.

KINANA AZURU KATA ZA MWAMBAO WA ZIWA TANGANYIKA LEO KATIKA ZIARA YAKE WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Mar 31, 2014

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa,  Hypolitus Matete (aliyenyoosha mkono), akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana mandahari ya eneo la Ziwa Tanganyika, linalotumiwa na wavuvi katika eneo la Kabwe wilayani Nkasi mkoani humo, Kinana alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzitatua katika eneo hilo la Wavuvi, leo.
Katibu Mkuu wa CCM akitazama eneo la uvuvi katika ziawa Tanganyika, kwenye eneo la Kabwe mkoani Rukwa leo

Mfanyabiashara ya kusafirisha na kusindika samaki kutoka ziwa Tanganyika, Mohamed Shibibi (wapili kushoto) akimpatia maelezo  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana jinsi anavyohifadhi samaki katika majokofu baada ya kuvuliwa, Kinana alipokagua shughuli za mfanyabiashara huyo, kwenye eneo la wavuvi wa Kata ya Kabwe, wilayani Kansi mkoani Rukwa leo. Kushoto ni Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume.
Mfanyabiashara ya samaki Abuu Kitandu, akimuonyesha Kinana ukaushaji wa samaki kwenye kituo cha wavuvi cha Kabwe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa
Kinana akitazama lundo la samaki aina ya migebuka kwenye kituo cha wavuvi cha Kabwe, katika ziwa Tanganyika
Mkazi wa Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa akiwa na mzigo wa migebuka aliowanunua kwa wavuvi katika ziwa Tanganyika
Mtoto Khalifa Saidi (5) akiwa amebeba samaki kwenye eneo la wavuvi la Kabwe, wilayani Nkasi
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wajengo la Ofisi ya CCM Kata ya Kabwe, mkoani Rukwa, leo.
Wananchi wa Kabwe, wakiwa wamebeba samaki mkubwa kutoka Ziwa Tanganyika, wakati Kinana na Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ali Kessy wakiwafuata kwa nyumba baada ya kutoka kukagua shughuli za wavuvi katika eneo lawafugaji la Kabwe mkoani Rukwa. 
Boti za wavuvi zikitia nanga ufukweni eneo la Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Kabwe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa leo.
Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume, akihutubia wananchi katika mkutano wa Kinana, uliofanyika leo kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Kabwe leo.
Wananchi wa Kata ya Kabwe wakimshangilia Kinana
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Makao Makuu ya CCM, Godfrey Chongolo, akiwa na kina mama waliokuwa wakikunja samaki aina ya migebuka katika mwambao wa ziwa Tanganyika eneo la Kabwe, Wilayani Nkasi mkoani Rukwa. (Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog)

'BIG RESULTS NOW' YAKUSANYA MABILIONI KWA KIPINDI CHA NUSU MWAKA

 Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, leo Machi 28, 2014. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now). 
 Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
 Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
**************************************************
Na Sufianimafoto Reporter, Kibaha 
Serikali imekusanya jumla ya shilingi bilioni 215.0 katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye maabara za “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi. 

Haya yamo katika taarifa aliyoitoa msemaji mkuu wa wizara ya Fedha Bi alipokuwa akitoa taarifa ya utaratibu huo kwa wanablogu, katika kikao maalum na wadau hao kilichofanyika nje kidogo ya mkoa wa Pwani, maeneo ya Misugusugu.

Bi Mduma alisema Wizara ya Fedha ni miongoni mwa Sekta zinazotekeleza utaratibu huu hususan katika eneo la utafutaji wa mapato (Resource mobilization), sekta nyingine ni Elimu, Kilimo, Maji, Uchukuzi na Nishati.  

Utekelezaji wa kila sekta unazingatia viashiria vilivyoibuliwa katika uchambuzi wa kimaabara ulioratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Malaysia. 
Alisema huu unaiwezesha Serikali kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usimamiaji wa miradi kwa kuweka wazi malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuainisha  viashiria vya utekelezaji ili kuongeza uwajibikaji kwa kila mshiriki. 

Aidha, viashiria hivi hutumika kupima hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele na hivyo kuweza kupima mafanikio yaliyopatikana. Kadhalika, utaratibu huu unasaidia kurekebisha mapungufu katika utekelezaji kwa kuchukua hatua mapema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matokeo makubwa kwa haraka. 

Bi Mduma amesema wizara yake imedhamirisa utafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16;

