Breaking News

Your Ad Spot

Sep 20, 2014

SHIRIKA LA NYUMBA LATOA MASHINE 28 ZA KUFYATULIA MATOFALI KWA VIJANA MKOANI PWANI


 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Pwani Pauline Mrango akisoma Hotuba ya makabidhiano ya mashine 28 za kufyatulia matofali kwa vikundi vya vijana katika halmashauri zote za mkoa wa Pwani. Mbali ya mashine hizo zenye gharama ya zaidi ya sh. milioni 12 ni pamoja na mafunzo ya wiki mbili kwa vijanai ambapo baada ya kumaliza mafunzo Shirika litatoa msaada wa sh.laki tano kwa kila kikundi kama mtaji .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa pwani Pauline Mrango kwa kutoa mashine 28 za kuwasaidia vijana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Pwani.
Mashine 28 zitawasaidia vijana mkoa wa Pwani kuondokana na tatizo la ajira, pili litasaidia sana katika utunzaji wa mazingira,zitasaidia wananchi kujenga nyumba za kisasa na kwa bei nafuu.(Adam Mzee)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages