Breaking News

Your Ad Spot

Sep 17, 2014

KINANA AHUTUBIA MAELFU YA WATU KISIWANI MAFIA, AWATAKA VIONGOZI CCM WAACHE KUENDEKEZA FITNA WAJIKITE KATIKA MAENDELEO YA WANANCHI

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkunguni, Stendi ya Mabasi, katika  Kisiwa cha Mafia, leo, Septemba 16, 2014, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mkoawa Pwani. Kinana amewataka viongozi wa CCM kisiwani humo, kuachana na maswala ya kufitiana kwa ajili ya kusaka uongozi badala yake wajikite zaidi ya maswalaya maendeleo ya wananchi kwa sababu kufanya hivyo ndiyo kutaimarisha chama na kukifanya kipendwe zaidi na wananchi.
 Mamia ya wananchi wa Mafia wakiwa kwenye mkutano huo wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mafia kwenye uwanja wa Mkunguni stendi ya Mabasi mjini Mafia.
Naibu Waziri Nishati Charles Kitwanga akihutubia wakazi wa Mafia ambapo aliwaambia Mafia ndio wilaya pekee itakayopata Umeme kwa asilimia mia moja.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages