.

RAIS KIKWETE ALIHUTUBIA TAIFA, ASISITIZA KINACHOJADILIWA BUNGENI NI RASIMU YA TUME YA JAJI WARIOBA NA SI VINGINEVYO

Jul 31, 2014


Rais Jakaya Kikwete amelihutubia Taifa  ambapo alizungumzia mambo mbali mbali, na kuwataka UKAWA kurudi Bugeni
  • Awataka kutumia vyema fursa ya majadiliano
  • Asisitiza hakuingilia mchakato wa Katiba mpya
  • Asema mgogoro uliopo sasa hauna maana kuendelea

NAIBU WAZIRI MAKALLA AKAGUA MIRADI YA MAJI MKURANGA


 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akipata maerlezo kutoka kwa kiongozi wa Mafundi wa Kampuni ya CDM Smith, John Donoherth, kuhusu ujenzi wa kisima kilichopo Mkwalia Mkuranga ambacho ni moja kati ya visima 8 vinavyofanyiwa utafiti maji wilayani humo. Makalla alifanya ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo. Pia alikagua mradi wa  kisima cha maji cha Nyamato chenye uwezo wa kutoa maji lita 26,000 kwa saa kitakachohudumia wakazi wa vijiji vya  Mvuleni, Nyamato na Kilimahewa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Waziri Makalla akiangalia mradi wa kisima cha Mkwalia ambacho kinafanyiwa utafiti

 Maji yakitiririka kwenye kisima hicho

 Makalaa akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kisima hicho,John Donoherth

 Naibu Waziri Makalla akielezea namna Kisima kipya cha Nyamato kikianza kufanya kazi kuwa kitakuwa kinatoa lita 26,000 za maji kwa saa na kuhudumia sehemu kubwa ya wananchi wilayani Mkuranga, Pwani. Atakizindua kisima hicho mwanzoni mwezi ujao kitakapowekwa pampu iliyoagizwa Afrika Kusini. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamage, Abdallah Kiyewehe ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maji kijijini hapo.

 Mama mkazi wa Kijiji cha Mvuleni, wilayani Mkuranga akielezea mbele ya waziri jinsi wanawake wa eneo wanavyopata taabu ya kuata maji karibu umbali wa Km 5, na kuonesha furaha ya kupata kisima hicho kitakachowaondolea adha waliyokuwa wanaipata.

 Eneo la Kisima cha Nyamato kilichogauliwa. Kisimamhicho kinasubiri pampu tu ili kianze kufanya kazi.

 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mvuleni baada ya kukagua kisima cha maji cha Nyamato, wakati wa ziara yake wilayani Mkuranga leo.

 Sehemu ya umati mkubwa wa wananchi ukimsikiliza Makalla akihutubia kwa kuwaeleza mikakati ya Serikali ya kuwaboreshea wananchi sekta ya maji., ambapo  zimetengwa zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya wilaya hiyo.

 Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makalla

 Katibu wa Kamati ya Maji ya Mradi wa Nyamato, Ali Salum akielezea jinsi mradi wa Nyamato unavyosuasua kuzinduliwa, akidai anayesababisha hivyo ni Mkandarasi wa mradi huyo ambaye hatoi taarifa yoyote juu ya ucheleweshwaji huo.

 Mkandarasi wa mradi wa maji wa Nyamato, Jamila Chibwana wa Kampuni ya Mac Consultant  akitoa majibu ya ucheleweshwaji wa mradi huo, ambapo alisema moja ya sababu zilizosababishwa ni kutopewa fedga za ujenzi kwa wakati na uagizaji wa pampu kutoka Afrika Kusini.

Makalla akiagana na wananchi baada ya mkutano kumalizika.

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

1a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
2a
Rais mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
3a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
4a
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
5a
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katik mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
6a
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.

MEMBE ASEMA DINI NDIKO KWENYE CHIMBUKO LA AMANI NA UTULIVU, ACHANGIA KITABU CHA MUFTI

Jul 29, 2014

 
HABARI KATIKA PICHA KUHUSU BARAZA HILO LA EID
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamilius Membe, akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, huku waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kulia) akifuatilia mazungumzo hayo kwa pembeni, wakati wakiwa kwenye hafla ya Baraza la Idd El Fitr, leo, Julai 29, 2014, kwenye Viwanja vya Kariamjee, Jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid ElFitr, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiingia kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, akisindikizwa na  Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Kassim.
 Pinda akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili ukumbini
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Shaaban Issa Simba baada ya kuwasili ukumbini.
 Pinda akimtazama kwa furaha wakati Mwinyi akizindua kitabu kwa furaha ambacho kimeandikwa na Sheikh Mkuu, Shaaba Issa Simba, kitabu hicho chenye jina la Al Muhtaswar ni makusanyo mbalimbali ambayo sheikh Mkuu huyo ameyakusanya na kisha kutengeneza kitambu kwa ajili ya kukisambaza nchini kote kusaidia waislam kuzingatia vyema dini hiyo. Pamoja na wadau kadhaa, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe amechangia kuwezesha uchapishaji wa kitabu hicho.
 Mtoto  wa jijini Dar es Salaam, Arafat Msham akiduusu kitabu hicho
 Membe, Dk. Salim na Sumaye wakisoma kitabu cha Sheikh Mkuu Shaaban Issa Simba
Pinda akitoa hotuba yake kwenye Baraza hilo la Idd
 Kinamama kwenye Baraza hilo la Eid ElFitr
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa na Mama Shamim Khan kwenye Baraza hilo la Eid 
 Mwanazuoni akighani kaswida maalum kwenye Baraza hilo la Idd
Wanazuoni wakitumbuiza kaswida kwenye Baraza la Idd
 Ustaadhi Mroki Mroki wa Habari leo akifuatilia kwa makini shughuli za hafla hiyo ya Baraza la Eid
 Baadhi ya Wasanii maafurufu wa Bongo Movie akiwemo Steve Nyerere  nao walihudhuria Baraza hilo
Membe akiagana na wadau baada ya shughuli za Maulid. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

MWANDISHI WA HABARI KILIMANJARO AFARIKI KATIKA AJALI YA PIKIPIKI

Jul 28, 2014


RAIS KIKWETE AMLILIA ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA BAKWATA, ALHAJ KUNDYA


JAJI LEWIS MAKAME ALAZWA HOSPITALI, RAIS KIKWETE AMJULIA HALI

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali  leo, Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Lewis Makame aliyelazwa katika hospitali ya AMI iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam l (picha na Freddy Maro)

PINDA ASHIRIKI MAZISHI YA DR. KIPORI

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika mazishi ya Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dr, Irenius Joseph Kapiri, nyubani kwa Marehemu, Mbezi Marambo Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waomboleaji wakiwa  wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dr, Irenius Joseph Kapiri, katika mazishi  yaliyofanyika nyubani kwa Marehemu,  Mbezi Marambo Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwili wa  aliyekuwa Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dr, Irenius Joseph Kapiri, ukitemswa kaburini katika mazishi  yaliyofanyika  nyubani kwa Marehemu,  Mbezi Marambo Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014. (picha na Ofisi ya

OBAMA AKUTANA LEO NA VIONGOZI WADOGO WALIOONYESHA DIRA TOKA NCHO ZOTE ZA AFRIKA JIJINI WASHINGTON DC

 Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiingia  kwenye ukumbi wa mkutano ambao baadaye yeye na viongozi vijana wenzie watakutana na Rais Barak Obama wa Marekani  atakapozungumza nao  jijini Washington DC.
Hii ni sehemu ya program ya mafunzo kwa viongozi wadogo walioonyesha dira toka nchi zote za Afrika (most promising young African leaders) . Program hii imeanzishwa na Rais Obama mwenyewe.
Miongoni mwa watanzania wachache waliopata fursa ya kuhudhuria ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Steven Masele na Mhe. Joshua Nassari. Watakutana pia na Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na Mke wa Rais Obama Bi Michelle Obama Pamoja na maseneta, Magavana, wafanyabiashara wakubwa an watu wengine mashuhuri

DIAMOND ALIVYONG'ARA TUZO ZA AFRIMMA, MAREKANI


UCHAGUZI DMV, CHAGUA SALMA MOSHA MGOMBEA WA UMAKAMU WA RAIS.