KINANA ATINGA NKASI LEO, MAMIA WAHUDHURIA MKUTANO WAKE MJI MDOGO WA NAMANYERE

Mar 30, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na kinamama wa hamasa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika, Jumapili, Machi 30, 2014, katika mji mdogo wa Namanyere, wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kizitatua, katika mkoa wa Rukwa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano huo uliofanyika katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Jumapili, Machi 30, 2014.
 Kijana Elias Yeremia akimuuliza swali Kinana jukwaani, katika mkutano huo wa Namanyere, Nkasi mkoani Rukwa
 Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akihutubia mkutano huo wa Namanyere
 Vijana wa Namanyere wakiwa wamepanda juu ya lori siyo kwa lengo la kusafiri bali kuhakikisha wanamuona Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
Wazee wakimsikiliza kwa makini Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere 
 Mamia ya wananchi kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete, akimshukuru Kinana kwa hotuba nzuri, mkuatno huo wa Namanyere 
 Kikundi cha matarumbeta kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
 Mzee Rogas Nkana akimpatia ushahidi wa vielelezo na nyaraka mbalimbali kuhusu mirathi ya binti yake ambayo amefuatilia kwa muda mrefu hadi sasa bila mafanikio. Mzee Nkana alidai mbele ya Kinana kwamba madai hayo kwa ajili ya mirathi ya kifo cha binti yake ambaye alifariki dunia mwaka 2000 akiwa mtumishi wa Wirzara ya Mambo ya Ndani katika Jeshi la Uhamiaji yamekuwa kitendawili licha ya kufuatilia katika ofisi husika. Mzee Nkana alipata fursa hiyo wakati Kinana alipoamua kukutana na waasisi wa Chama na mabalozi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali katika ukumbi wa Community Centre katika mji mdogo wa Namayere wilayani Nkasi. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATOA TATHMINI YA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO CHALINZE

  • Kampeni zinaendelea vizuri, ingawa kuna malalamiko kidogo juu ya uvunjwaji ama ukiukwaji wa sheria za uchaguzi na malalamiko hayo yapo kwenye vyombo husika yanafanyiwa kazi.
  • Malalamiko hayo yanahusishwa na kupigwa kwa Viongozi na kujeruhiwa, wafuasi wa vyama vingine kwenda kufanya kampeni kwenye mikutano ya vyama vingine,kushushwa kwa bendera pamoja na rushwa hasa za kununua shahada za kupigia kura
  • Msajiri pia amelaani vitendo vya lugha za kashfa na dhihaka zinazoendelea na kuwaasa wakazi wa Chalinze kuepuka vitendo vya rushwa
  • Vyama vya Siasa vimeonywa kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa vyombo husika kila wanapoona inafaa.
Sisty Nyahoza Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akitoa tathmini ya uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze wakati wa mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Maasai Lungwe ,Chalinze leo.

 Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Ndugu Sisty Nyahoza Msajili Msaidizi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa mkutano na waandishi hao.

KINANA ATUA SUMBAWANGA LEO KUANZA ZIARA YA SIKU 21 MIKOA YA RUKWA, KATAVI NA KIGOMA

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishuka kwenye Ndege, Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga baada ya kuwasili leo kwa ajili ya kuanza ziara ya siku 21, katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa,  Hypolitus Matete, akimlaki Kinana (kulia) Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, leo. Kushoto ni  Katibu wa CCM wa mkoa, Lahel Ndegeleke
 Chipukizi wa CCM, Sharifa Tamim akimvisha skavu Kinana Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
 Kinana akipita katika paredi la Chipukizi baada ya kulakiwa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
 Kinana akiwasalimia viongozi mbalimbali Uwanja wa Ndege wa Sumbawanja, anayesalimia (kushoto) ni Mjumbe wa NEC, Ali Karume
 Kinana akimsalimia Mwenyekiti wa CCM Sumbawanga mjini, Emmanuel Kilindu, baada ya kuwasili Uwanja wa Sumbawanga, Kati ni Mzee wa Chama, Clisant Msindakaya
 Kinana akisalimia wananchi Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
 Kinana na Karume wakiaga wananchi katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
 Kinana na Karume wakifurahia ngoma, Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
 Kinana akiwaaga wananchi waliompokea Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
 Kinana akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Rukwa kuzungumza na Kamati ya Siasa ya mkoa
Kinana akifurahia jambo na Mzee wa Chama, Chrisant Mzindakaya nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Rukwa. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog

KINANA KUTUA SUMBAWANGA LEO KWA AJILI YA ZIARA YA MKOA WA RUKWA

theNkoromo Blog, Sumbawanga
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Pichani), anatarajiwa kutua mjini Sumbawanga, leo saa tano asubuhi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani Rukwa.

Taarifa zilizopatikana kutoka Ofisi ya CCM mkoa wa Rukwa zilizopo mjini Sumbawanga zimesema, baada ya kuwasili Kinana atakwenda katika Ofisi ya CCM ya mkoa ambako atapewa taarifa ya Chama ya utekelezaji wa Ilani mkoani Rukwa na baadaye kufuatiwa na taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa ilani hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kupata taarifa za Chama na Serikali kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM, Kinana anaondoka mjini Sumbawanga na kwenda Wilaya ya Nkasi ambako ataanza rasmi ziara yake kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara. 

KINANA ALIVYOTIKISA MWEMBEYANGA DAR ES SALAAM

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga.
 Wananchi waliohudhuria mkutano huo, uliofanyika juzi,  kumpongeza Rais
Jakaya Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa wakati wa kuzindua Bunge Maalum la
katiba,linaloendelea mjini Dodoma.


 Kinana akionyesha kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na Ramadhan (kushoto).
 Wananchi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe maalumu.

 Balozi Ali Abeid Karume, akizungumza katika mkutano huo


 Mwenyekiti wa Chama cha SDF cha Cameroun, John Frundi, akizungumza katika
mkutano huo. Kushoto ni Kinana na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhan Madabida.

 WANACHAMA wa CCM, wakimpongeza Kinana kutokana na juhudi zake katika
kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Baadhi ya wajumbe waalikwa waliohudhuria mkutano huo. Picha zote na Khamis Hamad
ยช