.

PROGRAMU YA KUFUNDISHA HISABATI KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI YAZINDULIWA DAR ES SALAAM LEO

Sep 30, 2014

  Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtaalamu wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akizungumza katika uzinduzi huo. Kampuni ya Tigo, Nokia na Microsoft ndio wadau  mpango huo.
Meneja Mawasiliano wa Microsoft Mobile Devices, Lilian Nganda akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na 
Teknolojia Dk.Hassan Mshinda akizungumza katika 
uzinduzi huo.
 Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi huo.
 Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo (katikati), akiangalia simu wakati akiwaelekeza namna ya kutumia simu wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania,  Peter Riima (kushoto) na Mrashani Katebeleza, wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na vifaa vingine vya kielektroniki Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.
 Hapa uzinduzi huo ukifanyika.
 ' Ni kama anasema' Niacheni nipo kazini nachukua tukio hili nikawahabarishe wengine, chezea mimi nyiee
 Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye 
hafla hiyo ya uzinduzi.
Wadau na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Dotto Mwaibale

WANAFUNZI nchini wametakiwa kutumia mitandao hasa ya simu za mikononi kwa ajili ya kujifunzia masomo mbalimbali badala ya kutumia katika matumizi yasiofaa.

Mwito huo umetolewa na Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na vifaa vingine vya kielektroniki uliofanyika Dar es Salaam leo.

Alisema progamu hiyo imefika wakati muafaka na itawasaidia wanafunzi kujifunza somo hilo muhimu katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.

Alisema programu hiyo imeletwa nchini na Kampuni ya Nokia, Tigo kwa kushirikiana na Microsoft,  ambapo serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) inasimamia kwa karibu mpango huo.

Alisema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika programu hiyo imesaidia kupata mahudhui ya kihisabati jambo litakalo wasaidia wanafunzi kuwa makini kitaaluma.

Alisema matumizi hayo ya simu katika kujifunza hisabati yatakuwa yakifanyika katika muda wa ziada baada ya masomo kwa vile licha ya wanafunzi kumiliki simu lakini hawaruhusiwi kuwa nazo mashuleni.

Mgodo alisema mpango huo kwa sasa upo katika majaribio ukifanikiwa wanaweza kuuingiza katika mitaala ya taifa.

Mtaalamu wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska alisema mpango huo umekuwa ukiongeza weredi kwa wanafunzi katika somo la hisabati na ni muhimu katika kipindi hiki cha maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dk.Hassan Mshinda alisema tume hiyo ilifanyamchakato na kuukubali mpango huo ambao ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaupungufu mkubwa wa wataalamu wa sayansi wanaotokana na kufaulu kwa somo la hisabati.

"Mradi huu tuliona unafaa kwani utasaidia kuongeza wanasayansi hivyo tuliupokea kwa mikono miwili" alisema Dk.Mshinda.

KINANA ATINGA BUMBULI, ANG'AKA KIWANDA CHA CHAI KUFA MPONDE, ATAKA VIONGOZI WALIOHUSIKA WAWAJIBISHWE.

