Breaking News

Your Ad Spot

Jun 6, 2014

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA


Joka hilo kubwa aina ya Chatu likiwa nje ya Nyumba ya mfanyabiashara huyo, ambalo lilikutwa likiwa limefungwa Kitambaa cheupe kilichokuwa na maandishi ya Kiarabu, ambapo wananchi wamefananisha suala hilo na imani za kishirikina. Joka hilo baada ya kudhibitiwa liliburuzwa hadi katika Kanisa Katoliki la Karsamatiki lililopo eneo la Sakina jijini Arusha na kuanza kuuawa na wananchi.
Chatu huyo akiburuzwa kuelekea kucharangwa baada ya kuuawa.
  Nyoka aina ya chatu aliyetolewa nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Joseph Magesse akivutwa na wananchi kuelekea kwenye kanisa katoliki la karsamatiki eneo la Sakina jijini Arusha ambapo aliuawa kwa kucharangwa na shoka na wananchi wenye hasina na imani hizo za kishirikina
  ​​Kijana akiwa amembeba nyoka baada ya kucharangwa kwa mapanga akitoka naye nje ya uzio wa kanisa hilo
 Nyumba ya mfanyabiashara maarufu wa jijini Arusha, aliyetambulika kwa jina la Joseph Magese, alikotolewa nyoka huyo aina ya Chatu na kuuawa na wananchi kwa kucharangwa mapanga.
 Kitambaa chenye maandishi ya kiarabu alichokutwa nacho nyoka huyokikiwa mbele ya geti la nyumba ya mfanyabiashara huyo
umati wa watu waliofika kushudia tukio hilo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages