasilisha majina ya watu vinaowapendekeza wafikiriwe kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Taarifa iliyotolewa leo mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue na kusambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu pia Dar es Salaam, imesema taasisi hizo zimewasilisha majina yao kwa mujibu wa mwaliko uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa makundi yaliyobainishwa katika Kifungu cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83).

Taarifa hiyo imesema kuwa makundi hayo 50 yaliyowasilisha majina yanayopendekezwa kwa ajili ya uteuzi yanatokana na barua 169 zilizopokelewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.

Makundi ambayo yamewasilisha majina ni yafuatayo: Shirika la Wasaidizi wa Jamii Kabila la Wagogo, Tanzania Association of Social Workers (TASOWA), Teachers and Student Forum Tanzania, Tanzania Women Teachers Association, Umoja wa Wanawake Wajane Wilaya ya Karagwe na Kyerwa (UWK), Tanzania Peace and Development Society, Better World Organization (BWO), Youth Focus and Development, Association of Traditional Medicine Man, Registered Centre for Good Governance and Development in Tanzania, Chama Cha Kijamii (CCK), CHANETA na Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania.

Makundi mengine ni Legal Aid Iringa Village, Tanzania Kilolo Orphans and Social Development Organization, Legal aid and Social Welfare Association, Legal and Human Right Centre, Tanzania Lift Initiative NGO, Kilolo Paralegal Unit, Women Development and Social Activities Association, Defence of Human Right/Citizen Rights, DAWSEN Trust Fund, Baruti Development Association (BADEA), Living Hope Ministries Trust, EFATHA Ministry, Bethel Assemblies of God Tanzania, Muslim and Christian Brotherhood Society, Baraza Kuu la Waislamu wa Kondoa – Tanzania na Jesus Temple Inner Transformation News.

Taasisi nyingine ni Jumuiya ya Waithna Asharriyyah Tanzania,   Rehmatfi Sabilillah Trust of Tanzania,  Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), National Reconstruction Alliance (NRA), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia Makini, African Progressive Part – APPT Maendeleo, National League for Democracy, Tanzania Film Federation, Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni, Al-Amoud General Enterprises, Blue Belt and Water Sources Control, Community Development Training Institute – Tengeru,  Tanzania Medical Student Association, Tanzania Sea Farmers Union, Medical Association of Tanzania, Chama cha Wastaafu wa Mbinga, Union of Tanzania Press Clubs, Umoja wa Wanawake Tanzania, Alliance for Tanzania Farmers Party, Tanzania Social Economic and Environment and Wellbeing.

Kwa vile mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo ni tarehe 02 Januari, 2014, Balozi Sefue ametoa mwito kwa makundi mengine ambayo hayajawasilisha orodha hiyo kufanya hivyo kabla muda uliowekwa kuisha. Aidha, wakati wa kuwasilisha ni muhimu kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sheria na kama vilivyofafanuliwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 443 lililochapishwa tarehe 13 Desemba, 2013. Vilevile ni muhimu kuzingatia kuwa majina yanayopendekezwa na Taasisi au makundi yaliyoainishwa kwenye sheria na siyo mtu binafsi kujipendekeza mwenyewe.

 Kwa wale watakaojipendekeza wenyewe wajue kuwa watakuwa wanakwenda kinyuma na maelekezo.

AMIRIJESHI MKUU, RAIS JAKAYA KIKWETE AMWAPISHA MKUU MPYA WA JESHI LA POLSI TANZANIA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, leo jioni
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Abdulrahman Kaniki baada ya kumwapisha katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, leo jioni
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali mpya wa Polisi (IGP) Ernest Mangu na Naibu IGP Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo jioni
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali, Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali mpya wa Polisi (IGP) Ernest Mangu na Naibu IGP Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo jioni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Saidi Mwema, katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, leo jioni.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Ernest Mangu, Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Abdulrahman Kaniki. Picha na Ikulu

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AFUNGUA MAKAO MAKUU YA PBZ MJINI ZANZIBAR

RAIS Mstaaf wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi,akikata Utepe kuashiria kuifunga Makao Makuu ya Benki ya  PBZ Ismamic Bank ilioko katika jengo la Bima  Mpirani Zanzibar, kushoto Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee na Mkurugenzi  Mtendaji PBZ Bwa Juma Amour, ikiwa ni shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

RAGE AZIDI KUNG'ANG'ANIWA NA WANACHAMA ANG'OKE SIMBA

Kundi la watu waliojitambulisha kuwa ni wanachama wa Simba, wakizungumza kwenye ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam., kupinga hatua ya Shirikisho la Soka Nchini TFF, kuridhia Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Aden Rage kuiendelea na uongozi. Meza kuu, kutoka kushoto ni Husein Mwaikambo kutoka Iringa, Albino Willa na Fatuma Selemani maarufu wa jina la Hindu. (Picha:theNkoromo Sports)
Baadhi ya waandishi wakiuliza maswali

Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo wa wanachama wa Simba kutaka Rage ang'oke

RAIS KIKWETE AMTEUA MANGU KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI (IGP), ABDULRAHMAN KANIKI NAIBU IGP

Dec 30, 2013

IKULU, DAR ES SALAAM
Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Tanzania, Rais Jakaya Kikwete Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imemkariri Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, akisema kuwa Kamishna Mangu (pichani) anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

"Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi", tarifa hiyo imesema.

Taarifa hiyo imesema kuwa pia Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Taarifa hiyo imesema, Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

CCM YAIPONGEZA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA KWA KUKABIDHI RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA

*Yasema itazitafakari  hoja za Tume na kuamua ipasavyo
*Yasisitiza mchakato utumike kuwaunganisha Watanzania
DAR ES SALAAM, Tanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM),  kimeipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi iliyofanya kuufikisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya hatua ulipofika.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Joseph Warioba, kukabidhi kwa Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya pili ya katiba, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema CCM inaipongfeza Tume kwa sababu imefanya kwa umahiri na juhudi kubwa hadi hatua ilipofikia.

“CCM inaipongeza Tume kwa kazi waliofanya, tunatambua kazi kubwa waliyofanya, wamekamilisha tena kwa wakati na salama, kazi waliyotumwa. Sasa tuwaachie wanaondelea na mchakato yaani bunge la katiba na hatimaye wananchi. Tunautakia kila lakheri mchakato huu, utumike kutuunganisha watanzania badala ya kutugawa” amesema Nape

Kuhusu pendekezo la Tume la muundo wa Muungano wa serikali tatu Nape alisema CCM imesikiliza hoja za tume juu ya sababu za kuendelea kupendekeza muundo wa serikali tatu, imezisikia, itazichukua, kuzipeleka kwenye vikao vya Chama baada ya tafakuri ya kutosha itaamua ipasavyo.

Aidha Nape alitumia nafasi hiyo kuwatakia watanzania kila lakheri kwenye mwaka mpya wa 2014.

RAIS JAKAYA KIKWETE,DK. SHEIN WAKABIDHIWA RASIMU YA PILI YA KATIBA


 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya pili ya Katiba mpya, leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini, Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi.
Jaji Warioba akikabidhi rasimu hiyo pia kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
 Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Rasimu ya Katiba Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya (kushoto) baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Rasimu ya Katiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika hafla hiyo.
 Baadhi ya viongozi wastaafu na waasisi wa Tanzania, wakiwa wameshikilia rasimu hiyo, baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana. Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Job Lusinde, Sir George Kahama, Hassan Nassor Moyo na Jaji mstaafu, Mark Bomani na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya
Baadhi ya wananchi na wanazuoni wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa Rais Jakaya Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein, rasimu ya mwisho ya katiba.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba baada ya makabidhiano ya Rasimu ya pili ya Katika katika viwanja vya Karimjee Hall jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti  wa NCCR Mageuzi,  James Mbatia.
Rais Jakaya Kikwete, Dk. Shein, Dk. Bilal, Maalim Seif Sharif Mahad na viongozi wengine wakiwa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEOKAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA GNSM CONTRACORS CO. LTD INAYOENDESHA NA GEOFREY MUNGAI YATOA MSAADA WA CHAKULA CHA MWAKA MPYA KWA YATIMA TOSAMAGANGA

Dec 29, 2013

Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai kulia akikabidhi msaada  wa chakula na  vitu mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa mlezi wa  kituo cha watoto  yatima cha  Tosamaganga Sisita  Herena Kihwele. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

CCM YAPATA MSIBA SHINYANGA, DIWANI MWINGINE AFARIKI DUNIA

SHUNYANGA, Tanzania
Diwani wa CCM katika kata ya Mwakitolyo, katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Kasanga Lumala (75)  amefariki dunia  baada ya kuugua kwa muda mrefu kifua kikuu.

Taarifa iliyopatikana kutoka mjini Shinyanga, imesema, diiwani huyo alifariki  jana mida ya saa 10 jioni katika hospitali ya mkoa  alikokuwa amelazwa   kwa muda wa siku mbili baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani  wakati akiendelea kutumia  dawa .

Kaimu Mwenyekiti wa  Halmashauri hiyo, Ngassa Sosthenes  amesema hayo, akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga  na kufafanua kwamba katika uhai wake diwani huyo  alisumbuliwa na maradhi ya ugonjwa huo wa kifua kikuu licha ya kwamba alikuwa akipata katika hospitali  mbalimbali.

Alisema, Desemba 26 mwaha huu, walipata taarifa ya kuzidiwa kwa diwani huyo wakaamua kumpeleka haraka katika hospitali hiyo kwa kushirikiana na ndugu zake na madaktari kuendelea kumfanyia uchunguzi zaidi.

Amesema leo mwili  umetolewa  hospitali  na kuumpeleka kwenye kata yake  kwa ajili ya wananchi kwenda kutoa heshima za mwisho kabla ya mazishi kwenda kufanyika  mkoani Geita katika kata ya Mlele  walikozikwa pia wazazi wake.

Kwa mujibu wa Kaim Kwenyekiti huyo wa Halmashauri, Diwani huyo aliyezaliwa mwaka  1937, ameacha watoto saba wajane wawili na amekuwa diwani wa kata hiyo kwa awamu mbili mfululizo tangu mwaka 2005.

Msiba wa diwani huyo umekuja huku msiba mwingine wa Diwani wa  kata ya Nyida  ukiwa bado unaombolezwa na wananchi kufuatia diwani nao  Mshindikwa  Masele (40) kufariki dunia kutokana na ajali ya pikipiki yake aliyokuwa akiiendesha akitokea Isaka wilayani Kahama   Desemba  21, mwaka huu.

SEMVUA: KASI YA MTEMVU INAENDANA NA YA KINANA, NAPE

MWENYEKITI wa CCM Kata ya Kibamba, Ayoub Semvua akimpongeza Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam,  Abbas Mtemvu, baada ya kuzungumza kama mgeni mwalikwa kwenye Kichao cha kawaida cha Hamlashauri Kuu Kata ya Azimio jimboni humo, jana jioni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Esa Uswege.
=================
BASHIR NKOROMO, TEMEKE, Tanzania
Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Kibamba, Dar es Salaam, Ayoub Semvua, amesifu kuwa kasi ya utendaji kazi ya mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu ni kubwa na huenda inastahili kwendana na kasi ya utendaji wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itukadi na Uenezi Nape Nnauye.

"Nilipoitwa na rafiki zangu hawa wa Azimio, sikujua kama na wewe utakuwepo,  lakini nikawa nimenuia kuwa hata kama hutakuwepo nitakusifia kwa kazi kubwa unayofanya ya kimaendeleo katika kutekeleza ilani ya CCM katika jimbo hili la Temeke... na sasa kuwa nimekukuta nitakusifu hapa hapa, wewe kasi yako ya utekelezaji wa ilani ya CCM inatisha, na kwa kasi hii unaweza kuwa unastahili kasi ya viongozi wetu  Ndugu Kinana, Mzee Mangula na Kijana wao Nape", alisema Semvua alipopewa fursa ya kuzungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Azimio, ambacho alikuwa mgeni mwalikwa.

"Huyu Katibu wetu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti Mzee Mangula na kijana wao Nape, kasi yao ni kilometa 140 kwa saa. Kama kuna mtu aliyeingia katika uongozi wa CCM kwa lengo tofauti kasi hii lazima itamshinda na bora ajiondoe mwenyewe mapema",  Semvua aliongeza.

Semvua alisema, kutokana na utendaji bora na shirikishi wa Mtemvu, jimbo la Temeke limekuwa na sura tofauti kimaendeleo ikilingtanishwa na miaka 20 ikiongozwa na wabunge mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa sasa wa TLP, Augustine Mtema ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

"Mfano mzuri wa maendeleo, niliyoshuhudia ambao kila mtu anauona ni barabara za lami zilivyotanda katika maeneo mbalimbali ndani ya Temeke, tangu nimetoka Kibamba nimeteleza kwa lami moja kwa moja bila kugusa udongo hadi naingia kwenye Ofisi hii ya CCM Azimio", alisema Semvua.

Semvua alisema, kutokana na kasi inayoonyeshwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na viongozi wengine kama Mtemvu, CCM itashinda urais ba viti vingi vya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2014.

Aliwataka wana-CCM kuachana na tabia ya kuwa na nongwa aliyoifananisha na ya kinywaji cha kahawa, ambayo baadhi wamekuwa wakidumu nayo kiasi cha kuchagua wapinzani wakidhani wameikomoa CCM kumbe wamejikomoa wenyewe.

"Pale wilaya ya Kinondoni tumepoteza viti viwili vya ubunge na vingi tu vya udiwani na mitaa, sababu kubwa ni nongwa tu. Wanasema, Wakasema aaa,  bora tuupe upinzani tuheshimiane. Sasa ukiwauliza pale Kawe na Ubungo kwamba mliwapa ubunge wapinzani sasa heshima gani mnapata? hawana jibu zaidi ya kuinama chini", alisema Semvua.

Akifungua kikao hicho, Mtemvu aliwataka wana-CCM na wananchi kwa jumla kuwapima viongozi kwa utendaji kazi zao na sio kwa uhodari wa porojo nyingi kwa sababu wananchi wanachohitaji ni maendeleo.

Alisema, katika kipindi chake cha Ubunge, Temeke imeweza kuwa na barabara karibu 15 zenye lami hadi pembezoni mwa mji huo na kwamba zile zisizokuwa na lami zimeboreshwa kwa kiwango kibwa kiasi cha kupitika nyakati zote.

MICHUANO YA NETIBOLI TAIFA YAANZA UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM

Dec 28, 2013

 Mchezaji wa timu ya  Temeke Sekela Mwakanyuki (kulia) akitafuta njia ya kumpenya mchezaji wa Katavi Rose Ezrael, katika mechi hiyo  leo jioni. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Rais Kikwete atembelea na kuwafariji wagonjwa Muhimbili

 Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowatembelea na kuwafariji  baadhi ya wagonjwa katika wodi ya Mwaisela leo. (Picha na Freddy Maro) 

Dec 27, 2013

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI AKITOKEA MAREKANI KUCHEKIWA AFYA
 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake. Akiwa nachini Marekani Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Banki Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal baada ya kuwasili. ((Picha na Freddy Maro)

JAJI WARIOBA KUKABIDHI RASIMU YA KATIBA MPYA KWA RAIS KIKWETE, DK. SHEIN JUMATATU

JAJI WARIOBA
DAR ES SALAAM, Tanzania
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliuko ya Katiba, Assaa Rashid, imesema, Jumatatu ijayo ya Desemba 30, 2013, Tume hiyo itakabidhi rasimu hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

"Tume inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 saa 6:00 mchana katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam", taarifa hiyo imesema.
Taarifa imesema, hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa, Taasisi za kidini, Asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba anatarajia kuwakabidhi Waheshimiwa Marais, ripoti ya mchakato wa Katiba na rasimu ya Katiba.
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, anuani za posta, tovuti (www.katiba.go.tz) na ukurasa wa facebook wa Tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).

WAJUKUU WAMUUA BABU YAO KWA KIPIGO SIKU YA KRISMAS

TABOTA, Tanzania 
Watu wawili wamekamatwa na Polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa tuhuma za mauaji ya babu yao.

Watuhumiwa hao ni Mwashi Mipawa (17) na Kashinje Mipawa(15)wote wakazi wa kijiji cha Ibole kata ya Igurubi wilayani hapa.

Tukio hilo lilitokea Desemba 25 majira ya saa 7:30 jioni katika kijiji cha Ibole kata ya Igurubi wilayani hapa ambapo watuhumiwa hao ambao ni wajukuu walimpiga babu yao Makelemo Jagadi (55) na kusababisha kifo chache.

Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa amelewa pombe na alipofika nyumbani alianza kutukana hali ambayo ilipelekea kuanza kupigana na mke wake Milembe Mpela(50) na ndipo wajukuu zake walipoingilia ugomvi huo.

Aidha wakiwa katika ugomvi huo watuhumiwa hao walimpiga Babu yao Makeremo kwa kitu kizito kichwani kwenye paji la uso pamoja na kumvunja mkono wa kushoto na kusababisha kifo hicho.

Diwani wa kata ya Igurubi Bw.Edson Sadani alisema kuwa kufuatia ugomvi huo pia mke wa marehemu huyo aliumia na kusema kuwa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Igunga kwa matibabu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi Peter Ouma alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na polisi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

KIJANA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDAIWA KUZITANDIKA POMBE KRISMAS

Chibula Makorongo, Shy, Tanzania
Kijana  aliyejulikana  kwa jina la Godi Shaini Fanuel Mangala (34) mkazi  wa mtaa wa Majengo Mapya  kata ya Ngokolo mjini Shinyanga amefariki dunia huku ikidaiwa kuwa chanzo ni kunywa viroba vingi kupita kiasi.
 
Tukio hilo limetokea Desemba 25 mwaka huu siku ya Krismasi  majira ya saa moja jioni ambapo marehemu ambaye pia ni mfanyakazi wa kampuni ya simu ya za mkononi Tigo alifariki dunia baada ya kile kinachosemekana kuwa alikunywa pombe nyingi.
 
Walioshuhudia tukio hilo walisema awali marehemu alikuwa anakunywa pombe na wenzake katika  bwaro la polisi  mjini Shinyanga lakini baadaye mwenzao alizidiwa na kulazimika kumrudisha nyumbani kwake ili akapumzike na baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ndipo wakampeleka katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu lakini akafia njiani.
 
Mmoja wa mashuhuda hao ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa anashindana na wenzake kunywa pombe lakini pombe zilimshinda na kuzidiwa hadi kupelekea kifo chake.
 
Naye  rafiki wa marehemu John Maganya  alisema ameshtushwa na taarifa za kifo cha rafiki yake kwani enzi za uhai wake marehemu alikuwa ni mzoefu wa kunywa pombe na wakati mwingine akilewa alikuwa anazimia na akizinduka anaendelea na shughuli zake kama kawaida lakini siku hiyo hali ikawa tofauti.
 
“Kifo cha rafiki yetu God Shaini, kimenishtua sana kwani kama ni kunywa pombe alikuwa ni mzoefu na huwa akinywa anazimia na kuzinduka,nadhani pombe aina ya konyagi aliyokuwa anakunywa na wenzake inaweza kuwa chanzo cha kifo chake,kwani alikunywa mizinga mitano ya konyagi”,alisema Maganya.
 
Akielezea tukio hilo diwani wa kata ya Ngokolo mjini Shinyanga Sebastian Peter alisema  kabla ya kifo chake marehemu alikuwa analalamika kusumbuliwa na vichomi tangu asubuhi siku hiyo lakini na baadaye mida ya saa moja jioni akapewa taarifa na wanachi wake kuwa God Shaini  ambaye alikuwa mtunza stoo wa Tigo amefariki kutokana na kunywa pombe kupita kiasi.
 