Sep 29, 2014


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika kata ya Mponde, akiwa katika ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga, leo, Septemba 29, 2014.
      Akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Kijiji cha Mponde, Kinana ameitaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kiwanda cha Chai cha Mponde, kufa baada ya kubinafsishwa kwa njia zinazoashiria kutofuata utaratibu unaotakiwa.
     Pia Kinana ameahidi kulifikisha suala hilo katika vikao vikubwa ikiwemo cha Kamati Kuu ya CCM, ili kuhakikisha unapatikana ufumbuzi wa kero hiyo ikiwemo kuwachukulia hatua viongozi waliohusika.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili katika kijiji cha Mbuzii kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata ya Mbuzii, katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, leo Septemba 29, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadili kwa makini jambo na Mbunge wa Bumbuli, Waziri Januari Makamba, wakati wa kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, jimboni humo, leo, Septemba 29, 2014.
 Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba akizungumza wakati wa makaribisho ya katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM, Kata ya Mbuzii jimboni humo mkoani Tanga, leo Septemba 29, 2014. pamoja naye ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akizungumza wakati wa makaribisho ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Wapili kushoto), kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, katika jimbo la Bumbumuli, Lushoto mkoani Tanga leo Septemba 29, 2014. Watatu kushoto  ni Mbunge wa jimbo hilo, Januari Makamba.
 Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana eneo la Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, linalojengwa pamoja na ukarabati wa ofisi ya zamani ya Chama ambayo ilikuwa imechakaa kutokana na kuwa ya muda wa miaka mingi tangu enzi za Tanzania kupata Uhuru
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki Ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, leo Septemba 29, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na kukagua uhai wa Chama katika jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mkoa wa Tanga. Kulia ni Mbunge wa jimbo hilo, Januari Makamba akifanya 'kibarua' cha kumpa tofali Kinana..
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua jengo la zamani la Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii ambalo linafanyiwa upanuzi na ukarabati, alipofika kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo, leo katika jimbo la Bumbuli mkoani Tanga. Nyuma yake ni Mbunge wa jimbo hilo, Januari Makamba
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrah,man Kinana akisalimiana na Mzee aliyesema kwamba amewahi kuwa dereva wa wakoloni, alipokutana na Kinana aliyewasili kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, jimbo la Lushoto mkoa wa Tanga.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi fungua na hati za pikipiki, kiongozi wa madereva wa Bodaboda katika kijiji cha Dule B, Kata ya Mbuzii wilyani Lushoto mkoa wa Tanga. Pikipiki hiyo imetolewa na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwatazama Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba wakiendesha pikipiki za waendesha bodaboda wa Kijiji cha Dule B, Kata ya Mbuzii, katika jimbo hilo wilayani Lushoto mkoa wa Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Majid Mganga akiendesha boda boda wakati msafara ukienda kwenye uzinduzi wa shina la wajasiriamali la Maisha Plus kata ya Dule.
 Gari la Maofisa wa CCM na Waandishi wa habai walioko kwenye msafara wa katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana likiwa limevunjika kioo baada ya gari hilo kukwaruzana na lingine, wakati msafara ulipowasili katika Kijiji cha Dule B, kuzindua shina la wakereketwa wa CCM ambao ni wajasriamali wa mradi wa kufyatua matofali wa Kikundi cha Maisha Plus. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus wakati wa ziara ya Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana .
 Wakazi wa kata ya Dule B wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao kabla ya kuzinduliwa kwa shina la wajasiriamali la Maisha Plus.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus ambapo alizindua shina la CCM wajasiriamali wa Maisha Plus katika kata ya Dule B
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupasua mawe kwenye kambi ya Maisha Plus ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijiandaa kuukata muwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akila muwa, Maisha Plus
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuelekeza  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba namna ya kupiga randa  kwenye Kituo hicho cha Maisha Plus.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya CCM  kuzindua shina la wakereketwa Wajasriamali wa CCM Kikundi cha Maisha Plus, eneo la Dule B ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto.
 Maisha Plus Bumbuli.
 Abdulkarim Jambia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Vuga akionyesha juu kadi yake ya CCM baada ya kurejea rasmi CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mponde.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijionea namna mashamba ya chai yalivyogeuka vichaka . Katibu Mkuu ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba.
 Mamia ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, katika Kata ya Mponde, jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga, leo Septemba 29, 2014.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo wa Kinana
 Baadhi ya watu wakiwa wamekaa ,kilimani kuhakikisha wanamuona Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipohutubia Mkutano wa hadhara katika Kata ya Mponde kwenye jimbo la Bumbuli mkoani Tanga leo.
 Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba akieleza kero kuhusu zao la chai na kufa kwa kiwanda cha Chai cha Mponde, alipokaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akuzungumza na wapigakura wake.
Mwananchi wa Mponde akieleza kwa hisia, jinsi wananchi wa Bumbuli wanavyosumbuliwa na kero ya kufa kiwanda cha Chai kilichopo Kata ya Mponde kwa miaka mingi sasa. Asilimia kubwa ya wakazi wa Bumbuli ni wakulima wa Chai. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

