Breaking News

Your Ad Spot

Jun 6, 2014

Emirates yatoa punguzo maalumu la bei za tiketi kwa Watanzania wanaokwenda Chicago, Marekani

Wasilisha ombi la tiketi kabla ya Agosti 5 kwa safari za hadi Novemba 30, 2014


Shirika la Ndege la Emirates, linalosifika kwa kutoa huduma bora za usafiri wa anga kwa abiria kwa mataifa mbalimbali, limetangaza ofa maalumu kwa Watanzania watakaokwenda Chicago nchini Marekani, kupitia Dubai wakitokea Dar es Salaam. Punguzo hilo au ofa hiyo maalumu ni kwa madaraja ya abiria wa kawaida yaani Economy Class na daraja la wafanyabiashara ‘Business Class’.

Emirates ilitangaza ofa hiyo mapema Februari mwaka huu na ndege zake zitakuwa zikitua kwenye Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Chicago O’Hare. Safari hizo za kila siku zitaanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai, Terminal 5 ifikapo Agosti 5, 2014 na ndege ya Emirates itakayotumika ni aina ya Boeing 777-200 LR na hivyo kutoa fursa kwa Watanzania kutembelea jiji hilo la tatu kwa ukubwa nchini Marekani.

Gharama za tiketi ni kuanzia dola za Marekani 1,309 4,285 kwa tiketi ya daraja la abiria wa kawaida kwenda na kurudi na kwa abiria wafanyabiashara gharama ya tiketi ni dola za Marekani 4,285.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Emirates maombi ya ununuzi wa tiketi yafanywe kabla ya Agosti 5 na ununuzi wa tiketi hizo za ofa utafanywa kati ya Agosti 5 hadi Novemba 30, 2014. Kwa habari zaidi kuhusu gharama za tiketi na masharti mengineyo, wateja wanaombwa kufuatilia katika tovuti: http://www.emirates.com/tz.

Chicago iliyopewa hadhi ya jiji tangu mwaka 1837, ina idadi ya watu milioni 2.7na ni jiji linalosifika kwa mambo ya utamaduni na sanaa mbalimbali. Lakini pia jiji hilo linafahamika kwa kuwa bora katika michezo na hivyo hivyo kuwavutia watalii wengi kila mwaka. Inakadiriwa kuwa watalii wanaotembelea jiji hilo kila mwaka ni milioni 46.

Shirika la Ndege Emirates linafanya safari mbalimbali nchini Marekani na baadhi ya miji ambayo Watanzania wengi wamefikishwa na shirika hilo ni pamoja na Boston, Dallas Fort Worth, Houston, Los Angeles, New York City, San Francisco, Seattle na Washington D.C.

Abiria wa daraja la kawaida, pia wanaweza kununua tiketi kutoka Dar es Salaam kwenda Boston kwa dola za Marekani 1,534, kwenda Dallas Fort Worth 1,519, Houston 1,518, Los Angeles 1,854, New York City 1,533, San Francisco 1,854, Seattle 1,854 na Washington D.C dola 1,533. Gharama hizo ni kwenda na kurudi.

Kwa abiria wanaotaka kusafiri kutoka Dar es Salaam kwa daraja la wafanyabiashara kwenda na kurudi katika miji ya Marekani, gaharama ya tiketi ni kama ifuatavyo. Kwenda Boston dola 5,170, Dallas Fort Worth dola 5,810, Houston dola 5,810.

Kwenda Los Angeles ni dola 6,540, gharama ya New York ni dola 5,170 huku tiketi ya San Francisco ikiuzwa kuanzia dola 6,540 kwenda Seattle ni dola 6,540 na dola 5,170kwenda Washington D.C.

Emirates ilianza kusafirisha abiria kila siku kwenda Marekani mwaka 2004 na safari zake ni za moja kutoka Dubai hadi New York JFK. Kwa sasa safari zake zimepanuka na kuifikia miji ya Washington, Houston, Dallas, Seattle, San Francisco, Los Angeles. Huduma za kuelekea Chicago zitazinduliwa Agosti. Wasafiri ni mashuhuda kuwa tuzo ya ubora wa huduma iliyopewa Emirates inadhihirishwa kwa ubora wa huduma na uzoefu kutoka kwa wafanyakazi kutoka nchi 120 mbalimbali.

Abiria awapo safarini huburudishwa kwa aina tofauti za muziki wa kusikiliza na video. Mteja anaweza pia kuomba muziki autakao kulingana na matakwa yake. Ndege yenye namba EK 725 huondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kila sikua kuanzia saa 04:50 asubuhi na hutua Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 09:15 mchana. Ndege hiyo huruka kurejea Dubai saa 10:45 jioni na kuwasili saa 05:20 usiku.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages