.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAJUMBE WA KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA (TCD), DODOMA LEO

Aug 31, 2014

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo akiongea na Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Mhe Isack Cheyo walipowasili Ikulu ndogo mjini Dodoma kukutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo. Nyuma yao ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mwenyekiti wa UPDP Mhe Fahmi Dovutwa leo.TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP.
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo , Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Isack Cheyo, Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mhe Fahmi Dovutwa wakielekea chumba cha mikutano Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo 
Wajumbe  wa TCD wakielekea chumba cha Mikutano
Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mhe Joseph Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa wakiwasili Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na wakiwasili Ikulu ndogo mjini Dodoma leo
Wajumbe wa TCD wakielekea chumba cha Mikutano Ikulu ndogo mjini Dodoma leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na Tundu Lisu wa Chadema na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Slaa na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana Mwenyekiti wa CUF Profesa Lipumba na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ambaye pia ni mjumbe wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula baada ya kukutana na wajumbe wa TCD  leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiagana Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, ambaye pia ni mjumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania
 Rais Kikwete akiagana nna wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
Rais Kikwete akiagana na mjumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania na Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustune Lyatonga Mrema Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo. PICHA NA IKULU

TANESCO LISIKIKILIZENI KILIO CHA WAKAZI WA MWANAGATI-KITUNDA

 Wananchi wa Mwanagati-Kitunda jijini Dar es Salaam  na maeneo jirani wamelilalamikia shirika la TANESCO  kwa kukatiwa umeme kwa siku tatu mfululizo,bila taarifa yoyote kutolewa kwa wakazi hao.''hatuna umeme kwa siku 3 mfululizo usiku na mchana mpaka sasa na hakuna taarifa zozote toka shirika la umeme Tanesco kuelezea hali hii inayoendelea mpaka sasa'',alilalama mmoja wa wakazi  wa eneo hilo.

Wakielezea kwa masikitiko makubwa juu ya tatizo hilo,Wananchi hao wamesema kuwa hawakupata taarifa yoyote ile toka Tanesco, na mpaka sasa wengi wao wamepata hasara kubwa kibiashara kutokana na tatizo hilo la kukosekana kwa umeme.

Mbali na matatizo hayo, Mji huo mpya ambao una chanzo chao cha kipekee kikubwa cha maji,kinachotegemea umeme katika uzalishaji wa maji na kufanya wananchi hao kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yao kuwa magumu zaidi.

Tunaliomba shirika la TANESCO lisikilize kilio chetu haraka iwezekanavyo,na kuhakikisha tatizo la umeme linatatuliwa kwa wakati ili kutuepusha na adha tunayoipata sisi wakazi wa Managati-Kitunda

Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la umeme Tanesco ili kuelezea tatizo ili kwa wananchi wa Mwanagati - Kitunda zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii.

MWANAAFA MWINZAGO AIBUKA KINARA WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014 NA KUONDOKA NA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA KITANZANIA

Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza akitoa neno kwa wadau waliojitokeza kushuhudia fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililokuwa pia likirushwa live kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akishangilia Mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kumsaka Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City na Kuhudhuriwa na Mamia ya Watanzania.
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na wazazi wake na timu ya wafanyakazi wa TMT na washiriki wenzie mara baada ya kukabidhiwa mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mara baada ya Kuwabwaga Washiriki wenzie tisa na Kuibuka Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Nchini lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limefikia Ukingoni Jana Katika Ukumbi wa Mlimani City.
Washiriki wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 waliofanikiwa kuingia Kumi Bora wakiwa wanasubiri mshindi atangazwe 
Host Wa TMT 2014 Joti akimpongeza Baba wa Mwanaafa Mwizago kwa Mwanae kuibuka Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) na kuibuka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Mwanaafa Akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 na kuibuka na kitita cha Shilingi milioni 50.
Lulu akionyesha Bahasha iliyokuwa na JIna la Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) ambae ni Mwanaafa Mwinzago na Kumfanya kujishindia Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia fainali ya TMT ambayo ilikua ikirushwa live kupitia ITV.

MWANDISHI WA HABARI AJITOSA KUWANIA UJUMBE KAMATI KUU CHADEMA

 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi Maryam Ahmed Omar akimkabidhi Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho kundi la Zanzibar, katika Ofisi Kuu za Chadema kisiwani humo.
 Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar
 Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chjama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar
 Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Mwanamrisho Abama akimdhamini Mgombe Ujumbe wa Kamati Kuu wa Chama hicho Salum Mwalim katika ofisi za chama Zanzaibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar.
Salum Mwalim anaewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kundi la Zanzibar akitia saini kitambu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi kuu za chama hicho Zanzibar kw alengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo

MTEMVU: CCM ITAUPUKUTISHA UPINZANI TEMEKE UCHAGUZI WA MITAA, SIYO KWA NGUVU ILA KWA MATUNDA YA UTEKELEZAJI ILANI


Na Bashir Nkoromo
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ametamba kuwa, CCM itapukutisha kwa kishindo upinzani wote katika jimbo hilo kwa kushinda mitaa yote katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

"Wala hatutatumia nguvu bali tutaichukua mitaa yote hata hiyo michache iliyopo sasa chini ya upinzani, kwa kutumia mtaji wa mafanikio makubwa tuliyoonyesha katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi hiki", alisema Mtemvu.

Mtemvu alitoa tambo hizo wakati akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Jumuia ya Wanawake Tanzania, Kata ya Azimio, kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Sokoine, katika Kata hiyo, Temeke jijini Dar es Salaam.

Alisema, CCM inao uhakika wa kutwaa viti vyote hadi kurejesha vichache vilivyopo sasa chini ya upinzani kwa kuwa mengi ambayo CCM iliahidi kupitia yeye wakati akiomba kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliopita yamefanyika.

Mtemvu alitaja baadhi ya yaliyotekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ambazo karibu zote zimeboreshwa kwa kujengwa kwa kiwngo cha lami tofauti na awali ambapo ilikuwa kero kubwa kwa kuwa zilikuwa hazipitiki kutokana na ubovu tena za vumbi.

"Zamani nilikuwa kila nikisimama jukwaani mnaniolea matatizo na kero lukuki hasa kuhusu hizi barabara, sasa leo hatuzungumzii matatizo ya barabara, tunazungumzia tu sasa kuboresha taa kwenye mitaa na barabara hizi", alisema Mtemvu.

Alisema, kuanzia mwezi huu Septemba, taa zote katika barabara na mitaa kwenye jimbo hilo zitawaka ambapo sasa zinafanyiwa maboresho ili zitumie nishati ya jua (solar) ili kupunguza changamoto ya gharama za malipo ya umeme wa taa hizo.

Mtemvu alisema, kukamilika kwa taa hizo itakuwa janga kwa vibaka ambao wamekuwa wakitumia fursa ya giza kujificha wakati wakivizia kuiba kwenye nyumba za watu na pia kukwapua wapitanjia nyakati za usiku.

Alisema mbali na kuboresha barabara CCM pia kupitia uongozi wake imeweza kuboresha hali za wananchi hasa kina mama na vijana kwa kuviwezesha vikundi vyao vya ujasiriamali kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ambapo sasa zaidi ya vikundi 100 vimenufaika.

Mtemvu aliahidi kuendelea kushirikiana na wabunge wengine wa Temeke na mkoa wa Dar es Salaam kwa jumla kuhakikisha watendaji wabovu serikalini wanakabwa koo ili wawajibike ipasavyo kutumikia wananchi.

Pia aliahidi kuhakikisha anaedelea kupigania kupatikana kwa mazingira bora ya kufanya kazi zao mamalishe na bodaboda kwa kuwa wana mchango mkubwa katika maendeleao ya jamii.

"Najua haiwezekani bodaboda zote zikaingia mjini, lakini tunachofanya ni kupigania kuhakikisha unakuwepo utaratibu mzuri utakaowezesha baadhi kufika mjini bila kuharibu taratibu na sheria zilizopo. Pia Mamalishe kwa kuwa lazima waendelee na shughuli zao tunawatafutia utaratibu bora kufanya shughuli zao kwa amani badala ya kukimzwa kimbizwa na mgambo kila mara", alisema Mtemvu.

Katika mkutano huo, uliosheheni burudani mbalimbali ikiwemo msanii Omari Tego kuimba wimbo maalum wa CCM ambao ulikonga nyoyo za waliohudhuria, Mtemvu aligawa kadi kwa wanachama wapya 45 wa UWT.

HABARI KATIKA PICHA KUHUSU MKUTANO HUO
Mbunge wa Temeke, Abbas  Mtemvu akihutubia mkutano wa hadhara uliofabyika kwenye Uwanja wa shule ya Sokoine, Temeke jijini Dar es Salaam, jana, Agosti 30, 2014.
Mtemvu akishangiliwa wakati akihutubia mkutano huo wa hadhara
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimpa kadi ya Uanachama wa UWT Maridha Rajabu wakati wa mkutano huo, wanachama wapya 45 wa jumuia hiyo walipewa kadi
Mbunge wa temeke,  Mtemvu akimtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo
Mbunge wa temeke,  Mtemvu akimpongeza baada ya kumtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo
Umati wa wananchi ukiwa umefurika wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Azimio, Tatu Hassan akifungua mkutano huo, kwenye Uwanja wa Sokoine Temeke kabla ya kuhutubiwa na Mtemvu
Diwani wa Kata ya Azimio, Hamisi Mzuzuri akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo wakati wa mkutano huo
Ofisa Kutoka Makao Makuu ya CCM, Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Gifti Isaya akipata picha kupitia simu yake kwenye mkutano huo
Waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo. Wapili walioketi kulia ni Ofisa katika Idara ya Mambo ya Nje Makao Makuu ya CCM,  Gift Isaya akifuatilia kwa makini pamoja na wenzake
Msanii Yusuf Peter wa Kikundi cha hamasa Temeke, akionyesha vimbwanga vyake mbele ya mke wa Mbunge wa Temeke  Mama Mtemvu (kulia)
Msanii Ahmadi Juma wa kikundi cha hamasa Temeke, akionyesha uhodari wa 'kula' moto wakati kikundi hicho kikitoa burudani wakati wa mkutano huo
Mtemvu akiwatuza wasanii waliotia fora uwanjani wakati wa mkutano huo. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ALIVYOTOA SEMINA YA UGONJWA HUO KWA MADAKTARI WA TANZANIA NA WADAU WA SEKTA YA AFYA KWA UDHAMINI WA KAMPUNI YA MABIBO BEER WINES AND SPIRITS LTD

Aug 29, 2014

Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akiwa kwenye semina hiyo.
Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari wa kitanzania na wadau mbaliombakli wa sekta ya afya. Semina hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana, Hoteli ya Protea Courtyard Seaview.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akizungumza katika semina hiyo. Kampuni hiyo ilidhamini semina hiyo.
Profesa Anthony Pais, akiwa na madaktari wa kitanzania. Kutoka kushoto ni Executive Chairman Tanzania Creative Industries Network (TACIN), Anic Kashasha na Dk.Paul Mareale.
Profesa Anthony Pais (kushoto), akielezea jambo kuhusu ugonjwa huo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela(kulia), akizungumza na wadau mbalimbali katika semina hiyo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni mke wake ambaye ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benedicta Rugemalira na Profesa Anthony Pais.
Profesa Pais (katikati), akiwa na wenyeji wake. Kutoka kulia ni Dk.Paul Mareale, James Rugemalira, Dk.Malina Njelekela na Benedicta Rugemalira.
Profesa Pais akizungumza na waandishi wa habari.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto), akipeana mkono na daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka India, Profesa Anthony Pais (kulia), baada ya kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira, waliodhamini mafunzo hayo ya siku moja.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.
Wadau mbalimbali na maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela(kulia), akiteta jambo na viongozi wengine kwenye semina hiyo.
Profesa Pais akifurahia jambo na Executive Chairman Tanzania Creative Industries Network (TACIN), Anic Kashasha.
Wadau wakiwa kwenye semina hiyo. Kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni iliyokuwa ikifua umeme ya VIP, Joe Mgaya.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Hali halisi ya ugonjwa wa saratani ya matiti inasikitisha sana.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mama Rugemalira na Dk.Njelekela wakifuatilia matukio mbalimbali katika semina hiyo.
Dk. Mareale na Kashasha wakiteja jambo kwenye semina hiyo.
Dk.Fred (kushoto), akiwa na wadau wengine katika semina hiyo.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye semina hiyo.
Wadau hawa wakifuatilia kila tukio katika semina hiyo.
Hawa nao walikuwa makini kufuatilia kila jambo katika semina hiyo.
Wakina mama wakiwa wamepigwa butwaa na kushika tama baada ya kuona picha za matiti yenye saratani wakati zikioneshwa na Profesa Pais.
Profesa Pais akiwa na wenyeji wake.Hapa maswali kuhusu ugonjwa huo yakiulizwa.
Mzee James Rugemalira akichangia kuelezea jambo.

Wadau wakichangia kueleza chochote kuhusu ugonjwa huo.

Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kila jambo.
James Rugemalira na mke wake wakimpongeza Dk. Njelekeza baada ya kutoa hutuba yake.
James Rugemalira(kulia), akisisitiza jambo.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake. (Picha zote na Dotto Mwaibale wa mtandao wa www.habari za jamii.com na Philemon Solomon wa Full Shangwe)

Dotto Mwaibale
ULAJI wa nyama nyekundu imeelezwa uchangia kwa kiasi kikubwa kupatwa na ugonjwa wa saratani ya matiti ambao umekuwa ni tishio duniani.

Hayo yalibainishwa na Daktari  bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti Profesa Anthony Pais kutoka Bangarole India katika semina ya siku moja kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya iliyofanyika Dar es Salaam juzi.

“Ulaji wa nyama nyekundu na vyakula vyenye mafuta unachangia kwa kiasi kikubwa kupata ugonjwa huo ambao umekuwa tishio duniani” alisema Pais.

Profesa Pais alisema mfumo wa maisha wa kula vyakula bila mpangilio na kukosa kufanya mazoezi pia ni moja ya sababu inayoweza kumsabishia mtu kupata ugonjwa huo.

“Ni muhimu kujenga tabia ya kufanya mazoezi walau kwa dakika 20 kila siku itasaidia kupunguza changamoto ya ugonjwa huo.
Akizungumzia ugonjwa wa saratani ya matiti alisema hauwapati wanawake pekee bali na wanaume lakini kutokana na kukuwa kwa teknojia mpya wamekuwa wakiutibu bila ya kuliondoa titi lenye matatizo.

Alisema hivi sasa dunia imekuwa ikitumia gharama kubwa kwa matibabu ya  ugonjwa wa saratani huku vikifunguliwa vituo vingi vya kutibu ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela alisema ni muhimu sasa kwa madaktari wa kitanzania kujifunza teknolojia hiyo ya upasuaji wa saratani ya matiti bila ya kuliondoa titi husika.

Mshauri  wa Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira ambaye amemleta Profesa huyo hapa nchini amesema baada ya kuona changamoto ya ugonjwa huo aliona ni vema kumleta mtalaamu huyo ili kuona namna ya kusaidia.

Alisema profesa huyo pamoja na kutoa mafunzo hayo mafupi pia atapata fursa ya kutembelea mikoa kadhaa ya kanda ya kati ili kutoa uzoefu wake kuhusu ugonjwa huo.

Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ilidhamini semina hiyo iliyofanyika Hoteli nya Protea Courtyard kupitia vinywaji vyake vya Windhoek Draught na Windhoek Lager.
ยช