MLAPA NG’OSHA: KALALE PEMA (OFFICIAL VIDEO)

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Gabriel Samalu Ng’osha ‘Mlapa Ng’osha' ameachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Kalale Pema' aliyoelezea maisha ya mateso anayopata mama mjamzito.

Mojawapo ya picha katika video hiyo.
Video hiyo imetengenezwa chini ya prodyuza Melkiadi Oreje 'OJ' wakati audio ikifanywa na Lebo ya Audio Visual ya nchini Kenya chini ya maprodyuza Haptune & Douncher.

MSANII METTY KUZINDUA WIMBO WAKE MPYA "NAJUA" JUMATANO HII

Brand new song
Wimbo mpya ya msanii Metty iitwayo "Najua" inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 1 Octoba siku ya jumatano ya wiki hii  katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya Tanzania.

Wimbo huo amashirikishwa msanii Conrad anaekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki wa bongo flava ikiwa wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya watapata nafasi ya kumfahamu msanii huyo.
Najua ni wimbo uliotayarishwa katika studio mpya za kisasa Centric Records chini ya producer Eng.Davy Machords.

Metty amewaomba wadau na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kutoa ushirikiano wa nguvu katika kazi zake za muziki

MFUMO DUME NA MAWAZO MGANDO: KIKWAZO USHIRIKI WA MWANAMKE KATIKA UONGOZI

20140924_085545
Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio, Nuru Kalufya akisimamia usajili wa washiriki wa mafunzo ya Maadili, Jinsia na Kuandika Habari za Migogoro yaliyoanza katika kijiji cha Uvinza, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma tarehe 24 Septemba hadi 01 Oktoba 2014.
Na Mwandishi wetu, Uvinza.
Imethibitishwa kwamba mfumo dume ulioota mizizi katika jamii kwa kisingizio cha mila, desturi na dini unachangia kwa kiasi kikubwa katika unyanyasaji wa mtoto wa kike na mwanamke nchini.
Hayo yalithibitishwa na washiriki wa mafunzo ya maadili na jinsia yanayofanyika katika kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma wakati wakichangia mada ya Jinsia na Vyombo vya Habari iliyowasilishwa na mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Rose Haji Mwalimu.
Mshiriki kutoka Loliondo Joseph Munga ambae alizungumzia jinsi gani mfumo dume mgando unavyonyima haki za mtoto wa kike wa Kimasai, alisema kwamba mtoto wa kike hapaswi kwenda shule, kuna kiwango cha juu cha shinikizo la ndoa za utotoni, ukeketaji na wanawake kutokuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi.
“Ubaguzi unaanza katika familia, mtoto wa kike hana haki ya kuchagua mume anayemtaka au lini aolewe. Mtoto huyo huyo ni lazima akeketwe kwa sababu mtoto wa kike asiyekeketwa anaonekana ni laana katika familia na hawezi kupata mume. Kutokana na sababu hizo watoto wa kike huridhia kukeketwa ili waondoe laana hiyo lakini pia kwa kushinikizwa na wazazi wa kike.”
Hadi leo haijathibitishwa ni laana gani huwapata wasichana wasiokeketwa kwa maana kuna baadhi yao ambao hawakukeketwa, wameolewa na wanaendelea na maisha ya kawaida.
20140924_085927
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Maadili, Jinsia na Kuandika Habari za Migogoro katika maandalizi ya uchaguzi mkuu 2015.
Akizungumzia kuhusu uwakilishi kufikia 50/50 ifikapo mwaka 2015, Munga alisema kwamba bado kuna changamoto kubwa kwa mwanamke wa Kimasai kusimama na kugombea nafasi za uongozi kutokana na wanawake kutopewa nafasi ya kutoa maamuzi katika jamii ya Kimasai. Mathalani, moja ya tabia za mfumo dume mgando katika jamii hiyo ni mila na tamaduni za Kimasai ambapo mwanamke haruhusiwi kushiriki katika uongozi wa rika “laigwanang” kwa sababu jamii ya kimasaia inamlinganisha mwanamke na kumchukulia kama mtoto mdogo “nagara, ngara au ngarai”.
“Nafasi ambazo mwanamke anaweza kufaidika nazo ni zile za kuteuliwa tu basi,” alifafanua Munga.
Naye mshiriki kutoka kisiwani Tumbatu Ali Khamis alisema kwamba katika jamii yao mwanamke hana haki ya kutoa maamuzi katika ngazi ya familia na haruhusiwi kuhudhuria vikao vya harusi na misiba. Katika uongozi hali pia hairidhishi.
“Katika kisiwa cha Tumbatu viongozi wote wa ngazi za juu katika siasa ni wanaume. Ukianzia Afisa Tawala, masheha na madiwani ni wanaume, yupo mwanamke mmoja tu ambae ni wa kuteuliwa,” alisema Khamis.
Pemba ina majimbo 18 lakini hakuna mwanamke wa kuchaguliwa kisiasa wakati huo huo kisiwa cha Unguja ambacho kina majimbo 32 kuna wanawake watatu tu wa kuchaguliwa.
DSC_0036
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO akisisitiza jambo katika mafunzo yanayowashirikisha waandishi wa habari na watangazaji kutoka redio jamii nane nchini.
Mshiriki mwingine kutoka Uvinza mkoani Kigoma Leah Kalokoza alisema kwamba unyanyasaji kijinsia ni wa kiwango cha juu katika jamii inayouzunguka mji huo. Alisema kuwa mgawanyo wa kazi katika familia hauna uwiano kati ya mwanamke na mwanaume maneno ambayo pia yalithibitishwa na Balozi wa Barabara ya Kasulu Bi. Tabu Ramadhani.
“Wanawake ndio wanaotafuta riziki hususan kuvuna chumvi kazi ambayo ni ngumu sana, kulima na kulea watoto. Wanaume kazi yao ni kuuza chumvi hiyo, kukaa magengeni na kula hotelini wakati watoto nyumbani hawana chakula, kwa kweli wanatunyanyasa waume zetu.”
Tegemeo kubwa la kipato cha Uvinza ni chumvi pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa kipato hicho kimeshuka baada ya kiwanda hicho kubinafsishwa na mwekezaji mwenye asili ya Kiasia.
Akizungumzia uhuru wa kujieleza, Leah Kalokaza alisema kwamba wanawake hawaruhusiwi kuwasiliana na vyombo vya habari bila idhini ya waume zao. Tamko la Dunia la Haki za Binadamu kuwa na Haki ya Uhuru wa Kujieleza Ibara ya 19, linasisitiza uhuru wa kujieleza ni haki ya kila mtu, awe mwanamke au mwanamume.
Kutoka Mpanda mkoani Rukwa wanawake wananyanyaswa kwa kunyimwa elimu, kutokuwa na haki ya kumiliki kama ilivyo katika jamii nyingine na pia utu wao hudhalilishwa pale mabango katika nyumba za kulala wageni huwa yanakuwa na picha au ujumbe dhahiri wa mfumo dume.
DSC_0022
Mambo mengine yanayochangia udhalilishaji wa wanawake ni nyimbo mbalimbali ambazo humsifu mwanamume na kumkashifu mwanamke hususan sehemu za Usukumani.