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa alikiri kuupokea mwili  God Shaini ,ambaye alikuwa mfanyakazi wa  kampuni ya simu ya Tigo mjini Shinyanga, muda wa saa moja jioni Desemba 25 mwaka huu,akiwa tayari amefariki dunia na mwili wake kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
 
Aliongeza kuwa kutokana na siku hiyo kuwa ni siku ya sikukuu walitegemea pengine tarehe 27 Desemba wangefanya upasuaji wa maiti ili kubaini chanzo cha kifo hicho lakini ndugu wa marehemu walifika Desemba 26 asubuhi na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi hivyo kushindwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala alisema hajapata taarifa za kifo cha mtu huyo na kwamba ndugu wa marehemu hawajafika kituo cha polisi kutoa taarifa kuhusu kifo cha ndugu yao .
 
Tayari mwili wa marehemu God Shaini umesafirishwa kwa ajili ya mazishi hapo kesho Siku ya Jumamosi Desemba 28 nyumbani kwa mama yake  Mabatini mkoani Mwanza.

MSIKILIZE LIVE DAKTARI HUYU WA KUTIBU UMASKINI

MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA, JAMES KISAKA WAAGWA LEO MUHIMBILI, KUZIKWA KESHO KIJIJINI KWAO LUSANGA, MUHEZA, TANGA

Dec 26, 2013

 Waombolezaji wakipakia kwenye basi la Simba, jeneza lenye kwenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa Makipa wa timu hiyo, James Kisaka, baada ya kuuaga leo jioni kwenye Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Mwili huo unatarajiwa kusafirishwa kesho alfajiri kwenda Muheza mkoani Tanga kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika saa saba, kijijini kwao Lusanga. Picha zaidi ingia ukursa wetu wa theNkoromo Sports au BOFYA HAPA

INGIA THENKOROMO SPORTS KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI KILA SIKU

Mdau wa theNkoromo Blog, unajua kwamba blogu yako hii uipendayo inazo kurasa mbalimbali ukiwemo wa 'Michezo na Burudani' kwa ajili yako? Kama ulikuwa unajua endelea kuhabarika kupitia pia kwenye ukurasa huo unaokwenda kwa jina la theNkoromo Sports, na kama ulikuwa hujui basi ingia kidogo kwenye ukurasa huo uuone ulivyo, Tafadhali BOFYA HAPA

TFF YAOMBOLEZA MSIBA WA KOCHA WA MAKIPA WA SIMBA JAMES KISAKA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeeleza kupokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya soka ya Simba, James Kisaka (57) kilichotokea, asubuhi ya Desemba 25, mwaka huu, katika Hospitali ya Burhani, Dar es Salaam.

     Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo imesema, msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwa kuwa Kisaka kabla ya kuwa kocha alikuwa mchezaji katika nafasi ya kipa.
    Imesema taarifa  mbali ya Simba, timu nyingine alizowahi kudakia ni...Inaendelea>BOFYA HAPA

MSICHANA AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMVUTA KORODANI

Dec 25, 2013

MEATU, Simiyu, Tanzania
Mkazi wa kijiji cha Usiulize wilayani Meatu mkoani Simiyu anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake kwa kumvuta korodani kutokana na wivu wa kimapenzi.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu kamishina msaidizi mwandamizi Charles Mkumbo aiambia theNkoromo Blog kuwa tukio hilo lilitokea jana saa tisa usiku katika kitongoji cha mlimani kijiji cha Usiulize kata ya Mwamalole wilayani Meatu.
 
Alisema katika tukio hilo wapenzi wawili Jumanne Gunda (39) mkazi wa kijiji cha Kinyambuli wilayani Mkaramo wakiwa wamelala na mchumba wake Mariamu Khamis (49) mkazi wa kijiji cha Ibaga wilaya ya Mkaramo mkoani Singida ilitokea kutoelewana kati yao na kusababisha wagombane.
 
Katika ugomvi huo ambao chanzo chake ni wivu wa kimapenzi Mariamu alifanikiwa kuzivuta korodani za mpenzi wake na kusababisha mishipa muhimu kukatika na kusababisha kifo cha mpenzi wake Jumanne papo hapo.
 