Wana DMV mimi ndiye kiongozi wenu imara nisiyeyumba. Nitakuwa pamoja nanyi wakati wote kwenye shida na raha kwenye dhorubana shwari kwenye matatizo na mafanikio SITAJITOA na kuwaacha njia panda kama alivyofanya mgombea mwenzangu kwenye kikao ubalozini mbele ya Tume Board, Mh Balozi  na Wagombea July 18.

Alinyoosha kidole na akasema anajiuzuru, hatogombea tena. Viongozi aina hii ndio walioifikisha Jumuia pabaya, mguu ndani mguu nje ni kigeugeu. Hapa si mahala pa kujaribu  mimi nitakuwa nanyi katika kipindi chote mtakachonipa dhamana.

Kwa heshima na taadhima naomba kura zenu mimi SALIMA MOSHI mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais.

    ZIFUATAZO NI SERA ZA ZANGU
 UZOOEFU: Nina uzoefu wa kutosha  katika maswala ya uongozi  na maswala ya mawasiliano  nimekuwa kiongozi wa muda mrefu katika upande wa sanaa na eneo langu ambalo nilikuwa naishi nimeweza kukuza na kuinua vipaji na wasanii mbalimbali ambao ni maarufu.

Aidha kwa kudhihirisha kuwa ni kiongozi mtendaji na kuonyesha mfano niliweza kushiriki katika sanaa ya nyoka na kuliletea Taifa la Tanzania, sifa pia vijana kupata ajira na kipato  na ni mzoefu katika mawasiliano kwa rika zote, wakubwa, wadogo, vijana, wazee, wageni viongozi wa serikali kwa heshima na adabu kwa kuwaunganisha wote na kuleta umoja katika Jamiiyetu.

Nikiwa hapa DMV mimi na familia yangu tumekuwa tukisaidia wanajumuia kupata ajira na tumeshasaidia zaidi ya wana-Jumuia 25 ili kuweza kujikimu na kuhamasisha kudumisha umoja katika jamii yetu                                                                                                       


 UMOJA: Nitaimarisha 'network' ndani ya Jumuia yetu ili kuwa pamoja na kuvunja makundi na kuwa karibu na Jumuia zote zilizopo DMV na STATE nyingine na kote DUNIANI.

ELIMU: Nitaishawishi serikali kupanua wigo wa kutoa mikopo ya Elimu ya juu hata kwa walio nje ili wana DMV waweze kufaidika na mikopo hiyo ya Elimu ya juu.


KISWAHILI: Nitahakikisha tumepanga mipango madhubuti kuhusu darasa la kiswahili hasa kuhusu eneo la Darasa na Walimu  na kuliendeleza hadi kwa vijana  na kuwezesha kufungua darasa hata kwa watu wa hapa wanaotaka kujifunza kiswahili kwa kulipia ili jumuia kujipatia kipato.

Pia tutawafundisha watoto wetu wajue mila na desturi zetu, Kwa kutumia taaluma yangu ya sanaa nitaanzisha kikundi cha sanaa kwa watoto na vijana ili waweze kujua Utamaduni wetu wa kucheza ngoma sarakasi maigizo n.k. hapa DMV tuna vijana wanaweza kuimba kwaya na muziki wa dansi, tutaviendeleza vipaji vyao.

AFYA: Nitasimamia upatikanaji wa BIMA Nafuu ya Afya kwa wana Jumuia kuwasiliana na mashirika mbalimbali ya Afya ili wana-Jumuia kuwe na utaratibu wa kuchekiwa afya zao kila mwaka na kusaidia Wanajumuia kuwaelekeza maeneo kwa ajili ya huduma nafuu au ya bila malipo.

AJIRA: Nitahakikisha nimesimamia Jumuia yetu kuwa na miradi ya kuingizia kipato, pia itasaidia wana Jumuia kupata ajira kama 7-11 kwa wenzetu.

MAKAZI: Nitahakikisha nimesimamia Jumuia kuweza kununua nyumba kama mradi na wakati huohuo wanaJumuia kupata sehemu ya kuishi na kulipia katika Jumuia.

DMV COMMUNITY CENTER: Nitahakikisha tumefungua Community Center yetu ili iwe sehemu ya kubadilishana mawazona kupata vyakula vya Nyumbani.

MWANASHERIA: Nitasimamia upatikanaji wa mwanasheria wa Jumuia ili awe tayari kusaidia wana Jumuia katika maswala ya sheria.

WAZEE: Jumuia inahitaji Busara za wazee, nitahakikisha tumewashirikisha wazeena kukutana nao mara mbili kwa mwaka na ili kuwaenzi.

ARIDHI: Nitaishawishi Serikali kupitia wizara yake ya Aridhi kutupatia Eneo la Aridhi na kujenga kwa pamoja Nyumba za makazi kwa gharama nafuu kinakuwa kijiji cha wana DMV hiyo imewezekana kuna kijiji cha Wasanii mkuranga.

MIKOPO: Nitazungumza na Bank mbalimbali Nyumbani ili wanaJumuia waweze kukopeshwa mikopo ya Nyumba au Biashara kwa marejesho nafuu.

MAZISHI: Nitaishawishi serikali kuweza kuchangia gharama za Mazishi pale mwanaJumuia anapofariki kwa kutoa ubani wake kwani mwana JUmuia anachangia kiasi kikubwa maendeleo nyumbani pia nitaongea na NSSF kuweza kukubali kupokea michango nusu nusu kwa dhamana ya JUMUIA na kupunguza kiasi kwa kuwa italipwa kama kikundi.

URAIA PACHA: Nitasimamia na kushawishi serikali kupitisha uraia pacha ili mMtanzania aweze kuwekeza nyumbani bila kuonekana kama mgeni ndani ya nchi yake, Nitashirikiana na viongozi wote watakaochaguliwa ili tuweze kuleta maendeleo katika jumuia yetu


 Ndugu wana Jumuia wenzangu mtakumbuka tulikuwa na kikao kwa MH Balozi JULY18 na kuhudhuriwa na Board Tume na Wagombea Mgombea mwenzangu alitamka anajitoa na hataki kugombea tena huyu ni Nahodha kweli anabahatisha wakati wowote anaweza kuacha hataweza kuwavusha mifano tumeiona hatufanyi makosa tena mimi nitakua pamoja muda wote kwa hali yote kwa heshima naomba kura zenu ahasanteni.

MBUNGE WA TEMEKE ABASS MTEMVU AZIFIKISHA SALAMA KWA WADAU ZAWADI ZA RAIS KIKWETE

Jul 27, 2014

 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu na Mke wake, Mariam wakigawa zawadi za Rais Jakaya Kikwete kwa mdau, walipogawa zawadi hizo kwa viongozi wa CCM na Jumuia za Chama kutoka matawi yote katika jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, leo, Julai 27, 2014. Zaidi ya wadau 900 walipatiwa zawadi hizo ambazo ni seti za vyombo vya nyumbani, zilitolewa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kwa wabunge wote nchini ili kugawia wadau. Hata hivyo Mtemvu na Mkewe walinogesha kwa kumpatia sadaka ya sh. 10,000 kila mdau waliyemkabidhi zawadi hizo.
 Mke wa Mbunge wa Temeke Mariam Mtemvu, akigawa zawadi hiyo kwa mdau
 Mtemvu na mkewe wakigawa zawadi hizo kwa mdau
 Wadau wakifungasha vizuri zawadi zao baada ya kukavidhiwa na Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu ikiwa ni sehemu ya sadaka ya mwishoni mwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
 Kina mama wa jimbo la Temeke waliopata zawadi hizo wakisubiri kuondoka nazo
Vijana wakiondoka na zwadi zao baada ya kukabidhiwa na Mtemvu katika hafla iliyofanyika leo Julai 27, 2014, kwenye Viwanja vya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam. Picha na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
ยช