“Kwa mfano, kuna Wimbo unaosema, ‘kuzaa mtoto wa kiume jamii yote inafurahia, kuzaa mtoto wa kike ni maandalizi ya sherehe. Hii inaonyesha ni kwa namna gani mwanamke katika tamaduni za Kisukuma hana hadhi hata mbele ya mtoto aliyemzaa mwenyewe,” alisema Anatory John.
Mkoa wa Shinyanga umekumbwa na wimbi kubwa la mauaji ya vikongwe wanawake kwa tuhuma za uchawi, lakini ikija kwenye uganga wa jadi hawatambuliki.
“Waganga wengi wa Kisukuma ni wanaume kwa imani kwamba wanawake hawana uwezo wa kuzungumza na mizimu au miungu”, alielezea Anatory.
Vyote hivyo ni viashiria vya mfumo dume au mawazo mgandoyanayoendeleza tabia ya kumwona mwanamke ni mtu duni na mwanamume ni mtu mwenye uwezo wa pekee.
DSC_0010
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea kupata darasa kutoka Mkufunzi wao Bi. Rose Haji Mwalimu Uvinza mkoani Kigoma.
Kipengele cha Vyombo vya Habari katika Itifaki ya SADC kuhusu Jinsia na maendeleo kinaazimia kuhakikisha kuwa jinsia inaingizwa katika habari, mawasiliano na sera za vyombo vya habari, mipango, vipindi, sheria na mafunzo kulingana na Itifaki ya Utamaduni, Habari na Spoti.
Azimio la Jinsia na Maendeleo lililotolewa na Viongozi wa Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika au Serikali (SADC) linasisitiza uwakilishi wa uongozi katika ngazi ya maamuzi 50/50 ifikapo mwaka 2015.
Warsha ya Maadili na Jinsia inalenga kuwapa uwezo waandishi na watangazaji wa redio za jamii nchini kuandika habari zinatoa changamoto za mfumodume/mgando na matumuzi ya Lugha nyepesi inayohusisha jinsia zote bila kubagua hasa katika kipindi hiki tunakoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi wa raisi mwaka 2015.
Warsha hii ya siku nane ilijumuisha waandishi wa habari wa redio jamii 48 kutoka redio 8 za jamii Tanzania Bara na Visiwani.
Mradi huu unatekelezwa kwa pamoja kati ya UNESCO na Vyombo vya habari Jamii chini ya mtandao wa COMNETA na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP.
DSC_0014
20140925_142505
Washiriki wa mafunzo ya Maadili na Jinsia katika vyombo vya habari wakiwa katika vikundi kazi.
DSC_0178
Mshiriki wa mafunzo kutoka Redio Loliondo FM, Joseph Munga akichangia mada ya Jinsia na vyombo vya Habari katika mafunzo ya siku nane ya kuzipa uwezo redio jamii kuandika habari chanya cha uchaguzi na migogoro.
20140926_155057
Mshiriki kutoka Tumbatu FM Radio Kisiwa cha Tumbatu, Unguja Ali Khamis akizungumzia changamoto za mfumo dume na mawazo mgando yanayodumaza maendeleo ya mwanamke.
IMAG1321
Pichani ni mshiriki na mwandishi wa habari Uvinza FM Radio, Uvinza- Kigoma Leah Karokaza akichanganua masuala yanayoendeleza unyanyasaji wa kijinsia wilayani Uvinza.
IMAG1332
Anatory John kutoka Baloha FM Radio, Kahama akichanganua baadhi ya misemo na nyimbo zinazomdhalilisha mwanamke.
IMAG1327
“Mabango yanayotundikwa katika nyumba za kulala wageni yanadhalilisha sana wanawake”, ndivyo asemavyo Sharifa Selemani kutoka Mpanda FM Radio, Mpanda mkoani Rukwa katika picha.
20140925_163431
Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki wa mradi wa kuzipa uwezo uwezo redio jamii katika mchakato wa uchaguzi mwaka 2015.
ยช