Kufuatia kifo hicho Mariamu aliuburuza mwili wa mpenzi wake mpaka chooni kwa lengo la kuudumbukiza katika shimo la choo lakini hata hivyo kutokana na udogo wa tundu la choo alishindwa kuudumbukiza mwili huo chooni na hivyo kuamua kuutelekeza humo humo.
 
Asubuhi kulipopambazuka majirani wa nyumba waliyokuwa wamefikia wapenzi hao waliugundua mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa chooni na kutoa taarifa katika kituo cha polisi ambao walifika katika eneo la tukio na kumtafuta mtuhumiwa Mariamu.
 
Baada ya kukamatwa kwa Mariamu alikiri kumuua mpenzi wake katika ugomvi kati yao uliotokea usiku walipokuwa wamelala wote wawili ambapo alikiri kumvuta korodani zake na kusababisha kifo chake.
 
Kamanda Mkumbo alisema katika tukio lingine juzi majira ya saa 2.30 usiku huko katika kijiji cha Itubukilo kata ya Ngulyati wilaya ya Bariadi mwanamke mkulima wa kijiji hicho, Thereza Mtobangi (67) alitoka nje ya nyumba yake kwenda kujisaidia na wakati akirudi alidakwa na fisi aliyemshambulia aliyemburuzia kichakani ambako alimshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kifo chake.
 
Mjukuu wa marehemu aliyekuwa amemsindikiza Leah Maduhu (11) alipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa majirani baada ya bibi yake kukutana uso kwa uso na fisi huyo na majirani walipojitokeza walianza msaka na kufanikiwa kumkurupusha fisi akiwa vichakani akiwa ameisha muua bibi yake.
 
Hata hivyo majirani hawakufanikiwa kumkamata fisi huyo baada kuwahi kukimbilia vichakani ambako hivi sasa wanakijiji kwa kushirikiana na maofisa maliasili wanaendelea kumsaka fisi huyo.

HAPPY BIRTHDAY YA MAMAA WA MITINDO ASIA KHAMSIN IDAROUS YAFANA KWENYE KIOTA CHA NYUMBANI LOUNGE

DSC_1539
Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Mamaa wa Mitindo Asia Khamsin Idarous, akizungumza machache kabla ya kukata cake kwenye mnuso wake wa kumbukumbu ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye kiota cha Nyumbani Lounge. Picha kibao za tukio hili, Tafadhali BOFYA HAPA

ZAIDI YA 100 WAPATIKANA USAILI WA SHINDANO LA VIPAJI KWA WATOTO LA 'MO KIDS GOT TALENT 2013'

DSC_1678 (2)
Chief Judge wa Shindano la "MO Kids Got Talent", Salma Mziray, akitoa maoni yake kwa baadhi ya washiriki wa usaili wa shindano hilo uliofanyika kwenye hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji Neema Theobald na kushoto ni msanii wa filamu nchini Hidaya Njaidi wakiwa meza kuu.
DSC_1672
Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wakionyesha vipaji vyao mbele ya majaji.
DSC_1705
Binti huyu kipaji chake ilikuwa ni kuimba taarab.
DSC_1785
Mambo ya Alingo nayo yalihusika.
DSC_1797
DSC_1745
DSC_1768
Hapo sasa twende kazi.....!!!
A04A7088
Majaji wa shindano la "MO Kids Got Talent" wakishuhudia kipaji cha mmoja wa watoto wanaojua kuogelea akijitosa kwenye bwawa la kuogelea lililopo Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
A04A7095
Chief Judge, Salma Mziray, akizungumza na mmoja wa washiriki kabla ya kuonyesha kipaji chake.
DSC_1773
Pichani juu na chini ni baadhi ya watoto walioshiriki usaili huo hawakuondoka mikono mitupu walipewa zawadi ya madaftari pamoja na sabuni ya Unga ya kufulia MO Detergent.
DSC_1692 (2)
DSC_1756
DSC_1788
DSC_1802
DSC_1726
A04A7120
Meneja Mkuu Ledger Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi (kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fros Africa, Bw. Peter Sekasiko (katikati) wakijumuika na wazazi pamoja na familia zao kwenye fukwe za hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar leo.
ยช